Mwinyi ndiye Rais bora kuwahi kutokea katika Taifa hili, anaondoka wala hatuna kinyongo nae

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,842
Tafakuri Jadidi:

Mzee Mwinyi Anaondoka Na Hatuna Kinyongo Nae..

"Kila zama na kitabu chake"- Ali Hassan Mwinyi.
Na leo Watanzania zimetufikia habari za kuhitimishwa kwa Sura ya Mwisho ya Kitabu Cha Mzee Mwinyi. Ameifariki Dunia.

Umma umegubikwa na simanzi. Mzee Mwinyi tulimpenda sana.

Naam, kwamba ‘ Kila Zama Na Kitabu Chake’ maneno hayo yalipata kusemwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Ni miaka mingi iliyopita.

Kwenye kila zama na kitabu chake, Mzee Mwinyi anazungumzia juu ya nyakati. Uwezo wa kusoma alama za nyakati. Mwanafalsafa Benjamin Di Israel alipata kuzungumzia juu ya dhana ya kiongozi mzuri.

Kwamba kiongozi mzuri ni yule anayejijua mwenyewe na nyakati zinazomzunguka- He who knows himself and the time that sorounds him. (Zilikuwa nyakati nyingine, siku hizi Kiongozi Mkuu aweza kuwa mwanamke kama ilivyo kwetu.)

Na ilivyo kwa mwanadamu, hata anapogombea nafasi ya juu ya uongozi wa nchi, mbali ya matarajio ya chama kilichomteua, naye, kama mwanadamu, huwa na matarajio yake ya anayotaka akumbukwe nayo pindi atakapotoka madarakani. Inahusu legacy.

Kwa mtazamo wangu, na wengi wenye kufuatilia masuala ya kisiasa, Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa ' Mliberali'.

Alipoingia madarakani alikutana na jamii iliyozoea ' marufuku' ya hiki na kile. Mzee Mwinyi akaja na ' ruksa' kwa watu kufanya mambo yao alimradi wanafuata sheria. Ndio msingi wa kuitwa " Mzee Ruksa'.

Naam, zama za Mzee Mwinyi zilikuwa ni ' Zama za Ruksa'. Ni zama zilizofungua milango ya watu kufanya biashara na upana wa demokrasia ikiwamo uhuru wa watu kujieleza ikiwamo magazeti na hata Televisheni.

Na kwenye utawala wake, Mzee Mwinyi alivumilia maneno mengi dhidi yake. Mwinyi hakuishia kusemwa tu, kuna hata waliodiriki ' Kumtukana matusi ya nguoni' kama alivyotamka mwenyewe kwenye moja ya hotuba zake miaka ile ya 90 mwanzoni.

Lakini, Mzee Mwinyi hakuyumbishwa katika yale mema aliyoazimia kuwatendea watu wake.

Siku moja kabla ya kukabidhi madaraka kwa Benjamin Mkapa, Mzee Mwinyi, akiwa chini ya shutuma nyingi dhidi yake kwenye vyombo vya habari na hata Wana- CCM wenzake, alichagua kwenda kuzungumza na Wananchi pale Manzese.

Ndio, Mwinyi aliongea na wananchi wa hali za chini kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi; eneo la Manzese Uzuri. Nilikuwepo pale viwanjani kushuhudia tukio lile.

Mzee Mwinyi kwenye hotuba yake alianza kwa
kuwashukuru wananchi na baadae akasema;

"Ndugu zangu,

Nilipoingia madarakani niliwakuta mkipanga foleni ya sukari, unga, na hata mkinunua bidhaa muhimu kwenye ' Maduka ya Kaya, kweli si kweli?"

"weliii...!" Umma uliitikia.

"Je, leo mnapanga foleni ya sukari au kwenda kununua bidhaa muhimu kwenye maduka ya kaya tu?" - Mwinyi aliwauliza wananchi wale.

Jibu likawa la sauti ya jumla;

" Hapanaa!"

Mwinyi akaendelea na kuwapa mifano mingine kadhaa ya hali aliyoikuta akiingia madarakani, na kuwauliza wananchi wale kama hali imebaki hivyo hivyo kwa wakati ule akiondoka madarakani. Na majibu yakawa ni ' Hapanaa!"

Na siku ikawadia. Ni siku ya kwenda Uwanja wa Taifa kukabidhi mamlaka ya uongozi wa nchi kwa Benjamin Mkapa. Kuna wananchi waliojipanga kutoka Ikulu ya Magogoni kumpungia mikono ya kumsindikiza Mwinyi akielekea Uwanja wa Taifa.

Na pale uwanjani Mwinyi alipokewa na sauti za ' Ruksaa, Ruksaa!" Ni kutoka kwa Wananchi.

Naam, kila zama na kitabu chake.

Kwaheri Mzee Wetu Mpendwa, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

PS:

Na kwenye moja ya hotuba zake za kuwaaga Wananchi wake Mzee Mwinyi alisikika akisema;

"Na wote walonitukana, hata matusi ya nguoni mie sina kinyongo nao."
Nasi twasema, hatuna kinyongo na Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi.
 
Tafakuri Jadidi:

Mzee Mwinyi Anaondoka Na Hatuna Kinyongo Nae..

" Kila zama na kitabu chake"- Ali Hassan Mwinyi.
Na leo Watanzania zimetufikia habari za kuhitimishwa kwa Sura ya Mwisho ya Kitabu Cha Mzee Mwinyi. Ameifariki Dunia.

Umma umegubikwa na simanzi. Mzee Mwinyi tulimpenda sana.

Naam, kwamba ‘ Kila Zama Na Kitabu Chake’ maneno hayo yalipata kusemwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Ni miaka mingi iliyopita.

Kwenye kila zama na kitabu chake, Mzee Mwinyi anazungumzia juu ya nyakati. Uwezo wa kusoma alama za nyakati. Mwanafalsafa Benjamin Di Israel alipata kuzungumzia juu ya dhana ya kiongozi mzuri.

Kwamba kiongozi mzuri ni yule anayejijua mwenyewe na nyakati zinazomzunguka- He who knows himself and the time that sorounds him. ( Zilikuwa nyakati nyingine, siku hizi Kiongozi Mkuu aweza kuwa mwanamke kama ilivyo kwetu.)

Na ilivyo kwa mwanadamu, hata anapogombea nafasi ya juu ya uongozi wa nchi, mbali ya matarajio ya chama kilichomteua, naye, kama mwanadamu, huwa na matarajio yake ya anayotaka akumbukwe nayo pindi atakapotoka madarakani. Inahusu legacy.

Kwa mtazamo wangu, na wengi wenye kufuatilia masuala ya kisiasa, Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa ' Mliberali'.

Alipoingia madarakani alikutana na jamii iliyozoea ' marufuku' ya hiki na kile. Mzee Mwinyi akaja na ' ruksa' kwa watu kufanya mambo yao alimradi wanafuata sheria. Ndio msingi wa kuitwa " Mzee Ruksa'.

Naam, zama za Mzee Mwinyi zilikuwa ni ' Zama za Ruksa'. Ni zama zilizofungua milango ya watu kufanya biashara na upana wa demokrasia ikiwamo uhuru wa watu kujieleza ikiwamo magazeti na hata Televisheni.

Na kwenye utawala wake, Mzee Mwinyi alivumilia maneno mengi dhidi yake. Mwinyi hakuishia kusemwa tu, kuna hata waliodiriki ' Kumtukana matusi ya nguoni' kama alivyotamka mwenyewe kwenye moja ya hotuba zake miaka ile ya 90 mwanzoni.

Lakini, Mzee Mwinyi hakuyumbishwa katika yale mema aliyoazimia kuwatendea watu wake.

Siku moja kabla ya kukabidhi madaraka kwa Benjamin Mkapa, Mzee Mwinyi, akiwa chini ya shutuma nyingi dhidi yake kwenye vyombo vya habari na hata Wana- CCM wenzake, alichagua kwenda kuzungumza na Wananchi pale Manzese.

Ndio, Mwinyi aliongea na wananchi wa hali za chini kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi; eneo la Manzese Uzuri. Nilikuwepo pale viwanjani kushuhudia tukio lile.

Mzee Mwinyi kwenye hotuba yake alianza kwa
kuwashukuru wananchi na baadae akasema;

" Ndugu zangu,

Nilipoingia madarakani niliwakuta mkipanga foleni ya sukari, unga, na hata mkinunua bidhaa muhimu kwenye ' Maduka ya Kaya, kweli si kweli?"

" Kweliii...!" Umma uliitikia.

"Je, leo mnapanga foleni ya sukari au kwenda kununua bidhaa muhimu kwenye maduka ya kaya tu?" - Mwinyi aliwauliza wananchi wale.

Jibu likawa la sauti ya jumla;

" Hapanaa!"

Mwinyi akaendelea na kuwapa mifano mingine kadhaa ya hali aliyoikuta akiingia madarakani, na kuwauliza wananchi wale kama hali imebaki hivyo hivyo kwa wakati ule akiondoka madarakani. Na majibu yakawa ni ' Hapanaa!"

Na siku ikawadia. Ni siku ya kwenda Uwanja wa Taifa kukabidhi mamlaka ya uongozi wa nchi kwa Benjamin Mkapa. Kuna wananchi waliojipanga kutoka Ikulu ya Magogoni kumpungia mikono ya kumsindikiza Mwinyi akielekea Uwanja wa Taifa.

Na pale uwanjani Mwinyi alipokewa na sauti za ' Ruksaa, Ruksaa!" Ni kutoka kwa Wananchi.

Naam, kila zama na kitabu chake.

Kwaheri Mzee Wetu Mpendwa, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

PS:

Na kwenye moja ya hotuba zake za kuwaaga Wananchi wake Mzee Mwinyi alisikika akisema;

" Na wote walonitukana, hata matusi ya nguoni mie sina kinyongo nao."
Nasi twasema, hatuna kinyongo na Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi.
Kama sio ummat mudi... Basi unafiki unakusumbua
 
Namkubali sana Mzee Mwinyi lakini kusema ameondoka ikiwa watu hawana kinyongo nae, sio kweli.

Ameondoka kipindi ambacho wale waliopaswa kuwa na kinyongo nae wengi wao aidha washatangulia mbele za haki ama kama wapo ni watu wazima sana kama alivyokuwa yeye au hawakuwa na direct impact na uraisi wake (mfano kama kina sisi ambao tulikuwa watoto wadogo)

Leo hii Kikwete akikata moto kuna baadhi ya watu tutawasha mpaka mafataki kushangiliia sababu utawala wake bado ni mbichi kwenye kumbumbuku zetu ila akifa miaka 20 ijayo kutakuwa na sifa na mapambio tu juu yake..

All in all may Allah accord Mzee Mwinyi's soul the highest rank of Jannah.
 
Back
Top Bottom