Jamani tumezidi mno, sijasikia hata siku moja serikali imesitisha mishahara ya watumishi kwa mwezi mzima, ninachojua tarehe za malipo sio stable inategemea na ratiba ya mhazina, hivyo hata kama utakuja kupata December mwanzoni hakijaharibika kitu maana pesa ni ile ile utakayopata leo au kesho. Tujaribu kujenga tabia ya uvumilivu.
Nakumbuka awamu ya kwanza kulikuwa na matatizo ya usafiri ilibidi wasubiri hadi wiki mbili gari la ofisa elimu lifike kuwaletea mishahara walimu shuleni. Kuna kipindi ilibidi walimu watume mmoja wao aende kuwachukulia mishahara kwa vile shule nyingi ni mbali na mjini.
Malalamiko mengine hayana msingi.