Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #61
SEHEMU YA 51
“Ni mimi niliyeongoza mapambano ili auawe au afukuzwe kisiwani hapa.” Kalega alimwambia Bonza.
“Wako wapi ndugu zetu kiongozi wa mapambano?” Bonza alimuuliza Kalega huku akishuka kwenye farasi na kumsogelea.
“Tazama,” Kalega alizungumza kwa upole kwani ilibidi ajishushe.
“Ni mashujaa pekee hufia vitani, hatuna budi kuwapa heshima yao katika mazishi huku tukiandaa mauaji ya kinyamakwa adui ambaye tayari yupo mikononi mwetu.”
“Mazishi ya heshima hayawezi kupendeza bila mwili wa dada yako na mama yako,” Bonza alimwambia Kalega.
Watu wengine walishuka pia kwenye farasi zao.
“Hapana,” Kalega alizungumza kwa hamaki kisha akachomoa panga lake. “Si mimi niliyewaua ndugu zenu. Si mama yangu wala dada yangu.”
Hata hivyo kundi lile tayari lilikuwa limekwisha dhamilia kufanya maafa nyumbani hapo kwao Kalega. Lilimvaa kijana huyo na kuanza kupigana naye.
Baada ya kuona hivyo mama Cecilia na mwanaye walikimbilia ndani, harakaharaka walichukua vitu muhimu ikiwemo vipande vya mazao ya uhai kisha wakatoka nje tena.
“Kimbieniiii…” Kalega aliwaambia huku akiendelea kupambana.
Lakini mama yake moyo ulikuwa mzito kumuacha mwanaye akifa kwa ajili yake.
“Mama kimbieni nasema,” Kalega alirudia.
Wakati akimaliza kuzungumza hivyo, mara alichomwa mkuki wa mbavu, Twiii! Akapiga kelele za maumivu. Mama yake tumbo la uzazi lilikata.
Akakimbilia pale alipodondokea mwanaye. Naye akapigwa mshale wa mbavu na kufa papohapo.
Jemima kuona hivyo alamu ya hatari iligonga kichwani kwake na akafahamu ilikuwa ni zamu yake ya kuuawa.
Akiwa ameshika mazao ya uhai mkononi, msichana huyo alianza kukimbia kwa nguvu zake zote.
Hata hivyo baada ya kundi lile kuwamaliza mama Cecilia na Kalega, walianza kumkimbiza pia Jemima.
Jemima moyoni alikuwa ameamua kwamba, kama siku yake ya kufa ilikuwa imetimia basi kifo kingemkuta akijaribu kujiokoa na hakuwa tayari kukisubiri.
Msichana huyo aliedelea kukimbia kwa nguvu zake zote utadhani alikuwa kwenye mashindano ya marathoni na jambo la bahati nzuri kwake, baada ya kukimbia mita takribani elfu moja mia tano, alifika kwenye Msitu wa Sonve, akauvaa msobemsobe huku akiendelea kukimbia akihema kwa uoga.