Mwenye CV ya Mwl. Christopher Mwakasege aiweke hapa

Mwenye CV ya Mwl. Christopher Mwakasege aiweke hapa

Mwakasege ni kundi moja tu na hao kina Mwamposa and the like japo hajionyeshi waziwazi siyo baridi wala moto ni vuguvugu ndiyo maana anapata watetezi wengi akisemwa
 
Nadhani anaongelea fundisho la Mwl Mwakasege kwamba mzaliwa wa kwanza ndiye lango la baraka kwenye familia, hivyo ili mbarikiwe ni muhimu kumwombea huyo amjue Mungu. Kama mzaliwa wa kwanza atakuwa na mwelekeo mbovu basi atafunga baraka za watoto wengine wote.

Tunaweza kujadili hilo kwa mujibu wa maandiko wakuu

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Hili siyo kweli mkuu baraka hazitegemei mzaliwa wa kwanza bali uhusiano wa mtu binafsi na Mungu wake. Wap wazaliwa wengi waliokuwa waovu na bado wale waliobaki walioendenda sawa na Mungu walibarikiwa
 
Hili siyo kweli mkuu baraka hazitegemei mzaliwa wa kwanza bali uhusiano wa mtu binafsi na Mungu wake. Wap wazaliwa wengi waliokuwa waovu na bado wale waliobaki walioendenda sawa na Mungu walibarikiwa
Ni mweli mkuu, hata mimi naamini hivyo pia. Mwana hatouchukua uovu wa baba hivyo baraka ni mtu bunafsi mahusiano yake na Mungu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Nina historia kubwa na hawa watu wanaosema roho mtakatifu ddjkasema!Roho mtakatifu kasema agano hili la kichawi linavunjwa kwa sh.200000/=,kumkomboa mtoto kutoka kwenye mizimu sadaka ya 20,000/= roho kasema!!!NINA HISTORIA NA HAWA WATU NA MAHUBIRI YA SADAKA ZAO ZA UKOMBOZI NA UTAJIRI WA KUBARIKIWA SIJAKURUPUKA MIMI SIO MJINGA WA IMANI HIZI!!Niliwahi shiriki semina zake!!!!Acheni ujinga wa kuamini kila kitu!!
Mkuu funguka zaidi
 
Walokole bwana ukishawaambia Roho Mtakatifu ameongea na mimi, maswali yanaisha, akili zao zote zinapotea, unawaburuza tu.
 
Mi nimesema nilivosikia kosa langu ni lipi??Mi nawauliza swali JUZI JUZI kuna kijana wake amefariki kwa msongo wa mawazo ya kuachwa na mpenzi wake aliekuwa tayari na mtoto mmoja!!Sasa yeye kama mzazi na mtumishi hakuonyeshwa na roho wake kuwa uchumba wa mwanae hautodumu?hadi mtoto akafa kwa msongo wa mawazo??NAOMBENI MAWAZO YENU HAPA!!!

Mxiuuuuu
 
Si mchungaji ni Mwalimu
Hakuna Huduma ya Ualimu Mkuu; NI changamoto ya Kiswahili Chetu; Watu wengi wanapotea sana; Huduma ziko nne tu Uchungaji, Utume, Unabii na Uinjilisti.

Iko Ivi; Lugha Yetu ya Kiswahili na pia Kiingereza Kinachangamoto ya maneno sana.

Huo Mstari uko ivi 'Naye alitoa wengine kuwa mitume,na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti, na wengine Kuwa wachungaji (na) waalimu; Englishi iko ivi
And he gave some Apostles, and Some Prophets, and some evangelist and some pastors (and) Teachers

sasa Hiyo (and), (na) Sio Conjuction in Greek, greek ilitumia neno kai ambalo halina maelezo ya nayofuata sasa kai sio kiunganishi ni kama Connection ikiwa na maana ya (ambao, yaani na in englishi which is/are, therefore)

Hivyo from Original Language inabidi isome ivi:-
Naye alitoa wengine kuwa mitume,na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti, na wengine Kuwa wachungaji ambao/yaani waalimu.

Kuna changamoto sana, huwa naona wahubiri wengi especially Africa, wanamuachia Roho mtakatifu, pasipo kufahamu kwamba bible ni maandishi, bila kufuata Misingi ya uandishi lazima utafundisha vitu nje na ilivyo maanishwa tangu awali. Kumbuka biblia haiwezi kumaanisha Leo, kitu ambacho muandishi wa kwanza alimaanisha.
 
Walokole bwana ukishawaambia Roho Mtakatifu ameongea na mimi, maswali yanaisha, akili zao zote zinapotea, unawaburuza tu.
Kweli kabisa Mkuu, Kuna changamoto hapo kwenye hiyo kitu, Japo Roho mtakatifu is Real, but watumishi wanapotoa hiyo kitu.
 
Nina historia kubwa na hawa watu wanaosema roho mtakatifu ddjkasema!Roho mtakatifu kasema agano hili la kichawi linavunjwa kwa sh.200000/=,kumkomboa mtoto kutoka kwenye mizimu sadaka ya 20,000/= roho kasema!!!NINA HISTORIA NA HAWA WATU NA MAHUBIRI YA SADAKA ZAO ZA UKOMBOZI NA UTAJIRI WA KUBARIKIWA SIJAKURUPUKA MIMI SIO MJINGA WA IMANI HIZI!!Niliwahi shiriki semina zake!!!!Acheni ujinga wa kuamini kila kitu!!

Msimtaabishe THE BREED.
Yote aliyosema ni sahihi
Huyo nabii ni nabii wa uongo. Msidanganywe na zile mbwembwe na sauti zake. Ni mchumia tumbo lake na mwovu aliyemtuma.
 
Huyo Mwakasege mafundisho yake ni utata mtupu. Anatumia muda mwingi kufundisha sijui mzaliwa wa kwanza sijui vitu gani badala ya kuhubiri habari za Yesu Kristo. Ni mpigaji tu na anatumia udhaifu wa watu kuhusu mafundisho ya Mungu
 
Nipo Arusha kwenye semina ya mwakasege aisee huyu mzee ni mchungaji hasa anakipaji Cha kujenga hoja na kushawishi pia ni orator mzuri mno hachoshi kumsikiliza hakika amenibariki Sana. Jina la bwana lihimidiwe kupitia huyu mtumishi wa Mungu.

Naomba mwenye CV yake AIWEKE hapa na niliwahi kusikia ni mchumi mzuri na mkapa alimtumia naomba authentication ya haya.

Mungu mbariki mwakasege.
Mkuu kwa kuwa upo kwenye huo mkutano muombe Mungu atakuonesha hicho unachotaka kufahamu kwa huyo mtumishi lakin hapa kwenye hili jukwaa nafikiri sio mahali sahihi sana kwani wanajukwaa wengi wanacoment kwa hisia zao tu wakati mwingine wanaweza kumkosea Mungu kwa kuzungumza bila ushahidi, mim ni mkristo naamini kwamba ukimuomba Mungu katika roho na kweli atakuonesha kila kitu ikiwa ni pamoja na upako wa mtumishi yoyote anaefundisha neno lake.( kuomba kwa roho na kweli).
 
Nasikia alimtanguliza sedekia kuzimu hadi leo yupo kule anatumika kuimba!!!WANAOJUA WATUHAKIKISHIE!MI NILISHA POTEZA IMANI NA HAWA WATU!!!
Hahaha eti mtu mwenye uwakika atuhakikishie😂😂.
Kuna mtu alishaenda huko kuzimu huko na kumuona akiimba mpaka atuhakikishie? 🤔
 
Huyo Mwakasege mafundisho yake ni utata mtupu. Anatumia muda mwingi kufundisha sijui mzaliwa wa kwanza sijui vitu gani badala ya kuhubiri habari za Yesu Kristo. Ni mpigaji tu na anatumia udhaifu wa watu kuhusu mafundisho ya Mungu
Tofautisha kati ya mchungaji, mwalimu, muinjilisti, nabii na mtume.
Waefeso 4:11-13
"Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa.
 
NENO Linasema ijaribu kila roho ya kwamba imetokana na mungu!!!sasa wewe unaeamini kila mhubiri umekuwa punguani????hata yesu aliambiwa ana pepo sasa wachungaji wa sasa wasikosolewe???wao kina nani?mi nilisikia hayo REDIONI KUWA KUNA MTUMISHI ALIMTOA SADAKA MWIMBAJI WAKE KWA FREEMASON!TENA ALIMTOA KAFARA UGENINI TENA NCHI YA MBALI!!!SASA NIAMBIE SEDEKIA HAKUFIA ISRAEL?NITAJIE NANI MTUMISHI MAARUFU ALIEFIWA NA MWIMBAJI UGENINI TENA NCHI YA MBALI ?ZAIDI YA YEYE HAPA TZ???RFA KIPINDI SITOSAHAU!!!
Kwahiyo mkuu kila chakisikia redioni kipo sahihi? Kwanini wanasema kuna vyombo vya habari vinatoa habari kipropaganda, je propaganda ni ukweli? Jibu hapana so whatever you hear from media might be true or not
Kama una ishahidi usio na shaka tufanye na sisi wengine tuamini.
 
Ninachofahamu kuhusu CV yake;
1.Ni mzaliwa wa Tukuyu-Mbeya
2.Ni msomi na mhitimu wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam branch ya Morogoro(Kwa sasa ni SUA)
Ktk masuala ya uchumi kama
sikosei.
3.Aliajiriwa serikalini kama Afisa
Mipango na Udhibiti,huko Arusha.
4.Alipokea wito wa kumtumikia
Mungu,kisha akaacha kazi
serikalini ili ahubiri injili vilivyo.
5.Ni Mwalimu wa neno la Mungu.
6.Ni Mtumishi wa Mungu.
 
Hakuna Huduma ya Ualimu Mkuu; NI changamoto ya Kiswahili Chetu; Watu wengi wanapotea sana; Huduma ziko nne tu Uchungaji, Utume, Unabii na Uinjilisti.

Iko Ivi; Lugha Yetu ya Kiswahili na pia Kiingereza Kinachangamoto ya maneno sana.

Huo Mstari uko ivi 'Naye alitoa wengine kuwa mitume,na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti, na wengine Kuwa wachungaji (na) waalimu; Englishi iko ivi
And he gave some Apostles, and Some Prophets, and some evangelist and some pastors (and) Teachers

sasa Hiyo (and), (na) Sio Conjuction in Greek, greek ilitumia neno kai ambalo halina maelezo ya nayofuata sasa kai sio kiunganishi ni kama Connection ikiwa na maana ya (ambao, yaani na in englishi which is/are, therefore)

Hivyo from Original Language inabidi isome ivi:-
Naye alitoa wengine kuwa mitume,na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti, na wengine Kuwa wachungaji ambao/yaani waalimu.

Kuna changamoto sana, huwa naona wahubiri wengi especially Africa, wanamuachia Roho mtakatifu, pasipo kufahamu kwamba bible ni maandishi, bila kufuata Misingi ya uandishi lazima utafundisha vitu nje na ilivyo maanishwa tangu awali. Kumbuka biblia haiwezi kumaanisha Leo, kitu ambacho muandishi wa kwanza alimaanisha.
Asante mkuu.. Ingawa itakuwa nje ya Topic..
Basi tuseme Biblia iandikwe upya..kwa maana translation ifanyike from original scriptures... Ukiangalia hoja nyingi za kikatoliki zina kuwa defended na chagamoto ya Lugha..

Na unataka kusema Mwl. Mwakasege hajalijua hilo.?
 
Mkuu inatosha kusema kwamba inawezekana kati ya haya mawili:-
1. Inawezekana Anajua (ila alijua kwa kuchelewa wakati amesha-takeoff na sasa anahisi Guilty namna ya kuignore)
2. Inawezekana hajui kabisa ( Hapa wahubiri wengi ndio wanaangukia hapa, ignorant tu, ambayo kama effort ipo inatoka)

Ishu inayowakumba watumishi wengi ni Uvivu,Huwezi kuwakamilisha Watakatifu kama Efeso inavosema ukiwa Mvivu, Lakini pia Ishu inayowakumba Waamini wengi ni Uvivu pia, Kuna watu walikuwa wanaitwa Waberoya, wao Paulo alipokuja kuwahubiri, kabla ya Kuamini walidhibitisha kwanza kama Paulo anachohubiri ndivyo ilivyo, Lakini kuna wathesalonike wao walipokea Moja kwa moja; Lakini Changamoto Kubwa ya Christianity iliyopelekea kuwa na Doctrine Nyingi Kwanza kabisa ni Lugha; Ndio maana kwenye Muslim unakuta Migawanyiko ya Doctrine sio mingi maana wao Dunia Nzima wanajifunza Imani yao kutoka soma kutoka kwenye Lugha ya Asili. Lakini Pili ni Kwamba Pamoja na Hiyo Lugha, Bado wanashindwa Kutoa maana kwenye Bible verse wanatoa maana zao;
Lakini bado sisi Tunayonafasi, ijapo ilikuwa Hivyo Bado kama watakuwepo Wahudumu wazuri wa kuwakamilisha watakatifu , ambao wana Juhudi na Nia kabisa ya kutaka kujifunza na Kuelewa na kisha kuwaelewesha wengine Inawezekana.

Believe me ukisoma Kutoka kwenye Hebrew na Greek ( Hawatofautiani kabisa) Tofauti inaanza kuja kwenye English, na Kiswahili chetu;

Sio Nje ya Topic Mkuu; Ndio maana nikasema Kuna changamoto Kubwa Mno kwa Watumishi wa Mungu ikiwemo Yeye Pia; ROHO Mtakatifu sio Substitute ya Kanuni za Usomaji; Ili uelewe Biblia ambayo ni maandishi lazima Kuzingatia Kanuni za Uandishi na Usomaji; Biblia inahitaji Kusoma Pre text (Maandishi Kabla), Context (Mazingira kiini), Post Text (maandish Baada), Kuchukua Mstari mmoja kumegharimu mno Wahudumu wa Neno; Lakini pia Watumishi wengi ni wavivu, wanajificha kwenye kivuli cha Roho Mtakatifu hapo ndipo changamoto inaanza; Ukishakuwa na Huduma kati ya zile nne, Hakuna Option mzee; Ni muhimu ujifunze, vitu in deep kabisa;
 
Back
Top Bottom