Uovu Ndani ya CCM ni Imani Inayowaunganisha Waovu

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Ni nadra kabisa au hata tuseme haiwezekani kabisa, kuwe na uovu mkubwa kabisa kama vile wizi wa pesa ya umma, CCM isihusike. Na wengi ndani ya CCM, umoja wao umejengeka katika uovu. Na waovu wengi wanaiona CCM ndiyo pango salama la kujificha bila kusumbuliwa.

Kuanzia EPA mpaka ufisadi unaotajwa na CAG kila mwaka, lazima CCM inahusika. Ndiyo maana siku zote kukifanyika kitu ambacho CCM haitaki, lazima utasikia tamko la chama. Lakini huwezi kusikia tamko la CCM dhidi ya ugisadi unaoibuliwa na CAG. CCM miaka yote ndiyo inayounda Serikali, lakini huwezi kusikia CCM ikitoa kauli yoyote nzito dhidi ya mafisadi wanaotajwa kwenye report za CAG kwa sababu watu hao ni makada wao, na walichokifanya ni ndani ya imani inayowaunganidha.

Hayati Mkapa (RIP), siku zake za mwisho wa maisha yake Duniani, katika kitabu cha maisha yake, alitaja baadhi ya mambo ambayo alikuwa anajutia: moja alisema ni kuidhinisha wizi wa pesa ya umma kuipa CCM na mauaji ya Zanzibar. Wizi wa EPA ulihusiasha viongozi Nna makada wakubwa wa CCM. Wizi wa Kagodi ulihusisha wakubwa wa CCM. Na hata mikataba ya ufisadi mkubwa lazima ihusishe wakubwa wa CCM.

Hata ule mkataba mbaya kabisa kuwahi kutokea kwa taifa letu, mkataba wa DPW umehusisha wakubwa wa CCM, na umepongezwa na CCM, licha ya ukweli kuwa lile jinamizi la IGA linaendelea kusimama, na DPW ana haki ya kulitumia wakati wowote atakapoamua, uwezekano mkubwa ni hapo CCM itakapoondolewa. Wakati mkataba wa bandari ni wa miaka 30, IGA ambayo ndiyo mkataba mkuu, haina ukomo. Wajinga wamepofushwa na mkataba mmoja wa bandari, na kusahau uovu mkubwa uliopo kwenye IGA.

NCHI HII NI UOVU GANI MKUBWA ULIFANYIKA BILA YA CCM KUHUSIKA?

Bila ya kuja kuiondosha CCM, jitihada zote za Taifa hili kuondoka katika uduni wa maendeleo ni ndoto.

Kazi kubwa ya kiongozi, ni kuwapeleka anaowaongoza kwenye maono yake, sasa mna chama na viongozi waliobobea kwenye uovu, watu ambao wakati wote wanafikiria kuiba, kudhulumu haki za watu na maamuzi ya umma, watu wa namna hiyo, tunatarajia watupeleke wapi zaidi ya kulifanya Taifa zima kuangukia katika uovu wa dhuluma mbalimbali?

Wapi iliwahi kutokea watu wema, wakaliambia jambazi liache ujambazi, halafu na jambazi likasema, sawa sawa nimesikia maelekezo yenu, kuanzia leo naacha ujambazi? Sheria zote mbaya za nchi hii, zikiwemo zile zinazopalilia wizi wa kura na na maamuzi ya wananchi kudharauliwa, zimeundwa na CCM kwa nia ya kurahisha dhuluma dhidi ua umma. CCM ni chama jambazi dhidi ya haki, demokrasia na utawala wa sheria, halafu sisi tunaamini tunaweza kufanya makubaliano na jambazi aache ujambazi. Ni ndoto. Kama tunataka kuondokana na jambazi, ni lazima tujitoe na tuape kuwa iwe kwa shari au amani, katiba mpya lazima ipatikane, tume huru ya uchaguzi ipatikane, sheria nzuri ya uchaguzi wa haki ipatikane na iheshimiwe.

JAMBAZI HUWA HAPIGIWI MAGOTI BALI HUFURUSHWA AU HULAZIMISHWA KUBADILIKA, PEMBENI KUKIWA NA TISHO LA KUFURUSHWA KWA NGUVU KUTOKA KWA WANAODHULUMIWA.

Watu wanatakiwa kuheshimiwa sheria nzuri na za haki, lakini wana wajibu na haki ya kuzidharau na kuzipuuza sheria zote zinazotengeneza mazingira ya kuwanyang'anya haki na mamlaka yao.
 
Lakini pia wapo watawala wa haki. Fikiria mfalme Sulemani.
Mfalme Suleiman alikuwa anaongea na Mungu wa mbinguni

Ila akina Mbowe na Makonda kila Siku wanasimikwa Uchifu wa miungu tofauti tofauti katika hii Dunia
 
Ccm ndio adui namba moja wa Tanzania tangu enzi za uhuru wa Tanganyika hadi kesho
 
CCM ni kusanyiko la watenda maovu.

Hata humu JF, wafia CCM wote wana vimelea vya ushetani. Ndiyo hao kukitangazwa kutakuwa na mikutano au maandamano ya umma kupinga uonevu wa Serikali, utawasikia wanashabikia na kuhamasisha polisi ifanye uharamia: mara utawasikia wakisema wanataka polisi wawapige virungu watu watakaohudhuria, wengine utawasikia eti watakaohudhutia wakamatwe wapelekwe magerezani wakanyee debe, n.k. Ni watu ambao roho zao zimejaa uovu.
 
Ccm ndio adui namba moja wa Tanzania tangu enzi za uhuru wa Tanganyika hadi kesho

Hata wafanyabiashara haramu wakubwa wote, ama ni viongozi wa CCM, makada wa CCM au wafadhili wakuu wa CCM. Wafanyabiashara haramu wa pembe za ndovu, wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya na wafanyabiashara wakubwa wa biasha haramu ya binadamu, wote ama ni makada au ni viongozi au wafadhili wakubwa wa CCM.

CCM ni mahali salama kwa waovu wakubwa.
 
Ni nadra kabisa au hata tuseme haiwezekani kabisa, kuwe na uovu mkubwa kabisa kama vile wizi wa pesa ya umma, CCM isihusike. Na wengi ndani ya CCM, umoja wao umejengeka katika uovu. Na waovu wengi wanaiona CCM ndiyo pango salama la kujificha bila kusumbuliwa.

Kuanzia EPA mpaka ufisadi unaotajwa na CAG kila mwaka, lazima CCM inahusika. Ndiyo maana siku zote kukifanyika kitu ambacho CCM haitaki, lazima utasikia tamko la chama. Lakini huwezi kusikia tamko la CCM dhidi ya ugisadi unaoibuliwa na CAG. CCM miaka yote ndiyo inayounda Serikali, lakini huwezi kusikia CCM ikitoa kauli yoyote nzito dhidi ya mafisadi wanaotajwa kwenye report za CAG kwa sababu watu hao ni makada wao, na walichokifanya ni ndani ya imani inayowaunganidha.

Hayati Mkapa (RIP), siku zake za mwisho wa maisha yake Duniani, katika kitabu cha maisha yake, alitaja baadhi ya mambo ambayo alikuwa anajutia: moja alisema ni kuidhinisha wizi wa pesa ya umma kuipa CCM na mauaji ya Zanzibar. Wizi wa EPA ulihusiasha viongozi Nna makada wakubwa wa CCM. Wizi wa Kagodi ulihusisha wakubwa wa CCM. Na hata mikataba ya ufisadi mkubwa lazima ihusishe wakubwa wa CCM.

Hata ule mkataba mbaya kabisa kuwahi kutokea kwa taifa letu, mkataba wa DPW umehusisha wakubwa wa CCM, na umepongezwa na CCM, licha ya ukweli kuwa lile jinamizi la IGA linaendelea kusimama, na DPW ana haki ya kulitumia wakati wowote atakapoamua, uwezekano mkubwa ni hapo CCM itakapoondolewa. Wakati mkataba wa bandari ni wa miaka 30, IGA ambayo ndiyo mkataba mkuu, haina ukomo. Wajinga wamepofushwa na mkataba mmoja wa bandari, na kusahau uovu mkubwa uliopo kwenye IGA.

NCHI HII NI UOVU GANI MKUBWA ULIFANYIKA BILA YA CCM KUHUSIKA?

Bila ya kuja kuiondosha CCM, jitihada zote za Taifa hili kuondoka katika uduni wa maendeleo ni ndoto.

Kazi kubwa ya kiongozi, ni kuwapeleka anaowaongoza kwenye maono yake, sasa mna chama na viongozi waliobobea kwenye uovu, watu ambao wakati wote wanafikiria kuiba, kudhulumu haki za watu na maamuzi ya umma, watu wa namna hiyo, tunatarajia watupeleke wapi zaidi ya kulifanya Taifa zima kuangukia katika uovu wa dhuluma mbalimbali?

Wapi iliwahi kutokea watu wema, wakaliambia jambazi liache ujambazi, halafu na jambazi likasema, sawa sawa nimesikia maelekezo yenu, kuanzia leo naacha ujambazi? Sheria zote mbaya za nchi hii, zikiwemo zile zinazopalilia wizi wa kura na na maamuzi ya wananchi kudharauliwa, zimeundwa na CCM kwa nia ya kurahisha dhuluma dhidi ua umma. CCM ni chama jambazi dhidi ya haki, demokrasia na utawala wa sheria, halafu sisi tunaamini tunaweza kufanya makubaliano na jambazi aache ujambazi. Ni ndoto. Kama tunataka kuondokana na jambazi, ni lazima tujitoe na tuape kuwa iwe kwa shari au amani, katiba mpya lazima ipatikane, tume huru ya uchaguzi ipatikane, sheria nzuri ya uchaguzi wa haki ipatikane na iheshimiwe.

JAMBAZI HUWA HAPIGIWI MAGOTI BALI HUFURUSHWA AU HULAZIMISHWA KUBADILIKA, PEMBENI KUKIWA NA TISHO LA KUFURUSHWA KWA NGUVU KUTOKA KWA WANAODHULUMIWA.

Watu wanatakiwa kuheshimiwa sheria nzuri na za haki, lakini wana wajibu na haki ya kuzidharau na kuzipuuza sheria zote zinazotengeneza mazingira ya kuwanyang'anya haki na mamlaka yao.
Ukiwa mtu mkweli kabisa usiye na hata chembe ya unafiki, ukifanya uchunguzi wa kina kabisa kuhusu watu hao, lazima utakubaliana nami kwamba CCM ni Kusanyiko la Mahasimu au Kusanyiko la Waovu. Siyo Siri hata kidogo, ndani ya hivi vyama vya Siasa hasa hasa CCM watu Wanachukiana sana kupita kiasi, hawapendani hata kidogo na wamekuwa Wakifanyiana kila aina ya fitina, hujuma, na uovu mbaya sana. Tena wamekuwa wakifanyiana uovu mbaya wa Shetani, kamwe hawaaminiani hata kidogo, kila mtu huko amekuwa akimhofia mwenzake kwamba anaweza akamdhuru kwa namna mbalimbali kama vile kuwekewa sumu kwenye vyakula, maji, pombe au hata kurogwa. Uovu wa aina hii wamekuwa wakifanyiana sana huko, hasa katika nyakati za Uchaguzi wa kisiasa. Yaani ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom