Juma Duni "Babu Duni" Mwenyekiti, ACT Wazalendo; ACT Tumefarijika Sana na Rais Samia Kubadili Sheria, Tunaomba Ratiba ya Utekelezaji

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,640
Wanabodi

Nimekutana Face2Face c̅ Juma Duni Haji al maarufu "Babu Duni" Mwenyekiti, ACT Wazalendo, amesema "ACT Wazalendo wamefarijika sana na hatua mbalimbali ambazo Rais Samia Suluhu Hassan anazochukua kuimarisha demokrasia nchini ambapo kikao cha Bunge cha mwezi October, kitapokea miswada 3 ya kubadili Sheria, kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, kubadili sheria ya uchaguzi, na kurekebisha sheria ya Msajili wa vyama vya Siasa.

Juma Duni ameomba serikali itoe ratiba ya utekelezaji".

Msikilize Babu Duni.

View: https://youtu.be/YLjwcGPwzO8?si=cVk4I0D3d30aL32F

Paskali
 
kubadili sheria ya uchaguzi, na kurekebisha sheria ya Msajili wa vyama vya Siasa.
Kubadili sheria ni jambo moja lkn kama katiba itabakia kuwa hii hii inayomfanya rais kuwa Mungu mtu hakutakuwa na jipya.

Katiba mpya iandikwe ili rais apunguziwe madaraka. Asiteue kila kiongozi nchi hii na asiwe bosi wa kila mtu.

Sheria nyingi zinavunjwa kwasabb rais yuko juu ya katiba hivyo anaweza kuparaganya kupitia wateule wake na asifanywe kitu huyo mteule kwasbb katumwa na rais aliye juu ya katiba.

Sijui mnanielewa??
 
Wanabodi

Nimekutana Face2Face c̅ Juma Duni Haji al maarufu "Babu Duni" Mwenyekiti, ACT Wazalendo, amesema "ACT Wazalendo wamefarijika sana na hatua mbalimbali ambazo Rais Samia Suluhu Hassan anazochukua kuimarisha demokrasia nchini ambapo kikao cha Bunge cha mwezi October, kitapokea miswada 3 ya kubadili Sheria, kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, kubadili sheria ya uchaguzi, na kurekebisha sheria ya Msajili wa vyama vya Siasa.

Juma Duni ameomba serikali itoe ratiba ya utekelezaji".

Msikilize Babu Duni.

View: https://youtu.be/YLjwcGPwzO8?si=cVk4I0D3d30aL32F

Paskali

Pascal Mayalla, unaayaamini maneno ya mwenyekiti wa ACT Wazalendo aliyoyapokea kutoka kwa mwenyewe wa Chama Cha Mafisadi?
 
Wanabodi

Nimekutana Face2Face c̅ Juma Duni Haji al maarufu "Babu Duni" Mwenyekiti, ACT Wazalendo, amesema "ACT Wazalendo wamefarijika sana na hatua mbalimbali ambazo Rais Samia Suluhu Hassan anazochukua kuimarisha demokrasia nchini ambapo kikao cha Bunge cha mwezi October, kitapokea miswada 3 ya kubadili Sheria, kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, kubadili sheria ya uchaguzi, na kurekebisha sheria ya Msajili wa vyama vya Siasa.

Juma Duni ameomba serikali itoe ratiba ya utekelezaji".

Msikilize Babu Duni.

View: https://youtu.be/YLjwcGPwzO8?si=cVk4I0D3d30aL32F

Paskali

Kubadili sheria ni kitu kingine na utekelezaji ni kitu ingine kbs!!
 
Mmmhh, ni kwamba hatukuoni wala kujua ulivyokuwa huko nyuma? Kwa taarifa yako binadamu huwa kuna namna anajijua, na namna anavyojulikana. Unavyotaka tukujue sio ulivyo.
Kwa vile kuna watu wanawajua watu kuliko wanavyo jijua wenyewe, mimi ninajijua na wanaonijua wananijua ila pia ni rukhsa kumdhania mtu vyovyote utakavyo mdhania.
P
 
Hivi ACT Wazalendo si wanataka mamlaka kamili? Wameacha suala la Katiba na sasa ni sheria

Hawa watu ni wanafiki sana, kisa tu Rais ni Mzanzibar. Akija mwingine utasikia kelele za Katiba mpya na mamlaka kamili.

Huwezi kupata mamlaka kamili kwa katiba ya 1977 ni mbovu sana haiwezi kurepewa hata na Wajapan.

JokaKuu
 
Kwanini umesema hivyo ?.

ACT wako very strategic , Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza

Haya nitawauliza CUF.
P
ACT wako very strategic ila hawana mvuto kwa watu. Ukitaka kujua nenda kaangalie uchaguzi mdogo wa Mbarali, CDM hawashiriki uchaguzi wote umekosa mvuto. Hizo strategic za ACT ndio zilitakiwa impact yake ionekane kwenye chaguzi hizi.

Hizo strategic za kujipendekeza kwenye mikutano ya kupotezeana muda, ndio hao wanaoandaa hiyo mikutano wanafika na kuwaambia katiba haileti maendeleo.
 
Kwa suala la katiba mpya tuwe wakweli tu, kwamba Zitto na ACT Wazanzibar wamehujumu sana jitihada.

Tume huru ya uchaguzi ni upuuzi wa hali ya juu. Zitto na Duni si wanajua Zanzibar kulikuwa na tume huru ikiwa na 50/50 ya wajumbe CCM/CUF. Jecha kama mpini wa Dola aliwapiga chini CUF

Huwezi kuwa na tume huru wakati sheria kama ya usalama imebadilishwa na kutoa mkono wa chuma.

Kwa nguvu za ACT Wazanzibar kama wasingeshirikiana na CCM Katiba mpya ingepatikana hata December.

Unafiki ni kitu kibaya sana
 
Back
Top Bottom