Mzee Butiku awaita wazee kujadili amani, haki na maendeleo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Foundation) imeandaa mkutano wa mazungumzo kuhusu amani, umoja, haki na maendeleo ya watu, mkutano unaotarajiwa kufanyika Alhamisi ya Januari 22 mwaka huu (2026)

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Januari 19.2025, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Waryoba Butiku amesema mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi mkubwa wa mikutano wa taasisi hiyo uliopo Posta, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 03 asubuhi, unalenga kutoa nafasi kwa wazee kujadili na kutoa maoni kuhusu misingi iliyoundwa na kudumisha Taifa la Tanzania kuwa nchi ya amani, umoja, haki na yenye matumaini ya maendeleo endelevu ya watu

"Washiriki katika mkutano huu ni wazee katika maana pana ya watu wenye hekima na busara kutoka kwenye makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wa Dini, wasomi, wazee wastaafu, wanawake, vijana, vyama vya siasa, Tasnia ya Habari na Taasisi za Kiraia (AZAKI)" -Mzee Butiku

Mzee Butiku amesema umuhimu wa kufanya jitihada za kuimarisha amani, umoja, haki na maendeleo ya watu kwa sasa unatokana na matukio ya ghasia na matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.2025

Katika kusindikiza ujumbe huo Mzee Butiku amesema, "mazungumzo ndio nyenzo ya upatanishi na ujenzi wa amani".

 
Takataka mavi
 
Mazungumzo hayajawahi kuwa nyenzo ya upatanishi na ujenzi wa amani popote pale. Mazungumzo yanachelewesha amani na kuimarisha uovu. Amani inaletwa na kurekebishwa kwa kile ambacho kinamakosa kisiporekebishwa lazima industrial action itumike.
 
Kwani nchi hii ina wazee tu!?

Huyu Mzee ni useless kabisa.
 
Atuache tusikilize dhamiri zetu. Kama ambavyo alimshauri Polepole.
 
Huyu mzee toka amuuze Polepole kwa Mafwele nimemdharau sana ni mchumia tumbo tu.
 
Zee la hovyo hili, haipendezi mzee kuwa Chawa tena Dakika za jioni, ukifa una nini cha kutuachia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…