Kasie,
Dear Kassie.
Hii msg imeniliza. Nimelia sana sikutegemea kupata upendo wa namna hii hapa ndani.
Sikutegemea kama ungekumbuka kuna siku niliandika kwenye Uzi wako kuhusu mama. Kitendo cha wewe kukumbuka pamenifanya macho yangu kutiririsha machozi kama bomba.
Ndani ya ID fake lakini kuna mtu ambaye ana upendo wa dhati.Nashindwa kujizuia. How I real wish tungekuwa siblings. Nahisi hata maumivu niliyoyapata nisinge yapata.
Mama yupo nje ya Tanzania. Asante kwa kuonesha nia na upendo dear.
Thanks for these hugs, nimemsomea hadi mama amefurahi sana. Amefurahi kwamba ataondoka lakini kuna watu wema ambao bado watakuwa wananifariji.
Ni kweli anapitia maumivu mahali, ila anajikaza sana. Mpaka sasa anaweza kutumia simu yake kuchat na kuongea kwenye simu ambapo hauwezi kuamini kama ni mgonjwa.
Mpaka sasa hali yake imebadilika na unaonekana mwenye nguvu sana, anaimba Gospel na anacheza (kujitikisa ile). Anaweza kusoma pia Biblia. Unaweza hizi anapona ila hapa doctor anasema mgonjwa wa cancer kwenye hatua za mwisho huwa anapata nguvu.
Ila kwa Mara ya kwanza ameshindwa kunitofautisha mimi na twin sister. Na sisi hatutaki kumtesa kuanza kumfundisha kutofautisha. Baba yetu ameshindwa kuvumilia kumwona mama kwenye hiyo hali, tunaomba Mungu pia tusije tukampoteza na yeye pia.
Pia kwa sasa hapendi watu wamshangae usoni. Sisi anatuangalia tukiwa hatumwangalii, tukimwangalia anatazama pembeni, hivyo tumeacha kumwangalia direct ili tumpe nafasi ya kutuangalia yeye hadi aridhike.
Ameniambia Leo nilale pembeni yake nimkumbatie. Nimelala nae kidogo ndipo nilipogundua mama amekonda sana hata uti wa mgongo umetokeza juu hamna nyama. Ninasubiri kwanza asinzie maana hataki nimshangae nilale nae tena.
Kwenye hiki chumba tupo wote tunalala na mama, kasoro baba ambaye madaktari wameshauri aondoke hadi masaa ya mwisho ndio aje. Wakionana wote wanalia inafanya mama achoke zaidi.
Mdogo wangu wa kiume kaleta maua ya Christmas na happy new year. Tumeyapamba hapa ndani. Mama kafurahi anatamani angetupikia chakula cha sikukuu. Sikukuu huwa anapika vyakula vingi na mdogo wetu wa kiume huwa anadeka anakaa na mama jikoni ili aonje. Mama anataka sikukuu wote tuwe nyumbani tumpikie mdogo wetu. Hatujui kama tutampa furaha anayoipataga kwa mama. Ila tutajitahidi.
Kasie Nakupenda. Asante sana.