Mbunge Emmanuel Cherehani achangia ujenzi wa zahanati Busulwanguku

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ametoa kiasi cha Shilingi Milioni 5 kuchangia ukamilishaji wa jengo la Zahanati katika kijiji cha Busulwanguku kata ya Idahina Halmashauri ya Ushetu, Mkoani Shinyanga.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho Cherehani amesema, Kutokana na jitihada zilizofanywa na Wananchi kwa kujenga boma anaanza kwa kitoa fedha hizo na baadaye serikali itaongeza milioni 50 ili kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo ambapo sambamba na hayo pia ametoa madawati 40 kwaajili ya Shule ya msingi Busulwanguku.

Awali akisoma taarifa ya Kamati ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo, Mtendajiji wa kijiji hicho amesema kwa muda mrefu sasa Wananchi wa Kijiji hicho wanasafiri umbali mrefu kwenda katika kata na vijiji jirani kutafuta huduma za afya hali inayo hatarisha Maisha ya Wananchi hao.

Sambamba na hayo amesema kijiji hicho kinaupungufu wa madawati na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Busulwanguku.

WhatsApp Image 2024-02-19 at 15.43.36.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-19 at 15.43.37.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-19 at 15.43.38.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-19 at 15.43.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-02-19 at 15.43.39.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-19 at 15.43.40.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-19 at 15.43.40(1).jpeg
 
Back
Top Bottom