queeny
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 584
- 421
Wakuu hii hoja haiwezi kupita bila ya kutendewa haki.
Kabla sijaanza naomba kama Mamlaka husika hasa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dk.Pombe Magufuli watapitia huku jukwaani tunaomba wafahamu barabara hii ni zaidi ya kero, tunaomba ifumuliwe upya na ijengwe kulingana na misingi ambayo inaeleweka n ahata Waziri wetu huyu anaifahamu.
Ni aibu kwa barabara kubwa kama hiii inayotumika na takribani vigogo wengi wa Nchi hii akiwemo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina kasoro ambazo hata mimi ambaye sikusomea uhandisi wa barabara ninaziona wazi:
1. Inatakiwa gari inayopinda kuelekea kulia ama kushoto iwekewe diversion angle ambayo itawezesha gari hilo kupinda kona na kuliruhusu gari la nyuma yake kuendelea na safari kama ilivyo kwa barabara za Nyerere na nyinginezo.
Kama alivyosema mtoa hoja, kwa watu wanaongia barabara za pembezoni tukianzia eneo la Kwakomba, kuna barabara ya Zawadi inayoingia Mbezi juu kwa Mheshimiwa Mbunge Shekifu. Mtu anayetoka Mbezi juu kuelekea Mwenge amenyimwa juction inayomwezesha yeye kukata kulia kwake na kuingia barabara ya kuelekea mwenge mpaka kwanza akate kushoto nakuelekea Tegeta mpaka eneo la Tanki bovu ndipo apinde tena kulia na kurudi tena mpaka KwaKomba ndipo aendelee na safari yake ya Mwenge. Kwanini wasiweke sehemu ya kuingilia hapo hapo Zawadi Road? Kwanini wasifanye kama walivyofanya pale Makonde?
2. Kitu kingine cha hatari ni hizi sehemu za kugeuzia magarikutoka barabara moja kuingia nyingine ni finyu sana kiasi kwamba magari mawili yakikutana pale kuna uwezekano mkubwa wa kugongana hasa kwa kuwa kwanza hakuna ile diversion angle ambayo inamuelekeza mtumiaji kwamba sasa unaingia zone ya kupinda kulia au kushoto. Na ikitokea gari zimepigana pini tayari nyuma inakuwa foleni ndefu tayari imezaliwa.
3. Barabara ni finyu sana bila shaka watakuwa wametumia vipimo vya bajaji maana ukiangalia gari mbili kubwa zinapoeleka sehemu moja utaona uwazi unaoachwa katikati ni mdogo sana.
4. Barabara hata kukamilika haijakamilika tayari kutokea tanki bovu mpaka Tegeta tayari imetengeneza matuta utafikiri mkulima ameandaa shamba kwa ajili ya kupanda viazi.
Barabara hii ni majanga, mheshimiwa Magufuli tunaomba utumie na huku rungu lilelile ulilotumia barabara ya Kilwa kuponda wote waliozembea.
Na kwa kuongezea hapo mtu anayetoka tegeta kwenda interchick inamlazimu aende mpaka makonde then arudi nyuma tena via samaki samaki ndipo afike interchick. hii barabara ni ya ajabu sana