Acha kazi mara moja, roho yako inayo kuongoza haiwezi kukupoteza, nilifanya huko kazi lakini mafanikio niiyapata kwa rushwa tu, tena rushwa ndefu, bila rushwa mshahara wao hautoshi, tena wanakubana sana kila asubuhi uko kazini, hata muda wa kufikiri huna, kariakoo unaisahau. sasa ningeishije kwa wizi ?mpaka lini? nikayakoroga yasije nikuta
Ujue hao wanaopata raha serikalini wana ma-godfather wao wana tanua sana, au kama unaweza ujipendekeze sana kiasi cha kujidhalilisha, na kufanyiwa ya hovyo,
Wale wenye godfather wanapewa semina na mishahra ina panda kama kawa, wanapanda madaraja, wanapewa nafasi nzuri hata wa chini yako anawezakuwa na mshahara mkubwa kuliko wewe ilimradi tu ana godfather. wakiona umemenunua gari, umejenga umeenda kusoma, wanakuzushia tu ili uhame au
wanakukatia mshahara kwa muda usojulikana bila sababau ilimradi tu utumie resources zako zote,
kwa kufidia pengo la mshahra, utafuatilia mpaka miguu iote kutu, na usisubili hayo yakukute ondoka mara moja, huko serikalini imejaa misukule mitupu, yana visukari, ma high BP, ni shida sana huko. labda magufuli ayaondoe kwa sasa.
Top layer ya serikalini itakupenda Kama unaishi kwa shida shida sana, huna mpango wa kwenda kujiendeleza (kusoma), mfano mlevi, teja( mlandukaji), mgonjwa wa ukimwi, hapo hutoki, lkn eti kijana una afya yako mjanja unadundulize hela yako unapojua mwenyewe, ujenge nyumba gari weeee! utaona kila rangi ya fitina.
Navyo kuona wewe tayari ni mjanja, umeshtuka ka mshahara kadogo, ina maana utatengeneza vyanzo vingine vya pesa, wakikujua tu tegemea hayo hapo juu, Yaani wanaweza lengesha rushwa tu, kuna mawili godfather akutose, au aendelee kukuunga mkono hivohivo, akihamishwa umeumia.
UKIKAA KAA KI MAGUTU SANA ISIVO KAWAIDA. yangu ni hayo!
kila la kheri!