Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo, Juma Duni Haji ajiondoa kutetea nafasi ya Uenyekiti ACT

Wakati Babu Duni anakwenda kuchukua fomu, alipata wasaa wa kuongea na wanachama wa ACT kuhusu sababu za yeye kutaka kuendelea kuongoza chama hicho.

Babu Duni ambaye mm binafsi hupata raha sana kumsikiliza kutokana na ucheshi wake alieleza mengi na hasa ukweli kuwa bado ana uwezo wa kuongoza chama hicho.

Babu Duni ambaye amezunguka nchi nzima kuipromoti ACT amejikuta katika wakati mgumu kufuatia makamu wake kuchukua fomu na yeye kuambiwa ajitoe kwa sababu ni mzee.

Siku ile anaongea na wanachama wakati anachukua fomu alitoa mifano mingi akimrejea mzee Mandela, akamrejea Maalim Seif na viongozi kede kede.

Akasema na ninamnukuu, "Mm sina kiburi, siiiina."

Leo Babu Duni ambaye wanachama wake walijitokeza kupinga kiongozi huyo kudhalilishwa amejiondoa kugombea nafasi hiyo.

Sijui Babu Duni amepatwa na nini.

Babu Duni nimjuae mm sio muoga, sio urojo wala sio mnyonge lkn kwa Othman Masoud kaachia mwenyewe.Kwa.mtaji huo Babu Duni ndio amepotea kisiasa, atapewa nyadhifa nyingine lkn uenyekiti mtamu bana.Pole sana Babu Duni.
Ndio kheri yake. Apate muda wa kutosha kumtumikia Muumba wake. Kama kuipigania Zanzibar ashaipigania vya kutosha. Ishatosha sasa awaachie wengine waendeleze. Wenziwe ktk siasa wote washatangulia mbele ya Allah hilo ni funzo tosha kwake
 
ACT wazalendo mmekuwa mkipinga mgombea kupita bila kupingwa, leo mmemstaafisha siasa bila kupenda mzee Juma Duni Haji.

Mbona mnatuchanganya sana nyie, mnapinga mgombea kupita bila kupinga tena mapovu yanawatoka majukwaani halafu leo mnamshawishi Juma Duni amuachie Othman.
 
ACT wazalendo mmekuwa mkipinga mgombea kupita bila kupingwa, leo mmemstaafisha siasa bila kupenda mzee Juma Duni Haji.

Mbona mnatuchanganya sana nyie, mnapinga mgombea kupita bila kupinga tena mapovu yanawatoka majukwaani halafu leo mnamshawishi Juma Duni amuachie Othman.
Ayatollah Khomeini keshatoa maelekezo
 
Kitaasisi CCM imeviacha mbali vyama vya upinzani
1. shallow analysis, extremly shaloow analysis of issues. Unadhani watu hawataki kugombea urais na samia? Ukichukua fomr (kama wamechapisha mbili anyway) wanakufukuza uanachama and you are done.
2. CCM imesimama kwa vile ina DOLA nyuma yake. ndiyo maana mnakataa tume huru, marekebisho ya Katiba and the like. Taasisi inayojisimamia haiwezi kuogopa tume huru...., katiba mpya, kuwabambikia wapinzania kesi, kuzuia mikutano ..for about six yrs...UNAOGOPA NINI, WEWE SI TAASISI IMARA
 
Siasa za viini macho na ACT 😂😂😂
Hawa ACT Zitto alikuwa anaichambua kila report ya CAG awamu ya tano. Toka wapewe asali yupo kimya.

Hawa ACT, Zitto wakikuwa wanasumbua sana wakati wa awamu ya tano. Wamepewa asali wako kimya. Matatizo kibao nchini.

Hiko ni chama cha kupigania asali kwa ACT na Zitto sio maslahi ya Tanzania.
 
Kuna chama mwenyekiti wao kuanzia mwaka 2003 ni yeye tuu wengine wote hawawezi
 
Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo, Juma Duni Haji maarufu kama Babu Duni amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti ACT – Wazalendo na kumuunga mkono makamu wake, Othman Masoud Othman.

Babu Duni amejiondoa kutetea nafasi hiyo aliyokuwa akihudumu kabla ya muda wake kuisha leo Jumatatu Machi 4, 2024, ikiwa imesalia siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo utakaowachagua viongozi wakuu wa kitaifa.

Kabla ya hatua hiyo, umekuwepo mchuano mkali baina ya wawili hao, huku Babu Duni akilalamikia hujuma za watu waliokuwa wanamshinikiza ajiondoea kwa kuwa ni mzee na kitendo cha wenyeviti wa mikoa kumchukulia fomu mshindani wake.
Mpaka dak hii bado hajalipia kadi yake ya CCM (Ada kwa mwaka 1200)?
 
Back
Top Bottom