My opinion: CCM fukuzeni mapacha watatu sasa au nyamazeni

- Ukitaka kumua nyoka unaanzia kichwani kwanza! hawa mapacha watatu ndio hasa kichwa cha nyoka na magambas!

William @ NYC, USA.

Willy nakubaliana na wewe na hilo halina ubishi
Ila isiwe ndio ajenda maana wengine wanafikiria ukishwaondoa hao watatu ndio umetibu tatizo ila hawajaelewa kuwa hao ni kama tone kweney bahari
Mkakati uwe ni kulimaliza tatizo na sio kutafuta tiba halisi ya tatizo na sio kutibu dalili tuondoe mazalia ya mbu na sio kuja kutibu malaria
 
Lakini kwa nini mapacha watatu tu? Kwani katika CCM nzima hawa ndiyo mafisadi pekee? Serikalini hakuna mafisadi? Kwenye sekta zingine hakuna mafisadi?

Binafsi siamini kama hawa mapacha watatu ndiyo mafisadi pekee Tanzania.
Hao 3 ndio walikuwa CC ya CCM na CCM ndio inaongoza nchi,wananchi walipigia CCM kura ya chuki sababu ya hao jamaa 3 na hao ndio waliotuletea taabu ya umeme,EPA ndio waliofungua makampuni hewa na ndio walikuwa front Banki kuu ,CRDB ,Hazina kwenda kukwapua fweza zetu
 
Kwasasa CCM kujisafisha harakaharaka ni vigumu sana,na kufikiria RACHEL ndio tatizo pekee ndani ya CCM ni kujidanganya,kwa miaka mingi tumeshuhudia uozo ndani chama na serikali,mfumo mzima wa utawala chini ya CCM umeoza kwa rushwa,wizi na ukandamizaji wa haki za wananchi kuanzia kwa Rais,mawaziri,wabunge,makatibu,wakurugenzi wa idara na mashirika ya umma ni uozo mtupu.Watanzania tunachotakiwa kufanya ni kukitosa CCM na sio kusikiliza ngonjera zao za Mapacha watatu.Kwa CCM kuwatosa RACHEL haina maana wala haitafanya CCM kubadili au kuondokana na mfumo wao wa hiki chetu bali njia pekee ni kuwaweka benchi ilikubadilisha mfumo wa kiutawala na kiutendaji na ndipo hapo tutakapo weza kuwashughurikia akina RACHEL na wengine wengi kisheria bila kuogopana na kuoneana haya au kutishana 'eti ukimwaga mboga namwaga ugali'.
 
Ugomvi wa CCM (Kikwete) na hawa mapacha watatu ni issue ya uraisi 2015.

Issue kwamba hawa ni mafisadi imechukuliwa juu juu tu - yaani Kikwete na CCM yake wanataka kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

Kwamba uwafukuze mapacha watatu kwenye chama then ujisifu kwamba sasa mafisadi wameondoka??
 
William,

..na ufisadi uliotumika kumuingiza JK madarakani unaushughulikia namna gani?

..JK,Lowassa,na Rostam, wameunda mtandao ambao ni chama ndani chama[ccm].

..katika kufanya hivyo wametumia fedha chafu, mbinu chafu na fitina dhidi ya wenzao ndani ya CCM, rushwa na hongo ktk uchaguzi n.k n.k.

..haya mambo mlitakiwa myashughulikie tangu mwaka 1995 lakini hamkufanya hivyo. kuyashughulikia sasa hivi wakati mtandao wameshashika chama ndiko kunakusababisha muwe na kigugumizi.

..UGUMU WA KUWAFUKUZA LOWASSA NA ROSTAM NI KWAMBA MWENYEKITI NAYE NI MDAU KTK UFISADI MWINGI WALIOUFANYA.

NB:

..na kile kitendo cha Mwenyekiti wa Chama kuwapigia kampeni za waziwazi hivi hakistahili hata kutolewa karipio?

..hivi kitendo kile siyo dalili za wazi kwamba Mwenyekiti anawaunga mkono mafisadi?

..let me explain: Takukuru iko chini ya Ofisi ya Raisi. Sophia alikuwa waziri wa nchi Utawala Bora. Kwa msingi kisheria Waziri wa Utawala Bora, and particularly Takukuru, ni Raisi. sasa Raisi alipokuwa anawapigia kampeni watu wanaoshitakiwa na Takukuru kweli mnamuelewa. Halafu Takukuru ni chombo cha ulinzi na usalama, na Raisi ndiye amiri jeshi mkuu.

..sasa JK siyo kama haelewi uzito wa Amiri Jeshi Mkuu kufanya kitendo kama kile dhidi ya askari wake walio ktk medani ya kupambana na Rushwa. JK amepitia mafunzo ya kijeshi, ni senior commander mstaafu mwenye cheo cha Luteni Kanali.
 
Hao 3 ndio walikuwa CC ya CCM na CCM ndio inaongoza nchi,wananchi walipigia CCM kura ya chuki sababu ya hao jamaa 3 na hao ndio waliotuletea taabu ya umeme,EPA ndio waliofungua makampuni hewa na ndio walikuwa front Banki kuu ,CRDB ,Hazina kwenda kukwapua fweza zetu

Kwa hiyo ndo kusema Mkapa si fisadi na anastahili kubaki kuwa mwanachama wa CCM? Na Kikwete naye si fisadi hata kidogo. Ni msafi hana hata doa. Kaazi kweri kweri
 
Matumaini yangu ni kwamba baada ya kuwepo kwa tuhuma nzito dhidi ya watu hawa, ccm ilitakiwa i come out with solid evidence na hatimaye kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua stahiki. Kinyume na hapo tutachafuana na tena without the rule of law. come on ccm.
 
Facebook: William Malecela on Saturday, June 4, 2011 at 8:13am

@ NEW YORK CITY-USA: Nimeshitushwa sana na habari za CCM kuwaita Mapacha Watatu eti kwa mahojiano!, I mean mahojiano ya nini? Wananchi wa hili taifa tumechoshwa sana na hivi viini macho. Ni CCM wenyewe walio-raise the bar kwa kutangaza kujivua magambas na ni CCM iliyotangaza kuwaondoa kwenye NEC yake na CC, as a member of CCM I was incouraged na the news kwamba CCM ipo njiani kuwafukuza chama kabisa, sasa tena tunaposikia habari za mahojiano inaleta utatanishi! Mahojiano ya nini! mbona walishawaweka pembeni kwenye nafasi muhimu sana za ndani ya chama bila mahojiano? I mean sasa ni wakati wa CCM kutangaza kwamba imewafukuza tayari au ikubali kwamba haina huo ubavu!

- I mean nothing personal, na sio kwamba kufukuzwa kwa hao mapacha watatu kutaondoa matatizo ya wananchi kwa siku moja, lakini tunategemea kwamba wakishavuliwa uanachama wa CCM, ifuatie kuwapeleka kwenye mkono wa SHERIA!. Tanzania tunasumbuliwa sana na tatizo moja tu nalo ni hatuna RESPECT KWA THE RULE OF LAW OF OUR LAND!, ndio maana hata huku majuuuu wengi wetu tunaishi kwa taabu sana maana hatujui kuishi kwa kuheshimu sheria. Hawa mapacha watatu wakikiwapelekwa kwenye sheria, ni kwamba sasa unafungua milango ya wanasiasa wahalifu wote nchini kupelekwa kwenye sheria na wananchi kuanza kuheshimu sheria kwanza za Jamhuri, hatimaye wataheshimu sheria za makazini mpaka sheria za familia majumbani mwao, I mean Wa-Tanzania we are too corrupt tunahitaji kuanzia somewhere na hapa kwenye mapacha watatu ndio penyewe sana, So CCM it is either now, or forget it! and Never!

- CCM the burden is on us na wakati ni sasa, either tufanye kweli au tunyamaze, lakini habari za mahojiano maana yake ni kwamba somebody is not sure kama hawa waondolewe au la! Tunasema hivi sio tu wafukuzwe chama, isipokuwa wafikishwe kwenye SHERIA, na wengine wote wenye tuhuma za wizi wa mali zetu za umma na kodi zetu wananchi, ninasema mali zao zote zingekua frozen now na serikali, mpaka watakapothibitisha kwamba kwa miaka mitano ya uwaziri mtu unaweza kuwa Billionea na kuanza kusomesha watoto nje, na kununua magari ya kifahari pamoja na kuwa na hisa kila mahali kwenye makampuni makubwa na kujenga majumba ya ajabu. Ni muhimu sana kuwepo na Legal Facts ili haki zao watuhumiwa zisikiukwe, I mean we are not asking for a Mob Justice, au blind Justice! hapana tunataka Fairness Justice!

- So! CCM the time is up, either wafukuzeni chama SASA hawa Chenge, Rostam na Lowassa, au nyamazeni turudie tulipokuwa siku zote yaani kama kawaida, tusubirie kuwa chama cha Upinzani 2015, kama KANU. Na CCM let me tell you this, siku tutakapoishia kua upande wa pili wa the glass, ndio imetoka haitakuja kurudi tena! Uliza UNIP kule Zambia!

MUCH RESPECT! & MUNGU AIBRIKI TANZANIA!

William Malecela @ New York City, US.

Nafikiri Willie ama unakebehi watu ama haujaielewa CCM....kwanza nikuulize mafisadi CCM ni hao watatu tu?..Well kama una uvivu wa kuujua ama kuutafuta ukweli,ama kama umetekwa na cover la kitabu cha kujivua gamba unaweza sema ndio...CCM kamwe haiwezi kuwafukuza mafisadi hao watatu wala wale wengine,maana ukweli ufisadi hawakuufanya wao peke yao..ufisadi ulifanywa na CCM kwa manufaa ya CCM ili waendelee kuinyonya asali ya Tanzania..Kifupi Ufisadi na CCM havitengamani...sinema hii wanayoicheza CCM mimi nafananisha na mtandao wa maambukizi ya Ukimwi katika jamii fulani au kundi fulani then ikaamuliwa watatu wenye ukimwi wauae ili kuzuia maambukizi zaidi,wakati walioambukizwa ni 50..sasa ukiua watatu hawa 47 hawataendelea kuwaambukiza walio bado?.. Willie baba kuwa CCM siyo kigezo cha wewe kijana mwenye ufahamu kukumbatia CCM na mabaya yake....Taifa la kesho si CCM,amka sasa na acha kuendekeza magamba jiunge na CHADEMA kulikomboa Taifa...na bahati mbaya mzee wako naye anatajwa kuhusika na ufisadi...sorry for that lakini si lazima na wewe uunywe ufisadi eti kwa sababu mzee ni wale wale...Welcome CHADEMA!!
 
William,

..na ufisadi uliotumika kumuingiza JK madarakani unaushughulikia namna gani?

..JK,Lowassa,na Rostam, wameunda mtandao ambao ni chama ndani chama[ccm].

..katika kufanya hivyo wametumia fedha chafu, mbinu chafu na fitina dhidi ya wenzao ndani ya CCM, rushwa na hongo ktk uchaguzi n.k n.k.

..haya mambo mlitakiwa myashughulikie tangu mwaka 1995 lakini hamkufanya hivyo. kuyashughulikia sasa hivi wakati mtandao wameshashika chama ndiko kunakusababisha muwe na kigugumizi.

..UGUMU WA KUWAFUKUZA LOWASSA NA ROSTAM NI KWAMBA MWENYEKITI NAYE NI MDAU KTK UFISADI MWINGI WALIOUFANYA.

NB:

..na kile kitendo cha Mwenyekiti wa Chama kuwapigia kampeni za waziwazi hivi hakistahili hata kutolewa karipio?

..hivi kitendo kile siyo dalili za wazi kwamba Mwenyekiti anawaunga mkono mafisadi?

..let me explain: Takukuru iko chini ya Ofisi ya Raisi. Sophia alikuwa waziri wa nchi Utawala Bora. Kwa msingi kisheria Waziri wa Utawala Bora, and particularly Takukuru, ni Raisi. sasa Raisi alipokuwa anawapigia kampeni watu wanaoshitakiwa na Takukuru kweli mnamuelewa. Halafu Takukuru ni chombo cha ulinzi na usalama, na Raisi ndiye amiri jeshi mkuu.

..sasa JK siyo kama haelewi uzito wa Amiri Jeshi Mkuu kufanya kitendo kama kile dhidi ya askari wake walio ktk medani ya kupambana na Rushwa. JK amepitia mafunzo ya kijeshi, ni senior commander mstaafu mwenye cheo cha Luteni Kanali.


Penye rangi:
Kitendo hicho ndicho kilichompeleka JK chini kabisa mbele ya macho ya jamii! Hadi leo hii sipati jibu kwa nini alifanya hivyo.
 
- Ukitaka kumua nyoka unaanzia kichwani kwanza! hawa mapacha watatu ndio hasa kichwa cha nyoka na magambas!

William @ NYC, USA.

Hivi mmeshathibitisha (swithin CCM) kuwa jamaa wana makosa? Kumbuka tunapaswa kufuata utawala wa sheria
 
..labda CCM wangeanza na kueleza wamepokea MICHANGO kiasi gani toka kwa MAFISADI.

..baada ya hapo wangerudisha michango hiyo haswa fedha serikalini au kwa taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi wa kawaida.

..zaidi wawaombe radhi wa-Tanzania kwa kitendo chao cha kutumia michango ya mafisadi.

..mwisho wawavue uongozi wale wote waliosababisha CHAMA kikapokea MICHANGO toka kwa MAFISADI.
 
..labda CCM wangeanza na kueleza wamepokea MICHANGO kiasi gani toka kwa MAFISADI.

..baada ya hapo wangerudisha michango hiyo haswa fedha serikalini au kwa taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi wa kawaida.

..zaidi wawaombe radhi wa-Tanzania kwa kitendo chao cha kutumia michango ya mafisadi.

..mwisho wawavue uongozi wale wote waliosababisha CHAMA kikapokea MICHANGO toka kwa MAFISADI.
Hii Mkuu ni sawa na CCM kujivua gamba yenewe, wana ubavu huo?
 
Unaonyesha umezidikuparaganyika kisiasa, naomba upumzike kidogo au uende rehab. Tatizo la Tanzania ni CCM yenyewe. Naonaunaanza kutoka kimaslahi kama wanaCCM wenzako. Kumbuka hata mzee wako ni tatizo which means your a problem by implication. Ukitaka mambo yanyooke dissolve your party and put all thieves in jail, which is difficult because you are also an implied thief!
Branch lako la CCM NY limefika wapi? Umechanganyikiwa wile
Naona mkuu unachanganya mada sidhani kama willy na john wana mahusiano yoyote katika siasa
 
Kitu cha kuchekesha zaidi mahojiano hayo yamefanywa na makamu mwenyekiti pekee yake na hakuna mwingine zaidi ya watuhumiwa wa ufisadi na makamu anayejua ni kitu gani walihojiwa....................... hii ndio CCM ya JK, Msekwa, mafisadi.............na wenzi wao...
 
Heshima kwako W J Malecela.

Mkuu wangu niliwahi kukupa tahadhari kipindi fulani ulianzisha thread yako ya kushangilia kujivua gamba CCM nikakuonya hukutaka kusikia kabisa ukajiaminisha na kuwaamisha baadhi ya watu wenye mioyo ya kuku kwamba CCM itajivua gamba! .Nakumbuka nilikupa sababu kadhaa lakini moja kubwa ni kukosa msimamo kwa mwenyekiti wenu Rais J M Kikwete.Kama umefuatilia sakata zima lilivyoripotiwa na baadhi ya magazeti ya Raia Mwema ,Mwanahalisi na baadae kuthibitishwa na Mwananchi utagundua jambo moja muhimu sana "ukosefu wa msimamo madhubuti wa Mwenyekiti wa CCM taifa". Mwenyekiti wenu bado hajaonyesha msimamo wa kuchukia ufisadi na washiriki wa ufisadi kwa dhati,Washirika wakuu wa ufisadi walimsaidia sana kufika hapo alipo bado anawaonea aibu hata ingekuwa ni wewe ingekupa shida[dhambi ya kushirikiana na waovu].

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari Rais Kikwete alikutana na Lowassa kabla hajakutana na Mzee Msekwa.Mazungumzo baina ya Rais na Lowassa yaelekea hayakugusia kabisa suala la Lowassa kujivua gamba hata kama yaligusia huko yaelekea kabisa Lowasaa aliweza kupangua hoja zote kwa ukamilifu kabisa tofauti na alivyoshindwa kupangua hoja wakati Mheshimiwa Dr Mwakyembe alipowasilisha hoja za RICHIMOND mjengoni [ni siri baina yao].Yamkini yalikuwa ni mazungumzo ya kawaida sana pengine Lowasa alimkumbusha Rais Kikwete jinsi alivyomsaidia hadi akaukwa urais wa JMT,jinsi alivyoratibu ukusanyaji wa fedha hadi kufikia kukwapua fedha kibao Benki Kuu [BOT],jinsi alivyopambana na wapinzani wake waliokuwa wakitishia nafasi yake pengine alimwambia Kikwete unakumbuka tulivyompakazia Salimu A Salimu kwamba alihusika na mauaji ya Sheikh A Karume kwamba yeye ni HIZBU,unakumbuka tulivyonunua vyombo vya habari na nk.Baada ya siku kadhaa Lowasa anaitwa na makamu mweyekiti Mzee Msekwa na kuambiwa mambo ya ajabu eti ajivue gamba mara ohooo achana na ndoto za urais hata kama ni wewe lazima ushangae iweje mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa chama ashindwe kukuambia msimamo wa chama amwachie jukumu hilo Mzee Msekwa !.Mkuu wangu W J M wewe nimtu mzima sana hakuna ubishi kwamba Mwenyekiti wako akiwa na Lowasa anazungumza masuala tofauti na akiwa na Makamu Mwenyekiti wake.Kauli za katibu wa Itikadi Bwana Nape na Katibu Mkuu Bwana Mukama zilitosha kabisa kukupa ujumbe kwamba kujivua gamba ni aina ya maigizo yasiyokuwa na mwongozaji,kila mmoja anaamua namna ya kuigiza apendavyo.

TANU/CCM chini ya uongozi madhubuti Mwl J K Nyerere iliwahi kujivua gamba mara kadhaa na wananchi wa kawaida wakalishuhudia kwa macho yao tofauti na huu usanii wa sasa.Mwaka 1967 TANU baba wa CCM ilijivua gamba kwa kuanzisha Azimio la Arusha[Miiko ya uongozi iliasisiwa na hili azimio].Mwaka 1984 CCM ilijivua gamba kwa kumwondosha aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.Mwaka 1987 CCM ilijivua gamba kilipobaini vyombo vya serekali na taasisi za kiuchumi zilikuwa zimeshindwa kuwahudumia watanzania ipasavyo,Mawaziri na wakuu wa mashirika ya umma kama ATC,NASACO na TIB walikwenda na maji.

CCM chini ya uongozi lege lege haiwezi kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa.

Mkuu W J Malecela ni wakati wako wa kufanya maamuzi sahihi sasa kwakuwa naamini wewe ni mtu mzima umeona mengi si vibaya ukaachana na CCM ukaelekeza nguvu zako sehemu nyingine.Muasisi wa CCM Mwl Nyerere aliwahi kutamka hadharani kwamba CCM si Mama wala Baba yake baada ya kuchoshwa na uoza usiokwisha ndani ya chama alichokianzisha[kadi namba moja hadi leo hajapewa mwanachama mwingine bado anaendelea kuimiliki hata kama ameshatangulia mbele ya haki].Najua ni uamuzi mgumu sana kwako hasa ukizingatia umekulia huko,umekuzwa huko na sehemu ya mafaniko yako yameanzia huko ni wakati wako sasa kuachana na siasa za udanganyifu dunia ya leo watu wanataka haki,wanataka kumiliki uchumi wao katika hali ya usawa umeona mwenyewe yaliyotokea na yanayotokea Mashariki ya kati.

 
Mkuu WJ Malecela , kwetu sisi wana CCM tunaona mchezo unaochezwa kama filamu isyoisha na kuna mchezaji myuma ya pazia asiyetajwa ila ndio anaendesha mambo yote.
Hawa mafisadi watatu hawako peke yao , ni mpaka mchezaji nyuma ya pazia atolewe hadharani kama mwanga ndo mchezo utaeleweka!
Kwa hakika filamu hii ya mapacha watatu aka RACHEL inakera!

Huyo mchezaji wa nyuma ya pazia ndiye yupi? Au una maana ya mwenyekiti???
 
Back
Top Bottom