Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 941
KIJIJI CHA KWIKEREGE CHAAMUA KUJENGA ZAHANATI YAKE
Kijiji cha Kwikerege ni moja ya vijiji vitatu (3) vya Kata ya Musanja.
Kijiji hiki hakina zahanati, kwa hiyo wakazi wake wanapohitaji Huduma za Afya wanalazimika kutembea umbali usiopungua kilomita tano (5) kwenda kwenye Zahanati ya Kijiji jirani cha Rusoli.
Wananchi wameamua kujenga Zahanati ya kijiji chao.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliongozana na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma Vijijini (chini ya Mwenyekiti, Ndugu Denis Ekwabi) kwenda kupiga HARAMBEE ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kwikerege.
Hali ya utoaji wa Huduma za Afya Jimboni mwetu iko hivi, tuna:
Hospitali ya Halmashauri
*Ina hadhi ya Hospitali ya Wilaya
Vituo vya Afya sita (6)
*Baadhi, vipya, vinasubiri kupewa wafanyakazi na vifaa tiba
Zahanati 44
*24 za Serikali
*4 za Binafsi
*16 zinajengwa
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO kutoka Kijijini Kwikerege, Kata ya Rusoli - imeambatanishwa hapa
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumapili, 1.10.2023