My mother is dying of Cancer

My mother is dying of Cancer

Status
Not open for further replies.
Paula Paul....

Wish nije nikuone kama mama amelazwa hospitali ya hapa Dar. Kama hutojali bila kujitambulisha kuwa mimi ni flani na wewe ndo Paula, ukisema mama amelazwa hospital flani binafsi ntafika kumuona mama na kumtia moyo.

Najua haitapunguza maumivu anayopitia wala kumuongezea siku za kuishi au kuwa tiba kwake... (Who knows moyo wa binadamu unataka nini kwa wakati husika.... Ni siri ya mtu binafsi) ila si haba kama uwepo wangu walau utampa tabasamu mama japo yuko kwenye maumivu.

Ni BORA kumjulia hali mgonjwa akiwa kwenye matibabu na kuwatia moyo watu wa karibu wanaomuuguza kuliko kuja kuaga maiti au kushiriki mazishi. Mara elfu mama akasikia sauti za watu kuja kumuona kwa kumfariji na kumsemesha maneno ya upendo, amani na furaha (iwapo maneno ya daktari yatatimia) basi atakuwa ameondoka na kumbukumbu nzuri kutoka duniani haswa kipindi hiki cha mwisho.

Naamini kwa sasa mama anahitaji utulivu Ila pia anahitaji kusikia maneno ya kutia moyo, ya kumfaya asahau maumivu kwa muda hata kama ni nusu saa...

Natamani sana kuja kumuona mama yako si kwa nia ya kujionesha kuwa najali sana hapana au kujitambulisha mie ndo flani hapana, bali kumshika mkono, kumtia moyo, saa ingine hata kumshirikisha mambo yanayoendelea nchini (mfano jana Magu kasema hataendelea kuongoza zaidi ya muhula wake) that's good news to some people na kwa wengine ni bad news then huu ni mjadala iwapo ataweza sema chochote juu ya hili hapo utakuwa umeitoa akili yake kwa muda kufikiria mauti na maumivu....

Well am not a psychologist but I do care about well-being of a human.

Nakumbuka kwenye uzi nilioweka wa make any wish on Christmas, ulimtaja mama kuwa arejee kwenye afya yake.... Nakumbuka nilisema maneno pale.

Am touched about seeing her if it won't matter to you.

Lastly, kwa namna yeyote ile jitahidini msilie mbele yake.... Ukiona umebanwa sana toka nje liaaaaaaa piga keleleeeee na yoweeeee Ila mama asisikie wala asilie. Anahitaji kusikia vicheko hata kama itakuwa vya maumivu au kwa shida na nyie pia mnahitaji nguvu ya ziada, pain unayoipitia wewe, mama anaipitia kubwa zaidi ya hiyo. Sina uzoefu Ila nimeshasikia huko na huko watu wanasema kifo kina maumivu makubwa mno....@Mshana jr anaweza sema kitu juu ya hili.

Paula, have my hugs this morning I can write essays here but please touch your mama's palm this morning and smile at her for me. I wish to do the same to her, just a smile.

Smile Heals... yaani tabasamu ni dawa.

Uwe na asubuhi na siku njema Paula. If you can't say anything here just PM me please.

Kasinde.
 
Hello Guys,
My mother is dying of cancer. We tried everything we possibly could, but today we have been told by the doctors that she will likely die within two/three days. It feels like a nightmare.

She's not afraid of death, she want to die ASAP, because she has already gone through enough.

There is nothing we can do but make her remaining time comfortable and to spend the last 48hrs with her. It's just so tough and I am hoping for a miracle if it really exist.
Guys cancer is fvcking awful. I am scared to death.
I am in so much stress and pain right now, I don't know what to do.
Pole sana dada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paula Paul,

Pole sana Paula kwa maumivu unayoyapata na shukuru kuwa Dr amekueleza ukweli kuliko kukuficha, mpe na mwonyeshe mapenzi yote mama na mwisho utashangaa na kufurahi pale atakapofariki akiwa anacheka na wewe ..nasema hivyo kwani mama yangu alikufa kwa Cancer hivyohivyo na mpaka leo nikikumbuka tulivyokuwa tuna chat akiwa hoi kitandani na mpaka anakufa basi nafarijika sana moyoni na kujiona bado ningali naye
 
Madaktari wa aina hii nao ni janga katika jamii.
Kuuguza ni nusu ya kuugua...badala ya kutoa taarifa kama hizo, angeendelea kuwapa matumaini au angekaa kimya.

Pole Paula.

Siku hizi wanakuambia tuu yale mambo ya danganya toto yalishapitwa na wakati. Mi naona ni vizuri ili familia ijipange. Kuna point ikifika hata wewe mwenyewe usie daktari unakua umeshajua kinachofuata so hakuna cha kuficha.

Mleta mada pole sana ndio maisha sisi wote ni mavumbi.
 
YAK. :5:14
Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

YAK. :5:15
Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

HES. :23:19
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?

Nenda kanisa la waadventista wa sabato waje wafanye ibada ya maombi kwa mama Bwana yu aweza kutenda muujiza kwa mama ukawa ushuhuda kwenu wote, aliweza kumponya mfalme Hezekia aliyekuwa ktk hatua za mwisho za kifo akamponya na kumuongezea miaka 15 hawezi kushindwa kwa Mama pia
 
Mwambie aweke hio tiba hapa..kama wazungu hawajamtafuta kwa uvumbuzi,mnhh
Wazungu hawatamtafuta kwa uvumbuzi ,bali watampoteza kwa kuwaharibia biashara yao.
Mtafute Dr Sebi na machapisho yake.
Cancer inatibika na kuzuilika kwa vyakula tu
image.jpg
image.jpg
image.jpg
 
Mara zote natumia formula hii kujipa faraja na moyo mkuu wa kushughulikia matatizo/changamoto mbalimbali;

Swali: Je kuna tatizo?
Jibu: NDIO
Swali: Je tatizo lina ufumbuzi?
Jibu: NDIO
Relax, huna haja ya kuwa na wasiwasi, tatizo lako lina majibu.

>>Hapa unaacha kulialia na kuchukua hatua za haraka kukabili tatizo/changamoto husika.

Au

Swali: Je kuna tatizo?
Jibu: NDIO
Swali: Je tatizo lina ufumbuzi?
Jibu: HAPANA
Relax, huna haja ya kuwa na wasiwasi, tatizo lako halina ufumbuzi wa kibinadaam!!

>>Hapa uwezo wa kibinadamu umefika kikomo. Tumaini lililobaki ni rehema za mja tu. Suluhisho ni kuomba na kusali tu.

Pole sana mpendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paula Paul, Kuna Zoologist mmoja ambaye alianzia udaktari wa kawaida baadae akajiendeleza zaidi upande wa Zoology hadi kufikia level ya PhD. Ana kliniki yake Kibaha. Jamaa yupo vzr saana kwenye mambo ya tiba mbadala hasa ya magonjwa makubwa makubwa kama kansa. Alishamtibu mtu flani ambaye alikuwa na kansa ya Koo. Huyo mgonjwa alifikia hatua mbaya kweli ya kutokula kutokana na maumivu ya Koo. Alienda kwa huyo zoologist na kupata dawa. Huyo mgonjwa alipata tiba na afya yake imerejea , na kwa Sasa anakula Chakula chochote hadi ugali. Kwa kweli Sina uhakika Kama kansa imetoweka kwa 100% , Ila ninachokiona jamaa amepata improvement kubwa na anafanya mishemishe zake Kama kawaida.

Paula, kama utavutiwa na huyo zoologist nistue ili nikutafutie namba zake kutoka kwa yule jamaa. Pengine anaweza pata nafuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom