My opinion: CCM fukuzeni mapacha watatu sasa au nyamazeni

- Duh! loong time ago! ha! ha! ha!

William.
Duh!, kweli ni long time, mimi sikuamini yule William niliyemsifia kuwa ni bold , ndiye William yule yule niliyekutana naye Dodoma akipiga magoti kuwanyenyekea kina Lowassa kwa heshima zote katika kubembelezea kura za kula!.

Sasa Mkuu William umekuja ground zero, kati ya hoja yako ya CCM iwafukuze now or never na hoja yangu kuwa JK na CCM yake si lolote sii chochote dhidi ya mapacha watatu na hana ubavu wa kuwaondoa!, hoja ipi imesimama?.

Si umekuja na jee sasa si umeyaona mwenyewe?. Jee utaendelea kuling'ang'ania jahazi linalokwenda mrama hadi uzame nalo, ama uko tayari kuwa bold enough kusinama nawe uhesabiwe?.
 
Facebook: William Malecela on Saturday, June 4, 2011 at 8:13am

@ NEW YORK CITY-USA: Nimeshitushwa sana na habari za CCM kuwaita Mapacha Watatu eti kwa mahojiano!, I mean mahojiano ya nini? Wananchi wa hili taifa tumechoshwa sana na hivi viini macho. Ni CCM wenyewe walio-raise the bar kwa kutangaza kujivua magambas na ni CCM iliyotangaza kuwaondoa kwenye NEC yake na CC, as a member of CCM I was incouraged na the news kwamba CCM ipo njiani kuwafukuza chama kabisa, sasa tena tunaposikia habari za mahojiano inaleta utatanishi! Mahojiano ya nini! mbona walishawaweka pembeni kwenye nafasi muhimu sana za ndani ya chama bila mahojiano? I mean sasa ni wakati wa CCM kutangaza kwamba imewafukuza tayari au ikubali kwamba haina huo ubavu!

- I mean nothing personal, na sio kwamba kufukuzwa kwa hao mapacha watatu kutaondoa matatizo ya wananchi kwa siku moja, lakini tunategemea kwamba wakishavuliwa uanachama wa CCM, ifuatie kuwapeleka kwenye mkono wa SHERIA!. Tanzania tunasumbuliwa sana na tatizo moja tu nalo ni hatuna RESPECT KWA THE RULE OF LAW OF OUR LAND!, ndio maana hata huku majuuuu wengi wetu tunaishi kwa taabu sana maana hatujui kuishi kwa kuheshimu sheria. Hawa mapacha watatu wakikiwapelekwa kwenye sheria, ni kwamba sasa unafungua milango ya wanasiasa wahalifu wote nchini kupelekwa kwenye sheria na wananchi kuanza kuheshimu sheria kwanza za Jamhuri, hatimaye wataheshimu sheria za makazini mpaka sheria za familia majumbani mwao, I mean Wa-Tanzania we are too corrupt tunahitaji kuanzia somewhere na hapa kwenye mapacha watatu ndio penyewe sana, So CCM it is either now, or forget it! and Never!

- CCM the burden is on us na wakati ni sasa, either tufanye kweli au tunyamaze, lakini habari za mahojiano maana yake ni kwamba somebody is not sure kama hawa waondolewe au la! Tunasema hivi sio tu wafukuzwe chama, isipokuwa wafikishwe kwenye SHERIA, na wengine wote wenye tuhuma za wizi wa mali zetu za umma na kodi zetu wananchi, ninasema mali zao zote zingekua frozen now na serikali, mpaka watakapothibitisha kwamba kwa miaka mitano ya uwaziri mtu unaweza kuwa Billionea na kuanza kusomesha watoto nje, na kununua magari ya kifahari pamoja na kuwa na hisa kila mahali kwenye makampuni makubwa na kujenga majumba ya ajabu. Ni muhimu sana kuwepo na Legal Facts ili haki zao watuhumiwa zisikiukwe, I mean we are not asking for a Mob Justice, au blind Justice! hapana tunataka Fairness Justice!

- So! CCM the time is up, either wafukuzeni chama SASA hawa Chenge, Rostam na Lowassa, au nyamazeni turudie tulipokuwa siku zote yaani kama kawaida, tusubirie kuwa chama cha Upinzani 2015, kama KANU. Na CCM let me tell you this, siku tutakapoishia kua upande wa pili wa the glass, ndio imetoka haitakuja kurudi tena! Uliza UNIP kule Zambia!

MUCH RESPECT! & MUNGU AIBRIKI TANZANIA!

William Malecela @ New York City, US.

Naunga mkono hoja,vua gamba,vua gwanda, vaa uzalendo tusonge mbele habari ndio hiyo.
 
One year later.mapacha bado wanadunda ndani ya CCM isipokuwa yule aliyetangaza kuachana na siasa uchwala!!mahakamani!?Dont even go there!
 
PASCO what do you mean hapa? Kwamba Mapacha3 wameshinda na hivyo wanaogopwa na viongozi wote wa CCM, au una maana kuwa viongozi na mapacha3 lao moja japokuwa sisi wa nje tunapigwa changa la macho? AU una maana JK na viongozi wa cciyenu wameondoa hoja ya kuwafukuza kwa ajili ya woga?.

Suala la Wiliam nadhani kwa sehemu mimi ninampenda jinsi anavyochanganya mambo! Sometimes anakuwa radical (bila sababu zilizowazi) but in some cases he remains objective! Ni rahisi kufahamu upande upi anaangukia kulingana na upepo, but hoja zake nyingine kama alipoanzisha uzi huu ni nzito sana, na ni wana sisiyenu wachache wanaweza kuandika kwa uwazi namna hii. Hongera wiliyamu! QUOTE=Pasco;3959807]Duh!, kweli ni long time, mimi sikuamini yule William niliyemsifia kuwa ni bold , ndiye William yule yule niliyekutana naye Dodoma akipiga magoti kuwanyenyekea kina Lowassa kwa heshima zote katika kubembelezea kura za kula!.

Sasa Mkuu William umekuja ground zero, kati ya hoja yako ya CCM iwafukuze now or never na hoja yangu kuwa JK na CCM yake si lolote sii chochote dhidi ya mapacha watatu na hana ubavu wa kuwaondoa!, hoja ipi imesimama?.

Si umekuja na jee sasa si umeyaona mwenyewe?. Jee utaendelea kuling'ang'ania jahazi linalokwenda mrama hadi uzame nalo, ama uko tayari kuwa bold enough kusinama nawe uhesabiwe?.[/QUOTE]
 
Duh!, kweli ni long time, mimi sikuamini yule William niliyemsifia kuwa ni bold , ndiye William yule yule niliyekutana naye Dodoma akipiga magoti kuwanyenyekea kina Lowassa kwa heshima zote katika kubembelezea kura za kula!.

Sasa Mkuu William umekuja ground zero, kati ya hoja yako ya CCM iwafukuze now or never na hoja yangu kuwa JK na CCM yake si lolote sii chochote dhidi ya mapacha watatu na hana ubavu wa kuwaondoa!, hoja ipi imesimama?.

Si umekuja na jee sasa si umeyaona mwenyewe?. Jee utaendelea kuling'ang'ania jahazi linalokwenda mrama hadi uzame nalo, ama uko tayari kuwa bold enough kusinama nawe uhesabiwe?.

- Pasco siasa ni hoja sio ugomvi wala uadui, kwamba nnilipigia magoti anybody ni exaggerations, niliomba kura na kwa vile Lowassa ni mbunge na yeye nilimuomba kura, vipi ulitaka nianze kumrushia ngumi huku ninamuomba kura ndio ungenioan shujaa? hoja zingine hizi bana inafurahisha sana!!


William.
 
no sio upigane ngumi willy simamia hoja yako wala usiache isinzie,. kumzungumzia mtu namna hii ulivyomuelezea kwenye hii thread tayari kunaweka utafauti wa kisiasa baina yako na yeye, hivyo basi swala la kumuomba kura halikuwa la ulazima,ungelimwacha mwenyewe aamue kukupa kama anaona unafaa... hiyo ilikuwa ni sawa kwa kanisa kuomba sadaka ya jambazi/muuaji anayejulikana tena wazi kabisa
 
William thread hii ulianzisha tarehe 4/06/2011 leo ni tarehe 01/06/2012. Bado siku tatu utimie mwaka mmoja tangu wewe uhimize magamba wawafukuze mapacha watatu,Mkajinadi kwa kusema Mnavua gamba,Nape akapuliza tarumbeta na kujinadi kwamba yeye ni kiboko ya mafisadi,hadi leo hii hakuna kitu.Rostam alijiondoa tu ili kuendeleza biashara zake na akawaeleza kabisa hataki tena siasa zenu uchwara,hivyo ilionekana dhahiri hakujiuzulu kwa kufuata shinikizo lenu ambalo halikuwepo kwani kama CCM ilikuwa na nia kweli ya kuwafukuza kulikuwa hakuna haja ya kuwaambia eti wajiondoe wenyewe tena eti baada ya siku 90 za nini? WIZI MTUPU!.Cha ajabu bado hadi leo mnaendelea kupiga makelele ya kuisifu CCM hivi mna uelewa kweli ndugu zangu? mngekuwa waungwana si mngeona hii ni failure na kujiondoa CCM.chama kimekuwa cha mzaha mzaha tu maneno mengi vitendo negative. Anyway endeleeni kukumbatia upuuzi huu sisi ndio tunafurahi maana failure ya CCM ni failure ya mafisadi na ni success kwa chadema na wananchi wa Tanzania. hata maiti yangu haitakubali ku i support CCM
 
- Ukitaka kumua nyoka unaanzia kichwani kwanza! hawa mapacha watatu ndio hasa kichwa cha nyoka na magambas!

William @ NYC, USA.

William, William, William! Mbona unataka kuwa msahaulifu kiasi hiki? CCM gani chini ya Uenyekiti wa JK inaweza kuwa na ubavu wa kuwafukuza uanachama Lowasa, Rostam na Chenge?

  • Umesahau kwamba katika kupeleka form kugombea uraisi huko nyuma JK alikodi ndege kwenda Dodoma pamoja na Lowasa?
  • Umesahau kwamba katika kumteua Lowasa kuwa PM, pamoja na kupingwa na viongozi wengine, JK alisema hakukutana na Lowasa barabarani?
  • Umesahau kwamba katika mtandao wa JK kuwania uraisi, Rostam alikuwa ndiye mkusanyaji na mweka hazina wa fedha toka ndani na nje ya nchi (mataifa ya kiarabu), kinyume na sheria?
  • Umesahau kwamba katika mambo mengi ya kupindisha sheria kwa manufaa ya kina JK Chenge ndiye aliyekuwa Mwanasheria Mkuu?
  • Umesahau kwamba Lowasa aliongea wazi kwamba kwa lile la Richmond ikiwa angeweka mambo hadharani hata JK asingesimama?

Na pengine kikubwa unachosahau ni kwamba hawa mapacha watatu leo JK akiidhinisha kufukuzwa kwao, wanaweza kumuumbua kwa namna ambayo haijawahi kutokea raisi kuumbuliwa! Watafunguka kwa vyombo vya habari vya ndani na nje kwa namna ambayo haijawahi kutokea, scandal kama za Watergate zitakuwa ni cha mtoto kabisaaa!

Kuwafukuza uanachama mapacha watatu ni kuwaweka katika position ya kuwa na "nothing to lose" kwa jinsi ambavyo watakavyotoboa yale madhambi yote aliyofanya JK huko nyuma. Atakaye-lose hapa ni JK. Na nakwambia wazi, JK akiamua kusimamia mkutano wa kuwafukuza uanachama, itabidi aijiandae kuwa "impeached" kwa jinsi ambavyo watamuanika. Labda akawapigie magoti kwamba wasimuumbue anafanya hivyo kukiokoa chama. Suala ni kwamba, watakubali chama kiokolewe kwa wao kutolewa kafara?

Umewahi kujiuliza kwa nini Sitta yuko so bold kuisema serikali yake mwenyewe, na bado anadumu katika baraza la mawaziri?

Suala ni kwamba katika uongozi wake JK ameji-compromise mno, ameji-expose kushambuliwa, na hii imechangia sana kumfanya awe so permissive, au kwa watu wanavyoona, kuwa dhaifu katika maamuzi (exposure to blackmail). JK anapotabasamu akikemea rushwa za uchaguzi si bure. Hana freedom of speech kukemea rushwa ya uchaguzi, kwa kuwa anapofanya hivyo, kuna watu katika audience anayoi-address wanamuangalia kwa jicho la kusema "hata wewe unasema hayo?".

Ni rahisi sana kuona kwa nini suala la kuwavua magamba lilikwama - ni suala tu la yale magamba kumwambia JK "we lose - you lose brother" na kumfunga kinywa JK.

Kwa hiyo suala sio CCM hapa, suala ni kama JK atakubali madhambi yake ya huko nyuma kuanikwa hadharani, kufikia kiasi aachie uraisi kwa aibu kubwa.

Kwa hiyo basi, CCM iko mtegoni sana hapa. Je, wawafukuze mapacha watatu, na ku-risk hao mapacha kufunguka juu ya JK na kumuumbua, au wayaache magamba ili kutozusha tafrani juu ya raisi wa CCM aliyepo madarakani? Either way, CCM inaweza ku-lose big time na kuwapa Chadema nchi on a silver platter; both options are devils any president would be very uncomfortable with.

Kati ya devils hawa wawili, wewe ungekuwa JK, ungechagua yupi? Ni wazi sivyo? Kwamba kutowafukuza mapacha is the lesser devil of the two.
 
Sioni kama tatizo la ccm ni watu watatu,fikiri upya kwa maana wengi wanafahamika hujawataja na mengine mengi yata ibuka utafunga mdomo mwenyewe,tafuta chanzo cha hayo yote.
 
Back
Top Bottom