Mwenye taarifa huko serikalini jamani mshahara wa mwezi nov kimya!

Mwenye taarifa huko serikalini jamani mshahara wa mwezi nov kimya!

ndo mana hata mkitangaza migomo mnashndwa kuitimiza mana hata pesa za kuwawezesha kuish mwez mmoja mbele hamna inatakiwa kutengeneza mazingira ya kuwa na pesa itakayokuwezesha kuishi miezi 6 mbele
 
Kwani mbona mda bado? Kwani mwisho wa mwezi si kesho?
Usipopata leo utapata kesho. No hurry in Tanzania. Kadri unavyochelewa ndo unazidi kukusaidia wewe. Ukija haraka utaisha haraka. Wacha uchelewe ili uchelewe kumalizika

kweli wewe ni hekima teketeke. jinga kwel
 
Ninachojua mshahara wanaohangaikia watu ni wa mwezi Novemba ambao kwa mapokea hulipwa mwishoni mwa mwezi, sasa watu hata mwezi haujaisha wanalalakia nini tatizo kama si mazoea ya kujenga taiba ya kulalamika kitu kbla ya muda kufika. hayo unayosema ya uingereza hawalipi mshahara kwa muda usiofanyuiwa kazi bado na ndicho wanachodai watanzania, nadhani hapa utanipata ninachojadili.
Mkuu naona wewe umefungwa na tarehe 30 na sio siku 30. Kwasababu mshahara wa mwezi October ulilipwa between tarehe 24 hadi 27, kwa tarehe ya leo (29/11/13) siku 30 zishapita (ambazo ndo mwezi). Hapa bado unaona mwezi hujafika? bado unaona huyu mfanyakazi sio haki yake kujua kulikoni? By the way, sioni mantiki ya wewe kusema mtu akiulizia haki yake analalamika!
 
Watanzania tumezoea kulalamika sana, nilikuwa na mazoea hayo ya kuonja kama unavyoonja wewe, lakini nilipofika huko kunako nchi za walioendelea mshahara utapata wiki moja baada ya tadhimini ya muda unaomaliza unaotakiwa kupiwa mshahara. Sasa watu wanadai mshahara wa mwezi November wakati mwei haujaisha hapa haiingii akilini mwangu. Ingekuwa Desember ningeelewa. Tupange vizuri bajeti zetu, kisha tupunguze matumizi yasiyo lazima kama moja moto moja baridi, kupita kule kula kiti moto nk.
Mbona hutumii akili!Kama alilipwa October 23 ikifika November 23 anatakiwa apate mshahara wake.
 
Kumbe mishahara haitakiwi kuitumia vibaya kwani nimeona watu wengi wamekauka.
nashukuru mshahar uliopita niliacha akiba
 
Mbona hutumii akili!Kama alilipwa October 23 ikifika November 23 anatakiwa apate mshahara wake.

Asiyetumia akili ni yule anayelalamikia kitu kabla ya muda wake. Kama mwezi November uingeisha ningekuunga mkono kwamba tumeshaingia Desemba, lakini mwezi haujaisha watu wanavimbisha mishipa ni dalili ya kutopanga vema bajeti yao na kwa maneno mengine ni kuishi kwa pei cheki kwa pai cheki, thats from hand to mouth. Jamani tufanye mahesabu kwenye bajeti yetu ya kuishia.

The majority duniani kote hakuna mwenye kuridhishwa na mshahara wake, wachache mno wanaoneemeka na wengi ni shauri ya mpango mzima wa kubana matumizi kwa kwenda mbele.

Mimi pengine huwa nashtukia nimefikisha katikati ya mwezi bila kujua kama zilishaingia kwenye account yangu, sababu sipendi kuumiza kichwa kwa kufuatilia kinachoingia kwenye hazina yangu mradi tu nachungulia pay stub inatosha.
 
Mlio muleba kagera tujuzeni nasikia huko kitu kimesoma toka jana vipi inaukweli hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Mlio muleba kagera tujuzeni nasikia huko kitu kimesoma toka jana vipi inaukweli hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Kumbe mishahara haitakiwi kuitumia vibaya kwani nimeona watu wengi wamekauka.
nashukuru mshahar uliopita niliacha akiba

Hili ndilo wengi wanalotoka mishipa hapa na povu jingi ni sababu ya kushindwa kufanyia mahesabu na bajeti kuanza kupiga chenga. Jamani tupunguze kule kunakosababisha bajeti kutupiga chenga kama ifuatavyo:
  • Nyumba ndogo
  • supu
  • chips mayai
  • Nyama choma na kiti moto pamoja na sinia la ugani au kipwagus (wali)
  • moja moto na moja baridi na moja kwa escort wako akikurembulia macho unachomoa kama huna akili vile maana kumchomoa mtu ni mbinu na mafunzo wamepitia
  • kupitia sehemu kuangalia luninga ligi kuu ya uingereza itanibidi nichomoe kitu kupata kinywaji
  • kutumia pesa kwa M-Pesa kwa vidosho, hasa wanafunzi wa sekondari na vyuo wachomoaji sana, wasikudanganye nakupenda sana wangu bila wewe napata homa, ni wewe tu wangu, kumbe ana wengi anaowaambia viyo hovyo wakati anakopanga ana mtumishi anayempikia, kufagia na kumfulia nguo ndio wanachuo wa siku hizi huku wewe familia yako wanaishia mbatata.
  • Punguza milo ya mchana, tumia akiba yako kwa michemsho ya kuchukua toka home na full dinner ukishafika home kwa familia yako
  • Si lazima mechi zote tuende kuangalia uwanjani, luninga inasaidia kubana matumizi
  • Pool table inachomo mifuko hutakubali kushika mche bila mshiko wa kulainisha koo
  • Na mengineyo......
 
Tanga pia kitu hakijasoma. Ama kweli tunapaswa kuweka hakiba. Nimejifunza
 
Duuu kumbe ndo maana mtaani kuna heshima, Atm unaingia pekeyako....... 10 dyz more plz serikali..
 
piga keleleeeeeee... oyooooooo!!!! hatimaye boom tayari mazeee limeingizwa jioni hii....
 
I hate this kind of lifestyle!! Yani kusubiria mshaara tu!! I'm self made lakionea!!

Tunapaswa kuukataa utumwa huu. Hii ni hatari sana.
Mbaya zaidi, hata wale wanaiibia serikali muda, kwa kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato muda wa serikali, wamo kwenye mkondo mkuu kama vinara wakidai mishahara.
 
Back
Top Bottom