Mwisho wa Chenge umefika rasmi

Mwisho wa Chenge umefika rasmi

Kubwa la maadui, fisadi papaa aka A.Chenge...mie nilijua huyu atakaa kwenye system mpaka kuuzeeka kumbe Mwenyezi Mungu ni mkuu katoa maonyoo mchana kweupe...

Bado wale wengine waliochukua zile cash za stanbic unaweza kuta yupo mkuu wa kaya kwenye list hapo chachaaa

TUMSHUKURU SANA MUNGU na WAZUNGU , VINGINEVYO TUNGEKAMULIWA HADI DAMU ! HAWA WATU WANA ROHO MBAYA SIJAPATA KUONA !
 
Anaenda 'likizo' kula mafao yaek, ningeelewa vizuri zaidi kama angechunguzwa kisha kufilisiwa. huu upumbavu 'kuwajibishwa' tu, hautoshi.

Ngoja akale mafao yake vizuri sasa!!
 

Attachments

  • 1417531482760.jpg
    1417531482760.jpg
    29.8 KB · Views: 407
TUMSHUKURU SANA MUNGU na WAZUNGU , VINGINEVYO TUNGEKAMULIWA HADI DAMU ! HAWA WATU WANA ROHO MBAYA SIJAPATA KUONA !

Mkuu,

Hawa ni watanzania aina ya kipekee. Hawana huruma hata kidogo! Huyu jk sijui anajisikiaje anaposikia wanaume vijini wanazikimbia familia kwa sababu za michango ya maabara!
 
Mkuu,

Hawa ni watanzania aina ya kipekee. Hawana huruma hata kidogo! Huyu jk sijui anajisikiaje anaposikia wanaume vijini wanazikimbia familia kwa sababu za michango ya maabara!
Baada ya kusoma post yako nimejikuta nabubujikwa na machozi !
 
Mtafutie ushahidi wenye mashiko umburute kortini na usimamie kesi hiyo ili hukumu itoke kwa haki
Kuna kila dalili ya chenge kufungwa kabla mwaka huu haujaisha , cheo kimoja kimoja kinamdondoka !
 
rosemarie hilo ni dua la kuku kamwe halimpati mwewe..Chenge ni mtaalamu aliyebobea kwenye sheria na siasa hivyo ukimwona wa kazi gani duniani wanasema watampata lini....Usimwonee gere kwa kupata fedha hizo unachotakiwa kujiridhisha ni kama kweli fedha hizo hakustahili kulipwa au amekwiba....vinginevyo hata sala yako leo ilikuwa unamwomba shetani kwani Mungu hapokei dua za wenye husuda...

unamjua BOLLUSCON yuko wapi leo,kila asubuhi ina jioni
 
Wew unangali esrow , na RADA . Umesahau awamu ya pili ya akina sumaye. Mikataba yote ya serikali . barabara,10% amechukua yeye , mikataba yote ya madeni tanzanite , dhahabu, almasi na GES inayolikamua taifu yeye ndo mhusika mkuu .. Hapo bado manunuzi mengine makubwa ya SERIKALI kama magari na mengine huyu mtu ni TAJIRI kuliko inavyodhaniwa
Na bado escrow yumo.
Fikiri

Jamani chenge tuonee huruma yatosha sasa baba ...tavala na kerai
 
Mwenzenu navyo muinulia mikono chenge mpaka nahisi kwenye kashfa ya gesi hawezi kukosa
 

Mhhhhh kumbe unatabiri? Mi nilikuwa na shauku kuona Chenge kaishaje kumbe ndio kwaaaanza wewe unatabiri mwisho wake. Hata hivyo system yenu ilivyokuwa mbovu haijamuona na hatia yoyote and hata akiachia vyeo vyote ni mnampa likizo ya kwenda kula alivyochuma. I am sure kwa bilioni zote hizo alizokwapua hata akiachia ngazi haimtishi.
 
Alivyo jeuri si mlisikia alipokwa anazomewa bungeni wakati akimsaidia madame speaker kumpatia ''formulation'' nzuri ya maneno ya kuandika azimio kwa mkulu ,alisema wala hizo kelele hazimsumbui na alisikika waziwazi kwenye TV,jama ana ngozi ngumu kama ya kiboko mzee

Ila mwaka huu tutaichuna
 
Watanzania wenzangu,

kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho,Chenge ambaye kwa sasa ni Mbunge na Mwenyeketi wa kamati ya Uandishi wa Katiba mpya mwisho wake hakika hakika unakaribia kuliko jinsi tunavyoamini
huyu mtu amekuwa kwenye system kwa miaka mingi na tukumbuke ni mmoja wa wasomi wachache wa taifa letu waliosoma
harvard university

yaliyotokea mwisho wa week hii ndiyo chanzo cha kumalizika kabisa kwa fisadi huyu msomi ambaye katu hakuelimika na elimu yake

Chenge amen'golewa na nguvu ya maskini walewale aliokuwa akiwadharau siku zote,maazimio ya bunge yakisimamiwa na viongozi wetu tuliowatuma Bungeni yamesababisha kummaliza rasmi fisadi nguli Chenge,kwa taarifa tu ni kwamba Chenge ndiyo ametolewa rasmi kwenye system hii mbovu ambayo ni wajibu wetu watanzania wote kuitengeneza upya,fedha zote alizopata baada ya kuwasaidia wazungu ili watutapeli kwenye manunuzi ya rada zimefikia mwisho wake rasmi,fedha zote alizopata kwenye Escrow zinafikia mwisho wake,Kamwe Chenge hatarudi kwenye system hii milele na milele na kamwe hawezi kushinda ubunge tena na atakuwa mitaani na wana system wenzake watamgeuka na ATAVUNA ALICHOPANDA!

kilichobaki sasa hivi kwa Watanzania ni kuendelea kupambana kwa kutumia viongozi wetu na huku tukiwaombea na kuchangia vyama vyetu kwa nguvu zote ili tuweze kuendelea kuivunja system kidogo kidogo kwani system imeharibika mno kiasi kwamba tukisema ni ku offload once tutasababisha vita ya maangamizi kwenye taifa letu,

nimetoka kanisani na tumemshukuru Mungu kwa hapa tulipofika soo far,

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA VIONGOZI WAAMINIFU,AMEN!
Mkuu siku hazigandi............huyu bwana Chenge ndiye Waziri mkuu wa bwana EL kama atapita kuwa Raisi wa Tanzania........ni ajabu sana hawa mafisadi sijui wanawaona waTZ mapoyoyo.....? eti waziri mkuu wa EL ni chenge........!!!!??
 
ni tanzanian ambassador to the netherlands. Yule jamaa hana shida ukifika pale anakupokea vizuri sana.

Kwa kawaida Wahaya siyo mafisadi ..... ndiyo maana Ruge kajitahidi kuwakumbuka this time around. Nenda China ndiyo utajuwa Mafisadi wanabehave vipi!
 
Back
Top Bottom