Mzee wa Upako amchana live TB joshua

Mzee wa Upako amchana live TB joshua

Ni kweli kabisa ndugu, yani nimekua nikimsikiliza tb joshua, sikuwahi kumsikia akikashifu mtumishi yoyote wa Mungu au kujibu mashambulizi anayoyapata toka sehemu mbalimbali. Ana hekima ya ajabu sana mtu huyu.

Ni kweli kabisa Tb Joshua hajawahi kumkashifu mtu yeyote wa dini au dhehebu lolote
 
Hahaaa hawa wote wawili ni wasanii tena sana,yaani nyani haoni kundule
 
Sawa kabisa. Kwa nini asimuombe Mungu wake kusitisha machafuko yanayotokea Nigeria. Pia anaona raha gani kutoa utabiri wa maafa kutokea pasipo kutoa tahadhari ya kuzuia maafa hayo kwa kumuomba Mungu?

Nna mashaka hukumsoma vizuri MTAZAMO rudia tena kusoma.
 
Last edited by a moderator:
Nilijua tu....hamuwezi kusoma zaidi ya kusoma line moja na kuandika kama ulivyoandika.....:der:

Mkuu huyu jamaa nimemwambia arudie tena kusoma,,hii ndo aina ya wasomi tulio nao, anasoma line mbili ana-quote kwisha habari. Ni tabu kwa kweli
 
Huwezi kua na akili timamu ukamsikiliza lusekelo. Lusekelo ana uwezo mdogo wa kujenga hoja,anaropoka na kupayuka,anagombana na kila mtu,alianza na katotozi,akaenda kwa mwingira,akamsifia babu wa loliondo,yani anajiona yeye ndio yuko sahihi %mia. Alidanganya waumini wake mwaka 2011 hawataona tena mafuriko dar labda awe hayuko hai,wakampigia makofi sana,juzi mafuriko yametokea tena akiwa hai. Narudia tena huwezi kua na akili timamu ukamsikiliza yule jamaa.
 
TB Joshua aneni yatokayo kinywani kwake ila anachoambiwa na roho mtakatifu awezi kukulupuka kama lusekelo au kumjibu lusekelo kwa kuwa lusekelo anaongea anayoambiwa na mkwewe.roho wa MUNGU ni tofauti na roho wa shetani.TB JOSHUA ajahambiwa haongee kuusu boko haramu pindi roho wa MUNGU atakapo mruhusu ataongea.hata manabii wa zamani walikuwa wanahamlishwa na roho wa MUNGU na si kwa matakwa yao na pindi waombapo shida fulani uongozwa na roho jinsi ya kufanikishwa.upayukaji wa lusekelo ni wa kibinadamu yeye aongozwi na roho wa MUNGU na roho wa MUNGU awezi kuongea maneno ya kukashifu hapo ni pepo mchafu alimwingia anene hayo

ubarikiwe sana
 
Huwezi kua na akili timamu ukamsikiliza lusekelo. Lusekelo ana uwezo mdogo wa kujenga hoja,anaropoka na kupayuka,anagombana na kila mtu,alianza na katotozi,akaenda kwa mwingira,akamsifia babu wa loliondo,yani anajiona yeye ndio yuko sahihi %mia. Alidanganya waumini wake mwaka 2011 hawataona tena mafuriko dar labda awe hayuko hai,wakampigia makofi sana,juzi mafuriko yametokea tena akiwa hai. Narudia tena huwezi kua na akili timamu ukamsikiliza yule jamaa.

kuhusu mafuriko hata mimi nilimsikia kabisaa nikashangaa yakarudi tena.
 
Huwezi kua na akili timamu ukamsikiliza lusekelo. Lusekelo ana uwezo mdogo wa kujenga hoja,anaropoka na kupayuka,anagombana na kila mtu,alianza na katotozi,akaenda kwa mwingira,akamsifia babu wa loliondo,yani anajiona yeye ndio yuko sahihi %mia. Alidanganya waumini wake mwaka 2011 hawataona tena mafuriko dar labda awe hayuko hai,wakampigia makofi sana,juzi mafuriko yametokea tena akiwa hai. Narudia tena huwezi kua na akili timamu ukamsikiliza yule jamaa.

Mkuu mimi nna akili timamu na huwa inatokea mara moja moja niki-tune ch10, nakuta Lusekelo yuko on air. Huyu jamaa kama unafuatilia vzr utagundua mahubiri yake asilimia kubwa ni kuponda wahubiri wenzie sana sana TBJ.

Wakati flani TBJ alitoa unabii kuhusu kutekwa kwa raisi mmoja toka Afrika mashariki, TBJ alisema wazi kabisa raisi huyo atatekwa na magaidi, na akasema anatuma ujumbe kwa nchi husika juu ya nini kifanyike kuzuia hiyo hali.

Akihubiri katika moja ya ibada zake Lusekelo aliponda sana ule unabii, kwa macho yangu na maskio nlimsikia Lusekelo akisema maneno makali sana dhidi ya Mchungaji mwenzie TBJ, huku akishangiliwa na washirika wake Mzee wa upako alisema hakutakuwa na ugaidi eneo la E.Africa na kwamba hakuna raisi ataetekwa labda yeye (Lusekelo) afe ndo hilo jambo litawezekana.


Mungu ni mwema sana, haikupita muda serikali ya Sudan kusini ilituma ujumbe kwenda SCOAN, kumshukuru Mungu na kumshukuru TBJ kwa ule unabii na kwamba yale alotabiri kwa uwezo wa Mungu hayajatokea,,


Naunga mkono hoja, si busara sana watumishi wa Mungu kusemana wao kwa wao, na wale followers wa Lusekelo muende mkamshauri afanye kazi ya Mungu na sio kutumia nguvu nyingi kusema wachungaji wengine, huku akitunzwa kama msanii wa bongo fleva, aibu sana.
 
Kwa hayo maneno nimeamini Lusekelo anamatatizo kama wewe ni mtumishi Wa Mungu hupaswi kuwasema wenzako bali kuwaombea.Naona Lusekelo anatangaza biashara na sio neno la Mungu.
Tafakari
 
Mambo ya imani ni magumu sana ila tumwombe mwenyezi mungu atusaidie maana hata mchungaji kufanya mipasho ni hatari kwa kazi ya mungu
 
Dhambi hii anayo ifanya lusemelo itammaliza mwenyewe,kila nabii aliyekuja alikuja na unabii wake hawakufanana,nashangaa kitu kimoja kazi wanayofanya ni moja ya MUNGU anamkashifu nini acha wanao ponywa kupitia TB Joshua MUNGU anyanyuliwe,na wanao ponywa kupitia Lusekelu MUNGU ainuliwe pia ,wewe umewahi kutabiri nini kikatokea, hivi CIA wanauwezo wakujuwa kuwa ndege itapotea tena ya Nchi flani ,hivi CIA wanaweza kujuwa kuwa msanii flani marekani atakufa,hivi CIA wanaweza juwa kuwa kunakiongozi mkubwa wa Nchi flani atakufa ,hao ni CIA Wanaweza kumpa TB Joshua nguvu ya kum ombea asiyezaa apate Mtoto tena amtabirie kuwa atapata Mtoto wa jinsia gani na pia CIA anaowahonga wanampanguvu ya kuponya watu ambao wameshindikana kwa Kansa na magonjwa sugu .naimani CIA wa TB Joshua ni MUNGU aliye hai na Jina la MUNGU libarikiwe AMEN
Acheni kuamini huo uchafu hakuna mwenye uwezo huo labda mungu tu mnadanganywa na hao wachawi akina Joshwa kwa kuwafanyia viin macho angalia mtakuja kumkana na huyo yesu wenu! ndo maana webgine walidanganywa kupaishwa mbinguni kumbe maskini wamesalimisha mali zao na mwisho wakachomwa moto km mnamkumbuka mtu anaitwa nabii kibetele wa Uganda!
 
Mambo ya imani kila mtu afanye kazi yake bila kuingilia uhuru wa mtu mwingine. Kashfa kwa mtu yeyote anayefanya kazi ya Mungu ni dhambi. Kama Anthony Lusekelo anawakashifu ni kosa kubwa sio anachotakiwa kufanya. Yesu mwenyewe alikataliwa na kuwambwa msalabani, kwa hiyo siwezi kushangaa anachokifanya Lusekelo. Hicho anachotaka TB Joshua afanye na yeye pia anawajibu wa kukifanya ili kazi ya Mungu iendelee na nguvu za Mungu zionekane. Namuomba Lusekelo amuombe Mungu amuongezee upako ili watu tusipate shida ya kwenda mbali kutafuta huduma za maombezi, na upako hauwezi ongezeka kwa kutoa kashfa kwa watu wa Mungu.

Sasa kwani mtu anapewa maono aone kma Movie? Mtu anapewa maono ili atatue tatizo linalotarajiwa.. Na nabii wa ukweli wa enzi za biblia maono yao yalitoa solution ya matatizo. Kwa hiyo aliyosema huyu mzee wa upako yana ukweli.
Na kama mtabiri hatoi way foward anatofauti gani na watabiri wakawaida mpaka ajiite Nabiii?
 
God save us all maana nimesoma comments page moja moja, duh! How i wish siku moja wote tungekua kwenye the right side afu hiyo side iwe ndio side yenye kumuabudu Mugu wa ukweli.. Ila najua thats impossible kwa current situation hadi the end of days watakaoponamo... mtabishana wee ila mabishani haya yalikuwepo toka miaka hiyooo msidhani mtayamaliza leo
 
Nani alikwambia imani inahusiana PhD au Masters? Elimu yenyewe ya bongo ya vitini na tests??
Shida moja ni kuwa mnatumia ulimwengu wa mwili kwa mambo ya kiroho, hamtakaa muelewe mtaishia kubisha na kukashifu tu. Hivi hujui hata Yesu walimuita msanii nyakati zake? Sasa kama Yesu aliyeponya watu akafufua mpaka wafu walimuita msanii, unachoshangaa kwa TB Joshua ni nini? Hivi huyo mzee wa upako yeye kipi hasa cha kumuamini nacho ikiwa anakashifu watu wanaofanya kazi kama yake? Ni vema kujua, nyakati hizi shetani yuko very busy na wenye tamaa za mali na wavivu wa kufikiri. Nenda kiroho utaelewa ikiwa ni kweli au la.

Lakini Yesu tunaye msoma kwenye Bible alikuwa hatoi huduma ambayo ni Money oriented mfano kuuza Annointed Oil.... Fikiria Chukua Hatua.
 
Lusekelo ni mtumishi asiye haya. Wanao mfuata nawashangaa sana. Eti husema ukienda kanisani kwake hayupo Yesu pale wala Mungu. Yeye ndiye mwenye uwezo wa kukupatia hitaji lako kama gari na ajira Na siyo Mungu wala Yesu. nikimsikiliza napata shida. sijawahi sikia mchungaji mwenye kauli hyo zaid yake wala anayetuzwa pesa madhabahuni isipokuwa lusekelo. anyway hata Yesu alishasema "let the dead burry their own dead''. Yafaa sana tuyapime mafundisho ya Imani zetu na wanaotufundisha tuwapime. Siku za mwisho hizi.
 
kuhusu mafuriko hata mimi nilimsikia kabisaa nikashangaa yakarudi tena.

mbaya zaidi akasema mafuriko anayazuia kwa UWEZO WAKE YEYE MWENYEWE, sio wa Mungu. Mimi kama mkristo ninaejua maandiko yanasema sisi hatuwezi lolote bila Yeye yaani Mungu ila LUSEKELO ana uwezo wake yeye binafsi ambao hautoki kwa Mungu. tokea siku hiyo sijataka tena kumsikiliza. HUWEZI KUA NA AKILI TIMAMU UKAMSIKILIZA LUSEKELO.
 
Back
Top Bottom