Huyu Chenge ndie kinara wa ufisadi na kejeli kwa walalahoi! kila dili yumo! na huwa anapiga hela ndefu ya UMMA ambayo watakula kizazi chake cha tano kijacho! na wizi wao hutokana na kusahau kuwa cheo ni dhamana! na jeuri ya pesa wanazowaibia masikini wasiojua kuwa majasho yao yanaliwa na wajanja wachache kina Chenge!
Ila bado najiuliza kuna wabunge wangapi wana uwezo wa kupambanua issues na kuchangia kwa mantiki ili kuliokoa taifa na umaskini manake sirikali imeshindwa? na ndio maana ilitakiwa kigezo cha elimu kiwepo! binafsi nilidhani digrii moja ndo haswa ilifaa kuwa nayo mbunge wa zama hizi za Globalization! jamani tukatae tukubali , ukiwa na elimu ya form four huwezi kuwa sawa kiuelewa na mtu wa form six! form six hawezi kufanana na graduate! tunahitaji wabunge wasomi!huu si wakati wa mkoloni jamani miaka imeenda sana tubadilike kama wenzetu!
naamini umbumbumbu uko kila sekta bongo na hii ni kutokana na nepotism!! na hawa magamba hakuna mwenye nafuu, wote ni wale wale tu baba mmoja mama mmoja! ukitaka ushahidi wa ukweli taja gamba mmoja tu yoyote halafu waambie CAG na PCCB wamkague! utakayopata iwe siri yako! La maana tuwaondoe wote tuweke safu mpya uchaguzi wa 2015! UKAWA moto wa Escrow usizimike , upuliziwe mda wote! fanyeni operesheni kuelimisha wananchi wote vijijini!
Pia sasa ni wakati muafaka wa kudai na mikataba ya gesi ijadiliwe bungeni na sijui kwanini mlirudi bungeni kuridhiana na magamba, mngetoka moja kwa moja tukose wote potelea mbali tumezoea msoto miaka 50 sasa njaa na magonjwa ndio maisha yetu. Ila nawapongeza sana ZITTO , Kafulila na Ukawa kwa hatua waliyofikia katika kulimaliza sakata la escrow japo binafsi sijaridhika na maazimio kwakuwa bado naona yamewaacha huru mafisadi wote bila kujali ushahidi wa wazi wa wizi wao wa karne. kwangu mimi binafsi bongo imeandika historia ya kipekee duniani ya kuwaacha huru majangili ya taifa hili na kubariki wizi uliokubuhu wa kodi za walalahoi huku ushahidi dhahiri ukiwatia vitanzi mafisadi.
dhambi ya kuwafunga wanaovuta bangi kwa kukosa ajira na elimu na wezi wa kuku na kuwaachia kula bata bata majangili haya ya escrow na fisadi nyinginezo za nyuma itawahukumu wote wanaohusika! nawaza kuwa sasa hakuna chombo kinachoweza kuwajibisha wezi wa mabilioni ya umma hata wakamatwe red handed.na labda wanaowaza na wanaoendelea kuiba pesa ya umma sasa wataona kumbe poa tu kuiba mabilioni na hufanywi chochote! huwezi amini nilikuwa nikilipa bill 120,000 kwa mwezi kwa miaka miwili, nyumba ndogo, haina jiko la umeme , pasi mara moja kwa wiki, friji tunazima mchana! nilipofunga LUKU juzikati nimepigwa butwaa kwa maana kwasasa natumia 40,000 matumizi yote! sikujua kumbe hela zinaenda kwa haya majitu yasiyo na huruma wala aibu! ni mtazamo tu!