Sawa nimekuelewa. Ninachokikataa mimi ni huko kujikopesha kwenda kufanyia kazi zingine,wakati duka bado linahitaji liongezewe hela. (Labda mpaka utakaponiambia limejitosheleza). Yaani kujitosheleza kwa maana ya vifaa vilivyopo dukani,uwe na kama hivyo tena stool. Na hapo kila bidhaa itakayokosekana dukani usiwe na wasiwasi wa kuiagiza. Sio tena bidhaa haipo dukani,halafu ni muhimu,huku hela umejikopesha imekaa kwenye mahindi. Nakuhakikishia hivyo vyote utavifanya mbele,ila jitosheleze kwanza kwenye duka. Usiwe na tamaa ya kufanya vitu vingi utakwama mahala. Niamini. Deal na kitu kimoja kwanza. Hivyo vyote vitakuja tu mbele. Halafu umesema vijana dukani. Muda mwingi wewe uwe unakuwepo. Hesabu zote endesha wewe,agiza mzigo wote wewe. Usilidharau hilo duka kama una wateja. Wewe ndio utawakimbiza wateja kwa kukosa bidhaa muhimu,baada ya kujikopesha hela ya dukani