My opinion: CCM fukuzeni mapacha watatu sasa au nyamazeni

Mkuu Pasco,

Nimefuatilia michango yako na kwa kiwango kikubwa nakubaliana na wewe isipokuwa pale unaposema kuwa William ni bold enough eti kwa haya anayoyasema humu. Mimi sioni ujasiri wowote zaidi ya kutaka kupima joto na kiwango cha hasira za watu wanaofura kwa kuona kinachoendelea ndani ya nchi yetu kwa sababu ya mambo ya kipuuzi yanayofanywa na CCM. Ninazo sababu tatu kuonesha kuwa kujivua gamba ni attemp isiyowezekana hata kwa mtutu!
1. Wale wanaowashikia bango wenzao ama wametajwa kwenye lists of shame (part 1 and 2) na kwa hiyo hakuna anayeweza kumnyooshea kidole mwenzake. Na kama kuna aliyekashifiwa na hiyo list angeshaend mahakamani. Kwa vile hakuna aliyeenda basi hizo lists ni authentic (au nakosea???). Pia hata wale ambao hawakutajwa kwenye hizo lists, bado pandora box ikifunguliwa watajikuta nao wamenaswa na mtego wa panya wa kifisadi ndani ya CCM.
2. Kauli za Aliyekuwa karibu sana na JK, waziri wa zamani wa Utawala bora, Mama Sofia Simba zinahitimisha hoja zote. Kwamba ndani ya CCM hakuna aliye msafi (kuna anayebisha??) na pili kwamba Lowasa ni mwanamume wa shoka (sijui alitumia vigezo gani ila naamini echo yake inajulikana ndani ya CCM)!!
3. Matendo na maneno ya JK hayajawahi kunishawishi kwamba anao ujasiri wa kushughulikia ufisadi. Ukimwona anaongelea haya mambo mazito na kama wewe ni mwangalifu basi utagundua kuwa hamaanishi anayoyasema. Ndio maana anatumia maneno katibia 100 kuongelea kitu kimoja tu na misemo kibao tu isiyo na mshiko.

Kwa hayo niliyoyataja hapo juu (mnaweza kuongeza na mengine) hakuna kitu kama kuvua gamba perse!

Katika hili nitabaki kuwa Tomaso milele!!

- Ingekua kweli wasingeondolewa NEC na CC, ni maneno ya kawaida sana haya kwa a frutrated person, lakini hamna ukweli kabisa ndani yake, na si kweli kwamba CCM wote ni wachafu, mimi sio mchafu na wapo wengi sana wasafi sana kama Sophia Simbaa anaamini CCM wote ni wachafu wakati wake wa kujitokeza na ksuema hayo ulikuwa ni sasa mapacha wanaposulubiwa kwenye kila kona ya taifa letu, kwa nini hajitokezi sasa wanapomuhitaji sana kuliko anytime kule nyuma?


William @ NYC, USA.
 
- Mkuu sana wrong reading ya our politics, kwa sababu kwanza lazima ujiulize nani aliyemtoa Lowassa Uwaziri Mkuu, nani alimnyima Lowassa umakamu wa Mwenyekiti wa CCM, na nani aliyemtoa NEC, na CC, halafu ni kwa nini Rais hakuhudhuria harusi ya mtoto wa Lowassaa, halafu pia kuna politics za jimbo lake Lowassa la uchaguzi, ndio maaana ninakataa kabisa kumuhusiha Rais na mafisadi, hivi kweli Kikwete angetaka kuwa Billionea jamani nani angemzuia?

- Ninasema hivi Rais Kikwete, sio fisadi na wala hamuogopi kiongozi yoyote!


William @ NYC, USA.

serious? are you kidding me? kikwete ni msafi? hela za ikulu zilizotumika kwenye kampeni zinamfanya awe msafi?
Kushindwa kuwaondoa hao watu kwenye chama ni sign ya kutokuwa msafi. Kuwaondoa kwenye kamati kuu kumeleta mabadiliko gani?
Why cant he make a bold statement? Unaongelea mambo ya harusi hapa, as if kwenda kwenye harusi ni a significant political statement!
Mbona Obama hakwenda kwenye harusi ya mtoto wa Clinton? Was that a political statement pia?
Niambie kitu kimoja bold ambacho kikwete amefanya...
 
serious? are you kidding me? kikwete ni msafi? hela za ikulu zilizotumika kwenye kampeni zinamfanya awe msafi?
Kushindwa kuwaondoa hao watu kwenye chama ni sign ya kutokuwa msafi. Kuwaondoa kwenye kamati kuu kumeleta mabadiliko gani?
Why cant he make a bold statement? Unaongelea mambo ya harusi hapa, as if kwenda kwenye harusi ni a significant political statement!
Mbona Obama hakwenda kwenye harusi ya mtoto wa Clinton? Was that a political statement pia?
Niambie kitu kimoja bold ambacho kikwete amefanya...

- Alimuondoa Lowassa U-Waziri Mkuu, akamnyima umakamu wa CCM, amewaondoa wote kwenye NEC na CC!

William @ NYC, USA.
 
.........1. Mapacha watatu wafukuzwe CCM kwa sababu zilizowafanya waondolewe kwenye NEC na CC, na pia Lowassa kukimbia uwaziri mkuu bila kufukuzwa, na kujihusisha kwao sana kukivuruga chama ambapo kuna ushahidi wa kutosha sana, wafikishwe kwenye sheria na Jamhuri kwa sababu sio kazi ya CCM kuwafikisha mahakamani nafikiri unaelewa sana Katiba inasema nini on that.

Na inashangaza sana....kwamba wakulu wote (isipokuwa the one we know JKN RIP) walimkubali huyu.....jamaa mwenye siasa za Walionacho na Wasionacho..........

2. Nimesema kitendo cha Rais kwenda kuwanadi kwenye kampeni za uchaguzi ilikuwa wrong na pia a political mistake ambayo tayari Rais paid for kwa kupungukiwa sana kura za ushindi kuliko term ya kwanza, lakini haina maana yuko nao mafisadi hapana!

It is very difficult for people to comprehend this.........iwe hapa JF na huko mtaani ndio kabisaaa..........in short huwa tunasema SIASA NI MCHEZO MCHAFU..........hahaha...........I hope JK played his cards well.............

3. Kama mapacha watatu they are clean then let the law say that, kamati ya bunge haikusema hivyo, BAE haikusema hivyo, Ripoti ya Richmonduli haikusema hivyo, Ripioti za Dowans hazikusema hivyo, hao watatu sio wasafi hata kidogo ni wachafu sana!

Mkulu...........I could not agree with you more on this.....................
 
- Alimuondoa Lowassa U-Waziri Mkuu, akamnyima umakamu wa CCM, amewaondoa wote kwenye NEC na CC!


William @ NYC, USA.


Mkuu correct me if im wrong, hawa mapacha watatu wameondolewa kwenye CC na siyo NEC, sababu mheshmiwa Kinana aliwaomba wajumbe wote wa CC wajiuzulu ili kumpa mwenyekiti fursa ya kuteua wajumbe wengine. Ilipofika kwenye NEC Makongoro hakutafuna maneno kuwapa ukweli wao, lakini maamuzi magumu hayakuchukuliwa sababu Mwenyekiti alirudisha mpira kwa wajumbe ambao walishindwa kuteketeza watu baharini, na kinachoendelea sasa ni kutafuta namna ya kuwaondoa kabisa kwenye NEC, na hapo ndio ngoma inapokua nzito!
 


- Ingekua kweli wasingeondolewa NEC na CC, ni maneno ya kawaida sana haya kwa a frutrated person, lakini hamna ukweli kabisa ndani yake, na si kweli kwamba CCM wote ni wachafu, mimi sio mchafu na wapo wengi sana wasafi sana kama Sophia Simbaa anaamini CCM wote ni wachafu wakati wake wa kujitokeza na ksuema hayo ulikuwa ni sasa mapacha wanaposulubiwa kwenye kila kona ya taifa letu, kwa nini hajitokezi sasa wanapomuhitaji sana kuliko anytime kule nyuma?


William @ NYC, USA.


Hapo ndipo huwa nashindwa kukuelewa. Tunaeleza realities na wewe unatuona frustrated. Naamini ipo siku utajua nani yuko frustrated kati yangu (na wengine wenye mawazo kama yangu) na wewe mwenyewe.

Binafsi siishi kwa sababu CCM ipo au la. Kama ingekuwa hivyo basi nisingeona tatizo kuonekana nimechanganyikiwa. Waliochanganyikiwa ni wachumia tumbo ambao hawana uhakika kama wataendelea kuishi na kusalimia maliwato baada ya wananchi kuikomboa nchi yao. Naamini ipo siku mimi na wewe tutakuwa mashahidi!
 
Lakini kwa nini mapacha watatu tu? Kwani katika CCM nzima hawa ndiyo mafisadi pekee? Serikalini hakuna mafisadi? Kwenye sekta zingine hakuna mafisadi?

Binafsi siamini kama hawa mapacha watatu ndiyo mafisadi pekee Tanzania.


You have a right argument! In my opinion there must be a STARTING POINT....... TRINITY IS THE STARTING POINT.... TUTAENDELEA NAWENGINE!


God Bless Tanzania!
 
nimeipenda hii topic. Bora nyie mlioko kwenye mfumo mseme maana wakisema walioko nje ya mfumo wanaambiwa wana vijiba.
 
kama kuna CCM mpya itakayozaliwa, basi naweza nikasema wewe ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho japo sijajua kitakuwa kipya kwa maslahi ya taifa kama CDM au ndo upya wa sura na muundo tu. hongera sana mkuu kwa post yako.
 
Kama Chenge hana hatia kwenye scandal ya radar then Lowassa tunamwonea tu.
Kama Kikwete as a head of state with all the forces at his disposable (Police, military, usalama wa taifa, mgambo, Takukuru etc) mwenyewe anamwogopa Rostam, nani atathubutu kumwondoa?
 
William @ NYC, USA

Sasa unasema nini, Mapacha bado wapo na inavyoonekana kila mwana-CCM kuanzia amiri Jeshi Mkuu wana waogopa. Maoni ni kwamba kulikuwa hakuna nia yeyeote ya kumtimua mtu au kumwajibisha. Walitafuta jinsi ya kufumua sekretariet ya chama. Kumbuka walio fanya utafiti wa chama kufanya vibaya, ndio waliotoa jinsi ya kuvua gamba ndio waliopewa vyeo vipya. Approach yao ilikuwa kuvaa gamba kwa mapinduzi bila kujali nini wanafanya ili waingie ndani.

Sioni kama kuna nia ya dhati ya kumwajibisha mtu ndani ya CCM lolongo zitakuwa nyingi na mwishowe kila mtu atakaa kimya watasahau. Nape ameshakana kauli zake, na amesema maamuzi mengine hayatekelezeki.
Mukama kasema yeye ameshastaafu hivyo anasubiria kwenda kijijini kwake kuzeeka. Kwa maana nyingine hataki ugomvi na mtu.

CCM inakuwa ni uvuvuzela kuliko ushindani.
 
mkuu wj malecela , kwetu sisi wana ccm tunaona mchezo unaochezwa kama filamu isyoisha na kuna mchezaji myuma ya pazia asiyetajwa ila ndio anaendesha mambo yote.
Hawa mafisadi watatu hawako peke yao , ni mpaka mchezaji nyuma ya pazia atolewe hadharani kama mwanga ndo mchezo utaeleweka!
Kwa hakika filamu hii ya mapacha watatu aka rachel inakera!
wewe mpumbavu lolegwakisa huna maaana kabisa hahahaaaaaaaaaaaaaaaa!!!! Kichwa yako ina afya sana, nimekuita mpumbavu just kukukubali kwa hoja yako......... 2weeks ago nilikuwa mzee mmoja aliyekuwa ktk daruso na mzee six.....yeye anaamini kuwa hawa jamaa el,ra na ac watang'oka na kwamba kuna mtu yuko nyuma ana pressurize move hiyo invissibly.......hahahaaaaaaaaa, tuombe mmungu sana tuvuke salama. Lakini aliniambia watz wasiawaamini mwakyembe na sitta.....kwake yeye anasema hawa ni opportunist wa hali ya juu ktk kutaka mamlaka.
Nway wewe nimekukubali sana ktkmjadala huu
 
Back
Top Bottom