My opinion: CCM fukuzeni mapacha watatu sasa au nyamazeni

Kwa kuongezea Ndugu Unstoppable, nadhani William alitoa maelezo kwa ufahamu wake juu ya hizi tuhuma Mzee dhidi ya mtuhumiwa wa EPA. Na alileza kuwa wakati wa michango ya harusi mmoja wa watu walioleta mchango alikuwa Sophia Simba (correct me I am wrong), na Bi Sophia alileta kama group contribution ambamo ndani yake kulikuwa na mchango huyu mtuhumiwa wa EPA. Kwa hiyo technically Mzee anakuwa mbali kidogo. Hata hivyo ningependa kuamini in fact ninaamini William is his own man. Yes, loves his father and all that na achokisema hapa jamvini in fact kinaweza kutafsiriwa kama kuwa na mtazamo wa mbali kidogo na Mzee? but that goes to show the character of the man! Call a spade a spade!

I hope T.K utakuwa umeridhika walau kidogo na haya majibu na pia inatuonesha kuwa kupita hili jamvi tunaweza kutoa dukuduku zetu wakati huo huo tukapata mawazo kama si majibu ya dukuduku hizo. Tuzidi kushikamana maana taifa linatafunwa! chapa kazi William, chapa kazi T.K.

Nikiri tu kuwa sikupata kusikia maelezo kama haya toka kwa Williama, naamini yalinipita..........maelezo yako yamejitosheleza
 
- Wakuu please naomba sana tujadili hoja niliyoileta mezani, Rais wa sasa anamaliza muda wake soon na bado mpaka leo sijafikia hatua ya kuamini kwamba anahusika na ufisadi wa aina yoyote, so naomba tujadili hoja ya mezani kwanza!

William @ NYC, USA.

William hapo naomba nitofatiane na wewe, ni either mkuu anahusika moja kwa moja, au anahusika kwa njia tofauti ndio maana anaohopa kuchukua hatua sahihi.........kumbuka reaction yake baada ya Lowasa kujiuzulu yeye alisema "ni ajali ya kisiasa" pia wateule wake waziri mkuu na IGP wote wameshakiri hadarani kuwa mafisadi hawakamatiki na Pinda akasema wakikamatwa nchi itatikisika

yeye akiwa mkuu wa nchi kwa nini asamuru majina ya wamiliki wa Kagoda yawekwe hadharani?.....imethibitika ule mgodi wa kiwira ni ufisadi wa Mkapa, yeye kachukua hatua gani zaidi ya kusema kuwa "mwacheni mzee apumzike"??....inawezekana ni kweli katiba iliyoko sasa inamlinda mh.mkapa lkn yy anaweza akaanzisha mchakato wa kuondoa hiyo kinga ili siku za usoni wezi wa mali za taifa wasiwe na kinga.....CCM wameshasema mara nyingi kuwa mtu hawezi kuwa mwizi hadi atakapothibitika mahakamani, JK kama mwenyekiti wa chama tawala na mkuu wa nchi kwanini asitoe order DPP aanzishe prosecution kwa hao watu, yeye anahofu nini???....ndio maana mimi nitaendelea kuamini kuwa huyu rais anahusika
 
Willy,
Mkuu wangu shukran sana kwa kuweka ukweli huu ambao hauna ushabiki labda tu mtu apende kushabikia..Sisi wote hapa tunaomba hawa mapacha watiwe ndani kama walivyotangulia kina Yona na Mramba kwani tuna ushahidi mkubwa zaidi dhidi yao na mahla pekee panapoweza kuthibitisha kwamba wao ni innocent/Guilty ni mahakamani na as long as they are presumed innocent hakuna sheria inayokataza kukamatwa kwao.Hatuwezi kukataa ukweli huu kwa sababu ati kuna Mafisadi wengi CCM ama nchini kwani kama ingekuwa hivyo tusinge wakamata hata wezi maanake wapo wengi.

Nakumbuka wakati JK anaingia madarakani alisafisha Polisi na kukamata majambazi kiasi kwamba tuliweza kusafiri, kulala na kutembea kwa amani ingawa sii majambazi wote walokamatwa isipokuwa ilitoa onyo kali kwa majambazi. Na katika majambazi hao wapo walioshinda kesi zao na wengine kupelekwa lupango ndivyo sheria inavyo operate.

Na hata walipokamatwa Yona na Mramba, mkuu wangu rushwa iliogopwa kama ukimwi na kwa mara ya kwanza ilikuwa ukienda ofisi za serikali utahudumiwa haraka na bila kutoa rushwa. Lakini pamoja na yote haya hivi vilikuwa vita vya Titans, kumbe ilikuwa kugombea nafasi za Kufisadi lakini toka Lowassa ameondolewa madarakani serikali ya JK imekwenda likizo, yaonyesha JK hawezi kuongoza pasipo Lowassa na mtandao. Serikali hii imekuwa sii ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo Ujambazi na Ufisadi umerudi tena kwa kasi baada ya serikali kwenda rikizo.
CCM na JK kama kweli mnataka kujuvua magamba kukomesha Ufisadi basi ile ile dawa ya Lowassa na Sokoine itumike kupambana na Ufisadi kwani inawezekana. Sumu ya nyoka pia ni snake venom antidote!
Mkuu Mkandara, binafsi siungana na Will katika hili na nitamjibu separate. Kama ni kweli nhi yetu inaongozwa na utawala wa sheria, hawa mapacha watatu, waadhibiwe kwa kosa gani?.

Kama Mramba ana kesi ya ufisadi mahakamani na na JK huyu huyu ndio amesimama kumnadi kabla hajaangukia pua, leo JK huyu anayewanadi watuhumiwa ili hali kesi zao ziko mahakamani, ana ujasiri gani kuwatimua mapacha watatu ambao hawana kesi yoyote mahakamani?.

Kwenye posti hii, mimi nimeipenda ile hoja niliyoibold, Ile kasi yote ya JK mwanzoni, iliwezekana tuu kwa vile Lowassa was behind, JK mwenyewe as JK si lolote, si chochote, he is a weak leader na sio kwamba hawezi kuwafanya chochote hawa jamaa, bali hana ubavu huo!. Period.
 
Mkuu Kobello, CCM ya sasa hakuna katiba! Naomba ufahamu hivyo ni bora liende tu!.....Sasa hivi wanashindana nani atakuwa na mabilioni mengi kuliko mwingine na hii ndio inasababisha mikataba ya kifisadi au manunuzi ya kifisadi kuendelea kuwepo hata leo hii pamoja na Watanzania wengi kupigia kelele ufisadi na kusababisha nchi kuendelea kwenda mrama.

Kiongozi tuliye naye anajua wenzie wanazijua dhambi zake na ndio maana anashindwa kutumia uwezo mkubwa aliokuwa nao kama Rais wa nchi na hii inasababisha nchi kuendelea kuangamia na Watanzania wengi kupoteza imani na Viongozi waliokuwepo madarakani.

Kama kanuni ulizoandika hapo juu zingekuwa bado zinafuatwa basi kelele hizi tunazozipiga kila kukicha labda zingekuwa hazipo au zingekuwa chache sana.
Ningeomba mchango wa vijana wanaofikiria,
Based on my oservation,kuna mtu yoyote anaweza kuchangia kesi hii kwa kutoa mifano mingine ili kuinenepesha hii kesi?
Mpaka hapo bado naamini ni slam dunk....based on a fair judicial system.
 
Facebook: William Malecela on Saturday, June 4, 2011 at 8:13am

@ NEW YORK CITY-USA: Nimeshitushwa sana na habari za CCM kuwaita Mapacha Watatu eti kwa mahojiano!, I mean mahojiano ya nini? Wananchi wa hili taifa tumechoshwa sana na hivi viini macho. Ni CCM wenyewe walio-raise the bar kwa kutangaza kujivua magambas na ni CCM iliyotangaza kuwaondoa kwenye NEC yake na CC, as a member of CCM I was incouraged na the news kwamba CCM ipo njiani kuwafukuza chama kabisa, sasa tena tunaposikia habari za mahojiano inaleta utatanishi! Mahojiano ya nini! mbona walishawaweka pembeni kwenye nafasi muhimu sana za ndani ya chama bila mahojiano? I mean sasa ni wakati wa CCM kutangaza kwamba imewafukuza tayari au ikubali kwamba haina huo ubavu!
Mkuu William, kwanza siungani na wewe kuhusu kufukuzwa kwa hawa mapacha watatu, unataka wafukuzwe kwa kosa gani?. CCM si ndio chama tawala, kama hawa mapacha wana makosa, si muwafikishe mahakamani?. Kama Mramba ambaye tayari anayo kesi mahakamani, Mwenyekiti wako alisimama kumnadi kabla ya wananchi kukataa kwa kura kulikopelekea kuangua pua, sasa CCM ina ujasiri gani kuwaadhibu watu wasio na hatia?!.
- I mean nothing personal, na sio kwamba kufukuzwa kwa hao mapacha watatu kutaondoa matatizo ya wananchi kwa siku moja, lakini tunategemea kwamba wakishavuliwa uanachama wa CCM, ifuatie kuwapeleka kwenye mkono wa SHERIA!. Tanzania tunasumbuliwa sana na tatizo moja tu nalo ni hatuna RESPECT KWA THE RULE OF LAW OF OUR LAND!, ndio maana hata huku majuuuu wengi wetu tunaishi kwa taabu sana maana hatujui kuishi kwa kuheshimu sheria. Hawa mapacha watatu wakikiwapelekwa kwenye sheria, ni kwamba sasa unafungua milango ya wanasiasa wahalifu wote nchini kupelekwa kwenye sheria na wananchi kuanza kuheshimu sheria kwanza za Jamhuri, hatimaye wataheshimu sheria za makazini mpaka sheria za familia majumbani mwao, I mean Wa-Tanzania we are too corrupt tunahitaji kuanzia somewhere na hapa kwenye mapacha watatu ndio penyewe sana, So CCM it is either now, or forget it! and Never!
Kama ni kweli unafahamu The Rule of Law, kwanini tuwaadhibu kwa kuwafukuza watu wasio na kosa lolote, halafu ndipo tuwafikishe mahakamani?. Kama wana makosa, kwanini kwanza tusiwashitaki kwa makosa hayo, wakisha hukumiwa ndipo tuwafukuze?. As far as the rule of law is concerned, hawa mapacha watatu are all clean.
- CCM the burden is on us na wakati ni sasa, either tufanye kweli au tunyamaze, lakini habari za mahojiano maana yake ni kwamba somebody is not sure kama hawa waondolewe au la! Tunasema hivi sio tu wafukuzwe chama, isipokuwa wafikishwe kwenye SHERIA, na wengine wote wenye tuhuma za wizi wa mali zetu za umma na kodi zetu wananchi, ninasema mali zao zote zingekua frozen now na serikali, mpaka watakapothibitisha kwamba kwa miaka mitano ya uwaziri mtu unaweza kuwa Billionea na kuanza kusomesha watoto nje, na kununua magari ya kifahari pamoja na kuwa na hisa kila mahali kwenye makampuni makubwa na kujenga majumba ya ajabu. Ni muhimu sana kuwepo na Legal Facts ili haki zao watuhumiwa zisikiukwe, I mean we are not asking for a Mob Justice, au blind Justice! hapana tunataka Fairness Justice!
William, mbona hapa unajikanganya, haiwezekani wewe kwenye posti hii moja hapa ukasema hivi "Mahojiano ya nini! mbona walishawaweka pembeni kwenye nafasi muhimu sana za ndani ya chama bila mahojiano? I mean sasa ni wakati wa CCM kutangaza kwamba imewafukuza tayari au ikubali kwamba haina huo ubavu!", halafu kwenye posti hiyo hiyo wewe wewe tena ukasema hivi Legal Facts ili haki zao watuhumiwa zisikiukwe, I mean we are not asking for a Mob Justice, au blind Justice! hapana tunataka Fairness Justice", which is which?!. Principle ya kwanza ya Natural Justice ni "No one is condemned unhead", nadhani hiki ndicho chama chako kinachotaka kufanya, wewe unataka wahukumiwe kwa tuhuma tuu au shutuma bila kosa lolote?.
- So! CCM the time is up, either wafukuzeni chama SASA hawa Chenge, Rostam na Lowassa, au nyamazeni turudie tulipokuwa siku zote yaani kama kawaida, tusubirie kuwa chama cha Upinzani 2015, kama KANU. Na CCM let me tell you this, siku tutakapoishia kua upande wa pili wa the glass, ndio imetoka haitakuja kurudi tena! Uliza UNIP kule Zambia!

MUCH RESPECT! & MUNGU AIBRIKI TANZANIA!

William Malecela @ New York City, US.

William, kwa vile wewe ni CCM damu, umezaliwa CCM, umekulia CCM, na sasa unajiandaa kuifia CCM kwa uanzishaji hilo tawi huko ulipo, kwa hayo nilidhani, unaifahamu vizuri CCM kwa undani wake, kitendo cha kushauri hawa mapacha watatu wafukuzwe kabisa CCM, ni uthibitisho wangu tosha kumbe hata wewe huijui CCM!, ukidhani CCM inao ubavu wa kuwakuza uanachama. Kwa kukusaidia tuu, CCM haina ubavu huo, na hata kama CCM itaamua kuwafukuza ili kuwa 'sugar coat 'waTanzania kuwa CCM inaweza, nakuhakikishia, hao jamaa wote watatu wakisimama tena kwenye majimbo yao, kupitia vyama vyovyote, watayataa tena majimbo yao kwa ushindi wa kishindo, hata CCM mpeleke viongozi wenu wote kwenye kampeni za kuyatetea majimbo hayo. Hii ina maana hawa mapacha watatu, ni over and above CCM chama.

Pamoja na yote, nimefurahishwa na jinsi ulivyo bold kwa chama chako, watu wenye boldness ya kiwango chako ni asset kwa chama chochote. Hoja ya kMimi sina chama, ila nilisema nafuatilia kwa karibu sana huku kujivua gamba ili kujiaminisha CCM inao ubavu, iko serious kurudi kwenye the right track ya kuaminiwa na wananchi ili mwaka 2015, iendelee kupewa ulaji.
Big Up!

Wasalaam.

Pasco.
 
hivi nyie mkifukuza hao watu watatu mnafikiri ndio mtapendwa tena na watanzania????????????sisi tunataka mkapumzike mmechoka
hamna jipya mijitu ya ovyooooo!!!!!
 
Surely.......I like this Boldness from you Billy..........damn!.....hands down Mkuu...heshima mbele....
 
Kobello: Century Gothic]Katiba ya CCM imeonyesha wazi ni watu wa aina gani wanatakiwa wawe viongozi wa chama na serikali,sehemu ya kwanza ibara ya 5,kuanzia kifungu cha 3 na kuendelea vinaonyesha bayana kuwa uongozi uliokuwepo haufuati katiba na kanuni za chama na tukiungana wanachama tunaweza kuwapeleka mahakama kuu, ku question na ultimately dissolve their leadership based on contitutionality
Mkuu Kobello, kimantiki na ukomavu wa demokrasia hivyo ndivyo inatakiwa,lakini kwa mfumo wa vyama vyetu vya siasa ni 'impossible'.Nikukumbushe kuwa mapacha watatu walikuwa ndani ya CC na NEC. Walijua kuwa maamuzi ya serikali yanaanzia ndani ya chama. Sasa kama Chenge ndiye mkuu wa nidhamu utaanzaje kwenda mahakamani kabla hujavuliwa uanachama? Nikupe mfano hai, Spika Sitta na Richmond si unaona walivyotaka kumnyang'anya kadi. Mfano wa pili wabunge wa CCM hubaki kusema ndiyooo hata kama nchi inauzwa kwasababu ukisema hapana unanyang'anywa kadi. Mfano wa tatu Sumaye alipoanza kusema kama mtanzania si unaona alivyoshukiwa na chama, na mwisho Jiulize RA mwenye mabilioni kwanini ang'anganie NEC ya posho ya dola 50?

Babu Atakusema: ana hoja kuwa katiba haifuatwi kwasababu katiba sasa ni 'pesa' na ni mapacha watatu walioanzisha na kudumisha utamaduni huo kwa kile kinachoitwa 'mtandao'. Ukisimamia katiba mtandao una 'ku deal', yupo RA, EL na mkuu wa nidhamu CH, utatokea wapi huku wajumbe wote wakipata magao wao unaotoka kwenye wizi wa mali zetu.
Babu anasema aliyepaswa kunyoosha hali naye ni 'beneficiary' sasa katiba ipi itafuatwa ikiwa aliyekabidhiwa 'mwenyekatiba' hawezi kuifuata?
Nitakupa mfano, katika kuhoji mapacha zigo ametupiwa Mzee Msekwa kwasababu mwenye kigoda anaona haya na nafsi inamsuta.

Mkuu Pasco: Suala kubwa ni kuwa kuna kanuni na sheria. Kanuni ni makubaliano ya washirika au wanachama na zinatoa kitu kinaitwa maadili. Kimaadili kiongozi anapotuhumiwa anatakiwa akae pembeni ima kupisha uchunguzi, atuhumiwe au asafishwe, na zaidi kuokoa chama na aibu inayotokana na tuhuma hata kama hazijathibitishwa kwani kuzinasibisha tu ni kuchafua chama.

Mapacha watatu walitakiwa waachie ngazi za uongozi wenyewe, lakini wamegoma ndipo kanuni zinatumika kuwa basi ikiwezekana wafukuzwe kwani uwepo wao unaokiuka maadili utaleta sintofahamu kama tunazoziona sasa.
Ama sheria za wao kupelekwa mahakamani sio suala la chama bali serikali, ni kwa mazingira niliyoyaeleza awali,serikali kuwachukulia hatua ni mzigo kwani rafiki ndiye anapaswa awapeleke mahakamani na wao wamesema'mwaga mboga sisi tunamwaga ugali'.

Kwa mfumo wa vyama vyetu vya siasa unapokuwa na chama kichafu unakuwa na serikali chafu, kwahiyo safisha lazima ianzie ndani ya chama. Kwavile wamekubaliana mambo yao yanamalizwa ndani ya vikao,maamuzi ya kuwatimua yaliyotoka ndani ya vikao wayaheshimu kwasababu wameshindwa kuwajibika wenyewe na uwepo wao ni maafa kwa CCM na taifa.

Kikwazo si sheria au uthibitisho bali ni 'go ahead' kutoka kwa mkuu.Sote tunajua hawa ni wahalifu lakini tuanzie wapi na nguvu zipi endapo mzee ana nguvu zote ikiwa ni pamoja na za kutufungia mahabusu hata kama hakuna sababu!
 
- Niwe mkweli tu kwamba hilo halitakuja kutokea hata siku moja!, lakini ahsante sana kwa ukaribisho!

William @ NYC, USA.

Kwa hiyo wille wewe ni CCM tu hata ikifa,hata ikiendelea kufanya upupu iliouanza..CHAMA sio kabila waweza badili kama ulichopo hakifuati misingi ya haki na utawala bora....Sidhani kama una sababu za msingi za kutokukiacha chama cha magamba...ni dhahiri unamuenzi mzee..hapa haiko sawa,kuna wakati huwa tunalazimika kuwa tofauti hata na wazazi wetu pale tunaposimama katika kweli na haki....Na kikubwa wille naelewa propaganda chafu za CCM umeziweka kwenye mind yako kama reality,kwamba CHADEMA chama cha kikabila na kidini..Nimalize kwa kusema kama hautajiunga na CHADEMA basi nikutakie kila la kheri katika ku reform hicho chama chenu..ila wewe ni mdogo sana ndani ya CCM ni unajidanganya kusema una reform..CCM inaadhibiwa na MUngu kwa mabaya waliyoyafanya na Mauti ya CCM yatatoka ndani ya CCM..Well,inawezekana haunielewi ila si mbali sana,wataanza kunyamazishana kwa kuuana na kadhalika,ila siri kubwa na nzito zitakazokivuruga na kukiangusha chama zitaanikwa....ALL THE BEST IN SHAPING THE MAGAMBA'S PARTY,THOUGH TO ME YOU ARE GIVING YOURSELF HOPES OF PUSHING A 1 METRE THICK CONCRETE WALL BY YOUR TWO HANDS..
 
Chama kinaendeleaje NY City? Si mlianza kwa madai ya kuvua magamba! Endeleeni salama na kuuza nchi na utu wetu! Kumbuka historia haitakaa ikukumbuke kwa kuwa upande wa wanyanyasaji...
 
Remember, mapacha watatu walikua kwenye system mda mrefu sana. Wanajua mema na mabaya yote ya chama na viongozi wake. Ndio maana wanadiriki kusema mwaga ugali tumwage mboga. Leo ukiwafukuza kikatili unategemea nini? labda wauawe ili wanaobaki wawe salama. HAKUNA MSAFI CCM. Kinachofanywa sasahivi ni kuhakikisha mapacha wana-step down kwa amani ili kuwafurahisha wananchi na kulinda uovu wa chama usivuje.
 
Mkuu Mkandara, binafsi siungana na Will katika hili na nitamjibu separate. Kama ni kweli nhi yetu inaongozwa na utawala wa sheria, hawa mapacha watatu, waadhibiwe kwa kosa gani?.

Kama Mramba ana kesi ya ufisadi mahakamani na na JK huyu huyu ndio amesimama kumnadi kabla hajaangukia pua, leo JK huyu anayewanadi watuhumiwa ili hali kesi zao ziko mahakamani, ana ujasiri gani kuwatimua mapacha watatu ambao hawana kesi yoyote mahakamani?.

Kwenye posti hii, mimi nimeipenda ile hoja niliyoibold, Ile kasi yote ya JK mwanzoni, iliwezekana tuu kwa vile Lowassa was behind, JK mwenyewe as JK si lolote, si chochote, he is a weak leader na sio kwamba hawezi kuwafanya chochote hawa jamaa, bali hana ubavu huo!. Period.

Mkuu Pasco,

Nimefuatilia michango yako na kwa kiwango kikubwa nakubaliana na wewe isipokuwa pale unaposema kuwa William ni bold enough eti kwa haya anayoyasema humu. Mimi sioni ujasiri wowote zaidi ya kutaka kupima joto na kiwango cha hasira za watu wanaofura kwa kuona kinachoendelea ndani ya nchi yetu kwa sababu ya mambo ya kipuuzi yanayofanywa na CCM. Ninazo sababu tatu kuonesha kuwa kujivua gamba ni attemp isiyowezekana hata kwa mtutu!
1. Wale wanaowashikia bango wenzao ama wametajwa kwenye lists of shame (part 1 and 2) na kwa hiyo hakuna anayeweza kumnyooshea kidole mwenzake. Na kama kuna aliyekashifiwa na hiyo list angeshaend mahakamani. Kwa vile hakuna aliyeenda basi hizo lists ni authentic (au nakosea???). Pia hata wale ambao hawakutajwa kwenye hizo lists, bado pandora box ikifunguliwa watajikuta nao wamenaswa na mtego wa panya wa kifisadi ndani ya CCM.
2. Kauli za Aliyekuwa karibu sana na JK, waziri wa zamani wa Utawala bora, Mama Sofia Simba zinahitimisha hoja zote. Kwamba ndani ya CCM hakuna aliye msafi (kuna anayebisha??) na pili kwamba Lowasa ni mwanamume wa shoka (sijui alitumia vigezo gani ila naamini echo yake inajulikana ndani ya CCM)!!
3. Matendo na maneno ya JK hayajawahi kunishawishi kwamba anao ujasiri wa kushughulikia ufisadi. Ukimwona anaongelea haya mambo mazito na kama wewe ni mwangalifu basi utagundua kuwa hamaanishi anayoyasema. Ndio maana anatumia maneno katibia 100 kuongelea kitu kimoja tu na misemo kibao tu isiyo na mshiko.

Kwa hayo niliyoyataja hapo juu (mnaweza kuongeza na mengine) hakuna kitu kama kuvua gamba perse!

Katika hili nitabaki kuwa Tomaso milele!!
 
Tatizo kubwa la CCM ni kuwa tumbili kutaka kuficha macho wakati mwili mzima u wazi. RACHEL wanamakosa ya wazi ndani ya serikali ya Rada, EPA, Richmond nk. kuliko kutumia kiini macho ambacho hakiwezekani kwa nini wasishitakiwe ili sheria iwaondoa mpaka ubunge achana na uongozi wa CCM?

Ila CCM wanaogopa kwani huwezi kumshitaki mwizi mwenzako atakutaja mtaunganishwa kwenye kesi, huwezi kumfukuza mtu aliyekulisha miaka yote kwa wizi huku ukijua mnaiba wote, unampa michongo baraka na ulinzi, na akileta mnagawana na kulinda Chama kiendelee kustawi. Mmesaidiana kuiba mpaka demokrasia, leo hii umwambie auondoke sioni, hawakujua walifanyalo.

Kifo cha CCM kipo mikononi mwa mapacha 3. Kama kutakuwa na uthubutu wa kuwafukuza, CCM itachanika vipande vingi mwishowe kufa, Wakiendelea kubaki na mapacha + mafisadi wengine wengi ndani ya CCM, chama hicho ni pinzani soon. Moto juu moto chini.

Tatizo ni serikalio butu, mfu na kulindana.
 
Tuwe serious! C c M imechokaaa, na kawaida la kuvunda halina ubani. Yule mnajimu anajua hata tungefukiza ubani toka maskati
 
William hapo naomba nitofatiane na wewe, ni either mkuu anahusika moja kwa moja, au anahusika kwa njia tofauti ndio maana anaohopa kuchukua hatua sahihi.........kumbuka reaction yake baada ya Lowasa kujiuzulu yeye alisema "ni ajali ya kisiasa" pia wateule wake waziri mkuu na IGP wote wameshakiri hadarani kuwa mafisadi hawakamatiki na Pinda akasema wakikamatwa nchi itatikisika

yeye akiwa mkuu wa nchi kwa nini asamuru majina ya wamiliki wa Kagoda yawekwe hadharani?.....imethibitika ule mgodi wa kiwira ni ufisadi wa Mkapa, yeye kachukua hatua gani zaidi ya kusema kuwa "mwacheni mzee apumzike"??....inawezekana ni kweli katiba iliyoko sasa inamlinda mh.mkapa lkn yy anaweza akaanzisha mchakato wa kuondoa hiyo kinga ili siku za usoni wezi wa mali za taifa wasiwe na kinga.....CCM wameshasema mara nyingi kuwa mtu hawezi kuwa mwizi hadi atakapothibitika mahakamani, JK kama mwenyekiti wa chama tawala na mkuu wa nchi kwanini asitoe order DPP aanzishe prosecution kwa hao watu, yeye anahofu nini???....ndio maana mimi nitaendelea kuamini kuwa huyu rais anahusika

- Mkuu sana wrong reading ya our politics, kwa sababu kwanza lazima ujiulize nani aliyemtoa Lowassa Uwaziri Mkuu, nani alimnyima Lowassa umakamu wa Mwenyekiti wa CCM, na nani aliyemtoa NEC, na CC, halafu ni kwa nini Rais hakuhudhuria harusi ya mtoto wa Lowassaa, halafu pia kuna politics za jimbo lake Lowassa la uchaguzi, ndio maaana ninakataa kabisa kumuhusiha Rais na mafisadi, hivi kweli Kikwete angetaka kuwa Billionea jamani nani angemzuia?

- Ninasema hivi Rais Kikwete, sio fisadi na wala hamuogopi kiongozi yoyote!

William @ NYC, USA.
 
Willy,
Mkuu wangu shukran sana kwa kuweka ukweli huu ambao hauna ushabiki labda tu mtu apende kushabikia..Sisi wote hapa tunaomba hawa mapacha watiwe ndani kama walivyotangulia kina Yona na Mramba kwani tuna ushahidi mkubwa zaidi dhidi yao na mahla pekee panapoweza kuthibitisha kwamba wao ni innocent/Guilty ni mahakamani na as long as they are presumed innocent hakuna sheria inayokataza kukamatwa kwao.Hatuwezi kukataa ukweli huu kwa sababu ati kuna Mafisadi wengi CCM ama nchini kwani kama ingekuwa hivyo tusinge wakamata hata wezi maanake wapo wengi.

Nakumbuka wakati JK anaingia madarakani alisafisha Polisi na kukamata majambazi kiasi kwamba tuliweza kusafiri, kulala na kutembea kwa amani ingawa sii majambazi wote walokamatwa isipokuwa ilitoa onyo kali kwa majambazi. Na katika majambazi hao wapo walioshinda kesi zao na wengine kupelekwa lupango ndivyo sheria inavyo operate.

Na hata walipokamatwa Yona na Mramba, mkuu wangu rushwa iliogopwa kama ukimwi na kwa mara ya kwanza ilikuwa ukienda ofisi za serikali utahudumiwa haraka na bila kutoa rushwa. Lakini pamoja na yote haya hivi vilikuwa vita vya Titans, kumbe ilikuwa kugombea nafasi za Kufisadi lakini toka Lowassa ameondolewa madarakani serikali ya JK imekwenda likizo, yaonyesha JK hawezi kuongoza pasipo Lowassa na mtandao. Serikali hii imekuwa sii ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo Ujambazi na Ufisadi umerudi tena kwa kasi baada ya serikali kwenda rikizo.
CCM na JK kama kweli mnataka kujuvua magamba kukomesha Ufisadi basi ile ile dawa ya Lowassa na Sokoine itumike kupambana na Ufisadi kwani inawezekana. Sumu ya nyoka pia ni snake venom antidote!

- Mkuu Bob maneno yako ni mazito sana, lakini ninachokiona mimi ni style tofauti za uongozi kati ya Lowassa na Pinda, Lowassa media ilikuwa involved sana, lakini Pinda sio hivyo lakini wote ni wachapakazi sana, Rushwa labda maeneo ya chini kwa sisi wananchi, lakini kwenye level za juu hapana siku hizi mawaziri wanaogopa sana rushwa na hakuna anayeitaka tena, isipokuwa tu taifa hili hatuhitaji kiongozi mchapakazi ambaye sio muaminifu!

William @ NYC, USA.
 
- Mkuu sana wrong reading ya our politics, kwa sababu kwanza lazima ujiulize nani aliyemtoa Lowassa Uwaziri Mkuu, nani alimnyima Lowassa umakamu wa Mwenyekiti wa CCM, na nani aliyemtoa NEC, na CC, halafu ni kwa nini Rais hakuhudhuria harusi ya mtoto wa Lowassaa, halafu pia kuna politics za jimbo lake Lowassa la uchaguzi, ndio maaana ninakataa kabisa kumuhusiha Rais na mafisadi, hivi kweli Kikwete angetaka kuwa Billionea jamani nani angemzuia?

- Ninasema hivi Rais Kikwete, sio fisadi na wala hamuogopi kiongozi yoyote!

William @ NYC, USA.

kaka kumbe na wewe huwa una--- zidumu fikra za mwenyekiti, adumu mtukufu rais
 
mwaha mbukenyi
mimi nikushukuru kwa maoni yako na siamini kama ni wewe umeweza kutoa maoni kama hayo kwa uwazi zaidi pasipo kumwangalia nyani usoni

tunahitaji sana watu kama nyie,kwani ndani ya CCM waliowengi wanaogopa kusema ukweli kwa kuhofia kuhojiwa ama kuwekwa pembeni na chama
hii nchi tunahitaji vijana kama nyie wenye uwezo wa kusema black and white pasipo kumung'unya maneno,nalielewa hilo kwa kuwa nimetokea huko,wanachama waliowengi wamekuwa ni wa kusema ndio mzee pasipo kuhoji hata kitu chochote kile

nazidi kukuombea,endelea kutoa somo kwa wana CCM watambue kuwa kila kitu kitapiata,hakuna jambo lisilokuwa na mwisho

pamoja daima,kwa pamoja tutafika
 
Mkuu William, kwanza siungani na wewe kuhusu kufukuzwa kwa hawa mapacha watatu, unataka wafukuzwe kwa kosa gani?. CCM si ndio chama tawala, kama hawa mapacha wana makosa, si muwafikishe mahakamani?. Kama Mramba ambaye tayari anayo kesi mahakamani, Mwenyekiti wako alisimama kumnadi kabla ya wananchi kukataa kwa kura kulikopelekea kuangua pua, sasa CCM ina ujasiri gani kuwaadhibu watu wasio na hatia?!.
Kama ni kweli unafahamu The Rule of Law, kwanini tuwaadhibu kwa kuwafukuza watu wasio na kosa lolote, halafu ndipo tuwafikishe mahakamani?. Kama wana makosa, kwanini kwanza tusiwashitaki kwa makosa hayo, wakisha hukumiwa ndipo tuwafukuze?. As far as the rule of law is concerned, hawa mapacha watatu are all clean.
William, mbona hapa unajikanganya, haiwezekani wewe kwenye posti hii moja hapa ukasema hivi "Mahojiano ya nini! mbona walishawaweka pembeni kwenye nafasi muhimu sana za ndani ya chama bila mahojiano? I mean sasa ni wakati wa CCM kutangaza kwamba imewafukuza tayari au ikubali kwamba haina huo ubavu!", halafu kwenye posti hiyo hiyo wewe wewe tena ukasema hivi Legal Facts ili haki zao watuhumiwa zisikiukwe, I mean we are not asking for a Mob Justice, au blind Justice! hapana tunataka Fairness Justice", which is which?!. Principle ya kwanza ya Natural Justice ni "No one is condemned unhead", nadhani hiki ndicho chama chako kinachotaka kufanya, wewe unataka wahukumiwe kwa tuhuma tuu au shutuma bila kosa lolote?.

William, kwa vile wewe ni CCM damu, umezaliwa CCM, umekulia CCM, na sasa unajiandaa kuifia CCM kwa uanzishaji hilo tawi huko ulipo, kwa hayo nilidhani, unaifahamu vizuri CCM kwa undani wake, kitendo cha kushauri hawa mapacha watatu wafukuzwe kabisa CCM, ni uthibitisho wangu tosha kumbe hata wewe huijui CCM!, ukidhani CCM inao ubavu wa kuwakuza uanachama. Kwa kukusaidia tuu, CCM haina ubavu huo, na hata kama CCM itaamua kuwafukuza ili kuwa 'sugar coat 'waTanzania kuwa CCM inaweza, nakuhakikishia, hao jamaa wote watatu wakisimama tena kwenye majimbo yao, kupitia vyama vyovyote, watayataa tena majimbo yao kwa ushindi wa kishindo, hata CCM mpeleke viongozi wenu wote kwenye kampeni za kuyatetea majimbo hayo. Hii ina maana hawa mapacha watatu, ni over and above CCM chama.

Pamoja na yote, nimefurahishwa na jinsi ulivyo bold kwa chama chako, watu wenye boldness ya kiwango chako ni asset kwa chama chochote. Hoja ya kMimi sina chama, ila nilisema nafuatilia kwa karibu sana huku kujivua gamba ili kujiaminisha CCM inao ubavu, iko serious kurudi kwenye the right track ya kuaminiwa na wananchi ili mwaka 2015, iendelee kupewa ulaji.
Big Up!

Wasalaam.

Pasco.

1. Mapacha watatu wafukuzwe CCM kwa sababu zilizowafanya waondolewe kwenye NEC na CC, na pia Lowassa kukimbia uwaziri mkuu bila kufukuzwa, na kujihusisha kwao sana kukivuruga chama ambapo kuna ushahidi wa kutosha sana, wafikishwe kwenye sheria na Jamhuri kwa sababu sio kazi ya CCM kuwafikisha mahakamani nafikiri unaelewa sana Katiba inasema nini on that.

2. Nimesema kitendo cha Rais kwenda kuwanadi kwenye kampeni za uchaguzi ilikuwa wrong na pia a political mistake ambayo tayari Rais paid for kwa kupungukiwa sana kura za ushindi kuliko term ya kwanza, lakini haina maana yuko nao mafisadi hapana!

3. Kama mapacha watatu they are clean then let the law say that, kamati ya bunge haikusema hivyo, BAE haikusema hivyo, Ripoti ya Richmonduli haikusema hivyo, Ripioti za Dowans hazikusema hivyo, hao watatu sio wasafi hata kidogo ni wachafu sana!

4. CCM inao ubavu wa kuwafukuza kama ilivyowaondoa kwenye NEC na CC, kwa taarifa yako ni kwamba between jana na leo nimefahamishwa rasmi kwamba wamesahapewa barua, kwa hiyo it is the matter of time tu! Halafu ya mimi kujikanyaga hayapo nimesema kwanza wafukuzwe chama maana chama kinaweza tu kwuafukuza lakini chama hakiwezi kufikisha mahakamani kwa sababu hawakuiba hela za CCM, wakishafukuzwa CCM basi Serikali ina wajibu wa kuwapeleeka kwenye sheria, naona hapo umejikanyaga mwenyewe either ka kutoelewa au kwa makusudi.

5. Mapacha watatu hawana ushawishi wa kisiasa, isipokuwa wana pesa nyingi sana, ndio maana wakigombea wanaweza kushinda, lakini Lowassa akiondolewa kule jimboni, itampa nafasi nzuri sana Joseph Sokoine kushika lile jimbo, na huku kwa Rostam huyu mkuu wa madini atahsika lile jimbo bila tatizo na kule kwa Chenge wapo wengi sana CCM walikuwa wanasita sana na hili, lakini sasa wameshalipatia jibu, nimehakikishiwa kwamba wameshapewa barua, so!

Well, Pasco you siku zote kwamba you have my respect, karibu sana tulisaidie taifa letu
!

William @ NYC, USA.
 
Remember, mapacha watatu walikua kwenye system mda mrefu sana. Wanajua mema na mabaya yote ya chama na viongozi wake. Ndio maana wanadiriki kusema mwaga ugali tumwage mboga. Leo ukiwafukuza kikatili unategemea nini? labda wauawe ili wanaobaki wawe salama. HAKUNA MSAFI CCM. Kinachofanywa sasahivi ni kuhakikisha mapacha wana-step down kwa amani ili kuwafurahisha wananchi na kulinda uovu wa chama usivuje.

- CCM ni chama cha siasa sio cha mitulinga so maamuzi yake mengi hufanyika kisiasa, tupo wasafi wengi sana CCM hakuna wa kuwaga anything wameondolewa NEC na CC na sasa wameshapewa barua za kuondolewa CCM, karibu sana mkuu!

William @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom