Kuhani Musa Richard Mwacha ni nani?

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
18,007
30,919
Imani ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu; ni ile hali ya akili ya mtu kupokea ukweli uliofunuliwa na Mungu akiambatanisha nafsi yake kwa Mungu.

Kuhani Musa Richard Mwacha amejulikana kama mtumishi wa Mungu mwenye imani kwa Kristo. Na amekua na huduma yake katika jiji la Dar es salaam kwa miaka michache sasa.

Ukifuatilia ni muda mfupi tangu aanze huduma ila utakutana na mambo mengi sana na kati ya hayo mengi ni style ya mahubiri yake, miujiza na maajabu kwenye ibada zake na idadi kubwa ya waumini alionao ndani ya muda mfupi sana maana miaka 3 au mi4 bado huduma ni changa.

Watu wengi tunajiuliza mengi sana juu ya mtumishi huyu. Wengi wetu hatuamini kama yanayonekana kuotokea ni ya kweli lakini pia wapo wanaoamini ni kweli.

ILA SWALI MOJA LA MSINGI "KUHANI MUSA NI NANI HASWA?

Shuhuda zimetolewa hadharani, na ni shuhuda zinazodhihirisha mambo magumu kufikirika katika hali ya kawaida. Ila hawa walioshuhudia wapo kati yetu, mtaani kwetu hata majumbani kwetu, kigoma, chato, kilimanjaro, sumbawanga, kagera, Dar es salaam mmetisha sana. Wenyeji wa huko mnasemaje kuhusu Kuhani Musa?

Fred William Rwegasira.

Mr Rwegasira ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera, Bukoba kule, Mkazi wa Salasala - Dar es salaam. Na sasa anaishi kimara


Innocent Carol Paulo

Innocent Carol Paulo ni mzaliwa wa Chato. Na mkazi wa Tabata - Dar es salaam


Levina Lyamuya na mdogo wake

Levina ni mwenyeji wa Kilema, Moshi- Kilimanjaro

Malkia


Wakorinto
KUHANI MUSA RICHARD MWACHA NI NANI??
[/QUOTE]Sumbawanga mtoto afufuka
ttps://youtu.be/PHUUbiYOEBY


CancerBaada ya siku2Baada ya miezi 2
Mimi naamini kuna kuponywa na kufufuliwa kwa mtu/watu ikiwa anayeomba anamwamini Mungu na Mungu amempa karama ya uponyaji.

Walishafufuka wengi kabla na baada ya kuja Yesu Kristo.

Nimekuelewa sana. Ufufuo upo na uponyaji upo

mamad 3/4 ya mahubiri yake ni vita yake na wachawi na majini, kwa kutumia vifungu vya kuogofya toka agano la kale na ufunuo
Kwa sisi tulio kuwa naye Arusha kabla ya fani yake ya Sasa tunakumbuka aliwahi kupata matatizo ya afya ya akili na alipopata ahueni alidai alirogwa kwa kutupiwa jini
Kingine Google falsafa ya Freemansory ulinganishe na vita yake akitumia maskini tena wengine wa kike wakijiita ma malkia wa Freemasons
Cha kusikitisha anatumia watoto wadogo kudai wanaua mpaka watu mia na kula nyama za maiti ( upuuzi mtupu)

Babu Ochu; mimi, wewe, huyo malkia wa freemason sote ni watanzania. Kila kitu kiko wazi upande wa Kuhani Musa tena vipo online hapo.

Sasa nadhani ili kuuthubitishia umma kwamba huo ni upuuzi kama unavyosema lazima uthibitishe kwamba hizo shuhuda ni za uongo. Hivi vitu havihitaji hata hasira vinahitaji tuu kuthibitishwa

Kuhusu matumizi ya biblia vifungu vya kuogofya vya ufunuo na agano la kale sioni kama vinaogofya kuliko matendo yanayofanyika na wanadamu wa leo, na wala hauna kipande cha maandiko matakatifu kisichotakiwa kutumika

Zaidi ya yote ili neno liweze kuwasaidia watu lazima lihubiriwe kwa nyakati na mazingira waliyomo na wanayoishiMimi nimepona kupitia maombezi na mahubiri yake na sijachargiwa hata senti. Issue hii Iko kiimani zaidi na cha muhimu wenye shida wanaenda wenyewe. Kama utaniita mjinga Kwa kuwa nimeenda Kwa Kuhani Mussa haina shida.Sijavunja Sheria yoyote ya Nchi na hayajakufika.

Siruhusu MTU yoyote akubaliane na Mimi lakini hili ni Jambo lililonitokea Nina miezi miwili nasali pale hata sijaenda kushuhudia bado.Sina MTU/ kiongozi ninaemfahamu pale baada ya kuumwa muda mrefu nilimshirikisha Rafiki yangu Yuko Mkoani,na matatizo mengine ya binafsi akaniambia niende pale. Kwanza lazima nikiri SIJAWAHI kusali kwenye haya Makanisa sababu sikuwa NAYAAMINI. Baada ya kwenda pale hata ugonjwa uliokuwa unanisumbua Kwa miaka 12 UMEYEYUKA. Ndio maana nasema IMANI Kwanza Mimi yamenitokea na siwezi kunyamaza hata nikiitwa mjinga cha muhimu NIMEPONA.


'WATU' wakija kuamka tayari jamaa hawahitaji tena, ... na huenda akawa hata mbunge! 😅
mama D ameshakula fweza ya promo! ... KALAGA BAHO
..!

Kwanini tunaongea maneno mengi ya kukataa bila kusema hayo anaayofanya yapo au hayapo?

Turudi kwenye maada, tuje na shuhuda kwamba yanayotendeka pale ni ya uongo au ni ya ukweli kwa maslahi makubwa ya umma


Kuna hoja mbili ambazo kwenye mada kama hii zinapaswa kujibiwa.
Mtu akianza mara nabii, mtume au kuhani, mwulize ni nani aliyempa hicho cheo;

Kwenye miujiza kumekuwa na usanii mwingi, mara utasikia kafufua mtu dar, Moro , Mwanza, etc, wakati inakuwa ni usanii mtupu kama ule wa Gajwima kusema anafufua wafu.

Kiongozi wa dini akisema ana uwezo wa kufufua wafu, watu wandaamane naye mpaka mortuary iliyo karibu wakamkabidhi mwili ili aufufue, akishindwa wahakikishe wanamfungia huko mortuary. Hizi tabia za "kufufua "watu hai inabidi zikome.

Umesema "Mtu akianza mara nabii, mtume au kuhani, mwulize ni nani aliyempa hicho cheo;" mimi nitakuuliza je, kina Ibrahimu, Musa, Yakobo walipewaga vyeo vyao na nani

Nimepata video ya Kuhani Musa akielezea historia yake kwa ufupi sana
Kuhusu hilo la kuandamana kwenda mortuary na kiongozi wa dini ili akafufue wafu nalo ulifikirie vizuri.
Habari za miujiza ya kufufua wafu ipo tangu enzi za manabii na Yesu Kristo mwenyewe lakini sio kila mtu anayekufa alifufuliwa

Nimesikiliza baadhi ya shuhuda za watu kufufuka sikuona popote pale ambapo amesema anataka kuwafufua; waliofikwa na hayo matukio ndio wamerudi kupaza sauti ya ufufuoAsante. Ingawa hakuna sehemu yeyote Yesu alipokea pesa ili kumponya mtu au kiingilio cha kumuona.

Kingine nisichokipenda ni kutumia vitu kama maji, mafuta, juice au chumvi kama nyenzo ya uponyaji. Hii inakuwaje mtu yupo hapo na mtumishi yupo...kwa nini asiombe kwa jina la Mungu ili amponye? Ingekuwa maji yanaombewa na kupelekewa walio mbali hapo sawa.

Mimi binafsi siwezi kwenda mtumishi anayedai pesa. Never. Kwa sababu hakuna mtu anayemlipa Mungu pesa kulitumia jina lake.

1 Pet 1:18-19 inasema "Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu" bali kwa damu ya Yesu.​


Sijawahi kusikia hilo la kuwako na kiingilio au la kutoa pesa ili watu waponywe. Labda mama kubwa na wengine hao walioshuhudia hapo juu au ndugu na jamaa zao watupatie ukweli wa hili ili tumjue Kuhani Musa zaidiKuhani Musa Richard Mwacha ni nani?

Kutana Tausi wa Bongomovie na mwanae kwa Kuhani Musa.

Wana Dar es salaam wajulieni hali kina Faiza, Bibi Nyaulingo, Mama Zuu na Mama Jack

View attachment 2130043

View attachment 2130042


Majirani msisahau kumkumbusha faiza akabidhishe ile pete na mikufu kwa usalama wake

Viongozi wa ulinzi na usalama wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania mmesikia kina faiza wana mpango gani na rais wetu? Kama Rais hayuko salama na nyie hamko salama. Hili swala la nguvu za giza mliangalie kwa sura nyingine sasa😎😎GREAT THINKERS wa Jamiiforums hivi huyu KUHANI MUSA RICHARD MWACHA ni nani haswa?
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
15,114
55,237
Hii huduma ya kiroho siku hizi imekuwa biashara, na miongoni mwa vitu wanavyotumia kuvutia wateja ni kufufua misukule nk, bila mkristu kuutambua ukwelI huu utahangaishwa sana na hawa wajasiriamali wanaotumia jina la Yesu Kristu kwa biashara zao, watu wasome biblia huko ndiko kwenye njia ya kweli na uzima.
 

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
469
580
Mimi nampendeaga kwenye mahubiri yake yuko vizuri sana katika kufafanua mambo mbalimbali katika biblia. Kitu kinachonikwaza kwake ni namna anavyochelewesha ibada bila kujali watu wanatoka mbali mara nyingi nikipita tembeon siku za ijuma ana jumanne utawakuta watu wamezagaa kule had saa saba wanatoka ibadani kweli hii sio salama sana,ajitahidi amalize ibada walau saa mbili na nusu watu wawahi kwao.

Mengine jamaa yuko vizuri sana na nazani ndio maana amepata mafanikio Makubwa kwa muda mfupi an kuwazidi hata waliomtangulia
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
18,007
30,919
Hii huduma ya kiroho siku hizi imekuwa biashara, na miongoni mwa vitu wanavyotumia kuvutia wateja ni kufufua misukule nk bila mkristu kuutambua ukwelI huu utahangaishwa sana na hawa wajasiriamali wanaotumia jina la Yesu Kristu kwa biashara zao, watu wasome biblia huko ndiko kwenye njia ya kweli na uzima.

Ungepitia huo uzi wote ungekuja na maelezo ya kusaidia zaidi.

Sikiliza na mahubiri

 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
19,979
55,578
Watu wa Dar katika ubora wenu. Ngoja na mimi nitafute kibali nije nianzishe Ministry yangu. Maana kuna uwezekano hela zenu hazina matumizi mengi kama za huku Kijijini niliko.

Hivyo siyo mbaya nikija kula fungu lenu la 10 la mapato ghafi! 😋 Miujiza na mambo mengine yote, yatakuwepo.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
8,020
16,353
Pale Kuna maombi kulingana na kiwango chako Cha pesa kuna maombi ya laki laki maombi ya Elfu hamsini ,maombi ya Elfu ishirini na n.k

Uliona WAPI maombi kulingana na umaskini au utajiri WA MTU

Unahitaji kiwango Cha juu Cha upumbavu kumuelewa yule tapeli

USSR
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
18,007
30,919
Watu wa Dar katika ubora wenu. Ngoja na mimi nitafute kibali nije nianzishe Ministry yangu. Maana kuna uwezekano hela zenu hazina matumizi mengi kama za huku Kijijini niliko.

Hivyo siyo mbaya nikija kula fungu lenu la 10 la mapato ghafi! 😋 Miujiza na mambo mengine yote, yatakuwepo.

Tate Mkuu tuanze kujifunza kwa hawa waliotutangulia
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
18,007
30,919
Pale Kuna maombi kulingana na kiwango chako Cha pesa kuna maombi ya laki laki maombi ya Elfu hamsini ,maombi ya Elfu ishirini na n.k

Uliona WAPI maombi kulingana na umaskini au utajiri WA MTU

Unahitaji kiwango Cha juu Cha upumbavu kumuelewa yule tapeli

USSR

USSR umesikiliza hizo clips?
 

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
4,574
4,977
Imani ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu; ni ile hali ya akili ya mtu kupokea ukweli uliofunuliwa na Mungu akiambatanisha nafsi yake kwa Mungu.

Kuhani Musa Richard Mwacha amejulikana kama mtumishi wa Mungu mwenye imani kwa Kristo. Na amekua na huduma yake katika jiji la Dar es salaam kwa miaka michache sasa.

Ukifuatilia Kwa muda mfupi sana utakutana na mambo mengi sana na kati ya hayo mengi ni style ya mahubiri yake, miujiza na maajabu kwenye ibada zake na idadi kubwa ya waumini alionao ndani ya muda mfupi sana maana miaka 3 au mi4 bado huduma ni changa.

Ila swali moja la msingi huyu Kuhani Musa ni nani haswa?

Hizi shuhuda zimetolewa hadharani, ni shuhuda zinazodhihirisha mambo magumu kufikirika katika hali ya kawaida. Ila hawa walioshuhudia wapo kati yetu, mtaani kwetu hata majumbani kwetu, kigoma, chato, kilimanjaro, sumbawanga, kagera, Dar es salaam mmetisha sana. Wenyeji wa huko mnasemaje kuhusu Kuhani Musa?

Fred William Rwegasira.
View attachment 2123813
Mr Rwegasira ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera, Bukoba kule, Mkazi wa Salasala - Dar es salaam. Na sasa anaishi kimara


Innocent Carol Paulo
View attachment 2123832
Innocent Carol Paulo ni mzaliwa wa Chato. Na mkazi wa Tabata - Dar es salaam


Levina Lyamuya na mdogo wake
View attachment 2123876
Levina ni mwenyeji wa Kilema, Moshi- Kilimanjaro

Malkia


Bwana YusufuYusufu ni mzaliwa na mwenyeji wa kigoma

Sumbawanga mtoto afufuka
ttps://youtu.be/PHUUbiYOEBY

Mama D umeisha nasa tiyari, makuani wa Sasa sio wa kuamini mama D
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
8,020
16,353
Ndio nimeweka hapo washudiaji na uwenyeji wao na makazi yao ili tujue hayo maigizo yanafanyikaje

Bila proof ya unachokisema itazidi kuaminika na kubaki palepale kwamba miujiza inatendeka
Miujiza kutendeka sio ishu maana hata shetani ni mtenda miujiza ,MUNGU ni roho kama alivyoshetani , nguvu ya Giza(shetani)na nguvu ya Nuru (MUNGU)

Nvyojua pale Kuna nguvu ya Giza na inatenda KAZI kwa matambiki ya kigiza bila watu kujua

USSR
 

msonobali

JF-Expert Member
May 23, 2015
1,204
1,021
Mitazamo yetu inawezekana inatofautiana kwenye haya masuala ya kiimani, binafsi napenda zaidi kumtafuta na kumjua Yesu Kristu kwa njia zangu nikiamini hata kama kuna mahala nakosea ni yeye kupitia roho mtakatifu ndie atakayenisahihisha kwa wakati wake.
Kama watu wote wangejua hiki unachokisema Hawa manabii wangefunga huduma.

Tatizo watu siku hizi wanapenda miujiza na kutabiriwa Kama wayahudi wa wakati wa Yesu
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
18,007
30,919
Sio clips TU dada huyu yupo mitaa ninayoishi namsikia kila siku HASA USIKU ,ni mganga wa kienyeji TU aliyechangamka yesu alitoa Bure, hizi shuhuda ni michongo japo miujiza ipo

USSR


Fanya tumnase basi USSR
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom