Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani. Je, Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,582
Wanabodi,

Kila nipatapo nafasi, huwa naandika makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", makala hizi huwa zinachapishwa na magazeti mbalimbali, hivyo Wahariri kuweni free kuitumia makala yangu yoyote, na be free kui edit kwa kiwango chochote utakacho ona inafaa, maana hata mimi sitaki tena kuandika makala yoyote ya kuliponza gazeti lolote au Wahariri wake waitwe Dodoma au popote kuhojiwa na taasisi yoyote ikiwemo Kamati ya Bunge kwasababu za makala za Paskali Mayalla zenye kuhoji mambo magumu.

Makala zangu zote huandikwa kwa mtindo wa swali au maswali, kisha naweka hoja zangu, na kumalizia kwa lile lile swali, ili msomaji awe huru kusoma, kuelewa na kupata majibu mwenyewe, hivyo sitegemei tena kuitwa popote kuhojiwa na yeyote kuhusu maswali yangu ninayo hoji, ila ikitokea mtu yoyote una majibu yoyote, kuhusu swali langu lolote, ni ruksa kutoa majibu, (mfano lile swali nililouliza Je Bunge Linajipendekeza Kwa Serikali?, jibu lake lilikuwa rahisi tuu, "Bunge Halijipendekezi kwa Serikali).

Ile ule mtindo wangu wa kuuliza maswali magumu kwa viongozi, kwenye press conferences zao, au kwenye vipindi vyangu, bado unaendelea, natoa wito kwa viongozi wetu, msiogope maswali magumu ya waandishi wahojaji, na hata ikitokea ukaulizwa maswali magumu, na ukitokea huna jibu, uko free kutokujibu, uko free kunyamaza, au hata kumjibu mwandishi kitu kingine chochote tofauti na swali uliloulizwa.
( mfano, Swali: " Mkuu kiongozi, vipi kuhusu hili la...
Jibu: "Mayalla kwa kikwetu maana yake ni njaa)
Ni ni jibu tosha na sitauliza zaidi.

(By the way: siku ya Jumamosi ya kesho kutwa asubuhi kwenye kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari cha Star TV, nitakuwa live na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulie kwa Dar es Salaam, Dodoma atakuwepo Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, na Mwanza nguli Dotto Emanuel Bulendu kuizungungumzia Corona, huko ni maswali magumu, hakuna maswali rahisi)

Kwavile Corona ndio habari ya mjini duniani kote kwa sasa, mada yangu ya leo ya "Kwa Maslahi ya Taifa" pia itajikita mumo humo kwa kwa swali hili..."Kwa nini Nabii huwa hakubaliki nyumbani?!. Jee Rais Magufulini ni Nabii wa Mungu au ni mtu tuu wa kawaida?".

Nabii ni Nani?
. Nabii ni binaadamu au mtu yoyote anayeletwa duniani na Mungu kwa ajili ya kutimiza majukumu fulani. Nabii ni mtu mwenye maono fulani, kwa kesema maneno ya unabii yanayokuja kutokea au kutimia. Maona hayo huonyeshwa na Mungu kwa ajili ya kufanya kazi fulani ya Mungu, mfano wa Manabii ni kama Adam na Eva/Hawa, Ibrahimu, Mussa, etc. Tuna viongozi wengi wa dunia walioteuliwa na Mungu kama manabii akiwemo Mwalimu Nyerere.
Hata humu jf, tunao manabii kibao
TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums
(P'se Tofautisha Nabii na Mtume wa Mwenyeezi Mungu. Sijasema Magufuli ni Mtume, nimeuliza Magufuli ni Nabii?).

Maswali hayo yanafuatia, wakati kuna baadhi ya sisi Watanzania tunambeza rais Magufuli na serikali yake kwa baadhi ya hatua anazochukua kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili na kulikabili taifa letu, za kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo changamoto hii mpya ya ugonjwa wa Corona, kuna baadhi yetu sisi Watanzania, tunambeza!. Wakati sisi tuna beza, kuna baadhi ya wenzetu wa bara la Africa wao wanamlilia rais Magufuli wakitamani rais Magufuli ndio awe rais wao kwa hatua ambazo rais Magufuli amezitumia kwa Tanzania kupambana na janga la ugonjwa wa Corona, zilizopelekea nchi ya Tanzania kuwa ni nchi ya kupigiwa mfano, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kutamani juhudi za kupambana na Corona kwa bara lote zima la Africa ziunganishe kujenga nguvu ya pamoja kupambana na janga la Corona na kutamani rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndie ateuliwe kwa kauli moja kuwa Kamanda Mkuu wa Bara la Africa katika kuongoza Mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa Corona kwa bara lote zima la Africa!. Wakati sisi huku tunabeza, hatuoni, hatutambui, hatuthamini thamani ya Magufuli tuliye nae, wenzetu wasie nae, wanamtamani, wanamthamini, wana muhitaji, sasa nauliza, huyu Magufuli ni mtu tuu wa kawaida au ni Nabii wa kweli wa Mungu aliyeletwa kwa Tanzania kwa ajili ya kutuokoa na kutukomboa?.

Tukiangalia kilichotokea China, kinachotokea Marekani, Utaly na nchi za ulaya, halafu tukiangalia jinsi nchi za Africa wakiwemo nchi majirani zetu wanavyo panic na kufanya lockdown, huku Rais Magufuli akiwaongoza Watanzania kwa kuwasisitiza tuzingatie ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga kwa kuzingatia usafi, kupunguza mikusanyiko, kuweka social distancing lakini oia kuwaambia Watanzania, Tusitishane, na Tusitishwe, kwa kinachotokea nchi nyingine, sisi tuendelee kuchapa kazi kama kawaida na Tumtegemee Mungu,

Msimamo huu wa rais Magufuli na Tanzania tunavyo deal na Corona, unaonekana kama tunacheza au tunatania kwa jambo serious kama hili.

Baada ya rais Magufuli kulihutubia taifa kuhusu Corona na kusisitiza tusitishwe, kesho yake akaonekana aki relax kwenye majabali ya Ikulu ya Chamwino, Ma critics wa Magufuli wakamuona kama mtu ambaye sio serious na hajui atendalo, walitaka atishike, agope, ababaike na kuwatisha Watanzania, hao critics kazi yao ni kubeza na kuponda kila kitu, as if waliombea hali kama ya China, Italy na Marekani ndio itokee Tanzania ili Magufuli ambuke kwa kutochukua hatua kali za tahadhari, kama majirani zetu.

Leo baada ya usingizi kukata, usiku mkubwa, katika pita pita yangu na mitandaoni nikakutana na hii kitu

The Good, the Bad and the Worse in Africa’s Anti Corona Crusades; Lesson from Tanzania - JamiiForums
April 09, 2020
By John Njoroge, Africa54, SA.

The anti Covid-19 crusade(s) in Africa is yet again bringing into perspective diverse leadership from the Continent that is known for its strong immunity after countless years fighting known and unknown diseases. It worths our while to put Covid-19 into scrutiny.

Globally, as positive cases hit the 1 million mark this week, countries in Africa are on the front fighting the Corona malade from different viewpoints and strategies. The 54 countries Continent has a merely 9,000 plus positive Corona cases and not more than 500 deaths (compare with 78,000 deaths world wide).

It will be up to scholars to empirically verify and confirm which are the best strategies to handle Corona globally and in Africa, but we are already able to see the good, the bad and the worse in our Continent.

Two major schools of thought are emerging; the anxity model and the elasticity model.

Whereas the former focuses on a panic than a culculated fierce fight on the noval virus, the later involves some forms of resilience, choosing between fighting aggressively with the Corona and ensuring that there is life after Corona; maintaining the fundamentals of cohesion on the economic nd social set up.

China is known for its elasticity in fighting the Corona; they did not panic, it was deadly and noval virus to them but they chose their methods and tacticts in a way that retained the strength of their society. Today they remain stronger, together.

If it is to adopt and imitate western terminologies, the Chinese people would have locked down everything, curfew every street to the detriment of their own social bond. No, they maintained vigilance.

As a Kenyan, I love my counry, but I adore the Tanzania President, Dr. John Magufuli, who is adopting the Chinese "never panic mode," something that goes contrary to his fellows in the region. Compare: Uganda, Kenya and Rwanda.

President Magufuli, to my recollection, has thus far spent more than 3 speeches to warn Tanzanians on how deadly is Corona, encouraged them to take precautions and later on addressed the nation to augur well his point of view that Corona is deadly so should everyone work to prevent further spreads.

However, the Presdent went on to warn Tanzanians that the war on Corona should not be an excuse for hard work and it should not operate as a reason to "quarantine" the whole country and paralyze everything.

People have been encouraged to wash hands, sanitize, maintain social distance, avoid unnecessary gathering but must go to work in farms, industries, offices or personal businesses. I love this spirit. It is was supposed to be an Afrian spirit.

Dispite some misinterpretation to this approach, and contrary to his panicked peers, on the ground, Magufuli's government is taking Corona seriously; schools and colleges have been closed, sports and other social gatherings have been halted, 14 days quarantine for foreign arrivals imposed, national level committees are in place and research on cure are on. Nevertheless, the country is calm.

To the contrary, his counterparts in Kenya and Uganda and Rwanda, just like here in South Africa, are in anxity model; they shut down everything-borders, work and public outings.

Lockdowns have been imposed, curfews are on, people who get out of their homes are beaten (some to death) and salaries are forcefully cut. Just wondering, why is all this panic!

Kenyan police dragging a man who disobeyed a Covid-19 curfew in Nairobi.
Rwanda in particular, in a move that African country's must excercise prudence, has already secured a costly World Bank loan.

The branded as "Corona Response financial facility" package, essentially comprises of a modest grant but a huge loan facility in it that is attached with conditionalities.

I warn African countries to relax on their approaches but be firm in tackling Corona. They should not panic and find themself into a pending economic recession or debt trap.

We have already seen thousands here in South Africa flocking the streets as the stay-home-lockdown does not work for them; in Kenya a bodaboda cyclist has been attacked and killed by security organs as he returns from sending a pregnant woman to a local hospital. Africa why?

Africa my mother land, you have tackled malaria, typhoid, cholera and the deadly ebola with your usual ubuntu (strongness, togetherness and in a communal way), why do you fail on the Corona?
Kumbe huku sisi Tanzania, tunamponda rais Magufuli anavyo deal na Corona, kumbe kuna wenzetu wanamtaka Rais Magufuli ndio awe rais wa Africa kwa kuongoza mapambano ya Corona the African Way, na Kuichulia nchi ya Tanzania iwe ndio nchi ya mfano wa mapambano haya kwa nchi nyingine kuiga hiki rais Magufuli alichokifanya, na jinsi Tanzania inavyo pambana na janga la Corona.

Hongera Sana rais wetu Magufuli, na serikali yako kwa hatua mnazochukua dhidi ya janga hili la ugonjwa wa Corona, ama kweli inawezekana kabisa wewe ukawa ni Nabii wa kweli kwa taifa letu Tanzania ambaye tumepewa na Mungu mwenyewe, kwa sababu Mungu aliyajua yote haya kuwa yatatokea kabla, hata hayajatokea na akatupatia mtu sahihi wa kutuvusha kwenye majaribu haya.

Ama kweli Nabii huwa hakubaliki nyumbani, kuna akina sisi Matomaso wa Tanzania, na humu JF tuna Matomaso wengi, ambao tulimbeza sana Magufuli, tangu ile 2014 wakati unabii wa Magufuli ulipowekwa humu
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums

Lakini as times goes by baadhi ya maneno ya unabii ule yanakwenda yakifutika ila kuna mengine yanatimia moja baada ya jingine.

Hivyo inawezekana kabisa huyu Rais Magufuli ni mpango wa kweli wa Mungu kwa Tanzania?, Huyu ni mtu tuu au ni Nabii?. Mungu akisema YES, who would dare kusema No?!.

Kwenye hili vita ya Corona, Watanzania, tuweke tofauti zetu pembeni, tujiunge na rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake katika Mapambano dhidi ya janga hili la ugonjwa wa Corona, Together we can.

Mungu Mbariki Magufuli
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Africa
Nawatakia Alhamisi Kuu Njema.
Paskali
Update
Wanabodi, hili ni bandiko la swali kuhusu rais Magufuli kama jee ni Nabii?. Naomba mimi nisijibu,
msikilize Mhe. Dr. Mwigulu Nchemba wewe mwenyewe umsikie amesema nini kumhusu Rais Magufuli



P

Rejea za Paskali on Unabii.
  1. TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums
  2. Unaitwa nabii, nawe unachekelea? hatari sasa! - JamiiForums
  3. Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba! - JamiiForums
  4. https://www.jamiiforums.com/threads...asiabudiwe-asiogopwe-bali-aheshimiwe.1023305/
  5. Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba! - JamiiForums
  6. Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais... - JamiiForums
  7. "Nabii Kamuambukiza Mke wangu STD" - JamiiForums
  8. Mauaji ya Kisiasa, hali ngumu ya Uchumi na Utabiri wa TB Joshua juu ya hatima ya Tanzania - JamiiForums
  9. Pongezi Jeshi la Polisi. Japo Nabii hakubaliki nyumbani, Jeshi sasa ni Sikivu, Most friendly na very hospitable - JamiiForums
  10. Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani!, JK Ameanza Kukubalika?!. Watch ITV Leo Saa 3:45 Usiku Huu! - JamiiForums
  11. Nyakua Nyakitita: Mhadhiri DIT anayeokota makopo barabarani - JamiiForums
  12. Nabii Flora wa Mbezi Beach - JamiiForums
  13. TCRA: Vipindi vya Mahubiri Kwenye TV Pia Viangaziwe/Vithibitiwe!. Mungu Yupo Ila pia Shetani Yupo! - JamiiForums
  14. Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!. - JamiiForums
  15. Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo? - JamiiForums
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
 
Korona ilikuwepo tokea mwaka jana mimi nipo nafanya kazi na makaburu pamoja na wa australia kibao,kilicho tokea miongoni mwetu tunakijua mwanzoni mwa january na february,wanaopanic sasa waendelee kupaniki, the president is well informed ,believe this,hata wizara husika inalijua hili.nafikiri hata humu uzi umo nafikiri wa feb.23 watu walilalamika sana kupata mafua yasiyo ya kawaida.
 
Korona ilikuwepo tokea mwaka jana mimi nipo nafanya kazi na makaburu pamoja na wa australia kibao,kilicho tokea miongoni mwetu tunakijua mwanzoni mwa january na february,wanaopanic sasa waendelee kupaniki,the president is well informed ,believe this,hata wizara husika inalijua hili.nafikiri hata humu uzi umo nafikiri wa feb.23 watu walilalamika sana kupata mafua yasiyo ya kawaida.


Umeongea sahihi kabisa
 
Umeongea sahihi kabisa
mimi binafsi katika kipindi hicho karibu nimpoteze Mama alizidiwa na mafua na kikohozi,alikula dawa za hospitali,sauti iligoma kutoka mpaka hata kuongea na simu ilikuwa shida,ametumia sana majani pori na ilimchukua mda kupona,alibanwa kifua wewe acha.

Hapa kazini kati ya wafanyakazi kumi saba walikuwa wanakohoa na mafua makali,tulikuwa na vikohozi visivyosikia antibiotics,mpaka ikafika hatua ya kupimwa kifua kikuu na kufanyiwa XRAY,lakini tulivuka salama.Wengine walioyachoka maumivu ya mafua,na vikohozi walianza kula pombe kali na hata ukiwauliza ni dawa gani iliwaponyesha hawawezi kukutajia dawa.It passed over.
 
Korona ilikuwepo tokea mwaka jana mimi nipo nafanya kazi na makaburu pamoja na wa australia kibao,kilicho tokea miongoni mwetu tunakijua mwanzoni mwa january na february,wanaopanic sasa waendelee kupaniki,the president is well informed ,believe this,hata wizara husika inalijua hili.nafikiri hata humu uzi umo nafikiri wa feb.23 watu walilalamika sana kupata mafua yasiyo ya kawaida.

That’s very true sema umekosea kidogo Coronavirus ilikuwepo tangu mwaka jana mwanzoni na ilipamba moto November na December.

Hata Serekali inapotoa matamko kuhusiana na huu ugonjwa yamkini inajua wazi hatari iliyopo na iliyokuwepo.
 
Kumbe huku sisi Tanzania, tunamponda rais Magufuli anavyo deal na Corona, kumbe kuna wenzetu wanamtaka Rais Magufuli ndio awe rais wa Africa kwa kuongoza mapambano ya Corona the African Way, na Kuichulia nchi ya Tanzania iwe ndio nchi ya mfano wa mapambano haya kwa nchi nyingine kuiga hiki rais Magufuli alichokifanya, na jinsi Tanzania inavyo pambana na janga la Corona.
Hakuna lolote, the worst has to come yet! Time is ticking!
 
Bro serikali nyingi sasa hivi wakati sis tukielimishana juu ya kujikinga na janga hili wao pia wamefanya haya Lakin wameenda mbali zaidi kwa serikali zao kuweka funds kwenye makampuni yaliomo nchini mwao yasianguke..SERKALI zngne zmefka mbali kwa kupunguza kodi ktk biashara mbalimbali ili kuweza kulea ama kulinda ajira za watu wao!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom