Rais Samia afanyiwa dua Maalumu ya kumuombea Visiwani Pemba

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,325
9,748
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa kutambua kazi kubwa na nzito inayofanywa na Rais Samia, Uchapa kazi wake wake,uzalendo wake,ukarimu na uungwana wake, unyenyekevu na kujitoa kwake kulibeba Taifa letu katika mabega yake imewasukuma na kuwashawishi wanawake visiwa pemba kumfanyia Dua maalumu ya kumuombea Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Maombi hayo yamefanyika katika uwanja wa Tibirizi ,ambapo picha mbalimbali zilizosambaa DUNIANI kwote kwa haraka sana kama upepo,zimemuonyesha Rais wetu kipenzi akiwa amekaa chini kwa unyenyekevu mkubwa sana bila kujali cheo na wadhifa mkubwa alio nao. Jambo ambalo limegusa hisia za watu wengi sana Dunia kwote ambao wameendelea kutoa maoni yao na kumpongeza sana Mama yetu kwa namna alivyo na moyo wa unyenyekevu na hofu ya Mungu.

Wengi wamesema waziwazi kuwa Rais Samia pamoja na madaraka yake makubwa kikatiba na kisheria lakini bado moyo wake umejaa unyenyekevu mkubwa sana , kwa kutambua kuwa yeye bado ni mwanadamu, bado anahitaji Maombi ya watanzania katika kumtia nguvu na kuomba msaada wa Mungu, bado anahitaji uwepo wa Mungu karibu yake kama nguzo yake na tumaini lake. Ndio maana Anaendelea kuwa mnyenyekevu na kujinyenyekeza mbele za Mwenyezi Mungu.

Ndio maana wanawake hawa kwa kutambua mzigo mkubwa na majukumu makubwa aliyonayo Mheshimiwa Rais wetu, wameamua wamfanyie Dua maalumu ya kumuombea, ili Mungu aendelee kuwa pamoja na Rais wetu, aendelee kumuongoza katika majukumu yake, aendelee kuweka mkono wake juu yake, aendelee kumpatia maarifa na njia ya kuliongoza Taifa, aendelee kumpatia nuru na mwanga katika njia alipitishalo Taifa letu, aendelee kuleta neema na baraka katika Taifa, aendelee kulijalia amani, utulivu, upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa.

Rai yangu watanzania wenzangu nawaombeni kwa pamoja na umoja wetu kila mmoja kwa imani yake na dini yake tuendelee kumuombea sana Rais wetu, tuendelee kupiga magoti kumlilia Mungu wetu aliye hai aendelee kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania. Rais wetu amejipambanua katika kuwatumikia watanzania muda na wakati wote kwa uzalendo.ndio maana tunamuona akifanya kazi hata siku za mapumziko. Tuitunze sana zawadi hii tuliyo nayo mikononi mwetu ,kwa kuwa watu aina ya Rais Samia huja Dunia na kupatikana kwa nadra sana na sio maeneo yote ambako unaweza kuwakuta.Mungu katupatia Rais Samia .tusimkatishe Tamaa Rais wetu bali tumtie Moyo na kumpa faraja na kutoa ushauri pale tunapoona inafaa na atatusikiliza kwa kuwa ni Mama msikivu sana tena sana .

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Unamuongeleaje yule jamaa na bendera ya CCM kwenye v8 akisafirisha wahamiaji haramu
 
Aloo, nasikia jana PM alikuwa kijijini kwake na kuwatembelea bodaboda, wafanya biashara wadogo na wauza kahawa (tamka gahawa)

Basi sawa !
Ni kawaida kwa viongozi wa CCM kwenda kujumuika na wananchi na kuwasikiliza kero na changamoto zao bila kujali ukubwa wa vyeo vyao. Ndio maana ikifika wakati wa uchaguzi CCM huungwa mkono sana na kupewa kura za ndio kwa kishindo
 
Wazee wa paris club
720x540.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom