Mzee Warioba: Siyo lazima Mbunge aitwe Mheshimiwa

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Mzee wetu Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kulazimisha watu wakuite wewe kuwa ni mheshimiwa mbunge, mheshimiwa waziri, mheshimiwa diwani huko ni kuweka matabaka kwenye jamii ya watanzania.

Hii inapingana na Naibu Spika alivyogombana na Mbunge wa Mbeya Mjini Mbilinyi. Tulia alilazimisha kuitwa Mheshimiwa Naibu Spika

Hakika mzee Warioba ni tegemeo la watanzania kwa busara.

Chanzo dakika 45 itv.
 
Mtu aliyepewa cheo na wananchi ni mheshimiwa na ni vyema kupewa heshima yake hiyo! Mbunge amechaguliwa na wananchi kwahiyo ni mheshimiwa, mwenyekiti wa kijiji amechaguliwa na wananchi ni mheshimiwa pia! Gar la mbunge likipita linapeperusha bendera askari anarakiwa kuipigia salut bendera! Tuache wivu!
Amesema enzi za mwalimu yeye akiwa ni waziri mkuu viongozi walikuwa wanaitwa ndugu au mwananchi.
 
Wewe na yeye mzee Warioba nani anajua zaidi mambo ya kiutawala?

Huyo mzee ni waziri mkuu mstaafu unaleta usukununu wako hapa?
 
Mtu aliyepewa cheo na wananchi ni mheshimiwa na ni vyema kupewa heshima yake hiyo! Mbunge amechaguliwa na wananchi kwahiyo ni mheshimiwa, mwenyekiti wa kijiji amechaguliwa na wananchi ni mheshimiwa pia! Gar la mbunge likipita linapeperusha bendera askari anarakiwa kuipigia salut bendera! Tuache wivu!
Mbona viongozi wa dini anaitwa kwa Cheo Chao kisha jina.
Mf: Mchungaji D, Askofu D, shehe D nk.
Kwani Hawa wabunge tusiwaite Mb. K na sio kulazimisha tuanze na Mheshimiwa wakati wengine hawana hiyo heshima
 
Amesema enzi za mwalimu yeye akiwa ni waziri mkuu viongozi walikuwa wanaitwa ndugu au mwananchi.
Nakumbuka wakati wa Mwalimu hakukuwa na neno Mheshimiwa kwa mtu yeyote, viongozi wote walikuwa wakiitwa Ndugu kasoro Rais ambaye alikuwa pia akiitwa Mtukufu Rais! Baada ya Mwalimu Nyerere kutoka madarakani, ukaibuka mjadala Bungeni Wabunge wakitaka waitwe Waheshimiwa (Honorable).

Mwalimu alipinga lakini wakamwambia mbona Uingereza wanaitwa Honorable. Wakapitisha sheria wakaanza kuitana Waheshimiwa. Siyo wakati wa akina Waryoba kweli?? Tafuta wazee watukumbushe. Ila wakati Waryoba ni PM Rais wake alikuwa akiitwa Mtukufu Rais, na Mzee sikumsikia akisema kitu kwa kuwa labda alikuwa na kitu.
 
Mzee wetu Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kulazimisha watu wakuite wewe kuwa ni mheshimiwa mbunge, mheshimiwa waziri ,mheshimiwa diwani huko ni kuweka matabaka kwenye jamii ya watanzania.

Hii inapingana na Naibu Spika alivyogombana na Mbunge wa Mbeya Mjini Mbilinyi. Tulia alilazimisha kuitwa Mheshimiwa Naibu Spika

Hakika mzee Warioba ni tegemeo la watanzania kwa busara.

Chanzo dakika 45 itv.
Ni uqendawazimu mtu kutaka uotwe mheshimiwa. Sasa mtunkama Ndugai, ambaye kika mwenye akili anamdhaharau kutokana na unafiki wake, hata akiitwa mheshimiwa ndiyo ataheshimiwa? Si atabakia zuzu tu kama alivyo?
 
Mtu aliyepewa cheo na wananchi ni mheshimiwa na ni vyema kupewa heshima yake hiyo! Mbunge amechaguliwa na wananchi kwahiyo ni mheshimiwa, mwenyekiti wa kijiji amechaguliwa na wananchi ni mheshimiwa pia! Gar la mbunge likipita linapeperusha bendera askari anarakiwa kuipigia salut bendera! Tuache wivu!
Ni mwendawazimu pekee ndiye anayeweza kuamini kuwa unaheshimiwa kwa sababu umejiita au umeitwa mheshimiwa.

Mwalimu Nyerere, mpaka leo kila mtu anamheshimu lakini hakuwahi kuitwa mheshimiwa, na alikuwa hataki kabisa.
 
Wa kuheshimiwa ni yupi aliyempa mwenzake cheo na ama aliyepewa cheo na mwenzake. Nadhani imefika kipindi ambacho uijinga na upumbavu ambao tumekuwa tunauendeleza tuuache. Waheshimiwa ni sisi wananchi tunaowapa hao watu nafasi za kutukuwakilisha na bado tukawalipa mishahara,posho na bado tukawalipia magari na mafuta na wakaja kutudanganaya na mfuko wa jimbo na wakati pesa zote hizo ni zetu ambao tunalipa kodi
 
Nakumbuka wakati wa Mwalimu hakukuwa na neno Mheshimiwa kwa mtu yeyote, viongozi wote walikuwa wakiitwa Ndugu kasoro Rais ambaye alikuwa pia akiitwa Mtukufu Rais! Baada ya Mwalimu Nyerere kutoka madarakani, ukaibuka mjadala Bungeni Wabunge wakitaka waitwe Waheshimiwa (Honorable). Mwalimu alipinga lakini wakamwambia mbona Uingereza wanaitwa Honorable. Wakapitisha sheria wakaanza kuitana Waheshimiwa. Siyo wakati wa akina Waryoba kweli?? Tafuta wazee watukumbushe. Ila wakati Waryoba ni PM Rais wake alikuwa akiitwa Mtukufu Rais, na Mzee sikumsikia akisema kitu kwa kuwa labda alikuwa na kitu.
Acha uwongo. Nyerere hakuwa anaitwa mtukufu Rais. Alikuwa akiitwa Ndugu Rais. Kenya walikuwa wanamwita mtukufu Rais Arap Moi, wote watanzania tulikuwa tunashangaa. Wakati huo nikiwa chipukizi, nilimvisha Mwalimu skafu mara 2, mara zote nilimwita Ndugu Rais ..... Mwinyi ndiye kwa mara ya kwanza aliitwa Mtukufu Rais, na wabunge wakajiita waheshimiwa.
 
Back
Top Bottom