Mzee Warioba: Siyo lazima Mbunge aitwe Mheshimiwa

Haya mambo yapo kwetu tu, Ku sehemu hata Prof. Dr. nk huyasikii ovyo, hadi ujuwe huyu ni professor ni mda sana, njoo bongo sasa, PhD holder hataki kuitwa kwa majina yake, lazima utangulize Dr. Mwafulani.
 
Mzee wetu Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kulazimisha watu wakuite wewe kuwa ni mheshimiwa mbunge, mheshimiwa waziri, mheshimiwa diwani huko ni kuweka matabaka kwenye jamii ya watanzania.
Hii inapingana na Naibu Spika alivyogombana na Mbunge wa Mbeya Mjini Mbilinyi. Tulia alilazimisha kuitwa Mheshimiwa Naibu Spika
Hakika mzee Warioba ni tegemeo la watanzania kwa busara.
Chanzo dakika 45 itv.
 
Mwinyi aliitwa mtukufu na baada ya Mkapa kuingia madarakani akiwa bado mpya kabisa katika urais aliulizwa kama naye wawe wana mu-address kama mtukufu rais na akakataa katakata(but my take lile swali aliliandaa mwenyewe though maybe I was wrong) na pia akakataa sura yake kuwekwa kwenye pesa.
Kwa kumbukumbu nafikiri suala la kuweka sura ya rais kwenye fedha likipitishwa bungeni.

Sababu ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kuwa kila baada ya miaka 5 akipatikana rais tofauti basi fedha zetu zingekuwa na muonekano tofauti.
 
Umeanza vyema harakat!! Endeleza sasa uungwe mkono
HIZI SIO HARAKATI NI MAONI YANGU NA KUJARIBU KUELEZEA JAMBOAMBALO LILIKUWA MEZANI. KAMA UNAHISI NI HARAKATI NADHANI ASHAKUMU SIO MATUSI UMEKURUPUKA. NIMEPITIA REPLY ZAKO NIMEONA KAMA JAMBO HILI LIMEKUUDHI LAKINI HATUTASITA KUTOA MAONI YETU NA USHAURI WETU KWAKUWA BAADHI YA WATU HAWATAKI KUAMBIWA UKWELI
 
Mwinyi aliitwa mtukufu na baada ya Mkapa kuingia madarakani akiwa bado mpya kabisa katika urais aliulizwa kama naye wawe wana mu-address kama mtukufu rais na akakataa katakata(but my take lile swali aliliandaa mwenyewe though maybe I was wrong) na pia akakataa sura yake kuwekwa kwenye pesa.
Hakuna mtu nchi hii mwenye ubavu wa kuuliza swali hilo ana kwa ana mbele ya Rais! Kuhusu sura yake kuwa katika noti zetu ni kuwa bunge lilikubali lakini yeye alikataa na kutoa sababu ambazo hadi leo zinazingatiwa ingawa kuna baadhi ya watu walilianzisha chini kwa chini enzi za Magufuli, lakini pia aliwanyamazisha.
 
Mtu aliyepewa cheo na wananchi ni mheshimiwa na ni vyema kupewa heshima yake hiyo! Mbunge amechaguliwa na wananchi kwahiyo ni mheshimiwa, mwenyekiti wa kijiji amechaguliwa na wananchi ni mheshimiwa pia! Gar la mbunge likipita linapeperusha bendera askari anarakiwa kuipigia salut bendera! Tuache wivu!
Wengi hawakupewa cheo dhamana ya kuongoza na wananchi,vipi nao waitwe waheshimiwa??
 
Back
Top Bottom