KUNA tetesi kuwa baada ya Spika wa Bunge leo 28/6/2023 kumtangaza bungeni Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuwa alikuwa sahihi kuhusu kutotekelezwa kwa maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Mawaziri Mwigulu Nchemba na Januari Makamba wamekutana kwa kikao cha dharura kujadili uamuzi huo wa Spika.
Inasemekana kuwa wawili hao kwa muda mrefu walitumia nafasi zao kuzihadaa mamlaka za Chama na Serikali kuwa Mpina amekuwa akisema uongo kwa lengo la kuichafua Serikali ya Rais Samia jambo ambalo Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amekata mzizi wa fitna kwa kuweka wazi.
Hivyo kwa sasa wanahaha watakwenda kusema nini kuhusu Mpina ilihali walishaziaminisha mamlaka kuwa Mpina ni mpingaji wa Serikali ya Rais Samia.