Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #41
SEHEMU YA 31
Siku zilizidi kusonga mbele lakini hadi mwezi mmoja unakatika akiwa anaishi mahali hapo hakuwahi kuulizwa jambo lolote na wazee hao, kuhusu asili yake pamoja na mambo mengine.
Jambo hili lilimshangaza kwani mategemeo yake ilikuwa ni kuulizwa maswali ili aweze kufahamu wazee hao walikuwa wanawaza nini juu yake.
Hata hivyo yote tisa- kumi jambo lililomshangaza zaidi, kila siku usiku majira ya saa kumi, alikuwa akisikia watu wakizungumza kwenye vyumba vya nje ya kile alichopewa kuishi na baada ya hapo alisikia milango ikifunguliwa na hatua za watu wakiondoka.
Alipochungulia kupitia kidirisha kidogo cha chumba hicho anachoishi aliona wazee watatu, mmoja wao alikuwa ni mzee Makimbi, aliyempokea na wawili ni rafiki zake, wakiwa wamejifunga mashuka ya kimasai na waliondoka wakiwa pekupeku.
Suala hili lilimpa wasiwasi mno Azra. Alijiuliza watu hao walikuwa wanakwenda wapi kila siku usiku lakini hakuweza kupata jibu.
Ndipo siku moja alipoamua kujifunga mkanda kuwafuatilia ili aweze kufahamu ni wapi wanakwenda.
Kweli kama alivyopania hazikuchukua hata siku mbili za kutekeleza zoezi lake toka alipopata mawazo hayo.
Siku hiyo alijipanga.
Hakusinzia kabisa. Alilala akikapua mpaka yalipofika majira ya saa kumi za usiku. Kama kawaida alisikia milango ikifunguka na baada ya muda watu wakizungumza nje na hatua zilisikika watu hao wakiondoka.
Azra alikuwa anafuatilia vizuri kila kilichokuwa kinaendelea akiwa chumbani kwake. Baada ya wazee hao kupotea kwenye upeo wa macho yake, Azra alitoka kwenye chumba alichokuwa analala kisha kwa tahadhali kubwa alianza kuwafuatilia wale wazee.
Hakika ilikuwa siyo safari ya kawaida. Azra alitembea kuliko alivyowahi kutembea huko kabla. Saa zima lilikatika akitembea akiwafuatilia wale wazee mpaka walipofika eneo ambalo lilionekana ndiyo mwisho wa safari yao.
Baada ya kufika katika eneo hilo Azra akiwa amejibanza sehemu akiwafuatilia kwa macho wazee hao watatu, kiukweli alibaki ameduwaa haamini alichokuwa anakiona.
Eneo hilo lilikuwa ni sawa na kijiji kipya chenye watu wengi lakini hakukuwa na nyumba hata moja. Kilichomshangaza zaidi kila aliyemuona mahali hapo alfajiri hiyo alikuwa bize na shughuli fulani anafanya.