Dada wa kazi aongezewa mshahara kibabe

Dada wa kazi aongezewa mshahara kibabe

UWIMBABAZI

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
121
Reaction score
2
Dada wa kazi aliomba aengezewe mshahara lakini mama mwenye nyumba akakataa na akaomba apewe sababu 3 zakutaka kuongezewa mshahara

Dada: Ninaweza kupika zaidi yako
Mama: Nani kakwambia?
Dada: Kaniambia mume wako.
Mama: Sababu ya pili?
Dada: Ninaweza kupiga pasi na kunyoosha nguo zaidi yako.
Mama: Nani kakuambia?
Dada: Mume wako.

Mama: Eeh kumbe huyu ndo anakupa kichwa chakuwa na jeuri hizo ngoja arudi apa anione na nataka kukuambia kuwa mimi ndo mmiliki wa hii nyumba kama sijaamua mimi jambo la humu ndani yeye sio lolote hata uwe unaibeba hii nyumba na sisi tumo ndani tumelala huwezi kuongezewa mshahara hapa nitokee hapa na uso wake na kama unaanza tabia zako kesho nakukatia tiketi urudi kwenu kijijini maana unataka kuota mbawa, na kipi kingine ulichonizidi hebu niambie?

Dada: Nakuzidi kwa utundu kitandani
Mama: Pumbaaaavu na hivyo mkifanya huo upuuzi wenu na mpaka kaamua kukusifia si ndio?
Dada: Hapana sio yeye aliyenisifia hivyo.
Mama: Ni nani aliyekusifia huo upuuzi wako?

Dada: Ni dereva wako ndio aliniambia nimekuzidi kwa utundu kitandani.
Mama: Oooooh punguza sauti mwanangu nakuongezea mshahara tena mara mbili nlikuwa nakujaribu tu sawa mama?
 
Back
Top Bottom