Mkuu hata sielewi argument hapa. Debt % per GDP ya Mwinyi ilikuwa juu, inflation na karibu kila kitu ukiangalia wakati wake ndio tulikuwa vibaya zaidi lakini huu ndio undani wa uchumi kulingana na data hali wananchi walifurahia zaidi ruksa ambayo iliwapa uwezo wa kuiba mali zao wenyewe.
Wakati Mzee Mwinyi anachukua Madaraka, mwaka 1985 Inflation ilikuwa 36.1%, mwaka 1986 akafanikiwa kuipunguza kwa 7.76% na kufikia 33.3%. Mwaka 1987 akashusha inflation kutoka 33.3% na kufikia 32.4%. mwaka 1987, mwaka 1988 hakufanikiwa kuishusha hiyo inflation na matokeo yake ikapanda hadi 47.702% ikiwa ni ongezeko la asilimia 47.23. mwaka 1989 ilifanyika kazi ya ziada na inflation ikashuka kutoka hiyo 47.702% hadi 20.602% mwaka 1990 iflation ilikuwa 22.562%, mwaka 1991 ilikuwa 28.037%, mwaka 1992 ikashuka na kufikia 21.935%. mwaka 1993 ikawa 23.619%, na mwaka 1994 ikapanda tena hadi 37.146, na mwaka 1995 ikashuka hadi 23,969%. kwa hiyo kwa Mujibu wa hizi data ni dhahiri Mzee Mwinyi na serikali yake walikuwa wanapambana na mfumuko wa bei, wakati mwingine unapanda na mara nyingi zaidi wanaushusha. ukiondoa mwaka 1988 na mwaka 1994 ambapo mfumuko wa bei ulikuwa ni asilimia 47. 702 na 37.146%, miaka yote 8 iliyobakia ya utawala wake mfumuko wa bei ulikuwa chini ya mfumuko wa bei katika kipindi cha miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Nyerere(1980 hadi 1985).
mfumuko wa bei 1980 ulikuwa 30.205%, mwaka 1981 ulikuwa 30.3%, mwaka 1982 ulikuwa 25.7%, mwaka 1983 ulikuwa 28.9%, mwaka 1984 ulikuwa 27.1%, na mwaka 1985 ulikuwa 36.1%.
chanzo cha hizi data.
Tanzania Inflation rate (consumer prices) - Economy
Na kwa upande wa GDP per Capita.
data zinaonyesha kuanzia mwaka 1977 mpaka 1984 GDP per Capita ilikuwa inashuka wakati 1985 mpaka mwaka 1993 ukiondoa mwaka 1991 , GDP per Capita ya Tanzania ilikuwa ikipanda,
na data ziko kama hivi ifuatavyo.
mwaka 1977, GDP per Capita ilikuwa 968 (TSH), mwaka 1978 ilikuwa 950 Shillings, mwaka 1979 ilikuwa 944 shillings, mwaka 1980 ilikuwa 933 shillings, mwaka 1981 ilikuwa 915 shillings, mwaka 1982 ilikuwa 885 shillings, mwaka 1983 ilikuwa 853 shillings, mwaka 1984 ilikuwa 835 shillings, mwaka 1985 ilikuwa 840 Shillings.
wakati mwaka 1986 ilikuwa 843 shillings, mwaka 1987 ilikuwa 860 shillings, mwaka 1988 ilikuwa 880 shillings, mwaka 1989 ilikuwa 885 shillings, mwaka 1990 ilikuwa 890 shillings, mwaka 1991 ilikuwa 860 shillings, mwaka 1992 ilikuwa 904 shillings na mwaka 1993 ilikuwa 915 shillings.
source of information.
Macro-economic trends in the Tanzanian economy
Kwa mujibu wa data hizo hapo juu, theluthi ya mwisho ya utawala wa Nyerere kiuchumi ilikuwa chini kabisa kulinganisha na sehemu kubwa ya Utawala wa mzee Ruksa. na nadhani ndo maana Watanzania wa Kawaida, wanamheshimu sana huyu mzee kwa sababu sera zake zilikuwa ni kwa ajili ya kuwagusa watu moja kwa moja.