Nabii Frank Julius Kiwalah ni nani?

Nabii Frank Julius Kiwalah ni nani?

Kinachoponya ni power from within, nguvu za uungu tulizonazo ndani yetu, hata wewe unawezafanya mirracles! kufanya, ni namna ya kujua namna ya kufungua hizo nguvu.
 
Ni kweli huenda watu wanaponywa ila hawa manabii na mitume
99.9% ni waongo WANATUMIA MWAVULI WA JINA LA YESU hali ya kuwa wao ni waganga wa kienyeji
Hata Yesu alipotoa mapepo walisema anatumia zerbebuli (yule mkuu wa mapepo) sishangai kuona Hata we ukikosoa
 
Tafuta maana ya mpiga dili! Au wewe ndiye yeye? Nimekuchoma!
Haya umepona kapime ukimwi umepona- stupid! HIV virus anaondoka mwilini kwa kuguswa, stupid, kuwadanganya masikini wagonjwa!

Simfahamu Nabii Frank lakini kuna dada mmoja alitoa ushuhuda kanisani jinsi alivyoponywa HIV kwa nguvu za Yesu, alikuwa mwathirika na jinsi alivyoathirika, mchungaji alimwambia kuna kitu katika mwili wako kinahitaji maombi, wakati anaendelea na maombi, roho ilimtuma kufanya full medical check up, majibu yametoka ni HIV+. Alianza dawa huku akiwa anaendelea na maombi, alijikita kwenye maombi, aliamka saa nane za usiku na Bible na kuomumba Mungu, anasema katika kipindi hicho alipata maono ya ajabu na alipata ujumbe wa kupokea total healing, hii ni katika Spiritual world.

Baada ya miezi sita anasema hali yake ilitengemaa akiendelea kutumia ARV's, baada ya mwaka mmoja CD4 zilikuwa juu sana na aliambiwa na Dr. aache kutumia ARV's kwanza kwa muda waangalie, aliacha ARV kwa miezi sita level ya CD4 ikiwa pale pale, baada ya mwaka walimwambia virus viko dormant lakini awe anachekiwa kila baada ya miezi sita.

Kwake yeye anaamini ni total healing amereceive, scientifically wanadai virus viko dormant. Imani yake imemponya na ninaamini katika jina la Yesu hakuna kisichoshindikana ukiwa na Imani.
 
Masikini wagonjwa wana shida ya kuumwa. Ukimwambia lolote atakusikia maana anatafuta kupona. Maumivu ya ugonjwa. Anakutana na tapeli Kilawallah!
Sasa hapo ametapeliwa vipi?
Mkuu Siku ukija kuumwa ndio utajua kua Mungu yupo
 
1 .Miujiza ya Mungu, hutusogeza katika kumtumikia Yesu Kristo na kushika maagizo yake, na kutufanya kuwa watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Miujiza yoyote inayoambatana na maagizo yoyote yaliyo kinyume na Neno la Mungu, kama kutumia sanamu za watakatifu, kufukiza uvumba, kutumia rozari au maji ya Baraka, kuzuru makaburi, kuwaomba wafu tuwaombee n.k; haitokani na Mungu (KUMBUKUMBU 13:1-4).Mafundisho ya mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, hutufundisha kuwa watakatifu, na kuwa mbali na mapenzi ya Mataifa. Wote waliotumiwa sana na Mungu kufanya miujiza kama Paulo, Petro, Yakobo na Yohana, walifundisha hivyo (WARUMI 12:1-2; 1YOHANA 2:15-17; 1 PETRO 1:14-16; 2:12; 4:2-3; YAKOBO 4:4; 1 WAKORINTHO 4:3-4).

2. Miujiza ya Mungu hutolewa bure, hainunuliwi (MATHAYO 10:8; 2 WAFALME 5:14-16; DANIELI 5:16-17; 1 WAFALME 13:6-8; MATENDO 8:18-20). Namna yoyote ya kuomba hela ili kununua muujiza ni kinyume na mpango wa Mungu .Hata kama tutaona wakiuza vitambaa,leso na sabuni zilizoombewa ili zitusaidie, hatuna budi kujua mapanzi ya Mungu kwa watumishi wake ni kutoa huduma ya maombezi bure. Huduma yoyote inayochangisha mchango au kiingilio kwa ajili ya semina ya Neno la Mungu hiyo siyo huduma ya kimungu, ni huduma ya Shetani. Mungu anataka injili iwafikie watu wote.Mfano 1 wa huduma ya shetani ni huduma ya babu wa Loliondo. Bila kutoa sh: 500 usingeweza kupata msaada.Pia miujiza ya Mungu inatokana na Neno la Mungu kama tulivyoona hapo juu. Miujiza ya Mungu inakuwa na lengo la kuwaleta watu kwa Yesu.Watu wanaokuja kutafuta msaada kwa Yesu sharti waongozwe kutubu dhambi zao

kwanza ili kuwapatanisha na Mungu kwa ajili ya kufungua mlangio wa Miujiza yao.

3. Miujiza ya Mungu humtukuza mwana wa , Yesu kristo (YOHANA 11:4), wale wanaotumiwa na Mungu kufanya miujiza ya Mungu hubaki wanadamu na wao kukiri hivyo, na kumpa Mungu utukufu(MATENDO 14:8-18). Tunapomuona mtu akichukua utukufu kana kwa mba yeye ndiye anayetenda miujiza ndipo tunatambua kuwa huyo si mtumishi wa Mungu.

Maisha ya mtu anyetumiwa na Mungu kufanya miujiza yanapaswa kuwa sawasawa na Neno la Mungu. Watu wanaotumiwa na Shetani kufanya miujiza, huambatana na dhambi NNE zinazoonekana upesi-uzinzi au uasherati (1 WAKORINTHO 6:15-17), maneno ya kihuni (YAKOBO 3:10-12), maisha yaliyo sawa na mataifa katika kuvaa na kutenda (WARUMI 12:2; 1 PETRO 2:12; YAKOBO 4:4), maisha yasiyo na uaminifu katika masuala ya fedha na kusema uongo (NEHEMIA 7:2)

HUKUMU YA WATUMISHI WA SHETANI

Watumishi wanaotumiwa kufanya miujiza ya mashetani, mahali pao ni katika ziwa la moto (UFUNUO 19:20; KUMBUKUMBU 13:1-5; MATHAYO 7:22-23. Baada ya kuwa tumefahamu; ni wajibu wetu kujihadhari nao na kuwa mbali na mafundisho yao (MATHAYO 7:15-17; WARUMI 16:17).Mungu akuongoze kufanya maamuzi mazuri katika kuchagua mahali pa kuabudia (dhehebu au kanisa), maana kufanya makosav katika kuchagua mahali pa kulishwa NENO LA MUNGU kunaweza kukugharimu milele. Tafuta mahali ambapo utaelezwa kweli yote bila kufarijiwa kunyume na maandiko.
 
Nyakati tulizonazo leo,zinzitwa NYAKATI ZA HATARI..Biblia inasema kwamba siku hizi za mwisho,wengine watajitenga na imani,wakisikiliza ROHO ZIDANGANYAZO na MAFUNDISHO YA MASHETANI (2TIMOTHEO 3:1,1TIMOTHEO 4:1).Roho zidanganyazo zitafanya kila namna,kutudanganya,ili kile cha Mungu tukiite cha shetani,na kile kilicho cha shetani,tukiite cha Mungu.Leo,tunazungukwa na watu wanaosema,jihadhari usiende kule.Ingawa kuna miujiza mingi huko,miujiza hiyo,inatokana na ROHO CHAFU au MASHETANI.Mtu yule,anatoa pepo kwa kutumia DAWA au HIRIZI.Kutokana na mambo yake ya ushirikina,mtu akienda kumsikiliza mara moja tu,yeye naye ananyweshwa roho chafu na kudanganyika.Maneno haya,yanaweza yakawa ya kweli au yasiwe ya ukweli.Pasipokuwa na mafundisho,hatuwezi kupambanua kilicho cha Mungu na kilicho cha Shetani.Pasipo kuoambanua,tunaweza tukamwita mtu wa Mungu kuwa ni PEPO na kwamba anatoa pepo kwa BEELZEBULI,mkuu wa pepo,kwasababu tu HAFUATANI NASI (YOHANA 8:48-49; MATHAYO 12:22-24;LUKA 9:49-50).Mambo haya,hayapaswi kuwa hivi
 
Wewe kama unamfahamu tiririka watu wamjue, hakuna sababu ya kusema ni mpiga dili halafu hutaki kusema namna anavyopiga dili. Huenda unachosema ni kweli maana nimeona namba za mitandao na akaunti za benki kwa ajili ya kuchangia huduma zake lakini vipi ikiwa watu wanaopitia kwake wanapata uponyaji?
Kinachomshinda kwenda Muhimbili kuombea Wagonjwa wengine hata kujigeuza hawawezi sembuse kunyanyuka kumfuata ukumbini ni kipi?
 
Kinachoponya ni power from within, nguvu za uungu tulizonazo ndani yetu, hata wewe unawezafanya mirracles! kufanya, ni namna ya kujua namna ya kufungua hizo nguvu.

Tatizo hatuna imani kuwa mungu anatosha kumuomba mpaka tupitie kwa watu watuombee ndio hapa opportunist wanapiga hela
 
Manabii tu na mitume ndo hawaendi waumini wengine wanapita siku maalum wodi baada ya wodi kuombea wagonjwa mimi binafsi nishakutana nao
Kwa wana Legion of Mary, tunatakiwa kuwatembelea wagonjwa na kama wanahitaji sacrament ya maungamo kumfahamisha padre, pia ikiwezekana kuwachukulia vifaa vidogo vya kuwasaidia.
 
Wewe kama unamfahamu tiririka watu wamjue, hakuna sababu ya kusema ni mpiga dili halafu hutaki kusema namna anavyopiga dili. Huenda unachosema ni kweli maana nimeona namba za mitandao na akaunti za benki kwa ajili ya kuchangia huduma zake lakini vipi ikiwa watu wanaopitia kwake wanapata uponyaji?
Ukitaka kujifunze na kuwajua wapiga dili kwa jina la Yesu,jaribu kuwa unapitia tovuti ya Kikristo ya mwanzonews.com kuna uchambuzi wa kina sana kuhusu haya mambo mkuu! Uponyaji ni dhana ambayo imevuruga watu sana!
 
huyu jamaa anaponya 100% naaamini alimponya mdogo wangu alikua na kifafa ila sipendi watu wanavyomuabudu kanisani kwake akiingia wote mnampigia magoti hilo halikunifurahisha ila kwasababu nlikua na shida nlipiga na dogo akapona
Kwani si hata kwa waganga wa kienyeji kuna watu wanaponywa? Kupona sio issue, hata kidogo!
 
Cc Mshana Jr

Atufafanulie namna teknolojia ya kinabii inavyofanya kazi
 
Back
Top Bottom