My opinion: CCM fukuzeni mapacha watatu sasa au nyamazeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

My opinion: CCM fukuzeni mapacha watatu sasa au nyamazeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Jun 4, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  Facebook: William Malecela on Saturday, June 4, 2011 at 8:13am

  @ NEW YORK CITY-USA: Nimeshitushwa sana na habari za CCM kuwaita Mapacha Watatu eti kwa mahojiano!, I mean mahojiano ya nini? Wananchi wa hili taifa tumechoshwa sana na hivi viini macho. Ni CCM wenyewe walio-raise the bar kwa kutangaza kujivua magambas na ni CCM iliyotangaza kuwaondoa kwenye NEC yake na CC, as a member of CCM I was incouraged na the news kwamba CCM ipo njiani kuwafukuza chama kabisa, sasa tena tunaposikia habari za mahojiano inaleta utatanishi! Mahojiano ya nini! mbona walishawaweka pembeni kwenye nafasi muhimu sana za ndani ya chama bila mahojiano? I mean sasa ni wakati wa CCM kutangaza kwamba imewafukuza tayari au ikubali kwamba haina huo ubavu!

  - I mean nothing personal, na sio kwamba kufukuzwa kwa hao mapacha watatu kutaondoa matatizo ya wananchi kwa siku moja, lakini tunategemea kwamba wakishavuliwa uanachama wa CCM, ifuatie kuwapeleka kwenye mkono wa SHERIA!. Tanzania tunasumbuliwa sana na tatizo moja tu nalo ni hatuna RESPECT KWA THE RULE OF LAW OF OUR LAND!, ndio maana hata huku majuuuu wengi wetu tunaishi kwa taabu sana maana hatujui kuishi kwa kuheshimu sheria. Hawa mapacha watatu wakikiwapelekwa kwenye sheria, ni kwamba sasa unafungua milango ya wanasiasa wahalifu wote nchini kupelekwa kwenye sheria na wananchi kuanza kuheshimu sheria kwanza za Jamhuri, hatimaye wataheshimu sheria za makazini mpaka sheria za familia majumbani mwao, I mean Wa-Tanzania we are too corrupt tunahitaji kuanzia somewhere na hapa kwenye mapacha watatu ndio penyewe sana, So CCM it is either now, or forget it! and Never!

  - CCM the burden is on us na wakati ni sasa, either tufanye kweli au tunyamaze, lakini habari za mahojiano maana yake ni kwamba somebody is not sure kama hawa waondolewe au la! Tunasema hivi sio tu wafukuzwe chama, isipokuwa wafikishwe kwenye SHERIA, na wengine wote wenye tuhuma za wizi wa mali zetu za umma na kodi zetu wananchi, ninasema mali zao zote zingekua frozen now na serikali, mpaka watakapothibitisha kwamba kwa miaka mitano ya uwaziri mtu unaweza kuwa Billionea na kuanza kusomesha watoto nje, na kununua magari ya kifahari pamoja na kuwa na hisa kila mahali kwenye makampuni makubwa na kujenga majumba ya ajabu. Ni muhimu sana kuwepo na Legal Facts ili haki zao watuhumiwa zisikiukwe, I mean we are not asking for a Mob Justice, au blind Justice! hapana tunataka Fairness Justice!

  - So! CCM the time is up, either wafukuzeni chama SASA hawa Chenge, Rostam na Lowassa, au nyamazeni turudie tulipokuwa siku zote yaani kama kawaida, tusubirie kuwa chama cha Upinzani 2015, kama KANU. Na CCM let me tell you this, siku tutakapoishia kua upande wa pili wa the glass, ndio imetoka haitakuja kurudi tena! Uliza UNIP kule Zambia!

  MUCH RESPECT! & MUNGU AIBRIKI TANZANIA!

  William Malecela @ New York City, US.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu: Bado wanajadiliana. Hujui ktk suala la ufisadi kuhusu vigogo ni kujadiliana. Wale dagaa ni mahakamani mara moja!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Lakini kwa nini mapacha watatu tu? Kwani katika CCM nzima hawa ndiyo mafisadi pekee? Serikalini hakuna mafisadi? Kwenye sekta zingine hakuna mafisadi?

  Binafsi siamini kama hawa mapacha watatu ndiyo mafisadi pekee Tanzania.
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu WJ Malecela , kwetu sisi wana CCM tunaona mchezo unaochezwa kama filamu isyoisha na kuna mchezaji myuma ya pazia asiyetajwa ila ndio anaendesha mambo yote.
  Hawa mafisadi watatu hawako peke yao , ni mpaka mchezaji nyuma ya pazia atolewe hadharani kama mwanga ndo mchezo utaeleweka!
  Kwa hakika filamu hii ya mapacha watatu aka RACHEL inakera!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mie pamoja na kwamba nauchukia ufisadi na mafisadi, lakini hii ya mapacha watatu kukataa kujivua gamba inanipa raha sana -- hasa pale inapoonekana jinzi uongozi mzima wa CCM unavyotolewa kamasi za puani na watatu hawa!! Saizi yao kufanyiwa hivyo!!! Mimi nawapongeza sana maana msimamo wao unakifanya chama hicho kuwa kichekesho tu.

  CCM sasa hivi ni kama vile haina viongozi imara wa kuweza kutoa maelekezo/amri na kusikilizwa mara moja -- chama kimebakia kubembelezana katika masuala yoote!!
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Unaonyesha umezidikuparaganyika kisiasa, naomba upumzike kidogo au uende rehab. Tatizo la Tanzania ni CCM yenyewe. Naonaunaanza kutoka kimaslahi kama wanaCCM wenzako. Kumbuka hata mzee wako ni tatizo which means your a problem by implication. Ukitaka mambo yanyooke dissolve your party and put all thieves in jail, which is difficult because you are also an implied thief!
  Branch lako la CCM NY limefika wapi? Umechanganyikiwa wile
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kuna kuondoka kazini kwa kustaafu baada ya kufikisha umri wa kustaafu, kufukuzwa kazi baada ya makosa yako kuthibitiswa na kuachishwa kazi kwa sababu mbali mbali ikiwemo utovu wa nidhamu.

  Sijui hao wanaotakiwa kuondoka toka kwenye ajira zao za kisiasa wanaondolewa kwa sababu ipi? Kama ni "Redandancy" ni kawaida pawepo na maafikiano ya mafao yao kabla ya kuachishwa kazi. La kustaafu hili kwenye siasa ni hiari ya mhusika mwenyewe hivyo sababu hiyo haipo. La kufukuzwa bila makosa yao kuthibitishwa nalo ni gumu kutekelezwa. Kama wanaachishwa kwa utovu wa nidhamu hapa lazima wakubaliane na mafao
   
 8. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa ndio financiers wa CCM na fisadi MKONO.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Si bora wakahalalisha ufisadi? I mean wapeleke mswada Bungeni wa kusema 'ufisadi ruhusa kwani ni masuala ya wa mtu mmoja mmoja binafsi (individual issue)?'

  Mahayawani hawa ambao CCM kinadhani ni Wabunge wao wataupitisha tu mswada huo kutokana na uwingi wao!

  Ni bora kufanya kejeli hiyo kubwa na yaishe kuliko zile ndogo ndogo aet wanachukia ufisadi na wameamua kujivua gamba!
   
 10. J

  JACOBUDA Member

  #10
  Jun 4, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao ni wanachama hai wa ccm!na kila mwanachama ana HAKI ya kusikilizwa pia we cal it NATURAL JUSTICE!wacha wasikilizwe na sekretariat ndio itakayotoa maamuz!
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kaka leo umekuwa objective ndugu yangu more that you have ever said. Hongera sana na safi saaaaaana.
   
 12. a

  alex50 JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Kwa yeyote anefuatilia kwa karibu siasa za Chama tawala, anaelewa kuwa chama hakina ujasiri huo wa kuwaondoa mapacha watatu. Itakuwa inajivua nguo hadharani kwani tatizo sio mapacha watatu, ni mfumo mzima uliotumika kwa miaka takriban 15 wa kupata viongozi, kuanzia chipukizi, vijana hadi CCM, kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka kamati kuu. Asilimia zaidi ya 60 ya viongozi wa CCM ni wafuasi au wamewekwa madarakani na mapacha watatu. Haya ni matunda ya mtandao uliomweka madarakani Mwenyekiti wa Chama. Breki zimefeli mlimani, iliobaki ni kuomba Mungu.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 13. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #13
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Mkuu sana Nyani, katika kipindi cha uongozi wa Awamu ya Nne, hawa viongozi watatu ndio wamefanya ya ajabu yanazozidi wote toka tupate uhuru, kila awamu ina yake Awamu ya kwanza alikuwa Kambona RIP! sasa tunachosema ni kwamba wakianza na hawa inafungua njia ya kuwafikia wengine wote, cha muhimu ni haki zao za kisheria kuheshimiwa!

  - Lakini somebody has to start somewhere!


  William @ NYC, USA.
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Willy
  Tatizo la Tanzania sio hao mapacha watatu tuuu maana wako wengi ila hawavumi. Ubadhirifu ni kila sekta ufisdadi na kula mali za serikali ni kila sehem iwe Bank Kuu iwe halmashauri iwe mashirika ni kila sekta
  Sidhani kama kuwafukuza hao watatu ndo tutakuwa tumetibu mwarobaini wa matatizo au ufisadi
  hao ni kama punje tuu na na isitoshe hatuwatendei haki kwa kuwaonyesha kuwa wao ndo mwarobaini wa ufisadi na matatizo tuliyo nayo.
  Mfumo mzima umeharibika na twapaswa tuutibu kwanza mfumo mzima kabla ya kung'ang'ania kuwasema kuwa hao ndo kila kitu
   
 15. Ditto

  Ditto Member

  #15
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Well William, u deserve my first posting kwenye JF. Thank you so much for this useful thread.. Hope ndugu yetu Nape atakuwa amekusikia.. Tumechoka kabisa kuendelea kusikia huu upuuzi, na kwa vyoyote CCM inabidi wajiandae tu maana hizo siku tisini walizotangaza ndio zimekaribia kuisha.
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280


  Willy nani ana huo uwezo na ujanja wa kufanya hayo maana kama walikuwa na utashi there is no need ya kupeana siku
  Wenye uamuzi wanapopeana siku za kufanya mambo tunakuwa na wasi wasi na uwezo wao wa kuchukua maamuzi maana wana kila power kutoa maamuzi ila wameshindwa kufanya hivyo
  Na yule unayempa siku za kufanya jambo nae anakuona wewe huna nguvu za kufanya kile unachotaraji kufanya maana ulikuw ana nafasi ya kufanya hivyo ila umeshindwa au unamuogopa
  Dhana ya kuogopana na kushindwa kuchukuliana hatua ndio inaelekea kutufikisha kwenye sehem kuwa kila mmoja ana uwezo wa kufanya kile anachokipenda bila kuwa na wasi wasi wa kuchukuliwa hatua zozote
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hihihiiiii, jana nimeota hawa mapacha Watatu wanaimba "Hawaendi popote, CCM for LIFE......"

  Watu wakiwaona hao mapacha, wengine wanapoteza fahamu........ Bad Boys RACHEL wameingia mjengoni.

  No body will stop them now, They ain't going no where.... CCM for life....... I Live this RACHEL.....  William, huyu jirani yako huko NY, Msomali Sean John inabidi umsikilize sana maana nyimbo zake nyingine, zina maana hata Tanzania.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Sasa hivi nipo njiani kuelekea kwenye mkutano wa maandalizi ya ufunguzi wa Tawi, so tupo kwenye the right track, baba yangu hahusiki na anything kama huna cha kuchangia kwenye mjadala wa taifa ni bora ukakaa pembeni ukaachia wanaotaka kuelimishana, kama una tatizo na baba yangu wewe ni kumfungulia topic yake! ha! ha! siku njema sana mkuu!

  William @ NYC, USA.
   
 19. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #19
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Ukitaka kumua nyoka unaanzia kichwani kwanza! hawa mapacha watatu ndio hasa kichwa cha nyoka na magambas!

  William @ NYC, USA.
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Kwa uwazi na ukweli live bila chenga,afadhali wewe umesema bila kificho ,tena zaidi kwenye hili jukwaa,nategemea naye Makongoro Nyerere aje hapa jukwaani awaambie hao mapacha sugu 3 kuwa huko saiti tgumewachoka kwani wao ni nani ,bila CCM hawana jipya ndio maana wanang'ang'ania,tatizo ni mwenyekiti amekuwa muoga mno inaonekana naye si msafi ndio maana anatishwa na kufyata mdomo,jamani CCM si ya mapacha 3 tu .Tujiulize ED kuna nini ikulu unakoshupalia namna hii,na unasiri gani kubwa ambayo unaijua hadi kumtishia 'nyau@mwenyekiti wako ?je huo ndiop ustaarabu wa nyie viongozi wa CCM,hakika naona kiza mbele ya safari kama hao mapacha 3 watabaki CCM,kwanza ni siri iliyowazi kuwa hao 3 ni corrupt,kwanini tunamung'unye maneno,ilibidi wapelekwe segerea full stop.namshangaa mwenyekiti anaposhindwa kutumia mamlaka aliyonayo ,au hayo mamlaka yanatumika tu kwa watu wengine ambao mwenyekiti hawapendi au hawamtishi,hii ni AIBU,je wazee wa CCM kweli mmewashindwa hao jamaa 3?
   
Loading...