JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,702
- 6,498
Babu Duni amejiondoa kutetea nafasi hiyo aliyokuwa akihudumu kabla ya muda wake kuisha leo Jumatatu Machi 4, 2024, ikiwa imesalia siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo utakaowachagua viongozi wakuu wa kitaifa.
Kabla ya hatua hiyo, umekuwepo mchuano mkali baina ya wawili hao, huku Babu Duni akilalamikia hujuma za watu waliokuwa wanamshinikiza ajiondoea kwa kuwa ni mzee na kitendo cha wenyeviti wa mikoa kumchukulia fomu mshindani wake.