Hata mimi namkubali sana mzee Ruksa. kuanzia uhuru wa Habari ambao baadhi ya waandishi waliutumia vibaya kumshambulia, lakini baadae wakaja kuandika makala/barua ya kuomba msamaha kwa jambo hilo.
Urejeshwaji wa vyama vingi vya siasa.
Kuwapa uhuru wananchi kutumia jasho lao na akili zao kujitafutia mali na utajiri binafsi.
Kulinda vyema mipaka ya nchi yetu.
Kudhibiti majambazi (chini ya Augustine Mrema).
Kupunguza kero za muungano kwa kuondoa haja ya kuingia Zanzibar na Passport
Kuinua michezo kama vile soka na masumbwi, Kuimarisha , Umiseta, Umitashumta, na matunda yake katika kipindi hicho Simba ilitwaa ubingwa wa Afrika mashariki na kati( Sima vs- Sports club villa 1990), yanga nayo (Yanga Vs -sports club Villa 1992 kampala), Simba ilifika fainali CAF 1993, 1992 enzi za Kakakuona, akina Matumla nao haikuwa Nyuma katika masumbwi enzi hizo.
Uanzishwaji wa Tv binafsi, CTN, ITV, DTV.
Radio binafsi, Radio one.
Wananchi kuanza kutoka kwa wingi kwenda ng'ambo, vijana wengi enzi hizo walikwenda Dubai kuchukua bidhaa, na miongoni mwao kwa sasa ni matajiri wakubwa kabisa na walipa kodi wazuri tu kwa sasa.
Serikali kuendelea kuwekeza kwenye Elimu na udhibiti wa mitihani, mitahani haikuvuja hovyohovyo kipindi cha mzee Ruksa.
Kuonyesha uwajibikaji kwa mkuu wa nchi kwa kutimua baraza lote la mawaziri na kuunda jipya, precedence nzuri kwa maraisi wajao, ambapo naona kikwete alifuata nyayo hapo mwaka juzi.
Kingine ni utu na huruma ya huyu mzee, uwezo wa kustahimili kashfa na mashambulizi pasipo kuwapoteza watu Lupango nacho pia kinapendeza kwa kiongozi. Si mtu wa visasi wa kutumia hadi mbinu mbaya za kuwavua watu Uraia n.k
Lakini kingine ilikuwa ni uwezo wa kufanya maamuzi binafsi na kutoshinikizwa, Pamoja na Nyerere kuwa hai na kutetea sana misimamo yake, mzee Mwinyi yeye alikuwa anasikiliza lakini akifanya maamuzi anayafanya kwa jinsi anavyoona yeye inafaa na wala haendi kwenye malumbano.