Nabii Frank Julius Kiwalah ni nani?

Mtumia nguvu za Giza huyo,tapeli sana,anazunguka mikoan kuuza chumvi kwa bei ghali eti inaponya!wajinga ndio waliwao.
 
Don't judge you will be judged..! Huwa sihukumu watumishi wa Mungu maana walishaniponya kutoka kwenye marogo ya dunia na Nina tabia tu ya kuwa non-judgemental.

Nimeona na bango lake pale Posta kwamba atakuwa na Semina kubwa ya kuvuka Mwaka kuanzia tarehe 27 jijini Dar pale Boko Magengeni..nitahudhuria kusikiliza injili ya bwana.
Wewe ni kondoo, nenda kachinjwe. Maandiko yanasema, piga kelele usiache, uwaambie watu makosa yao.

Kumwambia mtu ni tapel, anayetumia jina la Yesu kujipatia mali, siyo kuhukumu. Ni kumtahadharisha aache Mungu hapendi.

Kuhukumu ni kama kusema, kesho utakufa. Hapo umehukumu.

Kumwambia mtu kosa lake ni jambo jema.

a713f9e5bfd76f60bcca07dfef644229.jpg
 
Simfahamu Nabii Frank lakini kuna dada mmoja alitoa ushuhuda kanisani jinsi alivyoponywa HIV kwa nguvu za Yesu, alikuwa mwathirika na jinsi alivyoathirika, mchungaji alimwambia kuna kitu katika mwili wako kinahitaji maombi, wakati anaendelea na maombi, roho ilimtuma kufanya full medical check up, majibu yametoka ni HIV+. Alianza dawa huku akiwa anaendelea na maombi, alijikita kwenye maombi, aliamka saa nane za usiku na Bible na kuomumba Mungu, anasema katika kipindi hicho alipata maono ya ajabu na alipata ujumbe wa kupokea total healing, hii ni katika Spiritual world.

Baada ya miezi sita anasema hali yake ilitengemaa akiendelea kutumia ARV's, baada ya mwaka mmoja CD4 zilikuwa juu sana na aliambiwa na Dr. aache kutumia ARV's kwanza kwa muda waangalie, aliacha ARV kwa miezi sita level ya CD4 ikiwa pale pale, baada ya mwaka walimwambia virus viko dormant lakini awe anachekiwa kila baada ya miezi sita.

Kwake yeye anaamini ni total healing amereceive, scientifically wanadai virus viko dormant. Imani yake imemponya na ninaamini katika jina la Yesu hakuna kisichoshindikana ukiwa na Imani.
huu ni uongo mtupu virus vya HIV vinakuwa dormant kwa muda kama unatumia ARV hata wasiokuwa na dini inawatokea hiyo
 
Don't judge you will be judged..! Huwa sihukumu watumishi wa Mungu maana walishaniponya kutoka kwenye marogo ya dunia na Nina tabia tu ya kuwa non-judgemental.

Nimeona na bango lake pale Posta kwamba atakuwa na Semina kubwa ya kuvuka Mwaka kuanzia tarehe 27 jijini Dar pale Boko Magengeni..nitahudhuria kusikiliza injili ya bwana.
Nani kakwambia ni mtumishi wa mungu huyo huo ndo ukosefu wa akili kitendo cha kumtambua MTU mtumishi wa mungu kimasialasiala namna ni laana
 
Lakini ukiacha kutumia ARV vinaactivate lakini kwa huyu dada vilibaki dormant.
amewadanganya kuna watu hata hizo ARV hawatumii na bado virus viko dormant.....inategemea na kinga ya mwili ya mtu..wengine white blood cell wanazo za kutosha sio rahis virus kuwa active hata kama hawatumii dawa....kuna jamaa ana HIV zaidi ya miaka 15 hatumii dawa na hajawahi kuugua hata homa.....miili inatofautiana nguvu.!!!!!
 
Leo wakati nawasha televisheni yangu ghafla nikakutana na kipindi chake cha uponyaji wa maradhi. Nimeona watu wakitoa shuhuda mbalimbali na wengine wakipokea uponyaji mbele ya camera, nikapata shauku ya kumfahamu huyu mtumishi ni nani maana inaonekana huduma zake si mchezo maana watu wanatoa shuhuda kupona maradhi wanayosema kwamba walishindwa kutibiwa hospitalini.
Ukitaka kujua hawa n wapiga deal mara nyingi wanahubiri kafanikio tu, hawahubiri juu ya watu kuacha dhambi na kumtii Mungu. Wanahubiri utajiri, kuponya magonjwa n.k
 
Mwizi tu, mhuni m1 anayewaibia wananchi mazezeta kwa kupitia maigizo yake hayo. Ni muhuni tu huyo hana Mungu huyo.
Tatizo serikali nyingi za kijinga ujinga zinaacha wananchi wake kuibiwa na matapeli wa kidini na kufilisiwa wezi na mafisadi wa kidini wanaishi kwa mgongo wa chama cha CCM na serikali yake wananchi wanaumizwa serikali zinaangalia tu azichukui hatua hata kukemea na kuonya zinashindwa tulisilia siku za nyuma viongozi wa makanisa ni wafanya biashara wa madawa ya kulevya najuzi magu alijidai kushugulikia madawa ya kulevya hadi leo atusikii chochote kinacho endelea policcm wana fanya kazi ya kuwasumbua wapinzani na vyombo vya habari kama jf kwa kutumia kivuli cha mahakama huku waalifu alisi wamefumbiwa macho zipowapi harakati za kuzuia madawa yakulevya zipowapi harakati za kupambana na mafisadi zikowapi harakati za kufuta mikataba michafu ya madini wakowapi mafisadi jela au walio nyongwa???? total stupid manki
 
Anajenga boonge la kanisa Pongwe Tanga
Utalaaniwa wewe!!!!! Usiseme anajenga kanisa utakuwa sawa na wanao mwita mtume na nabii sema anajenga kitega uchumi tanga cha wadanganyika
 
Leo wakati nawasha televisheni yangu ghafla nikakutana na kipindi chake cha uponyaji wa maradhi. Nimeona watu wakitoa shuhuda mbalimbali na wengine wakipokea uponyaji mbele ya camera, nikapata shauku ya kumfahamu huyu mtumishi ni nani maana inaonekana huduma zake si mchezo maana watu wanatoa shuhuda kupona maradhi wanayosema kwamba walishindwa kutibiwa hospitalini.
Kwani we umefika leo nchini mkuu? Mbona hizi mambo si news kabisa!
 
Don't judge you will be judged..! Huwa sihukumu watumishi wa Mungu maana walishaniponya kutoka kwenye marogo ya dunia na Nina tabia tu ya kuwa non-judgemental.

Nimeona na bango lake pale Posta kwamba atakuwa na Semina kubwa ya kuvuka Mwaka kuanzia tarehe 27 jijini Dar pale Boko Magengeni..nitahudhuria kusikiliza injili ya bwana.
Mkuu huu Urogo wa dunia ndo ugonjwa gani? Unafanana na HIV? Nahisi hichi ndo kinachoumiza watu vichwa (kupona HIV, Cancer etc.)-i.e Magonjwa yanayopimika hospitalini
 
Leo wakati nawasha televisheni yangu ghafla nikakutana na kipindi chake cha uponyaji wa maradhi. Nimeona watu wakitoa shuhuda mbalimbali na wengine wakipokea uponyaji mbele ya camera, nikapata shauku ya kumfahamu huyu mtumishi ni nani maana inaonekana huduma zake si mchezo maana watu wanatoa shuhuda kupona maradhi wanayosema kwamba walishindwa kutibiwa hospitalini.
Timu ya promosheni kazini. Ongezeni bidii wapumbavu wapo wa kumwaga kazi kwenu.
 
Nabii Frank Julius Kilawa nilishawahi kuhudhuria baadhi ya makongamano yake Ila nilichoona kutoka kwake ni kwamba mara nyingi anaponyesha watu wenye magonjwa kama Ukimwi,Kisukari ,Cancer pamoja na Magonjwa ya uzazi(ugumba).Kwanini nimetaja hayo? Nikwasababu hao ndio niliowashuhudia kwa masikio na macho yangu,Nilishawahi kwenda na ndugu yangu alikuwa na tatizo la miguu kufa ganzi(Paralysis) alifanikiwa kupata huduma lakini tatizo lake halikuisha.
 
Back
Top Bottom