Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #81
SEHEMU YA 64
JEMIMA akakubali. Safari ya Madagasca ikaanza. Wakiwa njiani walipita kwenye maeneo mbalimbali ambapo mapigano yalifanyika.
Wakashuhudia maiti nyingi za watu zilizokuwa ziking’ong’wa na nzi na ukimya wa ajabu ulikuwa umetawala kisiwani hapo. Bila kutegemea Jemima alijikuta roho ikimuuma.
Mungu wangu! Alijisemea moyoni.
Swadege imebadilika na kuwa hivi? Alijiuliza kwa mshangao akizitazama kwa wahaka maiti zilizosambaa kila mahali. Akiendelea kuzitazama kumbukumbu ya mauaji ya mama yake na kaka yake Kalega ikarejea kichwani.
Uchungu ukajaa moyoni, macho yakaongeza ung’aavu wa machozi kupigania kutoka, Jemima akameza funda kubwa la mate ya baridi yaliyojaa mdomoni kutokana na hasira.
Hata hivyo hakusema lolote, alimtazama Azra na moyoni akakili maisha aliyokuwa anaishi na ndugu zake kisiwani hapo yasingeweza kujirudia tena. Chaguo lake lilikuwa ni kuendelea kumsapoti mpenzi wake huyo. Wakasafiri mpaka Madagasca!
Walipofika Azra aliwasiliana na Marekani na kuwapasha habari ya maafa aliyosababisha. Kina Jaden Smith wakafurahi kwelikweli.
Siku hiyohiyo wakamtumia chopa kama tisa zenye wanajeshi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
Azra akarudi Swadege na kujitangaza kuwa mfalme wa kisiwa hicho na Jemima ndiye malkia.
Akaagiza kwa kutumia teknolojia iliyotokana na mazao ya uhai ajengewe bangaloo la maana ambalo ndilo litakuwa ikulu atakayoishi kwa raha mustarehe na mpenzi wake Jemima wakitafuna raha za dunia.
Wapambanaji wa Swadege wote waliosalia wakalazimishwa kumuunga mkono. Akawaamuru pia wapambanaji hao kuingia mtaani na kukusanya maiti zote na kwenda kuzitupa mtoni.
Hilo likafanyika, baada ya siku kadhaa Marekani ikaanza kuingia nchini humo na kubeba matani kwa matani ya Mazao ya uhai.
*** Mioyo za watu wa Swadege zilikuwa zinavuja damu. Kila mtu kwa wakati wake alikuwa akilia kuliko kawaida kutokana na hali ilivyokuwa. Kilichowauma zaidi alikuwa ni Jemima kushirikiana na adui aliyeangamizi maelfe ya ndugu zao.
Hata hivyo, huku Waswadege wakiumia, Jemima naye alijikuta kwenye sononeko la nafsi lililotokana na namna mazao ya uhai yalivyokuwa yanachukuliwa kwa kasi na Wamerekani, kingine ilikuwa ni tabia mpya za Azra kupenda wanawake.