Nitashiriki kuzuia maandamano ya CHADEMA Januari 24, 2024

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,318
12,622
Uhuru wangu utakomea pale unapoanzia uhuru wa mwenzangu. Kuna wanaotaka kuandamana na kuna wasiotaka kuandamana itakuwaje hapo? Kuna magari na waenda kwa miguu watakaosumbuliwa na maandamano haya yanayofanyika siku na saa za kazi. Chadema ilikutana na wananchi wanaolalamika wangapi lini na wapi waliowatuma viongozi wa chadema waondoe miswada bungeni?

Tusiotaka maandamano tuna haki zetu pia za kulindwa na serikali tusibughudhiwe kwenye nchi yetu. Nitamsaidia yeyote atakaesema anaenda kuzuia maandamano hayo yasifanyike ili kuzuia usumbufu, ajali na wizi.

Lala basi dada angu muda umeenda ati
UN mbona haifanyi kitu kule Gaza na Ukraine, ndio itafanya kitu tanganyika? hakuna kitu kama hicho. hata marekani Trump alilalamika uchaguzi haukuwa huru na haki na UN iko palepale Marekani mbona hakuna walichokifanya? tuache kuwatumia wananchi kujenga mahotel na majumba kwa kuwarubuni wananchi.
 
Uhuru wangu utakomea pale unapoanzia uhuru wa mwenzangu. Kuna wanaotaka kuandamana na kuna wasiotaka kuandamana itakuwaje hapo? Kuna magari na waenda kwa miguu watakaosumbuliwa na maandamano haya
ntajitahidi kukutembelea stakishari police post kiuno kikiwa legevu na taya zikiwa zimepishana ndugu nyumbu :cool:
 
Wewe kazi yako ni kuzuia maandamano? Kuna watu mnataka kufikingwa kwa lazima!. Watu wanapoandamana kumpomgeza Bibi tozo Kuna wanapenda kuandamana kuzuia? Wewe njoo utatukuta na bisibisi tutakutia za mataqo.
Mbona hamuandamani kupinga Wabunge na madiwani waliochanguliwa na walalahoi kwa taabu kubwa wanapowasaliti wapiga kura wao kwa kwenda kuunga juhudi (Manasari) CCM? Tumeona wabunge tuliowachangua wakinunua magari makubwa ya kifahari na kujenga mahoteli na majumba makubwa badala ya kutumia fedha hiyo kuimarisha vijijini. Tumeshuhudia viongozi na familia zao wakikimbia nchi na kwenda ulaya baada ya kuchafua huku na kutuacha sisi tusiokuwa na kwakwenda. hebu tuacheni waganga njaa nyiee wa kilimanjaro.
 
ntajitahidi kukutembelea stakishari police post kiuno kikiwa legevu na taya zikiwa zimepishana ndugu nyumbu :cool:
hahaha, jaribu uone!!! Kaka hakuna vyama vya siasa imara hapa kwetu kuna walanguzi wa kisiasa tu wanaotumia wananchi waliopigika kiuchumi kama mtaji wao na watoto wao. Sasa hivi wameshaweka passports zao standby tayari kwa kutoroka kupitia mpaka wa Nairobi.
 
hahaha, jaribu uone!!! Kaka hakuna vyama vya siasa imara hapa kwetu kuna walanguzi tu wanaotumia wananchi waliopigika kiuchumi kwa maslahi yao na watoto wao. Sasa hivi wameshaweka passports zao standby tayari kwa kutoroka kupitia mpaka wa Nairobi.
vyama vya upinzani 14 leo wamewazodoa Chama Cha mapanyarodi na manyumbu Chadema kwamba ni wabinafsi, wapingaji kila kitu bila sababu za msingi, na zaidi sana wamesma hayo maandamano ni haramu wananchi wayaepuke kama ukoma na kipindrupindruuuuu......
 
  • Thanks
Reactions: Tui

Afrika liko tatizo kubwa sana kuliko hata vyama vya siasa vinavyotawala na demokrasia. Shida yetu sio demokrasia, maana hata huko Oman, Dubai, Saudi Arabia, China, Urusi hakuna demokrasia lakini mambo yao yanakwenda ile mbaya. Hama Marekani hakuna demokrasia; yapo majimbo yanalalamika, watu wengi sana wako gerezani hasa wanaume, habari halisi zinafichwa na hakuna demokrasia kwenye kulipa kodi. Tusidanganyane hapa kwa kivuli cha demokrasia. Pale Uingereza kuna ukoo mmoja tu unatawala milele, Ireland haina uhuru wa kujiamulia mambo yao. Tuache uzuzu huu wa demokrasia badala yake tujikite kwenye kuwakata vinjwa hadharani wezi na wabadhilifu wa mali zetu za umma.
 
Kwa hiyo wewe inakuuma nini? shame on you
tunataka mitaa na barabara zetu ziwe wazi kwaajili ya raia kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila bughudha. Tatizo letu kuu ni uchumi sio demokrasia. Kama ukiitisha maandamano kupinga wizi na ubadhilifu pale bandarini au TRA au ofisi ya DPP au au au.... nitakuwa wa kwanza kuunga mkono na kuhudhuria maandamano hayo. Demokrasia demokrasia demokrasia, huo ni wimbo tuliofundishwa kuuimba na wakoloni wetu wa zamani tuuimbe bila kuwa na vina wala vituo (punctuation)
 
Mje na mumeo
 
Mje na mumeo
Chadema nadhani wanataka walalahoi wawasaidie kupata ubunge, udiwani na ikiwezekana ikulu kabisa bila kusema kama wakiingia ikulu elimu yetu itakuwaje, ajira itakuwa je, fedha watatoa wapi, masoko ya bidhaa zetu yatakuwa yapi, bei za mazao yetu kwenye soko la dunia zitakuwaje na nani atazipanga.
 
Afrika liko tatizo kubwa sana kuliko hata vyama vya siasa vinavyotawala na demokrasia. Shida yetu sio demokrasia, maana hata huko Oman, Dubai, Saudi Arabia, China, Urusi hakuna demokrasia lakini mambo yao yanakwenda ile mbaya. Hama Marekani hakuna demokrasia; yapo majimbo yanalalamika, watu wengi sana wako gerezani hasa wanaume, habari halisi zinafichwa na hakuna demokrasia kwenye kulipa kodi. Tusidanganyane hapa kwa kivuli cha demokrasia. Pale Uingereza kuna ukoo mmoja tu unatawala milele, Ireland haina uhuru wa kujiamulia mambo yao. Tuache uzuzu huu wa demokrasia badala yake tujikite kwenye kuwakata vinjwa hadharani wezi na wabadhilifu wa mali zetu za umma.
unawakataa wezi hadharani ukiwa wapi,
ukiwa na njaa au umeshiba,
na ukiwa na historia gani ya usafi wa hoja,
au ni matusi tu kama yote kisha unatamani kila moja awe mtukanaji na kuona unachodai na kujadili wewe na yeye akione hivyo hivyo......
Ni kazi sana aisee.....

Actualy lipo tatizo but wengi katika siasa za africa hususan Tz hawajabaini tatizo la msingi hasa ni lipi, na ndio maana leo wanadai hiki , kesho wanadandia kile tena kwa lugha na mtazamo tofauti kabisa miongoni mwa wanasiasa....

hawata fika mahala popote , hawawezi piga hatua kabisa......
 
Kwenye nchi moja bila kujali itikadi za siasa, dini wala kanda zetu lazima wote tukubaliane katika vitu vya msingi ambavyo havina haja ya kuhojiwa maana hivyo ni vya kwenu wote na nilazima vibaki hivyohivyo hata kama wewe huvipendi. Tanzania kuna vitu ambavyo woooote lazima tuvienzi kama vilivyo bila kubadilisha nukta. Vitu hivyo ni kama vile dini zetu, wimbo wa taifa, kiswahili, bendera, muungano na mipaka yetu ya nchi. Kila mtu bila kujali itikadi yake lazima avivumilie kama vilivyo hata kama havipendi. Mtu anapopanda jukwaa la kisiasa na kuanza kuhoji muungano, dini za watu, wimbo wa taifa, makabila au mipaka ya nchi yetu hatakiwi kuitawala nchi hii na itamchukuwa muda mrefu kufanikiwa kuitawala nchi hii. Wazee wetu kuna vitu vingi wamevipatia na kuvikosea kwaajili yetu kama vile wazazi wetu walivyokosea na kupatia katika kutupatia majina yetu. Aliyesema nchi yetu iitwe Tanzania alifanya hivyo kwa niaba yetu, hatutakiwi kumlaumu. Hata wazungu tunaosema wameendeleaa kuna vitu vilivyokosewa hawavihoji wala kuruhusiwa kuvihoji. Waingereza kuna watu wangependa kuhoji kwanini familia moja tu ya kifalme ndio inakula keki kubwa ya nchi milele, lakini hawana nafasi ya kuhoji, kule marekani kuna watu wanaohoji kuhusu majimbo yao hasa inapofika wakati wa uchaguzi wa marekani lakini watu hao hawapewi nafasi ya kuhoji maana babu zao walishaamua iwe hivyo kwa niaba yao na wajao.

Kitu cha msingi kinachowachelewesha vyama vya upinzani nchini kuingia Ikulu ni kuhoji Muungano wetu kila wanapopata nafasi ya kupanda jukwaani, ni kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali kinachowaudhi baadhi ya wananchi, hii husababisha nchi yetu ibaki nyuma kwenye maeneo fulani. Mfano, wapinzani wanatafuta kura kwa kupinga machinga wasiondolewe barabani na kwenye mitaro, wanapinga barabara kutanuliwa, wanapinga wamasai kuhamishiwa sehemu nyingine ili kupisha wanyama, watu kuhamishwa mabondeni, wanapinga ubinafsishwaji wa bandari, wanapinga bomba la gesi na mafuta visijengwe, wanapinga kila kitu kama mtaji wao wa kupata kura. CCM nao kwa kuogopa kukosa kura za hao watu wanaamua kuacha kuwapanga bodaboda, machinga, nk
 
uko sahihi ndugu kiongozi, nimekuelewa vema sana. Hata na hivyo..

ikibainika tatizo la misingi ni nini kwa hoja na ufafanuzi mujarabu hapatakua na tashwishwi yeyote kwa wananchi kuuangana bila kujali, dini, rangi, kabila au mirengo ya kisiasa na kufanya mageuzi wanayoyataka....

Kwa hali ilivyo nchini na pengine kwasabb ya malezi na itikadi za vyama ndio maana watu hupinga kila kitu na saa zingine bila hata hoja,

lakini pia hali hiyo imechochea tabia ya kudandia kila hoja, kitu ambacho kinadhihirisha dhahiri shahiri kwamba hakuna dhamira ya kweli ya kuongoza mageuzi na ndio maana kupuuzana na kubezana kumekua kwingi pia kwa viongozi wa kisiasa na vyama vyao 🐒
 
Back
Top Bottom