Nabii Josephat Mwingira anena Mazito kwenye Salamu za Heri ya Krismasi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,878
Salamu za Heri zinaendelea kumiminika. Hapa chini ni kutoka kwa nabii Mwingira:

IMG_20211226_145724_780.jpg


Salamu za kama hizi zinapoendelea kutufikia ni vyema kujitafakari. Ni wazi kuwa kama Taifa hatuko vizuri.

Walikuwapo kina Desmond Tutu, leo hatuko nao. Walifanya sehemu yao, wamekwenda. Angalia katika kuwaomboleza hakuna dongo hata moja.

"Tunayo ya kujifunza."

Kila mtu kwa nafasi yake anayo sehemu yake ya kufanya, atakayo kumbukwa nayo.

Ni wazi kuwa chuki tunazoziona kwetu ni matokeo ya kumea kwa mbegu zake tunazozipanda wenyewe.

Haki huinua taifa.

Barikiwa mtumishi wa bwana, nabii Mwingira.

=====

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 26/12/2021 KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM TANZANIA.
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
SOMO: GIZA NA NURU.

Mwanzo 1:1-2 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”

Ninapoiona nchi ninaona muumbaji alifanya kitu, Mungu ndio mwenye mali lakini hapa tunaona giza liliruhusiwa kuwepo tangu mwanzo. Katika vyote vilivyokuwa vimeumbwa kuna kinachoshinda vyote ambavyo ni Roho ya Mungu ambayo hata giza liko chini ya mamlaka hiyo.

Mwanzo 1:3 “Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.” Kwa nini alisema kuwe na nuru wakati mbingu na nchi ipo, giza pia lipo? Mwisho wa siku Mungu alitaka kitu kitokee kwa tangazo lakini vingine aliviumba tu na ikawa lakini kwa hili alitangaza. Nuru iko pale ili kufanikisha uzuri na ubora wa uumbaji wa Mungu;
• Nuru inafanya Mungu ajulikane kama Mungu na ubora wake.
• Nuru ipo ili uumbaji uoneshe ubora wake.

Haya mambo mawili giza haliwezi kufanya wala Roho ya Mungu lakini nuru inaweza.

Hapa tunaweza kuiona kazi ya nuru; Mithali 8:22-30 “………… Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi; Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake;” Hapa tunaona kuwa Nuru ni mtendaji na mboreshaji na Yeye ndiye mfanyaji wa mambo yaweze kuwa.

Wafilipi 4:8 “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.” Hapa anabainisha tofauti kati ya giza na Nuru, pasipo Nuru Mungu asingeitwa mwema, mzuri, Yeye ni wa rehema, asingeitwa ni wa fadhili wala asingeitwa ni wa upendo.

Hapa ndipo msingi wa kesho yako unapoanzia, unaanza wapi? Kwa wewe kufahamu ya kwamba Mungu aliumba mbingu na nchi na kwamba hiyo nchi aliyoiumba ilikuwa ukiwa na utupu lakini pia kwenye hiyo nchi giza lilikuwepo lakini kwa kupitia uwepo wake (huyo giza) hakusababisha chochote kiwepo, kwa nini? Kwa maana yeye si halisi, hana kweli yoyote kwa maana yeye hana anachoweza kumiliki na ndio maana anaitwa mwizi.

Serikali yoyote isiyo na uwepo wa Mungu ni wezi na ndio maana wanaweza kuiba mpaka kura kwa maana ni wa ibilisi. Mungu akaona alete Nuru ili isababishe mambo kuwepo na utupu na ukiwa usiwepo.

Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”

Kazi ya giza ni uongo, wizi na uuaji, mwizi hazalishi chochote na ndio maana anaiba, mwongo hazalishi pia kwa maana hakuna kweli ndani yake.
 
Salamu za Heri zinaendelea kumiminika. Hapa chini ni kutoka kwa nabii Mwingira:

View attachment 2058365

Salamu za kama hizi zinapoendelea kutufikia ni vyema kujitafakari. Ni wazi kuwa kama Taifa hatuko vizuri.

Walikuwapo kina Desmond Tutu, leo hatuko nao. Walifanya sehemu yao, wamekwenda. Angalia katika kuwaomboleza hakuna dongo hata moja.

"Tunayo ya kujifunza."

Kila mtu kwa nafasi yake anayo sehemu yake ya kufanya, atakayo kumbukwa nayo.

Ni wazi kuwa chuki tunazoziona kwetu ni matokeo ya kumea kwa mbegu zake tunazozipanda wenyewe.

Haki huinua taifa.

Barikiwa mtumishi wa bwana, nabii Mwingira.
Yeye mbona anawaibia waumini wake sadaka pale kanisani kwake mwenge? Na yeye pia wakala wa ibilisi tu
 
Yeye mbona anawaibia waumini wake sadaka pale kanisani kwake mwenge? Na yeye pia wakala wa ibilisi tu

Haya sasa si ndiyo yale ya BBC na Mbowe gaidi, mara chighafla imekuwa kumbe kuligomba kuheshimiana?
 
Kweli kabisa utawala wa ibilisi joka kuu ulikuwa umelaanika na wa kishetani kabisa. Ule wizi wa kura wa kishamba ambao haukuwahi kutokea katika sayari ya tatu 2020, ni dalili tosha shetani alikuwa ametamalaki.

Tulipo ni pa kuunganisha nguvu kama vipi akiwamo hata yule aliyeko kwenye mfungo wa kumng'oa amaleki katika nchi 😁😁.
 
Back
Top Bottom