Simulizi; Julai Saba...

kapingili

Senior Member
Jul 4, 2012
155
192
IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE

*********************************************************************************

Simulizi : Julai Saba
Sehemu Ya Kwanza (1)
Dunia inakumbwa na wimbi la ugaidi, matukio ya kutisha yanayopoteza maisha ya walio wengi katika pande mbalimbali za dunia ikiwemo Afrika hususan Tanzania. Nchi zinazoendelea zinajumuishwa kuwa na mahusiano na mataifa beberu ya Maghalibi. hivyo zinashambuliwa na makundi hayo.

Idara za usalama za Tanzania zinafanikiwa kumtia mkononi Jegan Grashan akihusishishwa na mlipuko wa ubalozi wa USA, Dar es salaam mwaka 1998. Swahiba zake wanaishinikiza serikali imuache huru kwa kutekeleza milipuko kadhaa, wanaipa siku saba iwe imekamilisha hilo. Je litawezekana?

Tiririka na mkasa huu mwingine unaomhusisha Kamanda Amata. Mkasa wa kusisimua. Mkasa wa Kigaidi.


CHAPISHO LA 01
1
MVUA KUBWA ilikuwa ikinyesha katika jiji la Dar es salaam, jiji linalosifika kwa joto kali linalowafanya watu wake kujutia kila siku kwa nini wanaishi hapo, lakini bado kuhama hawataki. Radi za hapa na pale ziliendelea kumulikan ardhi yote ya eneo la Tazara katika makutano ya barabara zenye majina ya viongozi wakubwa Africa, barabara ya Nyerere na ile ya Mandela, umeme ulikuwa umekatika na giza lilitawala kila mahali jioni hiyo, haikuwa usiku sana kwani ndiyo kwanza kipindi cha majira kutoka RTD kilikuwa kikianza, hakuna aliyeweza kuvuka katika makutano hayo, magari yalijaa kila upande mpaka kule kwenye service road, kelele za honi zilitawala na matusi ya hapa na pale, wengine wakijifanya ndiyo askari kuongoza magari lakini bado hali ilikuwa tete, si wakwenda Buguruni, wala Ukonga wote walitua pale, mvua iliendelea kunyesha kwa fujo na ngurumo zikitawala.

Katikati ya makutano yale kulikuwa na gari aina ya Peugeot imesimama hali inaunguruma, dereva wake alishuka na kupiga kelele za hapa na pale akiwaomba wengine wampishe lakini hakuwapo wa kumpisha, kwa hasira yule bwana aliubamiza mlango wa gari na kujichanganya na vijana waliojaa eneo lile, haikupita dakika mbili mlipuko mkubwa ulitokea katika gari ile, anga lote lilifunikwa na rangi nyekundu iliyochanganyika na moshi mweusi, watu walitawanyika huku na kule wengine wakitokea katika madirisha ya daladala, ilimradi tu kujiokoa. Vilio vilisikika huku na kule watu waliumia sana na wengine kupoteza maisha, gari zaidi ya ishirini zilidaka moto eneo lile.

Gari za zimamoto kutoka kampuni binafsi na lile la jiji yalifika huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwa tayari kusaidia majeruhi kuwakimbiza hospitali ya Dar Group, Temeke na wengine Muhimbili moja kwa moja, kazi ilikuwa ngumu kwa kila mtu aliyekuwa pale, wananchi wote walisogezwa mbali na eneo la tukio ili kupisha shughuli za uokoaji. Baada ya takribani dakika arobaini na tano gari ya jeshi ilisimama karibu kabisa na jengo la S.S Bakhresa, wakashuka na vifaa vyao kuelekea pale palipotokea mlipuko walilizungushia gari lile utepe maalum na kukusanya kila kilichoonekana na uhusiano na mlipuko ule kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Hali iliendelea kuwa tete eneo lile kila mtu alilia kivyake.

“Ingia kaka, umemaliza kazi” bwana mmoja alisema huku akiufungua mlango wa Toyota prado na kumruhusu huyo aliyemwita kaka kuingia kwenye gari hiyo, kasha ikageuza na kuchukua barabara ya Mandela kuelekea Buguruni.
“Bado, kazi ndiyo kwa nza inaanza” yule bwana aliwaeleza wenzake huku gari ile ikitokomea kwa kasi maeneo ya Sukita kuielekea Ubungo.

“Hii ni vita ya tatu ya dunia, na tunaiendelezea hapa Tanzania, kwa kuwa ulinzi wan chi hii hauko makini” aliongea bwana mmoja aliyeonekana kama ndiyo kiongozi wao.

Mlio mkali wa simu ulimshtua madam S usingizini, alisonya na kuiinua simu ile huku akiwa bado kitandani mapema namna hiyo.

“Hey, nani?” aliuliza kwa hasira.
“Madam S, washa runinga yako TBC kasha nitakupia baadaye kidogo” sauti ya upande wa pili ilitoa ombi, madam S bila kuchelewa aliichukua rimoti na kuiamuru runinga ile kufanya kazi. Alipigwa na butwaa na moyo ukaanza kumuenda mbio, ukizingatia na umri nao ulikuwa umekwenda, aliifutailia habari ile, na kwa mbali macho yake yalianza kujaa machozi. ‘Oh my God’ alijisemea moyoni, ‘Nini tena hii?’ alijiuliza mwenyewe wakati akimfuatilia Grace Kingalame akitoa maelezo ya moja kwa moja kutoka eneo la tukio. Madam S alinyanyuka kitandani na kuutafuta mlango wa bafu, baada ya kujiweka sawa alivalia suruali yake nadhifu na fulana yake nyeupe iliyoandikwa Naipenda Tanzania, na juu yake alijitupi kijikoti cheusi, bastola yake aliipachika sawia katika mkanda wa suruali aliyovaa na kutoka moja kwa moja aliiendea gari yake aina ya Toyota Spacio na kuondoka akiiacha nyumba yake ikibaki na mlinzi tu. Njia nzima madam S alikuwa akilaani kilichotokea hapo Tazara, kama kawaida yake alitamani huyo mtu amkamate mara moja ili amuoneshe shughuli nene kwa kufanya jambo kama hilo. Alifika eneo la tukio na kukuta shughuli zikiendelea hasa zile za uchunguzi, pale alikutana na wakuu wa polisi na vyombo vingine vya usalama kila mmoja akiwa hana la kusema juu ya tukio hilo, laana za kumlaani aliyetenda hilo na vizazi vyake vyote ndizo zilikuwa midomoni mwao.

“Atakamatika tu” Madam S alimwambia IGP walipokuwa katika mazungumzo huku wakiangalia shughuli ile ikikaribia kufika ukingoni.

Madam S aliinua simu yake na kuitazama, ilikuwa yapata saa tano usiku, aliwaaga wenzake na kuondoka eneo lile mara moja huku akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake.

Siku iliyofuata
“Miranda!” sauti nzito iliita kutoka mlango wa pili, ilikuwa ni sauti ya waziri wa ulinzi ambaye ndiyo kwanza alikuwa akiingia ofisini kwake asubuhi hiyo. Miranda alitii wito huo mara moja alikiacha kiti chake na kuufuata mkango mkubwa wa kioo uliokuwa kushoto kwake na kuufungua.

“Nimefika mzee!” aliitikia. Bwana Sixtus Maige, waziri mwenye dhamana ya ulinzi katika serikali ya Tanzania aliinua sura yake iliyoonekana usawajika kwa mawazo na kujawa mikunjo ya hasira na uchungu.

“Naomba uniitie Madam S, kitengo maalum usalama wa Taifa tafadhali, fanya hilo sasa hivi” aliamuru na Miranda mara moja alitii agizo alilopewa. Ndani ya ofisi yake aliandika fax ya haraka na kuituma kunakohusika, kisha akatulia akiendelea na majukumu yake mengine.

Dakika kumi na tano zilikuwa nyingi, mlango wa katibu muhtasi wa waziri wa ulinzi miss Miranda ulifunguliwa na mwanamama wa makamo aliingia ndani na kumtazama binti yule aliyekuwa anajitazama kwenye kioo huku akipaka rangi ya mdomo. Miranda alistuka aliposikia mlango ukifunguliwa na kugeuka haraka.

“Nimepata ujumbe msichana, mzee yupo?” madam S aliuliza na Miranda bila kujibu alimuonesha ishara ya kuingia katika ofisi ya mheshimiwa.

“Karibu sana madam S, nilikuwa nakusubiri kwa hamu kubwa, kwa kukuona tu nahisi kazi imekwisha” waziri wa ulinzi mheshimiwa Maige alimkaribisha mgeni wake na kumuonesha kiti cha kukaa naye bila kusita akafanya hivyo, kasha mheshimiwa akaendelea, “Madam S najua wazi kuwa unafahamu lile nililokuitia, sina haja ya kulieleza maana jana sote tulikuwa kule Tazara kwenye lile tukio. Wito wangu hapa ni kutaka kuona pamoja nawe jinsi ya kulimaliza hili swala na kuwakamata wahusika, mheshimiwa Rais amesema lifanyike mara moja, na mi nikaona kuwa wewe ndiye unaejua jinsi ya kuifanya kazi hii kwa utaalam”

“Ooh mheshimiwa, nimekusikia, nimetafakari sana juu ya hili swala tangu jana, lakini akili yangu haisomi”
“Kwa nini?”

“Sasa hivi sina watu, TSA 1 tumetuma huko China kwa ajili ya ile issue ya madawa ya kulevya, TSA 2 naye yupo kule Malawi kwa ajili ya kuweka mazingira tayari kwa ile kazi yetu, tufanyeje mheshimiwa, serikalai itakalosema sisi tutatii” madam S aliongea kwa msisitizo mkubwa.

“Ok! Nimekuelewa vizuri, sasa naomba TSA 1, kamanda Amata arudi mara moja kwa ajili ya kazi hii” waziri maige alitoa oda.

“Sawa mheshimiwa, litatekelezwa mara moja” madam S alijibu kwa heshima.
“Akifika nchini naomba moja kwamoja uje nae hapa” mheshimiwa aliongeza. Madam S aliinua mkono wake na kuitazama saa yake kasha akabonyeza kitufe Fulani na kuendelea kubonyeza vijitufe vingine juu ya saa hiyo aina ya casio, kasha akatulia na uendelea na mazungumzo na waziri Maige wakijadili hali halisi ya tukio zima lililotukia usiku wa jana.

Hong Kong – Cheung Sha beach, Lantau

Kamanda Amata alikuwa juu ya kitanda safi kilichotengenezwa kwa plastick huku akiwa amejilaza kifua chake alikiruhusu kipigwe na upepo wa pwani, akiitazama bahari tulivu iliyokuwa na mawimbi kiasi, pembeni yake mwanadada mrembo alikuwa amejilaza pamoja nae wakiongea mawili matatu.

Baada ya mazungumzo yao yaliyokuwa marefu kiasi na kujawa na vicheko vya mahaba, walinyanyuka kutoka kwenye vitanda hivyo na kuelekea hotelini alikofikia kamanda Amata kwa ajili ya kuendeleza mazungumzo yao kwa vitendo. Akiwa anakaribia katika ngazi za kuingilia mapokezi ya hotel hiyo alipishana na mtu mmoja aliyekuwa akimtazama sana, Amata hakumtilia maanani mtu huyo, mkono wake wa kuume ukiwa kiunoni mwa mwanadada akili yake isingeweza kuwa makini tena katika jambo lingine.

Walipanda ngazi kadhaa na kuufikia mlango wa chumba chake, Amata alikitazama kitasa cha mlango ule na kumrudisha kwa nyuma yule mwanadada kisha akatumbukiza ufunguo wake na kuufungua ule mlango, kwa hatua za hadhari aliingia ndani ya chumba ile, aliangaza huku na huku lakini hakuona dalili ya mtu ndani mle, lakini kila alipopiga hatua kwenda ndani alihisi damu ikikimbia na nywele kumsimama, alisogea kwa ndani ili kwenda kuichukua bastola yake aliyoificha chini yam to, hamad! Teke la nguvu lilitua tumboni mwake, kwa wepesi wa hali ya juu, Amata aliudaka ule mguu upande wa kanyagio na kuuzungusha kwa nguvu mpaka akauvunja, yowe la uchungu lilimtoka yule mtu, Amata alimsukuma na kumbamizia ukutani, akageuka nyuma haraka kumtazama yule mwanadada ndipo alipokutana na bastola iliyokwishatolewa usalama ikiwa mikononi mwa yule mwanadada ikimlenga yeye, Amata alijirusha kwa haraka na risasi iliyotoka ilichimba ukuta, kwa haraka aliuzungusha mguu wake na kumpiga ngawala safi yule mwanadada ambaye alipaa juu na kutua katika meza kubwa ya kioo huku bastola ikimtoka mkononi, iliokotwa na kamanda Amata na kushikwa barabara mikononi mwake. ‘Sina muda wa kupoteza,’ alijiwazia na kuifyatua ile bastola, risasi moja alifumua kichwa cha yule jamaa na nyingine ilizama moyoni mwa yule mwanadada, ‘Wanaharamu’, mara akasikia kamlio kadogo kama ka mashine ya typewriter kakilia kutoka katika kitu kama kitabu juu ya droo ya kitanda, alikawahi na kutoa kijikaratasi kirefu kilichokuwa na maandishi machache.

“Hali siyo nzuri, rudi haraka mgonjwa anahitaji msaada wako, Tena Sana Aisee” alikirudisha kile kikaratasi katika ile notebook bandia kumbe ilikuwa ni fax mashine akaifungua tena ile fax machine yake na kurudia kusoma kile kikaratasi, akabaki akishangaa ‘Nini kimetokea?’ alijiuliza kwa kuwa kazi aliyotumwa huko ilikuwa ndiyo kwanza imepamba moto, alinyanyauka na kufungua kabati la nguo kasha akapaki kila kitu begini, alipokamilisha akaitazama ile miili ya wale viumbe wawili waliotaka kuiondoa roho yake, akatoka taratibu katika chumba hicho na kujipanga kwenda uwanja wa ndege tayari kwa safari.

Dar es salaam
Kamanda Amata alikaribishwa na vichwa vya habari vya kutisha katika magazeti siku hiyo, ‘Mlipuko mkubwa waitikisa Dar es salaam’ na lingine likaandika, ‘Ugaidi waigubika Dar’, na mengine mengi yaliandika kila moja kwa jinsi zake.
Kamanda Amata aliinua uso wake na kumtazama waziri wa ulinzi kasha akamtazama madam S na kushusha pumzi ndefu.

“Yes, Kamanda, hiyo ndiyo hali halisi iliyoukumba mji wetu, taifa lipo kwenye maombolezo ya siku tatu, bendera nusu mlingoti. Serikali inaiomba ofisi yenu wewe pamoja na madam S kuikamilisha kazi hii kwa haraka na ufanisi mkubwa, tuko tayari kuto msaada wowote pale utakapoitajika, nawatakia mafanikio mema katika hili na Mungu awatangulie” waziri wa ulinzi mh Maige alimaliza rai yake

“Amin!” kamanda Amata alijibu na kumtazama madam S. akiwa ndani ya suti yake nyeusi Amata alinyanyuka kitini na kuongozana na madam S kutoka katika ofisi hiyo, walipita pale alipo Miranda na kugana nae, jicho la kamanda Amata lilimtazama kwa tuo mwanadaa huyo ambaye daima utamkuta akitengeneza kama siyo nywele basi rangi ya midomo kupitia kijikioo kidogo alichokihifadhi katika motto wa meza.

“Hata usipojiremba, we bado ni mrembo tu” Amata alianza uchokozi wa maneno kwa mwanadada Yule.
“Mmmmm kamanda, kuna warembo nitakuwa mimi?” alimjibu huku akiyarembua yale macho yake makubwa, “Nitoe lunch leo,” alitupa ombi huku akiendelea kujitazama kiooni.

“Usijali, mrembo kama wewe hakuna mwanaume atakayekunyima lunch, hata dinner kabisa” Amata alijibu huku akiwa ameushika mlango tayari kutoka.

Piipiiii, honi za gari ya madam S zilimshtua kamanda kwenye maongezi yale.
“Unaitwa na mama yako huko uende,” Miranda alimwambia Amata
“Ok Beibi, nitakucheki mida” alijibu na kutoka nje.
Aliingia garini na kuketi, kasha akajifunga mkanda wa usalama.
“Hivi hii tabia yako utaiacha lini? Wengine wake za watu hao!” madam S alimueleza Amata.
“Aaa bibi, hata mimi mtu jamani” alijibu kwa utani.
“Shauri yako hivi vingine vitakugharimu sana”
“Shaka ondoa”

“Hili bomu lilikuwa ni bomu la masaa, bomu ambalo hutegwa makusudi kwa malengo maalum, kwa hiyo siyo mlipuko wa kawaida ni wa kukusudiwa” kapteni Savana alikuwa akimpa ripoti ya kwanza ya uchunguzi kamanda Amata walipokutana pale makao makuu ya jeshi Upanga.
“Kwa hiyo unataka kuniambia mlipuaji alitega kwa malengo maalum?”
“Ndiyo”
Kamanda Amata alitazama lile faili lililo mbele yake na kuligeuzageuza. Baada ya mazungumzo ya kina waliagana na Amata akaenda mahali pengine kwa uchunguzi.

BREKI ilikuwa katika kituo cha polisi cha Tazara kuitazama gari ile iliyotumika kwa mlipuko ule. Mezani mbele yake alikutana na ASP Majegero.

“Kuna lolote mmepata kuhusu hii gari iliyobeba mlipuko?” lilikuwa ni swali la Amata kwa ASP majegero.
“Aaa hapana ila bado tunaendelea na uchunguzi ukizingatia gari yenyewe imeungua vibaya inakuwa ni ngumu kutekeleza hilo kwa wakati”

“Ok, hebu nilione.” Wote wawili walitoka na kuzunguka uani kuiona gari ile, Amata aliitazama jinsi ilivyochakaa, aliizunguka na mara akakutana na kile alichokuwa akikitafuta.

Plate namba ya gari hiyo iliyoungua vibaya kwa moto, Amata aliing’oa na kuitazama kisha bahati nzuri namba zake zilikuwa za kugongwa siyo zile za kupuliza, Amata alisoma namba zile kiurahisi na kuziandika kwenye kijitabu chake kidogo kasha akaagana na Yule askari polisi na kuondoka zake. Breki ya kwanza ilikuwa katika jingo la TRA pale Samora evenue, alishuka na kufika mapokezi ambapo aliomba kuonana na ya kuperuzi katika mtandao wao.

“Kadiri ya namba hii hiyo ni gari inayomilikiwa na mama mmoja anaitwa Miss Jesca Mdachi” Yule dada alimjibu Amata.
“Ok, maelezo yake mengine tafadhali” Kamanda Amata aliomba
Yule mwanadada aligeuka kwenye kompyuta na kuprint karatasi Fulani akarudi na kumpatia Amata.
“Kila kitu kimeandikwa hapa” alimwambia Amata
“Ok asante sana mrembo” Amata alishukuru.
“Kuna linguine tafadhali?” Yule dada alihoji kama kuna lingine anahitaji msaada nalo. Amata alimtazama Yule dada kwa uchu alivutiwa na kifua chake kilichobeba matiti yaliyojaa vizuri.

“Hapana kingine zaidi ya namba yako ya simu, kama upo radhi” Amata alitoa ombi lingine la binafsi, Yule mwanadada alimtabasamia Amata kisha akauvuta mkoba wake na kutoa business card na kumpatia, kisha Amata akaondoka zake.

“Hatutawaacha hai hata mara moja, kila tutakapoamua kulipua tutahakikisha tunaua watu zaidi ya hamsini. Kosa lenu mnalijua, kuingilia mambo yasiyowahusu, vita ya watu wa Maghalibi na sisi, ninyi haviwahusu, kwa nini mnaingilia. Sasa tunasema kwa sauti moja, tutawaua na tutawaua mpaka mtakapomuachia huru ndugu yetu Jegan Brashan mliyemfunga katika magereza yenu huko Tanzania. Tunawapa siku saba mumuwache huru zikipita bila kutekeleza mlipuko mwingine utatokea karibu kabisa na pua zenu…”

Waziri wa ulinzi bwana Maige aliizima cd ile iliyokuwa ikitoa ujumbe huo katika luninga kubwa iliyofungwa ofisini hapo, kisha aligeuka kuwatazama Amata na madam S pamoja na watu wachache waliokusanyika ofisini hapo baada ya wito wa dharula kutoka kwa waziri huyo.

“Hii cd imeletwa na Miranda ameikuta katika sanduku letu la posta asubuhi hii,” waziri Maige alilieleza lile jopo. Madam S alitoa kitambaa chake na kujifuta jasho ilhali hakuwa na jasho ilimradi tu akili yake ilikosa utulivu.

“Kazi tunayo, tena siyo ndogo” madam S alisema kwa utulivu.

“Sasa wewe mama ukisema hivyo sisi tutasemaje?” aliuliza mjumbe mwingine aliyekuwa katika kikao hicho. Wote wakabaki kimya kwa muda wakitafakari hili na lile.

“Lakini hawa ni nani? Al Qaeda, Al-Shabab, Boko Haram au ni nani?” alitupa swali mtu mwingine.
“Mimi na wewe hatujui, ndiyo maana niliwaita ili ninyi kama watu wa juu wa usalama wa nchi hii mlipatie ufumbuzi” waziri Maige alijibu.
“Ina maana baada ya siku saba tutegemee mlipuko mwingine sivyo?” aliuliza mjumbe mwingine.
“Ndiyo maana yake, hapa hatujui tunapigana na nani na wangapi na wako wapi, katika medani za ijeshi tunasema, adui mbaya ni yule aliye ndani yako. Sasa adui huyu tayari yuko nchini mwetu, tufanye juu chini kabla ya wiki tuwe tumefanikisha hilo” Madam S alizungumza kwa jazba.
“Wanataka tumuachie huru Jegan Brashan na wao wasitishe malipuzi yao, ninyi mnasemaje?” waziri aliuliza.
“Dunia itatushangaa sana kwa kufanya hilo, kumuachia Jegan! Hilo sijahafiki hata kidogo, tuone kwanza hii wiki moja tunafikia wapi,” madam S alijibu.
“Kamanda Amata mbona uko kimya sana? Huna la kuzungumza?” waziri alimuuliza Amata
“Jegan Brashan, hawezi kuwa huru hata iweje, hata iwe vita ya tatu ya dunia, mimi Amata TSA namba 1 sitalikubali, labda itoke maiti yake lakini si yeye kamili” alimaliza kwa kauli tata.
“Amata, unazungumza nini? Tunataka tupate muafaka wa hili,” waziri Maige alimkaripia kidogo Amata.
“Kwanza hiyo cd imenipa mwanga, nataka nianze na Jegan Brashan kisha hapo nitajua wapi pa kuendelea, naomba mnipe muda wa siku tano kisha tuone tena pamoja” Amata alimaliza kusema. Wote waliafikiana nae na kupeana kazi mbili tatu kisha wakatawanyika.

Gereza la Ukonga

“Jambo afande!” Amata alisalimu
“Jambo!” alijibu askari mmoja liyekuwa getini akiangalia usalama wa eneo hilo ambalo limehifadhi watu hatari kwa usalama wa taifa hili. Aliliendea gari la Amata na kuzungumza nae machache kisha akafunguliwa geti na kuingia, aliiacha ile njia inayoelekea chuo cha maafisa na kukunja kushoto kuufuata mlango amkubwa wa gereza hilo, baada ya mwendo wa kama mita mia mbili hivi aliegesha gari yake na kuteremka, alirekebisha tai yake na kujiweka koti lake vizuri kisha akauendea mlango ule na kutikisa kichuma Fulani, mara kajimlango kalikokuwa katikati ya ule mlango mkubwa kakafunguliwa naye akajitoma ndani.
“Naweza kuonana na bwana jela?” aliwauliza wale maafisa aliyowakuta pale.
“Bila shaka, nifuate…”
Kamanda Amata alimfuata yule askari na mara wakafika kwa bwana jela, yule askari akarudi na Amata akabaki pale.
“Naitwa Amata,” akajitambulisha na kutoa kitabulisho chake na kumkabidhi.
“Ndiyo bwana Amata, karibu sana chuo cha mafunzo, nikusaidie nini tafadhali?”
“Yah nahitaji kumuona mfungwa wa kigaidi bwana Jegan Grashan, nina mazungumzo nae”
“Bila shaka, je una kibali maalum? Maana huyu mfungwa hatakiwi kuonana na mtu yeyote wala kuona mtu yeyote”
“Nimetumwa na serikali, na kitambulisho changu ndiyo kibali” Amata alijibu kwa tindo huo.
“Ok, ngoja nikupe vijana wakupeleke, ila uwe makini sana tusije kupata lawama”
Baada ya dakika tatu hivi vijana wanne waliovalia sare nadhifu ya magereza, wenye maumbo ya kipiganaji hasa, mabegani mwao walikuwa na vile vibaka vya kijani, Amata mara moja alijua wale ni vijana wa kazi KMKGM.
Jegan Grashan, kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka thelathini hivi, alitokea kuwa gaidi tishio katika ukanda wa Africa Mashariki, akiwa anafanya kazi na kundi kubwa linaloendesha shughuli hizo sehemu mbalimbali za dunia. Alipitia mafunzo ya kijeshi huko Pakistan na kuwa mpiganaji hodari, lakini baada ya muda Fulani aliai jeshi na kujiunga na vikundi vinavyoendesha mapinduzi kwa njia za kigaidi ndani na nje ya Pakistani mapaka alipojikuta kwenye mtandao mkubwa na wa kimataifa na kutekeleza mauaji mengi sehemu mbalimbali, japokuwa dunia ilikuwa ikimsaka kwa udi na uvumba huko Mashariki ya kati, kumbe kijana huyu hatari alikuwa ameweka makazi yake Africa ya Mashariki katika mji wa Mombasa, Kenya, wakati dunia imeanza kumsahau kwa unyama wake, Jegan aliibuka tena mwaka 1998 Tanzania na Kenya, alipopanga milipuko iliyopishana dakika kumi tu, ule wa Dar es salaam ulitokea saa 4” na ndipo dunia ilipostuka na kutambua kuwa mtu huyu bado yupo asakwe mpaka apatikane. Ilipita miaka kadhaa serikali ya Tanzania ilipomtia mkononi Jegan katika viunga vya mji wa Tanga akiwa mbioni kutorokea ughaibuni. Ndipo ilimchukua na kumuweka jela katika gereza kuu la Ukonga akiwa anasubiri hatima yake isiyojulikana ni lini ingetimia.
??????
Jegan Grashan aliketishwa katika kiti cha chuma huku akiwa amefungwa minyororo madhubuti katika kiti kile, wale vijana wa KM wa magereza walitakiwa kusubiri nje ya chumba cha mahojiano, ndani alibaki Kamanda Amata na Jegan, wawili tu walioketi kwa kutazamana. Jegan alimtazama Amata kwa jicho la chuki na hasira, lakini Amata alikuwa akimtazama kwa jicho la upendo na ukarimu.
“Jegan, rafiki zako wametuomba tukuachie huru, upo tayari?” Amata alianza kumuuliza swali la kizushi.
“Usinifanye mimi mtoto, ninajua leo ni tarehe ngapi na ni nini kimetukia juzi” Jegan alijibu kwa sauti ya kukwaruza.
“Ok, je hiyo ndiyo njia ya wao kuomba uwachiwe huru?” Amata aliendelea
“Naam, na mtakwisha ninyi vibaraka wa Maghalibi, hii vita hamuiwezi kamwe, wao wanataka mimi niachiwe huru lakini mimi nimetumwa kwa Wamarekani nina ujumbe wao na wao wanaufahamu” Jegan alijibu huku akimwangalia Amata kwa gadhabu.
“Kwa hiyo ujumbe wao uliusafirisha kwa milipuko ya mabomu?”
“Ha ha ha ha Kamanda Amata, we ni mtoto mdogo sana na jina lako tunalo kati ya watu wanaotakiwa wachinjwe” Amata aliingiwa na hofu kidogo aliposikia mtu huyu akilitaja jina lake tena kwa ufasaha.
“Niambie ninyi ni nani na mna uhusiano gani na vitendo vya kigaidi vinavyosambaa duniani kote hivi sasa?”
“Usiniambie hujui kitu wewe mwana Intelijensia, hii ni vita kaka, tunapiga kila walipo adui zetu, 1998 tumepiga pale Dar, ile ilikuwa ni onyo na ile ilikuwa ni opereshen al – aqsa, ilipangwa kaka, na ile ya Nairobi ilikuwa ni opereshen kama hiyo, nakwambia haya yote nikijua wazi hutoyafikisha popote kaka. Kama wewe ni mwana historia kumbuka mlipuko wa bomu ulikuwa tarehe 7 august 1998 ambao ilikuwa ni miaka nane kamili tangu majeshi ya Marekani yaikalie Saudi Arabia. Una swali lingine?”
Amata alijikuta ameduwaa kwa kuwa mambo yale hakuwahi kuyaunganisha namna hiyo katika kazi zake na wala hakujua kama yana uhusiano mkubwa namna hiyo.
“Swali langu la msingi ni kuwa nani anayewatuma na kuwafadhili?”
“Kamwe sintokwambia, kwa kuwa haitakusaidia, lakini kwa kifupi mabosi wenu walioko Maghalibi ndiyo wanaotutuma”
Ilipita takribani saa nzima ya mahojiano kati ya wawili hawa, kamanda Amata alipata majibu mengi sana ya maswali ambayo labda angeyauliza miaka kumi liyopita ila yale aliyoyataka leo hakuyapata kabisa kwa wepesi.

MIAKA KADHAA ILIYOPITA

7 august, 1998
Gari aina ya Nissan Atlas iliyokuwa imepakiwa mlipuko wenye uzito wa kilogram 900 ambapo madini aina ya TNT yaliunganishwa na mitungi kumi na tano ya hewa ya Oxygen na kuzungukwa na mifuko minne ya amonium nitrate, waya uliounganishwa kutoka katika bomu hilo mpaka katika betri zilizokuwa upande wa nyuma wa gari hiyo na switch yake kuunganishwa chini ya dashboard. Gari hiyo iliegeshwa nje ya jengo la ubalozi pale katika barabara ya Bagamoyo, mlipuko wake haukuleta maafa sana kwa kuwa eneo lile hakukuwa na makazi ya watu jirani yake tofauti na Nairobi kule Kenya.
Ilikuwa ni kizaazaa katika eneo hilo watu walitawanyika ovyo, vioo vya madirisha vilivunjika, gari za zima moto na uokoaji hazikuchelewa kufika, taharuki iliukumba jiji lote la Dar es salaam.
Jegan Grashan alimaliza kazi yake aliyoikusudia na bila kuchelewa alipanda boti inayoelekea Pemba na kutokomea uko akisikilizia ni nini kitaendelea.
Vyombo vya dola vilianza uchunguzi wake mara moja kutafuta chanzo cha mlipuko huo, FBI kutoka Marekani nao walifika haraka sana kusaidia, na baada ya miezi kadhaa Jegan Grashan alikamatwa na kuhusishwa moja kwa moja na uandaaji wa milipuko hiyo (masterminds), baada ya kesi yake kuunguruma kwa kipindi kirefu alihukumiwa na kuwekwa katika gereza kuu la Ukonga.
??????
Kamanda Amata akaondoka eneo la gereza kurudi mjini, aliitazama saa yake ya mkononi, ilimuashiria kuwa ni saa saba mchana, alikanyaga mafuta kuwahi mjini kwani alikuwa na miadi na kimwana Miranda kwa chakula cha mchana, alipoanza kuteremka kilima kidogo cha kushukia Banana kuelekea alisikia kishindo kikubwa na gari yake ilianza kuyumba kushoto kulia, alijaribu kuiongoza vema lakini bado ilikuwa ikiyumba, kutokana na mafunzo aliyoyapitia ya uendeshaji gari wa kujihami ‘defensive driving’ aliyopewa alipkuwa ughaibuni aliiendesha gari hiyo kwa umakini mkubwa na alipoweza kuweka sawa alikutana uso kwa uso na lori la mchanga kishindo kikubwa kilisikika, gari ya Amata iligongwa na kukanyagwa vibaya...
KITENDO bila kuchelewa, Subaru moja nyeusi ilifika eneo hilo na kusimama jirani, watu wanne walishuka haraka na kuelekea kunako gari ya Amata, walichungulia huku na huku lakini hawakuona kitu wala mtu, mara ghafla kutoka upande wa pili wa gari ile ya mchanga kamanda Amata alijirusha na kumpiga double kick mmoja wao ambaye alidondokea katika michongoma iliyo jirani tu na barabara, kabla hajakaa sawa; tayari Beretta 92, bastola ya kiitaliano ilishafanya yake na yule mtu kuitwa marehemu, yule wa pili alijikuta ana kwa ana na kamanda Amata alijaribu kujitetea lakini haikuwezekana, mateke ya kuzunguka ya Amata yalimfanya ashindwe kujielewa na kuyumba vibaya alisimama na kujipanga kimapigano huku wale wenzake wakitafuta upenyo wa kuiondoa gari yao maana tayari gari zilikuwa zimejaa eneo lile, alirusha ngumi ambayo iliepwa na Amata, kisha Amata alijibu mapigo kwa makonde kadhaa ya mbavuni na kummaliza pumzi, wakati Amata anataka kupeleka mashambulizi mengine jicho moja liliwaona wale wanaotaka kutoroka mmoja akiwa na bastola tayari akimlenga na alipoifyatua tayari Amata alitoka eneo lile kwa kujiviringa chini na kupita uvungu wa lori na kuacha risasi ile ikipita kifuani kwa yule mwenza wao akipaishwa nakudondoka kama mzigo.
Amata alitokea upande wa pili, tayari hima hima bastola yake mkononi tena, alisikia kelele za tairi ya gari ikijigeuza barabarani lakini walichelewa bastola ya Amata alipasua kioo cha nyuma cha gari hiyo na kumjeruhi vibaya mmoja wao lakini dereva aliendelea kuiondoa gari ile kurudi uelekeo wa Pugu, kamanda Amata alitazama huku na huku akamfuata mwanamama mmoja aliyekuwa hapo na gari yake aina ya Toyota Harrier na kumtoa kwenye usukani kisha kukaa na kuiondoa kwa kasi kuifuata ile Subaru. Mwendo ulikuwa si wa kawaida, walipita mbele ya gereza la Ukonga na kuelekea pande za Gongo la Mboto, Amata alifanya juu chini asiipoteze ile Subaru ambayo ilikuwa ikienda kasi sana huku ikifanya ovateki za hatari, Amata naye alihakikisha anakwenda sambamba nalo, walipoimaliza Gongo la mboto na kuianza Pugu, tayari magari mengi yalipungua, Amata alikaza mguu na ile Harrier ilitii, dakika chache tu alikuwa anaikaribia ile Subaru. Kwa kasi ileile walipandisha mlima wa Pugu tayari Amata alishaanza kuipita ile Subaru mara ghafla akanyonga usukani upande wa kushoto na kuigonga ile gari kwa nyuma kidogo ya ubavu wake na kuifanya ile gari kuyumba upande wa kushoto na kupoteza muelekeo mara ikatumbukia na kubingirika katika bonde la mlima huo.
Amata alishuka katika gari yake bastola mkononi na kuifuata kule chini mpaka ilipokwama, alitazama ndani na kumuona yule dereva akiwa hoi pale kwenye usukani, akauvuta mlango kwa nguvu na kumtazama kwa makini yule bwana aliyejiinamia huku usukani ule ukiwa umembana kifuani, damu zilimtoka kinywani na puani, hakuna msaada, yule mwingine tayari alikwishakufa maana alionekana kuvurugwa kichwa chote kwa risasi ya kamanda Amata iliyofumua ubongo wake na kusambaratisha kichwa chake, alimsogelea yule aliyekuwa dereva wa gari ile na kumtazama vizuri, akamzaba kofi la shavu lililomfanya pamoja na maumivu yake kugeuka.
“Ninyi ni nani?” alimuuliza huku akimuwekea bastola kichwani, yule jamaa alionekana kutetemeka, “Sema, usipoteze muda!” aling’aka kamanda Amata huku akivuja damu sehemu ya paji la uso ambapo palichanika kwa vioo katika ajali ile. Yule jamaa alikuwa akihema kwa tabu sana, mara simu ya Amata ikaita, akaingiza mkono mfukoni na kuitoa alipotazama kwenye kioo aliona jina la ‘Miranda’ likiwakawaka, akabonyeza kitufe chekundu na kuirudisha mfukoni, alipogeuka kwa yule jamaa alimkuta tayari ameshakufa akiwa anamwagika povu na damu kinywani. Kamanda Amata aliirudisha bastola yake mahali pake na kumpekuwa yule jamaa, bahasha ya khaki ilikuwa katika mfuko wake, vitambulisho kadhaa na kadi za kibiashara, alipoona vinatosha alivihifadhi mfukoni mwake na kupanda kile kilima kuifuata ile gari aliyoiacha pale juu. Akajikung’uta vumbi na kujihifadhi ndani yake, aliiwasha na kuigeuza kisha taratibu kuifuata barabara ya Nyerere kurudi mjini, mbele kidogo alikutana na gari za polisi wakamuwashia taa kwa ishara ya kusimama nae akatii.
Amata alimuona yule mama aliyemnyang’anya gari akiwa na wale polisi wakimfuata, akashuka na kuwasubiri.
“Kijana tunakuweka chini ya ulinzi kwa kuwa umepora gari ya watu na kufanya mauaji” polisi mmoja alimwambia Amata huku akitoa pingu zake mfukoni mwake, Amata alinyoosha mikono yake na kufungwa zile pingu huku shati lake likiendelea kulowa kwa damu tiririka zilizokuwa bado zinadondoka kwenye jeraha lake. Akaingizwa kwenye gari Land Cruiser ya polisi na kuamuriwa alale chini kisha wale polisi wakasimama juu yake na ile gari ikageuzwa kurudi mjini huku polisi mmoja na yule mama wakiingia katika ile harrier na kuwafuata nyuma.
Mabatini polisi, Stakishari
“Weka ndani jambazi hili, linapora magari ya watu tu,” yule polisi alimwambia mwenzake huku akimsukumia Amata nyuma ya kaunta.
“Vua mkanda, vua viatu uingie pale kwa wakora wenzio” aliamuru polisi aliyekuwa nyuma ya kaunta karibu kabisa na WP mmoja aliyekuwa akiandikaandika katika daftari kubwa, aligeuka na kumuangalia Amata kwa makini juu mpaka chini, kisha akasonya.
“Unashangaa nini si umeambiwa uingie huko ndani” yule WP naye aliongea huku akibetua midomo yake.
“Tafadhali afande nakubali, ila naomba nimpe taarifa mke wangu ili ajue niko wapi” Amata aliomba
“Haya we afande Mary, msaidie ombi lake kisha aende huko ndani” amri ilitolewa na yule polisi aliyemleta Amata pale kaunta.
WP Mary alimtazama Amata kwa mara ya pili na kubetua midomo yake kinafiki.
“Unaomba tu upige simu unajua anayezilipia ni nani? Haya taja namba haraka watu tuna mambo mengi,” WP Maria alimueleza Amata kwa sauti kali, Amata alimtajia namba ile yenye takribani tarakimu saba, WP Maria alizungusha tarakimu zile kisha akaweka kile chombo sikioni.
“Haya inaita, ongea haraka,” WP Maria alimwambia Amata.
“Hello mama, mimi kijana wako, nakupa taarifa kuwa nimekamatwa na polisi nipo hapa kituo cha Mabatini Stakishari Ukonga, msaada wako tafadhari” Amata alirudisha simu kwa WP.
“Ongea na mama tafadhali” alimwambia
“ (…) Ee tumemkamata mwanao we njoo ndiyo utajua kosa lake, hatuna muda wa kuongea kwenye simu” WP Maria alimaliza na kukata simu.
“Haya ingia huko ndani,” alimwambia Amata, naye bila shida aliingia na kufungiwa selo pamoja na vijana wa kihuni wa kila aina ndani humo.
??????
“Jambo afande!” OCD Masoketi aliwasabahi polisi waliokuwa katika kaunta ya kituo hicho na wote wakakauka kwa kusalute kwa mkuu wao wa kazi, walionbekana wazi kujiweka sawa hapa na pale maana hawakutegemea ujio huo kwa muda wa adhuhuri kama ilivyotoke. OCD Masoketi alisimama karibu na ile kaunta na kuwaangalia wale vijana walioonekana busy na kazi mbalimbali.
“Afande, kuna mtu mmemkamata na kumuweka ndani hapa mida hii?” OCD akauliza
“Ndiyo mkuu, ni jambazi aliyepora gari ya huyu mama tunayemchukua maelezo sasa,” alijibu WP Maria
“Mna uhakika gani kama ni jambazi?”
“Kwa maelezo ya huyu mama, ni kuwa gari yake alinyang’anywa katika eneo la ajali pale karibu na Banana na kabla ya hapo anasema huyu mtuhumiwa alikuwa anarushiana risasi na watu wengine. Na hapa tumemkuta na bastola aina ya Berreta 92 vyote vimehifadhiwa mkuu” alijibu polisi mwingine aliyemleta Amata pale kituoni.
“Muwe makini na kazi yenu nyie vijana, nimeshawaambia mara nyingi jinsi ya kumhiji na kumchunguza mtuhumiwa, au hamjajifunza CCP? Haya nifungulieni huyo mtu haraka mniletee ofisini kwangu” OCD Masoketi aliongea huku akiwanyooshea mkono uliokuwa na redio call mkononi. Kamanda Amata alifunguliwa kutoka selo na kuongozwa na WP Maria mpaka ofisini kwa OCD.
“Karibu kamanda, keti kitini, WP mletee kinywaji baridi tafadhali” OCD alitoa oda na kutekelezwa na WP kwa haraka, huku kichwani mwake akitafakari ni nani huyu anayeitwa kamanda. Mazungumzo yalifanyika ofisini mle kwa dakika chache tu na yule mama alipewa maelekezo ya kufuata ili kesho yake apewe gari ingine kwa kuwa ile ilikuwa imeharibika sana upande wa mbele, baada ya kumaliza kila kitu alirudi kaunta na kurejeshewa vitu vyake vyote alipovikagua viko salama, akachomoa kadi yake moja ya biashara na kumtupia WP Maria.
“Baadae unitafute,” alisema huku akiteremka ngazi na kusimama kwa muda. Yule mama aliondoka na tax aliyolipiwa na Amata na kuiacha ile gari yake pale kituoni, akiwa bado na mazungumzo na OCD mara freelander ya kijivu ilisimama kando kidogo ya mti mkubwa uliokuwa hapo, wakaagana na OCD kisha akaiendea ie gari na kuingia ndani.
“Amata nini tena? Mbona una majanga kijana?” ilikuwa sauti nyororo ya Gina, katibu wake muhtasi katika ofisi yao ya AGI International-clearing and forwading.
“Ah Gina we acha tu, hebu nipeleke hospitali kwanza kisha tukapate lunch mahali”
“Kwanza nashangaa kukuona hapa, we si ulikuwa China!?”
“Nimerudi jana ila sikukwambia makusudi ilikuwa surpries tu,” kisha wote wakacheka na kugonga viganja vya mikono yao.
“Haya bwana nimefurahi kukuona tena nilikuwa mpweke kweli bora umerudi mtu wa kunipa faraja” Gina aliongea huku akiingiza gari barabara ya Nyerere na kuiacja ile ya Segerea.
“Mmm unataka nipigwe na Malick?” Amata akamtania Gina huku wakipotelea mjini.
??????
Betram aliinua mkono wake na kutazama saa yake ilikuwa tayari saa tisa na dakika kadhaa, akiwa bado amesimama katika dirisha la ghorofa ya tano akiangalia chini getini labda atawaona vijana wake wakirudi haikuwa hivyo, moyo wake ulianza kukumbwa na wasiwasi, alitoka pale dirishani na kuindea meza kubwa yenye kompyuta na vitu vingine vya mawasiliano ambapo kulikuwa na mtu mmoja wa makamo.
“Kaka! Hawa jamaa sidhani kama wamefanikiwa misson tuliyowatuma naona muda unakwenda, vipi unawapata kwenye GPS?” Betram alimuuliza Shakrum mtaalamu wao wa mawasiliano.
“Hapana hata huku siwaoni kabisa nafikiri kwa vyovyote watakuwa wamepata tatizo maana hata simu zao hazipatikani kabisa” Shakrum alijibu, huku akijaribu kubofyabofya tena simu iliyopo pale mezani akijaribu kuwatafuta swahiba zao hao. Alipojaribu kupiga ile simu kwa mara nyingine iliita kwa muda mopaka ikakatika, moyo ukaanza kumuenda mbio, kabla hajasema lolote simu ya mezani iliita akainyakuwa kwa shauku.
“Fungua TV yako utazame TBC” sauti ya upande wapili ilimwambia kisha simu ikakatika. Shakrum alinyanyuka haraka na kuindea TV kubwa iliyopo hapo sebuleni na kuiwasha kisha kuchagua ile channel aliyoambiwa.
“Mama yangu mzazi!” Betram alitamka kwa sauti huku mikono yake ikiwa kichwani kwa mshangao, walitazama ile habari ya wakati huo ikionesha ajali iliyotokea mchana ule na nini kiliendelea, kisha gari iliyokutwa katika bonde la mlima wa Pugu na maiti za watu wawili ambazo hazikutambulika kwa mujibu wa polisi.
“Shakrum, fanya haraka funga vitu vyako tuondoke hapa siyo pa kukaa tena, twende Mombasa tukajipange upya tuendeleze kazi yetu, hatukati tamaa” Betram alimweleza Shakrum kwa kumsisitizia huku akiingia chumbani kwake na kukusanya kila kinachomhusu, ndani ya nusu saa walikuwa tayari kwenye gari yao aina ya Toyota Prado tayari kwa kuondoka. Mara simu ya Betram ikaita
“Ee ndiyo tunaondoka sasa na jamaa zetu wane wameuawa katika sakata hilo wameshindwa kufanikisha mission yetu (…) yeah nimekusikia boss, tutakuwa hapo alfajiri ya kesho.”
??????
Usiku huo Kamanda Amata aliegesha gari yake karibu na barabara ya kuingia hosteli za chuo kikuu zilizopo Mabibo, kisha akateremka na kutembea kwa tahadhari akiufuata ukuta unaotenganisha kiwanda kimoja na magenge ya wauza mboga, ilikuwa kama saa nane hivi eneo lote lilitawaliwa na ukimya wa hali ya huu, watu walishalala zamani waliobaki nje ni makahaba, wezi, wachawi na wale tu wenye kazi maalum. Aliendelea kuambaa ambaa na ule ukuta mpaka upande wa nyuma na hapo alijikuta karibu na jingo refu la ghorofa kama saba hivi lililojengwa ndani ya wigo ule, sauti za watu zilisikika zikitoka upande wa ukuta ule kule alikotoka, kwa utulivu mkubwa alijibana kati ya ukuta na nguzo kubwa ya umeme, hakuweza kuonekana na mtu hasa kutokana na mavazi yake meusi yaliyomfanya afanane na kiza cha usiku huo. Vijana kama watatu walipita eneo lile wakiwa na vitu mbalimbali wamevibeba huku wakionekana kulaumiana kwa jambo Fulani, vibaka. Walipopita tu, taratibu Amata alikwea ile nguzo ya umeme na kujikuta juu ya ukuta, kisha akatua ndani taratibu na kuchuchumaa kwa ustadi uliowafanya walinzi wa eneo lile wasistuke kama kuna kiumbe kimeingia. Kisha akatazama huku na huku ili aone wapi pa kuelekea, mlinzi mmoja alipoenda upande wa pili Amata alikimbia kwa tahadhari na kujificha nyuma ya matank ya maji yaliyowekwa pembezoni mwa jengo lile, alitazama mlango wake wa kuingilia ndani kisha akauendea na kupachika ile funguo yake maalum kisha akaingia na kuufunga nyuma yake, ngazi ndefu zilikuwa zikimsubiri, akapanda ya kwanza na ya pili akakutana na milango kadhaa, hakujua hasa mlango gani anaoukusudia, alisimama kidogo kisha akatoa simu yake na kuipiga namba Fulani, akasikia mlio wa simu inaita ghrofa ya juu, akaikata na kutulia kidogo kisha akaendelea kupanda ngazi hadi gorofa mbili zinazofuata na kukuta mlango mmoja tu, akatoa funguo zake na kupachika tunduni alipozungusha tu mlango ulilegea na kufunguka.
Sebule kubwa lilimkaribisha lililojazwa vitu vya thamani vya kisasa aliichunguza ile sebule kwa macho kisha akaenda kwenye meza kubwa iliyokuwa na kompyuta juu yake akaiwasha na kujaribu kupekuwa hapa na pale lakini hakuna cha maana alichokiona, akaiacha na kuingia chumbani hakuna mtu, akafikiri kwa muda akaona windo lake alilolitegemea amelikosa akageuka kuondoka, lakini macho yake yakavutwa na karatasi moja iliyo chini ya kabati, akaiendea na kuiokota akaifungua harakaraka ilikuwa ni tiketi ya ndege ya iliyobeba jina la Shakrum Shakran, raia wa Khazakistan, aliyeingia nchini siku nne nyuma kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar, kamanda Amata aliitia mfukoni tiketi ile na kutoka katika jengo lile kwa mtindo uleule.

Kenya Bay Beach Hotel – MOMBASA

Ukimya ulitawala katika meza moja ya duara iliyozungukwa na watu takribani saba waliokaa kwa kutazamana, hakuna aliyeongea kabisa ilionekana kama wote wamepatwa na mshangao. Aliyeonakana kama kiongozi wao alikohoa kidogo na kuwatazama wenzake walioonekana kama wamegutushwa kwa kukohoa huko.
“Leo ni siku ya tatu tangu tutekeleze ule mlipuko pale Dar, tunawasikiliza kama watatimiza takwa letu la kumuacha huru Jegan Grashan, lazima tumkomboe mwanamapinduzi wetu kwa damu iwayo yote. Tanzania wametuchokoza, kuwaua vijana wetu wane kwa siku moja ni dharau kubwa sana, tutahakikisha tunalipiza kwa mamia ya damu. Sasa tusuke mpango mwingine wa kuwamaliza mpaka aikulu yao itikisike kwa hofu” aliongea kwa jazba na kupiga meza kwa ngumi. Kila mmoja lionekana kushusha pumzi nzito.
“Mbaya zaidi yaani mtu mmoja awamalize watu wanne, watu waliofuzu mafunzo ya kijeshi, ya upiganaji wa silaha na ana kwa ana, bado sijaamini, Betram, inawezekanaje?”
Betram alitulia tuli hakuwa na jibu la uhakika kwa maana kama ni taarifa alikwishaifikisha jinsi ilivyo.
“Aah inaonekana walifanya makosa kidogo, kwa sababu tulipofika Tanzania kwanza tulianza kufanya uchunguzi wetu wa wapi pa kuanzia, tukagundua kwamba kuna mtu wao mmoja ambaye ni matat sana katika kugundua hujuma kama hizi, kwa hiyo nikawapanga kumshambulia na kumpoteza mara moja, lakini ndiyo hivyo badala yake ni yeye pekee aliyewamaliza wote wanne.” Betram alijibu.
“Ok, sasa tunabadilisha mbinu, nitakuongezea wtu wawili wa juu, ambao wao wanaijua kazi yao sawasawa na hawaweai kufanya makosa kama hayo. Sasa hebu Shakrum, weka hiyo DV cam niwape onyo kali” yule kiongozi wao aliyejulikana kwa jina la Beishal alitoa amri na mara moja ile mashine ya kurekodia ikategwa tayari kwa kumrekodi, kama kawaida akavaa ile sox yake usoni.
“…Imebidi kuwapa onyo hili mapema kwa kuwa mmetupotezea wapiganaji wetu wane ambao mtawalipia kwa damy nyingi kutoka kwa wananchi wenu wasio na hatia, tunakuja tena kwa nguvu mpya badala ya zile siku saba sasa mlipuko mkubwa muutegemee ndani ya saa 48 tu. Vijana wetu wane thamani yao ni sawa na wananchi wenu mia moja, kaeni tayari, hatutawaacha kwa kuwa mmejiingiza kwenye vita isiyowahusu, na kwa tukio la jana mmechokoza nyuki, tutawauwa mpaka mumuachie huru kaka yetu Jegan Grashan mpigania haki asiyechoka…”
Kama kawaida yao wakaituma ile DVD kwa njia ya DHL ili ifike kwa haraka zaidi.
“Betram, nakubadilisha nafasi yako, wewe utakwenda Somalia na Shailan wa Somalia ataongoza vita baridi huko Tanzania na vijana wengine watatu nitawaongeza, mmoja nitamtoa Mali mwingine Afghan na Pakistan nina uhakika watamaliza kazi ndani ya wakati kwa mbinu yoyote ile” Beishal alimaliza na kuwtaka kila mtu kurejea katika kazi yake na mapinduzi yaendelee kama yalivyopangwa.
Dar es salaam
Waziri wa ulinzi alionekana wazi akitetemeka baada ya kuitazama DVD ile iliyowafikia mchana wa jua kali la saa saba, alishika remote na kuitoa katika ile mashine maalumu kwa kazi hiyo, aliirudisha kwenye kasha lake na kuiweka mezani kisha akamtazama IGP aliyekuwa ameketi hapo.
“Unafikiri wapi hawa jamaa watalenga kwa sasa?” sauti ya kitetemeshi kutoka kwa waziri Maige.
“Aaa hapa nikujipanga kila kona yenye mikusanyiko ya watu, inabidi CID wetu wafanye kazi ngumu ya kujichanganya na watu, na sasa hatuwezi kuilinda Dar peke yake wanaweza kwenda kulipua Kigoma, hawa jamaa hawana mana kabisa” IGP alimueleza waziri.
“Mwisho wa yote ni nini?” alitupa swali na waziri wa mambo ya ndani akajibu.
“Hawa jamaa wana mtandao mkubwa sana, kwa hiyo kupambana nao inabidi kutumia vyombo vyetu vyote vya usalama nchini kwa sababu hujui watatokea wapi.”
Maazimio ya kikao hicho yalipitishwa na kila kona kulimwagwa polisi wa kutosha na ukaguzi kila sehemu zenye mikusanyiko ya watu, hakika hali ilikuwa tete, ilikuwa ni sawa na kupigana na gizani maana humuoni unayemshambulia, ilmradi tu kila sehemu kulikuwa na ulinzi wa kutosha.
??????
Amata alishusha simu yake kutoka sikioni na kuiweka mezani kwake kisha akainua kikombe cha kahawa na kupiga funda moja. Akavuta gazeti mojawapo lililokuwa hapo mezani na kusoma habari nzito iliyobeba kurasa ya kwanza (good copy) iliyosomeka
‘Magaidi watoa kitisho kingine, kuishambulia Dar es salaam muda wowote’
aliisoma habari ile kwa kina sana na kuielewa vizuri, kichwani mwake mawazo mengi yalimzunguka akifikiri nini cha kufanya kwenye sakata hilo wakati wakiwa wamebakiwa na siku nne tu walizopewa na magaidi wale. Alivuta kitabu chake cha kumbukumbu na kufungua karatasi kadhaa alizokuwa akiandika andika na kusoma mambo Fulani, mara simu yake ikaita, akainyanyu kwa haraka.
“Yes hello! (…) Ok asante (…) sasa hivi natuma mtu” aliishusha simu yake na kumuita Gina ambaye muda huo alikuwa akichapa kazi Fulani katika computer yake ndogo.
“Niambie kaka” aliitika wito
“Kuna kazi kidogo, nenda pale ofisi za Qatar airways kuna mzigo watakupatia uniletee haraka” alitoa maagizo. Gina bila kuchelewa aliiacha ofisi na kukodi bajaji ili aweze kuwahi kazi aliyotumwa.
Ofisini alibaki Amata peke yake akiumiza kichwa kujua jinsi ya kulimaliza swala hilo mara kengele ya mlango ikalia, akafikiri kidogo na kuivuta droo yake, akatoa bastola yake aina ya Beretta 92 na kuitia katika mfuko wa koti huku ameishikilia tayari tayari maana hakuna kuaminiana nyakati hizo, aliuendea mlango na kuufungua kwa tahadhari ya hali ya juu, hakuyaamini macho yake, mwanadada mrembo alisimama mbele yake akiwa amevalia vazi refu kutoka juu mpaka chini, alimtazama Amata kwa jicho la mahaba na kutaka kuingi ofisini mle, Amata alibaki tu kumtazama msichana yule aliyekadiriwa kuwa na umri kama wa miaka 28 hivi.
“Karibu sana, wewe ni nani?” kamanda Amata aliuliza
“Nimeagizwa kuleta mzigo ofisini kwako, bila shaka wewe ni kamanda Amata” alijibu yule msichana. Kengele za hatari kichwani mwa Amata zikagonga.
“Nipe tafadhali na uniambie ni nani aliyekutuma” Amata alimwambia.
“Sawa twende ndani,” akisema yule msichana huku akivuta hatua kuingia ofisini kwa Amata, Amata alijikuta akimruhusu kupita ofisini kwake na moja kwa moja akaketi katika kiti kinachotazamana na kile alichoketi Amata, mara akasikia mlio wa alarm ukitoka kwenye saa yake ambayo alikuwa ameivua na kuiweka mezani hapo kwa muda mrefu. Mlio ule ulizidi kuwa mkali, Amata akachomoa bastola yake na kumuelekezewa yule msichana.
“Simama haraka, haraka” alimuamuru. Yule msichana akataka kuwa mbishi.
“Nitakufumua kichwa chako sasa hivi, shetani wewe simama” alimuamuru tena na ile saa ilizidi kupiga kelele kuashiri imeditect aina ya mlipuko ulio jirani sana na eneo ilipo. Amata aliona anapoteza muda na kifo kilikuwa dhahiri mbele yake, hakupenda kumpoteza kwa risasi kiumbe yule mrembo mwenye sura ya kuvutia, alirudisha bastola yake kiunoni na kumtandika makofi mawili ya haja mpaka yule msichana akasimama.
“Vua hilo nguo lako haraka?” alimuamuru, yule msichana alichomoa bastola kutoka kwenye ile nguo yake na bila kusita aliiondoa usalama tayari kufyatua, lakini alichelewa, ticktack iliyopigwa na Amata iliitoa ile bastola mkononi mwake na kufyatuka ikiwa hewani, ngumi moja ya usoni ilimchanganya yule msichana kabla hajakaa sawa, teke moja lililopigwa nyuma ya magoti yake lilimfanya apige magoti, Amata kwa wepesi alimvua lile gauni lake refu kwa kulivuta juu na kumuacha msichana yule chuchu nje akibaki na chupi tu. La haula la kwata bomu lilitegwa kwa saa lilikuwa limefungwa kuzunguka tumbo lake dogo, likiwa na milipuko kadhaa, na saa ya kidigitali ilikuwa ikiwakawaka kuonesha ni dakika mbili tu zilibakia. Kwa wepesi wa ajabu alichukua kiberiti chake na gazeti alilokuwa akisoma akaliwasha na ule moshi wake akauruhusu uwende kwenye sensa maalum ya kusensi moshi, punde tu kengele kali zikalia jengo zima na na vifaa maalum vya kumwaga maji kusaidia uzimaji moto vikafunguka kila kona maji yalimwagika tayari kuzima moto wowote ambao upo eneo lile, watu walitawanayika milango ilibamizwa wote wakitaka kutoka nje kuokoa maisha yao. Kwa kisu chake cha kukunja alikata ule mkanda maalum uliofungiwa lile bomu na kufanikiwa kulitoa tumboni mwa yule msichana, kwa haraka akatoka nalo likiwa mkononi kuelekea nje huku akiwapiga vikumbo watu waliokuwa koridoni wakikimbia kuokoa maisha yao. Alifanikiwa kufika katika ngazi za kushuka chini au kupanda juu, aliitazama saa ya lile bomu ilisoma bado sekude 55 tu, aliingia kwenye lifti na kuiamuru ipande ghorofa ya juu kabisa nayo ikatii. Sekunde 40 alikuwa juu kabisa ya jengo la JM MALL, aliisoma ile saa hakuwa na ujanja, alijaribu kufanya anachoweza ilipotimu bado sekunde 2 alilirusha juu lile bomu na kisha kulala chini, mlipuko mkubwa ulitokea angani watu waliochini walishtuka hawakujua nini kimetokea, moshi mzito ulitawanyika juu na mtikisiko wake ulifanya baadhi ya vyoo vya madirisha ya majengo mengine kupasuka na kutawanyika barabarani, watu walikuwa wakikimbia ovyo huku na kule. Kamanda Amata aliinuka kutoka pale alipolala na kushuhudia mshikemshike uliokuwa huko chini, alirudi haraka kwenye lifti na kuingia kisha kuimauru iteremke mpaka pale pale alipopandia.
Aliusukuma mlango wa ofisini kwa nguvu na kuingia kwa minajiri ya kumuwahi yule msichana, peupe, hakuna msichana wala nguo yake, altazama huku na huku hamna mtu, aliichomoa bastola yake na kuwahi chini ya jingo lile ambapo vurugu kubwa ilikuwa pale katika korido kubwa karibu na supermarket ya Shopprite, ailisimama na kutazama huku na kule asimuone, akasogea karibu na barabara kubwa, barabara ya Samora, huku na huko alimuona mtu aliyevaa vilevile akamkimbilia na kumkamata, sio yeye, Amata alichanganyikiwa, akendelea kusaka huku na huko, hakuna mtu, kila mtu alimuona kama amechnganyikiwa.
Gari za polisi zilianza kuingia eneo lile kwa mbwembwe zikifuatiwa na zile za zimamoto, tayari askari wa usalama barabarani walishaifunga barabara ya Samora kuanzia mnara wa sasa mpaka makutano na barabara ya Morogoro ili kuruhusu shughuli za uokoaji kuendelea kama inabidi. Kamanda Amata akiwa na bastola yake mkononi aliteremka ngazi na kufika barabarani ambako kulikuwa na vurugu za watu tu wakikimbia na kukanyagana kelele za ‘bomu, bomu’ zikitawala eneo lote hilo.
Watu wa zimamoto waliingia ndani ya jengo hilo tayari kwa kazi yao ya uokoaji, watu waliobakia ndani walikuwa wakitolewa na kupakiwa kwenye gari za wagonjwa kwa kukimbizwa hospitalia. Amata alirudisha bastola yake kiunoni na kusimama sehemu akitazama pilikapilika zilizokuwa zikiendela huku macho yake yakipepes kiufundi kuangalia kila anayeingia au kupita eneo hilo. Moyo ulimpiga kwa nguvu alipoona wafanyakazi wawili wa zimamoto wakiwa wamemshika msichana mmoja wakitoka naye nje katika harakati za kuuokoa lakini cha kushangaza msichana yule hakupakiwa kwenye gari la wagonjwa bali walimpakia kwenye gari ya zimamoto kisha wale jamaa nao wakapanda, ile gari aina ya Dennis iligeuzwa na kuanza kuondoka eneo lile ikichukua barabara ya Samora kuelekea picha ya askari kisha kuifuata barabara ya Maktaba.
Kamanda Amata aliijua ile ni trick na alijua kuwa kwa vyovyote ilikuwa ni mbinu ya kumuokoa binti huyu, hakuwa na muda wa kujiuliza maswali mara mbili, alitazama huku na huko na kumuona askari mmoja aliyekuwa na Honda ya kipolisi 350 CC, alimfata na kumuamuru ashuke mara moja, kisha akakaa juu ya lile pikipiki na kuingiza gia ya kwanza, alilizungusha kwa ufundi mkubwa na kuiacha barabara ya Samora na kuichukua ile ya Morogoro, alipofika barabara ya Bibi Titi alikunja kulia kwa kutumia upande usio sahihi ili kuikabili ile gari ya zimamoto, hakukosea kwani aliiona ikija upande huo mara moja akaitoa ile bastola yake ya kiitaliano na kulenga tairi ya ile gari, shabaha ya kwanza haikuwa sahihi, dereva wa gari ile aliliona hilo akayumbisha gari na kufanikiwa kuiepa ile risasi, Amata aliuma meno, wakiwa jirani kabisa kabla hajafanya lolote, kishindo kiliskika , pikipiki ya kamanda Amata ilikanywagwa na kupondwapondwa kabisa.
Amata alijirusha pembeni upande wa jingo la wizara ya Vijana na kutua sawia kwa goti moja bastola mkononi, shabaha ya pili ilipiga tairi ya nyuma na kuifumua vibaya, ile gari iliyumba barabarani na kusababisha ajali kadhaa lakini hakuna aliyefuatilia, jamaa waliijua vyema kazi yao, ile gari ikaacha barabara ya Bibi Titi pale kwenye mataa ya DIT na kukunja kulia kuelekea Faya, kamanda Amata alibaki chini barabarani hana la kufanya ile lori imeshaondoka, ‘Hayawani wakubwa hawa’ aliwatukana kimoyomoyo na kujinyanyua lakini alijikuta akirudi chini na maumivu makali kwenye bega lake la kulia, aliiokota bastola yake na kuiweka mahali salama, watu walianza kujaa wakijuwa kuwa hilo ni jambazi wengine walitwaa mawe tayari kumpiga, kamanda Amata aliona hiyo ni hatari, aliichomoa bastola yake na kufyatua risasi kadhaa hewani na kuwafanya watu wale kutawanyika, kwa haraka alinyanyuka pale alipo licha yakuwa alikuwa na maumivu alijikokota na kuifikia tax ya jirani na kuomba apelekwe eneo la tukio na mara yule dereva akfanya hivyo.
Madam S, alitulia tuli kama maji ya mtungini huku akili yake ikizunguka kwa kasi, akitafakari jaribio lile ambalo kama si Amata basi jengo la JM MALL lingekuwa likiteketea na kusababisha vifo vingi hasa cha kamanda Amata ambaye ofisi yake ya siri iko hapo katika jengo hilo. Hakuwa anajielewa sawasawa, mbele yake mezani kulikuwa na mafaili kadhaa ambayo labda alitaka kuyafanyia kazi au sijui alitaka afanye nini nayo. Aliinuka na kupekua faili moja baada ya jingine kisha akachukua moja na na kulitia katika begi maalum na kufunga ofisi, alijipakia katika gari yake na kuondoka eneo lile.
Breki yake ilikuwa mbele ya ofisi ya wizara ya ulinzi, moja kwa moja aliingia ofisini kwa mheshimiwa Maige na kulitoa lile faili kisha kulitupia mezani kwa waziri huyo.
“Mheshimiwa, mi naona ili tuifanye kazi yetu vizuri, muachilie huyu mtu huru” madam S aliongea kwa jazba.
“Oh! Madam, vipi tena? Mbona hasira mchana huu?” waziri Maige aliongea huku akiwa amesimama.“Hivi leo wangekufa watu mamia, kama si Amata kufanya aliloweza, msichana yule alitaka kujitoa mhanga kwenye ghorofa ya ngapi sijui, hapana mheshimiwa, mpe removal order huyo mtu atoke arudi kwao”
Juu ya meza ya waziri Maige faili lililoandikwa ‘JEGAN GRASHAN’ lilikuwa limetulia likisubiri amri ya waziri ili lifanyiwe kazi. Waziri Maige aliliangalia faili lile na kutikisa kichwa chake kuonesha kama hajakubaliana na kitu Fulani.
“Madam!” hili swala lipo juu ya uwezo wangu, inabidi mheshimiwa Rais ndiye aamue juu ya huyu mtu kama kutoka au la”
“Mheshimiwa waziri, naomba ulishughulikie hili haraka iwezekanavyo. Mi nafikiri tukimuachia huyu, tutakuwa katika hali ya utulivu sana hapo tunaweza kuwasaka hawa jamaa kwa taratibu tu mpaka tuwakamate”
Gereza la Ukonga
“Kwa nini watu wako wanafanya milipuko ya namna hii? Wanafikiri kwa kufanya hivyo ndiyo tutakuwacha huru?” kamishna wa Magereza Tanzania alikuwa akimuuliza Jegran, huku akiwa na jopo la watu wengine, waziri Maige na madam S walikuwa miongoni mwao.
“Kwa nini mnaniuliza swali kama hili? Ninyi wenyewe mnajua na wamekwishawaambia wanataka nini, mkitekeleza wanalotaka mtakuwa huru dhidi ya mashambulizi haya, msipotekeleza mtaendelea kuangamia,” Jegran alijibu kwa sauti yake kavu nay a upole.
“Serikali ya Tanzania inataka kukuacha huru! Uko tayari?” waziri wa ulinzi bwana Maige alimuuliza.
“Hata mi nashangaa kwa nini mmenifunga bila kosa, sina kosa mimi” Jegran alijibu.
“Huna kosa!? Kuulipua ubalozi wa Marekani hapa nchini si kosa?” Madam S aliuliza kwa jazba
“Nililipua ubalozi wa Marekani, wangenikamata Wamarekani, sasa ninyi mmenikamata kwa kosa gani? Ndiyo maana mnapata misukosuko, na sasa jiandaeni kwa maangamizi”
Madam S alishikwa na hasira na kuuma meno. Baada ya mazungumzo hayo na tayari wakikubaliana kumuachia huru gaidi huyo, jopo hilo lilitoka katika eneo hilo na kuondoka zao.
??????
Akiwa na bandage yake mkononi, kamanda Amata alitembea taratibu pembezoni mwa barabara ya Morogoro katika eneo la Jangwani ambapo ile gari ya zimamoto ilikuwa imetelekezwa hapo na jeshi la polisi lilikuwa likifanya jitihada za kuiondoa katika eneo hilo.
FK Security Group, ilikuwa ni nembo iliyong’aa sana katika ubavu wa gari ile, kamanada Amata aliitazama nembo ile na kuipiga picha kwa sababu mbalimbali za kazi yake, kisha bila kuongea na mtu yeyote aliingia kwenye tax na kuomba kupelekwa eneo la Mikocheni.
FK Security Group
Taratibu aliuendea mlango ulioandikwa FK Security na kubofya kitufe cha kengele, alipoitikiwa aliufungua na kuingia ndani. Msichana mrembo alikuwa nyuma ya kompyuta kubwa akiendelea na kazi.
“Karibu kiti kaka, nikusaidie nini?” alimuuliza Amata.
“Naitwa Stephen Amalutwa, muandishi wa gazeti la Dar es salaam leo, nimekuja hapa kuulizia juu ya sakata la gari lenu la zima moto kutumika katika jaribio la kigaidi pale JM MALL ghorofa ya saba” alijitambulisha huku akiweka kitambulisho chake mezani, kitambulisho cha uandishi wa habari.
“Gari yetu sisi, imetumika? Ipi hiyo, mbona mi sina taarifa na nadiye ninaeratibu shughuli zote za ofisi hii?” aliuliza yuke dada.
“Inawezekana, lakini gari ile ni ya kwenu,” Amata, muandishi bandia akatoa simu yake na kumuonesha ile picha ya gari hiyo na namba zake za usajiri, yule dada alipatwa na mshtuko na akanyanyuka na kumwambia Amata asubiri, kisha akaenda na kuingia katika ofisi Fulani, na baada ya dakika kadhaa alitoka na kurudi pale alipokuwa mwanzo.
“Bwana Amalutwa, haya ingia ofisi namba tatu pale utapata majibu yako yote” aliambiwa.
Kamanda Amata aliinuka na vifaa vyake, na kuelekea katika ofisi aliyoelekezwa.
Mbele yake aliketi bwana mmoja mnene kidogo ambaye alikuwa na ndevu nyingi zilizouzunguka uso wake kwa upande wa mashavuni, walitazamana na Amata kisha wakasabahiana na kuanza mazungumzo yao.
“Kutokana na maelezo yako bwana Amalutwa, sisi hatuna gari ya uokoaji yenye namba hizo, gari zetu zote ni hizi hapa” aliongea yule bwana aliejitambulisha kwa jina moja tu, Scoletti. Alitoa faili kubwa na kufungua kadi original za usajiri wa magari yale, Amata alitazama na kweli hakuona gari iliyosajiriwa kwa namba hizo.
“Na unasemaje kuhusu hii nembo yenu ya kampuni katika gari ile?” alimuuliza
“Aaaa itakuwa ni wahuni tu wameamua kutumia jina letu tu ili kutuharibia biashara, kama unavyojua sisi ndiyo kampuni ya kwanza ya binafsi kuanza kutoa huduma hii” Scoletti alijibu huku akirudisha lile faili. Kwenye shelf maalum lililo katika kabati moja kubwa pembezoni mwa ukuta. Amata aliandika vitu Fulani katika kijitabu chake, kwa macho ya kipelelezi aliiangalia ofisi ile na kuona sehemu zote zenye ulinzi na vifaa vya ulinzi moyoni mwake aliahidi kurudi usiku huo kwa upekuzi zaidi. Waliagana na kuondoka katika ofisi hiyo.
Scoletti alitoka ofisini kwake akiwa amefura kwa hasira mapaka kwa secretary wake.
“Wewe, nikwambie mara ngapi unielewe? Nimeshakwambia sitaki umruhusu mtu au uongee na mtu kitu usichokijua, wengine hawa wanatupeleleza, utasababisha kampuni hii kufungwa wewe. Sasa nakupa likizo ya mwezi mmoja na malipo yote yanayokustahili, utarudi kazini baada ya mwezi mmoja” alimkemea yule dada.
“Lakini Boss, yule si ni mwandishi wa habari nae alikuwa katika majukumu yake ya kazi?” aliuliza yule dada.
“Nani aliyekwambia? Yule ni mpelelezi wa serikali, mpelelezi anayetegemewa hapa Tanzania. We unaruhusu watu tu waingie, tunaweza kuuawa humu ndani na we usijue” kisha akampa sonyo refu. Baada ya dakika mbili akaja na hawala ya fedha mkononi na kumkabidhi yule dada.
Yule secretary hakuwa na la kufanya, likizo ya dharula ilikuwa mezani kwake, hawala ya fedha kwa likizo ilikuwa mkononi mwake, milioni mbili zilisainiwa, machozi yalikuwa yakimlenga yule dada kwa kosa alilolifanya, aliichukuwa ile barua na ile hawala kisha akaagana na boss wake na kuondoka. Alisimama nje katika barabara ya Bagamoyo, akaangalia kushoto kulia hakuona anachokitafuta. Mara akatoa kadi ya kibiashara na kuitazama juu yake iliandika kwa wino mweusi na maandishi ya kuremba Mr Stephen Amalutwa, ikifuatiwa na namba kadhaa za mtu huyo, aliinua simu yake na kupiga namba Fulani kisha akaweka sikioni.
“Halo, yeah mimi ni secretary wa FK Security, sijui naweza kukuona kaka yangu (…), hapana we nambie nikuone wapi mi nitakuja” aliongea na simu ile na miadi ya kukutana saa kumi nambili jiono ilikuwa dhahiri kwake, kukutana na mwandishi bandia Mr Amalutwa. Moyoni mwake yule dada alikuwa na uchungu wa kupewa likizo ile maana alijua anaweza kufuatiwa na barua ya kuachishwa kazi muda wowote, lakini milioni mbili alizopewa zilikuwa zikimfariji na kumfuta machozi katika hilo.
??????
ITAENDELEA
 
Malimi TODAYS

JULAI SABA - 2

Simulizi : Julai Saba

Sehemu Ya Pili (2)

Gari aina ya Toyota V8 yenye vioo vya giza iliinga katika geti kubwa la jingo Fulani huko maeneo ya Mabibo. Vioo vyake vya tinted havikuruhusu mtu wa nje kuona kilichopo ndani ya gari hiyo, kwa mwendo wa taratibu iliegeshwa na milango yake ikafunguliwa vijana wawili na mtu mwingine wa makamo wakateremka na kuufungua mlango wa nyuma, mwanadada mmoja akateremshwa na kupelekwa ndani ya ghorofa iliyopo ndani ya wigo huo.
“Ni mwanamke mjinga sana wewe!” ilikuwa sauti ya yule mtu wa makamo aliyetambulika kwa jina la Shailan aliyekuja kuchukua nafasi ya Betram, “ Tumekulipa pesa nyingi, tumekupa mafunzo ya kujitoa mhanga, sasa umefanya nini? Unazidi kutuingiza matatizoni, kaa hapo na leo hii tunakuchinja kwa sababau wewe tayari umeshakufa” alimalizia luongea kwa jazba kubwa.
Yule msichana alisukumiwa ndani ya chumba fulani chenye giza na kufungiwa. Kisha akaketi na wenzi wake pale mezani.
“Bora mmempata, maana wangempata wao, sijui tungemwambia nini Beishal, na ameshaamuru huyu msichana auawe mara moja, kwa hiyo baadae hiyo kazi ifanyike na mwili wake mtajua mtautupa wapi”
“Lakini kwa nini tusimuache kwanza tumbane atueleze kama kuna chochote alichoongea na hawa watu, ili tujue labda tuna la kufanya” aliongea kijana mwingine.
“Lakini pia ni wazo zuri, tumbane kwanza tukishapata tunachokitaka ndiyo tummalize” aliongezea Shailan, akanyanyuka katika kiti kile alichokalia na kuelekea katika chumba kile walichomfungia yule msichana, wakaufungua mlango na kuwasha taa,
“We mwanake mjinga, uliyeahirisha kifo ulichokiuza mwenyewe sasa utakipata kwa maumivu makali” Shailan alimueleza huku akilifuta jambia lake lililokuwa liking’aa huku na huku kutoka katika ala yake.
Yule msichana alikuwa ameketi kinyonge katika kona ya chumba hicho akiwatazama wanaume wale kwa huzuni.
??????
kuhusu
FARJAH
Farjah, msichana yatima kutoka Mombasa aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu huko Mombasa, baada ya mama na baba yake kufa katika ajali mbaya ya gari, msichana huyu alibaki bila msaada huku akiwa ameachiwa wadogo zake wane wa kuwalea bila msaada wowote, akiwa katika harakati hizo alijikuta akiingia katika biashara haramu ya ukahaba ili kujipatia chochote kwa minajiri ya kusomesha na kusaidia wadogo zake kimaisha.
Siku moja usiku wa manane akiwa kwenye moja ya miahngaiko yake ndani ya club maarufu ya usiku ya ‘Mombasa by Night’ ndipo alipokutana na Shakrum Shakran ambaye alimtongoza mrembo huyo na kwenda kulala nae katika hoteli moja kubwa ambayo alifikia. Huko ndiko alikosuka mpango huo na kumshawishi Farjah kukubali mpango huo kwa malipo ya pesa nyingi sana ambazo zingeweza kusomesha wadogo zake na kuwaweka katika mazingira mazuri kwa miaka ishirini mpaka watakapoweza kujitegemea wenyewe, aliposaini pesa hiyo wadogo zake walijengewa nyumba kubwa na kuwekewa kila kitu na kulipiwa ada ya masomo yao, kisha Farjah alimuomba shangazi yake awalee wadogo zake hao wakati yeye anaenda nje ya nchi kwa muda mrefu, shangazi yake alikubali na Farjah alisafirishwa kwenda Somalia kupata mafunzo maalum ya kujitoa mhanga, mafunzo ya kutoogopa kifo, mafunzo ya kutumia bunduki za aina mbalimbali, na tayari akiwa huko alishatekeleza mashambulizi mbalimbali Somalia na Sudani, sasa alipewa kazi yake ya mwisho kuja kuifanya Tanzania maana mkataba wake ulikuwa mwishoni.
Masaa machache nyuma
Farjah alitafakari sana alipokuwa njiani kutoka Somalia kuja Tanzania, alifanya mashambulizi mengi sana ya mauaji lakini yalikuwa tofauti sana na haya anayotakiwa kufanya Tanzania.
Akiwa ameketi kwenye kochi kubwa la kisasa alionekana kuwa na mawazo mengi sana, kiasi kwamba iliwatia shaka mabosi wake.
“Farjah, mzima au?” aliuliza Shailan.
“Hapana, nipo vizuri tu” alijibu huku akiwa ameangalia chini, akitafakari kifo chake kinachofuata baada ya masaa machache.
“Farjah najua wazi kuwa una mawazo lakini wewe tayari hitima yako tumekwishaifanya, haupo duniani kama mkataba wetu ulivyo, tunakushukuru kwa kazi yote uliyotufanyia, na sasa unakwenda kumalizia na roho yako itapumzika mahali pema huko peponi” Shailan alikuwa akimwambia Farjah ambaye alionekana wazi kuvujwa jasho japo kiyoyozi cha LG kilikuwa kikitengeneza baridi kali ndani ya chumba hicho, Farjah alishusha pumzi ndefu na kujitupa kwenye kiegemeo cha sofa hilo. Mbele yake aliletewa ramani kubwa ya jengo la JM MALL.
“Ok, tazama hapa Farjah, jengo tunalolitaka ni hili, hapa ni floor ya saba, unapotoka tu katika lifti, kunja kushoto kuna milango kadhaa, utazipita ofisi zingine na wewe unatakiwa ufanye mlipuko wako ndani ya ofisi hii, pale utamkuta kijana mmoja matata sana na binti ambaye ni katibu wake, hakikisha unanionana na huyu kijana na mlipuko huu ufanyike ukiwa na huyo kijana, jihadhari huyu kijana ni mjanja sana na IQ ya hali ya hali ya juu, usipoteze muda. Mwisho wako ndiyo huo. Ole wako ulete ujinga na uzembe,” Shailan alimaliza kumuelekeza Farjah kisha akanyanyuka na kuelekea chumba fulani, Farjah akiwa katika kutafakari hili na lile mlango mwingine ulifunguliwa na kijana jalali akaingia akiwa na begi jeusi mkononi, Farjah alishtuka kumuona kijana huyu, alimfahamu, alinyanyuka na kumkumbatia kwa bashaha, Shakrum Shakran hakuwa na muda wa kukumbatia msichana, aliitazama saa yake na kuushusha ule mkono.
“Tunachelewa, vua hilo baibui lako,” ilikuwa sauti tulivu ya Shakrum, Farjah alipoisikia sauti hiyo aliikumbuka jinsi ilivyokuwa ikimbembeleza katika chumba kimoja cha hoteli huko Mombasa ikimwambia ‘vua mpenzi nataka nione umbo lako zuri, jeupe, lenye mvuto,’ lakini leo iliongea kwa mkato tu.
Farjah hakuwa na lakusema alivua lile baibui lake na kiblauzi kidogo ndani yake, chuchu zilizosimama zilikuwa zikimtazama Shakrum, kwa shida kidogo alimeza mate lakini haikuwa kazi iliyokusudiwa. Begi jeusi likafunguliwa na kitu kama mkanda kikatolewa na mbele yake kulikuwa na kitu kilichotunatuna, Shakrum akakizungusha kile kitu tumboni mwa Farjah na kuzunguka mgongoni mwake akakikutanisha na kufunga sawia kwa kutumi namba za siri (code number) ambazo ni yeye tu alikuwa akizijua. Akarudi upande wa mbele wa msichana huyu, akafungua kifuniko Fulani kidogo na kubonyeza vitufe kadhaa, mara kukawaka vinamba vilivyojiandika sifuri sifuri kama sita hivi na kutengenishwa na nukta mbili zilizobebana kila baada ya siruri mbili (colon), kisha akaseti vijinamba fulani, na alipoachia vikaanza kujihesabu, bomu la saa!
Shakrum alimwangalia usoni Farjah aliyekuwa amelowa jasho mwili mzima akitetemeka kwa hofu, akamshika kwa viganja vyake vya mikono mashavuni na kumbusu kwa kumnonya ulimi, usaliti!
“Farjah, fanya unalotakiwa kufanya na si vinginevyo” Shakrum alisema hayo na kuchukua ile baibui na kumvesha, kisha akamchukua hadi chini kulikokuwa na Prado nyeupe ikiwasubiri, wote wakaingia ndani na kuondoka eneo hilo.
˜ ˜ ˜
Katika kijibarabara cha watembea kwa miguu eneo la Buguruni Chama kuelekea Y2K bar, msichana mmoja alikuwa akitembea kwa hatua za haraka haraka huku akiangalia nyuma mara kwa mara, na kukibana kipochi chake kwa mbele, sketi fupi aliyoivaa ilimnyima uhuru wa kuongeza kasi, jioni hiyo watu wengi walikuwa katika harakati za kurudi majumbani, hivyo kijibarabara hiko kilikuwa na kazi ngumu ya kukanyagwa na ymati huo. Alipokaribia katika lango la kuingia kati ile bar, aliitoa simu yake katika pochi na kubofya namba fulani kisha akaiweka sikioni na kuonekana akiongea na mtu fulani huku akiwa hana amani kabisa, mara akairudisha simu ile na kuingia ndani ya ile bar, alipokelewa na mhudumu wa bar hiyo aliyevalia nadhifu kabisa, akamuongoza mpaka meza Fulani iliyokuwa na mtu mmoja tu, mwanaume aliyevalia kaunda suti kuukuu na kichwani akiwa na kofia aina ya pama, mezani kwake kulikuwa na safari bia iliyokua nusu na nyingine ikiwa katika bilauri. Yule msichana aliketi kwa woga akimwangalia mtu yule ambaye alihisi hajapata kumuona kabla, yule mtu akatoa kadi ya kibiashara nyingine na kumuwekea mezani, yule msichana alipoisoma jina akalikumbuka lakini mbona hafanani ndiyo swali alilojiuliza.
“Stephen Amalutwa!” alitamka kwa upole huku akiisukuma juu ile kofia yake, “Nilipata simu yako ndo maana nikakwambia tuonane hapa, ningependa kukujua kwanza kwa jina, kisha ndiyo unambie shida yako”
“Naitwa Mwada, mwadawa, naishi Magomeni Makuti nyumba namba 12C, mi nimekutafuta nikuulize kitu, ulipokuja ofisini na ulipoondoka bosi wangu kanikaripia sana kwa kukukaribisha, kisha kanipa likizo ya muda, hii hapa barua na kanilipa cheki ya millioni mbili, mi nimeshindwa kuelewa nini kimejificha” alijieleza Mwadawa
“Nafikiri mimi ningepaswa kukuuliza swali hilo, sivyo? Kama bosi wako kaupa likizo kwa kitendo cha mimi kuja kuandika habari kutoka ofsini kwenu, nini kimejificha hapo?” kamanda Amata, Stephen Amalutwa wa bandia aliligeuza lile swali, Mwadawa alitulia tuli akitafakari anachoulizwa,
“Mi kaka sijui, ninachoshangaa ni boss hatua aliyoichukua,” alijibu, Amata alimwangalia kwa jicho la chini,
“Ina maana wewe kama secretary wa ofisi hujagundua kitu tofauti siku hizi ofisini kwenu au nyendo tofauti na zile za kawaida za boss wako?” Amata alirusha swali, na ukimya ulitawala kati yao.
“Hapana zaidi ya wageni wengi wanaokuja siku hizi, ambao tunatambulishwa kuwa ni ndugu zake”
“Wageni wa namna gani?” kamanda aliuliza
“Ni hao ndugu zake, huja na kukaa hapa wiki au mwezi, wakibadilishana na kuwa na vikao visivyokwisha” alijibu Mwadawa.
Baada ya mazungumzo marefu na kamanda Amata kuridhika kiasi na majibu ya dada huyo waliagana.
“Kwa sababau umechelewa sana basi ngoja nikufikishe nyumbani” Amata alimwambia
“Oh, no acha tu bwana nitafika mwenyewe”
“Ok, take care!” Amata alimuaga Mwadawa, akabaki kasimama akimwangalia mwanadada huyo anavyopotelea nje ya bar hiyo maarufu hapo Buguruni ambayo daima huzungukwa na akina dadapoa wengi wanaofanya kuwavuta watu kufika hapo kila jua lilalapo.
Kamanda Amata, alimalizia kinywaji chake na kutoka katika bar hiyo, moja kwa moja aliiendea gari yake aina ya LandRover 110 TDI na kuingia ndani yake kisha kuelekea mitaa ya kati ya jiji la Dar es salaam, aliifuata barabara ya Uhuru mpaka katika mataa ya Karume na kukunja kushoto kuelekea Magomeni kupitia barabara ya Kawawa, pale Magomeni alinyoosha moja kwa moja na breki ilikuwa katika bar nyingine maarufu Kinondoni kwa Manyanya. Mara tu baada ya kusimamisha gari yake binti mmoja aliisogelea na kuzunguka upande wa kushoto kisha kuingia kiti cha mbele.
“Mungu anakupenda mrembo” Amata alianzisha mazungumzo
“Kwa nini wasema hivyo honey?” ilikuwa sauti tamu ya Gina, sauti inayoweza kumtoa nyoka pangoni, sauti yenye mtetemo wa kutatanisha inayoweza kukufanya kijana kupoteza network ya kichwa chako hata ukiambiwa uandike cheki ya milioni kadhaa utatii tu maana uatakosa la kufanya.
“Kwani sakata la leo hulijui? Yaani hapa nyaraka zote zimelowa huko ofisini,” Amata alieleza kisha akatulia kwa muda na kumtazama Gina, “Ungekuwa saa hii unalia mpaka unazimia maana tayari ningekuwa hata sura haijulikani, hawa jamaa ni hatari sana lazima nihakikisha nawafutilia mbali katika uso wa dunia kwa mkono wangu huu”. Ilionekana wazi hasira ya Amata ilikuwa moyoni mwake, kijana mcheshi anayependa kucheka muda wote hata na asiyemjua.
Gina alimtazama Amata usoni kisha akauweka mkono wake begani mwa kijana huyo,
“Pole!” alimtuliza.
“Ok, nipe tafutishi zetu” Amata alimwambia Gina.
Gina akatoa bahasha ndogo na kuchambua karatasi fulani Fulani na kumpatia, Amata alizichukua na kuzisoma kwa makini akatikisa kichwa kukubaliana na kilichoandikwa ndani yake.
“Shakrum!” Amata alitamka hilo jina, “Asante sana mpenzi, umefanya kazi kubwa,”
Alizikunja zile karatasi na kuziweka katika droo ya dashboard na kuwasha gari na kuondoka na binti huyo.
“Wapi Amata jamani?” Gina aliuliza huku akiuvuta mkanda wa usalama na kuufunga vizuri.
“Hapo tu mbele unisindikize, kwa chakula cha jioni”
˜ ˜ ˜
Addis in Dar, jioni hiyo watu wengi walikuwa wakiingia katika hoteli hiyo kwa mlo wa jioni, wengi walionekana na wapenzi wao wakishikana kimahaba kuingia ndani ya hotel hiyo nzuri yenye vyakula vya kuvutia vya tamaduni tofauti hasa vile vya Ethiopia. Amata alishuka garini akiongozana na Gina mpaka ghorofani na kuketi katika meza moja iliyopo katika kona ya ukumbi huo nadhifu, waliagiza vinywaji na vyakula kadhaa na kuwa wakila huku wakibadilishana mawazo.
“Gina, nisubiri hapa nakuja muda si mrefu!” alimwambia Gina
“Wapi tena Amata?” kuna rafiki yangu nina miadi naye nakuja, nipe lisaa limoja tafadhali” akanyanyuka na kumpa funguo za gari na kumuacha hela za kulipia chakula kisha yeye akateremka chini na kuondoka. Kwa hatua za harakaharaka aliifuata barabara ya Ursino kuelekea upande wa barabara ya Bagamoyo, aliikatisha na kupita mbele ya Kanisa la Kristo kisha akakunja kulia na kusimama karibu na mti wa mnazi ambaye ulilingana naye kimo, alitazama huku na huko hakuona dalili ya mtu, tayari ilitimu saa tano usiku, alitembea tena haraka haraka na kulipita geti lililosomeka FK Security na kuzunguka upande wa nyuma wa ukuta wa uzio, aliangali kama kuna usalama wowote akaona hamna shida, kwa kutumia mti wa mwarobaini ulioota upande huo aliukwea na kufika juu ya ukuta huo mrefu kisha kujirusha ndani na kutua kwa utulivu kwenye ardhi tifutifu, kishindo hafifiu kilimfanya mlinzi wa upande huo kusogea, Amata alitulia kwa mtindo uleule na kumsubiri, alipomkaribia kwa haraka aliruka na kumpiga karate moja ya nyuma ya shingo kisha kumdaka na kumshusha chini taratibu na kumvutia karibu na pipa la takataka, akamuhifadhi hapo na kuvuta hatua kwenda upande wa pili, pale alikuta magari kadhaa yamewekwa na mojawapo likiwa gari kubwa la zimamoto ndani yake kulikuwa na watu sita waliojilaza, akanyata taratibu akatoa mfukoni kichupa chake kidogo chenye dawa kali ya usingizi iliyochanganywa na dawa ya Halcion na kupuliza kwa kupitia dirishani, haikupita sekunde kumi wote walikuwa hoi kwa usingizi, Amata akauendea mlango mmoja ulio pembeni mwa jingo hilo na kutia funguo yake maalum mlango ule ulikubali na kufunguka, akaingia ndani na kuurudishia nyuma yake, kisha akaiendea korido ndefu kidogo yenye milango michache lakni yeye aliuchagua ule uliondika Director na kuutomasa kidogo kwa funguo zake ukafunguka akaingia ndani.
Aliiangalia ile ofisi nadhifu ambayo mchana wake tu alikuwa pale, kwa tahadhali aliizunguka na kuketi juu ya kiti kile cha bwana Scolleti, akaanza kuvuta droo moja baada ya nyingine huku akisaidiwa na tochi yake ndogo mfano wa peni yenye mwanga unaomulika pale tu upatakapo. Alipofungua kabati alikaribishwa na mafaili mengi sana ila alivutiwa na moja tu, akalishusha na kuliweka mezani kisha kuchambua nyaraka moja baada ya nyingine na hii ilimvutia, kadi za gari, sasa uongo ulijulikana. Kamanda Amata aligundua wazi kuwa lile lori la zimamoto lililotumika kumuokoa yule binti lilikuwa ni lao, walichokifanya ni kuibadilisha namba ya usajili, alipoendelea kuichunguza ile namba ya usajili akagundua kuwa ni namba ya Toyota Premio, Amata akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameridhika kwa hilo, alitoa mashine yake ndogo yenye uwezo mkubwa wa kutoa photocopy, mashine ambayo huweza hata kuiweka katika mfuko wa shati na usiijue, akatoa vivuli vya kadi zile na kuzihifadhi vyema kisha akarudisha lile kabrasha mahala pake. Akavuta hatua kuliendea kabati lingine na kutoa faili lililoandikwa ‘ Wageni’ ndani yake kulikuwa na faili moja tu lililolazwa kana kwamba limesahaulika mle ndani, alilivuta na kuliweka mezani, akalifungua, kopi za hati za kusafiria zilikuwa humo za watu ambao labda atawahitaji wakati Fulani, nazo alifanya vilevile. Akavuta hatua za tahadhari kuuelekea mlango lakini kitu kilimvutia, kabla hajatoka, katika chano moja iliyoandikwa IN kulikuwa na kijimemo kidogo, akakirudia na kukinyanyua, ilikuwa ni miadi tu ‘Tuonane saa tisa alasiri kesho, White Sand hotel’ kisha kufuatiwa na namba Fulani ya simu. Amata aliirudisha ile kadi mahali pake na kuuendea mlango kisha kutoka na kuufunga nyuma yake.
Alitoka nje taratibu kwa kufuata njia ileile, alipofika kwenye ule mlango wa kutokea kwenye ule uwanja alisikia mngurumo wa gari kubwa na watu wakiwa wanazungumza, akawasikiliza kwa makini.
“Wamesema kulekule Kunduchi” sauti moja ilisema.
“Kunduchi ni mbali kwa nini isiwe jirani tu, si kesho wataokota” sauti nyingine ilijibu, kisha ule mlango ukafunguliwa, Amata akajibanza kwa nyuma yake, vijana wawili wenye sare ya kisecurity wakashuka na kuchukua kitu kama mfuko wa saruji na kutoka wakisaidiana huku na huku.
“Aaa hapo safi, kesho mtainjoy jioni,” ilisema sauti ingine ikifuatiwa na sauti ya lile gari iliyoonesha wazi kuwa dereva alikuwa amekanyaga pedeli ya mafuta, kutoka pale alipo, kwa kasi alaijitupa chini na kujiviringa mpaka uvungu wa lile lori, ijapokuwa kulikuwa na walinzi eneo lile kwa muda huo lakini hakuwa aliyemuhisi, sembuse kumuona. Amata alijishikia vizuri sana kwenye chuma imara cha chessis huku akiwa mbali kidogo na lile propeller Shaft lililokuwa likizunguka kwa kasi. Ile lori ikatoka getini na kuiendea barabara ya New Bagamoyo, wakati likijiandaa kuingia barabara kubwa Amata alitoka na kuliacha liende peke yake.
Akajinyanyua pale alipojitupia na kujikung’uta vumbi na nyasi kavu zilizonasa mwilini.
˜ ˜ ˜
3
Asubuhi ilofuata
Kikombe cha chai kilishindikana kufikishwa kinywani mwa Madam S wakati macho yalipogongana na habari ya kipolisi kuwa mwili wa mwanamke mmoja mwenye asili ya Kihabesh umeokotwa kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi huko maeneo ya Kunduchi. Kisha picha kadhaa zilipitishwa kwenye luninga, na wakaomba kama kuna mtu aliyepotelewa na ndugu yake basi akautambue mwili huo katika chumba cha maiti pale Muhimbili.
Madam S, aliendelea kunywa chai huku akisikiliza watu wanaohojiwa juu ya tukio hilo, kwake yeye halikuwa na uzito sana kwani mara nyingi imetokea matukia kama hayo kusikika, labda tu watu wameuana kwa wivu wa mapenzi, hivyo hakufuatilia lolote. ‘Kazi za kipolisi’, alijiwazia.
Aliinuka kitini na kukusanya vifaa vyake kisha kuondoka kuelekea kazini, kama kawaida alikuwa kwenye foleni ndefu ya magari ya kuingia barabara ya Ally Hassan Mwinyi ili aelekee upande wa Posta, alifungua redio na kusikia tena habari ile ile aliyoiacha kwenye televishen, lakini katika redio hii kitu fulani kilimvutia, habari iliyosema kuwa marehemu ametupwa usiku uliotangulia na watu wasiojulikana. Alijaribu kuchanganya kichwa kama kuna lolote muhimu kwake lakini hakuona hilo, aliendelea na safari yake.
Mwananyamala hospitali
“YEAH, huu ni mwili wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na miaka 25 hadi 30, ameuawa kwa kuvunjwa shingo,” Dr Semeni alikuwa akimueleza Amata aliyekuja kujua kilichojiri juu ya mwili ule uliookotwa kule Kunduchi Beach siku hiyo asubuhi. Aliufunua ile shuka iliyofunikwa mwili mzima na kuruhusu uso kuwa wazi, akatingisha kichwa kuashiria ameelewa kitu.
“Vipi?” Dr Semeni aliuliza.
“Hapana, nimekubaliana na uchunguzi wako” Amata alijibu. Amata aliugundua mwili ule, mwili wa msichana aliyekuja na bomu jana yake pale katika jengo la JM MALL kwa minajiri ya kujilipua, tena ofisini kwa Amata. ‘Inaonekana wamemuua baada ya kushindwa kutekeleza lile jaribio,’ alijiwazia Amata, huku akiandika andika katika kitabu chake cha kumbukumbu.
˜ ˜ ˜
“Mheshimiwa Rais ametuachia hilo jukumu sisi, kama tunaona ni vyema kumuachia huyu jamaa au la!” waziri wa ulinzi aliongea huku akiwaangalia mjumbe mmoja mmoja katika kikao hicho waliokaa kwa mtindo wa nusu duara, wakiwa katika majadiliano hayo na utayari wa kuandaa remove order, mara mlango ulifunguliwa na Amata akawa amesimama nyuma ya wale wajumbe wengine akitazamana na waziri uso kwa uso, wajumbe wote waligeuka nyuma kumtazama kijana huyu aliyeingia hapo bila kualikwa. Madam S alimtazama kijana wake kwa macho makali sana.
“Amata! Unafanya nini hapa, kikao hakikuhusu,” madam S aliongea huku akiinuka kitini kumkabili Amata.
“Mnisamehe kwa kuingia ghafla lakini imebidi nifanye hivyo kwani ningechelewa kidogo tu mngefanya kile nisichokitaka” Amata alizungumza kwa kujiamini.
“Kipi hicho?” waziri aliuliza.
“Swala la kumuachia huru Jegran Grashan, siliungi mkono hata kidogo, najua mna nia nzuri, lakini mimi naona mkifanya hivyo mtakuwa mmeharibu sana na watu watawashangaa kwa hatua hiyo, mimi suing mkono hata kama sina uwezo wa kuwazuia kufanya maamuzi yenu” Amata aliongea kwa hasira iliyomfanya kila mtu kutulia, “Wenyewe mnajua nilivyompata kwa shida hata kuhatarisha maisha yangu, halafu aachiwe kirahisi namna hiyo! Haiwezekani, kumuacha yule tutakuwa tumeonesha udhaifu mkubwa sana wa kiutendaji katika ngazi ya kiusalama. Sitakubaliani na hilo, yule akae ndani kama ilivyo sasa na hawa washirika wake ndiyo tutawapata kiurahisi, kitendo cha kumuachia ni kuwaweka mbali maadui zetu, sikubaliani na mnalotaka kufanya,” Amata alimaliza na kutoka ofisini mle kisha kuufunga mlango nyuma yake. Aliingia katika gari yake na kuketi nyuma ya usukani akionekana wazi kupoteza network kiasi Fulani.
Mara kioo cha dirisha la upande wake kikagongwa, alipogeuka akagongana macho kwa macho na madam S, walitazamana kwa nukta kadhaa kisha Amata akashusha kioo.
“Nione Ofisini,” Madam S akaongea kwa kifupi na kuielekea gari yake. Amata akawasha gari yake na kuondoka eneo lile.
Baada ya dakika kadhaa alikuwa tayari ofisini mwa madam S akiwa ameketi kwa mtindo wa kutazamana na mwanamama huyu, mkuu wake wa kazi.
“Umefanya nini Amata?” madam S aliuliza, “Unadiriki kuingia katika kikao kama kile bila idhini yoyote! Amata,”
“Ilibidi iwe hivyo kwani nilijua mnalolizungumzia mimi nalipinga kadiri ya mwenendo wa kazi hii” Amata alimjibu.
“Hukutakiwa kufanya vile, kwa nini hukusubiri kikao kiishe, kisha utoe rufani yako?”
“Isingewezekana ukizingatia nyote mliokuwa pale tayari mlikuwa na adhma moja tu, kumuacha huru Jegran, mimi hilo siwezi kulivumilia, nilimpata kwa tabu sana yule mtu, kumbuka mwenyewe madam jinsi ile kazi ilivyokuwa ngumu…”
Miaka minne iliyopita …
“HATA kama nimejeruhiwa, hakika siwezi kumuachia hayawani huyu aondoke aende akadhuru watu wengine, sambaza picha yake mipakani na mijini labda tutapata fununu juu yake,” Amata alizungumza kwa uchungu huku machozi yakimtiririka, mkono wake wa kushoto ulikuwa ukivuja damu baada ya kujeruhiwa na risasi na kusababisha jeraha katia nyama zake za juu ya kiwiko, lakini uzuri ni kuwa hakuna mfupa uliovunjika.
“Pole kamanda” Madam S alimpa pole huku akimwangalia kwa huzuni pale kitandani alipokuwa akipata tiba.
Baada ya kila kitu kukamilika, kamanda Amata na madam S walitoka hospitalini hapo na kurudi mjini, jua lilikuwa tayari likiuacha mji wa Dar es salaam na kupotelea Maghalibi kama ilivyo desturi mji ulianza kuchangamka wengine wakirudi nyumbani ilhali wengine wakiingia mjini kuanza kazi zao haramu na halali.
“Kumpata huyu jamaa ipo kazi kamanda” madam S alizungumza.
“Yeah, ni kazi ngumu sana lakini lazima tumpate, na atapatikana tu” alijibu kamanda Amata.
“Unafikiri tufanye nini ili tumtie mkononi?”
“Kwanza kabisa mpaka sasa sitegemei kama yupo Dar, kwa vyovyote atakuwa ameshatoka mji huu ili kutaka kukimbia”
“Ni ngumu, makachero wengi tumewasambaza katika sehemu muhimu ili kumnasa ama yeye au aliyefanana naye”
“Tutumaini, jamaa alitaka kufanya kitu kibaya sana pale uwanja wa ndege, tumshukuru Mungu niliwahi kuokoa lakini sasa hivi tungeongea mengine.” Amata alisema
“Ah, kwa kweli unastahili pongezi” madama S alimpongeza Amata
“Aah, tuwapongeze wale waliotufahamisha kuhusu Jegan kuwa pale, maana alijua wazi kuwa tumebana kila kona hivyo atumie njia ya kawaida kuondoka, ka kujibadili sura yake kiasi fulani”
Masaa machache yaliyopita
Uwanja wa ndege wa kimataifa Dar es salaam, DIA
JASMINE aliinua kichwa chake kumtazama mtu aliyekuwa mbele yake, alipata shaka na hati yake ya kusafiria, alimtazama kwa makini usoni kisha akarudisha macho katika hati ile, mashaka.
Aliichukua ile hati na kumkabidhi mwenzake aliaitazame upya.
“Samahani subiri pale kwenye kiti,” alimwambia mtu yule aliyekuwa na mandevu mengi kidevuni mwake. Yule mtu aliketi kitini na kuuweka mfuko wake wa plastiki pembeni yake, akisubiri kuona kinachojiri.
“Mh! Hii hati mbona yanitia mashaka?” mtumishi mwingine wa idara ya Uhamiaji alimuuliza Jasmine.
“Ndiyo maana nikakupa” Jasmine alijibu. Yule bwana akaiweka kwenye mtambo maalum na kuifanyia scan kisha akamrudishia le Hati Jasmine.
“Samahani kwa kukuchelewesha, tulikuwa tunaikagua kidogo hati yako, wakati mwingine unapoingia nchini kumbuka kupata kibali (visa) cha muda mrefu, maana hapa inaonekana kibali chako kimeisha tangu juzi,” Jasmine alimueleza yule bwana mwenye mandevu kisha akampa hati yake na kumruhusu kuendelea na utaratibu mwingine baada ya kumgongea mihuri kadhaa, kilichomshangaza juu ya huyu Bwana alikuwa haongei wala hajibu chochote isipokuwa kukutazama tu kwa macho yake mekundu.
Baada ya kuiscan ile hati, aliichukua kielektroniki ile picha ya mtu huyo na kuingiza kwenye mtandao maalum wa usalama wa taifa unaoweza kuitambua sura yoyote ya mtu na kukupa taarifa zake. Chiba akiwa nyuma ya kompyuta yake maalum kwa kazi hiyo, safari hii akiwa ndani ya sare za ofisa uhamiaji pale uwanja wa ndege alitulia tuli, akisubiri ule mtandao ufanye kazi huku akimtazama yule mtu asipotee machoni mwake.
Mlio fulani ulisikika kwenye kompyuta yake na alipoitazama, kwenye kioo kulikuwa na picha mbili, ile aliyoiscan na pembeni yake kulikuwa na nyingine iliyoletwa kwa msaada wa mtandao na maelezo kadhaa chini yake.
Jegan Grashan, mzaliwa wa Yemen; kisha zikafuatili tarehe za kuzaliwa na maelezo mengine mengi, lakini katika ile hati kulikuwa na maelezo tofauti kabisa. Jasmine aliitilia shaka kutokana na mihuri ya kibali chake cha kuwapo nchini ilifanana sana na ile ya idara ya uhamiaji isipokuwa kitu kimoja kidogo sana ambacho kwa raia wa kawaida huwezi kukitambua hakikuonekana katika mihuri ile.
Chiba alibofya vitufe Fulani kwenye hiyo kompyuta yake kisha akaandika ujumbe na kuutuma mahali. Alinyanyuka kutoka alipoketi na kuiweka tayari bastola yake kicha kuipachika katika mkanda wake wa suruali na kujitupia koti lake la buluu liliofunika vyema bastola ile.
˜ ˜ ˜
Akiwa kitandani na msichana mrembo, Kumbuka, kamanda Amata alikuwa akiendelea na shughuli hiyo nyeti ambayo haistahili kusimuliwa mbele ya watoto, alikuwa akitoa miguno iliyochnganyika na sauti nyembamba ya mahaba yaliyosindikizwa na raha kutoka kwa msichana huyu aliyeonekana wazi kuipagawisha roho ya Amata mchana huo wa jua kali katika hoteli fulani hapo Dar.
Kumbuka alimsukumia upande wa pili Amata na kujinasua katika mikono ya dume hilo lililokuwa bado likiendeleza libeneke wakati mwenzake alikuwa amekwishamaliza mizunguko yake. Kamanda Amata alitulia kitandani akimwangalia Kumbuka alipokuwa akikimbilia bafuni huku nyama zake za nyuma zikitisika kwa mpangilio hadimu ambao huwezi kuuona kirahisi kama hukumpembua mavazi binti huyu wa kihehe. Akiwa katika butwaa hilo mara saa yake ilimfinya kwa meno maalum yaliyo chini ya mfuniko. Akabofya kitu fulani na kutulia, mara mkanda mdogo ukatoka katika ile saa, Amata aliusoma ujumbe uliokuwamo katika kijimkanda hicho.
‘Mzigo wetu upo hapa Airport, njoo haraka, Tena Sana Aisee’
Amata, alikurupuka kitandani na kukimbilia bafuni, alijiswafi haraka haraka na kuvaa nguo zake.
“We vipi mbona hueleweki?” ilikuwa ni sauti ya Kumbuka, akimuuliza Amata wakati akiwa kwenye harakati hizo.
“Nitakutafuta baadae kuna dharula hospitalini” alimdanganya. Alipomaliza kujiweka tayri alitoka na kumuachia noti zenye thamani ya elfu hamsini kisha yeye kuliendea gari lake na kupotelea.
Madam S nae alikuwa njiani kuelekea hapo sambamba na kamanda Amata. Dakika chache Amata aliingia uwanja wa ndege na kuiwiweka maegeshoni gari yake, ulinzi tayari uliimarishwa na askari waliovaa kiraia, madam S naye aliteremka na kuongoza moja kwa moja katika mlango wa kuingilia wasafiri wenye kibao kilichoandikwa ‘Departure’.
“Geti namba 38” sauti ya Chiba ilifika masikioni mwa madam S aliyeonekana kuwa kikazi zaidi, tayari alikwishavuka huo mlango na kusimama mahali Fulani akipepesa macho yake huku na kule, kwa mbali alimuona Amata naye akiwa amebana kwenye kona Fulani.
“Chiba! Nenda pale alipoketi mwambie kuwa hati yake ya kusafiria ina mashaka kisha akikufuata tumtie nguvuni” Amata alimwambia Chiba kwa kutumia saa yake maalum inayoweza kusafirisha ujumbe wa sauti.
“Amata, nipe mpango wako!” Madam S alipeleka ujumbe wa sauti ka Amata.
“Chiba atakwenda kumueleza kuwa hati yake ina shida hivyo amfuate ofisini, kisha tutambana huko, najua lolote linaweza kutokea madam, watu wameshakaa kila kona kwa tahadhari” Amata alimjibu madam S.
“Ok, kamanda nakuaminia, hakikisha hasitoroke mshenzi huyo” madam S alimaliza kuongea kwa kutumia ile saa yake na kujiweka tayari. Amata akiwa kona ya upande wa pili aliweza kuona kila kinachoendelea.
Jegan Grashan alikuwa ameketi huku akisoma gazeti la Daily News, alionekana kutokuwa na utulivu maana kila wakati alikuwa akiiangalia saa yake. Chiba alivuta hatua ndogondogo mpaka pale alipoketi Jegan na kusimama mbele yake.
“Mheshimiwa!” Chiba aliita, na Jegan aliinua uso wake kumuangalia, “Samahani kwa usumbufu kuna tatizo dogo kwenye hati yako ya kusafiria, naomba unifuate ili tukairekebishe.” Jegan alimtazama Chiba kwa tuo,
“Mimi?” alimuuliza
“Ee ndiyo wewe bwana Hassanail Hussein” Chiba aliongeza na kumtaja kwa jina alilotumia katika hati yake. Jegan, gaidi la kimataifa, lilianza kuhisi harufu mbaya ya hatari, alitazama huku na huku na kwa mbali alimuona Amata amejibanza kwenye kona Fulani, akamtambua akaona hatari na janja inayotumika. Jegan alimkazia macho Chiba na Chiba akafanya vivyo hivyo huku akizisoma hisia za gaidi huyo, Chiba aliona wazi kuwa sasa kazi imeamka kazi ambayo hakuitarajia alitamanai Kamanda Amata awe jirani. Amata aliona kila kitu na akamtupia signal madam S, taarifa zikafika kwa wanausalama wa nje ya uwanja kujiweka tayari kwa lolote muda wowote.
“Ok twende,” Jegan alijibu, kisha akanyanyuka na kuongoza, hatua chache alimuona Amata akitoka kwenye ile kona aliyosimama. Jegan akasimama na kujifanya anafunga kamba ya kiatu, teke moja la nyuma lilimtoka na kumpepesua Chiba ambaye alienda chini bila pingamizi, kelele za wasafiri zikaamsha vurugu kwenye chumba cha kusubiria safari, Chiba alinyanyuka na kuchomoa bastola yake.
“Freeze!!!” alipiga kelele, lakini Jegan alijirusha kwa ustadi na kutua juu ya ngazi za umeme zilizokuwa zikielekea chini.
“Watu wote lala chini !” sauti ya Amata ilisikika na kila aliye ndani ya ukumbi ule alijitupa sakafuni. Polisi mmoja alimjia mbele Jegan, kosa. Jegan aliruka sarakasi na kutua miguu yake kifuani mwa polisi huyo na kumpeleka chini huku bunduki yake aina ya SMG ikimtoka kiurahisi mikononi na kudondokea pembeni, alipotaka kunyanyuka teke moja kali lilitua shavuni na kumvunja taya, Jegana sasa alikuwa na ile bunduki mikononi mwake, akaiondoa usalama tayari kwa mashambulizi.
‘Mambo yashaharibika’ Amata alijisemea akiwa anaelekea kule kwenye mapigano. Jegan alifyatua risasi kadhaa hewani na watu wote walitulia chini, alipoona Amata anamkaribia alimuinua mama mmoja wa Kihindi na kumuweka ngao.
“Ukiniletea shida namuua huyu mama” Jegan alimueleza Amata aliyekuwa kasimama mbele yake tayari na bastola mkononi. Jegan aliididimiza mtutu wa ile bunduki kwenye shingo ya yule mama, “weka silaha yako chini” alimuamuru Amata, Amata akaiweka chini bastola yake, “Vizuri, sasa isukumie kwangu kwa kutumia mguu wako” alitoa amri nyingine, Amata akatii na kuipiga kwa teke ile bastola nayo ikaseleleka kumuelekea Jegan, Jegan alimsukuma yule mama na kuiwahi ile bastola baada ya kufyatua magazine ya SMG na kutengeanisha na ile bunduki, alipogeuka kwenda uapande wa pili, alikutana na ngumi nzito toka kwa Chiba, kabla hajakaa sawa Chiba aliruka double kick na kumfanya ayumbe, wakati huo tayari Amata alikuwa jirani, Jegan alipanda ngazi haraka kuelekea upande wa juu akageuka na kufyatua risasi moja iliyotawanya vyoo kila upande,
“Kamanda…!!!!” ilikuwa sauti ya madam S, Amata aligeuka upande ule na kumuona madam S akimrushia bastola, Amata akaidaka kwa ustadi na kugeuka upande alipo Jegan hakumuona, kwa hatua za kunyata alipanda ngazi kuelekea juu na kufika tena pale kwenye sehemu ya kusubiria wasafiri, alisimama kwa utulivu akitazama huku na huku, ‘Uko wapi hayawani?’ alijiuliza mwenyewe huku akitembeza bastola yake huku na kule. Amata alijikuta akipigwa karate moja kali kutoka nyuma yake, akajirusha sarakasi na kutua mbele kama hatua tatu hivi kisha kugeuka kumkabili adui, aliruka juu na kuichanua miguu yake kwa mtindo wa kujizungusha na kumpata sawia Jegan ambaye hakutetereka bali alisimama kidete akamsubiri Amata kutua sakafuni, kama alivyotarajia, Amata alitua kwa mguu mmoja lakini kabla hajakaa sawa, Jegan alipiga teke kali na kuufyatua ule mguu, sasa Amata alianguka vibaya sakafuni lakini alipotua tu naye alipiga teke moja sehemu ya nyuma ya magoti na kumfanya Jegan apige magoti, teke la pili lilitua usoni na kumfanya aanguke chali. Amata alijinyanyua na kumuendea huku Chiba na madam S nao wakija kwa kasi, Jegan alinyanyuka na kumpiga dafrao Amata kisha kwa kasi ya ajabu alikimbi na kujirusha kwenye kioo kikubwa na kutoka nje huku milio na risasi vikimfuati kwa kasi lakini havikufanikiwa, Jegan alikuwa tayari nje ya jingo chini kabisa na kukimbia kuelekea pande za Kipawa, walinzi wa nje walipata wakati mgumu kumkamata haikuwezekana.
Amata alibaki kasimama huku kajishika kiuno pembeni yake madam S akionekana wazi kukasirika kwa kumkosa hayawani huyo. Amata alisonya na kuelekea pale kwenye lile tundu kubwa la kioo alipopitia Jegan.
“Amkeni, poleni kwa usumbufu” madam S aliwaambia abiria. Kisha akifuatana na kamanda Amata na Chiba waliteremka ngazi mpaka nje ya jengo hilo ambapo walikuta polisi wakiwa kwenye kibarua kizito cha kumsaka Jegan wakiwa na mbwa maalum kwa kazi hiyo.
Katikati ya vichaka vya eneo hilo ambalo wakazi wake walikwishahamishwa ili kupisha upanuzi wa uwanja huo mbwa wote waliishia kwenye kiatu kilichokuwa hapo, hawakuendelea zaidi, Jegan hayupo….
Rejea ofisini kwa Madam S
“Sasa mtu kama huyo kweli, ee! Madam, tumuachie? Watanzania takriban saba wamepoteza maisha pale ubalozini mwaka ule, na Wakenya zaidi ya mia mbili, hapana mkimuachia mi namuua, naapa!” Amata alimwambia madam S, akasimama na kutaka kuondoka.
“Kamanda hebu rudi kwanza hapa!” madam S alimuita, Anata akarudi na kusimama akimtazama boss wake, kisha madam S akaendelea, “Unalosema ni sahihi, lakini we unafikiri tufanyeje? Kwa maana hata mheshimiwa amelibariki hilo.”
“Sikatai, lakini si kwamba tumeshindwa kuliangamiza hili genge?” Amata aliuliza
“Hilo niachie mimi, nitaongea na wadau tuone njia mbadala,” Madam alimpoza jazba Amata. Amata akatoka nje na kuiacha ofisi ya madam S akiwa mwenye mawazo mengi sana.
˜ ˜ ˜
Aliingia kwenye gari yake na moja kwa moja alielekea ofisini kwake pale kwenye jingo la JM MALL, aliegesha gari na kuteremka, huku na huku aliangalia usalama na kuufunga mlango kisha kuingia ndani kupitia mlango mkubwa wa mbele, mlango wenye watu wengi wanaoingia na kutoka kwa kuwa ndani yake kulikuwa na supermarket kubwa ya Shoprite, alipiga hatua chache na kutulia kusubiri lift ya kumpeleka ghorofa ingine ambamo ofisi yake ilikuwamo, alifika na kubonyeza kengele kwa mtindo ule waliowekeana na Gina, mlango ulifunguliwa na akaingia moja kwa moja akaenda kujitupa katika kiti chake akiwa mwenye mawazo lukuki, Gina kama kawaida yake, aliandaa kahawa ya kiitaliano inayojulikana kama ‘Capucino’ na kumpelekea pale mezani,
“Karibu kamanda” alimkaribisha huku akitoa tabasamu pana lililomrudishia nguvu Amata,
“Asante mrembo, ndiyo maana nilikuajiri ofisini kwangu” alimsifia huku akijiweka sawa kitini, na kumkaribisha Gina kiti cha pili yake, kisha akatoa camera yake ndogo na kuiwasha sehemu ya kuangalia picha zilizokwishapigwa ambazo zimehifadhiwa humo, akachagua akachukua na waya wake wa USB na kuuchomeka kutoka kwenye camera mpaka kwenye kompyuta yake, sekunde chache zile picha zikaanza kuonekana pale katika kioo cha kompyuta.
“Gina, unamjua huyu?” Amata alimuuliza Gina, Gina alikodoa macho kuangalia ile picha, picha ya mtu asiye na uhai, mwana dada mweupe mwenye nywele ndefu zilizoijaza machela ya chuma ya chumba cha kuhifadhia maiti cha Mwananyamala.
“Hapana, simfahamu” Gina alijibu
“Huyu ndiye aliyekuja hapa kufanya ule mlipuko, lilikuwa bomu hai,”
“Umempataje hadi kumuua?” Gina alisaili
“Hapana, sijamuua, wamemuua wenyewe, unajua hii ni mikataba, unapokwenda kujitoa mhanga maana yake wameshakulipa na wameshakuwekea matanga kwamba wewe nai marehemu hivyo uende ukaue na wewe ufe ukohuko, sasa huyu inaonekana kafeli hivyo wamemuua, wamemnyonga shingo” Amata aliposema hayo alimuona Gina akisisimka mwili.
“Watu wabaya!” Gina aliongea
“Sio kidogo!” Amata akaongeza, aliinua kikombe chake na kunywa ile kahawa kisha akakishusha n kujiweka vyema kitini.
“Nipe mrejesho, maana tangu juzi ile hatujakaa kuongea, nilikupa kazi, unakumbuka?” Amata aliuliza.
“Nakumbuka sana, nitakuwa sekretari gani kama nasahau kazi ninazopewa na boss?!” aliuliza kwa kejeli
“Na utakuwa mke gani kama utakuwa unasahau majukumu unayopewa na mumeo?” kisha wote wakacheka. Gina akanyanyuka na kuiendea meza yake na kuivuta saraka, akatoa kabrasha moja na kuja nalo pale mezani, akalifungua na kumpa karatasi moja Amata, aliipokea na kuisoma kwa makini.
“Ok! Gina nakupa kazi ingine, nenda ofisi ya Idara ya uhamiaji pale makao makuu waulizie jina hili Shakrum Shakran, yuko nchini kwa shughuli gani na wakupe anuani ya wapi kafikia,” Gina alitikisa kichwa kuwa amekubali, lakini kabla hajaondoka, “Gina, tafadhali usitumie simu, sawa?”
“Sawa Bro,” alijibu kisha akarudi katika meza yake na kufungafunga, akahakikisha anakariri lile jina kichwani kisha akaaga na kuondoka, Amata akaendelea kufanya kazi zilizopo kwa wakati huo ikiwa ni kupanga mipango mabalimbali ya kuhakikisha anamaliza mchakato huo mapema ili ikiwezeka akamsaidie Chiba huko China kwenye sakata lile la Watanzania waliokamatwa na madawa ya kulevya na kuchafua jina la nchi hii tukufu yenye unono wa maziwa na asali.
WHITE SAND HOTEL
KIJUA cha alasiri kilikuwa kinaendelea kuchoma ardhi katika mchanga wa pwani ya White Sand, kila mtu alikuwa na hamsini zake, wengine wakiogelea, wengine wakipata vinywaji, wengine wakicheza mpira wa mikono kwenye mchanga ilimradi tu kwamba kila mtu alikuwa na shughuli ya kufanya.
Mawimbi makali yalikuwa yakipiga huku na huko, hali ile watoto wa Kihindi waliifuarahia sana na iliwafanya hata wengine kutoka katika madimbwi ya kuogelea na kukimbilia huko baharini wakiwa na furaha ya ajabu.
Kamanda Amata, aliibuka kutoka katikati ya mawimbi makali akiwa ni mmoja na wale waogeleao kwa furaha, kwa hatua za kujivuta kidogo alijaribu kupingana na maji ya bahari huku akielekea pwani akiwa ndani ya bukta ya kuogelea, mwili wake ulioonekana wazi sehemu kubwa uliwavuta watoto wengi kumshangaa jinsi alivyojaza misuli kimazoezi na kujijenga mwili mithili ya ‘Daniel Craig’, alitoka mpaka pwani akasimama kidogo na kuangalia huku na huku kisha akakatiza katika ule mchanga kuiendea meza moja iliyo chini ya msonge maridadi, pale palikuwa na msichana mmoja wa kihindi ameketi akijisomea kitabu cha riwaya ‘ISABEL’ kilichoonekana kumkuna kwelikweli, Amata hakumuacha msichana huyu hapo, lakini alishangaa kumkuta ameketi pale bila wasiwasi wowote, Amata alichukua taulo lake na lilitengenezwa kwa mfano wa koti na kulivaa,
“Waoh!” yule msichana alitoa mshangao.
“Vipi mbona unashangaa?” Amata alimuuliza
“Aaaa, mmmm! Umejazia mbaba mpaka napata..”
“Unapata nini?” Amata alimkatisha, yule msichana wa kihindi akaita mhudumu na kuagiza juice mbili, mara zikaja, akachukua glass moja na kumpa nyingine Amata, Amata alitupa jicho la wizi kwa msichana huyu hasa kiuno chake kilichojengeka vyema na makalio ya kubinuka kidogo, ‘Huyu Mhindi au Mbantu?’ alijiuliza,
“Cheers!” alitamka yule msichana huku akigonga glass yake na ile ya Amata zikalia nge! Yule mdada akapiga funda, Amata alipokaribia mdomoni mara alimuona Gina kafika na kusimama katikati yao, Gina akaichukua ile glass na kuirudisha mezani, kisha akamgeukia yule msichana wa Kihindi na kumsonya,
“Mxiuuuuu! Acha waume za watu,” kisha akamvuta mkono Amata na kuongozana nae upande wa malocker maalum ya kuhifadhi nguo na vifaa vingine kabla hujaenda kuogelea, akamgeuza Amata mbele yake na kumuoneshea ishara ya kimya yaani kidole chake cha shahada akakiweka kukatisha midomo yake, “Shhhhhhhh!!!!!!, ile juice ina sumu Amata, ungekunywa tu umekwisha” Gina alimwambia.
“Asante sana, Malaika wangu mlinzi, umefikaje hapa na umejuaje niko hapa?” Amata aliuliza.
“Usichezee mtoto wa kike wewe!” nilijua wazi huku kunaweza kuwa na hatari ndiyo maana nikaja kukuchunga. Gina alimuachia Amata, wakatazamana, “Nipo ghorofa ya juu kwenye ukumbi wa chakula, nenda kaendelee na mpenzi wako” Gina alipokwishakusema hayo akageuka kuondoka, Amata akamdaka mkono kabla hajafika mbali,
“Gina, njoo, upo na nani?”
“Nipo mwenyewe tu, usijali swahiba nakulinda,” akafungua pochi yake kumuonesha ndani mlikuwa na bastola mbili zilijoaa vizuri na magazine nyingine tatu za akiba, “Hapa kitanuka Amata, utaniona mi nani leo, lete ujinga na huyo Malaya wako.” Gina akaondoka akamuachia Amata kifaa maalum cha kunasa sauti kati yao wawili.
Dakika tano zilikuwa nyingi, kamanda Amata akawa ndani ya suti nadhifu ya kijivu iliyotanguliwa na shati la buluu bahari safari hii hakuweka tai aliuruhusu upepo wa pwani upite kwenye shingo yake na kuingia mpaka kifuani. Kwa hatua za kibrotherman alitembea kuielekea tena meza ileile akiwa na shauku ya kujua ni nani yule mrembo na alikuwa akitaka nini kwake, aliifikia ile meza, peupe! Hakuna mtu, mezani kulibaki na juice glass moja na ile nyingine ipo nusu, kitabu cha riwaya ‘ISABEL’ alichokuwa akisoma yule dada kilikuwa kimefunguliwa kurasa Fulani na kulaziwa kisu juu yake, kwenye ile kurasa kulikuwa na tone moja la damu na sentensi Fulani ilipigiwa mstari kwa wino mwekundu, akaisoma harakaharaka iliandikwa
…“Kamwe hamtoweza kufisha juhudi za kimataifa, mpango huu umesukwa na kusukika”…
…“Mimi ni mwanamapinduzi halisi, nipo hapa kwa kazi moja tu ya kuondoka na roho yako”…
Kamanda Amata akatoa kifaa chake cha mawasiliano na kupachika earphone sikioni mwake,
“Umewahiwa kijana” sauti ya Gina ilimnong’oneza
“Kaelekea wapi?” Amata aliuliza lakini kwa kuwa alikuwa akipigwa na upepo mkali wa bahari alijisika sikio ili asikilizane vizuri na anayeongea naye,
“Amata!, toa mkono sikioni haraka” sauti ya Gina ilimkaripia, Amata akashusha mkono wake na kubaki hajui afanye nini.
hiyo Gina binti Komba Zingazinga, akiwa ghorofa ya juu katika ukumbi wa chakula wa hoteli aliweza kuona matukio mengi yanayoendelea pale chini akiwa kavaa miwani yake maalu yenye auto focus ambayo si yo rahisi mtu mwingine kujua, pindi unapotua jicho kwenye kitu Fulani na kutulia miwani ile iliweza kukisogeza karibu uweze kukiona kwa usahihi zaidi. Gina aliiba miwani hii ofisini mwa Amata pindi tu aliporudi na kutomkuta ofisini alijua wazi kuwa atakuwa ameelekea White Sand kwani alimpa habari hiyo tangu usiku uliopita kuwa atafanya hivyo ili akajue nini na nani wanakutana, Gina alishaona hali hiyo ya hatari, hivyo alimua kufuatilia kwa mbali ili kumsaidia boss wake inapowezekana, alifika pale hotelini na moja kwa moja akapanda ghorofa ya juu na kutega mambo yake huko.
“Geuka nyuma uketi kiti cha upande huo!” Gina akamueleza, Amata akatii akageuka na kuketi, alipotazama mbele akamuona Scolleti akiwa amekaa kitini peke yake akijisomea gazeti, Amata aliitazama saa yake, ilikuwa imetimu saa tisa kasoro dakika kumi, aliishusha na kujituliza, alimwita mhudumu na kumuagiza soda baridi lakini kabla akamuomba aondoe vile vitu pale mezani.
Soda ilipokuja akawa anakunywa taratibu, mara kutoka lango kuu akaona gari moja aina ya Toyota V8 nyeupe ikiingia na kusimama jirani kabisa na banda lile aliloketi Scolleti watu wawili wakashuka. Mara hiyo muuza magazeti alipita jirani na Amata, akamwita na kununua gazeti Mwananchi na kuliafungua kisha kuanza kusoma lakini bado aliweza kuona kinachoendelea. Watu wawili walioteremka katika ile prado waliielekea ile meza ya Scolleti na kusalimiana kabla ya kuketi. Shakran Shakrum alikuwa amefuatana pamoja na Shailan boss wake. Amata alikuwa akiwatazama tu na kuhakikisha wasije kumtoroka, mara kwa mbali alimuona binti yule wa Kihindi akitokea kwenye bwawa la kuogelea akiwa na nguo za kuogelea, Amata alimtaza kwa shauku na kusahau kilichomleta, msichana yule alitembea kwa madaha akipita mchangani mpaka pale alipoketi Amata, akageuka na kumpa mgongo Amata, “Mmmm, magnificent view” Amata alitamka, yule msichana akageuka na kutoa tabasamu la wizi na kuchukua taulo lake kama lile la Amata na kulivaa, kisha akageuka na kutoka eneo lile,
“Shiiiit!” sauti ya Gina ilimgutua Amata alipotazama pale mezani hakuona mtu, wameondoka.
“Gina, wameelekea wapi?”
“Sijui, mi nilikuwa nakuangali wewe na huyo Malaya wako nageuza macho siwaoni” Gina akajibu.
“Ok, shuka twende, hapa si salama tena” Amata akiwa katika kuongea hilo, Nissan cedric ya kijivu ilipita mbele yake na kufunga breki kali kama mita ishirini hivi, watu wawili wenye sox zilizoficha nyuso zao wakachomoza kama umeme na kumdaka yule dada wa kihindi na kumvutia ndani ya gari kisha ile Nissan ikatoka kwa kasi na kusugua ile barabara kwa nguvu, Amata aliichomoa bastora yake na kujaribu shabaha, risasi ya kwanza ilivunja kioo cha nyuma, ya pili ikalikosa tairi, lo tayari ilikwishachukua barabara ya kuelekea barabara kubwa ya Bagamoyo, Amata alikimbilia pale alipoegesha gari yake na kuingia ndani akafunga mkanda, na kuitia moto kabla ya kuiweka barabarani, na kuondoka kwa kasi,
“Amataaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!” Gina aliita kwa sauti kali, Amata alifunga breki kali na Gina aliingia kwa kupitia dirishani kisha gari ilitolewa kasi huku watu wakishuhudia miguu ya Gina ikimalizikia kuingia ndani ya gari ile. Wakiwa karibu na barabara kubwa ya kuelekea Bagamoyo, aliiona ile Nissan ikisaga lami kuelekea upande wa Bagamoyo, Amata naey akaingia barabarani na kuzifanya daladala kupiga honi ovyo, akakunja kulia na kuifukuza kwa kasi, barabara ilikuwa nyembamba kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kuwafikia, Gina alikuwa ameketi nyuma akiwa ametulia tuli kwa woga akiangalia jinsi kamanda anavyofanya ovateki za hatari huku akiacha ajali nyingi nyuma yake.
“Kamanda polepole” Gina alipiga kelele
Kamanda Amata kama hakumsikia, bastola mkono wa kulia, usukani mkono wa kushoto, ngoma ipo 110 Km/h, baada ya dakika kadhaa alikipita kiwanda cha saruji cha Wazo na kuipita Tegeta, sasa walibaki wawili tu barabarani mwendo mkali wakielekea Boko. Ile Nissan ilikuwa ikienda kasi sana kiasi kwamba Amata aliona wazi hatoweza kuipata, akamtazama Gina kwenye kioo cha ndani akamuona kajikunyata kama kifaranga cha kuku.
“Gina! Njoo uendeshe hapa nimalizie kazi!” alimwita
“No! kamanda mi siwezi,” Gina alijibu kwa kelele
“Come on, Gina, njoo haraka” Amata alipiga kelele huku akipigapiga usukani wa gari ile. Gina alipita katikati ya viti huku gari ikiwa kasi sana, Amata alhamia kiti cha abiria huku mkono mmoja wa kulia sasa ukiwa umeshika usukani, Gina alipenya chini ya mkono wa Amata na kuketi nyuma ya usukani na kuikamata gari ile barabara kabisa.
“Uuuuuuuuuuuuiiiiiiiiiiiiiii Kamandaaaaaa!!!!!!” Gina alipiga kelele baada ya Amata kumuachia usukani alijikuta akishindwa kuimudu na gari ile ikayumba vibaya kisha akairudisha barabarani. Amata akavuta saraka katika dashboard ya gari yake na kutoa sortgun aina ya Double Barrel na kuivunja katikati, ndivyo inavyowekwa risasi hivyo jamani, akatumbukiza risasi mbili, kwa maana aina hii ya short gun inabomba mbili na lazima uweke risasi mbili na unapopiga hutoka zote mbili. Kamanda Amata alipohakikisha ameiweka vizuri akarukiti cha nyuma na kutokeza dirisha la kulia nyuma akitanguliza ule mtutu, kichwa nje alibana jicho moja sawia na kulitafuta tairi la ile Nissan, alipohakikisha lipo kwenye shabaha, alipotaka kufyatua trigger tayari kupiga, alihisi gari yao ikiyumba nakisha ikazunguka mchoro wa S, barabara yote ikitoa harufu ya mipira na kusimama ikiangalia ilikotoka, katikati ya barabara. Kamanda Amata aliangukia kwenye kiti cha nyuma na kukaa, damu zilikuwa zikimtoka pembeni kidogo ya pua yake, shortgun yake ikiwa mapajani.
“Gina umefanya nini sasa? Tumepoteza nafasi nzuri sana ya kutegua kitendewili chetu” Amata alimueleza Gina amabaye alikuwa anatetemeka kama mgonjwa mwenye homa kali, “Gina, Gina!” Amata aliita na alipojinyanyua kuangalia kule kwa Gina, “Shiiiiiiit!!!!”….
Nyoka mkubwa aina ya black mamba alikuwa akitoka chini ya kiti cha dereva na taratibu akawaakijizungusha karibu na mguu wa Gina, Kamanda Amata alimtazama huku akiuma meno, aliichomoa bastola yake na kumlenga sawia na kukifumua kichwa chake, risasi ile ilisambarataisha kichwa cha nyoka yule. Gina alishusha pumzi na kufungua mlango, akatoka nje akiwa hajiamini. Kamanda Aamata alitoka na kwa kutumia mtutu wa ile shotgun kamtoa nje yule nyoka, alikua nyoka mkubwa sana, kisha akavaa miwani yake na kuchungulia chini ya kiti kimoja baada ya kingine na kuhakikisha hakuna hatari yoyote.
“Washenzi sana, saa ngapi walituwekea huyu nyoka?” alijisemea huku akiizunguka gari yake na kutoa sonyo refu kisha akamuendea Gina aliyekuwa bado kasimama hajielewi, akamshika mkono na kumvutia upande wa pili, “Pole mrembo, panda twende,” alimsihi na kisha kumfungulia mlango, naye akaingia upande wa dereva kisha akageuza gari na kurudi mjini.

˜ ˜ ˜

“Siku ya nne sasa inaisha, deni letu kwa serikali linabakia siku tatu, mnafikiri watatekeleza ombi letu?” Shailan aliwaeleza wenzake.
“Hata kama siku zimebaki tatu, tena tuseme mbili kwa sababu hii ya nne inaisha, bado tuendelee kuwasubiri kwa maana hatujui wana lengo gani.” Shakrum akajibu.
“Hata hivyo, lazima tuanze kuandaa mazingira ya shambulizi la mwisho, shambulizi baya kuliko yote ambalo dunia lazima itetemeke kwa hofu na Afrika iishi kwa wasiwasi, wakati Tanzania itajutia uamuzi wake,” Shailan alimjibu Shakrum.
Scollet muda wote alikuwa akiwasikiliza, alikuwa kimya kabisa kama mtu ambaye hayupo pale, kisha kama aliyegutushwa kutoka usingizini, “Sasa mnataka kufanya nini?” aliuliza.
“Hilo kwa sasa hatuwezi kuzungumzia kwa sababu kuna mawili, maana hili jukumu inabidi limalizwe Julai 7 na mtu wetu awe mikononi kwa njia yoyote ile, lakini kama watakuwa na shingo ngumu kama ya Firauni basi watajua sisi ni nani, kesho watapata ujume wao wa mwisho,” Shailan alimalizia kauli yake, alikuwa akiongea kwa jazba sana wakiwa wamesimama pwani karibu kabisa na bahari ya mti kwenye mchanga mweupe wa White Sand Hotel baada ya kuhama pale walipokuwa wameketi kwanza baada ya kupewa taarifa ya kujihami na walinzi wao waliokuwa eneo lile.
“Itabidi tuombe silaha mbili za kutumia kwa mara nyingine, silaha hai,” Shakram alimwambia Shailan.
“Yeah, huo ndiyo mpango!”
Mazungumzo ya watatu hawa yaliendelea kwa takriban nusu saa kisha wakiwa kulekule pwani, boti moja ndogo ilikuja na kusimama umbali kama wa mita hamsini, wote wakaingia majini na kuingia kwenye hiyo boti kisha wakaondoka zao eneo lile. Walifanya hivyo kadiri ya maelekezo ya walinzi wao waliowaweka pale tangu mapema kuangali kama kuna lolote baya juu yao, hivyo wakawashauri waondoke kutumia usafiri wa maji kwani hakuna usalama barabarani kwa wakati ule, hivyo waliliacha gari lao pale kwa minajiri ya kuja watu maalumu kwa kazi hiyo na kuliondoa eneo lile.
Shakrum, alichukua simu yake ya upepo na kubofya kitufe Fulani, “Vipi mzigo umefika salama?”
“Yeah, umefika salama japokuwa tulipata msindikizaji njiani” alijibiwa.
“Msindikizaji?! Mliweza kumng’amua hakuwaletea shida?” Shakrum aliuliza
“Yeah, na kama si mbinu aliyotumia Staina saa hizi tungeongea mengine,”
“Atakuwa nani huyo?”
“Nafikiri ni kachero wa serikali”
Shakrum alishusha simu yake na kupumua kwa nguvu, Shailan alimtazama na kumtupia swali, “Vipi?”
“Jamaa wanasema walipata msindikizaji njiani,” Shailan alishtuka kidogo kwa jibu hilo. Mpaka dakika hiyo hawakugundua uwepo wa Amata eneo lile hivyo wao walizitazama hatari nyingine tu.
˜ ˜ ˜
Geti kubwa lilifunguliwa na gari ndogo aina ya Subaru iliingia taratibu ndani ya yadi hii kubwa iliyosheheni malori ya mafuta yasiyopungua mia moja, gari ile iliegeshwa pembeni na milango yake kufunguliwa, vijana wane walishuka na msichana yule wa Kihindi,
“Huku tafadhali,” mmoja aliwaongoza, na wengine wakafuatia wakiwa wamemshika yule mwanamke uku na huku ijapokuwa walimfunga kamba za katani mikono yake. Walitembea nae mpaka kwenye jengo lingine lililoonekana kutumiwa kama ofisi, wakaingia na kumtupia yule dada wa Kihindi na kumfunsia ndani ya kijichumba fulani.
“Aaah, Mungu mkubwa, sikutegemea kama tutafika salama,” mmoja wao aliyekuwa ndiye dereva aliwaambia wenzake, aliliendea jokofu kubwa lililokuwa katika ofisi hiyo ndogo na kuchukua konyagi ndogo kisha akaifungua na kupiga funda moja na kuirudisha jokofuni.
4
KAMANDA Amata alijitupa kwenye kochi kubwa na kuvuta chupa ya maji iliyokuwa mezani na kuigugumia yote kama mtu aliyetoka jangwani na kuteseka kwa jua na vumbi.
“Gina, unaendeleaje?” alimuuliza Gina aliyekuwa hoi katika kochi lingine upande wa pili.
“Sijiamini kama nimefika hapa salama, Amata naogopa sana nyoka, leo sijui kama ntaweza kulala nyumbani peke yangu” alijibu.
“Usijali utalala hapa kwangu kama shida ni uoga, angalau hata jiko langu leo liwashwe” kisha wote wakacheka.
“Gina, asante kwa kuniokoa, hivi yule mwanamke wa Kihindi ni nani?”
Gina badala ya kujibu akacheka kwanza na kumtazama Amata usoni.
“Amata, siku yako ya kufa utakuwa umelala na mwanamke kitandani, maana ndiyo udhaifu wako huo. Ile juice haikuwa na sumu ni mimi tu nilitaka uwe makini na lililokupeleka na siyo kufuatilia wanawake wa watu,” Gina alijibu. Amata akasonya na kujiweka vizuri, “Na we ulikujaje kule?”
“Ha, mi si ni secretary wako, lazima nijue uendako na nikuandalie kila kinachotakiwa ikiwamo usalama. We mwenyewe ulinambia kuwa utaenda kule kwa sababu hizi, lakini sikuweza kutulia kwa kuwa naona wivu, wanawake wengine wakafaidi na mi nipo hapa nakula kwa macho. Nikatangulia, nikachukua tax na kuja kisha nikaketi juu ghorofani nikiangalia mazingira, tangu unaingia nilikuona na kila ulichofanya, ulipokwenda kuogelea ndipo yule mwanamke wa Kihindi alikuja pale ulipoketi kwanza, ulipoacha taulo lako naye akaketi. Kiukweli sijui alikuja wakati gain na ni nani lakini nilimuona pindi tu alipokuja pale ulipoketi. Mwanzoni nilijua wamekuwekea mtego ndiyo ulikuwa wasiwasi wangu lakini nimeshangaa kwa nini wale jamaa wamemteka tena, ina maana si mwenzao?” Gina alieleza na kuuliza.
“Mi sijui, maana nimeona wakiondoka nae, ndiyo maana niliwafukuza ili niujue ukweli,” Amata alijibu na kubaki kimya kwa muda.
Mara pale kwenye kochi simu ya Amata ikaanza kuita kwa fujo, akaangalia namba haijui, akatulia na kuiacha, baada ya muda meseji ikaingia, akaichukua nakuisoma
‘…Natafutwa, nafuatiliwa na watu nisiowajua, naomba msaada… Mwad…”
Kamanda Amata akashusha pumzi na kuisoma tena ile meseji, kisha akampa simu Gina naye akasoma.
“Nani huyo?” akauliza Gina
Amata akamsimulia Gina kisa chote cha msichana Mwadawa, tangu walipokutana pale ofisini na kisha kuachishwa kazi.
“Mh! Itakuwa wanamuwinda sana” Gina alijibu.
Kamanda Amata alijaribu kuipigia ile namba lakini mara ya kwanza haikupatikana, alipojaribu mara kadhaa aliipata na kuongea naye. Mwadawa alikuwa akiongea kwa sauti ya chini.
“Bwana Stephen, nipo matatizoni unisaidie tafadhali” sauti ya Mwadawa ilisema
“Uko wapi sasa?” Amata (Stephen wa bandia) aliuliza.
“Nimejificha huku Kariakoo shimoni” alijibu
“Ok, subiri hapo nakuja” alimueleza, “ Gina twende,”
“Aah we nenda mwenyewe, saa hizi muda wa kazi umeisha” Gina aliongea na kucheka.
Kamanda Amata alijiweka tayari bastola zake mbili kiunoni, akaenda stoo na kuchukua pikipiki lake kubwa kisha kutokomea mjini.
******
MTAA wa Tandamti ulikuwa na shughuli nyingi kama kawaida yake, watu wengi wakubwa kwa wadogo walionekana wakitafuta hiki na kile, magari ya lioegeshwa bila mpangilio yalisababisha msongamano na kufanya mtaa ule kuwa vigumu kupita, achilia mbali wale walioweka bidhaa zao chini nao walileta tabu kwa watumia njia hiyo.
Kamanda Amata aliiacha barabara ya Msimbazi na kuchukua ile ya Swahili kuelekea soko kuu la Kariakoo, kwa mwendo wa wastani alipita huku akingalia huku na kule, watu walilishangaa sana pikipiki lile na jinsi lilivompendeza muendeshaji wake, punde kidogo alisimama mbela ya posta ndogo karibu na kituo cha daladala za Mwenge, akatulia kidogo akijaribu kupanga na kupangua ili ajue aanzie wapi. Aliitazama saa yake, muda ulikuwa unamtupa mkono, akaondoa pikipiki lake na kuzunguka upande wa pili wa soko hilo kubwa mpaka pale kwenye foleni ya malori yanayosubiri kuingia shimoni ili kushusha mazao yaliyobeba kutoka mikoani na sehemu mbalimbali za nchi, akachukua simu yake na kubonya namba Fulani Fulani kisha akaiweka sikioni,
“…yeah, niko hapa kwenye lango la kuingilia magari, njoo utanikuta…” kisha akatega sikio kusikia sauti ya upande wa pili,
“…naogopa kutoka wananifuata…” alijibiwa
“…njoo nakusubiri hapa hakuna lolote litakalotokea…” alimhakikishia usalama kisha akasubiri pale nje bila kushuka kwenye lile pikipiki lake.
Mwadawa Said alitokeza taratibu kwenye lile lango na kuanza kupandisha kuelekea huko yalikopaki yale malori. Kamanda Amata alitulia pembeni mwa lori mojawapo akiwa bado kavalia ile kofia ngumu na mikono ikiwa mfukoni akiangalia wote watokao na waingiao, kwa mbali alimuona yule binti akiwa anakuja kwa mwendo wa uwoga uwoga, alipokaribia kumaliza lile lango vijana wawili walitokea kwa nyuma yake na kumfuata taratibu, walizidi kumkaribia, kabla Mwadawa hajamaliza ule muinuko wa ile njia kuyafikia yale malori wale vijana walimshika mmoja mmoja mkono huu na mwingine mkono mwingine kisha wakbadili uelekeo na kupita kati ya malori yaliyokuwa yameegeshwa hapo.

ITAENDELEA
 
Ahahahaha na watu wasio julikana KWANI HAUKO KWENYE GRP langu la wasap?
 
kuku mweus JULAI SABA - 3

Simulizi : Julai Saba

Sehemu Ya Tatu (3)

Kamanda Amata alizunguka upande wa nyuma wa malori yale na kupita kati yake, uso kwa uso akiwa anatazamana na wale vijana walikuwa wakielekea kukutana kati ya malori yale. Hatua kama tano hivi walikutana katikati, Amata alisimama, na wale vijana walifanya vivyo hivyo, akakisukuma juu kioo kilichozuia macho yake cha lile kofia gumu la kuendeshea pikipiki, akawatazama wale vijana waliomshika Mwadawa, wakabaki wakitazamana na hakuna aliyeongea kati yao, Kamanda Amata akawaoneshea ishara kuwa wamuachie yule msichana, lakini amri hiyo hakuna aliyeitii badala yake wakageuka naye na kurudi walikotoka, mara nyuma yao wakasikia mlio wa bastola inayoondolewa usalama tayari kwa kazi, wakageuka na kutazamana na domo la bastola iliyofungwa kiwambo cha sauti ikiwa kwenye mikono imara ya Amata, bastola yenyewe, sura ya aliyeishika vyote viwili havikuonekana kuwa na masihara hata kidogo, hawakuwa na ujanja, walijikuta mikono yao ikilegea na kumuachia yule msichana, Mwadawa akatoka kwa hatua za haraka na kujificha nyuma yake, bado wakiwa katikati ya malori yale hakuna mtu yoyote eneo lile aliyejua kinachoendelea, Amata hakuona haja ya kuanzisha timbwili katika eneo lile kwa kuwa kungeweza kuleta madhara kwa Watanzania wengi ambao amani imewafanya wajinga hata kupenda kushangaa matukio ya hatari kama hayo kana kwamba wanaangalia sinema. Alimchukua Mwadawa, na bastola yake mkononi na kugeuka kuanza kuondoka huku akionesha kuwa hajali nyuma kuna nini, wale viajana walimtazama mpaka alipoishia katika yale malori akiwa na windo lao.
Mwendo wa dakika kumi na tano, Kamanda Amata alimfikisha Mwadawa nyumbani kwake, na kumkuta Gina amekwishaandaa chakula, akawakaribisha na wote wakaketi vitini.
“Asante Stephen,” ilikuwa ni sauti ya Mwadawa iliyoongea katika hali ya kutojiamini.
“Karibu sana, hebu nambie hawa jamaa wamekufuata tangu lini?” Kamnda aliuliza, wakati huo alikuwa ameiwasha simu yake yenye uwezo wa kurekodi sauti.
“Jana jioni niliwaona watu hawa karibu na nyumba ninayoishi, lakini sikuwafuatilia ijapokuwa walikuwa eneo lile karibu siku nzima, leo asubuhi nilikuwa nina shughuli zangu mjini ndipo nilipowaona kila ninapokwenda mpaka mchana huu nilipoona sasa hali inakuwa zaidi, walijaribu kunikamata mara mbili lakini nikawa nawakwepa kwa kujichanganya na makundi ya watu, mara ya mwisho hii nilijifanya nanunua matunda pale soko dogo nikawaona mmoja kushoto na mwingine kulia, nikaondoka nikakimbilia kule shimoni, nikaikumbuka kadi yako ulonipa ndo nikakupigia.” Mwadawa alieleza. “Kabla ya hapa uliwahi kuwaona hawa watu?” lilikuwa swali lingine zuri kutoka kwa Amata.
“Kwa kweli hapana sijawahi kuwaona kabisa,” alijibu mwadawa.
“Ok, hebu leo niambie ukweli bila kuficha, kampuni yenu ya ulinzi na matukio ya milipuko ya mabomu vina uhusiano wowote?”
“Aah kwa kweli bwana Stephen, mi sina uhakika sana, ila tu siku ile ulipokuja ofisini nilisikia jambo moja likiongelewa ambalo lilinitia wasiwasi,” aliposema hayo Amata akajiweka vizuri, “Enhe, jambo gain hilo?” aliuliza.
“Nilisikia wakiongelea sana lile jengo la JM MALL kwa sababu mimi nilikuwa nawapelekea chain a kahawa kule ofisini nilikuwa nasikia hilo pia walikuwa na ramani nahisi ni ya jengo hilo,” Mwadawa alieleza kwa kusitasita, Amata akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu nyingine aina ya Nokia Lumia na kufungua sehemu ya picha, “Huyu unamjua?” ilikuwa ni picha ya msichana aliyeonekana kama chotara wa kiarabu na kiswahili, Mwadawa aliichukua ile simu na kuangalia vizuri, akawa kama anajaribu kumgusa mwanadada huyo pichani, “Niambie unamjua?” swali la Amata lilimshtua Mwadawa, “Ndiyo namjua, nilimuona siku moja kabla yaw ewe kuja ofisini, alikuja pale ofisini kwetu akiongozana na kijana mmoja wa kiarabu lakini ni raia wa Kazakhistan,” alijibu kwa ufasaha.
“Ok, unaweza kunambia ana uhusiano na boss wako bwana Scolleti?”
“Bwana Scolleti, alinitambulisha hawa watu wote kuwa ni business partiners wake kutoka mbali, hivyo wana vikao vya kubadilishana mawazo juu ya biashara zao,” Mwadawa alieleza. Kamanda Amata akaichukua ile simu na kutafuta picha ingine akamuonesha Mwadawa, “Huyu unamjua?” lilikuwa swali lingine kwa Mwadawa.
“Uuuuuuhhhhh!!!! Yeah, si ndiyo yule dada au?” alijibu kwa swali na kushusha pumzi ndefu. Amata akaizima ile simu na kuiweka mfukoni mwake, akajiweka vizuri pale alipoketi.
“Ameokotwa amekufa jana, una habari na hilo?” Amata alimuuliza Mwadawa ambaye alijibu kwa kutikisa kichwa chake kushoto kulia kwamba hajui chochote, kisha akabaki ameduwaa, na mara machozi yakaanza kumdondoka.
“Unalia nini?” Amata aliuliza
“Dah, Stephan, huyu dada wakati anaondoka pale na wale vijana alinipa noti ya dollar mia moja ya Kimarekani akanambia, hatutaonana tena hela hii itakuwa kumbukumbu yako na msaada mkubwa kwa watakaohitaji, akanikabidhi na kuondoka,” Mwadawa aliangusha machozi ya haja kwa kilio. Kamanda Amata akainuka kutoka alikoketi kwenda kwenye kikabati kidogo na kutoka na kitu kama kitambaa laini akampatia Mwadawa kwa ajili ya kufuta machozi yake. Amata akatazamana na Gina aliyekuwa ameketi pembeni akijinywea coca cola yake huku akingali runinga kubwa iliyokuwa mbele yake. Baada ya kunyamaza kulia kule wote watatu walienda mezani na kupata chakula cha mchana, lakini Amata bado alikuwa kaidadisi huku na kule.
“Boss wako Scolleti, ana biashara gain au kampuni ngapi?”
“Kwa hapa Tanzania ana huu mradi wa zimamoto na pia ana kampuni kubwa ya kusambaza mafuta, ananunua mafuta Uarabuni na kuyaleta hapa, ana tanker zake zaidi ya mia mbili zinapeleka karibu nchi zote za SADC”
“Du, amejiimarisha kweli, na yard yake ipo wapi?” Amata aliendelea kuchimbachimba
“Yadi moja ipo pale External Mabibo karibu na hostel za chuo kikuu, lakini ile ni ndogo, kubwa kabisa ambayo pia ina matank makubwa ya mafuta ipo Bunju njia ya Bagamoyo, pale ndiyo kila kitu”
“HARAKATI za ukombozi zinaendelea huko duniani na tunaamini ndani ya masaa sabini na mbili yajayo utakuwa huru ijapokuwa bado wamekaakimya hadi sasa” Mtu mmoja wa makamo alikuwa amesimama upande wa pili wa nondo za gereza akiongea na Jegan Grashan kwa lugha ambayo watu waliokuwa hapo hawakuelewa.
“Itapendeza kuona taifa letu linakuwa huru dhidi ya utawala wa kibeberu wa Maghalibi, wao ni nani hata watake kuitawala dunia, ndugu piganeni kwa nguvu zote, na siku ya kiyama mtapata thawabu yenu, mimi nimepigana kadiri ya uwezo wangu na sasa niko hapa gerezani ila naamini wazi kuwa nitakuwa huru na nitaendelea na mapambano mpaka tulikomboe taifa nyonge ambalo Wamaghalibi hawataki kuliona duniani, Mungu mkubwa ndugu,” Jegan aliongea kwa hisia huku akiwa ameishika mikono ya ndugu yake huyo aliyeonekana kuwa ni mtu wa makamo kwa jinsi uso wake ulivyoonekana ukiwa na mikunjo michache na ngozi iliyoanza kuchoka kwa mbali.
“Usichoke kuomba, ndugu zako tutapigana mpaka mwisho,” alimalizia mazungumzo yake na kuziachia zile nondo, alipopiga hatua kadhaa alisimama na kugeuka nyuma kumwangali ndugu yake huyo Jegan Grashan ambaye pamoja na kukimbia katika mikono ya vyombo vya usalama nchi mbalimbali za dunia hatimaye alijikuta akinasa katika idara makini ya usalama ya Tanzania, idara isiyofanya mzaha kwenye kazi kama hiz, ikiongozwa na viongozi makini na ikifanya kazi na watu makini walio makini katika mambo yanayohitaji umakini. Ijapokuwa mara ya kwanza alijaribu kutoroka pale JNIA (Julius Nyerere International Airport) lakini mwisho wa yote alitiwa mkononi na vikosi mahiri vya usalama hapo Handeni Tanga akiwa mbioni kutoroka nchini shida ilikuwa ni jinsi gani ya kuvuka mpaka kwa maana kila uchochoro ulidhibitiwa kuhakikisha kiumbe huyu hatari asiye na chembe ya huruma hatoki nchini labda ageuke njiwa au upepo. Kila mtu alikuwa makini na kitengo chake mpaka pale walipopata fununu kutoka Mkoa wa Tanga kuwa inasadikiwa gaidi huyo amejichimbia huko.

*>>>>>Rudi Miaka Mitatu nyuma>>>>>Handeni Tanga
BAADA ya msako na uchunguzi mkali wa makachero wa serikali, takribani ya mwaka mmoja iliwachukua kupata fununu kuwa Jegran Grashan alikuwa huko Tanga katika eneo la Handeni, kwenye moja ya nyumba ambayo inasadikiwa huwa hakuna mtu anayeishi isipokuwa hutumiwa kama stoo ya kuhifadhia makorokoro kutoka katika kiwanda cha mkonge. Iliposadikiwa hilo mmoja wa makachero ambaye alipanga chumba eneo hilo la makazi ya watu ila ni mbali kidogo na lile shamba la mkonge ambako kunai le stoo tajwa. Baada ya kuishi eneo hilo na kuzoeleka na waenyeji alianza kufuatilia kwa umakini wote juu ya lile eneo na kuchukua kila kilichokuwa kikiongelewa kwenye vijiwe vya vijana au vilabu vya pombe, mara kadhaa amekuwa akienda kule shambani kwa ajili ya kujipatia kibarua cha siku moja au mbili, mara nyingine alipata na mara nyingine hakupata. Ndipo wakati Fulani zilipotangazwa nafasi za vibarua wenye ujuzi, naye alijitokeza akiwa na ujuzi wa kuendesha trekta, Mungu si Athumani akajipatia kazi ile na hapo ndipo alipoanza kwa umakini juu ya kazi yake iliyompeleka pale.
Siku moja alipangwa kupeleka takataka huko katika ile stoo, kwake ilikuwa ni nafasi nzuri kwake. Kijana huyu ambaye daima aliizowesha jamii kuwa yeye ni mpenda miwani siku hiyo kama kawaida alikuwa na miwani yake nzuri, daima alipokuwa kazini miwani ile aliivua na kuiweka mahala ili aweze kufanya kazi zake, hata mabosi wake wale maburushi walimzoea kwa hilo. Ilikuwa ni mchana kama wa saa nane hivi alipoegesha treat lake karibu kabisa na mlango wa ile stoo, wale vibarua alokuwa nao wakafungua geti naye akaingiza lile trela la trekta kisha akashuka na kuingia mle ndani kwa minajiri ya kuwasidia wale wenzake kushusha zile takataka, akaivua miwani yake na kuiweka juu kwenye kidirisha Fulani ambacho kilitazamana na mlango mmoja ulioonekana katika jumba hilo. Baada ya kushusha takataka zote walionsoka na kurudi kazini. Muda ulipotimu wakafunga kazi na kuondoka, akiwa tayari keshaliacha lile eneo na wenzake akajifanya kukumbuka miwani yake, kwa kweli alionekana kuchanganyikiwa kwa namna moja au nyingine lakini walimpoza kuwa asijali siku ya pili ataiona miwani hiyo.
Siku iliyofuata…
KAMA kawaida vibarua waliingia kazini na jambo la kwanza yule kijana aliivua miwani nyingine aliyoivaa siku hiyo, hakuonesha kujali juu ya ile miwani aliyoiacha kule. Ilipotimu saa nane kama kawaida alikuwa juu ya trekta na wenzake wakienda kule stoo, walipofika jambo la kwanz ayule kijana akaiendea miwani yake nakuikuta kama ilivyo akaichukua na kuwaonesha wenzake kuwa ameikuta salama, kila mtu alifurahi. Baada ya kila kitu kumalizika walirudi kazini na kufunga ofisi kisha kutawanyika kila mmoja na anakoishi. Yule kijana aliketi chumbani kwake na akiwa kajifungia mlango, akaichukua ile miwani na kubetua kioo kimoja ambacho kilitoka katika ile fremu yake, akamisnya sehemu Fulani palepale alipotoa kioo kile na mara memori kadi ndogo ikatoka, akaichomoa na kuchukua dvcam yake kisha akaipachika ile kadi na kuwasha ile dvcam, sekunde kadhaa ikaonekana kwenye kile kioo kidogo picha ya watu watatu walioingia eneo lile jioni wakiwa na bunduki nzito zilizosheheni risasi, waliongea mambo mengi ambayo yote yalisikika vyema katika mashine ile, watu wale watatu aliwatambua vyema kwa kuwa mara nyingi aliwaona hata pale kiwandani, picha ikaendelea, mtu wa nne alionekana kuongezeka baada ya kama nusu saa ya ile picha kuendelea, huyu hakumjua, alimzoom mara kadhaa lakini sura yake haikuonekana vizuri kutokana na mwanga hafifu wa mbala mwezi, wasiwasi ulimjaa na kuamini maneno ya watu kuwa ndani ya stoo ile kuna watu wanaishi. Tafutishi yake ya pili ilimpa jibu sahihi la kuwa kuna mtu zaidi ya walinzi hujumuika usiku, lakini bado hakuwa na uhakika ni nani mtu huyo, taarifa hizo zenye kila dalili ya mafanikio zilifika makao makuu ya idara ya usalama wa Taifa, Kamanda Amata aliyekuwa akifuatilia na ndiye aliyemtuma kijana yule mbichi kabisa katika kazi hiyo alifurahi kuona majibu anayoyapata kuwa yalikuwa na uelekeo chanya.
Jegan Grashan, mara baada ya kutoroka pale uwanja wa ndege mwaka mmoja uliopita, na kuwaacha Kamanda Amata, Madam S na Chiba hoi alipotelea mitaa ya Kujichanganya na wakazi wa eneo hilo waliokuwa kwenye pilikapilika nyingi, hakuna aliyemtilia shaka kwani utulivu wake ulikuwa na ngao tosha ya kujifunika, alikodi tax na ikampeleka moja kwa moja mpaka Posta kwenye bandari ndogo ya Zanziba na kuiwahi boti iliyokuwa inaondoka muda huo, wakati taarifa zinasambazwa kubana kila mahali tayari ile boti ilikuwa kilomita moja kutoka kwenye gati hiyo, Jegan Grashan aliiona Dar es salaam ikizidi kuwa ndogo na mara ikamezwa na maji ya bahari, baada ya dakika tisini ile boti ya Sea Express ilikuwa tayari ikiingia katika bandari ya Zanzibar, akiwa kama gaidi mzoefu alielewa wazi kuwa lazima pale langoni kutakuwa na ulinzi wa kumnasa, hivyo aliposhuka tu hakupita katika mlango mkuu bali alishuka na kuyaelekea madau yaliyoegeshwa mahali hapo na kukodi moja limpeleke Pemba, kutokana na pesa aliyolipa dau lile lilimpeleka mpaka Pemba usiku huo, masaa nane yaliisha wakiwa baharini kwenye mawimbi na dhoruba kali, Jegan Grasha alikaa Pemba kwa muda mfupi na kuondoka kwa dau lingine mpaka Tanga alipopokelewa na swahiba zake ambao walikuwa wkijua kila kinachoendelea na wakaja kumuhifadhi hapo wakimpatia kila kitu, walinzi waliokuwa wakiendelea kulinda stoo ile kubwa walielewa mchezo mzima, na daima walipoketi walikuwa wakijua kuwa mtu huyo anatafutwa hivyo walimshauri akae hapo kwa muda mpaka mambo yatakapotulia kumbe hawakujua kuwa kimya kingi kina mshindo mkuu.
Katika idara ya utambuzi ya usalama wa Taifa, Picha zilizopigwa na ile camera ya kisasa iliyofungwa katika miwani aliyokuwa akiitumia yule kijana zilifanyiwa uchunguzi wa hali ya juu katika vifaa vya kisasa kabisa vilivyoweza kufananisha picha za mtu zaidi ya mia moja na baada ya kufanya utafiti huo uliochukua takribani siku nne jibu lililokuja lilikuwa lilelile kuwa mtu huyo si mwingine bali ni Jegan Grashan. Kazi ikawa ni jinsi gani ya kumtia mkononi mtu huyo hatari ambaye bila shaka yoyote lazima atakuwa na silaha za kujihami ambazo hazitojali kukuua iloimradi yeye aokoke, mkakati ukapangwa, wanajeshi watatu mahili wakaungana na Kamanda Amata kufanya kamato hilo usiku wa manane. Chopa la kijeshi liliandaliwa na usiku huo liliruka kutoka uwanja wa ndege wa jeshi majumba sita ukonga na kuelekea Handeni Tanga, wakiongozwa na signal maalum iliyowekwa katika jengo lile katikati ya takataka na yule kijana alipoenda kumwaga taka siku ile.
“Heyyyyyy!” zilikuwa kelele za rubani wa chopa ile akiwashtua wapiganaji wake, kisha akawaonesha ishara kuwa tayari wamekaribia. Kila mtu akajiandaa kwa kuvaa gas mask zao zilizowaficha sura zao, bunduki kubwa za kivita na silaha ndogondogo zilikuwa sambamba nao, rubani wa chopa ile aliishusha pembeni kidogo ya stoo ile, walinzi walipoona hayo wakahamainika na kuanza kutaka kuishambulia ile chopa, yule rubani akawasha taa kali sana iliyofungwa mbela ya chopa hiyo na kuwanya wale walinzi kushindwa shabaha na kuficha macho yao, Kamanda Amata na wale wapiganaji wa jeshi waliteremka kwa kuruka na kuvamia moja kwa moja jengo hilo, upinzani ulionekana dhahiri, kwani wale walinzi walionekana kumudu hasa mapigano ya silaha, walipoamuriwa kusalimu amri walibisha vikali na kushambuliwa kwa risasi ma kuuawa, moja kwa moja msako uliamia ndani ya jengo hilo huku askari wawili wakibaki nje kulinda usalama, Kamanda Amata na mmoja waliingi ndani, hawakutegemea kukuta jumba kubwa la kifahari lililojengwa chini ya ardhi, ndani ya chumba kimoja walimkuta Jegan Grashan akiwa ameketi bila wasiwasi wowote, hakuonesha upinzani wowote kama ilivyotegemewa, Kamnda Amata alitulia kwanza kuona mtu huyo katulia namna ile, akamwita Jegan asimame kutoka pale alipokaa na asogee, lol Jegan alikuwa amekalia bomu ambalo lilibaki muda mchache kulipuka, hakuna kulala.
Yule mwanajeshi alimshika mkono Jegan na kumvuta kutoka naye nje, walipofika nje hawa kumaliza hata geti, ishara waliyoitoa kwa rubani ndiyo iliyosaidia rubani yule kuelewa na kuligeuza lili chopa haraka kuliondoa eneo lile, “Chiniiiiiiii !!!!!!” yule mwanajeshi alipiga kelele na wote wakalala chini pamoja na wale walioimarisha ulinzi walilala chini, mlipuko mkubwa ulitokea ile stoo yote ikateketea. Kamanda Amata alinyanyuka akiwa na maumivu makali mkononi mwake, kipande cha chuma kilimchoma na kumuumiza, walimkokota Jegan umbali kidogo na kuifikia ile chopa ambayo sasa ilikuwa imesimama kwenye mikonge wakampakia na kumfuga pingu na minyororo ya miguu, kisha wakaondoka zao.
DUNIANI kuna mvutano mkubwa sana juu ya utwala na tawala zenyewe, huyu anasema hili juu ya mwenzake na huyu anatamka vile dhidi yake. Mvutano mkubwa unaonekana waziwazi kati ya taifa la Marekani na washirika zake wa Ulaya dhidi ya mataifa machache ya Mashariki ya kati, mataifa yanayosadikiwa kwa mbinu chafu za kigaidi za kuteketeza mamia ya wanadamu katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kwa njia tofauti wanazozijua wao. Mataifa yanayojiita makubwa duniani yana ndoto za kufutilia mbali enzi na ujeuri wa mataifa haya machache ambayo yamejidhatiti na hayatetereki na vitisho kama hivyo, ambayo leo kesho yako tayari kuingia vitani dhidi ya mabeberu hawa wa maghalibi.
Kitendo cha Marekani na washirika wake kuivamia ardhi ya Mashariki ya kati kwa minajiri ya kukomesha tawala za kidekteta zinazonyima watu haki zao kiliwachukiza watawala wa mataifa haya na ndipo walipoanza kujitutumua na kuendesha vita yao dhidi ya mataifa makubwa popote yalipo duniani, yalizalisha magaidi wakubwa, watu hatari ambao kwa namna moja au nyingine walijifunza mbinu zote za medani za kivita ndani ya mataifa yao na kufundishwa na wao wenyewe kisha wakageuka kuwa silaha mbaya zenye akili ya ajabu na kuitikisa dunia. Vichwa vinauma, mioyo inadunda, akili hazitulii, vikao vya mara kwa mara vinaitishwa vya kuangalia jinsi ya kukomesha hali hii, na muda huohuo vikao vingine vinaitishwa kuona jinsi gani ya kutengeneza shambulio lingine, la namna gani na wapi wakalitekeleze. Ni akili mbili zisizochangamana zilikuwa zikizungukana pande mbalimbali za sayari hii na kuwafanya watu kuishi pa si na amani. Wkati wao wanaanzisha kambi za jeshi kila kona ya dunia ndani ya ardhi za nchi za wengine hasa wanyonge kama Afrika, na wenzao waliimarisha makundi yao kila kona hasa Afrika.
˜˜˜
Kikao kizito kilikuwa kikiendelea katika ofisi moja nyeti ya serikali, hoja ilikuwa ni ileile ya kuachiwa kwa Jegan Grashan au la, mara hii muda ulikuwa umekwisha sana hivyo kufanya kikao hicho kuwa na mvutano mwingine wa kipekee. Zilikuwa zimebaki siku tatu tu ili zile siku saba walizopewa kumuachia huru mtu huyo zitimie na endapo hatoachiwa basi shambulizi kubwa na lisilotegemewa lilikuwa limepangwa. Vikosi vya usalama havikulala, usiku kucha vilijipanga hapa na pale kuhakikisha wanansa kila aina ya milipuko inayosadikiwa kubebwa au kuwekwa mahali Fulani. Mitambo ya kisasa ilifungwa katika sehemu mbalimbali za mikusanyiko ya watu kama kwenye supermarket, vituo vya mabasi kama Ubungo, uwanja wa ndege na sehemu nyinginezo nyingi, askari kanzu walizagaa kila eneo kuhakikisha wananusa kila aina ya mazungumzo, usiku ndo usiseme, ilikuwa tabu sana kwa wale wapenda giza, vibaka, machangudoa, walevi, wazururaji na wote wanaofanana na hao. Idara ya uhamiaji nayo ilikuwa makini kuchunguza kila anayeingia nchini iwe kwa ndege, meli, gari au hata pikipiki kama sio baisikeli, vibali vya kusafiria vilipekuliwa kwa umakini wa hali ya juu kwa mitambo ya kisasa iliyoweza kugundua alama fichwa mbalimbali katika vijitabu hivyo, wapo waliokamatwa na hati feki lakini walipoonekana hawana dalili ya wale wanaowatafuta basi waliwaacha na adhabu kubwa kwao ilikuwa ni kuwarudisha kwao tu. Computer maalum iliyounganishwa na zile za usalama za mataifa ya maghalibi zilifanya kazi kubwa maana ziliweza kutambua mtu mpaka kijiji ulichozaliwa hata kama wewe ulikisahau kwa kuwa zilikuwa zimelishwa kumbukumbu nyingi.
Muafaka ulikuwa mgumu sana katika kikao hicho lakini ukweli ni kwamba wengi walionekana kukubali bwana huyo kuachiwa ili kukomesha mauaji yanayofanyika na kupoteza maisha ya Watanzania wasio na hatia. Madam S bado alikuwa na ushawishi mkubwa wa kuwafanya wajumbe wa kikao hicho kubadili mawazo na kuytomuachia huru Jegan, kila alipokumbuka kauli na mifano ya kijana wake Amata au Kamanda kama ilivyozoeleka kuitwa alijikuta ana dei la kuzuia kuachiwa kwake, lakini wengine wote walitaka aachiwe. Waziri mwenye dhamana alijaribu kuwasihi jambo hilo lifanyike haraka maana ni masaa sabini na mawili yalikuwa yakijihesabu ili lile wasilolijua lifanyike. Walibaki kizani, kiza kinene kwa kuwa walipigana na adui wasiyemjua wala kumuona, ilikuwa ni kama kupiga ngumi gizani.
Kikao kilifikia tamati, uamuzi wa kusubiri masaa ishirini na nne ulipitishwa na kila mjumbe alirudi katika majukumu yake wakati waziri mwenye dhamana alikwenda kuonana na mkuu wa nchi kujadili swala ilohilo.
˜˜˜
*>>>>>Upande wa pili nako kikao kiliendelea.*

“Hawataki kumuachia mpiganaji wetu,” yalikuwa maneno manne ya Shailan, aliyaongea huku akiwa akishikashika zile ndevu zake nyingi.
“Kama hawatii tunachotaka basi tufanye yetu, hapa tuna masaa yasiyopungua sabini tu so hatuna budi kuanza kazi, nimeongea na Beishal, tayari amesema kuna watu wako njiani kuingia hapa wao watakuja kumaliza kazi kwa jinsi ambayo watabaki na hofu kuu maana hataitegemea kutokea.” Shakrum alizungumza kwa kujiamini sana huku taratibu akiwa anakunywa ile kahawa yake chungu kabisa ambayo upendwa kunywewa na watu wa Pwani.
“Wasipotekeleza itakuwa ni kaburi lao sasa, kama wanakumbuka septemba 11 pale New York sasa wataona kwa macho yao kitachotokea hapa mbele ya macho yao,” Shailan aliijibu hoja ya Shakrum. Wakiwa katika kikao chao cha watu wachache mara simu ya mezani iliita na Shailan akampa ishara Shakrum aipokee naye akafanya hivyo. Baada ya dakika kadhaa alirudi kitini na kutazamana na Shailan, muda wote huo Scolleti alikuwa kimya bila hoja.
“Vipi?”Shailan aliuliza
“Mzigo tayari, Beishal kasema tusubiri, kutoka upande tusioujua jamaa watatokea na watakua hapa ndani ya masaa ishirini na nne,” Shakrum aakajibu.
“Ok! Tuwasubiri tufanye kazi”
Kimya cha ghafla kikapita kwa sekunde kadhaa, kisha wote wakacheka pamoja.
“Shailan, kumbuka tuna yule Malaya wa jana, lazima ashughulikiwe,” Shakrum alikumbusha
“Ooh gud, nenda ukamfanyie kama yule mwingine kisha nipe ripoti, na hakikisha Mwadawa anapatikana kuna mabo anayajua yule binti asije akayatapika,” Shailan akasisitiza.
Shakrum akainuka kitini na kuvuta droo iliyokuwa kwenye kikabati kidogo na kuchukua bastola na kisu chenye urefu wa futi moja. Kisha akaondoka zake na kumuacha Shailan na Scolleti.

˜˜˜>>>MALAWI>>>

Uwanja wa ndege wa Karonga
Karonga, mji mdogo ulio katika mkoa wa kaskazini katika nchi ya Malawi, maghalibi mwa ziwa Malawi au ziwa Nyasa kama linavyoitwa hapa kwetu.Ndege ndogo aina ya Sessna ilitua subuhi na mapema katika uwanja huo, ilipokwishaegeshwa mahali pake, mlango ukafunguliwa, watu wawili wanaume waliteremka na kuelekea eneo la mapokezi ambako watu wa uhamiaji walikuwa pale tayari kuwapa msaada wanaouhitaji. Haikuwa na shaka wala haikuwa na tabu, ndani ya dakika ishirini walikuwa nje ya uwanja huo tayari kuelekea kule wanakokutaka. Tax, ilikuwa ni usafiri pekee uliowapeleka moja kwa moja mpaka katika moja ya hotel za kawaida na kujipatia chakula huku wakipanga mikakati yao jinsi ya kuingia Tanzania, walishatahadaharishwa kuwa huko waendako kuna ulinzi wa hali ya juu hivyo watumie mbinu zote wawezazo kufanikisha adhma hiyo.
Ndani ya lisaa limoja walikuwa kwenye Pwani ya Ziwa Malawi, pale walikuta shughuli nyingi za wavuvi zikiendelea, wakatazama huku na kule, wakaona boti moja iliyofungwa injini, wakaona ndiyo iwafaayo, wakaiendea na kumkuta kijana mmoja aliyekuwa akisuka nyavu zake tayari kujiandaa kwenda kuvua. Wakamwita na kuzungumza nae kuwa wanaomba awafikishe katika kijiji kingine mbele katika mwambao huo, alipotaka kuleta ubishi wakampatia pesa za kimarekani, akakubali, lakini akaomba wakubali aene na mwenzake, hawakupinga.
Watu wanne walikuwa botini na safari ikaanza, boti ile ya mti ilikuwa ikikata maji kwa mwendo wa kasi kwani injini yake iliruhusu hilo. Walipofika mbali na pale walipotoka ndipo walipofanya lile walilopanga, waliwaua wale vijana na miili yao wakaitupa majini kisha wao wakamiliki ile boti, na kwa kuongozwa na dira waliyokuwa nayo, waliongoza chombo hicho kuelekea kaskazini maana kiliwapa uelekeo sahihi. Masaa manne hayakuwa haba wao kufika katika mapori Ludewa ambako walikitelekeza chombo hicho na wao kupotelea katika misitu hiyo mpaka Ludewa mjini, sasa wakagawana kila mtu kutumia usafiri wake na miadi ilikuwa ni kukutana Dar es salaam, mahala walipoelekezwa, kwa muda waliopanga.
˜˜˜
Shakrum aliingia katika stoo kubwa waliyomfungia yule binti wa kihindi, akapigwa na butwaa kukuta mlango mdogo wa chumba cha siri walimomficha yule binti uko wazi, akasita, akasimama na kaungali kwa makini, kisha akanyata hadi kwenye ule mlango na kuangalia ndani yake, hakuna mtu, kamba waliyotumia kumfunga yule binti walizikuta pale chini, si kwamba zimekatwa bali zimefunguliwa na aliyefungwa ametoroka kwa amani. Shakrum hakuamini kilichotokea, akatazama huku na kule, juu na chini hakugundua kitu, ‘Ametokea wapi mwanaharamu huyu?’ alijiuliza lakini hakuna jibu alilopata, akiwa kashika kisu chake kwa mkono wa kulia na ule wa kushoto akiwa kama anajaribu kujua makali ya kisu kile kwa kugusagusa kwa vidole vyake, kijasho chembamba kilimtiririka na kurusu mvujo uliokuwa ukilowesha fulana yake aliyovaa, alipogutuka, alitoka nje haraka na kuwaendea walinzi kuwaliza kama wamemuona mtu yeyote kupita eneo hilo, lakini walidai hawakuona, Shakrum alisikitika sana lakini pia alijilaumu kwa kuwa hakuwaambia walinzi tangu kabla kama kuna mtu aliyefungiwa ndani ya jengo hilo. Hakuwa na la kufanya aliinua simu yake na kupiga kwa Shailan ambaye alishtushwa na habari hiyo pia. Wote walibaki midomo wazi hakuna aliyeamini kama binti yule angeweza kutoroka katikla mazingira kama yale, lakini ndiyo ilikuwa tayari imetokea.
˜˜˜
ShaSha, alijificha nyuma ya kibanda kidogo ambacho hakikuwa mbali na geti la mlinzi, jirani kabisa na tenki kubwa la mafuta lililowekwa hapo, aliweza kuwaona Shakrum na wale walinzi walipokuwa wakiongea pale karibu na geti, alipoondoka na kuwaacha pale, ShsSha alinyata huku akiambaa na ukuta mpaka nyuma ya kibanda cha mlinzi na kutulia hapo, akawaangalia walivyokaa kizembe wakicheza draft hali silaha zao wameziweka chini, akakizunguka kile kibanda upande wa geti na kuona limefungwa akatazama huku na kule hakuna mtu akajitokeza, na kwa kasi ya ajabu akaruka teke lilitoa kisogoni mwa mmoja wao na kumsukuma mbele ambako aligongana kichwa na yule mwingine na wote kuanguka, kbla hawajakaa sawa, aliruka na kutua pale walipo, pigo moja la nguvu lilitua nyuma ya shingo ya mmoja wao na kumpotezea fahamu kisha yule mwingine alimpiga kwa kumkanyaga na kumrudisha chini sakafuni kwa kishindo, kwa jinsi alivyopiga kisogo pale chini alipoteza fahamu pia, ShaSha akawasachi na kutoa funguo kisha akajifungulia geti na kutoka nje, akachukua tax haraka na kumuamuru dereva amfikishe Ilala Hotel. Walipofika alimwambia amsubiri pale chini, kisha akaj na kumpatia pesa yake. ShaSha akaona wazi kuwa hapo sasa si mahala salama akafunga mabegi yake na kuondoka, akabadili hotel na kuhamia Kinondoni kwa Manyanya kwenye hotel ya kawaida ya Manyanya Hotel na kuweka kambi hapo.
ShaSha, kama anavyojiita, msichana wa kihindi kwa umbo lake dogo lakini ni mtu mzima aliyestahili kitwa mwanamke, alikuwa nchini kwa kazi moja tu aliyotumwa na serikali yake kuja kumchunguza Scolleti na mambo yake maana katika nchi nyingi bwana huyu alimopita serikali nyingi zimelalamikia uwepo wake kwa kusaidia kutekeleza ama ujambazi au kuhatarisha hatari ya nchi hiyo kwa namna moja au nyingine. Mara hii serikali yake ya India iliamua kuingia kazini kumchunguza kila aendako ni nini anakifanya, sasa Tanzania, Scoletti anawasaidia freedom fighters kutekeleza lile taraja lao la kudai haki ya kufunguliwa ndugu yao, wakitekeleza milipuko mikubwa na mibaya na kuuwa mamia ya watu.
ShaSha alikuwa pale White Sands hotel katika nyendo zake za kumfuatilia tajiri huyu, alipokutana na Amata na kumkaribisha juice, Amata alivutwa na uzuri wa sura ya binti huyu na macho yake yasiyo na pazia hayakuweza kuinyima raha roho yake iliyofungiwa ndani ya kifua chake kwa kuutalii mwili mdogo, shupavu wenye umbo la kuvutia. Angekosa kuwapo Gina katika eneo lile basi tayari labda mapenzi yangeamka, ama kweli, Inzi hufia kwenyew kidonda.
˜˜˜
Kamanda Amata alikunja nne kwenye kiti chake cha kuzunguka, huku akimwangalia Gina aliyekuwa bize na kuchapa kazi mbalimbali alizopewa siku hiyo. Akiwa na mawazo mengi hakuna kingine alichofanya kwa siku hiyo zadi ya kushinda ofisini tu akitega skio huku na kule kuona kama atasikia lolote kat i ya yale anayoyahitaji, lakini mpaka muda huo haluna kilichojiri kabisa.
Magazeti yote alikwishayapitia, hakuna jipya. Redio zote alshasikiliza lakini habari zilkuwa zilezile, hakuna kigeni. Alivuta kjitabu chake kidogo cha kumbukumbu na kutazama kurasa chache za kufanyia kazi, akajikohoza kdogo na kuendelea kusoma kumbukumbu zake.
“Gina,” aliita, Gina akagutuka na kumwangalia Amata.
“Niambie,” akatika kwa mtindo huo wa kipekee.
“Nataka nikutume sehemu wewe kama katibu wangu muhtasi ukaniombee miadi ya kukutana na manager wa eneo hilo,” Amata alimueleza.
“Bila shaka, ni wapi huko?” Gina akauliza.
“Unakumbuka Mwadawa alitueleza juu ya ile kampuni ya Scolleti ya kusafirisha mafuta?”
“Ndyo,”
“Hapo sasa, uende, uombe miadi, nataka kukutana na manager ili tuongee maswala ya kibiashara,” akavuta mtoto wa meza na kutoa kadi ya kibiashara na kumpa Gina, “Hilo ndilo jina langu,” alongeza. Gina aliisoma kwa makini ile kadi huku akigeuzageuza kwa jinsi livyokuwa nzuri, yenye kuvutia kwa rangi rangi anuai, JOHN SIZIMBA, ilisomeka hivyo kwa maandishi ya rangi ya dhahabu.
“Kijana una majina mengi ! hivi unayakumbuka yote?” Gna aliuliza huku akiiweka ile kadi katika mkoba wake.
“Yote nayakumbuka,” akajibu. Baada ya kumaliza kazi yake, Gina alinyanyuka na kumuaga Amata kuwa anaenda huko alikomtuma, “Tunaenda wote. Mi nakuacha uingie utanikuta nje.”
Baada ya kupambana na foleni za jiji la Dar hasa ile barabara ya Bagamoyo, iliwachukua lisaa limoja na nusu kufika Bunju, mbele kidogo ya Baobab Sekondari na moja kwa moja kwenye maegesho ya yadi kubwa lililoshehen malori kadhaa ya mafuta. Amata alegesha gari nje na kumtaka Gina kuwenda huku akiwa amemuunganisha na kinasa sauti katika sidiria yake. Gina alishuka na kuanza mwendo wake wa mikogo kulielekea get kuu, akagonga na kufunguliwa, akajitoma ndani.
Kamanda Amata akajiweka sawa, na kukiwasha kiredio maalumu ambacho kingempatia mawasiliano yote yanayotoka humo ndani.
“Karibu mrembo!” ilikuwa ni saut nene na nzto kutoka kwa pande la mtu alyekuwa ameketi nyuma ya meza kubwa iliyostahili kuwapo ndani ya ofisi hiyo nadhfu ilipambwa na kunukia udi.
“Asante sana, nimekaribia,” Gina aliitikia, “Naitwa Gina Zingazinga, kutoka kampuni ya SCOTT,” alijtambulisha na kueleza kwa kifupi juu ya kazi wafanyayo. Yule bwana alionekana akifuatilia kila kitu kwa makin kabisa, Gina akamaliza utambulisho wake na kueleza kile kilchomleta.
“Ok nimekuelewa, haina tatizo, tuna nafasi nzuri sana ijumaa baada ya swala ya mchana, tena utakutana na mkurugenzi mkuu atakuwepo, natumaini atafurahia ujio wenu,” Yule bwana alyejitambulisha kwa jina la Aidan,a alieleza kwa kirefu.
“Asante sana,” Gina alishukuru na kuaga, akasindkizwa na Aidan mpaka katika uwanja ule ambao ni maegesho ya yale malori, wakaagana na kutoka. Akiwa anatoka katika geti lle kubwa alipishana na gari moja aina ya Prado nyeupe iliyokuwa ikiingia ndani ya yadi ile, aliitazama kwa jicho la wizi na kukumbuka vizuri gari ile.
“Aidan!” Amata allitaja hilo jina mara tu Gina alipoketi kitin katka ile gari. Akageuza na kuondoka eneo lile na kurudi mjini. “Tutakuja ijumaa mchana,” Amata alirudia maneno yale yai le miadi.
˜˜˜
“Karibuni sana Tanzania,” Shailan aliwakaribisha vijana wawili walioonekana kuchoka sana kwa safari. Vijana waliosafiri kutoka nchi ya mbali kuja kuungana na wenzi wao katika kile wanachokiita ‘kupigania uhuru’, hawakuja kufanya starehe bali walikuja kufanya kazi, kazi ya hatari ambayo kishindo chake kila mtu atashtuka na dunia itazizima kwa hofu kuu, walipania, walidhamiria, waliamua kufanya kile kinachoitwa mauaji ya kimbari, lakini wangeikumbusha vipi serikali kuwa wanamhitaji ndugu yao, kaka yao, aliyeko gerezani? Yote ilikuwa ni mipango inayosukwa chini kwa chini na watu hao hatari katika uso wa dunia.
“Tumeshapata la kufanya, kabla ya lile tulilodhamiria, lazima tuwape tashwishwi kwanza kwa tukio dogo tu halafu watakapokuwa wameshtuka sasa tunawapa onyo kisha wasipojibu tunafunga kazi kabisa,” mmoja wa wale vijana alieleza.
“Sasa tukiwashtua, huoni tutakuwa tumewapa mwanya wa kuongeza ulinzi?” Shailan aliuliza.
“Hapana, lipi tumefikiria kufanya kama hitimisho kwa ndugu yetu hata wafanye vipi hawawezi kufikiria hilo, wataspigwa na mshangao tu, limetokeaje, watabaki midomo wazi wakishuhudia mamia ya wananchi wao yakiteketea kikemikali, hapo hawatakuwa na ujanja tena zaidi ya kutupatia kaka yetu na wao kubaki wakiomboleza, na hili litatokana na ugumu wa shingo zao,” aliongea kijana wa pili kwa sauti ya upole.
“Ok, tumebaki na masaa 48 hivi, nina wasiwasi mmoja hivi, kuna spy wao mmoja hatari sana, huyu jamaa nashindwa kumuelewa ni intelijensi kiasi gani, tusipomwangalia atakuwa kikwazo katika mkakati wetu,” Shailan alieleza kwa masikitiko, akadakiwa na Scolleti, “Yeah ni kweli kabisa, anaitwa Kamanda Amata, mwanzoni wa mission yetu amewaua vijana wetu na sasa amekuwa ni kikwazo kikubwa sana.”
“Nipe picha yake kama mnayo,” yule kijana aliomba. Shailan akachukua laptop yake ndogo na kufungua picha Fulani, kisha akamuonesha yule kijana.
“Sasa, huyu tuachieni sisi, kabla ya tukio hili atakuwa tayari marehemu, na mipango yote itaenda kama ilivyopangwa, tutahahakisha kabla ya jua la jioni kesho mwili wake upo mikononi mwetu,” walijigamba.
“Muwe waangalifu sana, Amata si mtu wa kuchezea hata kidogo, one mistake one goal, ameshakwamisha mambo mengi sana aisee,” Scolleti alizungumza.
“Hamna shaka, Shakrum, endelea na ule mpango wetu kama tulivyoongea, hakikisha ile kemikali imesogea eneo la tukio hilo ndilo la maana, mimi na huyu swahiba tunamfungia kazi Amata ndani ya masaa kumi tu,” yule kijana aliongea kwa majigambo. ‘Unamjua Amata au unamsikia?’ alijiuliza Shakrum moyoni mwake. Kikao kikaendelea na mikakati mibaya ikapangwa dhidi ya Watanzania wasio na hatia, hali tete.
˜˜˜
Mlango wa chumba cha Mwadawa uligongwa na watu wawili wakajikaribisha wenyewe mpaka ndani. Mwadawa alikuwa amejilaza kitandani akiangali habari kupitia runinga yake ya kisasa iliyofungwa sambamba na ukuta, alikurupuka kuwaona watu hao wawili waliojikaribisha baada ya kugonga mara moja tu, akaketi kitandani na kuwatazama, “Ninyi ni akina nani? Mbona mnaingia kwa mtu kibabe hivyo?” akawauliza.
“Usijali utatujua tu, umejaribu kutukimbia lakini sasa tumekupata, sasa, sisi na wewe tuondoke mguu kwa mguu jioni hii,” mmoja wao alisisitiza
“Mnipeleke wapi?” Mwadawa aliuliza kwa woga.
“We utajua ukifika, fanya tunalotaka kabla hatujatumia nguvu,” walimuamuru. Mwadawa aliwatazama kwa zamu watu wale ambao hawakuwa hata na chembe ya tabasamu, mmoja wao alipoona msichana Yule anataka kuleta ubishi, akachomoa bastola na kumuoneshea, “Sasa unaondoka na sisi au tukubakishe ukae hapa ndani mpaka watu wasikie harufu ya uozo wako?” aliuliza mwingine huku akiifunga kiwambo cha sauti ile bastola. Mwadawa alijawa na woga, alitetemeka mwili mzima. “Tunayasitisha maisha yako kwa kuwa umejifanya kimbelembele na kumpatia siri usiyoijua Kamanda Amata, sasa hizi ni salamu kutoka kwa bosi wako Scolleti,” Yule mwenye bastola akailengesha kwenye paji la uso wa Mwadawa na kuifyatua mara kadhaa, Mwadawa alijibwaga kitandani akiwa chapachapa kwa damu, kisha wale vijana wakaondoka zao na kuufunga mlango kwa mtindo wa kuurudishia.
Kamanda Amata aliitazama simu yake mara kwa mara hakuona ujumbe wowote kutoka kwa Mwadawa ambaye walikuwa wakichati muda si mrefu, alishangazwa na ukimya huo, akabofya ile namba na kupiga lakini wapi, haikupokelewa kabisa, akaishusha taratibu na kuitazama tena, akafungua meseji ya mwisho; ‘Magomeni Makuti, nyumba namba 434B, ukifika nishtue,’ ilikuwa ni moja kati ya meseji za miadi iliyokuwa ikipangwa kati ya wawili hao yaani Mwadawa na Kamanda Amata. Mwili wa Amata ulikuwa ukisisimka mara kwa mara, akhisi kuna jambo la hatari lakini hakuwa na uhakika ni jambo gani, alijinyanyua na kuifuata gari yake huku akiwa hajui ni wapi anakoelekea.
Ilikuwa yapata saa mbili na nusu usiku alipoegesha gari yake mbele ya nyumba namba 434B, Magomeni Makuti, akashuka na kuzipanda ngazi chache zilizo kwenye kibaraza cha nyumba hiyo, alipoukaribia mlango mkubwa alikuta na mbibi mmoja akiwa anatoka ndani, akamsabahi na kumuuliza chumba cha Mwadawa, Yule bibi akamtazama Kamanda na kumtupia swali, “Na we nani tena? He huyu binti ana hatari huyu, hivi magonjwa yote haya haogopi?” Amata akacheka na kurudisha swali, “Bibi, kwa nini unasema hivyo, mimi ni bnamu yake bwana.”
“Aaaaa binamu ndiyo hana maana kabisa, binamu nyama ya hamu wenyewe mwasema, haya bwana anaishi mlango huo wa tatu kulia, uwe mwangalifu kijana kuna madume mawili yameingia muda si mrefu,” Yule bibi alijibu huku akitoka nje na kumuacha Kamanda akiwa anaelekea ndani ya nyumba ile. Korido ndefu ilimkaribisha, akaipita na alipoukaribia ule mlango alihisi mwili ukisisimka na nywele kumsimama, akasita kidogo, akautazama na kugonga, haukufunguliwa, akainua simu yak e na kupiga, akaisikia ikiita ndani ya chumba hicho, akagonga tena na tena lakini hakupataa jibu, kengele za hatari zikamgonga kichwani, akatazama kupitia tundu la ufunguo, la haula, hakuamini akionacho, mwili wa Mwadawa ulijilaza kitandani, akagonga tena mlango lakini haukufunguliwa, wala Yule Mwadawa hakutikisika, akaufungua nao ukafunguka bila ubishi, hakuamini akionacho, sura wa Mwadawa aliyokuwa ikimwangalia ililowa damu na kisogoni mwake ndio kabisa, damu ilitapakaa na kuchafua shuka yote, Kamanda Amata alishikwa na ganzi, hakuamini kilichotokea na anachokiona, akavuta hatua zaidi na kuutazama mwili ule, alitikisa kichwa kuonesha masikitiko, hasira ikamtawala, alipotaka kugeuka, akagundua kitu, katika kiganja cha mkono wa Mwadawa, kipande cha karatasi, akakichomoa taratibu kana kwamba hataki kumuamsha huyo aliyelala, akakifungua na kukisoma kiliandikwa JULAI 7, hakuelewa maana ya ujumbe huo lakini pia hakuupuzia, akakiweka mfukoni na kutoka nje, akamuona tena Yule bibi.
“Mbona watoka kwa masikitiko, vipi, amekusaliti huyo, unaona!” Yule bibi aliendelea na swaga zake, Amata alipitiliza katika gari yake na kuondoka kwa kasi mpaka Yule bibi akabaki kushangaa. Alipotulia akapiga simu ya dharula kituo cha polisi na kuongea askari wa zamu pale Mgomeni, akawapa taarifa ya kutokea mauaji hayo na kuwaelekeza nyumba. Haukupita muda polisi wale walifika na gari yao mpaka katika ile nyumba, wakateremka na kuangalia hali halisi ya tukio lile, vipimo vya kitaalamu kama alama za vidole zilichukuliwa katika maeneo mbalimbali na walipomaliza, waliubeba mwili wa marehemu, huku nyuma wakiacha askari wakiendelea na mahojiano na wapangaji wengine. Kamanda Amata aliifuatili gari ya polisi kwa nyuma mpaka ilipofika Muhimbili na kuhifadhi mwili ule, walipoondoka, yeye akaingia na kukutana na Dr Jasmine ambaye alikuwa zamu siku hiyo, yeye kama daktari pia alibobea katika maswala ya uchunguzi wa maiti.
Kamanda Amata aliutazama mwili wa msichana Mwadawa uliokuwa umelala katika kitanda cha mochwari pale Muhimbili, pembeni yake akiwepo Dr Jasmin, aliutazama tena na tena hakuamini kilichotokea lakini ukweli ulibaki kuwa uleule tu, Mwadawa ameuawa.
“Vipi Kamanda?” Dr Jasmin aliuliza
“Ah! Nilikuwa sijamaliza kazi na huyu msichana, alinisaidia katika sakata hili lakini najua wameshajua hilo ndo maana wamemmaliza,” Kamanda alimjibu Jasmin huku akijifuta kamasi jembamba lilioashiria uchungu wa ndani kwa ndani, akaufunika mwili ule na kuongoza nje ya chumba hicho kisichopendwa na watu akimuacha Dr Jasmin aendelee na uchunguzi wake wa kitabibu.
>>>>Siku ilofuata
Gina aliegesha gari katika maegesho ya kampuni ile ya uchukuzi na usambazaji mafuta, wakateremka wote wawili akitangulia Kamata Amata, JOHN SIZIMBA wa bandia. Wakakaribishwa na walinzi na kuongozwa hadi kwenye ofisi ya secretary, pale walimkuta mwanadada mrembo, mweupe, mwenye asili ya kiarabu aliyewakaribisha kwa heshima ya hali ya juu, “ Karibuni, bila shaka ni ugeni kutoka SCOTT,” Amata akatikisa kichwa kuashiria kuwa yuko sahihi, wakaongozwa mpaka kwa meneja mkuu, kutokana na Amata jinsi alivyojibadili ilikuwa vigumu kumgundua. Ndani ya ofisi ile ya meneja walikutana na mtu mnene mwenye tumbo kubwa aliyejaa vema katika kiti chake cha magurudumu kinachokuruhusu kuweza kuzunguka ufanyapo kazi ya hapa na pale. Mtu huyo ambaye nae alikuwa na asili isiyojulikana, mhindi si mhindi, mwarabu si mwarabu, tukimwita chotara tunakosea, tukimwita mwafrika tunajidhalilisha.
Aliwapokea na kuwakaribisha viti, kisha yule sekretari akachukua kiti kingine na kuketi akiwa na makabrasha machache mkononi mwake.
“Naitwa Mr John Sizimba, na huyu ni katibu wangu, kutoka kampuni ya Scott,” Amata alitoa utambulisho upande wake na baada ya hapo ukafuatia utambulisho wa upande wa pili, ndipo mazungumzo mengine yalipoendelea juu ya mambo ya kibiashara, baada ya hapo yule meneja aliwachukua Amata na Gina na kuwapeleka kwenye chumba maalum ambacho waliweza kuona uwekezaji huo jinsi ulivyojikita nchini na nje ya nchi, marafiki zao wa kibiashara sehemu mbalimbali za ulimwengu hasa katika bara Hindi. Kamanda Amata hakuwa akisikiliza kwa makini ila alikuwa akikichunguza chumba kile kila kona jinsi kilivyoweka nakshi na ile screen kubwa ambayo iliweza kuwaonesha mambo mengi sana, wakiwa katika chumba hicho, kijana mmoja aliingia ndani na kumnong’oneza kitu yule meneja.
“Oooh Mr John, uniwie radhi, kuna dharula imejitokea sina budi kuagana nanyi, lakini karibuni wakati mwingine,” yule meneja aliagana na Kamanda Amata na Gina. Akili ya Kamanda Amata ikafanya kazi haraka sana, akagundua kwa vyovyote watakuwa wamemgundua, nae akaagana nae kisha yule sekretari akawaongoza nje, walipofika kwenye uwanja wa yadi ile, kulikuwa na wafanyakazi ambao kila mmoja alionekana kuwa na shughuli yake, wakapita mpaka geti kubwa pale wakakutana na kijana mmoja mwenye asili kama ya yule meneja, Amata akayasoma haraka macho ya yule mtu ambayo yalimpa majibu ya jambo alilolifikiria, hatari. Akatoka nje ya geti hilo na hapo pia akakutana na kijana mwingine mithiri ya yule wa kwanza, nywele za Amata zikasimama kuashiri kuna jambo si jema. Gina alilielekea gari lakini Kamanda Amata alimshika mkono na kumvutia upande wa pili kisha wakakodi tax mojawapo kati ya nyingi zilizopo nje ya eneo hilo na kuondoka zao. Hakuna aliyeongea katika tax hiyo mara kwa mara, Amata alikuwa akiangalia nyuma kuhakikisha kama kuna anayewafuata lakini hali ilikuwa shwari, hakukuwa na jipya.
6
SHAILA Shavrij ‘ShaSha’ aliendelea kutulia palepale njiapanda ya Ursino Road akisubiri kile alichokuwa akikisubiri, akiwa ndani ya gari ya kukodi kutoka kampuni Fulani ya jijini Dar, hakushusha hata kioo kimoja bali kiyoyozi kilifanya kazi yake ya kumrejeshea ubaridi, hali iliyo hadimu katika jiji la Dar es salaam. Akiwa gari yake kaitazamisha kule kwenye jingo la Kanisa la Kristo, macho yake hayakutaka kupoteza hata sekunde kuisubiri ile gari aliyoifuatilia ambayo ilikuwa imeingia pale kwenye ile barabara.
Ama kweli, subira huvuta heri, dakika cache tu, ile gari ilitokea njia ileile na kuchukua barabara ya Bagamoyo kuelekea Mwenge. ShaSha naye akafanya hivyo hivyo, kati yake na lile gari aliruhusu magari mawili tu kumpita. Taa za barabarani zililipendezesha jiji hasa katika njia hii ielekeayo Bagamoyo.
“Hakikisha hajui uwepo wako, maana malalamiko ya watu yamekuwa mengi, kwani Scoleeti ni nani au anafanya nini zaidi ya ufanya biashara aliyonayo?” ShaSha aliikumbuka sauti ya bosi wake siku alipokuwa akimpa majukumu ya kumfuatili tajiri huyu muuza mafuta.
Scoletti Ramjo, mzaliwa wa Bombay, lakini alipitisha maisha yake ya ujana huko Mumbai, India, muumini wa dini ya Kiboora aliondokea kuwa mfanya biashara maarufu sana aliyewekeza katika nchi mbalimbali ndani na nje ya Asia, daima alikuwa ni mtu wa kubadilisha makazi kutoka haya kwenda yale, hakutulia mahali pamoja. Kila nchi aliyokaa mfanya biashara huyu, haikuchukua muda ama alifukuzwa au alisababisha matatizo ya kidiplomasia kati ya nchi hizo, alituhumiwa kushirirkiana na vikundi vya kigaidi, kutekeleza mipango michafu dhidi ya binadamu na ubinadamu wenyewe, kuhifadhi wahamiaji haramu ambao hata hawakujulikana kazi yao katika nchi enyeji. Baada ya kufukuzwa huku na huko, Bwana Scolleti aliingia Africa Mashariki miaka kadhaa, akaishi Nairobi na baadae kuhamia Dar es salaam ambako alianzisha kampuni mbili kubwa, moja ya kusafirisha mafuta kwenda nchi za SADC na nyingine ni ile ya zimamoto iliyopo Dar es salaama na kueneza matawi yake katika mikoa mikubwa mingine. Kama kawaida ya Tanzania, taifa la amani, huwa alimfuatilii mtu, linaamini kuwa kila mtu ni mwema, kumbe wapo chui katika ngozi ya kondoo.
Alipokutana na waziri wa Viwanda na Biashara katika moja ya mikutano ya kimataifa ya kibiashara uliofanyika huko Tokyo, Japan, ndipo alipopitisha ombi lake la kuja kuwekeza katika nchi hii tulivu, wakati huo akiwa ametimuliwa kutoka Thailand baada ya kugundulika kuwa alikuwa akfadhili kikundi cha Tamir Tiger kwa kuwapa silaha kupigana na serikali huku yeye akifanya biashara zake haramu. Akakubaliwa, mipango ikawekwa mezani, mimi na wewe hatujui, labda kuna kiasi kilitolewa kama takrima kwa mabwanyenye, akaingia nchini, haikuchukua muda akaanzisha kampuni yake ya zimamoto na uokoaji yenye vifa vya kisasa kabisa, ilikuwa ni mapinduzi kwani tangu hapo huduma hiyo ilitolewa na kampuni ya jiji tu iliyobaki na gari noja lilichoka kila idara. Baada ya hapo akaanzisha ile ya uchukuzi na usafirishaji wa mafuta, akiwa mbioni kuiomba serikali wampe moja ya visiwa vya Mafia kunakosadikika kuna mafuta ili achimbe. Scolleti pamoja na washirika wake wakajikita katika mwamvuli huo na wakati wa mlipuko wa ubalozi wa USA hapa Dar na Nairobi, alishiriki kikamilifu katika kuwahifadhi na kuwapa kila wanalohitaji wataalamu hao mpaka wakafanikiwa.
“Tumechoka, kila nchi inatulaumu sisi juu ya huyu mtu,” aliongea bwana Premji, afisa usalama wa India, akimweleza ShaSha.
“Uende Tanzania, maana tumeshajua kuwa yuko huko kwa muda sasa, hakikisha ukishajua anachofanya, haina haja ya kuwa hai, utajua utafanya nini, sisi tunataka ripoti tu.”
ShaSha, mwanausalama mtukutu anayejulikana natika kazi, kwa kujiamini kwake na utendaji bora. Alikabidhiwa kabrasha la Scolleti ahakikishe anamtia mkononi kwa hali yoyote ile. shaSha baada ya kukabidhiwa jukumu lile alianza moja kwa moja kwanza kwa kutafuta ni mahali gani katika dunia hi alipojificha, haikuwa kazi ndogo, ilimbidi kusafiri sana kila nchi apitayo, mwisho akajikuta ndani ya Tanzania, akikabiliana na Scolleti, mtu ambaye hajawahi kumuona live isipokuwa kwenye picha tu. Katika chunguzi zake sasa anajikuta anagundua mambo mbalimbali yafanywayo na Scolleti, sasa akaanza kumfuatilia kila mahali akichukua picha mpaka za maswahiba zake, mara ya kwanza alimuona pale White sands Hotel alipokuwa na kikao na swahiba zake wenye ule mpango halifu, lakini Scoletti katika kujilinda ana macho mengi, alishajua uwepo wa SaSha eneo lile hivyo vijana wake wakaweza kumteka na kutoweka nao.
SaSha aliitazama saa yake ya kwenye gari, ilimuonesha kuwa ni saa nne usiku na dakika kadha wa kadha, aliiacha ile gari ikiingia kwenye yadi kubwa pale Bunju na yeye akapiliza kama mtu yoyote asiye na shughuli na eneo lile, alipakumbuka sana kwa kuwa alishawahi kutekwa na kuhifadhiwa ndani ya yadi hiyo. Kwa mwendo wa taratibu akaegesha gari yake katika moja kilabu kikubwa cha pombe za kizungu mita kama mia nne kutoka ile yadi, akashuka na kujichanganya na wanywaji wengine, kila mtu alimuonea kijicho mtoto huyo wa Kihindi aliyeingia eneo kama hilo, wakware mate yaliwadondoka, wazinzi mioyo ilienda mbio na suruali kupata shida. SaSha, msichana mfupi, mwenye mwili wa wastani kadiri ya kilo 65 hivi, aliyevali fulana nyeusi iliyopambwa na maandishi ‘Mtoto wa Bongo’ ilifunika vijititi vidogo kama vya msichana ambaye hajavunja ungo, jeans nyeusi yenye kigozi ‘Lee’ ilisitiri eneo la chini la mwili wake likiyaficha makalio manene kidogo yaliyoning’inia kwenye kiuno chembamba kabla ya kubebwa na miguu iliyoonekana mikakamavu ingawaje ilikuwa ndani ya suruali.
Hatua chache zilimfikisha katika kaunta ya bar hiyo na akaagiza kinywaji aina ya Savanna, kwa kuwa aliona jinsi alivyokuwa akitolewa macho na midume ile, akawaagizia pombe kila mmoja.
Muda ulienda na masaa mawili yakakatika, binti yule akapita njia ya kwenda chooni na kuruka ukuta kutokea nje, upande wa pili wa bar hiyo, akapenyapenya mpaka akatoke barabara kubwa na kuiendea ile yadi. Mwanga mkali wa taa za pikipiki ulimmulika usoni, akajificha macho huku akiipa mgongo ilipompita alishangaa kuiona ikisimama eneo Fulani si mbali sana na pale, hakulifuatilia hilo, aliendelea na yake.
SHAILAN na watu wake walikuwa katika meza ya duara ndani ya ukumbi mdogo wa mikutano katika yadi ndogo ya Mabibo, walikuwa wakihesabu masaa arobaini yaliyowabakia tangu kuishinikiza serikali imuachie huru ndugu yao mpigania uhuru, Jegan Grashan aliyefungwa na serikali ya Tanzania katika gereza kuu la Ukonga kwa miaka kadhaa. ?Unafikiri watamuachia?? mmoja wa wale vijana wageni aliyejulikana kama Tajan aliuliza. ?Tajan, unakata tama au vipi?? Shakrum alimtupia swali. ?Hapana kaka maana sioni jibu lolote kutoka kwao,? ?Wasipomuachia sisi kuanzia kesho ni kama tulivyoongea na tulivyopanga,? ?Na kuhusu Amata?? Tajana aliuliza tena, ?Maana tulitega bomu kwenye gari yake ila jamaa yule ana machale sana, akapanda tax, tukamkosa,? aliendelea. Shailan akawakatisha, ?Na hakikisheni Kamanda Amata anadhibitiwa vyema, hivi tunavyoongea ni kumzingira nyumbani kwake, haina haja kumkamata bali kumpoteza kabisa,? ?Ila Shailan, usikumbuke kupambana na Amata ukamsahau yule msichana wa Kihindi, hawa wawili wakiungana , maana sijui kama bado au tayari, tutakuwa na hali ngumu,? Shakrum akadakia. ?Usijali, kesho nchi hii itatetema kwa hofu na viongozi wao watapumua hewa ya mauti, dunia itazizima maana yale ya Nigeria, Somalia na Kenya ni cha motto, tutawaonesha patgazeti kisha picha lenyewe linakuja,? Shailan alijitamba huku akiipuliza kahawa yake ipoe kidogo, akainywa na kuagana na maswahiba zake, wakiwa tayari kila mmoja kachukua majukumu yake usiku huo. Tajan na kijana mwingine waliondoka na gari yao kueleka Kinondoni kwa Kamanda Amata, wakati Shakrum aliingia katika chumba kidogo cha mawasiliano. Giza lilikuwa limetawala, hakuna hata mbala mwezi iliyong?aa usiku huo isipokuwa nyota za mbinguni tu. Tajan aliegesha gari yake karibu na geti la nyumba ya Amata, akashuka pamoja na yule mwingine, wakaizunguka nyumba kila mtu upande wake, hakukuwa na njia nyingine zaidi ya ukuta mrefu ambao kuukwea ulitakiwa ujasiri wa hali ya juu, lakini hiyo haikuwa kazi kubwa kwa Tajan, alirudi nyuma hatua kadhaa na kuupanda kwa kasi kama ambavyo buibui apandavyo, na dakika moja tu alikuwa ndani ya wigo huo. Alitulia tuli, akisubiri kusikia kama kuna mchakacho wowote, alipoona kimya alitembea taratibu huku akiwa ameinama na bastola yake mkono ikiwa tayri kufuata amri itakayopewa na mshikaji, alilifikia dirisha kubwa la mbele, akajinyanyua kidogo kurusu paji la uso wake litangulie na macho yafuatie, hakukuonekana dalili ya mtu ndani mle. Akauendea mlango, akautazama kwa jicho lake kali, akachomoa funguo yenye uwezo wa kufungua loki kadhaa za ulimwengu huu, alipoitumbukiza tu, mlango ukajibu, akausukuma taratibu na kujitoma ndani. Hakuruhusu kelele yoyote isikike, akalivuta vazi lake na kufunika uso wote akabaki macho tu, mikono yake iliyovikwa gloves iliikamata bastola kwa ustadi, kwa mwendo wa kunyata, mwendo wa kininja, aliipita sebure na kukuta milango kadhaa, kati ya milango ile, mmoja ulikuwa unawaka taa hafifu na sauti ya muziki laini ilisikika kwa mbali. Tajan akajua sasa windo lake kalipata, akataka kuufungua mlango wa chumba kile, akasita, akabadili mawazo, akaiendea switch kuu ya umeme na kuiweka off, nyumba nzima ikawa giza, akatulia dakika kama mbili ili aone kama kuna mchakacho wowote baada ya giza hilo, hakuna. Akavuta hatua mpaka kwenye ule mlango, akanyonga kitasa, kikanyongeka, mlango ukajiachia kuruhusu nafasi ya mtu kupita, Tajan akaingia ndani na kutulia karibu na kabati paliponing?inizwa makoti na suruali kadhaa, alimuona mtu aliyelala kitandani na kujifunika mwili wote isipokuwa kichwa tu, alitulia palepale na kutoa kikopo kidogo chenye dawa kali ya usingizi, akanyunyiza, hewa ile ikajaa chumba kizima. Alipohakikisha zoezi hilo tayari, akakiedea kitanda na kumsukasuka aliyelala hapo, hakuwa Amata, bali Gina alikuwa kajipumzisha, hakuona haja ya kumuua, ?huyu nikimchukua, Amata atakuja mwenyewe? ≈≈≈ Utulivu wa ndani ya jengo hilo usiku ule ulimfanya ShaSha afanye upekuzi wake taratibu sana, akichunguza kila droo na kila karatasi aone kama atapata vile avitakavyo, alivuta hili akavuta lile, alifunua hiki akafunua kile, lakini alihakikisha anarudisha katika mtindo ambao wewe au mimi si rahisi kugundua kuwa hapa pamepekuliwa. Taratibu akatoka ndani ya ofisi hiyo ambayo aliona wazi kuwa haina tija kwake, akavuta hatua chache za kunyata katika kigiza cha koridoni na kuufikia mlango mwingine, akautazama kwa makini hata jinsi ambavyo alikuwa anautazama ni kiintelijensia zaidi, akashika kitasa chake na kukinyonga, akashangaa kikiachia na mlango ule kufunguka taratibu. ShaSha akatulia kwanza, akavuta pumzi, akajua huu kwa vyovyote ni mtego, akavuta hatua fupi fupi za tahadhari huku akaingalia pande zote kwa makini mkubwa, akauachia mlango na kukamata bastola yake mkononi, kwa harakaharaka alikikagua chumba kile na kugundua kuwa pia ilikuwa ofisi nyingine kubwa ya kifahari, alihisi kuwa ile itakuwa ndiyo hasa anayoitafuta, alitulia kidogo, ukimya wa ndani ya ofisi hiyo ulimpa faraja ya kujua kuwa hakuna tatizo lolote kama sio shida, akairejesha bastola yake mahala pake nay eye kuiendea meza kubwa iliyopo hapo ambayo juu yake ilibeba kibao chenye maandishi mazuri ya kupendeza yaliyochorwa kwa nakshi safi ya rangi ya dhahabu ?Managing Director? na chini ya hiyo ?Mr Scolleti?, maandishi haya yalimvutia sana ShaSha. Moja kwa moja alianza na motto wa meza akavuta taratibu na kuangali makabrasha kadhaa yaliyopo hapo, akayachambua kwa harakaharaka, alipoona hayana tija akaamia upande mwingine na kufanya vilevile, lakini hapa alipata kitu tofauti, kabrasha moja inaonekana lilimfurahisha zaidi, aklichambua harakaharaka na katika baadhi ya kurasa zake alitumia kamera yake ndogo lakini yenye nguvu sana kupiga picha baadhi ya kurasa hasa mle anamomuhitaji. Alipojiridhisha akarudisha kama vilivyo, na kuweka kamera yake mahali husika kisha akatoka taratibu katika chumba hicho na kuurudishia mlango kama ulivyokuwa.
Kamanda Amata alijua moja kwa moja anchokwenda kukifanya katika jengo hilo lililojengwa ndani ya yadi kiubwa ambayo mchan wake tu alikuwa hapo. Kwa kupitia nyuma ya ukuta wa yadi ile Amata aliweza kuruka na kuingia ndani kwa utulivu, akajibanza kando kidogo ya tenki bovu la mafuta lililotelekezwa hapo, akatulia akiangalia ustaarabu, alipotaka kutoka eneo lile alisikia mchakacho wa hatua zikija upande wake, akazisikiliza kwa makini ili agundue kama ni za mnyama au binadamu, lakini aligundua kuwa ni za miguu miwili, za binadamu, akatulia palepale bila kujitikisa, mara mtu aliyemkuwa akivuta hatua hizo akafika eneo lile, akasimama karibu kabisa na alipo Kamanda Amata lakini hakugundua kama kuna mtu. Yule mlinzi alitazama huku na huku, kimya, akaamua kuondoka, kabla hajavuta hatua ya pili, Kamanda Amata kama umeme aliibuka na kumpiga karate moja ya shingo iliyomfanya alegee na kuanguka, fahamu zikimtoka, Amata akamdaka na kumuweka chini taratibu asilete kokolo wala kelele. Akamruka na kuelekea upande wa pili, akajificha karibu kabisa na choo, akitazama walinzi jinsi walivyojipanga katika eneo lile. Ilikuwa ngumu kwake kuvuka kuelekea jengo lile lenye ofisi kwa sbabu kati yake na lile jengo palikuwa na uwazi mkubwa sana na taa zilizomulika kwa mwanga mkali, hivyo alitulia akipiga mahesabu jinsi ya kuvuka eneo hilo bila kuonekana na walinzi aliyoweza kuwahesabu na idadi yao kufikia kama sita hivi, wazo la haraka likamjia, akamkumbuka yule aliyemzima kwa karate kule nyuma, akageuza kurudi ili afanye lile alilolikusudia Tajan akajua sasa windo lake kalipata, akataka kuufungua mlango wa chumba kile, akasita, akabadili mawazo, akaiendea switch kuu ya umeme na kuiweka off, nyumba nzima ikawa giza, akatulia dakika kama mbili ili aone kama kuna mchakacho wowote baada ya giza hilo, hakuna. Akavuta hatua mpaka kwenye ule mlango, akanyonga kitasa, kikanyongeka, mlango ukajiachia kuruhusu nafasi ya mtu kupita, Tajan akaingia ndani na kutulia karibu na kabati paliponing?inizwa makoti na suruali kadhaa, alimuona mtu aliyelala kitandani na kujifunika mwili wote isipokuwa kichwa tu, alitulia palepale na kutoa kikopo kidogo chenye dawa kali ya usingizi, akanyunyiza, hewa ile ikajaa chumba kizima. Alipohakikisha zoezi hilo tayari, akakiedea kitanda na kumsukasuka aliyelala hapo, hakuwa Amata, bali Gina alikuwa kajipumzisha, hakuona haja ya kumuua, ?huyu nikimchukua, Amata atakuja mwenyewe?
Kamanda Amata alijua moja kwa moja anchokwenda kukifanya katika jengo hilo lililojengwa ndani ya yadi kiubwa ambayo mchan wake tu alikuwa hapo. Kwa kupitia nyuma ya ukuta wa yadi ile Amata aliweza kuruka na kuingia ndani kwa utulivu, akajibanza kando kidogo ya tenki bovu la mafuta lililotelekezwa hapo, akatulia akiangalia ustaarabu, alipotaka kutoka eneo lile alisikia mchakacho wa hatua zikija upande wake, akazisikiliza kwa makini ili agundue kama ni za mnyama au binadamu, lakini aligundua kuwa ni za miguu miwili, za binadamu, akatulia palepale bila kujitikisa, mara mtu aliyemkuwa akivuta hatua hizo akafika eneo lile, akasimama karibu kabisa na alipo Kamanda Amata lakini hakugundua kama kuna mtu. Yule mlinzi alitazama huku na huku, kimya, akaamua kuondoka, kabla hajavuta hatua ya pili, Kamanda Amata kama umeme aliibuka na kumpiga karate moja ya shingo iliyomfanya alegee na kuanguka, fahamu zikimtoka, Amata akamdaka na kumuweka chini taratibu asilete kokolo wala kelele. Akamruka na kuelekea upande wa pili, akajificha karibu kabisa na choo, akitazama walinzi jinsi walivyojipanga katika eneo lile. Ilikuwa ngumu kwake kuvuka kuelekea jengo lile lenye ofisi kwa sababu kati yake na lile jengo palikuwa na uwazi mkubwa sana na taa za helogene zilimulika kwa mwanga mkali, hivyo alitulia akipiga mahesabu jinsi ya kuvuka eneo hilo bila kuonekana na walinzi aliyoweza kuwahesabu na idadi yao kufikia kama sita hivi, wazo la haraka likamjia, akamkumbuka yule aliyemzimishaa kwa karate kule nyuma, akageuza kurudi ili afanye lile alilolikusudia. Aliusukasuka ule mwili uliolala, akaona hakuna dalili ya mtu huyo kuamka muda huo, akatazama nguo zake, na kuona suruali inashahabiana na ile aliyovaa, akamvua koti na kulivaa kisha akachukua ile bunduki yake kubwa, gobole, akalipachika mgongoni, taratibu akatoka kwa kupitia upande ule alikotokea yule mlinzi, alipofika kwenye kona akasimama, kidogo, kama aliyekumbuka kitu, kweli alisahau kitu kimoja, sigara, yule mlinzi alikuwa anavuta sigara, akaenda na kuinyofoa kinywani mwake kisha akaipachika kati ya vidole vyake viwili cha kati na cha shahada, mkono mwingine ukiwa na tochi, akajitokeza. Mwendo wa kama mita mia akapishana na kundi la walinzi watatu, akajikausha na kujifanya mmoja wao, akapita katikati yao bila kuwaogopa. Baada ya kuyapita malori kadhaa, alilifikia jingo ambalo alilidhamiria, akauendea mlango mdogo ulio upannde wa nyuma nakufanya vitu vyake, sekunde chache alikuwa ndani ya jingo hilo, akatulia kutazama usalama kwa maana alijua wazi kuwa mle ndani kuna camera za usalama kwa kuwa aliziona mchana ule. Ndani ya kijichumba alimokuwamo hakukuwa na kitu kingine zaidi ya mandoo ya takataka, akasonya kwa hasira ya kuwa amekosea mlango, akageuka kutoka lakini akasita, aliporudisha macho ukutani kwa juu kidogo akakuta kuna kamera ndogo mfano wa taa iliyopachikwa kiufundi sana, akatikisa kichwa kuashiria kuwa chumba hicho si bure, kuna jambo, chumba cha takataka kiwekwe camera. Akatuliza akili na kuendea kwa upande wa pili ile camera ili isiweze kupata picha yake alipoifikia alifyatua kiwaya kidogo kilichokuwa kikipeleka mawasiliano kwenye chumba kingine. Akautazama ule ukuta kwa makini ulikuwa umepigwa chuping, akayasukuma sukuma magudulia ya uchafu, akagundua kuwa kumbe kilikuwa choo, choo cha kutumia maji, lakini hakuona kijitenki cha maji isipokuwa bomba dogo pembeni, haina mana. Kamanda Amata hakuelewa hata kwa nini chumba hicho ambacho kilikuwa choo, mara cha takataka kiliwekwa camera, akaachana nacho akaamua kutoka, alipotikisa mlango umefungwa, lo! Yeye hakuufunga, ?Nani kaufunga mlango?? alijiuliza, ?Au wameujua uwepo wangu?? hakupata jibu. Akiwa katika mawazo, alijiegemeza ukutani, mara akahisi kitu kama msumari kikimchoma, akageuka na kupapasa akakutana na kitu hicho, akakitazama kisha akageuka upande wa kulia na kugundua kuwa ile camera ilikuwa ikitazama pale, akatikisa kichwa, akajaribu kukibonyeza, mara ukuta wa mbele yake ukagawanyika taratibu na kuacha uwazi mkubwa, Kamanda Amata akatabasamu na kuvuka kwa tahadhari eneo lile mpaka upande wa pili. Sasa likiona kile chumba anachokitaka, akakijongea na kuufanyia kazi mlango wake kisha akaingia, na kuanza upekuzi wake, ofisi ya ?Managing Director?, akiwa amefanikiwa kupata kabrasha alitakalo ambalo lilikuwa kwenye sefu ya siri sana ambayo si rahisi kuigundua kwa mtu wa kawaida, aliamua kuitoa fotokopi yote katika mashine iliyopo hapohapo ofisini na kisha kuhifadhi vivuli vyake. Akiwa anajiandaa kutoka akaona mlango ukifunguliwa taratibu, akarudi nyuma na kujificha pembeni mwa kabati karibu kabisa na ua la plastick, hakuamini macho yake alipomuona mwandada yule wa Kihindi akiingia, naye akichakurachakura makabrasha lakini alishangaa kuona yeye kachukua kabrasha lingine, hakujua kwa nini.
Barabara ya Mandela
“Hakikisha unachomea vizuri, usiruhusu hewa hata kidogo kutoka,” Shakrum alikuwa akimwambia kijana mchomeaji aliyekuwa akifanya kazi ya kutengeneza kitu mfano wa tank la mafuta lakini likiwa na umbo la wastani. Ilikuwa usiku mnene kazi hiyo ilipokuwa ikifanyika, haikuwa kazi rahisi kwa jinsi ambavyo kijitanki hicho kilikuwa kikiendelea kusukwa.
“Hapa vipi braza?” aliuliza Shakrum.
“Hapa poa, sasa watatia akili, lazima taifa liteteme kwa hofu,” sauti ya Shailan ilikuwa ikijibu swali la Shakrum.
Kazi iliendelea mpaka karibu na alfajiri, wakiwa mezani wanakunywa kahawa mara gari moja ndogo ikaingia
Shakrum aliiacha meza na kuiendea hiyo gari, akafungua mlango na kukuta mwanamke aliyelazwa katika kiti cha nyuma, akamtazama na kutikisa kichwa.
“Tajan, Amata yuko wapi?” akamuuliza.
Tajan akafungua kitambaa kilichokuwa shingoni mwake akachukua sigara na kuiwasha, akaipachika kinywani na kupiga pafu kama nne za nguvu, kisha akamtazama Shakrum, “Amata hayupo nyumbani kwake, nimemchukua Malaya wake huyo, najua kwa vyovyote atamtafauta ndipo tutakapomkamata na yeye kiurahisi,” akajibu.
“Ok, wazo zuri sana,” Shakrum alimpongea Tajan, akawaita walinzi na kuwaamuru wampeleke kwenye chumba maalum, wakafanya hivyo.
˜˜˜
Kamanda Amata alitoka kwa upole wa hali ya juu katika ngome ile kwa kufuata ujia mrefu ambao hakujua hata ni wapi ulikoelekea, alijua wazi kuwa kurudia njia aliyoingilia ni hatari kubwa hivyo akaamua kutafuata njia nyingine kuweza kuwa huru nje ya jumba lile. Akiwa katika kupitapita ndipo alipokutana na kitu kama kivuli kikitua nyuma yake mita kadhaa kutoka yeye alipo, hisia zake zilimtuma hivyo akaamua kugeuka ili akubaliane na hisia hizo, kosa, alipogeuka tu kabla hajakaa sawa alijikuta akipata mateke mawili yaliyotua usoni mwake kwa mtindo wa round kick, Kamanda Amata alijitahidi kukwepa ijapokuwa lilikuwa ni shambulizi la ghafla lakini hakufanikiwa, aliyumba kidogo lakini mara akawa sawa na kuangalia uelekeo wa adui yake ambaye sasa alimuona akijiviringa chini kwa ufundi mkubwa, akajua kuwa adui yake si mtu wa mchezo hata kidogo, akajiweka sawa. Yule mtu akajiinua kwa kasi ya upepo lakini kabla hajakaa wima alijikuta akipata pigo takatifu lililotua kifuani mwake na kumpotezea uelekeo, Kamanda Amata baada ya kutoa shambulizi lile, kwa mguu wake wa kulia alikanyaga ukuta na kujizungusha hewani alipotua chini mikono yake mikakamavu ilitua na karate safi katika shingo ya adui yake na kumpeleka chini. Kamanda Amata alitulia wima akiwa kajipanga kwa shambulizi linguine lakini hakumuona adui yake pale mbele yake, kabla hajageuka kuangalia nyuma alihisi akipigwa ngwala kutokea upande wa nyuma, akaruka juu kwa sentimeta kadhaa, hakukosea kucheza na hisia zake katika kigiza kile kilichomfanya kila mmoja apambane na adui yake kwa tahadhari.

ITAENDELEA

TODAYS
 
JULAI SABA - 4

Simulizi : Julai Saba

Sehemu Ya Nne (4)

Adui wa Amata alikua ni mjanja kupita maelezo, alijizungusha na kupiga ngwala ya miguu miwili ule uliotangulia ulipita sentimeta kadhaa kutoa sakafuni na Amata aliukwepa kwa kuruka lakini ule wa pili ulifuatia juu kidogo ya ule wa kwanza, huu ulimpata sawia kabisa katika visigino vyake na kutokana na kasi ya mguu ule, Amata alijikuta akikosa umakini hivyo kwa wakati huo akili yake ilifanya kazi haraka na kujirusha samasoti lakini alisahau kuwa eneo hilo ulikuwa ni ujia mdogo ambao haukuzidi mita moja na nusu kwa upana, so kwa uamuzi wake huo akajikuta akijigonga kichwa ukutanni na kitendo hicho kilifanya kengele za tahadhari za siri katika jingo lile kupata uhai, alipotua chini kama mzigo taa kali ziliwaka katika ujia ule na hakuna aliyeweza kujivuta hata sentimeta kumi, ndipo Amata kwa shida sana aliweza kumuona adui yake, akagundua kuwa alikuwa akipambana na mwanamke wa Kihindi, ShaSha, alimtazama kwa shida huku akiona taswira inayofifia machoni pake, akajitahidi kupambana na hali hiyo lakini haikuwezekana hata kidogo, akapoteza nuru kutokana na kupiga kicha chake kwa nguvu ukutani.
˜˜˜
“Kazi imekamilika bila kuitolea jasho kiongozi,” Shakrum alikuwa akimueleza Shailan huku usoni akionesha furaha ya wazi kabisa isiyofichika, “kamanda Amata, Yule Malaya wa kihindi na mwanamke wa Amata, wote tunao mikononi bila tabu, ni sisi tu wa kutoa hukumu juu yao, nikiwa na maana kuwa siku hizi mbili tulizobaki nazo tuna uwezo wa kuitikisa dunia katika mhimili wake kupitia nchi hii nyonge na dhaifu,” aliendelea kuongea. Shailan alibaki katumbua macho tu kwani hakuamini anachoambiwa kuwa watu hao wote ambao walikuwa wanatishia juhudi za kazi zao sasa wapo mikononi mwao, bado ilikuwa ni kama simulizi ya alfu lela ulela, Shalan hakuamini kama Kamanda Amata wanae.
“Shakrum, unalolisema lina ukweli au ndio sikukuu yua wajinga?” Shailan aliuliza.
“Tangu lini nakutaniaga wakati wa kazi muhimu kama hii? Nimepewa ripoti kutoka yadi kubwa kule Bunju hawa jamaa wamejiingiza wenyewe katika mtego huo, na hivi sasa wapo katika chumba cha chini na pingu mbilimbili kila mmoja kuhakikisha hawatoroki,” Shakrum alizidi kusisitiza.
“Habari njema, basi kwa ujumla tumemaliza kazi yetu kwa urahisi ambao hatukuutegemea. Haya mpe taarifa balozi tukutane pale yadi kubwa haraka iwezekanavyo,” Shailan hakuweza kuificha furaha yake, muda uohuo alituma fax haraka kule Mombasa kwa mkubwa wao naye aliwapongeza kwa hilo akaamuru watu hao wachinjwe mara moja na miili yao ihifadhiwe kwenye kaburi la siri ambalo limejengwa ndani ya yadi kubwa kupitia chumba maalum kilicho ndani ya chini ya ardhi.
Haikupita hata lisaa limoja timu yote ya kikosi kazi cha ‘Freedom Fighters’ pamoja na balozi wao hapa nchini Mr Scolleti walikuwa wamekusanyika katika chumba maalumu pale yadi kuu, Bunju.
“Tumepewa Baraka zote, za kuwakata vichwa hawa mabwana, na mi sioni haja ya kupoteza muda kwani kama kutusumbua wametusumbua sana hasa huyu Amata, na huyu nahitaji kumuua kwa mkono wangu huu,” Shailan aliongea kwa jazba mbele ya jopo lote hilo, akatulia kidogo akimtazama mmoja baada ya mwingine kisha akaendelea kusema, “Sasa hakuna po, kukipambazuka ni onyo la mwisho kwa serikali kwani sasa tayari ni wakati muafaka, afunguliwe kaka yetu, mpigania uhuru mwenzetu, anayejua kile anachokifanya, Jegan Grashan, awe huru na keshokutwa turudi naye nyumbani ambako atapokelewa kwa furaha,” akamalizia.
Baada ya majadiliano machache, wote wakashuka kwa chombo maalum mpaka chini ya ardhi ambako walifika kwenye chumba hicho cha siri, chumba madhubuti kwani mlango wake ulifungwa kwa namba maalum ambazo ni mtu mmoja tu aliyezijua, Shakrum.
“Ah ha ha ha ha !!!!” lilikuwa cheko la Shailan, cheko la dharau ambalo lilifika moja kwa moja masikioni mwa Kamanda Amata aliyekuwa amelala chini na pingu mbili mkononi mwake, alisikia kwa uzuri kila lizungumzwalo na watu hao lakini alijifanya bado hana fahamu ilhari akijua hila zao, ShaSha yeye alikuwa katulia tuli, hana la kufanya katika hilo maana pingu zile zilikuwa zimeimaban mikono na miguu yake pale chini, alikutana mzcho kwa mzcho na adui yake Scolleti, alyetumwa kwake kuja kuichukua roho yake tu baada ya serikali ya India kuchishwa na malalamiko ya mataifa mbalimbali yaliyopelekea mengine kuwa na mgogoro wa kidiplomasia na taifa hilo.
Scolleti, alivuta hatua chache sana na akamfikia ShaSha pale alipoketi, akamsukuma kwa mguu wake, ShaSha akainua kichwa na kumtazama mtu huyo.
“Hivi wewe mwanamke, nchi yako imekutuma na kukuamini kuja kunichunguza mimi, we unanijua mimi wewe, wenzako wote walionifuatilia mpaka sasa hawajulikani walipo, na wewe leo ndio zamu yako kuwafuata, kifo chako hakitakuwa na maazishi, wala maiti yako haitakuwa na mapambo yoyote, nani aliyekwambia binadamu anaweza kufuata nyayo za samba pa si kudhurika? Karibu sana katika himaya ya Shetani, na sisi sote ni wafuasi wake watiifu,” Scolleti aliongea kwa sauti yake nzito, huku akimsukasuka ShaSha. Bila kutegemea, Scolleti alijikuta akitemewa mate usoni na mwanamke huyo jeuri, aliyejiamini hata ndani ya pingu na minyororo ya watesi wake.
“Hata ukiniua mimi bado wapo wanaokuja kukutafuta, yupo ambaye atakutia mkononi na kuivunja shingo yako hata kama si mimi, Shetani mkubwa wewe, unayepoteza maiSha ya watu kwa kufadhili na kuhifadhi magaidi sehemu mbalimbali duniani, ilahali kule kwetu India unajifanya mwema kuwasaidia masikini na kuwajengea mashule na mahospitali ili kuilagha serikali, sasa umefika wakati, msaada wako ni takataka mbele ya wanaokujua na sasa kinachopangwa na kutenganisha roho yako na mwili wako ambao tungewapa ndege wa angani wafaidi nyama iliyojaa damu ya ibilisi ndani yako,” ShaSha hakumaliza kauli yake kwani teke la nguvu lilitua ubavuni mwake, na kumlete maumivu makali, hajakaa sawa teke lingine na lingine, kisha Scolleti akaenda kwa Shakrum na kumvua mkanda wa kijeshi uliofungwa kiunoni mwake, vichapo kadhaa vilimuacha ShaSha hoi hajitambui, damu zikimtoka puani na kinywani, hasira zilizotawala damu yake zilimfanya ajaribu kujitikisa labda pingu zile zingemuachia huru amuoneshe kazi mzee huyu lakini haiku hivyo alibaki kuuma meno tu. Shakrum akamuendea Scolleti na kumvuta pembeni, “Braza, usifanye kazi ambayo bado muda wake,” alimwambia. Tajan akaingia ndani ya chumba hicho akiwa na dvcam moja iliyofungwa juu ya miguu maalumu ya chuma, akaiweka mbele yake na kuigeuzia kule aliko Amata na ShaSha, Shailan akajifunga kitambaa cheusi usoni mwake na kusimama mbele ya camera ile kisha akaanza kuongea, kutoa ujumbe wakati chombo kile kikinasa picha ile. Nusu saa baadaye walikuwa wamekamilisha zoezi lao, waliamua wawachinje watu hao watatu siku iliyofuata huku wakipiga picha zingine ambazo zingekuwa ni salamu ya mwisho kwa serikali kama wasingekubali kumfungulia ndugu yao, kaka yao, mpigania uhuru mwenzao.

>>>>>

ASUBUHI ya siku iliyofuata ilimkuta Madam S katika ofisi yake akiendelea na majukumu yake kama kawaida, ndani ya ofisi yake kubwa na nzuri iliyobeba heshima zote za kuitwa ofisi. Kila mara aliangalia saa yake kana kwamba kuna mtu au kitu anachokisubiri ambacho mi na wewe hatukukijua isipokuwa yeye peke yake. Ilipita nusu saa ikawa saa, Madam S aliinua simu yake ya mezani na kubofya namba kadhaa kisha kutega chombo cha kusikilizia sikioni mwake lakini baadae alikishusha na kukiweka palepale alipokitoa.
Kwngele ya mlangoni kwake ililia, nae kwa kutummia chombo maalum aliweza kumuona Yule anayegonga kengele hiyo, Madam S akabonyeza tarakimu kadhaa zilizotengenezwa maalum juu ya meza yake na mlango ukajiondoa kitasa chake na kuruhusu mtu huyo kuingia ndani.
DHL, ni kijilebo kidogo kilichoning’inizwa katika box kubwa lililowekwa katika meza ya kando kidogo ofisini mwa Madam S, mlinzi wa getini alilileta ndani humo. Madam S alilisogele na huku akiwa ameshika saa yake akichezea kidubwasha Fulani, alipolikaribia akasimama na kuliangalia vyema, kabla hajalifungua alipiga simu getini na kumuita Yule mlinzi kumuuliza ni nani aliyeleta kasha lile, akajibiwa kuwa ni mfanyakazi wa DHL ambaye alikuwa na pikipiki. Kwa uzoefu wa kazi za kipelelezi kwa maiaka mingi, madam S aligundua wazi kuwa lile kasha halikutoka DHL kwani ufungwaji wake ulikuwa tofauti na ule aliouzoea, alilichunguza tena na tena na kugundua mambo mengi ambayo ni tofauti na utaratibu wa DHL, akalichukua na kuingiza kwenye kikabati maalumu chenye mitambo ya x-ray ili kuweza kuona ndani kuna nini kabla ya kulifungua. Mtambo ule baada ya kuwashwa ulionesha ndani ya kasha lile mlikuwa na kitu mfano wa dvd, akalitoa ndani na kulifungua, hakukosea, ilikuwa ni dvd moja ikiwa katika kasha lake, akaitoa na kuigeuzageuza, kisha akaifuata luninga yake kubwa iliyopo hapo ofisisni na kuitumbukiza dvd ile, akasubiri kuona kitu kitakachofuata.
Mtu aliyevalia vazi jeusi lililomfunika mpaka usoni, alionekana ametulia tuli, kisha akaanza kuongea kufikisha ujumbe ule alioukusudia. Madam S alisikiliza kwa makini ujumbe huo wenye vitisho vingi vya mauaji ya kutisha kutoka kwa magaidi waliokuwa wakidai kufunguliwa kwa mwenzao Jegan aliyefungwa na serikali ya Tanzania. Mwisho wa dvd hiyo aliziona picha za mateka waliowakamata akiwemo Kamanda Amata, Gina na mwingine asiyemjua. Kijasho kilimtoka Madam S, moyo ulimuenda mbio, akanyanyua simu iliyopo mezani na kubonya namba Fulani Fulani,
“Yes, nakuja sasa hivi, kuna ujumbe mzito umetufikia asubuhi hii,” Madam S akakata simu baada ya kuongea maneno hayo, alionekana wazi kuchanganyikiwa kwa hilo, akanyanyuka na kuondoka zake.
Breki ya kwanza ilikuwa katika jengo la wizara ya ulinzi, kwa kasi alishuka katika ngari yake na kuuendea mlango ambao aliufungua bila kubisha hodi, moja kwa moja alikutana na mheshimiwa waziri aliyekuwa akimsubiri kwa hamu.
“Ndio madam,” alimkaribisha huku akiipokea ile dvd na kuelekea kwenye luninga yake, akatumbukiza kwenye chombo maalum cha kusoma dvd hiyo na kutazama,
“…tumesema tumechoka, nah ii sasa ni mara ya mwisho, hatutarudia tena, tunaomba mumuachie huru ndugu yetu, mpigania uhuru mwenzetu mliyemfunga katika gereza lenu la Ukonga, Jegan Grashan. Tuliwapa siku saba lakini sasa tumeona wazi kuwa hamna nia ya kutekeleza ombi letu. Basi kama ilivyo ada kwa kuwa imebaki siku moja na masaa machache, matukio mabaya ya kutisha yatakayoondoa roho za walio wengi yatatukia mara tu mmalizapo kutazama dvd hii, watanzania makumi, mamia kwa maelfu watateketea kutokana na ugumu wa mioyo yenu, muachieni huru kaka yetu nasi tuwaachie nchi yenu, la, damu itamwagika na kamwe matukio haya hayatasahaulika katika historia ya taifa lenu, kizazi hata kizazi. Kama mlikuwa mnajidai na mpelelezi wenu kutuharibioa mipango yetu, sasa ni huyu hapa tunae, hata mumtafute vipi kamwe hamtompata, muachieni Jegan tumuachie Kamanda Amata, siku yetu Julai Saba imefika, nchi itatetemeka kwa hofu na kilio kikuu, lakini utangulizi wa yote mtaupata sasa, kaeni chonjo…”
Ujumbe ule uliishia hapo na mheshimiwa waziri aliona picha ile ya kwa uzuri kabisa, kamanda Amata aliyekuwa hoi bin taaban chini sakafuni, mheshimiwa waziri alionekana wazi akitetemeka.
“Madam, hapa hatuna ujanja, twende Ikulu haraka,” Mheshimiwa waziri aliyasema hayo huku tayari alikuwa ameitoa ile dvd na kushika njia kuelekea nje, gari yake ikaja jirani mara moja, wote wawili wakaingia na kuondoka..

KIVUKONI – DAR ES SALAAM

Honi ya pantoni ilisikika watu walikimbilia na kuingia ndani ya chombo hicho ili wapate kuvuka kutoka Kigamboni kuelekea upande wa pili uliojulikana maarufu kama Ferry. Watu wengi walijaa, wakubwa kwa watoto, wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara, wote wakiwa kwenye michakato ya kuwahi shughuli zao za kila siku, nahodha wa chombo hicho alipoona kimejaa na tayari kuondoka aling’oa nanga na pantoni ikaanza kusogea majini taratibu, kwa mwendo wa madaha.
Katika banda la kupumzikia abiria upande wa Kigamboni, palibaki watu wachache ambao walifika pale dakika kadhaa baada ya kile chombo kuondoka, hivyo iliwapasa kusubiri kitakaporudi.
“Wewe ni msafiri au? Maana naona umekaa hapa karibu dakika ishirini sasa, wengine wakiondoka na wengine wakifika, we upo hapahapa, hapa si kijiwe cha wavuta bangi kaka, kama huvuki basi uondoke hapa,” Mgambo mmoja alikuwa akimsemesha kijana aliyekuwa ameketi katika moja ya vibench vilivyopo hapo, Yule kijana aliomba samahani na kuondoka eneo hilo, mkononi mwake alikuwa na redio ndogo iliyokuwa ikikoroma kana kwamba haipati mawimbi ya sauti, nay eye alikuwa akijaribu kuirekebisha mara kwa mara, akatoka na kuielekea tax iliyokuwa imeegeshwa jirani kabisa na kituo cha polisi, akaingia na kuketi kiti cha nyuma, akageuza shingo yake na kutazama nyuma kule baharini.
Muziki wa Bob Marley, ‘So Much Trouble in In the World’ ulikuwa ukisikika kutoka katika spika zilizofungwa juu ya chombo hicho, kilendelea kukata maji kuelekea Ferry, na sasa kilikuwa katikati ya upande wa Kigamboni na Ferry, watu walikuwa wakitazama mandhari safi ya jiji kongwe la Dar es salaam, wakibadilishana mawazo, hili na lile, wanafunzi wakifikiria kufika mashuleni haraka huku wakiwaza jinsi gani watapata usafiri kutokana na manyanyaso ya kondakta dhidi ya wanafunzi, tabia iliyokithiri katika jiji la Dar es salaam, tabia inayopelekea wanafunzi wa kike kupata mimba ovyo kwa sababu ya urahisi wa usafiri hawana budi kujirahisisha ama kwa madereva tax au makondakta wa daladala, serikali inashindwa kuwatetea katika hilo, ikawahi kuanzisha mradi wa mabasi ya wanafunzi uliokuwa ukiendeshwa na vijana wa chama lakini pesa zote zikaliwa na mradi ulikopotelea si mimi wala wewe tunajua.
Wakiwa katikati ya maji, kitu kisichotegemewa kikatokea, huku walio Ferry wakiitazama pantoni ile ikiwa inakuja taratibu na wale wa Kigamboni wakiiangalia ikiwa inaenda taratibu, sasa zilikuwa zikipishana inayotoka Ferry na inayotoka Kigamboni. Mtu mmoja aliyekuwa akisubiri katika banda la kusubiria usafiri huo upande wa Ferry aliinua mkono wake na kuitazama saa yake iliyomwambia ni saa tatu na nusu asubuhi, aliishikashika saa yake na alipoiachia alishtushwa na mtikisiko mkubwa mkubwa, mlipuko mzito ulioacha kitu kama tetemeko la ardhi la sekunde kadhaa, watu walionekana kutawanyika huku na kule wakiwa hawajui hata wapi wanakimbilia au nini kinawakaimbiza, mji wa Dar es salaam ulizizima kwa kishindo hicho. Moshi mzito, mweusi, uliobebwa na moto mwekundu sana vilionekana katikati ya bahari eneo la kuvukia vyombo hivyo vya usafiri, vilio vilitawala, hakuna aliyejua nini kimetokea.
“Zimegongana! Zimegongana!” wengi walisikika wakisema hivo, “Hapana zimelipuka!” wengine walisikika namna hiyo, kizaazaa. Mamia ya wasafiri walikuwa wakiteketea kwa moto, nani wa kuwaokoa, vyombo vyetu vya zimamoto havikuwa na uwezo wa kufika pale, hakukuna na hata meli ya kusogea kufanya uokozi zote ziliogopa mlipuko kwani nazo zinatumia mafuta. Moto mkubwa ulikuwa ukiendelea kuwaka, pantoni zilikuwa zikiendelea kuteketea na abiria wengi walioko ndani, wenye uwezo walijirusha majini, wengine waliojua kuogelea wakafanya hivyo, wenzangu na mimi walibaki wakihangaika kunusuru pumzi zao za mwisho.
˜˜˜
“Hawa jamaa hatuna njia ya kuwadhibiti sasa, kama Amata aliyekuwa akiongoza operesheni hii nae wamemteka, tutafanya nini?” Makamu wa Rais alikuwa akiongea na wadau wa usalama ofisini kwake katika Ikulu ya Tanzania, aliwatazama mmoja mmoja kwa zamu, hakuna aliyeonekana kama ana jipya katika hilo, Madam S, waziri wa mambo ya ndani, waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa, IGP, Mkuu wa majeshi na kamishna mkuu wa Magereza, kimya kiliwakumba, giza likawatawala.
“Mheshimiwa hayupo, lakini sina budi kufanya maamuzi ya haraka, nitampigia simu na jibu tutatoka nalo sasa hivi kabla hali haijawa mbaya,” makamu wa Rais alipomaliza kusema hayo, aliitazama saa yake ya mkononi na alipoishusha alisikia mtetemo kama kishindo kizito cha kudondoka kitu, picha kubwa zilizokuwako ukutani zianguka na kuvunjika vipande vipande, kisha utulivu ukarejea tena. Jopo lote lililokuwa katika kikao hicho cha dharula lilihamanika kwa kishindo hicho, “Nini?” aliuliza makamu wa Rais, “Bila shaka ni mlipuko mzito umetokea, kwa kishindo hiki, itakuwa ni maili mbili au zaidi,” Mkuu wa majeshi alikuwa akisema hayo huku akinyanyuka kitini, mara simu ya IGP ikapata uhai, akainyakua kutoka mfukoni mwake ili kuizima asiharibu mkutano, lakini alipotazama kioo cha simu hiyo ilijiandika ‘Detective’, akaona ilikuwa ni habari nzito, “Inspector General of police,” IGP aliitikia kwa kujitambulisha cheo chake moja kwa moja, hii ilitokana na uzito wa simu iliyopigwa, simu ambayo inaweza kukaa hata miezi mitatu isipigwe, simu iliyoandikwa ‘detective’, simu nyeti, kwa mambo nyeti.
“Mlipuko mkubwa umetokea maeneo ya Ferry, pantoni zote mbili zimewaka moto kwa mara moja wakati zikipishana,” ilikuwa sauti ya upande pili, “Umesomeka chukua hatua, nafika sasa hivi,” IGP alijibu na kukata simu. Sura yake iliyojikunja ilionekana wzi mbele yaw engine, akawapa ujumbe na wote wakaonekana wazi kuchanganyikiwa, makamu wa Rais akatoa amri ya kufuatailia swala hilo nay eye akisubiri taarifa hiyo.
“Ugaidi,” Madam S alisikika akiongea kwa sauti ya chini, akipigisha viganja vya mikono yake kuashiria ameshindwa afanye nini. Iliwachukua dakika tano tu kufika eneo hilo, hali waliyoikuta ilikuwa tete, wapiga mbizi kutoka jeshi la polisi la wanamaji lenye kituo chake jirani kabisa na Ferry wakishirikiana na kikosi cha jeshi la wanamaji kutoka Kigamboni ‘Navy’ walikuwa wakishirikiana katika uokoaji huku gari za zima moto zikiwa zimefika lakini haziwezi kusogea eneo la tukio.
Vilio vya wenye ndugu vilisikika kila kona, wakati gari za wagonjwa zilipokuwa zikitoka na kuingia kukusanya majeruhi ambao wameopolewa kutoka majini. Siku ilikuwa nzito kwa viongozi wa serikali, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kukutana tena na tena kujadili swala hilo, msiba wa kitaifa.
Madam S alisimama kwenye njia panda ya kuingia Ferry na ile inayokuja Posta ya zamani akiangalia kila kinachoendelea huku akiwa hajui hata wenzake aliokuja naoi wamepotelea wapi, midomo ilimchezacheza kwa hasira, machozi yalimtiririka kwa uchungu, alitamani amuone huyo anayesababisha haya yote ili amfundishe adabu, lakini hakumjua, alimkumbuka sana Kamanda Amata katika sakata kama hili tayari angekuwa amekwishajua fununu za mhusika, maana wakati mwingine alipenda kumuita ‘The black dog’ kutokana na tabia yake ya kugundua vitu haraka, Madam S aliifananisha na kunusa. Hakuwa na uamuzi, ahata alipokuja kushikwa mkono na Chiba kuondolewa eneo lile yeye bado alikuwa hajielewi.
“Chiba, Kamanda ametekwa!” Madam S alimwambia Chiba wakiwa ndani ya gari.
“Unasema?” Chiba aliuliza kwa mshtuko, Madam S akamueleza kwa kirefu sana juu ya ile dvd. Chiba alibaki kusikitika, akachukua kompyuta yake ndogo na kuifungua kisha akaanza kubonyezabonyeza namba Fulani Fulani na kufuatilia aina ya mchoro uliokua unajionesha ukijichora kitu kisichojulikana.
“Unafanya nini Chiba?” Madam S aliuliza.
“Natafuta uelekeo wa micro chip ya Amata labda itaniambia yuko wapi, ili tujue tunafanya nini,” Chiba alimjibu Madam. Baada ya muda mfupi wa Chiba kuchokorachora kompyuta yake, alimgeukia Madam S, “Madam” Chiba aliita, akamtazama Madam ambaye alikuwa amejiinua kutoka katika siti aliyokuwa amekaa katika mtindo wa kujilaza, “Signal, inanionesha Kamanda yupo maeneo ya Bunju,”
“Bunju?!” Madam aliuliza.
“Ndiyo ni Bunju,” Chiba alijibu.
“Ok, fanya unaloweza ujue alipo na ikiweza upange rescue haraka, hawa jamaa inaonekana wameshatuweza kwa kumteka Kamanda” Madam alimwambia Chiba, mara Simu yake Madam S ikapata uhai kwa mara nyingine, akaichukua haraka kutoka katika mfuko wa koti lake na kutazama, private namba, akaifyatua kitufe cha kusikilizia na kuweka sikioni, ilikuwa ni simu inayomhitaji mkutanoni haraka.
“Chiba nipeleke ofisi kuu,” aliamuru Madam S na Chiba alitii amri ya boss wake, akawasha gari na kuingia barabarani, muda mfupi baadae alikuwa tayari mbele ya jingo hilo chakavu la kizamani, jingo la mkoloni, city hall.
“Fanya nililokwambia, kasha nipe mrejesho wa siri,” madam alimwambia Chiba, akashuka na kuingia ndani ya jingo hilo.
“Mimi nilishasema, hawa jamaa watafanya kitu mbaya, tumuachie huyo mtu wao tuishi kwa amnai, sasa tazama jinsi watu wasio na hatia wanavyotekea, tutafakari mara mbili ndugu zangu, sio tunasikiliza ubishi wa mtu mmoja tena asiye na maamuzi kati jopo hili. Yuko wapi sasa? Si hawa wameshamteka!” alilalama Waziri wa ulinzi mheshiimiwa Maige. Wajumbe wa mkutano huo wote walikuwa kimya hakuna aliyethubutu hata kunyanyua mdomo wake, kila mtu alikuwa akimlaumu mwingine ndani ya moyo wake. Mara mlango ukafunguliwa na katibu wa ofisi hiyo, Miranda, na baada yake akaingia bi mkubwa Madam S, akavuta kiti kilichokuwa wazi na kuketi.
“Mi nafikiri, sasa turejee uamuzi wetu, kwa kuwa leo ni tarehe sita mapema hii, kesho tarehe saba wanayomtaka mtu wao, hatujui mi na wewe nini wamepanga kufanya hiyo kesho, ina maana ulinzi uliowekwa haukuwa sawa?” mkuu wa majeshi akauliza, IGP akamtazama kwa jicho baya sana.
“Lazima tujue tunapambana na watu wanaojua medani za vita, wameangalia wapi tumelegeza wametumia nafasi, hatutakiwi kulaumiana ila tunatakiwa tuamue la kufanya kwa kuwa muda ndiyo huo unakwenda na Julai 7 imekaribia.” IGP nae alitoa hoja yake. Mara mlango ukafunguliwa tena akaingia Miranda na karatasi mkononi na kumkabidhi Waziri wa ulinzi, akaitupia macho na kasha akaiweka mezani. “Ripoti ya awali ya ajali hii hapa,” Waziri aliwaeleza wajumbe na kila mmoja aliipitia na kuirudisha mezani.
“Vijana wetu wa Jeshi la wananchi wameng’amua kuwa mlipuko ule ni wa bomu, na bado wanachunguza ni bomu la aina gani, maiti zilizoopolewa ni kama sabini hivi na majeruhi wengi sana wamekimbizwa hospitali,” waziri maige aliangusha machozi alipokuwa akisema hayo. Wote katika mkutano ule walibaki kimya kwa muda. Mara ngumi nzito ya nguvu ikatua mezani mpaka kufanya glass za maji kuanguka na maji kuwalowesha wajumbe, “Nasema hivi Jegan aachiwe mara moja na watu wake waondoke nchini ndani ya masaa kumi na mawili,” Waziri wa ulinzi alitamka kwa hasira, karatasi ikaletwa na akamkabidhi waziri wa mambo ya ndani aandike hati hiyo ya kuachiwa huru kwa gaidi huyo. Madam S aliinyakuwa ile karatasi na kuikunjakunja kasha akaitia katika chombo cha takataka, kila mmoja akamatazama mwanamke huyu aliyeonekena kuvimba kwa hasira mpaka mishipa ya uso ilidinda.
“Tusiamue mambo kama watoto, kwa kutumia hasira, tumuachie!? Na damu za Watanzania hawa zilipwe na nani, na Kamanda Amata yuko wapi? Siafiki, siafiki, lazima tuingie kwenye mapambano ya nkono kwa mkono, kama mnaogopa kikosi changu na mimi mwenyewe tutaingia kazini kuanzia sasa,” Madam S alifoka, baadae kila mmoja akaona usahihi wa maneno hayo. Ulikuwa mvutano uleule ambao ulitokea siku tatu nyuma, kutokuelewana kukaendelea katika hilo. Mwisho wa yote, ikaundwa kamati ya watu watatu ili wakakutane na makamu wa Rais, kutoka kwao watapata lile wanaloona linafaa kuamuriwa.
˜˜˜˜
Sherehe iliendelea katika ukumbi mdogo ndani ya yadi ile ya Bunju, freedom fighters walikuwa wakijipongeza kwa kazi waliyoifanikisha siku hiyo, huku ikiwa tayari kazi ya julai 7 imwkamilika bado kufyatua tu.
“Sasa vijana, tumefikia tamati ya maafikiano yetu na serikali hii isiyo na masikio, leo tumewapa onyo lakini kesho wataiona kazi yenyewe watakapookota maiti zilizokuwa jivu mia kwa mamia, lazima dunia itikisike. Sasa Shakrum, weka kamera yako tayari twende kuchinja wale mbuzi,” Shailan aliwaambia swhaiba zake, kasha wote wakashuka kwenye kila chumba cha chini, chumba walichomfunga Amata na Yule Mkorea, walipofungua hawakuamini macho yao, hakuna mtu ndani. Shailan na wenzake wote wakajikuta wamepigwa na butwaa hawajui watu wale wametokaje mle ndani, kila mtu alimtazama mwenzie, wote wakatoka tena nje na kuufunga mlango ule. Wakatawanyika na kuwauliza walinzi ambao waliwaeleza wazi kuwa hakuna mtu aliyetoka nje, lazima watakuwa ndani umohumo, msako mkali ukaanza kila pembe ya jengo na kila chumba kilichopo ndani humo.
Kamanda Amata na Shasha walikuwa wamejificha katika katika bomba kubwa la maji machafu lililopita chini tu ya chumba hicho walimofungiwa. Amata aligundua hilo baada ya kusikia kitu kama maji yanayotembea wakati alipokuwa amelala pale chini, baada ya kutoka wale jamaa, alijivuta mpaka kwa Yule binti wa Kikorea na kumchomoa pini iliyobana nywele zake, maana alijua wazi kutokana na ile shepu ya pini angeweza kufungua pingu walizofungwa, alipoichomoa kwa meno akaibana hivo na kujaribu kuingiza katika tundu la ufunguo la pingu aliyofungwa ShaSha na kufanikiwa kuifungua, kasha ShaSha akamalizia kufungua zilizobaki pamoja na zile za Amata, katika kutazama huku na huko waligundua kuwa kuna mlango uliozibwa kwa mbao laini, wakautoa uzibo huo kwa umakini sana na kujikuta kwenye choo kingine, wakang’oa sinki lake na kupata tundu la kutosha ambalo chini yake kulikuwa na lile bomba kubwa la maji machafu ambalo lilikuwa limekusanya maji ya mtaa huo. Ijapokuwa ilikuwa ni tabu kupita kwa kutambaa na kupambana na harufu mbaya na chafu lakini hawakuwa na budi kujiokoa kwa njia hiyo. Waliendelea kutambaa humo bombani kwenye hewa nzito sana ambayo kama hauna mazoezi ya kutumia pumzi lazima ufie njiani. Mwendo kama wa lisaa limoja walianza kuona mwanga wa jua mbele yao uking’aa kupitia yale maji, hapo wakapata moyo kuwa sasa wamefika nchi kavu, wakaongeza nguvu zilizokuwa zikipungua muda baada ya muda, walitambaa na kujikuta wanatokea baharini, ShaSha na Kamanda Amata walijikuta baharini, hiyo kwao ilikuwa ni faraja sana waliogelea kidogo kuondoa harufu na uchafu uliyowaganda mwilini, wakaogelea kuondoka eneo lile mpaka mbali penye maji safi, wakatoka nchi kavu na kujitupa kwenye mchanga. Kamanda Amata alimgeukia ShaSha, “Wewe ni nani?” alimuuliza,
“ShaSha, kutoka India” akajibu
“Unafanya nini hapa? Huoni unahatarisha maisha yako?” Kamanda aliuliza
“Nipo kazini,” akajibu kwa kifupi huku akijinyanyua kwenye ule mchanga akasimama wima lakini bila kutegemea alijikuta akipigwa ngwala kali na kudondoka, kabla hajafika chini Amata alaijivingiriha na kumdaka kwa ustadi, akamkumbatia.
“Kuwa muangalifu ShaSha,” akamwambia kasha akamtupia pembeni.
“Tuko wapi?” ShaSha akauliza
Amata aliangalia mazingira yale lakini hakuyajua kutokana na mikoko mingi iliyojaa eneo hilo, akampa ishara ya kuondoka, ShaSha akanyanyuka na wote wakafuatana wakitembea juu ya mchanga huo mweupe wakiwa hawajui wapi wanaelekea. Baada ya mwendo mrefu waliona madau ya wavuvi yakiwa yameegeshwa, wakaendelea kusogea mpaka eneo lile, “Bagamoyo,” Amata alimwambia ShaSha. Kisha akaendelea kutembea mpaka nchi kavu na kuyapita yale madau mpaka kwenye barabara kubwa. ShaSha akajiangalia na kujaribu kujinusa hapa na pale, akaona bado ananuka uchafu, akamnusa na Amata vivyo hivyo. Kamanda Amata alaimshika mkono ShaSha na kutembea taratibu wakapita mitaa kadhaa na kutokea katika hoteli kubwa ya Paradise, wakaingia mpaka kaunta, kila mtu aliyewaona akajishika pua kutokana na hali hiyo, mlinzi wa hoteli alaikwenda kuwazuia lakini meneja akampa ishara ya kuwaacha wafike kaunta.
“Habari Kamanda Amata,” Yule meneja mwenye asili ya kipemba alimsabahi Kamanda
“Si salama, naomba chumba change cha kawaida tafadhali,” Kamanda alitoa oda, na mara moja wakaongozwa mpaka ghorofa ya pili na kukabidhiwa funguo ya chumba hicho. Kabla ya yote kila mtu alijikuta akiuendea mlango wa bafuni wakakutana mlangoni mikono yao miwili ikiwa imekamata kitasa cha mlango huo. Wakatazamana, macho yakakutana, ShaSha akaona aibu akainama chini, Kamanda Amata akiwa bado kashika kitasa juu ya mkono wa ShaSha akakinyonga na mlango ukafunguka, bafu kubwa la kisasa likawakaribisha, wakaingia na kila mmoja akajitupa ndani ya beseni kubwa linaloweza kuwabeba wote wawili, michezo ya kuogeshana ikaanza na kumwagiana maji, kila mmoja akimmwagia mwenzake mwisho Kamanda Amata alimdaka ShaSha na kumvutia kwake, akamtazama usoni kwa tuo, ShaSha akaelewa lugha inayozungumzwa na macho ya Kamanda, vinywa vyao vikakutana, ndimi zao zikacheza pamoja, miili yao ikakutana, viungo vyao vikabadilishana mawazo, wote wawili wakazama katika bahari ya mapenzi.
KAMANDA AMATA ALITOKA ndani ya bafu hilo la kisasa katika hoteli ya Paradise pale Bagamoyo, akiwa na taulo kiunoni mwake alipita kabisa na luninga, akili yake ikamtuma kwanza kuwasha luninga hiyo kujua nini kimejiri huko duniani muda ambao yeye hakuwepo huko. Luninga ile ilimkaribisha kwa moshi mzito uliokuwa ukionekana kwenye kioo chake, akatamani kujua kilichotokea akaketi kwenye kitanda na kukodoa macho akiizama ‘breaking news hiyo’, baada ya dakika tatu za kuangalia habari hiyo alikurupuka kama kichaa, ShaSha alikuwa bado akijivuta kama kawaida ya wananawake wengi, kujivutavuta dio mpango mzima kwao.
Kamanda Amata tayari alikuwa ndani ya suti nyeusi safi iliyomtoa kweli kweli. ShaSha alipofika chumbani alimkuta Kamanda amekwishajiandaa, “Vipi, mi nilijuwa tunakula fungate, mbona mwenzangu hivyo?” ShaSha aliuliza kwa kiingereza chake kilichochanganywa na lafudhi ya kihindi. “Hapana mama hapa ni kazi,” Amata alijibu huku akimuonesha ile luninga pale.
“Tayari, ugaidi umeshafanyika bila kificho na kesho ni Julai saba, lazima niwahi kuokoa jahazi,” kamanda Amata alimalizia kuongea huku akifunga kiatu cha mwisho, akamwangalia ShaSha pale aliposimama, “Twende au utakuja baadae?” akamuuliza.
“Hapana tunaondoka wote, habaki mtu hapa,” ShaSha alijibu huku akinyakuwa moja ya gauni zuri la kibuluu lililokuwa limening’inizwa katika vining’inizio kadhaa vilivyowekwa hapo, wakati yeye anavaa, Kamanda Amata alikuwa akishushia glass iliyojaa pombe aina yaVodka ili akili yake ichangamke vizuri.
Dakika kumi baadae wawili hao walikuwa tayari nje ya hotel hiyo wamekwishakukamilisha itifaki zote. Waliingia ndani ya tax moja ilikuwa imeleta mgeni hotelini hapo, “Bunju tafadhali, karibu na Baobab,” Amata alimwambia Yule dereva, naye akatii bila hata kuuliza. Kutokana na ustadi aliouonesha dereva Yule kwa kuendesha gari, haikuwachukua muda wakafika eneo hilo, ShaSha aliiona gari yake ikiwa imepaki palepale katika ile pub aliyoingia jana yake. Dereva akaegesha gari kwa mbele kidogo, Amata na ShaSha wakashuka, Amata akampa noti za elfu kumi tatu, ambazo alipewa pale kaunta katika hotel ile.
“Ile pale gari yangu,” ShaSha alimwambia Amata, wakatazamana. “Subiri hapa,” Amata alimwambia ShaSha, akachomoa miwani yake na kuipaika usoni kisha akainedea gari ile mpaka pale, akashika saa yake na kuizungusha katika mtindo Fulani, ile saa ikatoa mlio Fulani hafifu, akarudi kwa ShaSha na kumwamru wasonge mbele kidogo.
“Vipi mbona umeiacha?” ShaSha aliuliza
“Imetegwa bomu, haiku salama,” wakatembea mwendo mfupi wakafika kwa jamaa wanaouza na kufyatua matofali, “Subiri hapa,” akamwambia, Kamanda Amata akawasalimu wale vijana na kupita mpaka eneo ambalo wao huwa wanatumia kuteka maji au pi kujipumzisha, pana kijito kilichopita kuelekea baharini lakini kimezungukwa na machaka mengi utafikiri hakuna mtu anayefanya shughuli eneo hilo. Wale vijana wakawa wakimshangaa hawakujua ni wapi anaelekea, “Mheshimiwa choo hiki huku!” mmoja wao alipaza sauti kumwambia Kamanda akijua kuwa kaenda kujisaidia, akapotelea vichakani bila kumjibu yeyote. Aliikuta pikipiki yake ipo salama, akaitazama tena kwa jinsi ileile, akaikuta ko salama kabisa.
Kutoka ndani ya kichaka, wale vijana walishuhudia bonge la pikipiki la Kirusia likiibuka kama kifaru cha jeshi ‘Cagiva’, “Twende zetu” alimwambia ShaSha aliyekuwa kabaki mdomo wazi, kwa wepesi wake alijirusha na kutua katika kiti cha mashine hiyo huku mikono yake akimutana mbele ya tumbo la Amata. Haikuwa mwendo wa kitoto, dakika chache walikuwa wakiipita Boko na kuitafuta Tegeta ambako hawakujali fole za kuja Mbezi mpaka Mwenge wao walipita pembeni pembeni na kujikuta wakifika katika mataa ya Mwenge mapema kuliko walivyotegemea. Muda wote ShaSha alikuwa kimya ametulia katika mgongo wa Kamanda Amata akisikiliza mlio mzuri wa pikipiki hilo.
˜˜˜˜
Shailan bado hakuamini kile ambacho alikishuhudia, Kamanda Amata amewezaje kutoroka kwa jinsi walivyomdhibiti kwa minyororo na kumuweka katika chumba ambacho kwao kilikuwa ni chumba pekee chenye usalama wa asilimia mia moja. Alikuwa amesimama akiangali nje ya nyumba hiyo kupitia dirisha kubwa lililomruhusu kufanya hivyo. Shakrum alikuwa ameketi katika kiti kingine ndani ya sebule hiyo ndogo. “Tunahitaji kikao cha haraka,” Shailan alimwambia Shakrum, Shakrum ahakuhitaji kuhoji aliiendea meza ya mbele yake na kutuma ujumbe kwa wote wanaohusika kukutana hapo mara moja, na haikuchukua muda ndani ya nusu saa wajumbe wote walikuwa wamekwishafika, na kukusanyika katika meza kubwa ya duara, simu zao zote zilikusanywa na kuzimwa maana hakukutakiwa kuwe na mawasiliano yoyote kutoka nje.
“Nimekuiteni, ndugu zangu, sina mengi, leo tumefanya kazi nzuri na tumejipongeza lakini kilele cha pongezi zetu kimeingia shubiri, mateka wetu wametoroka,” Shailan aliwaambia wajumbe. Scolleti alikuwa wa kwanza kushtuka akamtazama Shailan kwa jicho kali, “Na Yule msichana wa Kihindi je?” akauliza.
“Nimesema mateka wetu wote isipokuwa Yule tuliyemhifadhi kule Mabibo,” Shailan aliwaeleza, ukimya ukachukua nafasi yake.
“Sasa hatujui kama hiyo kesho wanatupatia mtu wetu au la, maana hapa nimeanza kupata wasiwasi.” Shailan aliendelea kuongea kwa huzuni.
“Shailan, kama tulivyopanga, kesho kila kitu kipo tayari, tumefanya uchunguzi wetu tumeshajua kuwa tukio tunalolitaka litakuwa ni saa nane kamili, na sisi tumeomba watupatie mtu wetu saa saba kamili, wakichelewa tu tunafanya yetu halafu kuanzia hapo ni mashambulizi mfululizo,” Shakrum alizungumza huku akipigapiga meza kwa ngumi yake.
“Mimi nipo tayari kwa msaada wowote mtakaouhitaji kwa hizo shughuli zote, ila naomba Yule msichana wa Kihindi kihwa chake mniletee,” Scolleti aliongezea.
“Msiwe na shaka, Amata atakuja tu, maana atakuta ujumbe wake kuwa malaya wake yupo huku,” Tajan aliongeza kuwatia moyo wenzake. Basi kikao kikavunjika, na siku hiyo wote waligawana maeneo ya kufanya kazi zao za kuchunguza mambo mbalimbali.
˜˜˜˜
Gina alirudiwa na fahamu zake baada ya kutoka katika usingizi mzito usiopimika, akajigeuza na kujikuta kwenye sakafu baridi, akiwa amelazwa na minyororo mikononi mwake, alijishangaa, alikuwa kwenye nguo ya kulalia tu, hakuelewa kinachoendelea hapo, aljaribu kutazama na kuchunguza chumba kile, kilikuwa kitupu kabisa hakina samani yoyote, wala hakikuwa na picha wala dirisha la kuwezesha kuona nje. ‘Niko wapi?’ alijiuliza, ‘Nimekujaje?’akazidi kuzama katika maswali yasiyo na majibu. Akatulia chini kwenye sakafu baridi na chumba hicho kilionekana wazi kuwa kilikuwa ni ‘cold room’ chumba cha kuhifadhia nyama na vitukama hivyo. Baridi ya chumba hicho ilimuingia mwilini bila huruma, alihisi kuganda lakini hakuwa na la kufanya. Mara akaona kitasa cha mlango ule mzito wa chuma kikifunguliwa kwa jinsi kilivyokuwa kikiinamia upande wa chini, moyo wake ulianza kwenda mbio kwani hakujua anayeingia ni adui au rafiki, akajituliza palepale, mara kijana mmoja mwenye asili ya kiarabu au kihindi lakini alikuwa na ngozi nyeusi iliyokata tama aliingia kwa mwendo wa kunyata kama anayewinda kitu, alimwogopa nani ilhali alikuwa pekee ndani humo. Alisimama na kumtazama Gina aliyekuwa kajikunyata pale katika kona ya chumba hicho, uso wake ukiwa umekutanishwa na magoti yake, gauni lake la kulalia alilovaa lilimwagika chini na kururuhusu mapaja yake manene kubaki wazi, alijua fika kuwa huo ni mtego tosha kwa kijana huyo, Yule jamaa alimfikia Gina na kuanza kumpapasa kimahaba, Gina aliinua uso wake na kumtazama jamaa huyo alienokana kujawa na mate kinywaji kwa uchu wa penzi laharaka haraka, alianza kumshikashika Gina kwa fujo, mara mapajani mara sijui wapi, huku bastola yake akiwa kaiweka pembeni kabisa, Gina alijifanya kujilegeza na kutoa sauti ya kukataa jambo hilo, Yule jamaa alimbembeleza na kumuahidi kumletea chakula mchana huo kwani yeye ndiye alikuwa kwenye lindo, Gina alimtazama tena na tena jinsi suruali yake ilivyotuna.
“Sasa tutafanyaje mapenzi huku nina minyororo?” alimuuliza Yule kijana, badala ya kujibu akawa anachekacheka tu alipoanza kuyaona matiti ya Gina sasa yakiwa nje ya kigauni hicho, Yule jamaa alijipapasa mifukoni na kutoa funguo, akaifungua ile minyororo, hakika penzi kitovu cha uzembe. Alipokuwa akiiweka pembeni ile minyororo ndipo alipokutana na kabali maridadi kutoka kwa Gina iliyopigwa kwa miguu yake miwili, Yule jamaa alikukuruka lakini wapi, alikutana na miguu ya Gina yenye nguvu ya ajabu, baada ya dakika mbili alilegea na kutulia, Gina alimuachia taratibu, akamvua fulana yake na kuivaa yeye kwa haraka kisha akamtoa na suruali, akamuacha humo ndani, akaokota ile bastola na kuuelekea mlango kwa hadhari kubwa. Aliufungua taratibu kwa kuuvuta ndani kisha akachungulia akiwa na bastola yake mkononi, akajitokeza na kujibanza pembeni mwa ukuta huo, akaangalia kwa makini ili agundue ni wapi alipo lakini ilikuwa ngumu maana macho yake yalipambana na ngaxi nyingi hata yeye mwenyewe hakujua ni wapi aweze kupita, pale ambapo moyo ulimtuma ndipo alipoikwea ngazi ya mbele yake kwa haraka mpaka korido ya juu, akaambaa na ukuta na kuipita milango kadhaa, mlango mmoja uliokuwa mbele yake alipotaka kuupita alisikia sauti za watu wakiongea, akasimama na kutulia kusikiliza ni nini hasa walikuwa wakiongea. Gina alitulia pale kama dakika tano hivi alivutiwa na mazungumzo ya humo ndani hata akajisahau kama yupo eneo la hatari.
Kutoka chumba cha usalama katika jengo hilo mtu aliyekuwa akicheza na camera za usalama alikuwa anamuona Gina kila alichokuwa akifanya tangu alipotoka katika chumba cha siri mpaka alipofika hapo, akainua simu yake ya upepo, “Gadi namba sita tafadhali, mateka wetu ametoroka ulinzi, yupo ngazi namba sita katika mlango namba 7 hakikisha hafanyi madhara yoyote, ova” Yule bwana alibonya kitufe kimojawapo katika ile redio yake, “Nimekusoma, linafanyiwa kazi,” Yule mlinzi aliyepigiwa alijibu.
Gina bado aliganda palepale akisikiliza kile kilichokuwa kikizungumzwa mle ndani, akajisahau kabisa, mara alihisi akiguswa begani, Gina akatulia kisha akageuka kwa kasi na kuachia konde moja ambalo lilimpepesua Yule mlinzi akajibamiza kwenye mlango wa chumba kingine, kabala Gina hajamfikia Yule mlinzi akanyanyuka kutoka pale alipoangukia na kusimama wima lakini bunduki yake ilikuwa iko mbali kidogo, kabla hajaichuku Gina aliruka juu na kutua kifuani mwake kwa miguu miwili, wote wawili wakaanguka chini na kishindo kile kikawashtua wale walio katika ule mkutano, wakatoka na kukuta pigano lile, wote kwa pamoja wakamvamia Gina.
Ilikuwa ni ngumu kujitutumua, wakamkamata na kumfunga kamba.
Tajan aliyekuwa katika mkutano huo alimtazama Gina kwa jicho la gadhabu sana, akihema kama mbwa aliyekosa windo lake, alirusha teke likatua shavuni mwa Gina na kumtupa upande wa pili, akamfuta na kumkanyaga kichwani kwa nguvu kisha kuutuliza pale mguu wake. Gina alihisi maumivu makali sana, damu zilimtoka mdomoni, hakuweza kufanya chochote kutokana na zile kamba za mikononi walizomfunga kwa nyuma. Wakamchukua na kuondoka naye.
˜˜˜
Kamanda Amata aliwasili eneo la Kivukoni pale Magogoni mchana ambapo pilikapilika za uokoaji zilikuwa zimekwishapungua ila bado watu walikuwa ni wengi na polisi nao wengi. Aliegesha pikipiki yake na kuteremka akifuatiwa na ShaSha, akavuta hatua kuelekea geti la kuingilia abiria. Ijapokuwa ilikua ni shida kidogo lakini alijitahidi kupenya na hadi kufika ndani ambako miili mingi ya watu waliopoteza maisha ilihifadhiwa, alisimama na kutazama hali ile isiyovumilika, moyo wake ulipata uchungu uliochanganyika na hasira mbaya.
“Kamanda!” sauti moja iliita kutoka nyuma yake, akageuka na kumuona kijana mmoja aliyevalia sare za kijeshi za kikosi cha wanamaji, wakasalimiana kisha akamvuta pembeni, “Okoa jahazi Kamanda, Watanzania wanakufa kama hivi,” aliongea huku akitoa machozi, Kamanda Amata aligundua kuwa Yule kijana ni daktari wa jeshi baada ya kumuona akiwa na Stetoscope (BP Machine) shingoni mwake.
“Usijali dokta, ndio nimefika, tutalifanyia kazi,” Kamanda Amata alijibu, akabaki hana la kusema zaidi ya kusikiloiza vilio na kuangalia miili ile iliyolala bila roho kwa dhambi na ukatili wa watu wachache, ‘Jegan Grashan!’ alijisemea huku akiuma meno alipoinua uso wake macho yake yakautana na ule mnara mkubwa wa kuongozea meli uliojengwa kwa mtindo wa meli pale pembezoni mwa soko dogo la samaki, aliutazama na kuutazama, akili yake ikamwambia kitu, akatoka haraka na kuelekea kwenye ule mnara. Alipigana vikumbo na watu ili apate njia, huku akikimbia na huku akitembea, akafika pale mnarani na kuingia katika ofisi za kwanza pale chini kisha akaiendea lifti na kupanda kwenda juu kabisa, alipofika mlangoni akakuta mlango umefungwa, akajaribu kubofya kengele mara ukafunguliwa na akaingia ndani. Katika kile chumba kulikuwa na vijana wawili na msichana mmoja walikuwa kwenye viti wakifanya kazi zao katika mitambo maalum iliyofungwa ndani humo.
“Karibu, tukusaidie nini?” Yule msichana aliuliza
“Umeiona ile Pantoni iliyolipuka leo?” kamanda akauliza. “Sidhani kama kuna mtu aliye eneo hili ambaye hakuiona,” Yule mwanadada akaejibu. “Sawa, nahitaji kuona kamera zenu za usalama kabla ya tukio na mpaka dakika kumi baadae, tafadhali,” Kamanda Amata alitoa amri. “Mkuu, utaratibu hauendagi hivyo mkuu, hizi ni ofisi za watu,” kijana mwingine akasema lakini kabla hajamaliza alikatishwa na Kamanda Amata, “Sikia we kijana, hicho kiti unachokalia utakiacha sawa, haya ni amri tekeleza ninalotaka haraka,” wale vijana hawakuwa na jinsi, “Shida mheshimiwa funguo hatukai nazo sisi za hicho chumba chenye hizo tv,” Yule mwanadada akaongezea. Kamanda akaupigab teke ule mlango unaoingia kwenye hicho chumba nao ukaachia, akaingia ndani na kuketi kati kiti akazitazama zile tv zilikuwa kama ishirini hivi zikionesha pande tofauti. Akaangali ile inayopiga picha za Kigamboni, Kivukoni akaipata, akarudisha lile tukio nyuma mpaka dakika mbili kabla na kutazama kwa makini. Aliweza kuona jinsi zile Pantoni zilipokuwa zikitoka mpaka zilipolipuka, haikumpa maana sana, akairudia tena na tena, kitu kimoja kikamjia kichwani, aliona wakati watu wote wakiwa wameingia katika Pantoni upande wa Kigamboni kulikuwa na mtu mmoja aliyebaki, ijapokuwa hakuona vizuri lakini alihisi hivyo, ‘sasa hiki kina maana gani?’ alijiuliza, akaona hakuna chochote cha kumsaidia, alipotaka kuondoka, akasita, akakaa tena, kurudisha ile picha lisaa limoja nyuma, na kutazama safari zingine kama tatu hivi za pantoni ile. Sasa aliona Yule aliyedhania kuwa ni mtu bado akiwa ameketi pale tangu safari tatu nyuma, wasiwasi ukamuingia, ‘Kama si msafiri alikuwa akifanya nini pale,’ akawaza hakupata jibu. Akatoka na kuteremka chini bila kuongea na mtu yeyo mle ndani, safari ya miguu ikamfikisha palepale kivukoni, kichwani akiwa na mambo mawili tu lakini kabla ya kuyatekeleza. Akafika kwenye geti la kuingilia pale wanaposubiria abiria, akapenya na kuifikia ofisi ya mkuu wa kitengo, lakini hakuwa ofisini, akauliza baadhi ya watu aliowaona kuwa ni wafanyakazi wakamuitia. Wakiwa wawili tu ofisini mazungumzo yakaanza.
“Unaweza kuniambia mlipuko huu ni wa nini?” Kamanda aliuliza. “Kwa kweli sijui, yaani mi nilikuwa ofisini nikasikia tu kishindo, hata wewe mwenyewe tazama vioo vya madirisha jinsi vilivyovunjika,” akajibu Yule mzee alieonekana tangu machoni kuwa hajui lolote lakini pia mwenye hofu kuu na moyo wa kuchanganyikiwa.
“Sasa sikia, huu ni mlipuko wa bomu, na ni bomu ambalo lilitegwa kwenye Pantoni moja wapo kati ya zile mbili, sasa basi nahitaji orodha ya wafanyakazi wako waliokuwa zamu siku ya jana na leo,” Amata aliongea kwa ukali. Yule mzee akasukuti, akamtazama Kamanda, “Sikia kijana hapa sisi hatuna zamu, tunafika wote na kutoka wote,” akamjibu. “Sawa sasa naomba uniitie wafanyakazi wote hapa ili tuone tunafanya nini kwa pamoja sawa”, zoezi hilo likafanyika mara moja, wafanyakazi walikusanywa wote eneo Fulani, “Wote mpo?” Kamanda akauliza, “Hapana si wote, ukiacha wale waliofariki kwenye ajali ambao ni kama sita hivi hapa sijajua ni nani na nani” alijibu Yule mzee huku akiwa anatokwa na machozi. Kamanda Amata alisogea pembeni na kuonge na OCD wa kituo cha polisi cha kati, akimwambia wale wafanyakazi wopte wapelekwe polisi kuhojiwa haraka iwezekanavyo. Dakika mbili tu gari za polisi zilifika na kuwasomba wote wakaondoka nao. Kamanda Amata sasa alikuwa akifanya jambo la pili, alikiendea kituo cha pilisi cha wanamaji kilichopo hatua chache kutoka Magogoni na kuwaomba wamvushe kwa boti yao ya akiba wakafanya hivyo.
˜˜˜˜
MADAM S alitoka katika kikao na kutokea geti kuu akiwa hajielewi sawasawa baada ya maamuzi yaliyopitishwa katika kikao hicho, waliombwa kukutana tena jioni ya siku hiyo ili kujua nini cha kufanya, wakati huo pia akisubiriwa mkuu wa nchi kufika kwani alikuwa nje kwa ziara ya kikazi.
Chiba alikuwa tayari amefika katika katika eneo hilo na gari yake, akamchukua Madam S, kisha kwa mwendo wa taratibu akaingia barabarani kama anaelekea stesheni ya treni, kisha akakata kulia na kuzunguka mnara wa saa na kurudi barabar ya Samora kuja picha ya askari, “Yes madam,” Chiba alimchokoza. “Nipe habari za Kamanda,” Madam alirudisha mazungumzo kwa mtindo huu. “Kamanda yupo kazini, kama masaa mawili sasa,” Chiba alijibu, “What? Don’t tell me!!!” (Nini? Usiniambie!!!), Madam S alichanganyikiwa kwa jibu hilo, haraka sana akamuamuru Chiba kuelekea Magogoni, walipofika pale hawakumkuta Kamanda, wakaenda kwa mmoja wa vijana wao, akaweleza Kamanda Amata amevuka ng’ambo mara moja. “Tangu amefika ameshafanya nini?” Madam akauliza. “Kiukweli amefika hapa nilimuona anaongea sana na mtawala wa eneo hili mara baadae kakusanya wafanyakazi wote kapeleka polisi, mwenyewe anajua kwa nini, lakini pia nilimuona akielekea kule kwenye mnara wa kuongozea meli.” Yule kijana alijibu. “Ok asante,” Madam akamalizana na huyo kijana kisha akatoka na Chiba na kurudi garini. “Sasa nina amani, kama kamanda amerudi, lakini nampa pole kwa kuwa Gina ametoweka,” Madam S alizungumza wakati alipokuwa akikaa vyema kitini. “Unasemaje Madam? Gina ametoweka?” Chiba akauliza kwa mshangao, “Ndiyo, nimemtafuta sana lakini sijampata na si kawaida yake msichana huyu,” Madam S alimaliza huku akitafuna jojo yake.
Saa moja baadae, Kamanda Amata alirudi upande wa Magogoni, na mara moja aliigundua gari ya Chiba iliyoegeshwa pembezoni kabisa mwa kituo cha daladala akaisogelea na kumuona akiwa na Madam S, akaufungua mlango wa nyuma na kuketi. Madam S aligeuka ghafla na kukutana na Amata, furaha yake ndani ya tabasamu pana haikuweza kujificha. “Pole sana Kamanda,” Madam alimpoza. “Asante Madam, ndio kazi zetu, unapotea kisha unapatikana lakini inapobidi, unapotea kabisa. Madam tuna kazi ngumu sana na hawa jamaa inabidi tujipange vya kutosha, hiyo kesho sijui itakuwaje, mimi usiku huu lazima nifanye kazi ya ziada kuvuruga mipango yao yote, cha msingi ni kwamba nimeshajua kambi zao zilivyo haitanisumbua, leo ni usiku wa kazi Madam, sehemu zote nyeti ziwekewe ulinzi madhubuti,” Amata aliongea kwa jazba. “Sikia Kamanda, we kapumzike kidogo, kisha jioni saa kumi na mbili tunakutana pfisi kuu, uje tafadhali halafu kutoka pale tutapanga kikosi kazi.” Madam S alimueleza Kamanda, Chiba akavuta droo ya dashboard na kutoa kimkebe kidogo, akampatia Kamanda, wakaagana na kila mtu akashika hamsini zake.
§§§§§
“Hatukuwa na jinsi kwa maana watu wetu wanakufa tu, kwa nini tung’ang’anie kukaa na mtu mmoja gerezani wakati mamia yaw a kwetu yanateketea?” Makamu wa Rais alikuwa akiongea Mheshimiwa Rais alipokuwa amerudi ghafla kutoka nje ya nchi kwenye mkutano wa kimataifa wa nchi zinazoendelea.
“Ok, kama mmeona kwa pamoja na watu wa vyombo vya usalama mi sina neno, mtoeni huyo mtu na hao watu wake waondoke nchini ndani ya masaa machache,” Mheshimiwa Rais alitoa amri.
Hakukuwa na lingine zaidi ya kutekeleza lililokuwepo, hati ya kuachiliwa Jegan Grashan iliandaliwa na wanaohusika na kazi hiyo.
Madam S bado alikuwa akiumiza kichwa katika hilo, kwa kuwa ni yeye peke yake ambaye alipinga kuachiwa kwa gaidi huyo hivyo hakuwa na budi kwa sababu Waswahili wanasema wengi wape. Kama alitegemea amri au uamuzi tofauti kutoka kwa mheshimiwa Rais basi haikuwa hivyo kwani uamuzi wake ulipita mlemle ambamo wengine waliamua. Maneno ya Kamanda Amata yalimrudia mara kwa mara akilini mwake, ‘Mkimuachia mi namuua’ lilikuwa likikifanya kichwa chake kutotulia.
Kamanda Amata alichanganyikiwa kutomkuta Gina nyumbani, alipompigia simu hakumpata, akaingia ndani ya chumba ambacho Gina mara nyingi huwa akilala kila ajapo kumtembelea. Kitanda kilikuwa kama kilivyo, kwa jinsi shuka ilivyobakia, Kamanda Amata alijuwa wazi kuwa Gina hakuamka mwenyewe bali alibebwa na kitu au mtu, akatoka na kuingia kwenye kichumba chake cha siri ambacho humuonesha mambo yote yaliyotukia nyuma, akijifungia kwa ndani na kuwasha viscreen vyake na kutazama matukio yaliyopita hasa kwenye chumba cha Gina, ndipo alipoona nyendo za mtu anayenyata, hila zote alizofanya na kumbeba Gina kisha kuondoka naye.
Akajaribu kumsogeza uso wake mtu huyo lakini kutokana na giza hakuweza kumuona sawia ila alijua wazi kuwa watakuwa ni wale wale wabaya wake, alipiga ngumi mezani ya hasira, ‘ama zao ama zangu’ akanyanyuka na kuingia chumbani kwake ambako alichukua silaha zake muhimu kwa kazi za usiku, akilini mwake akiiwaza ile Julai saba 7 ambayo jamaa hao wanajivunia, hakujua kwa uwazi ni nini wanataka kufanya. Mara simu yake ya mezani ikaita, akaiendea na kuinyakuwa mara moja, akaiweka sikioni, hakuongea lolote bali alimtegea mtu wa upande wa pili aseme lolote, alisikia sauti ya mtu anayepigwa na kelele za kilio cha kike, aliitambua sauti hiyo kuwa ni Gina, uchungu ukaushika moyo wake, akauma meno kwa hasira.
“Tunajua kuwa umetutoroka, usalama wa huyu Malaya wako ni wewe kujisalimisha kwetu,” kisha ile simu ikatulia, “Nakuja kujisalimisha kaeni tayari kunipokea,” kisha akakat simu ile.
Kama kuna kitu ambacho Kamanda Amata alikichukia ni dharau kama hizo, aliitazama saa yake, tayari ilitimu saa 11 jioni, akaendeloea kujiweka sawa. Jambo linguine lilimchanganya ni kuwa wapi Gina atakuwa amefichwa, Bunju au kwenye yadi ndogo Mabibo, hakujua, alihisi wazi kuwa anahitaji msaada, msaada wa mtu mwenye akili kama yake, akamkumbuka ShaSha, yuko wapi, hajui. Alikumbuka tu kuwa mara ya mwisho walikuwa wote pale Kivukoni lakini sasa hajui alipokwenda, ‘atakuwa wapi?’alijiuliza bila kupata jibu.
§§§§§
SHASHA baada ya kuona kamanda Amata amegubikwa na mambo mengi pale Kivukoni, akaamua kumtoroka, alitafuta tax na kupata kisha akamuamuru dereva kumpeleka Manyanya hotel, Kinondoni.
Alipofika jambo la kwanza alifungua laptop yake na kuweka flash yake ili ajue kati ya vile alivyovichukua kwenye kompyuta ya Scolleti kama vina tija. Kompyuta yake ikawaka na kuanza kuonesha mafaili mbalimbali, makabrasha na nyaraka anuai za Scolleti. Kati ya makabrasha hayo, moja lilimvutia zaidi lilionesha habari nyingi za Scolleti kote alikokuwa akipita na kufanya mambo yake, siri ya utajiri wake na mipango anayoipanga, kitu kilichomshtua zaidi ni ufadhili wa pesa nyingi anaoufanya kwa vikundi vya wakorofi sehemu mbalimbali za dunia, kuwapa nguvu kufanya mapinduzi ili yeye afaidi mkataba mnono na wao wakishaipindua serikali au wakisha miliki maeneo Fulani. Alianzia huko Thailand mara tu baada ya kutoka India na kuwa mfanyabiashara maarufu. Pale India katika mji wa Bombay alikuwa akimiliki mahoteli kadhaa aliyoachiwa na wazazi wake na kwa kuwa yeye alisomeshwa maswala ya biashara, ndipo alipoweza kuyaendesha mahoteli hayo na pia kujenga mengine makubwa zaidi ya hayo katika miji mbalimbali ya India kama Delhi, Mumbai, Bangalore na mingine mingi. Kama haitoshi aliamua kuongeza mabishara sasa akaingia kwenye maswala ya uingizaji mafuta ndani ya India kutokea Mashariki ya kati, katika sakasaka zake za biashara hizo ndipo siku moja alipokutana na mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Muntazil da Silva, mtu huyo alikuwa ni chotara wa Kihindi upande wa mama na Kibrazil upande wa baba, lakini yeye alikuwa akiishi India na kufanya shughuli zake huko Brazil na Chile.

SCOLLETI
MIAKA 25 NYUMA- BOMBAY, INDIA

ILIKUWA asubuhi ya saa 4:30, katibu wa Scolleti alipompigia simu bosi wake akimwambia kuwa kuna mgeni anayetaka kuonana naye, japokuwa siku hiyo ilikuwa ni siku ambayo Scolleti hakupenda kuonana na wageni lakini ilibidi amkaribishe mgeni huyo baada ya kuwa jina alilotajiwa alilifahamu fika.
“Karibu sana bwana Muntazil,” alimkaribisha huku akiwa amesimama wakipeana mikono.
“Kwanza samahani bwana Scolleti, nimekuja bila miadi lakini nilikuwa na jambo muhimu la kukueleza, kesho mimi ninasafiri kwenda Saudi Arabia kwenye mambo yangu ya kibiashara, lakini nimeona nikualike tufuatane ili nawe ukaone nini tunafanya labda utavutiwa kuwekeza katika nyanja kama zangu,” Bwana Muntazil alimueleza kwa tuo bwana Scolleti. Akiwa kimya huku akiandikaandika katika kitabu chake cha kumbukumbu, aliinua uso wake na kumtazama mgeni wake huyo, “Nakusikiliza, bwana Muntazil,” Scolleti alimwambia mgeni wake. “Sasa ujio wangu hapa ukiachilia mbali kuwa nimeonana na wewe, lakini nilitaka kukuomba kufuatana name, kwani mwenzio nilianza hivihivi kwa mahoteli, mashule, maduka, lakini nikaja kuingia kwenye mgogoro na serikali ya Delhi wakataifisha vitu vyote, ndipo nilipoondoka nchi hii na kwenda kwa mama zangu huko Brazil ambako mjomba wangu alinipa mtaji mdogo tu lakini leo hii nimewekeza kwenye Nyanja nyingi huko America ya kusini, Africa na mashariki ya kati, sasa siku moja na wewe utaangukia kwenye mikono hii hii ya dola, unafikiri utajikwamua vipi, twende huku halafu utaamua,” Muntazil alimshawishi Scolleti kwa kina mpaka Scolleti akakubaliana naye na siku hiyo wakapanga safari.
Siku ilofuata wawili hao pamoja na whudumu wachache walikuwa hewani kwenye ndege binafsi inayomilikiwa na bwana Muntazil wakielekea Saudi Arabia ambako wangekaa siku mbili kisha kuelekea Brazil na Chile kabla ya kurudi India.
Wakiwa Saudi Arabia, Scolleti alijifunza mengi sana huko mashariki ya kati, biashara ya kusafirisha mafuta na kumiliki visima vya mafuta ambayo bwana Muntazil alikuwa akiifanya na ilikuwa ikimuingizia pesa nyingi sana. Scolleti aliitamani sana biashara hiyo ambayo ilimtoa udenda kwa jinsi ilivyoingiza pesa nyingi kwa muda mfupi. “Bwana Muntazil, biashara hii nimeipenda sana, je waweza kunisaidia nami nipate kama si kumiliki basi kusafirisha,” Scolleti alimwambia Muntazil. “Usijali swahiba, hatujamaliza bado, inawezekana ukakutana na biashara nzuri kuliko hii, subiri tumalize ziara yetu kisha utachagua,” Muntazil akmwambia Scolleti. Baada ya siku hizo mbili waliondoka kwa ndege ileile na kutua Chile, ambako walifikia kwenye nyumba ya kifahari yenye kila kitu ndani yake, wahudumu wa kumwaga wakikuhudumua kila utakalo. Scolleti aliushangaa sana utajiri wa bwana huyo, wakati kule India alikuwa akimiliki shule moja tu lakini ilikuwa yakisasa kuliko shule nyingine yoyote katika nchi hiyo. “Muntazil, hili jumba ni la kwako au umekodi?” Scolleti alimuuliza Muntazil. “Bwana Scolleti, nilishakwambia kuwa mimi nimewekeza nje zaidi, hii ni nyumba yangu mwenyewe, na hawa wote ni wafanyakazi wangu wa kike kwa wa kiume nawalipa vizuri kuliko wanavyolipwa serikalini, ndani ya jumba hili nina wafanyakazi mia moja,” Muntazil alimwambia Scoleeti alieonekana kushtuka kwa maneno hayo.
“Mbona hawa hata ishirini hawafiki? Au wanaingia kwa zamu?” Scolleti aliuliza.
“Hapana bwana Scolleti, wote wanaingia muda sawa na wanakaa humu humu hawatoki, asilimia 90 kati yao ni yatima, nimewakusanya na kuwaweka hapa wakifanya kazi na kulipwa ujira mzuri sana,” Muntazil alimwambia Scolleti wakiwa mezani kwa chakula cha jioni. Scoletti alijiona mwenye bahati sana kujifunza hayo yote kwa rafiki yake huyo. Naye alitamani kuwa kama yeye, tamaa ya kujiwekea mali nyingi ikamfika, “Sasa bwana Muntazil, hapa Chile umewekeza katika nini?” akauliza Scolleti. “Hapa nimewekeza kwenye kilimo, nina heka za kutosha za mashamba makubwa ya mimea ambayo kwayo naingiza hela nyingi sana, usiku huu tutakwenda huko, tusubiri helkopta inakuja kutuchukua,” Muntazil alijibu.
Majira ya saa tano usiku, helcopta kubwa ya kisasa ilitua katika uwanja wa jumba lile, Muntazil na mgeni wake waliondoka na kuingia katika helkopta hiyo na kuondoka zao. Safari ilikuwa ni kwenda katika mashamba ya Muntazil yaliyopo kusini mwa nchi ya Chile, katika jimbo la Temuco. Walifika usiku huohuo na kuingia mashambani, mataa makubwa ya umeme yaliangaza kiasi kwamba uliweza kuona kila kitu vizuri kabisa, mahindi manenen yaliyojaza vyema yalilijaza shamba zima. “Muntzail. Mahindi yiote haya unamuuzia nani au unatoa msaada?” Scolleti aliuliza.
“Hapana, kaka, mahindi haya ni jalada tu kitabu chenyewe kipo ndani, twende kwa maana usiku huu huu inabidi turudi Santiago,” Muntazil alimwambia Scolleti kisha wote wakapanda ndani ya kigari maalumu na kuingia nshambani usiku huo wakiifuata njia ndogo inayopita katikati ya mahindi hayo.
Uwanda mkubwa ulikuwa katikati ya shamba lile la mahidi, mimea iliyokuwa na rangi ya kijani iliyokolea ilionekana wazi kuwa katika udongo wenye rutuba nyingi, “Hii ni chai?” Scolleti aliuliza, “Hapana hii ni cocaine,” Muntazil alijibu huku akihamia upande wa pili wa eneo hilo walilosimama. “What? Umesema nini? Au sijasikia vyema?” Scolleti akuliza tena, “Hiyo ni cocaine, nikivuna hapa robo heka tu, nina uwezo wa kujenga mahoteli kama yako yote na zaidi, je unaonaje hii siyo biashara ya kujipatia kipato nawe uwe wa tisa kati ya wale G8?” Muntazil alimwambia Scolleti. Baada ya hapo alimpitisha sehemu mbalimbali na kumuaonesha jinsi wanavyovuna na kuifunga vizuri kabla ya kwenda kiwandani kwa usindikaji na usafirishaji katika maeneo mbalimbali. Walipomaliza ziara yao huko Temuco, usiku huohuo walirudi kwa helcopta mpaka Santiago kwenye jumba lilelile la Muntazil. “Vipi Scolleti mbona upo kimya sana?” Muntazil akamuuliza, “Nafikiria juu yah ii biashara ya kule Temuco, inakuwaje kama serikali ikigundua unachokifanya?” Scolleti akauliza. “Sikia Scolleti, serikali zote duniani zinaongozwa na mwanadamu, na huyo mwanadamu anaongozwa na pesa, na hiyo pesa tunayo sisi, unafikiri nini kinakuja hapa? Mkuu wan chi hii anajua kila ninachokifanya, wana usalama alikadhalika, hakuna lolote, mi nVuna nasindika, nauza kwa wafanyabiashara wengine kisha wao ndiyo wanasafirisha nje, mimi sisafirshi nje nauzia humuhumu ndani na baadhi ya wanunuzi wangu ndio haohao uliowataja, serikali,” Muntazil aliongea kwa kujiamini.
Scolleti aliangalia saa yake ilikuwa ni saa 10:45 alfajiri, alijihisi uchovu sana, lakini ziara yao ilikuwa inakaribia mwisho, wakatoka tena na Muntazil ndani ya jumba hilohilo wakaingia milango kama mitano tofauti kisha wakatokea mahali ambapo wanafungia farasi, Muntazil akaingia na kumuamuru Scolleti kufanya hivyo, kisha akafunga ule mlango. Ndani ya banda hilo kulikuwa na farasi wawili weupe, “Usiku huu farasi wa nini Muntazil?” Scolleti aliuliza. “Hapana hatuchukui farasi, simama hapa,” Muntazil alimwambia Scolleti nae akasimama karibu kabisa na ukuta wa nyuma juu ya nyasi kavu, Muntazil akatoa mfukoni kitu kama rimoti na kubonyeza vitufe kadhaa mara lile eneo likaanza kushuka chini na kuacha wale farasi wakiwa kulekule juu. Mara wakasimama na kutoka kwenye kile kipande kilichowashusha chini na chenyewe kikarudi juu. Muntazil na Scolleti walitembea kwa mwendo wa wastani katika jumba lenye vyumba vingi sana humo ndani. “Scolleti, hapa ndio eneo la usindikaji, wanafanya kazi wanawake tu, kwa hiyo uwe mvumilivu ila kama utamtamani mmoja wao niambie nitampa taarifa atkuhudumia kabla hatujaondoka kisha mimi nitamlipa, usijali, upo tayari?”
Muntazil akauliza. Moyo wa Scolleti ulianza kudunda maana hakujua nini maana ya kauli ya swahiba wake. Mlango ukafunguka, wakaingia na kukaribishwa na mwanadada mmoja mrembo sana mwenye kiuno kilichojigawanya sawia, kwa rijali yoyote hapo lazima apige goti na mwenyekiti wa kijiji hana budi kusimama. Scolleti alipigwa bumbuwazi baada ya kuona wasichana wengi sana takribani thelathini wakiwa wametingwa na kazi katika mashine zao, hakuna aliyeonekana kuongea na mwenzake, nyuso zao zilifichwa kwa barakoa maalum iliyofunika mdomo na pua na kuruhusu macho tu, zaidi ya hapo hawakuwa na vazi linguine, matiti yao yaliyopishana kwa umbo na ukubwa yalibaki nje, viuno vyao ambavyo kila mmoja alikuwa na shepu yake vilionekana wazi, cha namba nane, tano hata namba moja kilikuwepo. Kwa ujumla wasichana wale walikuwa wakifanya kazi bila nguo, uchi wa nyama na walikuwa wanawake tupu. Muntazil alimgeukia Scolleti na kumuona akiwa kachoka ghafla, eneo la chini ya kitovu lilikuwa limetuna kama mtu aliweka kipande cha muhindi. “Scolleti, pole sana, usijali, mmoja atakupoza munkali wako, hapa ndipo tunasindika madawa, hawa wadada hawavai nguo ili kuepusha wizi, maana akitoka na kete moja au tatu tayari anatengeneza pesa ndefu,” akamwambia. Baada ya hapo walitoka na kwenda upande wa wanaume nako ni hivohivo, walipomaliza wakapanda lifti sehemu nyingine na kuja juu katika lile jumba la bwana Muntazil. “Sasa, huyu mhudumua atakupeleka katika chumba, utapumzika na saa tano asubuhi tutaondoka kwenda Amazonia, Brazil ambapo tutakuwa na kikao cha dakika kumi na tano tu kisha tunarudi India.
Scolleti akaondoka na Yule mhudumu mpaka chumba cha ghorofa ya juu, akakaribishwa na kuingia ndani kisha akajifungia mlango kwa ndani, alipogeuka nyuma kukielekea kitanda, lo, alibaki hana la kufanya kwa kile alichokiona kitandani. Msichana mmoja kati ya wale aliowakuta kule katika kitengo cha kusindika dawa za kulevya, Scolleti alikumbuka jinsi alivyokuwa akimtolea macho kwa umbo lake zuri la kuvutia, walitazamana, Scoletti hakuelewa la kufanya lakini alijikuta hali yake imekuwa mbaya huko chini, mapozi aliyokuwa akiweka Yule msichana pale kitandani yalimmaliza Scoletti, akiwa katika kutafakari hayo, yul;e binti alinyanyuka na kumfuata pale aliposimama huku kidole kimoja kikiwa kinywani kikibanwa kwa meno ya mbele ya taya la juu na la chini, Yule msichana akamkumbatia Scoletti huku mkono mmoja akianza kuchezea sehemu nyeti za bwanyenye huyo. Hali ikawa mbaya wakakokotana mpaka kitandani na kubwagana. Scoletti alitolewa nguo zote na kubaki kama alivyo kisha akapewa michezo ya ajabu iliyomtoa jasho na mara nyingine alijikuta akilia kama mtoto.
§§§§§

>>>>>RIO DE JENEIRO

UPEPO MKALI ulikuwa ukipiga kutoka baharini na kuishia kwenye kuta za nyuma zilizojengwa katika ufukwe huo. Kwa wengine ilikuwa ni burudani lakini kwa wageni ambao hawakuizoea hali hiyo ilikuwa ni kero kubwa, kila mara walionekana kugeuza sura zao kule ambako upepo huo ulikuwa ukielekea.
Katika moja ya nyumba zilizopo katika ufukwe huo, kulikuwa na kikao cha watu kumi na mbili kikiendelea katika ulinzi mkali, ulinzi wa siri ambao duru za usalama hazikuujua kama upo hapo.
Muntazil na mgeni wake Scoletti walikuwa wamekutana na watu wengine kumi katika moja ya vyumba vya jengo hilo ambalo ukiliona kwa nje ni bovu kupita maelezo lakini kwa ndani lilikuwa linalingana na hoteli ya nyota tano. Meza kubwa yenye umbo la ovali iliwaunganisha wadau hao, kila mmoja akiwa na chombo maalum cha kuongelea na pia cha kusikilizia, hakuna mtu wa pembeni aliyeweza kusikia mazungumzo hayo isipokuwa tu Yule mwenye vyombo hivyo.
Scoletti alitambulishwa kwa watu hao, nae akajua kuwa kumbe mbele yake amekutana na viongozi wa makundi hatari sana kama Tamil Tiger kikundi cha waasi cha Thailand, Hamas wa Palestina, Gorilla wa Peru na vikundi vingine asivyovijua. Scolleti alikuwa akifuatilia kila linalozungumzwa akagundua biashara haramu ya Muntazil ya kuwafadhili wapiganaji hao kwa pesa na silaha kali za kivita ili waendeleze mapigano katika nchi zao, wadhibiti sehemu nyeti kama zenye madini, mafuta na utajiri mwingine, wakati majeshi ya serikali yakipambana na vikundi hivyo wao upande mwingine wakivuna utajiri ule uliopo katika maeneo hayo. Scoletti alifuataili na kusikiliza, hakuongea lolote wala kushauri, alikuwa akisikiliza taarifa zinazowasilishwa na watu hao huku akisikiliza maelekezo na utekelezaji wa kikauli kutoka kwa Muntazil lakini hakuona hata wakati mmoja Muntazil akimkabidhi mmoja wao bastola au jiwe, alichosikia tu ‘nitawaongezea mabomu ya mkono tani moja,’ wengine akawaambi, ‘Nitawaletea jeep za kivita kumi na tano,’ engine wakaahidiwa kupewa RPG za kutosha na kupewa mafunzo maalumu ya kikombandoo ili kuutingisha utawala wan chi yao. Mara baada ya kujibu matakwa yao hayo sasa ikawa zamu ya wale watu kusema wanachotoa kwa msaada huo, wengine walisema ‘kilo kadhaa za dhahabu,’ wengine ‘makasha ya almasi,’ wengine wakamwambia ‘tutateka sehemu nyingine yenye mafuta ili uendelee kugema na hapo,’. Scolleti aligundua mzunguko mzima wa ulimwengu na matukio yake, akashusha pumzi nzito na kuzifiikiria roho za watu wanaopoteza maisha katika masakata hayo yasiyo na macho.
Kilichomshangaza ni kuwa hakusikia hata sehemu moja wakisema ‘tutajenga shule’ au ‘hospitali,’ haikuwapo hiyo. Baada ya dakika kumi na tano tu kikao hiko kiliisha, na kila mtu akaondoka bila kumuaga mwenzio, hakuna kupeana mikono wala nini.
“Muntazil, hii ni biashara gani?” Scoletti akamuuliza swahiba wake.
“Hivi ndivyo dunia inavyoendeshwa, wewe ukijenga shule wenzio wanakuja kubomoa,” Muntazil alijibu, akakohoa kidogo na kuendelea, “mimi nikifadhili hawa kwa dola milioni thelethini, kwangu zinarudi na kuwa dola milioni sitini na ushehe, ni biashara nzuri sana naipenda sana, nina uwezo wa kuinunua ikulu ya Marekani na kuihamishia Afrika ya Mashariki bila kuivunja,” maneno hayo ya jeuri yalimtoka Muntazil na kumwendea Scoletti. Muntazil akamtazama Scolleti ambaye bado alikuwa ameketi kitini kama aliyepigwa shoti ya umeme, “Swahiba, dunia haina mwenyewe, kila mtu ataiacha, unafikiri matajiri wakubwa wanaojenga mahospitali, au mashule , au vyuo, pesa wanatoa wapi? Changamka kaka, mi nitakuongezea mtaji wa dola milioni kumi, kisha upate kikundi kimoja tu cha waasi ambacho utakifadhili kwa silaha na kila kitu chenyewe kitakupa mzigo wa maana, upo tayari?”
Muntazil alimshawishi Scoletti, kimya kikatawala kati ya hao wawili, wakabaki wakitazamana. Scoletti alitamani kiloa kitu lakini alitakiwa aanze na kimoja. Baada ya mapatano, Scoletti aliamua kuanza na waasi. Kikundi chake cha kwanza kukifadhili kilikuwa ni kikundi cha waasi cha huko Mali, kilichofanya mauaji ya kutaka kuipindua serikalim akiwapa silaha na yeye kupata madini ya aina mbalimbali, pesa ikamnogea, akapata kikundi kingine cha huko Mexico cha kuuza na kusambaza madawa ya kulevya, akajitengenezea hela chafu. Baada ya hapo akajikita katika nchi mbalimbali, kila alipokuwa anajulikana hila zake alitimuliwa kwa masaa ishirini na nne, serikali ya India ikishutumiwa kwa ajili ya huyo raia wake, lakini walifumba macho. Baada ya malalamiko mengio yaliyotishia kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia ndipo walipoamua kumfungia kazi mtu huyo. Scoletti alijikuta Africa, Africa ya Mashariki na kubwa lililomleta ni ufadhili wa Freedom Fighter wanaotokea huko Mashariki ya kati wakija kutekeleza lile wanaloliita vita ya ukombozi, akawafadhili kwan kila kitu wakafanikiwa kulipua balozi za Marekani katika nchi ya Tanzania na Kenya. Bahati mbaya au nzuri wana usalama wa Tanzania walifanya kazi kubwa chini ya idara nyeti, idara ya juu inayoongozwa na mwanamama mahiri kwa kazi za kijasusi, Madam S, na kufanikiwa kumtia mbaroni mlipuaji huyo, Jegan Grashan ambaye amesumbua mataifa mengi na walishindwa kumpata. Kilichokuja kutokea ni kuwa vita ile ya ukombozi ikaamishiwa katika ardhi ya Tanzania, kumkomboa ndugu yao mwanamapinduzi mwenzao. Serikali ya India ikamtuma mwanadada ShaSha kufanya uchunguzi na kumjua kwa undani mtu huyo, kutokana na kuchoka na lawama, ShaSha alipewa kibali cha kuua, “Mkamate akibisha mlipue!” maneno aliyoambiwa na bosi wake wa idara nyeti ya usalama wa Taifa huko India.
§§§§§
SHASHA aliridhika na alichokisoma kwenye makabrasha hayo, akayatuma katika idara ya usalama wa Taifa huko India. Sasa kwake kazi ilikuwa ni moja tu, kumsaka popote alipo ili ikibidi ammalize, ShaSha hakuona haja ya kubishana na kiumbe huyo majinuni. Akanyanyuka na kuliendea kabati la chumba hicho na kutazama vifaa vyake kama vyote vipo katika hali nzuri, alipofungua kabati tu, pande la mtu likatoka ndanii ya kabati hilo na kisu kikubwa mkononi mwake, ShaSha akamuepa kisha akampiga karate hatari nyuma ya shingo yake, Yule mtu alikuwa imara, ijapokuwa aliyumba kidogo lakini alisimama na kurusha ngumi moja nzito ambayo ilikuta ShaSha bado yupo eneo lilelile ikatua shavuni na kumpeleka chini. Yule bwana akjirusha mzimamzima akitanguliza jisu lake lenye hasira ili kumchoma ShaSha lakini alibugi, ShaSha alijiviringa pembeni na kujiinua kwa ustadi kisha kumfumua teke moja kali lililopiga tumboni mpaka Yule bwana akatema damu na kujibwaga chini kama mzigo. ShaSha akasimama pembeni akiwa tayari kwa mashambulizi mengine lakini alichelewa, kutoka nyuma yake kitu kizito kilipiga kisogoni, akayumba na kupoteza fahamu, akaanguka chini juu ya lile jitu la mwanzoni. ShaSha akajaribu kupambana na giza lililokuwa likimfunika macho lakini ilikuwa ngumu, akajikuta akifunikwa na giza hilo kisha kuishiwa nguvu, kimya kikuu kikakijaza kichwa chake, akalala usingizi mzito, usingizi usio na ndoto.
Kelele ya mapangaboi ya helkopta yalikuwa ykisikika katika masikio ya ShaSha, “Vipi ameamka?” alisiki kwa mbali watu wakiulizana, “Bado, lakini si muda mrefu atakuwa ameamka,” sauti nyingine ilijibu, “Akiamka tu, umpeleke kwa boss mambo yote yataishi huko,” ile sauti ya kwanza ilikuwa inaelekeza. ShaSha alihisi maumivu makali sana sehemu ya nyuma ya kichwa chake, alikumbuka kuwa hapo ndipo alipopigwa na kitu kile ambacho hakuwahi kukifahamu mara moja. Aliendelea kujifanya hajapata fahamu ili ajue kinachoendelea ndani hapo, alijaribu kufumbua macho kwa mbali, akagundua kuwa alichokuwa akifikira ni mapanga ya helkopta kumbe ni feni la juu lilikuwa likizunguka huku likipiga kelele kwa ubovu wake.

8
HASIRA zilikuwa zimekitawala kichwa cha Kamanda Amata, aliamua kufanya maangamizi ambayo hayatasahaulika katika historia ya nchi hii, kwanza kwa kitendo cha kuua raia wale kwenye pantoni bila sababu maalumu, pili kwa kumteka Gina, kipenzi chake. Kamanda Amata aliapa lazima kisasi kifanyike na baya zaidi lilikuwa ni lile la kuachiwa huru Jegan Grashan, ilhali yeye alifanya kazi ngumu sana kumkamata mtu huyo aliyeshindikana kila kona ya dunia. ‘Lolote liwalo wacha liwe!’ alijiwazia mwenyewe huku akiendelea kutega saa za mabomu yake kadhaa aliyeokuwa nayo katika yadi ndogo ya freedom fighter pale Mabibo, mabomu kama matano aliyoyatega kiustadi kabisa akikumbuka alichofundishwa kule Cuba.
Alipohakikisha yote kayaweka sehemu sahihi ambayo alijuwa hata yakilipuka hayatawadhuru raia wa pembezoni ila uharibifu utakaotokea katika jengo hilo utasababisha moto mkubwa, hilo alilifanya akihakikisha ndani ya jengo hilo hakuna Gina baada ya kusaka kila chumba na kuhakikisha hayupo, ‘Kesho saa nne’ alijisemea mwenyewe huku akisonya, kisha akatafuta njia ya kutoka katika yadi hiyo, ndipo aliposikia mtu akikohoa nyuma yake, aligeuka kwa haraka na kukutana na dhoruba kali ya mateke ya usoni, japokuwa alijitahidi kuyapangua lakini mawili ya kwanza yalimfikia. Kamanda Amata akarudi nyuma hatua kadhaa na kuepa teke moja kisha kupiga ngumi mbili maridadi zilizotua kwenye korodani za mtu huyo, nae bila kipingamizi alitua chini kama mzigo, Kamanda Amata akakanyaga shingo kwa nguvu zote na kusikia wazi mifupa iliyoshika shingo hiyo ikivunjika, akapiga goti kutaka kumuuliza kitu akakuta tayari mtu huyo hana uhai, akamvuta na kumuhifadhi kwenye jaba kubwa lilillokuwa tupu akalifunika juu yake.
Akatembea kwa hadhari na kufanikiwa kutoka nje ya jengo hilo huku akiwaacha walinzi hawana habari yoyote juu ya lililoendelea ndani. Akatoka na kuiendea pikipiki yake aliyoiegesha kwenye moja ya club za usiku hapo mabibo, alipoitazama saa yake ilikuwa imetimu saa nane za usiku, akaliswasha pikipiki hilo na kuifuata Barabara ya Mandela kuelekea Ubungo, pale akanyoosha na kupita barabara ya Sam Nujoma mpaka Mwenge akapinga kushoto na kupiga gia kuelekea Bunju ambako kuna yadi kubwa kabisa ya jamaa hao, kichwani mwake alijua kwa vyovyote watu hao wamehifadhiwa katika moja ya yadi hizo ili watekeleze mauaji yao. Huku akiwa na mawazo mengi juu ya Gina, akiwa hajui ni wapi atakuwa amefichwa na mashetani hao. Mara saa yake ikaanza kumfinya usiku huo, huku akiwa mwendo wa kasi katika pikipiki lake hilo aliinua mkono na kuiruhusu saa hiyo kutoa ujumbe kwa kuibonyeza kitufe Fulani, saa ile ikaanza kutema mkanda wa maneno, ‘uelekeo wapi?’ ujumbe ulikuwa ni kutoka kwa Madam S, hakuufuatilia kujibu aliendelea kusonga na pikipiki lake, mpaka alipofika eneo husika na kuficha pikipiki lake sehemu kisha kurudi kwa mguu mpaka jengo hilo lililozungukwa na ukuta mkubwa sana. Akafanya analoweza na kuukwea ukuta ule ambao siku hiyo haikuwa mara ya kwanza kwake kuukwea, ilikuwa ni mara ya pili, lakini leo ni kwa shari kidogo.
Alitua chini taratibu bila kushtua hata mbu, akatulia katika hali hiyo kwa sekunde kadhaa, kisha akaanza kutembea na kuuelekea mlango ule aliutumia siku ya kwanza, lo, haukuwa mlango tena bali ulizibwa wote kwa matofali na kupigwa plasta kabisa na rangi nyeupe juu. Sasa hakuwa na budi kutumia mlango wa mbele kuingia ambao ni mlango wa hatari zaidi kwani ulinzi wote uko huko, kwa kuwa alikwishajua kuwa jengo hilo lina camera za usalama kila kona alikuwa tayari amejiandaa kwa hilo. Akaendelea kuvuta hatua ndogo ndogo huku akiwa ndani ya mavazi meusi yaliyomficha kila kitu isipokuwa macho tu ambayo yalifunikwa kwa miwani maalumu yenye uwezo wa kuona gizani. Alitazama na kuwaona walinzi waliokuwa wakitembea huku na huku wakiwa katika doria ya ndani humo.
Akiwa kama paka anayetaka kumkamata panya, Kamanda Amata alinyata taratibu sana kuuendea mlango uliokuwa jirani yake. Lakini kichwani aliona wazi kuwa hatoweza kufikia lengo lake bila ya kuonekana na walinzi hao ambao walikuwa wakiranda huku na huku. Akajibana kwenye tenka moja la mafuta na kumsubiri mlinzi aliyekuwa anakuja upande huo, alipofika tu, alimvuta na kumpatia kabali ya maana, Yule mlinzi hakutoa hata sauti, alilegea na kuwekwa chini kwa upole, kamanda akampigapiga kichwani kumpa salamu ya pumziko la milele, akajivuta tena kwa kupita chini ya tenka lile ambalo lilikuwa limewekwa juu ya vyuma virefu na kuweza kupita bila kuuinama. Mlango ulikuwa umbali wa mita kama mia moja hamsini hivi, lakini katikati ya eneo hilo hakukuwa na kitu hata kimoja, hivyo ingekuwa rahisi kwake kuonekana, hakuna ujanja, alichomoa bastola yake iliyofungwa kiwambo cha sauti na kasha akajaribu kupita kwa kasi katika eneo hilo, lakini kabla hajaufikia mlango, risasi kutoka upande wa walinzi zilisikika, Kamanda Amata alijitupa chini na kusota kwa mgongo huku bastola yake ikianza kazi, shabaha zisizokosa ziliwa maliza walinzi wale wane, ‘Sikutaka kuwaua lakini imebidi’ alijisemea moyoni, kisha Kamanda akanyanyuka na kujificha karibu kabisa na ua kubwa pembeni mwa mlango. Akasikia nyayo za watu wanaokimbia, akatulia na kiliskiliza nyayo hizo, kwa harakaharaka alishajua kuwa wapo watatu.
Mara utulivu ukarejea, hakusikia tena zile nyanyo, nay eye akaendelea kutulia palepale ili kuona kitakacho endelea, akiwasubiri hao waliokuwa wakija upande huo. Kivuli cha mtu aliyekuwa akija kwa mwendo wa kunyata kilionekana kwenye mwanga wa taa kikiibuka kutoka nyuma ya ukuta, Kamanda Amata aliendelea kutulia palepale, akakitazama kivuli kile na kugundua mtu huyo alikuwa na bunduki mikononi mwake, akamsubiri ili ajitokeze waziwazi.
Amakweli, subira huvuta heri, Yule mlinzi aliyekuwa akinyata akajitokeza, bado akiwa katika hali ya kujihami alitazama huku na kule bunduki ikiwa mkononi, Amata nae akajipanga kwa shambulizi la ghafla wakati huo akijua kuwa wengine watakuwa maeneo hayohayo, akaona ngoja asubiri kinachoendelea labda na wengine watajitokeza ili aone ni vipi ataanzisha shambulio lake. Yule mlinzi wa kwanza alipoona utulivu na hajkujua adui yake yuko wapi, akatoa ishara ya mkono kuwaita wengine, mara wale waliobaki wakajitokeza waziwazi tena wakitembea bila woga kuzielekea zile maiti mbili nza walinzi wenzao. “Wamekufa!” mmoja akawaambia wenzake, “Wamekufa?!” mwingine akauliza kwa sauti ya tashwishwi, baada ya hapo wote wakalundikana katika zile maiti wakijaribu kuangalia hiki na kile, “Wamepigwa risasi, unaona majeraha haya?” Yule wa kwanza aliwaambia wenzake. “Sasa mbona hatukusikia mjibishano wa risasi? Mi nimesikia risasi mbili tu za wao,” mwingine alionesa shaka.
“Tumevamiwa,” Yule aliyesimama karibu na Amata, aliyekuwa wa kwanza kujitokeza aliewaeleza wenzake, kisha wakatawanyika kumsaka muuaji, “Hakikisheni mnampata, yumo humuhumu!” akawasisitiza kisha nay eye akachukua nafasi nyingine nzuri ya kumtafuta adui.
Kamanda Amata akawa akicheka moyoni akiwasikiliza kwa kila walilokuwa wakiongea, akwasubiri watawanyike ili aanze kufanya vitu vyake. Alipohakikisha kuwa eneo lile kabaki Yule mlinzi wa kwanza tu, na wakati huo alikuwa ametoa simu akijiandaa kupiga mahali, Amata akaona kuwa hapo hapo ndio nafasi ya kufanya mambo yake, alichomoka kutoka pale alipojificha kwa kasi na kuruka hewani amako miguu yake ilitua mgongoni mwa Yule mtu, simu ikamponyoka nay eye mwenyewe kujikuta akisukumiwa mbele kwa kasi na kujibamiza kwenye gari ya mafuta iliyokuwa imeegeshwa eneo hilo. Kabla hajajiweka sawa Kamanda Amata alikuwa tayari amefika na kumsindikizia kichapo kikali kilichomzimisha jamaa huyo.
Alipohakikisha ametulia, alimsogeza na kumuweka jirani na kichwa cha lori hilo, akamuinua na kumuegemeza kasha akamuashia sigara na kumpachika kinywani mwake kiasi kwamba ukija haraka haraka utasema mtu huyo amepumzika akivuta sigara. Kamanda Amata akauendea mlango na kuuchezea kwa namna ya ajabu, ilikuwa sekunde kadhaa tu alipojikuta ndani ya ujia mrefu, akarudisha mlango nyuma yake na kutulia akiangalia kama kuna kamera ya usalama eneo hilo, alitazama darini hakukuwa nayo wala pembezoni hakukuwa na kitu kama hicho, taa ya mwanga hafifu sana ilikuwa ikiwaka kumulika kijia hicho, ‘Usalama kwanza,’ akachomoa bastola yake na kufumua ile taa, giza likatawala katika ule ujia, Kamanda Amata akaona kijitaa chekundu kikiwakawaka palepale alipoipiga ile taa, akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameng’amua kitu. Akasogea taratibu mpaka eneo lile, kwa akaichika ile kamera iliyokuwa ikining’inia, akakta nyaya zake kasha akaungania ule mweusi na mwekundu pamoja, akafasha shoti sakiti. Fuse inayolinda kamera hizo katika ‘distribution box’ ikaungua kwa kitendo kile na kufanya kamera zote kushindwa kufanya kazi.
Kamanda Amata akaendelea mbele huku akisoma milango iliyoandikwa majina na vyeo vya wahusika, alipofungua chumba kimoja baada ya kingine hakupata anachokitafuta. Katika chumba cha mwisho amako ndani yake kulikuwa na makorokoro mengi, pampu za mafuta na mambo kibao, ndipo alipopata hisia ya kuwepo kwa Gina eneo hilo. Baada ya kupekua na kukagua kila kilichomo, kwa kutumia kurunzi ndogo kama kalamu, aliweza kuiona heleni moja ikiwa chini, akaiokota na kuigeuzageuza, “Gina,” alijisemea kwa sauti ya chini. Akaichukua na kuitazama tena kwa makini, akatabasamu, ilikuwa ni heleni ya Gina, heleni ambayo mara kadhaa alimwambia akijikuta kwenye matatizo kama hayo aidondoshe chini kama ikibidi kuondolewa eneo hilo. Kamanda Amata akaichuku na kuibana sikioni mwake huku kitufe chake cha urembo akiwa amekipachika katika sikio lake kwa ndani, haikuwa heleni ya kawaida, bali mtu alipoivaa ni heleni ila kwenye kazi kama hizo unatakiwa kukifungua kitufe ca urembo na kukipachika kwenye tundu la sikio hapo utaweza kusikizana na Yule mwenye heleni ilobakia na mkfanya mawasiliano bila shida.
SCOLLETI alikuwa katika hatua za mwisho za mazungumzo na watu wake, Shailan, Shakran, Tajan na wengine wawili wakiweka mambo sawa.
“Jamani tayari julai saba imefika, tumejipanga vya kutosha?” Scolleti aliuliza.
“Hapa tuko tayari, kila kitu kimepangwa kwa sababu kuna mambo makubwa mawili, kesho watamfungulia Jegan saa nne kamili asubuhi, hivyo sisi tutakuwa kule kwenye point yetu kama kawaida wakati wa tukio hilo, hawa jamaa nina wasiwasi nao sana, tukijitokeza pale kumchukua Jegan usishangae wote tukakamatika.” Shakran aliwaeleza wajumbe.
“Sikilizeni, mpango upo hivi, Jegan atachukuliwa na watu wa ubalozi wa nchi yake kesho muda huo, sisi kama alivyosema Shakran tutakuwa tayari kwenye point husika kwa ajili ya kuwapa shukrani Watanzania, kikosi cha ukombozi kitakuwa tayari katika bahari ya hindi kwa kutumia boti iendayo kasi ambayo itatufikisha Mombasa kesho jioni,” Shailan alieleza.
Kwa ufadhili alioutoa bwana Scolleti, boti ya kasi kutoka Ugiriki ilikuwa tayari katika pwani ya Pemba ikisubiri utekelezaji wa amri itakayofuata, ili iweze kusogea karibu na Bagamoyo kwa zoezi la kuwatorosha freedom fighters.
Scolleti akatingisha kichwa kuonesha kuwa ameridhika na matumizi ya fedha nyingi alizokuwa amewekeza kwa jamaa hao kwa makubaliano ya yeye kupata mafuta kutoka visima vinavyomilikiwa nao huko Mashariki ya kati kwa muda wa miaka mitano zaidi. Aliendelea kukenua huku akiwatazama mmoja mmoja, “Kwa hiyo leo kuanzia saa nne asubuhi televisheni za Tanzania zitapendeza kwa maua mazuri mtakayorusha kumpokea Jegan uraiani?” Scolleti akawauliza.
“Kabisa yaani kama ulikuwepo,” Shailan akajibu.
“Na vipi kuhusu huyu mwanamke wao?” Scolleti aliuliza akimaanisha Gina.
“Huyo nia yetu tumtumie kama chambo cha kumnasa Kamanda Amata, lakini sijajua mpaka sasa kinaendelea nini, hakuna taarifa katika yadi zote mbili,” Shailan akajibu. Shakrum akainua redio call yake na kuita.
“Yadi moja, yadi moja, ova”.
“Yadi moja tunakupata, ova,” akajibiwa.
“Usalama tafadhali, nipe ripoti, ova”
“Kila kitu salama, hakuna tatizo, ova” akajibiwa kwa kupewa taarifa hiyo ambayo kwa walinzi hao ilikuwa sawa, baada ya hapo aliita yadi ya pili ili kujua nako nini kinaendelea, majibu hayakuwa tofauti, lakini kumbe hakujua kama aliyejibu kutoka yadi mbili alikuwa kawekewa mtutu wa bastola kichwani akishinikizwa kujibu hivyo, shinikizo la Kamanda Amata. “Ok sasa twende kwenye point yetu na tusubiri muda ufike, Tajan utabaki yadi mbili kusubiri kama kutakuwa na lolote, ikiwa hakuna basi saa nne umuue Yule mwanamke kisha uje kwenye point yetu,” Shailan alikuwa akipanga kikosi, akamgeukia Yule mwingine, “Tashrini, wewe utakuwa gereza la Ukonga pale kutujulisha kila kinachoendelea, ukishahakikisha Jegan ameondolewa eneo lile ufuate msafara na uhakikishe amefika ubalozini bila kugundulika, baada ya hapo uje kwenye point, saa tano kamili tutaondoka wote kwenye point kuelekea Mombasa tukiwa na Jegan Grashan, Scolleti kama ulivyopewa maelekezo, ila kwa sasa tunakushukuru kwa msaada wako, asante,” Shailan alimaliza na kila mtu akawa katika hali ya kwenda kwenye kitengo alichopewa.
§§§§§
GINA akiwa amechoka sana, mwilini mwake akiwa na nguo ya kulalia tu, alikuwa chini ya ulinzi mkali, walinzi wanne walikuwa nje ya kibanda alichofungiwa wakizungukazunguka na bunduki zao zilizosheheni risasi zikiwa mikononi mwao huku vidole vyao vikiwa vimepachikwa katika kifyatulio tayari kwa amri yoyote itakayotolewa. Mara sikio la Gina likaanza kupata ukelele wa kitu kama mluzi, kwataabu kidogo akanyanyua mkono na kukifyatua kile kitufe cha heleni na kukipachika sikioni mwake.
“Heyyy!!” akanong’ona, kisha akajibiwa vivyo hivyo.
“Uko wapi Gina,?” Kamanda Amata aliuliza kwa kunong’ona maana huwezi kuongea kwa sauti eneo kama hilo.
“Wamenifunga chini ya ardhi, tafuta mlango uliondikwa ‘Kisima’ ” Gina alitoa maelekezo. Mara Yule askari wa jirani yake akasikia mnong’ono ule.
Akamuendea Gina mpaka pale alipo, akamtazama usoni akiwa kamuinamia.
“We mwanamke, unaongea na nani au umepata kichaa?” Yule askari akamuuliza huku akiwa kamshika kichwani na bunduki yakeikiwa imeshikwa kwa mkono mmoja.
“Naongea na shetani, unataka kumuona?” Gina akamuuliza Yule askari.
“Unaleta upumbavu sio! Akarusha mkono ili amtandike kofi Gina, Gina akaepa lile kofi na kumpiga kichwa askari huyo, akaangukia upande wa pili, Ginaakajinyanyua na kumuwahi koromeo, alimkaba kwa nguvu zake zote,Yule askari alijitahidi kujikukurusha kutoka katikamikonoya Gina ambayoilisukumwa na nguvu za hasira. Yule askari akainua miguuyake na kuidaka shingo ya Gina kisha akamvuta nyuma kwa miguu yake. Gina aliiachia shingo ya askari huyo na kutaka kujinusuruna ile kabali ya miguu toka kwa askari Yule, alipoona kuwa njia hiyo anayotumia ni ya kizamani alijifayatua na kukubali uole mvutonwa ile miguu, akajirusha nyuma na kuchomoka bilatabu katika miguu hiyo, kwa haraka akasimama wima. Kelele za askari wengine wakiitana nakuja upande huo kutoa msaada zilimfikia Gina sawia kabisa, Yule askari pale chini alipotakakujiinua alizimishwa kwatekekali la usoni,akarudi chini na ile bunduki ikamtoka mikononi, Gina akaiwahi na kuimiliki mikononi mwake, akaiweka sawa na risasiya kwanza ikamteremsha askari aliyekuwa juu ya ngazi akiteremka kuja chini, akajibwaga kama mzigo. Gina alianzakufanya kazi ya kujinasua kutoka huko kisimani, akayapita mapipa kadhaa ya mafuta nakutoke upande mwingine.
“Kamanda Amata!” aliita.
“Nakusoma, Gina niko njiani kuelekea huko,” aliongeakwa kunong’ona kama awali.
“Nimedhibiti kisima, usiwe na shaka,” Gina alimpa taarifa Kamanda Amata ambaye alikuwa mbioni kwenda kumuokoa.
Majibizano ya risasi za Gina na wale askari yalisikika wazi kabisa. Gina alijikuta anaingia katika pambano la hatari na askari hao huku akitafuta njia ya kutokea ndani humo.
“Tulia hivyo hivyo mwanamke hayawanimkubwa wewe!” sauti ilitokea kwa nyuma, Gina akageuka wakati akiamuriwa kuweka silaha yake chini na kunyoosha mikono yake hewani.
“Unajifanya komandoo wa kike sio?” Yule askari aliongea huku akimfuata Gina na shotgun yake ikiwa tayari kwa lolote lakini kabla hajamfikia, alipaishwa juu na kujibwaga chini kama gunia jirani kabisa na miguu ya Gina, Gina akainua shingo uso kutazama kule risasi hiyo ya ukombozi ilikotokea maana alijua wazi kama Yule askari angemfikia basi ilikuwa ni kipigo cha mbwa mwizi, akamuona Kamanda Amata kama kawaida yake akirusha karanga moja moja kinywani mwake.
“Kamandaaa!” akaita kwa furaha huku akimkimbilia.
“Ginaaaa!” Naye alijibu wakakumbatiana kwa furaha, kisha wakaanza harakati za kutoka nje, Kamanda alitangulia mbele na Gina alifuata nyuma. Njia ilikuwa nyeupe ya kutokea nje kwani Kamanda alikuwa tayari kafanya kazi kubwa ya kuwateremsha wote waliokuwa hai ndani ya jengo hilo.
Walitoka nje ya jengo hilo na kuuendea ukuta upande wa nyuma, akaikutanisha mikono yake kwa nyuma kwa kuifunganisha viganja.
“Gina kanyaga hapo uruke nje!” akamwambia Gina. Baada ya Gina kuruka na kutua nje ya ukuta huo naye akapanda kiufundi zaidi kisha wote wawili wakatokomea na kuacha maafa katika yadi hiyo, akaenda alipoficha pikipiki yake na kuitoa, akakaa nyuma ya usukani na Gina akatulia nyuma yake.
“Kamanda kabla hujaondoka sikiliza, kuna mpango mbaya sana hawa jamaa wameupanga dhidi ya Watanzania leo saa nne asubuhi, lakini sijajua ni wapi wanataka kutekeleza unyama huo,” Gina aliongea haraka harakakiasi kwamba ilikuwa ni ngumu kwa Kamanda kuipata vizuri sentensi hiyo. Gina akarudia alilolisema akisisistiza kuwa amewasikia wao wenyewe wakiongea katika kikao chao usiku huo. Kamandaa akaitazama saa yake, akaona jinsi ilivyopanga vishale vyake, kile kifupi kwenye namba nne juu kidogo na kile kishale kirefu kilikaribia namba sita, yaani saa kumi na dakika ishirini na kadhaa, akaishusha na kuwasha pikipiki lake kisha akaondoka kwa kasi.

§§§§§

ITAENDELEA
 
Simulizi : Julai Saba

Sehemu Ya Tano (5)

Baada ya kikao cha Scolleti na watu wake kukamilika, Scolleti alibaki peke yake katika ofisi hizo za FK Security Group, alipohakikisha kila kitu kipo sawa na hakuna mtu mwingine mle ndani, akabonya kitufe Fulani kilichofichwa ukutani nyuma ya kalenda, mara mlango mkubwa ukafunguka kwa chini na ngazi ndefu zikaonekana zikishuka, akateremka taratibu na ule mlango ukajifunga nyuma yake. Akalegeza tai yake na kuvuta suitcase yake iliyokuwa kitandani, akapekuwa ndani na kukuta kila anachokihitaji kipo sawa, akapekua hapa na pale na kuweka sawa hati mbalimbali ikiwemo ya kusafiria, tiketi ya ndege iliyokuwa iondoke saa mbili asubuhi ya julai saba kuelekea Nairobi kwa kikao kingine na hao watu wake wa Freedom Fighters. Akafunga mkoba huo na kuingia maliwato, akajiswafi na kutoka nusu saa baadae. Alipohakikisha yuko kamili akaburuza hiulo sanduku lake na kutoka njea kwa mlango mwingine. Kelele za majogoo zilikuwa tayari zikipasua anga kuashiria kuwa kumekucha. Saa kumi na moja alfajiri, Scolleti alishika kitasa cha mlangowa gari yake aina ya Land Cruiser VX, akapakia sanduku lake na kisha yeye mwenyewe kuingia mlango wa dereva. Akaketi tayari kwa kuondoka, mara akahisi kitu baridi kikimgusa nyuma ya shingo yake.
“Tulia, fuata maelekezo ninayokwambia, washa gari na utoke nje ya eneo hili,” ilikuwa sauti nya kike iliyopenya masikio ya Scolleti, haikuwa sauti ngeni. Akawasha gari na kutoka getini akifunguliwa na walinzi kisha akafuata barabara hiyo mpaka katika barabara kubwa ya Bagamoyo karibu kabisa na mataa ya Morocco. Yule mwanamke akamuamuru kufuata barabara ya kwenda Mwenge naye akafanya hivyo, alipoingia tu barabara kubwa kuelekea Mwenge na muda huohuo Kamanda Amata alikuwa akiwasili eneo hilo, akapiga kona kali na pikipiki lake na kuanza kuifuata ile VX kwa maana alikuwa anaifahamu sana. Aliifuata taratibu mpaka maeneo ya Tangi bovu ile VX ikasimama pembeni. Akateremka akiwa mikono yake iko kichwani.
ShaSha nae akateremka chini akiwa kamnyoshea bastola Scolleti.
“Kila kona watu wanalalamika juu yako, nimetumwa kwa jambo moja tu, serikali yako ya India imekuchoka, imechoka kulalamikiwa na nchi rafiki hata kupelekea kuharibu uhusiano wa kidiplomasia kwa ajili yako haya yote,” ShaSha aliongea kwa lugha ya Kihindi, Kamanda Amata na Gina walisimama kwa tahadhari nyuma kidogo ya nguzo kubwa ya chuma iliyobeba tangazo kubwa la Safari Lagera, alikuwa akisikia wanachokiongea alikuwa akielewa kidogo lugha hiyo.
“Siko tayari kurudi India,” Scolleti alijibu.
“Swala sio kurudi India, kwanza hakuna anayekutaka kule, hata mimi nimetumwa kuchukua nafasi ya Israel ambaye anachelewa kuja kwako kutimiza kazi yake, nimetumwa kukuua,” ShaSha aliongea kwa uchungu. Scolleti aliposikia swala la kuuawa akashusha mikono yake na kugeuka mzima mzima na kutazamana na domo la bunduki ya mwanamke huyo.
“We msichana, wenzako hawakuwa wajinga kukutuma, ni kwa sababu ya kimbelekimbele chako tu, nani hapa duniani mwenye uwezo wa kupambana au kumkamata au kumuua Scolleti? Kwa taarifa yako ni Mungu tu, na hata huyo Mungu mpaka leo anajishauri anianzie wapi,” Scolleti aliongea kwa kujiamini huku mikono yake kajishika kiunoni.
“Unajiamini sio?” ShaSha akauliza.
“Sio najiamini, ila nataka nikwambie kitu ambacho wewe hukijui, sikiliza, wewe na serikali ya Tanzania nani mwenye uwezo wa kunikamata? Kama wao wamenipokea na kila mwezi nawapa pesa nzuri iliyotakata viongozi nao wananihifadhi ujue wazi utafia hapa. Kila mtu atakushangaa kusikia umeniua, Watanzania watakushangaa sana na kukupiga mawe,” akasonya, “Toa kibunduki chako hapa,” akaipiga kwa kofi ile bunduki ya ShaSha nayo ikatoka mkononi na kuanguka chini, alipotaka kuiokota tu Scolleti akawa tayari na bastola mkononi.
“No no no no, usijaribu hilo kabisa,” Scoleti alimwambia ShaSha huku akimuelekezea bastola kubwa lenye nguvu, revolver, kichwani mwake, “Kama unataka utajiri we sema, nitakupa pesa na si kunifatafata mimi, mi sifuatwifuatwi namna hii, unanidhalilisha, sasa kwa taarifa yako mimi sikamatiki, na kila anayeifuata harufu yangu lazima nimmalize kama nitakavyokufanya wewe, polisi wengi na wapelelezi wan chi hii na nyinginezo wametajirikakwa pesa zangu, mimi ndio Scolleti Shang’harandha, nakuua halafu ukawaambie kuzimu kuwa chini yaofisi yangu kuna ghala kubwa la silaha za kisasa, sawa?” Scolleti alipomaliza kusema hayo. Aliondoa usalama wa bastola yake, kidole kwenye kifyatulio akakikunja huku akibana meno, ShaSha akajishika kichwani kwa mikono yote miwili akijua kuwa sasa nay eye siku yake imekwisha.
“Aaaaaaaiiiiggghhhh!!!!” Scolleti alitoa ukelele wa uchungu huku ile bunduki yake ikimtoka mkononi, na mkono wa kushoto akijishika kiganja cha ule mkono ulioshika bunduki, damu zikitiririka. ShaSha aliiwahi ile bunduki yake pale chini na kuiweka tayari kutekeleza lile alilotumwa.
“Nani alikwambia kuwa serikali hii inakuogopa?” Ilikuwa ni sauti ya Kamanda Amata akisogea taratibu pale aliposimama Scolleti, “Unajifanya unatoa misaada ya kibinadamu kumbe nyuma yake unafanya maovu makubwa ya kumuangamiza binadamu huyohuyo, sasa leo ndiyo mwisho wa yote haya.”
Kabla Amata hajamalizia kauli yake, ShaSha aliyekuwa sasa hataki kupoteza nukta, alifumua kifua cha Scolleti kwa risasi tatu, bwanyenye huyo akajibwaga chini kwenye vumbi.
“Go Bastard !” (nenda mwanaharamu ), ShaSha aliishusha bunduki yake huku akihema kwa hasira, kisha akageuka na kumtazama Kamanda Amata.
“Sorry Kamanda, najua, labda ulimtaka akiwa hai, lakini nimetimiza nililotumwa, na wakuu wangu wa kazi watapenda kuona picha za mwili huu leo hii ukiwa hauna uhai, lakini asante sana kwa kuniokoa”. ShaSha alimwambia Kamanda huku akimwendea na kumkumbatia kwa nguvu, akampa busu la ulimi. Gina kutoka pale alipo alisonya na kuita “Kamanda!”. ShaSha na Kamanda wakageuka, na kuachana.
“Gina, huyu ni ShaSha, detective kutoka India,” kisha akamgeukia Gina na kumtambulisha kwa ShaSha.
Baada ya kupiga picha kadhaa kwa kamera yake ndogo wakasaidiana na kuupakia ule mwili katika buti la ile VX kisha Kamanda Amata akapiga namba ya dharula, 112, na kuwataarifu polisi juu ya mauaji hayo akijitambulisha kama raia mwema.
Juu ya pikipiki moja wote watatu walitosha na kuondoka eneo hilo. Tayari muda huo watu walianza kutoka majumbani mwao na kuanza shughuli mbalimbali, saa kumi na mbili asubuhi.
§§§§§
9

Pambazuko la
Julai 7

MADAM S alitulia kando ya dirisha lake la ofisini, ilikuwa ni saa moja imepita tangu aingie ofisini asubuhi hiyo, hakujisikia kufanya lolote siku hiyo, mawazo na akili yake yote vilisimama, kwa ujumla alikuwa ni mtu wa mawazo mengi sana. Aliitazama saa yake na kuona bado dakika tisini Yule gaidi aachiwe huru kutoka gerezani. Akainua simu yake na kumpigia kijana wake.
“Chiba, naomba uwe unanipa taarifa yoyote ya kinachoendelea hapo Ukonga mi sijisikii kuja huko kisha tuonane hapa mchana wa leo,” akakata simu. Akabonya namba nyingine na kuweka sikioni.
“Kamanda Amata, saa nne kamili Jegan Grashan anaachiwa huru..” kabla hajamaliza kusema sauti ya Amata iliikata ile ya Madam S.
“Sikiliza Madam! Kwanini tunakuwa waoga hivi, kazi ya kukimaliza kikundi chao inawezekana kabla ya hiyo saa nne, kwa nini mnamuachia mtu ambaye amedhulumu maisha ya binadamu wengi duniani, sikubaliani na ninyi, mkimuachia najua nitachofanya lakini Grasha hawezi kuiacha hii ardhi ya Tanzania akiwa hai,” Kamanda akakata simu.
Madam S alishusha pumzi ndefu na kurudi katika kiti chake akajitupa na kuchukua kitambaa cha kufutia jasho akajifuta uso wake.
Kwa ujumla Madam S alikuwa amechanganyikiwa, hajuila kufanya, mara simuyake ikaita tena, ilikuwa nisimu ya Kamanda Amata, akaitazama na kisha akaipokea mara moja.
“Madam, hao jamaa mnaotaka kumuachia ndugu yao, wametega bomu kama si mabomu katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere pale Sabasaba, taarifa hiyo nimeipata kutoka katika tafutishizangu zausiku wa leo. Naomba kwa amri yako ulishughulikie hilo haraka sana kabla Watanzania wengine hawajapoteza maisha,” kamanda Amata alimwambia Madam S kisha akakata simu na kuizima kabisa.
Madam S, alikiona kiti cha moto, kila alipopiga simu kwa Kamanda Amata haikupatikana, mara alijishika kichwa mara akaijisjika kiuno, aliliendea dirisha kubwa lililo katika ofisi yake linaloangalia barabara kubwa, akatfakari, na kuitaza kalenda yake ya ukutani, Julai 7 iliipamba kurasa ya mbele, siku hiyo ambayo ni mapumziko ya kitaifa Tanzania ilikuwa ni siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya saba saba, maonesho ya kimataifa ya biashara ambayo hujumuisha makampuni makubwa kutoka mataifa mbalimbali, aliwasha luninga yake na kukuta matangazo ya moja kwa moja kutoka katika uwanja huo wa Mwl Nyerere. Mamia kama si maelfu ya Watanzania walikuwa wakizidi kumiminika ndani ya uwanja huo.
Madam S akakurupuka kutoka katika mawazo ambayo yalimchelewesha kutoa maamuzi, akainua simu na kupiga moja kwa moja kambi ya jeshi la Mgulani na kuwapa hiyo taarifa na kuwaomba wasiipuze.

UWANJA WA MAONESHO SABASABA

Saa 2:57 asubuhi

MUDA HUO kila aliye nyumbani alikuwa akitoka kama sin a familia yake basin a marafiki kwenda kujionea bidhaa mbalimbali zinazooneshwa huko katika viwanja vya sabasaba. Tarehe saba mwezi wa saba daima ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi wa kila aina hapa nchini isipokuwa tu wale wenye idara nyeti.
Mambo mengi sana yalikuwa huko kama vinywaji, vitafunwa, bendi mbalimbali za muziki zikitumbuiza katika mabanda mbalimbali ya biashara, michezo ya watoto kama mabembea, treni ndogo ambayo inakuzungusha kuona mandhari ya uwanja huo na kadhalika. Mistari mirefu ya Watanzania ilikuwa ikisubiri kuingia ndani ya uwanja huo asubuhi hiyo, kila mtu alitaka kuwahi kuingia ili akaitumie pesa yake vizuri, ilikuwa ni kawaida kwa kila mwaka kuwapo na tukio hilo. Polisi wenye farasi na mbwa walizagaa tayari kwa lolote maana penye wengi pana mengi.
Siku hii ikuwa mheshimiwa waziri mkuu wan chi aje kutembelea maonesho hayo, hivyo ulinzi uliimarishwa kila kona.
Katika moja ya mabanda yaliyomo humo ndani hili lilionekana kuvutia wengi sana, watu walikuwa wakijazana kuangalia umahiri wa vijana aliokuwa wakionesha katika kukabiliana na majanga ya moto na mambo ya uokoaji. Wakiwa wamevaa maguo yao ya kiung’aa ambayo hayashiki moto, kila mtu alipenda kwenda hapo kujifunza juu ya kujikinga na kuukabili moto, moto na athari zake, aina za moto na jinsi gani ya kumsaidia mtu aliyepatwa ajali ya moto. Kutokana na hilo kila mtu alisogelea banda hilo hilo kuangalia na kujifunza.
§§§§§
Ngrrrrrrrrrrrrrrrr ngrrrrrrrrrrrrrrr, simu iliita kwa fujo katika moja ya ofisi za jeshi Mgulani. Huyu bwana aliyekuwa katika chumba cha mawasiliano alikuwa amesinzia hata hakusikia kelele zote hizo za simu hiyo ya kizamani ambayo ikiunguruma lazima uzibe masikio kwa kelel zake. Akakurupuka kama aliyetoka kufumaniwa, akainyakuwa na kuiweka sikioni.
“Hallo, hapa ni kikosi cha jeshi Mgulani, nikusaidie nini?” aliongea askari Yule.
“Unaongea na idara ya usalama wa taifa, naweza kuongea na mkuu wa kambi?” sauti ya madam S iliunguruma katika chombo hicho. Yule askari akatulia kwa pozi na taharuki, kisha akajibu, “Subiri na usikate simu tafadhali,” alijibu.
Baada ya sekunde chache Madam S aliunganishwa na mkuu wa kambi hiyo, kambi ya Generali Twalipo, taarifa ya tetesi za bomu ilimfikia mkuu huyo, Meja Jenerali Kisanga, naye akapeleka taarifa panapohusika, muda huohuo wakapewa taarifa wataalamu wa milipuko wa jeshi, wakajiandaa na kila kitu kinachohitajika wakaingia kwenye jeep takribani tatu za kijeshi, safari fupi ya kufika eneo hilo ikawadia.
Kila mtu alishangaa katika ule uwanja wa maonesho, wanajeshi kama thelethini wakiwa na vifaa vya ajabu waliteremka na kusimamaisha zoezi la watu kuingia ndani ya uwanja huo, kisha kutoa taarifa kwa wanausalama waliopo humo ndani kuanza kutoa watu wote waliomo ndani ili uwanja huo ubaki mweupe yaani bila watu. Kiongozi wa oparesheni hiyo alitoa amri mara moja watu wote kutolewa nje, msafara wa waziri mkuu ukasitishwa kutoka nyumbani kwake kwenda katika viwanja hivyo, hali ikawa tete, milango ya kuingilia uwanja huo haikuwa ikitosha kutokea, kila mtu alifikiri kuokoa maisha yake.
Wanajeshi waliokuwa na vifaa mikononi vya kuweza kutambua milipuko waliingia ndani ya uwanja huo na kutembea kila mahali kutafuta uwezekano wa kuwepo aina yoyite ya mlipuko.
Counter-IED kifaa maalumu kwa kazi hiyo kinachofanya kazi peke yake bila kushikwa na mtu kilitumwa kuingia katioka uwanja huo, kilikuwa kikitembea barabarani taratibu kikisimama hapa na pale, huku wanajeshi wengine wakitapakaa sehemu mbalimbali. Bado watu walikuwa wakiendelea kutoka katika uwanja huo, ilikuwa ni patashika kweliweli.

GEREZA LA UKONGA

Saa 09:00 asubuhi

GARI za ofisi ya ubalozi wa nchi ya Jegan Grashan ziliingia katika geti la Magereza lililoko upande wa kaskazini mwa ngome hiyo, zikajivuta taratibu kuelekea lango kuu la gereza mpaka kwenye maegesho. Waandishi wa habari kama kawaida walikuwa hapo wakitaka kushuhudia na kupiga picha za gaidi huyo ambaye siku hiyo alikuwa akiachiwa huru. Askari wa KM wa Magereza walikuwepo kulinda usalama kama kuna hatari yoyote itakayotokea.
Kamishna wa magereza, mkuu wa magereza mkoa wa Dar es salaam na wahusika wengine walikutana kwenye chumba maalumu kwa ajili ya kukabidhiana mfungwa huyo. Maofisa wa ubalozi walikuwa pale tayari kumchukua raia wao. Ilikuwa utata mtupu. Jegan Grashan aliletwa ndani ya chumba hicho akiwa na pingu pamoja na minyororo miguuni mwake akasimamishwa sehemu ndani ya chumba hicho hicho.
Saa 09:15 asubuhi
Kamanda Amata, alikuwa juu ya pikipiki lake akielekea Ukonga kushuhudia zoezi hilo, Madam S alikuwa akifunga ofisi na hajui aende wapi, ama sabasaba au Ukonga, alikuwa akijishika kichwa kila mara kujiuliza la kufanya, hali ilikuwa sio nzuri kichwani mwake, mama huyu alijiona kwa siku hiyo moja kazeeka ghafla.
Wakati huohuo, freedom fighters walikuwa tayari kwenye sehemu waliopangiana kukutana, lakini walishangaa wawili kati yao walikuwa bado kufika, wakajaribu kupigiana simu ili kujua kulikoni majibu waliyoyapata yalikuwa tata. Maafa, maafa ni hali iliyowakata matumaini ya kumpata mwenzao, mara kidogo wakapata taarifa ya kuuawa kwa Scolleti hapo wakachanganyikiwa, hawakujua wafanye nini. Shailan aliamua kuwapanga vijana wake upya, akawaita hao wote walio katika yadi zile waende haraka katika point ya kukutania ambapo wenzao wote tayari walikuwa kwenye boti maalumu wakisubiri kufuinguliwa kwa ndugu yao, waondoke naye.
Saa 09:30 asubuhi
Madam S anazinduka, anawasha gari kuelekea Ukonga, ilikuwa ni mapumziko hivyo hakukuwa na foleni barabarani, aliendesha kwa kasi gari yake aina ya BMW, ili awahi tukio hilo, alipuuzia simu zote zilizokuwa zikiita, wakati huo. Akili na mawazo yote yalikuwa kuwahi Ukonga.
Kamanda Amata alikuwa tayari kawasili eneo la tukio, akaegesha pikipiki lake nje ya wigo na kutulia usawa kabisa wa lango kuu, akitenganishwa na barabara ya Pugu na seng’enge iliyolinda gereza hilo, alimuona Madam Salipokuwa akiingia getini na gari yake, Kamanda akatikisa kichwa kuashiria, ‘kazi imeamka’.
Kichwani mwake Kamanda alikuwa na mambo mengi lakini alishindwa afanye nini, Sabasaba aliamini kabisa kuwa JW watakamilisha hiyo kazi ya kuutafuta huo mlipuko, lakini magaidi wengine walikuwa wametoroka na mpaka hapo hakujua wamekwenda wapi, alikuwa akisubiri milipuko aliypitengeneza katika yadi zile ifanye kazi, lakini zaidi alikuwa akitaka kumuona huyo Jegan Grashan akiachiwa huru, akabaki juu ya pikipiki lake huku akili ikiwa imesawajika, haijui jema wala baya.

§§§§§

SHAILAN aliinua mkono wake kutaza saa yake aina ya casio, tayari muda ulikuwa ukiyoyoma, alikuwa akisubiri taarifa ya kutoka kwa Tashrini aliyekuwa pale gerezani, ili awaambie tu kuwa ndugu yao kaachiwa nao waanze sherehe kwa kufungua champagne.
Yote yalikuwa sambamba, vijana wa JW wakati huo kijasho kikiwatoka kusaka huo mlipuko walioambiwa lakini bado walikuwa hawajang’amua chochote, walianza kukata tama, wakisema hakuna mlipuko wowote kwani kila mahali ni salama kabisa, walitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya usalama. Na wao kujipanga kuondoka kurudi kambini.
Chiba na Gina walikuwa wakielekea uwanja wa maonesho ya sabasaba kushuhudia hali ilivyo, wakapata taarifa hiyo ya kuwa kila kitu kiko salama.
“Hapana Chiba, kuna mlipuko kule umewekwa, naamini kabisa, kwa maana walipokuwa wanautengeneza nilisiki amazungumzo yao!” Gina aliongea kwa jazba huku akipigapiga dashboard ya gari ya Chiba.
“Basi mama utavunja gari yangu wakati hata mkopo benki sijamaliza,” Chaba akajibu kwa utani.
Mara Chiba akaitoa gari yake baranbarani na kuiweka pembeni alipokuwa maeneo ya polisi ufundi.
“Vipi?” Gina aliuliza.
“Kuna mawimbi ya kielektroniki ya kigeni kabisa yamepita kwenya kompyuta yangu,” akafungua dashboard ya gari kwa kubonyeza mahali Fulani, kulikuwa na kijikompyuta kidogo, akaingiza nywila zake nayo ikaanza kufanya kazi, akabonya hapa na pale, akaanza kusikia mawimbi mbalimbali ya sauti, huku yakiwa yanajichora kwa mistari ya kuyumbayumba lakini pia yalikuwa yakifanya sauti Fulani. Chiba alijaribu kuiweka sawa sauti hiyo ili aweze kupata tafsiri ya mionzi hiyo, akajaribu na kujaribu lakini ilikuwa ngumu kuigundua kirahisi, akapima umbali inapotoka na inapokwenda kwa kutumia namba maalumu anazojua mwenyewe.
“Gina, kuna hapa kuna kitu hakiendi sawa, nikizungusha antenna yangu, inaniambia kuna mawimbi mapya na mageni yanatokea mashariki kuelekea, range yake sio mbali sana,” Chiba alikuwa akituamia chombo maalumu kilichofungwa katika gari yake, chombo kinachojulikana kwa jina ‘MiniGRAIL’ kinachoweza kunasa mawimbi yoyote ya kielektroniki yanayopita hewani. Chiba akachuku laptop yake yenye nguvu, akapachika vifaa maalumu vya kusikilizia, kisha akamwambia Gina aendeshe gari kuelekea uwanja wa sabasaba.
Saa 09:45 asubuhi
“Jegan Grashan, uliyefungwa kwa tuhuma za ugaidi katika ofisi za balozi ya Marekani, unaachiwa huru na serikali ya Tanzania kwa tamko la Rais wan chi, kuanzia saa nne kamili leo hii utakuwa raia huru. Pamoja nahayo, serikali inakutaka kuondoka nchini ndani ya masaa 12 kwa njia yoyote, na hutakiwi kukanyaga tena ardhi ya Tanzania, iwe wewe, mkeo au watoto wako, imesainiwa jana tarehe 6 Julai na kugongwa mhuri wa Ikulu.” Hati hiyo ‘removal’ ilisomwa na kamishna wa MagerezaTanzania huku akitetemeka, alipomaliza, alimtaka Jegan kusaini mahali Fulani, akafanya hivyo kisha nay eye akasaini pale panapomstahili, wakapeana mikono na zoezi hilo likakamilika, Jegana akatakiwa kuketi chini kusubiri saa nne kamili ili atoke nje ya gereza.
Madam S aliyefika kwa kuchelewa kidogo, alikuta ndiyo wakisoma hiyo hati kutoka Ikulu, akatulia na kushuhudia huyo jamaa akimwaga wino wa kuondoka kama raia huru. Ijapokuwa ilimuuma lakini hakuwa na jinsi, ikishaandikwa na Rais basi haiwezi kubadilika labda abadili yeye mwenyewe.
Japokuwa siku hiyo ilikuwa ni mapumziko lakini pia ilikuwa siku ya maombolezo ya watu waliopoteza maisha kwenye pantone eneo la Kivukoni siku iliyotangulia.

§§§§§

Gina aliegesha gari nje ya uwanja wa maonesho ya biashara ‘sabasaba’ Chiba akashuka na kompyuta yake akawa akieelekea ndani ya uwanja huo. Moja kwa moja akiongozana na Gina walifika kwenye banda kubwa la maonesho, banda la zimamoto, liliandikwa kwa nakshi nzuri, FK SECURITY and FIRE BRIGADE, banda hilo lilijawa na watu kama mwanzo wakiangalia hayo maonesho ya uokoaji. Chiba alipofika eneo hilo, akaingia ndani ya ofisi kubwa iliwekwa vitu mbalimbali, sasa akagundua kuwa yale mawimbi aliyoyanasa yanaishia hapo kati banda hilo. Akavua makorokoro yake na kuyaweka mezani akachukua simu yake na kubofya namba flani.
“Chiba anaongea,” alizungumza mara tu baada ya simu ile kupokelewa na Madam S,
“Ndio Chiba niambie,” Madam S alimwambia.
“Kuna mawimbi ya kielektroniki nimeyagundua katika mtambo wangu, na nimeyafuatilia sasa nipo hapa uwanja wa sabasaba, nina wasiwasi na banda hili la FK Security maana signal zinaonesha kuwa hapa niliposimama ndio point ziro, nipe mamlaka nifanye kazi inaonekana kuna hatari kubwa sana eneo hili,” Chiba alimaliza. Kila mtu aliyekuwa ndani ya banda hilo alimshangaa Chiba, hakumuelewa ni nini alikuwa akisema.
Madam S, alijikuta akidondokwa na simu mikononi, akiwa kapigwa na bumbuwazi, akili ikamchanganyika, akamtazama Jegan pale kwenye kiti, kisha akaiokota simu yake.
“Fanya lolote kuzuia hali hiyo,” Madam S alijibu, kisha akapiga namba ya Kamanda Amata na kumpa taarifa hiyo, akatoa tena taarifa Jeshini kwa mara nyingine.

§§§§§

Shailan, Shakrum wakiwa ndani ya boti wakimsubiri Jegan, muda wao ulikuwa umefika wa kile wanachokiita ‘kutoa shukrani kwa Watanzania’, Shakrum alifungua briefcase yake kubwa na kuanza kubofya hapa na pale akipanga renji na kila kitu, kisha akawasha kuitafuta sakiti aliyoitengeneza ndani ya tanki la mafuta lakini lililojazwa gesi aina ya methane upande mmoja na mwingine liquefied petroleum gas (LPG), vyote vilikuwa vimeshindiliwa kwa mkandamizo mkubwa sana kiasi kwamba zikidaka moto basi ilo tanki lote lazima ligeuke kombora baya kuliko kombora lenyewe.
Shakrum alipofanikiwa kupata uelekeo wa sakiti hiyo na kuanza kuhesabu muda wa kuiwasha ili itengeneze moto ndani ya tanki hilo, tayari Chiba alikuwa ameyanasa mawimbi hayo, hivyo alichokifanya hapo sasa ilikuwa ni jinsi gani ya kuyakata, ili kusiwe na mawasiliano kati ya vitu hivyo viwili. Chiba akaendele kucheza na kompyuta yake, ilikuwa ngumu kuelewa ni nini anakifanya kwa ni ni namba tu zilizokuwa zikonekana kupishana na katika kioo cheusi cha kompyuta. Kwa kutumia program maalum kwa kazi hiyo ambayo Chiba aliipata wakati akiwa katika mafunzo huko NASA alifanikiwa kuyakamata mawimbi yale na kuyafanya yasitende lililokusudiwa, kisha akaanza kufanya ukaguzi sehemu mbalimbali za jengo lile.
“Oooh shiiit!” Shakrum alionekana wazi kuchanganyikiwa kwa hilo, aligundua kuwa kuna muingiliano wa mawimbi umetokea, kila alipojaribu bado alijikuta anakwama, nywele zikamsimama.
“Washenzi wameyaingilia mawimbi yangu,” akamwambia Shailan.
“Inawezekanaje?” Shailan akauliza. “Itakuwa kuna mtaalam wa mambo haya ndiye kafanya hili” Shakrum akajibu.
“Sasa tutafanyaje?” Shailana akauliza.
“Hatuna jinsi kama inawezekana hapa ni kufika eneo husika na kutumia mbinu nyingine, mbinu mbadala ya kulipua lile tank bila ya sisi kudhurika,” Shakrum alieleza huku akiisogeza kompyuta byake pembeni, akakizungusha kiti na kugeuka walipo wenzake. Mara simu ya Shailana ikaita, alipoitazama ilikuwa namba ya Tashrini, akajua mambo yameiva, kwa vyovyote vile.
“Ndiyo Tashirini, nipe taarifa,” Shailan alizungumza kwenye simu.
“Jegan yuko huru na sasa anatoka gerezani, nasikia kelele nyingi za wafungwa wengine, zikimsindikiza nje,” Tashrin akajibu.
“Mungu mkubwa, kamwe hamtupi mja wake, hii ndiyo njia pekee ya kuwashinikiza hawa wanaojipendekeza kwa mataifa ya Maghalibi,” Shailan alijibu huku wengine wote wakishangilia.

Saa 04:00 asubuhi – Gereza la Ukonga

JEGAN Grashan aliachiwa huru, hakuwa na pingu za mikono wala za miguuni. Alitembea kwa hatua zake mwenyewe ijapokuwa alikuwa na uchovu kidogo. Madam S na wakuu wengine waliokuwa pale, walimshuhudia gaidi huyo akiondoka taratibu katika gereza hilo, akipita katika mlango mkubwa na kuelekea katika gari la ubalozi lililoandaliwa huku akisindikizwa na maofisa usalama wa ubalozi wa nchi yake, akaingia na kufunga mkanda sawia, akashusha kioo na kumuonesha Madam S alama hya mkono akiashiria kuwa amemtukana tusi baya kabisa, ile gari ikaondoka. Msafara wa gari nne zenye namba za njano kwenye kibao cha kijani zililiacha geti la gereza na kushika barabara ya Nyerere kuelekea mjini.
Kamanda Amata akawasha pikipiki lake na kuvaa kofia yake ya usalama iliyomficha uso wake, moyo wake ulijawa na gadhabu ya kuachiwa huru Jegan, hakupenda hata kidogo. ‘Liwalo na liwe,’ akajisemea na kuaca kati yake na wao magari kama sita hivi kisha akaingia barabara ni na kuondoka.
Uwanja wa maonesho sabasaba
Gina alisikia mlio wa beep kutoka eneo Fulani lililokuwa na matanki makubwa kwa ajili ya maonesho ya kampuni hiyo.
“Chibaaaa!” akamwita kwa ukelele, Chiba akaacha kompyuta yake na kukimbilia kwa Gina, akausikia mlio wa beep hiyo, haraka sana akapanda juu ya tanki moja na kulifungua kwa shida mfuniko wake, ule mlio ulikuwa ukiongezeka. Wakati hayo yakitukia, polisi waliokuwemo uwanjani wakisaidiana na vijana wa skauti kutoa watu nje ya uwanja, na kuwaweka mbali na eneo hilo, vijana wa jeshi walirudishwa tena kuhakikisha usalama huo.
Chiba alikuwa akifungua ule mfuniko kwa tabu maana aulifungwa kwa kifungo maalum, haikuwezekana kukata kwa gesi maana unaweza ukasababisha mlipuko usio wa lazima.
§§§§§
Kamanda Amata akiwa tayari kwenye pikipiki yake aliingia barabara ni, nyuma ya msafara wa gari zilizombeba Jegan, kichwa chake kilishatawaliwa na gadhabu mbaya juu ya mtu huyo, hakuamini kabisa kuwa anakuwa huru na kuacha uovu wake, hapana, bali aliamini wazi kuwa bado maadamu yupo hai basi ataendelea kufanya yale anayokusudia kwa raia wengine wasio na hasira, alivuta mafuta na kutafuta sehemu nzuri ambayo angeweza kufanya yake, kufanya lile alilokusudia. Kama unavyojua kasi ya gari za ubalozi haikuwa ya kawaida, yakiwa yamewasha vimulivimuli na kupishwa yalikuwa yakienda kasi kwelikweli. Mara saa ya Kamanda ikaanza kutoa kamlio hafifu, akauinua mkono na kuisikiliza inasemaje.
“Kamanda Amata, Chiba hapa,” alikuwa ni Chiba aliyekuwa akimpigia Kamanda wakati huo.
“Nimekusoma chiba endelea,” kamanda aliirusu simu hiyo.
“Nipo, uwanja wa maonesho wa sabasaba hapa Mtoni Mtongani,” akaendelea kusema.
“Endelea,” Kamanda akamruhusu aendelee kuzungumza.
“Kuna aina ya mlipuko ambayo imetegwa hapa, sasa najaribu kutafuta chanzo lakini naona kidogo utaalam unaniishia, pamepekuliwa kwa mitambo ya kisasa lakini hakujaonekana bomu wala kitu kinachofanana na hicho, nipe aidia mpya tafadhali,” Chiba alieleza lile linalomsibu.
“Ok, jaribu kutazama mitungi ya gesi kama ipo maana nayo inaweza kufanya milipuko mibaya kuliko bomu lenyewe, hakikisha kwa amri yako umeclear eneo lote ili kama itabidi kufa basi ufe peke yhako kama kiapo chetu kinavyosema, niko njiani kuja huko huko, Jegan Grashan amekwishaachiwa huru,” Kamanda Amata alimjibu na kukata simu ile kisha akarudisha mkono kwenye usukani wa pikipiki na kuongeza kasi zaidi na zaidi, alikuwa akipita gari kwa overtake za hatari mpaka madereva wa magari walikuwa wakitukana kila mtu kwa lugha yake. Dakika mbili baadae aliziona zile gari za ubalozi zikiwa kasi katika eneo la Karakana karibu na Tazara, sekunde chacahe akawa ameufikia msafara huo.
‘Mtu wenu anaachiwa ninyi bado mnataka mtulipue, sasa leo ama zangui ama zenu,’ Kamanda alijisemea huku akiupita ule msafara kwa kasi na kuwa mbele yake. Kisha kama mtu aliyepagawa alikunja kona kali na kuwa mbele yao, zile gari nazo zikafunga breki kali mbele ya pikipiki hiyo zikisota na kufanya ukelele mkali kwa msuguano wa tairi za barabara, gari mbili za nyuma ziligongana zenyewe kwa zenyewe na ile ya mbele almanusura imgonge Kamanda ambaye tayari alikuwa na bastola mkononi, alikwishaiondoa usalama na alikuwa akiitafuta shabaha yake anayoitaka. Kidole cha shahada kikaitekenya ile bastola, risasi tatu zilipasua kioo na kufumua kifua cha Jegana Grashan.
Muda na saa hiyohiyo
Milipuko mikubwa ilitokea katika maeneo mawili tofauti, mmoja katika yadi ya Bunju ya kuhifadhia mafuta iliyokuwa ikimilikiwa na Scolleti nay a pili yadi ya Mabibo, kwa nukta na sekunde ileile mabomu yaliyotegwa na Kamanda Amata yalifanya mambo yaliyokusudiwa.
Mji wa Dar es salaama ulipatwa na hekaheka siku hiyo kwani barabara ya Ally Hassan Mwinyi ilifunikwa na gari za zima moto na ile ya Mandela nayo vivyo hivyo. Moshi mkubwa ulitanda anga ya Dar es salaam. ‘Kama walijifan ya wao magaidi basi hawakujua kama na mimi ni gaidi zaidi yao,’ Kamanda alijisemea huku akipita vitongojo vya katikati vya wilaya ya Temeke, akafika mahali kulikuwa na nyumba nyingi zilizobanana, Kamanda Amata alipinda kona na kuingia katika ua wa nyumba hiyo, moja kwa moja akaiegesha pikipiki yake kwenye stoo ndogo ya mkaa, akaizima, akina mama waliokuwa wakifua na kuosha vyombo walipiga kelele na kuwanyakua watoto wao.
Kamanda Amata akashuka na kuvua ile kofia ngumu akaipachika juu ya kioo cha kutazamia nyuma, akavua yale mavazi ya kuendeshea pikipiki na kuyaweka pale juu, akabaki na suti safi nyeusi iliyopambwa na tai ya buluu, hakuongea na mtu alitoka haraka na alipofika nje alipanda tax aliyoikuta barabarani.
“Sabasaba tafadhali,” alimwamuru dereva.
§§§§§
Watu wa usalama wa ubalozi walijitahidi kumsaidia Jegan Grashan lakini walichelewa, ilikuwa ni mvurugano eneo lote, wamachinga walikimbia huku na huku , wakiijaribu kunusuru maisha yao.
Wanausalama wa ubalozi hawakuwahi kumkamata Kamanda Amata kwani tayari Alishakwisha waacha mbali. Wakabaki wakitizamana hawana la kufanya.
Muda si mrefu, Land Cruiser moja nyeusi ilipunguza mwendo katika eneo hilo la ajali ambapo polisi wa usalama barabarani alikuwa tyari yuko kazini na wale maofisa wa ubalozi wakiwa wamezagaa nje na bastola zao mikononi. Kioo cha gari ile kikateremka taratibu, Madam S, akatzama lile tukio, akatikisa kichwa chake na kupandisha kioo kisha gari ikaongeza mwendo na kupotelea mjini.
§§§§§
Habari mbaya zilimfikia Shailan na Shakrum waliokuwa katika boti wakisubiri wenzi wao ili watoroke na kuwaachia Watanzania vilio vikuu ndani ya siku wanayoipenda, siku ya Julai saba. Shailana alihisi kuchanganyikiwa, kwanza kwa habari ya kifo cha Scolleti, pili milipuko ya yadi zote mbili, haikumuuma sana kwani si mali yao, ila hili la kifo cha Jegan Grashan, Shailan na Shakrum walilia machozi huku wakiwa wamekumbatiana, na walikuwa hawajui hatima ya wenzao waliokuwa katika yadi hizo ambao walikuwa wakiwasubiri pamoja na Tashirni aliyeleta taarifa hiyo. Shakrum akaiendea televisheni na kuiwasha, hakukosea, kioo kilikuwa kimepamba kwa maua ya moshi mzito na wakati mwingine kwa tukio la Kalakana pale Tazara, hasira akazima Tv na kurudi kwenye kompyuta yake, akaketi lakini alipojaribu kuichezea akakuta imefungwa kwa codes maalum ambazo hakujua ni nani aliyefunga, “Shiiiiiittttt!” akapiga ukelele nan kuipiga ngumi ile kompyuta.
Shakrum na Shailan hawakuwa na la kufanya, walitamani waondoke peke yao lakini hawakuona vema, akaendelea kusubiri wenzao mpaka muda waliopanga.
Saa 4:30 asubuhi
Simu ya Kamanda Amata ikaita tena wakatyi akiwa maeneo ya Tandika kuelekea sabasaba, akaitazama, Madam S, akatabasamu, ‘Lazima kapata salamu zangu pale barabarani’ akajiwazia.
“Kamanda, upo wapi?” akauliza kwa ukali.
“Nipo Sabasaba Madam vipi?” Kamanda akajibu.
“Hivi we una akili kweli?” Madam akafoka kwenye simu.
“Kwanini Madam? Nina akili timamu kabisa,” Kamanda akajibu.
“Unajua unachokifanya wewe? Sasa umeshaharibu na we mwenyewe unalijua hilo,” Madam akaendelea kufoka kwenye simu.
“Madam tutaongea ofisini mi nipo kazini kwa sasa,” Kamanda akajibu na kukata simu.
Madam S alikasirishwa sana na kitendo alichokifanya Kamanda Amata, alipopita katika eneo lile la tukio na kuona hali halisi alijua wazi ni Amata kwa sababu alikwishasema mbele yake na alishakula yamini juu ya hilo. Alijua nini kinakuja kumkuta Amata, Madam alilia machozi kwa hilo, alisikitika na kuumia sana, lakini lilikuwa limekwishatokea, hakukuwa na jinsi. Aliendesha gari yake taratibu kuelekea uwanja wa maonesho ya sabasaba.
§§§§§
Chiba alifanikiwa kuufungua mfuniko wa tanki kubwa la gesi, kosa moja alilolifanya ni kuwa hakujiandaa kwa hali hiyo, ijapokuwa aliipata sakiti iliyofungwa chini tu ya mfuniko huo lakini yeye mwenyewe aliathirika sana na ile gesi mbaya. Gina alimshuhudia Chiba akianguka kutoka katika lile tanki kwa msukumo mkubwa sana, akajishika mdomo kwa kiganja cha mkono wake, akili ikaja haraka, akageuka huku na kule, na kuona kabati lenye gas mask, akalivunja na kuchukua, akaivaa haraka kisha akakimbilia kule aliko Chiba akiwa na mask nyingine iliyojazwa hewa ya oksijeni na kumvika Chiba.
“Msaada!” alipiga kelele ndipo vijana wa jeshi walipoona jambo lile, nao haraka wakawahi mask na kwenda kufungaa mfuniko wa tanki lile kwa tabu sana kwani mkandamizo wa gesi ulikuwa ni mkubwa hivyo mvujo wake nao ulikuwa wa nguvu sana. Bkutokana na ujasiri na ukakamavu wa vijana hao walifanikiwa kuufunga na kupunguza athari ya gesi hiyo.
Hali ya Chiba ilikuwa mbaya, Gina akamkokota na kutoka nae katika eneo leneye hewa, kwa bahati nzurti katika banda hilo kulikuwa na gari ya wagonjwa iliyowekwa kwa ajili ya maonesho, kmpakia Chiaba nay eye akaketi katika usukani, na kuitoa gari hiyo kwa kasi eneo lile huku akiwa amewasha ving’ora vyote. Akainua simu na kumpigia dokta Jasmine. Dr Jasmine akamwelekeza moja kwa moja ampeleke hospitali ya taifa Muhimbili, Gina alitoka katika geti la uwanja huo kwa kasi na kuingia barabara ya Kilwa kurudi mjini.
Kamanda Amata alipishana na ile gari ya wagonjwa lakini hakujua kuna nini ijapokuwa dereva wa gari ile aliweza kumfananisha. Alikimbia haraka mpaka kwenye banda husika na kukuta vijana wa jeshi wakihaha huku na huku kujarib u kudhibiti hali iliyokuwepo hapo. Kamanda Amata alipofika alizuiwa kupita eneo hilo lakini kwa kitambulisho chake alairuhusiwa huku akipewa mask na kuivaa, akaingia ndani ya banda hilo na kukuta baadhi ya wanajeshi wakijaribu kutoa huduma ya kwanza kwa wafanyakazi ambao walikuwamo ndani ya banda hilo lakini gesi ile iliwaathiri. Kamanda Amata akaiwahi kompyuta ya Chiba iliyokuwa juu ya meza Fulani, ilikuwa inaendeleaa na kazi ambayo Chiba alikuwa anaifanya.
Akatazama kwenye kioo cha kompyuta hiyo, akaelewa kilichokuwa kinafanyika mara ya mwisho. Chiba kabla hajaenda kutafuta sehemu ya mlipuko alikuwa akijaribu kutafuta uelekeo wa wapi mawimbi yale ya kielektroniki yalikuwa yakitokea, mpaka yeye anaiacha kompyuta hiyo bado ilikuwa ikiendelea, Kamanda Amata akasoma nyuzi (degrees) zilizojiandika, akaelewa, kilikuwa kipimo cha ardhi katika longitude na latitude, na eneo husika lililolengwa kadiri ya nyuzi hizo aligundua ni maeneo ya Kigamboni, akaendelea kuperuzi na kwa chini kidogo, akasoma kwa makini sana namba zile zilizokuwa zikibadsilishana hapa na pale ili kupata uelekeo sahihi.
“Kigamboni Kaskazini,” akajisemea na kisha akiinua ile kompyuta na kutoka nayo mpaka nje, akatzama huku na kule na kuiona gari ya chiba akaiendea, akaingi na kujifungi ndani yake, kama anavyofanya Chiba, akaunganisha ile kompyuta na kijimtambo maalum kilichofungwa ndani ya gari hiyo, sasa akaweza kusoma eneo halisi kwa kutumia screen ndogo iliyopo ndani ya gari hiyo, akaiwasha na kutoka katika uwanja huo, akachukua simu ya upepo iliyo ndani ya gari hiyo na kubofya kitufe Fulani.
“Madam S, Madam S,” akaita kwa mtindo huo.
“Nakupata Chiba,” madam S akajibu.
“Hapana sio Chiba, hapa ni Kamanda Amata,” akamrekebisha.
“Nimekusoma nipe ripoti,” akaendelea Madam.
“Natoka uwanja wa maonesho wa sabasaba, hali sio mbaya sana lakini Chiba inaonekana ana hali mbaya ameondolewa na Gina kuelekea hospitalini, la pili inaonekana kuna jambo maeneo ya Kigamboni kadiri ya tafutishi nilizozikuta katika kioo cha Chiba, niko mbioni kuelekea huko, haraka iwezekanavyo.” Kamanda akabofya kitufe kingine katika redio hiyo.
“Umesomeka Kamanda, mama anabadili uelekeo, tukutane Kigamboni,” madam S akamaliza na kukata ile simu.
Simanzi na majonzi viliwajaa Shakrum, Shailan na wengine waliokuwa ndani ya boti, ukimya ulitawala wakati injini ya boti hiyo ikiwa inaunguruma kwani muda ulikuwa tayari umewadia wa kung’oa nanga. Kutoka mbali Shailani aliona kitu kama boti ndogo inayokuja kwa kasi, akachukua darubini na kutazama hakuamini macho yake kwa kile anachokiona, Tashrini na wengine wawili walikuwa katika boti hiyo wakija kwa ajili ya safari. Ingawa wao walisalimika lakini maumivu makaubwa yalibaki kwa ndugu yao Jegan Grashan. Dakika tatu tu ile boti ilifika ukingoni kabisa mwa ile boti kubwa ya akini Shakrum, wakashuka na kuhamia katika boti hiyo kisha milango ikafungwa tayari kwa kuondoka.
“Maafa yaliyotokea ni makubwa sana,” Tajan alimweleza Shailan.
“Nini?” aliuliza Shakrum.
“Akiba yote ya mafuta kamanda Amata kalipua yadi zote mbili hivi tunavyoongea zinateketea kwa moto. Scolleti amekwishauawa na Yule mwanamke wa Kihindi, Jegan nae kapigwa risasi na mtu asiyejulikana,” Tajan alitoa ripoti. Shakrum alikuwa amesimama akimsikiliza, mara hiyo akajiegemeza katika moja ya nguzo zilizo katikati ya boti hiyo akiwatazama wenzake hao.
“Na mlipuko wetu umetenguliwa kule sabasaba, wametuweza, kiukweli sikufikiri kama hawa jamaa watakubali Jegan aondoke hivihivi,” Shakrum alieleza.
“Jamani, hapa tumeshacheza pata potea, washa mashine tuondoke, si ajabu na sisi wakatukamata hapahapa au wakatushushia kombola moja tu tukapotea wote,” Shaiilan aliwaeleza wenzake, injini ikawashwa, milango ikafungwa, kiyoyozi kikaanza kuyoyoza, taratibu chombo kikaanza kuondoka eneo hilo kikichanganya polepole na kugeuka kuelekea upande mwingine, kila mmoja ndani ya chombo hicho alikuwa tayari ameketi mahala pake aliyekuwa anafungua kinywaji sawa, aliyesoma gazeti sawa, tayari walikuwa wamekwishaamua kuondoka.
§§§§§

OFISI ZA UBALOZI WA KHAZAKISTAN

Gari za ubalozi ziliingia katika kiwanja cha ofisi hizo, maofisa wa usalama wakashuka na kuiendea gari iliyokuwa haina kioo, ndani yake alikuwamoi Jegan Grashan.
“Nilijua hawawezi kukuacha hivihivi,” alisema mmoja wa maofisa hao alipokuwa anamvua bullet proof Jegan.
“Dah! Mungu mkubwa, nashukuru mlijiandaa Yule jamaa alikuwa ananimaliza kabisa,” Jegan alijibu huku akimkabizi Yule mwanausalama lile koti. Jegan Grashan akateremka garini na kukanyaga ardhi ya uraiani, kwa hatua za polepole huku akiwa ameshikwa mkono na mmoja wa wanausalama ambaye mkononi mwake alikuwa amekamata short gun alisindikizwa kuingia ndani ya jengo hilo.
“Ni saa nne sasa karibu na dakika arobaini na tano, boti itakuwa inang’oa nanga, kwa vyovyote vile wao wanajua wewe umekwishakufa,” ofisa mwingine wa ubalozi alimweleza Jegan.
“Haina shaka, naweza ungana nao sasa na kuondoka, asanteni sana,” Jegan aliwashukuru na kuwakumbatia mmoja mmoja, kisha akakiendea chombo cha mawasiliano na kuwasiliana na ndugu zake hao walioko ndani ya boti.
Jegan aliingizwa kwenye chombo maalum na kufungiwa ndani yake kisha ikabonyezwa swichi Fulani na chombo kile kikawasha injini zake ndani ya chumba maalumu kilichojazwa maji ambacho moja kwa moja kinatokea kwenye mkondo wa bahari. Dakika moja baadaye kile chombo kikasukumwa kwa nguvu na kutoka ndani ya jengo kwa kupitia kidirisha Fulani, kikapaa na kujibwaga baharini kisha kwa mwendo wa kasi kikapotelea baharini.
Ndani ya boti saa 4:45 asubuhi
Furaha na shangwe ziliijaza boti hiyo baada ya kusikia sauti ya mpendwa wao Jegan ikawahakikishia kuwa yuko hai, hajafa. Furaha ilikuwa mara mbili ya ile ya kwanza pale walipokipokea chombo maalumu kilichomhifadhi Jegan, na walipofungua ndani walimtoa ndugu yao huyo na sherehe ikawa sherehe, shampein, risasi za hewani vyote vililindima katika boti hiyo, nyimbo zikaimbwa na kuchezwa, kati yao wote hakuna aliyepotea, wote walikutana tena kama ndoto yao ilivyokuwa.
“Nimeachiwa huru, asanteni sana kwa juhudi zenu za kuishinikiza serikali ya Tanzania, mmefanya lililo jema hata sasa niko nanyi. Lakini huu sio mwisho wa mapambano, huu ni mwanzo, lazima tuikomboe nchi takatifu kutoka katika mikono ya watu wa Maghalibi na vibaraka vyao. Nisingeelewa kanchi kama haka ka Afrika mashariki kajifanye kana sauti ya kupambana na sisi, dunia yenyewe inapiga magoti mbele yetu, wao ni nani? Hawakujiuliza kuwa kwa nini Amerika na washirika wake kama Uingereza, Ufaransa na wengineo wako kimya? Wote hao wanajua kuwa freedom fighters tunajua tunachokifanya wanajua hilo ndo maana walibaki kimya,” Jegan Grashan alitoa hotuba ya nyodo katika boti na kufuatiwa na nderemo za wafuasi wake. Hakukuwa na linguine zaidi ya kuondoka, safari ikaanza taratibu, boti ile ilikuwa ikiambaa na maji ya bahari ya Indi ikichana mawimbi kuelekea Mombasa ambako wenzi wao walikuwa wakiwasubiri.
§§§§§
Kamanda Amata alijirusha majini na kupiga mbizi, akipita chini kwa chini kuielekea ile boti ambayo ilionekana kwa mitambo maalumu ya kijeshi pale kigamboni. Msoma rada alieleza wazi kuwa walikuwa wakiichunguza boti hiyo karibu masaa kumi tangu imefika eneo hilo, hawakuitilia nashaka kwa kuwa ilikuwa ikipepeza bendera ya ya Tanzania. Siku hii ndipo walipogundua kuwa haikuwa boti ya kawaida bali imeingia hapo kwa shughuli maalumu.
Madam S alimtazama Amata akipotelea majini, nay eye alirudi upande mwingine ambako kulikuwa na wanajeshi wanamaji waliojiandaa tayari kwa lolote lile. Kamanda Amata alipewa maagizo ya kuhakikisha kuwa waliopo wanakamatika wakiwa hai na uhai wao. Aliifikia ile boti kwa muda mfupi tu, bahati nzuri alipoifikia na chombo kilichombeba Jegan Grashan kilikuwa kikiwasili, aliona pale kilipoingilia ma yeye akajipenyeza hapohapo.
Wakiwa ndani ya boti wanashangilia ushindi huo, ndipo Kamanda Amata alipomshuhudia Jegan Grashan ambaye alijua wazi kuwa amemuua kule Tazara akiwa hai mbele ya macho ya wengine. Jambo hili lilimtia hasira na uchungu, akabadili mpango wake haraka na kujitokeza mzima mzima. Wakati wao wanapiga shampeini na risasi za hewani kushangilia ushindi, Kamanda Amata alikuwa kazimama mbela yao kama mzuka.
“Jegan Grashan, nani aliyekwambia kuwa utaondoka ndani ya nchi hii ukiwa na pumzi yako? Kama ulijuwa kuwa umepona sasa ndio mwisho wa maisha yako, nafikiri hukutaka kufa peke yako ulikuwa na akili sana na sasa mtakufa wote pamoja kwa mkono wangu huu, wasalimie kuzimu, mwanaharamu, mwanadamu ambaye hukustahili hata kuzaliwa,” Kamanda Amata alishikwa na hasira kali, akisema maneno hayo hakuna aliyeamini kama mbele yao yupo kiumbe huyo anayeogopwa kila kona ya sayari yetu, kabla hawajajiweka sawa wakiwa bado kwenye butwaa, kichwa cha Jegan Grashan kilifumuliwa kwa risasi mbili kutoka katika bastola ya Amata, mara hii alihakikisha anakufa.
Kamanda Amata alijirusha upande wa pili na risasi yab tatu ikamfumua Yule aliyeshika shotgun aliyekuwa akimlenga Kamnda, hola! Alifanikiwa kupiga viti na vyupa vya pombe wakati Kamanda akijiviringa kuelekea upande mwingine. Ilikuwa ni hali ya taharuki kwa freedom fighters.
“Muueni shetani mweusi!” Shakrum alipiga kelele huku akitafuta pa kujificha. Tayari watu watatu walikuwa chini bila uhai.
“Jegannnnnn!!!!!!” Ilikuwa sauti ya Shailan aliyekuwa akilia kwa uchungu aliposhuhudia mwana mapinduzi wao akifumuka kichwa. Dakika moja baadae wote walikuwa chali sakafuni, Shakrum alibaki hai kwa kuwa aliwahi kujificha. Kamanda Amata akatazamana na Shailan.
Jicho la hasira la Kamanda Amata lilikuwa likimwangalia Shailan aliyekuwa amemshika Jegan mfu akilia kwa uchungu.
“Kama kuna aliyewaambia kuwa mtaondoka nchi hii mkiwa hai amewadanganya kabisa, hamkustahili kuishi wala kuzaliwa,” Kamanda Amata aliongea hayo na kufyatua risasi moja iliyopiga kifua cha Shailan na kumtupa nyuma. Alipotaka kufyatua risasi ya pili akajikuta ameishiwa risasi. Mara akajikuta akidakwa kwa nyuma, kabla hajakaa sawa, alikabwa shingo. Amata akafikiri la kufanya kwa haraka, akainama na kumyanyua huyo mtu na kumbwaga mbele, Shakrum. Hasira za Amata zikawaka maradufu, Shakrum akanyanyuka na kumkabili Kamanda Amata.
“Nilikuwa nakutamani sana wewe kiumbe! Na sasa umeingia mkononi mwangu, sitakupa hata nukta ya kuomba sala ya mwisho,” Shakrum alimwambia Kamanda Amata, alipomaliza sentensi yake alimvamia Kamanda kwa jinsi ya ajabu, akampiga ngwara moja maridadi, Kamanda alijirusha hewani akaichanua miguu yake na kuipata shingo ya Shakrum, alimpiga teke kwa mguu wake wa kulia nyuma ya shingo, Shakrum aliyumba na kujipigiza ukutani. Akaruka sarakasi na kusimama wima, akaweka mikono katika mtindo wa kuvutia wa mapigo ya karate, Kamnda Amata naye akajipanga kivingine. Shakrum alitoa mapigo ya kasi mfululizo kumuelekea Kamnda Amata lakini hakuna hata pigo moja lililomfikia Amata, mapigo yote yalipanguliwa kiufundi sana, mwisho wa yote Kamanda Amata akajirusha sarakasi na kumpa Shakrum nafasi ya mita kama tano kutoka kwake. Kwa sekunde chache alizozipata Amata alijipanga na kupeleka mapigo ya kazi ambayo yote yalimuioshia Shakrum na kumtupa chini akiwa hoi.
“Mi nilifikiri unajua kupigana kumbe ni mwanafunzi namna hiyo!” Amata alimwambia shakrum aliyekuwa akitambaa chini huku yeye akimfuata kwa nyuma.
“Ulipigania Jegan kuachiwa huru, sasa wewe utakaa jela badala yake,” Amata alimwambia Shakrum na kumkamata ukosi wa fulana yake na kumvuta kwa nguvu mpaka kijana huyo akakohoa, akamuinua kwa nguvu na kumbamiza ukutani. Shakrum hakuwa na la kufanya, Kamanda Amata akatoa pingu tayari kumfunga Shakrum lakini lo, bomu aina ya grunet lililoondolewa pini ya usalama likaanguka kutoka mkononi mwa Shakrum na kutua chini liokadunda mara ya kwanza na likaelekea kugoinga sakafu mara ya pili.
Shakrum alimshika kamanda kwa nguvu zake zote.
“Hatoki mtu hapa, kama wewe umeua ndugu zangu, lazima nawe ufe na sisi,” Shakrum alimwambia Amata.
“Kamwe haiwezekani!” Kamanda Amata akajibu na kumpiga kichwa cha nguvu kilichomfanya Shakruma amwachie. Kamanda Amata hakupoteza sekunde, alikimbia kwa kasi yake yote, hakukuwa na mlango ila dirisha kubwa la kioo mbele yake, alichumpa na kutanguliza kichwa akakipiga kioo nay eye mwenyewe kutoka nje kupitia hapo. Nyuma yake ulitokea mlipuko mkubwa, ile boti yote ikateketea kwa moto.
§§§§§
Madam S alijishika kichwa baada ya kuushuhudia mlipuko ule kupitian chomb o maalumu katka kambi ya jeshi la wanamaji Kigamboni.
“Oooh! My son! (Oooh Kijana wangu!)” alipiga kelele.
Moyo ulimwenda mbio hakujua afanye nini. Akikumbuka Chiba kaumizwa na gesi, sasa Kamanda ndani ya mlipuko, Madam S alijikuta anabaki peke yake, machozi ya uzee yalimdondoka huku mikono yake ikifunika kinywa chake kwa uchungu.
Chumba kizima walichokuwa maofisa wa Jeshi pamoja na Madam S wakishuhudia tukio lile kilikuwa kimya, hakuna hata aliyekohoa. Madam S alihisi akishikwa bega. Akageuka na kumtazama aliyemshika, alikuwa waziri wa ulinzi aliyefika muda huo katika kambi hiyo ya wanamaji.
“Pole Madam, lakini vijana wetu wamekufa kishujaa!” alimwambia Madam S.
“Nani aliyekwambia vijana wangu wamekufa?” madam S alijikuta akipiga kelele kupingana na kauli hiyo. Mara kelele zikaibuka katika chumba kile, Madam alipogeuka alimuona Kamanda Amata akiogelea majini baada ya kuibuka.
“Mpe msaada haraka!” illikuwa ni sauti ya waziri wa ulinzi, na mara hiyo hiyo boti iendayo kazi ikaanza safari yake na kumfuata Kamanda Amata.
Madam S alijikuta akifurahi kwa tukio hilo, hakuamini kab isa anachokiona mbela yake.
“Mungu mkubwa!” alishukuru.
MADAM S aliinua simu yake baada ya kushusha pumzi ndefu, katika sakata hilo ni yeye tu aliyekuwa upande wa peke yake tangu mwanzoni baada ya kusikiliza kile ambacho Kamanda Amata alimwambia tangu mwanzo kuwa hakubaliani na kuachiwa huru Jegan. Ijapokuwa Madam S aliwasikiliza wajumbe wengine katika jopo lile la baraza la usalama la taifa chini ya waziri wa ulinzi, aligeuka baadae kwa kuungana na kijana wake, TSA 1 lakini swala moja walikuwa wakitofautiana. Kamanda Amata aliapa wazi kuwa laiti Jegan akiachiwa huru yeye atamrudisha kwa risasi, uamuzi huu ungekuwa kinyume na maadili ya kazi kama kungetolewa hati ya jambo hilo. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Kamanda Amata alimpiga risasi Jegan Grashan katika msafara wa gari za ubalozi. Ijapokuwa Jegan alikuwa amevikwa nguo zisizoingia risasi na kusalimika katika tukio hilo. Aligadhibika sana alipomuona Jegan akiwa hai ndani ya boti ile, akipongezana na wenzake na kutoa maneno ya kashfa, Kamanda Amata hakushindwa kutumia bastola ile ile iliyofanya kazi katika tukio la kwanza, na sasa alifumua kichwa kabisa maana labda angekuwa na nguo nyingine isiyopitisha risasi. Alijua alilolifanya.
‘Liwalo na liwe!’ alijisemea moyoni huku akiitazama boti ile iliyokuwa ikiteketea kwa moto, hakuna hata mtu aliyetoka, hakikusalia hata chuma juu ya chuma kingine. Kazi ilikuwa imekwisha namna hiyo. Akajigeuza na kuendelea kuogelea kuelekea pwani ambako palikuwa na umbali kidogo lakini alipoanza kuogelea tu, aliona helkopta kubwa ya jeshi ikija eneo lile, akaipungia mkono na chombo kile kikasogea hadi pale alipo na kumteremshia kamba iliyofuingwa kwa mafundo mafundo, akaikamata na dude lile likaondoka nae kutoka pale kwenda nae nchi kavu.

KIGAMBONI – KAMBI YA JESHI LA WANAMAJI

saa 7:14 mchana
MADAM S alisimama kwenye uwanja wa kushukia helkopta, pembeni yake kulikuwa na waziri wa ulinzi, walikuwa wakimwangalia Kamanda Amata alipokuwa akija upande wao akiwa chapachapa, ametota maji.
Madam S alimkumbatia Kamanda Amata kwa nguvu zote bila kujali kama kalowa maji, alimbusu mashavuni.
“Kazi nzuri kijana wangu, nimefurahi sana kwa ulilofanya, nina uhakika hakuna aliyetoka mle ndani,” Madam S alimwambia Amata.
“Hakuna anyeweza kutoka kwenye mikono ya Kamanda aamuapo jambo, si Jegan, si Shailan wala Shakrum, wote leo nyama zao zinaliwa na watoto wa samaki, lazima ulimwengu ujue kuwa kuna wana usalama makini katika kazi, Mungu ibariki Tanzania, nahitaji kumuona kaka yangu Chiba,” Kamanda alimwambia Madam S, akamtazama waziri wa ulinzi kisha akapita b ila kumsalimia na kuingia kwenye gari ya usalama, akaketi katika siti ya nyuma na Madam akaingia siti ya mbele nyuma ya usukani wakaiacha kambi hiyo na kuelekea mjini.
MUHIMBILI saa 7:54
CHIBA alitolewa kwenye chumba cha daktari na kupelekwa sehemu maalumu ambayo ni yeye peke yake alikuwa amehifadhiwa humo, chumba maalum chenye mitambo tiba ya kila aina ambayo ina uwezo wa kukushikia roho yako wakati wewe ukifanya mambo mengine. Alilazwa kitandani na kuwekewa hewa ya oksijeni ili imsaidie kupumua huku mitambo mbalimbali ikishirikiana kuonesha mwenendo mzima wa maisha ya mtaalamu huyo. Ijapokuwa ni yeye alikuwa mtaalamu wa kompyuta lakini mara hii kompyuta zilikuwa zikimuongoza yeye. Hakuweza kufungua macho ndani ya ubongo wake alikuwa akipitiwa na mapito mengi mabaya nay a kutisha, aliota Kamanda Amata anakufa kifo cha moto, na mara akaota Kamanda Amata anafukuzwa kazi. Ndoto mbaya zaidi ilikuja baada ya muda mfupi, alipoota wapelelezi wawili maarufu sana wa Tanzania wakiuawa vibaya katika sehemu moja ya Afrika wakiwa wanataimiza majukumu yao ya kiserikali. Mara vile vyombo vikaanza kupiga kelele na kuonesha kuwa mapigo yake ya moyo yanashuka kwa kasi. Muuguzi aliyekuwa hapo akamwita dakatari haraka. Dr Jasmin, alikuwa akitokwa na jasho akijaribu kuokoa maisha ya Chiba, Chiba alikuwa akipigania maisha yake ya mwisho, ulikuwa mpambano mkali na shetani. Katia maono yake alikuwa akipambana na joka kubwa lenye vichwa saba, haukuwa mpambano wa kitoto, lakini Chiba alijitahidi kutumia nguvu na ujuzi wake wote ili kulishinda joka hilo, lakini haikuwa hivyo. Joka lilimdhibiti Chiba likamkaba mwilia wake na kumnyonga.
Mitambo tiba iliyokuwa ikipima mwenendo wa moyo wa Chiba ilionesha mstari ulionyooka kuashiria kuwa Chiba hana uhai tena. Dr Jasmine alishindwa kuvumilia hali hiyo alijikuta akilia kama mtoto. Nukta hiyohiyo Madam S na Kamanda Amata waliingia ndani ya wodi hiyo wakiwa haihai walipofika pale walikuta vurugu ya madaktari wakisaidiana na wauguzi, wakati huo Gina alikuwa hana hali kwa kilioo cha vikwifuvikwifu.
“Nini Gina?” Kamanda aliuliza.
“Man down Kamanda,” Gina alimwambia huku akilia. Kamanda Amata alielewa haraka maana ya neno hilo likimaanisha Chiba amekufa, Kamanda Amata hakusubiri linguine, haraka alikimbilia walipo madaktari ambapo tayari Madam S alikuwa amekumbatiana na Dr Jasmine wakilia kwa uchungu.
“Noooooooooo!!!!!!!” kamnda Amata alipiga kelele na kuwatawanya madaktari waliokuwa pale, wengine wakaanguka na wengine wakayumba na kusimama wima. Kamanda Amata alimtazama Chiba ambaye alikuwa ametulia kimya macho yake yakiwa meupe, mboni zake hazikuonekana, “No my brother, don’t leave me!!!!!!” (Hapana ndugu yangu, usiniache peke yangu,) Kamanda Amata kama kawaida yake huwa hakubali kushindwa jambo, wakati madaktari wakimshika amuache Chiba hakukubaliana nao, alitazama huku na huku, akaona waya wa umeme wa 6.0mm uliokuwa ukipitisha umeme kuelekea kwenye mitambo ya oksijen, Kamanda kutoka aliposimama alikanyaga kimeza cha dawa za mgonnjwa na kuukamata ule waya akaning’inia nao mpaka ule waya ukachomoka katika joint box, akashika jirani na miisho yake ambayo ilikuwa ni nyaya mbili, nyekundu na nyeusi, bila huruma wala kuchelewa akampiga shoti Chiba akiwa kitandani, akarudia mara ya pili.
Jambo lisiloaminika likajitokeza, mashine iliyokuwa ikipima mapigo ya moyo ikaanza kusoma mapigo ya juu sana na baada ya sekunde kumi ikatulia na kuonesha mapigo yaliyo sawa. Chiba akafumbua macho, akamtazama Kamanda, Madam S, Madaktari na wauguzi waliopo katika wodi ile. Chiba akaondoa mwenyewe kwa mikono yake ile barakoa ya oksijeni, akainuka na kuketi kitandani.
“Kamanda Amata, umepona?” akauliza Chiba.
“Nimepona kaka,” Kamanda akajibu.
“Jegan najua amekufa na wenzake je?” Chiba akauliza tena.
“Wote wamekufa, hakuna aliyesalia,” Kamanda akajibu, Chiba akampa ishara Kamanda Amata ya kuwa asogee jirani, akamkumbatia kwa nguvu. Kamanda akautupa ule waya chini, na wakati huo fundi umeme alikuwa keshafika baada ya kuitwa haraka.
“Asante Kamanda Amata,” Chiba akashukuru.
“Asante na wewe kwa kuokoa maisha ya Watanzania wengi,” Kamanda akamshukuru Chiba. Wale madaktari wakamchomoa vifaa vyote vilivyokuwa mwilini mwake. Chiba akatoka kitandani na kuongozana na Madam S, Kamanda Amata, Gina na Dr Jasmine wakatoka na kuingia kwenye gari kisha wakaliacha eneo la Muhimbili na kutokomea zao.
§§§§§

BAADA YA SIKU MBILI
OFISI NYETI

KAMANDA Amata akiwa amesimama mbele ya meza kubwa, safi ambayo unaweza kujiona mwenyewe, alikuwa akitazamana na Madam S ambaye naye alikuwa amesimama wima, wote wakiwa katika vazi la kufanana, suti nyeusi, shati jeupe na tai ndefu nyeusi kasoro Madam S. Chiba alikuwa pembeni na watui wengine wawili akiwamo Dr Jasmine.
“Tukisimama hivi unaelkewa kabisa kuwa tunahitaji nkuongea kiofisi zaidi,” Madam S alimwambia Kamanda Amata ambaye alikuwa kimya bila kujibu lolote, akatoa kitambaa chake cheupe na kufuta machozi yaliyokuwa yanayajaza macho yake angavu, kisha akaendelea, “Baada ya kikao cha jopo lilelile lililokuwa likikaa tangu mwanzo wa sakata hili mpaka jana limekaa tena. Na agenda kubwa ilikuwa ni juu yako Kamanda wangu, kwanza unapongezwa sana kwa kazi nzuri uliyoifanya kwa kushirikiana na wenzako wote, mmeudhihirishia ulimwengu kuwa usalama wan chi hii upo mikononi mwetu wenyewe, lakini pamoja na pongezi hizo Kamanda, kuna habari mbaya nay a kusikitisha juu yako na juu ya ofisi yetu pia,” akakohoa kidogo na kuendelea tena, “Siku zote kwenye kitambaa cheupe kinachoonekana ni doa jeusi tu, watu hawaangalii wema ila mabaya yako na kukupatiliza kwayo, ndani ya kazi yako nzuri ambayo sisi kama wanausalama tumeiweka kwene kablasha linalojulikana kama JULAI 7, Kamanda umeonekana kufanya kazi kijeuri bila utii kwa maamuzi yako mwenyewe na kupinga maagizo ya jopo la usalama na kwa sababu hiyo baraza la usalama limekupa barua ya kusimamisha kazi katika kitengo cha ujasusi cha TSA, utakivua cheo chako cha TSA1 na kukabidhiwa mtu mwingine kuanzia nimalizapo kusema haya, haijatolewa kama ombi bali ni amri na itekelezwe mara moja, imesainiwa na waziri wa Ulinzi kwa niaba ya baraza zima la usalama wa taifa.” Madam S alimaliza na kufuta machozi.
Kamanda Amata alitulia kama dakika moja, kimya kilitawala, hakuna aliyeongea isipokuwa kufuta machozi na makamasi yaliyokuwa yakiwatoka waliopo kwa uchungu. Aliyekuwa ngangari ni katibu wa wizara ya ulinzi tu, akasogea na bahasha ya khaki, akatoa karatasi tatu nyeupe zilizochapwa kwa mashine ya kisasa, upande mmoja ilisainiwa na waziri wa ulinzi na upande wa pili zilibaki saini mbili moja ya Kamanda na nyingine ya Madam S kama mkuu wa kitengi maalumu, kitengo cha kijasusi kisicho na mipaka. Akaipokea ile barua na kusaini kisha akampa Madam S nae akazisaini kisha, wakagawana moja kwa ofisi ya baraza la usalama wa Taifa, nyingine kwa ofisi ya TSS nay a mwisho akapewa Kamanda Amata, naye akamkabidhi Gina.
Baada ya hapo, Kamanda Amata akavua beji maalumu ya usalama wa taifa na kumkabidhi Madam S, beji ya dhahabu, kimkoba kidogo cha bastola ambacho ndani yake kilikuwa na vifaa kadhaa vya kijasusi ambavyo alikabidhiwa pindi alipopewa kazi hiyo maalumu. Mwisho akapeana mikono na wote waliopo ndani ya ofisi hiyo nyeti.
Ilikuwa ngumu kuzuia machozi ya kila mmoja lakini hali halisi ilikuwa hiyo.
“Nakuhitaji nyumbani Kamanda ndani ya masaa matatu, wewe na wenzi wako kwa chakula,” Madam S alimpa ujumbe Amata.

NYUMBANI KWA MADAM S

“Sikuweza kukutetea tana Kamanda, ijapokuwa wapo nwaliojaribu lakini wengine walikazia ufukuzwe kazi” Madam S alimwambia Kamanda Amata walipokuwa wameketi katika bustani kubwa ya nyumba hiyo, Gina, Chiba na Dr Jasmine walikuwa ndani wakiendele kupata vinywaji.
“Usijali Madam, yote maisha, mimi nimetoka TSS atakuja mwingine naye kutimiza wajibu wake,” Kamanda alimwambia Madam S.
“Najua, lakini kwa sasa kumpata mtu shupavu, mwelevu, mwepesi, mwenye mbinu na ujuzi wa mipango ya kumsaka adui au kummaliza, mbabe kama wewe itachukua miaka mingi sana, usijali Kamanda naamini kuwa muda mfupi tu mataifa makubwa yatakuchukua, mi nakutakia maisha mema sana Kamanda, kwa lolote tuwasiliane mimi ni mama yako na wewe ni mwanangu,” Madam S akamaliza, wakakumbatiana kwa nguvu kila mmoja akimwaga machozi ya uchungu kisha wakaachana na kurudi ndani.
§§§§§
Gina na Kamanda Amata waliondoka kwa Madam S na kupitia vijiwe kadhaa kabla hawajafika nyumbani.
“Nikupeleke kwako au?” Kamanda akauliza.
“Sitaki, leo nataka kulala kwako,” Gina akamwambia Kamanda Amata kisha wakaendelea na safari mpaka nyumbani kwa Kamanda Amata. Walikuwa wamelewa, Gina alifika na kuingia chumbani akifuatiwa na Kamanda. “Kamanda Amata, uliyekuwa TSA1 wenye roho mbaya wamekufukuza kazi, usijali mimi leo nataka nikupe kazi njione kama kweli we mwanaume,” Gina aliongea kwa sauti ya kilevilevi.
“Gina ulale sasa,” Kamanda alisititiza na kutoka kwenda sebuleni. Gina akachukua nafasi hiyo kwenda maliwato, akaoga na kurudi kisha akaingia ndani ya kitanda kikubwa na kujifunika kwa shuka safi yenye maua ya kuvutia, akazima taa kali na kuwasha ile ya buluu.
Dakika chache baadae Amata aliingia chumbani, naye vivyo hivyo, akaenda kuoga na kurudi, Gina kwa hila zake akajifunua shuka na kulitupa pembeni akabaki kama alivyozaliwa.
“Njoo Kamanda, najua una mambo mengi leo, njoo nikufariji,” Gina alimwambia Kamnda huku akiwa anjipindapinda pale kitandani.
Kamanda Amata akamtazama mrembo huyu ambaye siku zote walikuwa wakiheshimiana sana lakini leo hii heshima ilikuwa inataka kubadili uelekeo.
Gina alikuwa akimtazama Kamanda, Kamanda alikuwa akimtazama Gina aliyekuwa kajilaza pale kitandani, mwanga wa taa buluu ulifanya umbo la Gina lionekane kama madini ya Tanzanite, lilimvtia Kamanda, akapatwa na wakati mgumu, kabla hajaamua la kufanya. Gina aliinuka na kumtoa taulo Kamanda kisha akaizungusha mikono yake na kuiokutanisha nyuma ya shingo ya Kamanda Amata.
“Nakupenda sana Kamanda Amata”.

MWISHO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Julai Saba

Sehemu Ya Tano (5)

Baada ya kikao cha Scolleti na watu wake kukamilika, Scolleti alibaki peke yake katika ofisi hizo za FK Security Group, alipohakikisha kila kitu kipo sawa na hakuna mtu mwingine mle ndani, akabonya kitufe Fulani kilichofichwa ukutani nyuma ya kalenda, mara mlango mkubwa ukafunguka kwa chini na ngazi ndefu zikaonekana zikishuka, akateremka taratibu na ule mlango ukajifunga nyuma yake. Akalegeza tai yake na kuvuta suitcase yake iliyokuwa kitandani, akapekuwa ndani na kukuta kila anachokihitaji kipo sawa, akapekua hapa na pale na kuweka sawa hati mbalimbali ikiwemo ya kusafiria, tiketi ya ndege iliyokuwa iondoke saa mbili asubuhi ya julai saba kuelekea Nairobi kwa kikao kingine na hao watu wake wa Freedom Fighters. Akafunga mkoba huo na kuingia maliwato, akajiswafi na kutoka nusu saa baadae. Alipohakikisha yuko kamili akaburuza hiulo sanduku lake na kutoka njea kwa mlango mwingine. Kelele za majogoo zilikuwa tayari zikipasua anga kuashiria kuwa kumekucha. Saa kumi na moja alfajiri, Scolleti alishika kitasa cha mlangowa gari yake aina ya Land Cruiser VX, akapakia sanduku lake na kisha yeye mwenyewe kuingia mlango wa dereva. Akaketi tayari kwa kuondoka, mara akahisi kitu baridi kikimgusa nyuma ya shingo yake.
“Tulia, fuata maelekezo ninayokwambia, washa gari na utoke nje ya eneo hili,” ilikuwa sauti nya kike iliyopenya masikio ya Scolleti, haikuwa sauti ngeni. Akawasha gari na kutoka getini akifunguliwa na walinzi kisha akafuata barabara hiyo mpaka katika barabara kubwa ya Bagamoyo karibu kabisa na mataa ya Morocco. Yule mwanamke akamuamuru kufuata barabara ya kwenda Mwenge naye akafanya hivyo, alipoingia tu barabara kubwa kuelekea Mwenge na muda huohuo Kamanda Amata alikuwa akiwasili eneo hilo, akapiga kona kali na pikipiki lake na kuanza kuifuata ile VX kwa maana alikuwa anaifahamu sana. Aliifuata taratibu mpaka maeneo ya Tangi bovu ile VX ikasimama pembeni. Akateremka akiwa mikono yake iko kichwani.
ShaSha nae akateremka chini akiwa kamnyoshea bastola Scolleti.
“Kila kona watu wanalalamika juu yako, nimetumwa kwa jambo moja tu, serikali yako ya India imekuchoka, imechoka kulalamikiwa na nchi rafiki hata kupelekea kuharibu uhusiano wa kidiplomasia kwa ajili yako haya yote,” ShaSha aliongea kwa lugha ya Kihindi, Kamanda Amata na Gina walisimama kwa tahadhari nyuma kidogo ya nguzo kubwa ya chuma iliyobeba tangazo kubwa la Safari Lagera, alikuwa akisikia wanachokiongea alikuwa akielewa kidogo lugha hiyo.
“Siko tayari kurudi India,” Scolleti alijibu.
“Swala sio kurudi India, kwanza hakuna anayekutaka kule, hata mimi nimetumwa kuchukua nafasi ya Israel ambaye anachelewa kuja kwako kutimiza kazi yake, nimetumwa kukuua,” ShaSha aliongea kwa uchungu. Scolleti aliposikia swala la kuuawa akashusha mikono yake na kugeuka mzima mzima na kutazamana na domo la bunduki ya mwanamke huyo.
“We msichana, wenzako hawakuwa wajinga kukutuma, ni kwa sababu ya kimbelekimbele chako tu, nani hapa duniani mwenye uwezo wa kupambana au kumkamata au kumuua Scolleti? Kwa taarifa yako ni Mungu tu, na hata huyo Mungu mpaka leo anajishauri anianzie wapi,” Scolleti aliongea kwa kujiamini huku mikono yake kajishika kiunoni.
“Unajiamini sio?” ShaSha akauliza.
“Sio najiamini, ila nataka nikwambie kitu ambacho wewe hukijui, sikiliza, wewe na serikali ya Tanzania nani mwenye uwezo wa kunikamata? Kama wao wamenipokea na kila mwezi nawapa pesa nzuri iliyotakata viongozi nao wananihifadhi ujue wazi utafia hapa. Kila mtu atakushangaa kusikia umeniua, Watanzania watakushangaa sana na kukupiga mawe,” akasonya, “Toa kibunduki chako hapa,” akaipiga kwa kofi ile bunduki ya ShaSha nayo ikatoka mkononi na kuanguka chini, alipotaka kuiokota tu Scolleti akawa tayari na bastola mkononi.
“No no no no, usijaribu hilo kabisa,” Scoleti alimwambia ShaSha huku akimuelekezea bastola kubwa lenye nguvu, revolver, kichwani mwake, “Kama unataka utajiri we sema, nitakupa pesa na si kunifatafata mimi, mi sifuatwifuatwi namna hii, unanidhalilisha, sasa kwa taarifa yako mimi sikamatiki, na kila anayeifuata harufu yangu lazima nimmalize kama nitakavyokufanya wewe, polisi wengi na wapelelezi wan chi hii na nyinginezo wametajirikakwa pesa zangu, mimi ndio Scolleti Shang’harandha, nakuua halafu ukawaambie kuzimu kuwa chini yaofisi yangu kuna ghala kubwa la silaha za kisasa, sawa?” Scolleti alipomaliza kusema hayo. Aliondoa usalama wa bastola yake, kidole kwenye kifyatulio akakikunja huku akibana meno, ShaSha akajishika kichwani kwa mikono yote miwili akijua kuwa sasa nay eye siku yake imekwisha.
“Aaaaaaaiiiiggghhhh!!!!” Scolleti alitoa ukelele wa uchungu huku ile bunduki yake ikimtoka mkononi, na mkono wa kushoto akijishika kiganja cha ule mkono ulioshika bunduki, damu zikitiririka. ShaSha aliiwahi ile bunduki yake pale chini na kuiweka tayari kutekeleza lile alilotumwa.
“Nani alikwambia kuwa serikali hii inakuogopa?” Ilikuwa ni sauti ya Kamanda Amata akisogea taratibu pale aliposimama Scolleti, “Unajifanya unatoa misaada ya kibinadamu kumbe nyuma yake unafanya maovu makubwa ya kumuangamiza binadamu huyohuyo, sasa leo ndiyo mwisho wa yote haya.”
Kabla Amata hajamalizia kauli yake, ShaSha aliyekuwa sasa hataki kupoteza nukta, alifumua kifua cha Scolleti kwa risasi tatu, bwanyenye huyo akajibwaga chini kwenye vumbi.
“Go Bastard !” (nenda mwanaharamu ), ShaSha aliishusha bunduki yake huku akihema kwa hasira, kisha akageuka na kumtazama Kamanda Amata.
“Sorry Kamanda, najua, labda ulimtaka akiwa hai, lakini nimetimiza nililotumwa, na wakuu wangu wa kazi watapenda kuona picha za mwili huu leo hii ukiwa hauna uhai, lakini asante sana kwa kuniokoa”. ShaSha alimwambia Kamanda huku akimwendea na kumkumbatia kwa nguvu, akampa busu la ulimi. Gina kutoka pale alipo alisonya na kuita “Kamanda!”. ShaSha na Kamanda wakageuka, na kuachana.
“Gina, huyu ni ShaSha, detective kutoka India,” kisha akamgeukia Gina na kumtambulisha kwa ShaSha.
Baada ya kupiga picha kadhaa kwa kamera yake ndogo wakasaidiana na kuupakia ule mwili katika buti la ile VX kisha Kamanda Amata akapiga namba ya dharula, 112, na kuwataarifu polisi juu ya mauaji hayo akijitambulisha kama raia mwema.
Juu ya pikipiki moja wote watatu walitosha na kuondoka eneo hilo. Tayari muda huo watu walianza kutoka majumbani mwao na kuanza shughuli mbalimbali, saa kumi na mbili asubuhi.
§§§§§
9

Pambazuko la
Julai 7

MADAM S alitulia kando ya dirisha lake la ofisini, ilikuwa ni saa moja imepita tangu aingie ofisini asubuhi hiyo, hakujisikia kufanya lolote siku hiyo, mawazo na akili yake yote vilisimama, kwa ujumla alikuwa ni mtu wa mawazo mengi sana. Aliitazama saa yake na kuona bado dakika tisini Yule gaidi aachiwe huru kutoka gerezani. Akainua simu yake na kumpigia kijana wake.
“Chiba, naomba uwe unanipa taarifa yoyote ya kinachoendelea hapo Ukonga mi sijisikii kuja huko kisha tuonane hapa mchana wa leo,” akakata simu. Akabonya namba nyingine na kuweka sikioni.
“Kamanda Amata, saa nne kamili Jegan Grashan anaachiwa huru..” kabla hajamaliza kusema sauti ya Amata iliikata ile ya Madam S.
“Sikiliza Madam! Kwanini tunakuwa waoga hivi, kazi ya kukimaliza kikundi chao inawezekana kabla ya hiyo saa nne, kwa nini mnamuachia mtu ambaye amedhulumu maisha ya binadamu wengi duniani, sikubaliani na ninyi, mkimuachia najua nitachofanya lakini Grasha hawezi kuiacha hii ardhi ya Tanzania akiwa hai,” Kamanda akakata simu.
Madam S alishusha pumzi ndefu na kurudi katika kiti chake akajitupa na kuchukua kitambaa cha kufutia jasho akajifuta uso wake.
Kwa ujumla Madam S alikuwa amechanganyikiwa, hajuila kufanya, mara simuyake ikaita tena, ilikuwa nisimu ya Kamanda Amata, akaitazama na kisha akaipokea mara moja.
“Madam, hao jamaa mnaotaka kumuachia ndugu yao, wametega bomu kama si mabomu katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere pale Sabasaba, taarifa hiyo nimeipata kutoka katika tafutishizangu zausiku wa leo. Naomba kwa amri yako ulishughulikie hilo haraka sana kabla Watanzania wengine hawajapoteza maisha,” kamanda Amata alimwambia Madam S kisha akakata simu na kuizima kabisa.
Madam S, alikiona kiti cha moto, kila alipopiga simu kwa Kamanda Amata haikupatikana, mara alijishika kichwa mara akaijisjika kiuno, aliliendea dirisha kubwa lililo katika ofisi yake linaloangalia barabara kubwa, akatfakari, na kuitaza kalenda yake ya ukutani, Julai 7 iliipamba kurasa ya mbele, siku hiyo ambayo ni mapumziko ya kitaifa Tanzania ilikuwa ni siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya saba saba, maonesho ya kimataifa ya biashara ambayo hujumuisha makampuni makubwa kutoka mataifa mbalimbali, aliwasha luninga yake na kukuta matangazo ya moja kwa moja kutoka katika uwanja huo wa Mwl Nyerere. Mamia kama si maelfu ya Watanzania walikuwa wakizidi kumiminika ndani ya uwanja huo.
Madam S akakurupuka kutoka katika mawazo ambayo yalimchelewesha kutoa maamuzi, akainua simu na kupiga moja kwa moja kambi ya jeshi la Mgulani na kuwapa hiyo taarifa na kuwaomba wasiipuze.

UWANJA WA MAONESHO SABASABA

Saa 2:57 asubuhi

MUDA HUO kila aliye nyumbani alikuwa akitoka kama sin a familia yake basin a marafiki kwenda kujionea bidhaa mbalimbali zinazooneshwa huko katika viwanja vya sabasaba. Tarehe saba mwezi wa saba daima ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi wa kila aina hapa nchini isipokuwa tu wale wenye idara nyeti.
Mambo mengi sana yalikuwa huko kama vinywaji, vitafunwa, bendi mbalimbali za muziki zikitumbuiza katika mabanda mbalimbali ya biashara, michezo ya watoto kama mabembea, treni ndogo ambayo inakuzungusha kuona mandhari ya uwanja huo na kadhalika. Mistari mirefu ya Watanzania ilikuwa ikisubiri kuingia ndani ya uwanja huo asubuhi hiyo, kila mtu alitaka kuwahi kuingia ili akaitumie pesa yake vizuri, ilikuwa ni kawaida kwa kila mwaka kuwapo na tukio hilo. Polisi wenye farasi na mbwa walizagaa tayari kwa lolote maana penye wengi pana mengi.
Siku hii ikuwa mheshimiwa waziri mkuu wan chi aje kutembelea maonesho hayo, hivyo ulinzi uliimarishwa kila kona.
Katika moja ya mabanda yaliyomo humo ndani hili lilionekana kuvutia wengi sana, watu walikuwa wakijazana kuangalia umahiri wa vijana aliokuwa wakionesha katika kukabiliana na majanga ya moto na mambo ya uokoaji. Wakiwa wamevaa maguo yao ya kiung’aa ambayo hayashiki moto, kila mtu alipenda kwenda hapo kujifunza juu ya kujikinga na kuukabili moto, moto na athari zake, aina za moto na jinsi gani ya kumsaidia mtu aliyepatwa ajali ya moto. Kutokana na hilo kila mtu alisogelea banda hilo hilo kuangalia na kujifunza.
§§§§§
Ngrrrrrrrrrrrrrrrr ngrrrrrrrrrrrrrrr, simu iliita kwa fujo katika moja ya ofisi za jeshi Mgulani. Huyu bwana aliyekuwa katika chumba cha mawasiliano alikuwa amesinzia hata hakusikia kelele zote hizo za simu hiyo ya kizamani ambayo ikiunguruma lazima uzibe masikio kwa kelel zake. Akakurupuka kama aliyetoka kufumaniwa, akainyakuwa na kuiweka sikioni.
“Hallo, hapa ni kikosi cha jeshi Mgulani, nikusaidie nini?” aliongea askari Yule.
“Unaongea na idara ya usalama wa taifa, naweza kuongea na mkuu wa kambi?” sauti ya madam S iliunguruma katika chombo hicho. Yule askari akatulia kwa pozi na taharuki, kisha akajibu, “Subiri na usikate simu tafadhali,” alijibu.
Baada ya sekunde chache Madam S aliunganishwa na mkuu wa kambi hiyo, kambi ya Generali Twalipo, taarifa ya tetesi za bomu ilimfikia mkuu huyo, Meja Jenerali Kisanga, naye akapeleka taarifa panapohusika, muda huohuo wakapewa taarifa wataalamu wa milipuko wa jeshi, wakajiandaa na kila kitu kinachohitajika wakaingia kwenye jeep takribani tatu za kijeshi, safari fupi ya kufika eneo hilo ikawadia.
Kila mtu alishangaa katika ule uwanja wa maonesho, wanajeshi kama thelethini wakiwa na vifaa vya ajabu waliteremka na kusimamaisha zoezi la watu kuingia ndani ya uwanja huo, kisha kutoa taarifa kwa wanausalama waliopo humo ndani kuanza kutoa watu wote waliomo ndani ili uwanja huo ubaki mweupe yaani bila watu. Kiongozi wa oparesheni hiyo alitoa amri mara moja watu wote kutolewa nje, msafara wa waziri mkuu ukasitishwa kutoka nyumbani kwake kwenda katika viwanja hivyo, hali ikawa tete, milango ya kuingilia uwanja huo haikuwa ikitosha kutokea, kila mtu alifikiri kuokoa maisha yake.
Wanajeshi waliokuwa na vifaa mikononi vya kuweza kutambua milipuko waliingia ndani ya uwanja huo na kutembea kila mahali kutafuta uwezekano wa kuwepo aina yoyite ya mlipuko.
Counter-IED kifaa maalumu kwa kazi hiyo kinachofanya kazi peke yake bila kushikwa na mtu kilitumwa kuingia katioka uwanja huo, kilikuwa kikitembea barabarani taratibu kikisimama hapa na pale, huku wanajeshi wengine wakitapakaa sehemu mbalimbali. Bado watu walikuwa wakiendelea kutoka katika uwanja huo, ilikuwa ni patashika kweliweli.

GEREZA LA UKONGA

Saa 09:00 asubuhi

GARI za ofisi ya ubalozi wa nchi ya Jegan Grashan ziliingia katika geti la Magereza lililoko upande wa kaskazini mwa ngome hiyo, zikajivuta taratibu kuelekea lango kuu la gereza mpaka kwenye maegesho. Waandishi wa habari kama kawaida walikuwa hapo wakitaka kushuhudia na kupiga picha za gaidi huyo ambaye siku hiyo alikuwa akiachiwa huru. Askari wa KM wa Magereza walikuwepo kulinda usalama kama kuna hatari yoyote itakayotokea.
Kamishna wa magereza, mkuu wa magereza mkoa wa Dar es salaam na wahusika wengine walikutana kwenye chumba maalumu kwa ajili ya kukabidhiana mfungwa huyo. Maofisa wa ubalozi walikuwa pale tayari kumchukua raia wao. Ilikuwa utata mtupu. Jegan Grashan aliletwa ndani ya chumba hicho akiwa na pingu pamoja na minyororo miguuni mwake akasimamishwa sehemu ndani ya chumba hicho hicho.
Saa 09:15 asubuhi
Kamanda Amata, alikuwa juu ya pikipiki lake akielekea Ukonga kushuhudia zoezi hilo, Madam S alikuwa akifunga ofisi na hajui aende wapi, ama sabasaba au Ukonga, alikuwa akijishika kichwa kila mara kujiuliza la kufanya, hali ilikuwa sio nzuri kichwani mwake, mama huyu alijiona kwa siku hiyo moja kazeeka ghafla.
Wakati huohuo, freedom fighters walikuwa tayari kwenye sehemu waliopangiana kukutana, lakini walishangaa wawili kati yao walikuwa bado kufika, wakajaribu kupigiana simu ili kujua kulikoni majibu waliyoyapata yalikuwa tata. Maafa, maafa ni hali iliyowakata matumaini ya kumpata mwenzao, mara kidogo wakapata taarifa ya kuuawa kwa Scolleti hapo wakachanganyikiwa, hawakujua wafanye nini. Shailan aliamua kuwapanga vijana wake upya, akawaita hao wote walio katika yadi zile waende haraka katika point ya kukutania ambapo wenzao wote tayari walikuwa kwenye boti maalumu wakisubiri kufuinguliwa kwa ndugu yao, waondoke naye.
Saa 09:30 asubuhi
Madam S anazinduka, anawasha gari kuelekea Ukonga, ilikuwa ni mapumziko hivyo hakukuwa na foleni barabarani, aliendesha kwa kasi gari yake aina ya BMW, ili awahi tukio hilo, alipuuzia simu zote zilizokuwa zikiita, wakati huo. Akili na mawazo yote yalikuwa kuwahi Ukonga.
Kamanda Amata alikuwa tayari kawasili eneo la tukio, akaegesha pikipiki lake nje ya wigo na kutulia usawa kabisa wa lango kuu, akitenganishwa na barabara ya Pugu na seng’enge iliyolinda gereza hilo, alimuona Madam Salipokuwa akiingia getini na gari yake, Kamanda akatikisa kichwa kuashiria, ‘kazi imeamka’.
Kichwani mwake Kamanda alikuwa na mambo mengi lakini alishindwa afanye nini, Sabasaba aliamini kabisa kuwa JW watakamilisha hiyo kazi ya kuutafuta huo mlipuko, lakini magaidi wengine walikuwa wametoroka na mpaka hapo hakujua wamekwenda wapi, alikuwa akisubiri milipuko aliypitengeneza katika yadi zile ifanye kazi, lakini zaidi alikuwa akitaka kumuona huyo Jegan Grashan akiachiwa huru, akabaki juu ya pikipiki lake huku akili ikiwa imesawajika, haijui jema wala baya.

§§§§§

SHAILAN aliinua mkono wake kutaza saa yake aina ya casio, tayari muda ulikuwa ukiyoyoma, alikuwa akisubiri taarifa ya kutoka kwa Tashrini aliyekuwa pale gerezani, ili awaambie tu kuwa ndugu yao kaachiwa nao waanze sherehe kwa kufungua champagne.
Yote yalikuwa sambamba, vijana wa JW wakati huo kijasho kikiwatoka kusaka huo mlipuko walioambiwa lakini bado walikuwa hawajang’amua chochote, walianza kukata tama, wakisema hakuna mlipuko wowote kwani kila mahali ni salama kabisa, walitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya usalama. Na wao kujipanga kuondoka kurudi kambini.
Chiba na Gina walikuwa wakielekea uwanja wa maonesho ya sabasaba kushuhudia hali ilivyo, wakapata taarifa hiyo ya kuwa kila kitu kiko salama.
“Hapana Chiba, kuna mlipuko kule umewekwa, naamini kabisa, kwa maana walipokuwa wanautengeneza nilisiki amazungumzo yao!” Gina aliongea kwa jazba huku akipigapiga dashboard ya gari ya Chiba.
“Basi mama utavunja gari yangu wakati hata mkopo benki sijamaliza,” Chaba akajibu kwa utani.
Mara Chiba akaitoa gari yake baranbarani na kuiweka pembeni alipokuwa maeneo ya polisi ufundi.
“Vipi?” Gina aliuliza.
“Kuna mawimbi ya kielektroniki ya kigeni kabisa yamepita kwenya kompyuta yangu,” akafungua dashboard ya gari kwa kubonyeza mahali Fulani, kulikuwa na kijikompyuta kidogo, akaingiza nywila zake nayo ikaanza kufanya kazi, akabonya hapa na pale, akaanza kusikia mawimbi mbalimbali ya sauti, huku yakiwa yanajichora kwa mistari ya kuyumbayumba lakini pia yalikuwa yakifanya sauti Fulani. Chiba alijaribu kuiweka sawa sauti hiyo ili aweze kupata tafsiri ya mionzi hiyo, akajaribu na kujaribu lakini ilikuwa ngumu kuigundua kirahisi, akapima umbali inapotoka na inapokwenda kwa kutumia namba maalumu anazojua mwenyewe.
“Gina, kuna hapa kuna kitu hakiendi sawa, nikizungusha antenna yangu, inaniambia kuna mawimbi mapya na mageni yanatokea mashariki kuelekea, range yake sio mbali sana,” Chiba alikuwa akituamia chombo maalumu kilichofungwa katika gari yake, chombo kinachojulikana kwa jina ‘MiniGRAIL’ kinachoweza kunasa mawimbi yoyote ya kielektroniki yanayopita hewani. Chiba akachuku laptop yake yenye nguvu, akapachika vifaa maalumu vya kusikilizia, kisha akamwambia Gina aendeshe gari kuelekea uwanja wa sabasaba.
Saa 09:45 asubuhi
“Jegan Grashan, uliyefungwa kwa tuhuma za ugaidi katika ofisi za balozi ya Marekani, unaachiwa huru na serikali ya Tanzania kwa tamko la Rais wan chi, kuanzia saa nne kamili leo hii utakuwa raia huru. Pamoja nahayo, serikali inakutaka kuondoka nchini ndani ya masaa 12 kwa njia yoyote, na hutakiwi kukanyaga tena ardhi ya Tanzania, iwe wewe, mkeo au watoto wako, imesainiwa jana tarehe 6 Julai na kugongwa mhuri wa Ikulu.” Hati hiyo ‘removal’ ilisomwa na kamishna wa MagerezaTanzania huku akitetemeka, alipomaliza, alimtaka Jegan kusaini mahali Fulani, akafanya hivyo kisha nay eye akasaini pale panapomstahili, wakapeana mikono na zoezi hilo likakamilika, Jegana akatakiwa kuketi chini kusubiri saa nne kamili ili atoke nje ya gereza.
Madam S aliyefika kwa kuchelewa kidogo, alikuta ndiyo wakisoma hiyo hati kutoka Ikulu, akatulia na kushuhudia huyo jamaa akimwaga wino wa kuondoka kama raia huru. Ijapokuwa ilimuuma lakini hakuwa na jinsi, ikishaandikwa na Rais basi haiwezi kubadilika labda abadili yeye mwenyewe.
Japokuwa siku hiyo ilikuwa ni mapumziko lakini pia ilikuwa siku ya maombolezo ya watu waliopoteza maisha kwenye pantone eneo la Kivukoni siku iliyotangulia.

§§§§§

Gina aliegesha gari nje ya uwanja wa maonesho ya biashara ‘sabasaba’ Chiba akashuka na kompyuta yake akawa akieelekea ndani ya uwanja huo. Moja kwa moja akiongozana na Gina walifika kwenye banda kubwa la maonesho, banda la zimamoto, liliandikwa kwa nakshi nzuri, FK SECURITY and FIRE BRIGADE, banda hilo lilijawa na watu kama mwanzo wakiangalia hayo maonesho ya uokoaji. Chiba alipofika eneo hilo, akaingia ndani ya ofisi kubwa iliwekwa vitu mbalimbali, sasa akagundua kuwa yale mawimbi aliyoyanasa yanaishia hapo kati banda hilo. Akavua makorokoro yake na kuyaweka mezani akachukua simu yake na kubofya namba flani.
“Chiba anaongea,” alizungumza mara tu baada ya simu ile kupokelewa na Madam S,
“Ndio Chiba niambie,” Madam S alimwambia.
“Kuna mawimbi ya kielektroniki nimeyagundua katika mtambo wangu, na nimeyafuatilia sasa nipo hapa uwanja wa sabasaba, nina wasiwasi na banda hili la FK Security maana signal zinaonesha kuwa hapa niliposimama ndio point ziro, nipe mamlaka nifanye kazi inaonekana kuna hatari kubwa sana eneo hili,” Chiba alimaliza. Kila mtu aliyekuwa ndani ya banda hilo alimshangaa Chiba, hakumuelewa ni nini alikuwa akisema.
Madam S, alijikuta akidondokwa na simu mikononi, akiwa kapigwa na bumbuwazi, akili ikamchanganyika, akamtazama Jegan pale kwenye kiti, kisha akaiokota simu yake.
“Fanya lolote kuzuia hali hiyo,” Madam S alijibu, kisha akapiga namba ya Kamanda Amata na kumpa taarifa hiyo, akatoa tena taarifa Jeshini kwa mara nyingine.

§§§§§

Shailan, Shakrum wakiwa ndani ya boti wakimsubiri Jegan, muda wao ulikuwa umefika wa kile wanachokiita ‘kutoa shukrani kwa Watanzania’, Shakrum alifungua briefcase yake kubwa na kuanza kubofya hapa na pale akipanga renji na kila kitu, kisha akawasha kuitafuta sakiti aliyoitengeneza ndani ya tanki la mafuta lakini lililojazwa gesi aina ya methane upande mmoja na mwingine liquefied petroleum gas (LPG), vyote vilikuwa vimeshindiliwa kwa mkandamizo mkubwa sana kiasi kwamba zikidaka moto basi ilo tanki lote lazima ligeuke kombora baya kuliko kombora lenyewe.
Shakrum alipofanikiwa kupata uelekeo wa sakiti hiyo na kuanza kuhesabu muda wa kuiwasha ili itengeneze moto ndani ya tanki hilo, tayari Chiba alikuwa ameyanasa mawimbi hayo, hivyo alichokifanya hapo sasa ilikuwa ni jinsi gani ya kuyakata, ili kusiwe na mawasiliano kati ya vitu hivyo viwili. Chiba akaendele kucheza na kompyuta yake, ilikuwa ngumu kuelewa ni nini anakifanya kwa ni ni namba tu zilizokuwa zikonekana kupishana na katika kioo cheusi cha kompyuta. Kwa kutumia program maalum kwa kazi hiyo ambayo Chiba aliipata wakati akiwa katika mafunzo huko NASA alifanikiwa kuyakamata mawimbi yale na kuyafanya yasitende lililokusudiwa, kisha akaanza kufanya ukaguzi sehemu mbalimbali za jengo lile.
“Oooh shiiit!” Shakrum alionekana wazi kuchanganyikiwa kwa hilo, aligundua kuwa kuna muingiliano wa mawimbi umetokea, kila alipojaribu bado alijikuta anakwama, nywele zikamsimama.
“Washenzi wameyaingilia mawimbi yangu,” akamwambia Shailan.
“Inawezekanaje?” Shailan akauliza. “Itakuwa kuna mtaalam wa mambo haya ndiye kafanya hili” Shakrum akajibu.
“Sasa tutafanyaje?” Shailana akauliza.
“Hatuna jinsi kama inawezekana hapa ni kufika eneo husika na kutumia mbinu nyingine, mbinu mbadala ya kulipua lile tank bila ya sisi kudhurika,” Shakrum alieleza huku akiisogeza kompyuta byake pembeni, akakizungusha kiti na kugeuka walipo wenzake. Mara simu ya Shailana ikaita, alipoitazama ilikuwa namba ya Tashrini, akajua mambo yameiva, kwa vyovyote vile.
“Ndiyo Tashirini, nipe taarifa,” Shailan alizungumza kwenye simu.
“Jegan yuko huru na sasa anatoka gerezani, nasikia kelele nyingi za wafungwa wengine, zikimsindikiza nje,” Tashrin akajibu.
“Mungu mkubwa, kamwe hamtupi mja wake, hii ndiyo njia pekee ya kuwashinikiza hawa wanaojipendekeza kwa mataifa ya Maghalibi,” Shailan alijibu huku wengine wote wakishangilia.

Saa 04:00 asubuhi – Gereza la Ukonga

JEGAN Grashan aliachiwa huru, hakuwa na pingu za mikono wala za miguuni. Alitembea kwa hatua zake mwenyewe ijapokuwa alikuwa na uchovu kidogo. Madam S na wakuu wengine waliokuwa pale, walimshuhudia gaidi huyo akiondoka taratibu katika gereza hilo, akipita katika mlango mkubwa na kuelekea katika gari la ubalozi lililoandaliwa huku akisindikizwa na maofisa usalama wa ubalozi wa nchi yake, akaingia na kufunga mkanda sawia, akashusha kioo na kumuonesha Madam S alama hya mkono akiashiria kuwa amemtukana tusi baya kabisa, ile gari ikaondoka. Msafara wa gari nne zenye namba za njano kwenye kibao cha kijani zililiacha geti la gereza na kushika barabara ya Nyerere kuelekea mjini.
Kamanda Amata akawasha pikipiki lake na kuvaa kofia yake ya usalama iliyomficha uso wake, moyo wake ulijawa na gadhabu ya kuachiwa huru Jegan, hakupenda hata kidogo. ‘Liwalo na liwe,’ akajisemea na kuaca kati yake na wao magari kama sita hivi kisha akaingia barabara ni na kuondoka.
Uwanja wa maonesho sabasaba
Gina alisikia mlio wa beep kutoka eneo Fulani lililokuwa na matanki makubwa kwa ajili ya maonesho ya kampuni hiyo.
“Chibaaaa!” akamwita kwa ukelele, Chiba akaacha kompyuta yake na kukimbilia kwa Gina, akausikia mlio wa beep hiyo, haraka sana akapanda juu ya tanki moja na kulifungua kwa shida mfuniko wake, ule mlio ulikuwa ukiongezeka. Wakati hayo yakitukia, polisi waliokuwemo uwanjani wakisaidiana na vijana wa skauti kutoa watu nje ya uwanja, na kuwaweka mbali na eneo hilo, vijana wa jeshi walirudishwa tena kuhakikisha usalama huo.
Chiba alikuwa akifungua ule mfuniko kwa tabu maana aulifungwa kwa kifungo maalum, haikuwezekana kukata kwa gesi maana unaweza ukasababisha mlipuko usio wa lazima.
§§§§§
Kamanda Amata akiwa tayari kwenye pikipiki yake aliingia barabara ni, nyuma ya msafara wa gari zilizombeba Jegan, kichwa chake kilishatawaliwa na gadhabu mbaya juu ya mtu huyo, hakuamini kabisa kuwa anakuwa huru na kuacha uovu wake, hapana, bali aliamini wazi kuwa bado maadamu yupo hai basi ataendelea kufanya yale anayokusudia kwa raia wengine wasio na hasira, alivuta mafuta na kutafuta sehemu nzuri ambayo angeweza kufanya yake, kufanya lile alilokusudia. Kama unavyojua kasi ya gari za ubalozi haikuwa ya kawaida, yakiwa yamewasha vimulivimuli na kupishwa yalikuwa yakienda kasi kwelikweli. Mara saa ya Kamanda ikaanza kutoa kamlio hafifu, akauinua mkono na kuisikiliza inasemaje.
“Kamanda Amata, Chiba hapa,” alikuwa ni Chiba aliyekuwa akimpigia Kamanda wakati huo.
“Nimekusoma chiba endelea,” kamanda aliirusu simu hiyo.
“Nipo, uwanja wa maonesho wa sabasaba hapa Mtoni Mtongani,” akaendelea kusema.
“Endelea,” Kamanda akamruhusu aendelee kuzungumza.
“Kuna aina ya mlipuko ambayo imetegwa hapa, sasa najaribu kutafuta chanzo lakini naona kidogo utaalam unaniishia, pamepekuliwa kwa mitambo ya kisasa lakini hakujaonekana bomu wala kitu kinachofanana na hicho, nipe aidia mpya tafadhali,” Chiba alieleza lile linalomsibu.
“Ok, jaribu kutazama mitungi ya gesi kama ipo maana nayo inaweza kufanya milipuko mibaya kuliko bomu lenyewe, hakikisha kwa amri yako umeclear eneo lote ili kama itabidi kufa basi ufe peke yhako kama kiapo chetu kinavyosema, niko njiani kuja huko huko, Jegan Grashan amekwishaachiwa huru,” Kamanda Amata alimjibu na kukata simu ile kisha akarudisha mkono kwenye usukani wa pikipiki na kuongeza kasi zaidi na zaidi, alikuwa akipita gari kwa overtake za hatari mpaka madereva wa magari walikuwa wakitukana kila mtu kwa lugha yake. Dakika mbili baadae aliziona zile gari za ubalozi zikiwa kasi katika eneo la Karakana karibu na Tazara, sekunde chacahe akawa ameufikia msafara huo.
‘Mtu wenu anaachiwa ninyi bado mnataka mtulipue, sasa leo ama zangui ama zenu,’ Kamanda alijisemea huku akiupita ule msafara kwa kasi na kuwa mbele yake. Kisha kama mtu aliyepagawa alikunja kona kali na kuwa mbele yao, zile gari nazo zikafunga breki kali mbele ya pikipiki hiyo zikisota na kufanya ukelele mkali kwa msuguano wa tairi za barabara, gari mbili za nyuma ziligongana zenyewe kwa zenyewe na ile ya mbele almanusura imgonge Kamanda ambaye tayari alikuwa na bastola mkononi, alikwishaiondoa usalama na alikuwa akiitafuta shabaha yake anayoitaka. Kidole cha shahada kikaitekenya ile bastola, risasi tatu zilipasua kioo na kufumua kifua cha Jegana Grashan.
Muda na saa hiyohiyo
Milipuko mikubwa ilitokea katika maeneo mawili tofauti, mmoja katika yadi ya Bunju ya kuhifadhia mafuta iliyokuwa ikimilikiwa na Scolleti nay a pili yadi ya Mabibo, kwa nukta na sekunde ileile mabomu yaliyotegwa na Kamanda Amata yalifanya mambo yaliyokusudiwa.
Mji wa Dar es salaama ulipatwa na hekaheka siku hiyo kwani barabara ya Ally Hassan Mwinyi ilifunikwa na gari za zima moto na ile ya Mandela nayo vivyo hivyo. Moshi mkubwa ulitanda anga ya Dar es salaam. ‘Kama walijifan ya wao magaidi basi hawakujua kama na mimi ni gaidi zaidi yao,’ Kamanda alijisemea huku akipita vitongojo vya katikati vya wilaya ya Temeke, akafika mahali kulikuwa na nyumba nyingi zilizobanana, Kamanda Amata alipinda kona na kuingia katika ua wa nyumba hiyo, moja kwa moja akaiegesha pikipiki yake kwenye stoo ndogo ya mkaa, akaizima, akina mama waliokuwa wakifua na kuosha vyombo walipiga kelele na kuwanyakua watoto wao.
Kamanda Amata akashuka na kuvua ile kofia ngumu akaipachika juu ya kioo cha kutazamia nyuma, akavua yale mavazi ya kuendeshea pikipiki na kuyaweka pale juu, akabaki na suti safi nyeusi iliyopambwa na tai ya buluu, hakuongea na mtu alitoka haraka na alipofika nje alipanda tax aliyoikuta barabarani.
“Sabasaba tafadhali,” alimwamuru dereva.
§§§§§
Watu wa usalama wa ubalozi walijitahidi kumsaidia Jegan Grashan lakini walichelewa, ilikuwa ni mvurugano eneo lote, wamachinga walikimbia huku na huku , wakiijaribu kunusuru maisha yao.
Wanausalama wa ubalozi hawakuwahi kumkamata Kamanda Amata kwani tayari Alishakwisha waacha mbali. Wakabaki wakitizamana hawana la kufanya.
Muda si mrefu, Land Cruiser moja nyeusi ilipunguza mwendo katika eneo hilo la ajali ambapo polisi wa usalama barabarani alikuwa tyari yuko kazini na wale maofisa wa ubalozi wakiwa wamezagaa nje na bastola zao mikononi. Kioo cha gari ile kikateremka taratibu, Madam S, akatzama lile tukio, akatikisa kichwa chake na kupandisha kioo kisha gari ikaongeza mwendo na kupotelea mjini.
§§§§§
Habari mbaya zilimfikia Shailan na Shakrum waliokuwa katika boti wakisubiri wenzi wao ili watoroke na kuwaachia Watanzania vilio vikuu ndani ya siku wanayoipenda, siku ya Julai saba. Shailana alihisi kuchanganyikiwa, kwanza kwa habari ya kifo cha Scolleti, pili milipuko ya yadi zote mbili, haikumuuma sana kwani si mali yao, ila hili la kifo cha Jegan Grashan, Shailan na Shakrum walilia machozi huku wakiwa wamekumbatiana, na walikuwa hawajui hatima ya wenzao waliokuwa katika yadi hizo ambao walikuwa wakiwasubiri pamoja na Tashirni aliyeleta taarifa hiyo. Shakrum akaiendea televisheni na kuiwasha, hakukosea, kioo kilikuwa kimepamba kwa maua ya moshi mzito na wakati mwingine kwa tukio la Kalakana pale Tazara, hasira akazima Tv na kurudi kwenye kompyuta yake, akaketi lakini alipojaribu kuichezea akakuta imefungwa kwa codes maalum ambazo hakujua ni nani aliyefunga, “Shiiiiiittttt!” akapiga ukelele nan kuipiga ngumi ile kompyuta.
Shakrum na Shailan hawakuwa na la kufanya, walitamani waondoke peke yao lakini hawakuona vema, akaendelea kusubiri wenzao mpaka muda waliopanga.
Saa 4:30 asubuhi
Simu ya Kamanda Amata ikaita tena wakatyi akiwa maeneo ya Tandika kuelekea sabasaba, akaitazama, Madam S, akatabasamu, ‘Lazima kapata salamu zangu pale barabarani’ akajiwazia.
“Kamanda, upo wapi?” akauliza kwa ukali.
“Nipo Sabasaba Madam vipi?” Kamanda akajibu.
“Hivi we una akili kweli?” Madam akafoka kwenye simu.
“Kwanini Madam? Nina akili timamu kabisa,” Kamanda akajibu.
“Unajua unachokifanya wewe? Sasa umeshaharibu na we mwenyewe unalijua hilo,” Madam akaendelea kufoka kwenye simu.
“Madam tutaongea ofisini mi nipo kazini kwa sasa,” Kamanda akajibu na kukata simu.
Madam S alikasirishwa sana na kitendo alichokifanya Kamanda Amata, alipopita katika eneo lile la tukio na kuona hali halisi alijua wazi ni Amata kwa sababu alikwishasema mbele yake na alishakula yamini juu ya hilo. Alijua nini kinakuja kumkuta Amata, Madam alilia machozi kwa hilo, alisikitika na kuumia sana, lakini lilikuwa limekwishatokea, hakukuwa na jinsi. Aliendesha gari yake taratibu kuelekea uwanja wa maonesho ya sabasaba.
§§§§§
Chiba alifanikiwa kuufungua mfuniko wa tanki kubwa la gesi, kosa moja alilolifanya ni kuwa hakujiandaa kwa hali hiyo, ijapokuwa aliipata sakiti iliyofungwa chini tu ya mfuniko huo lakini yeye mwenyewe aliathirika sana na ile gesi mbaya. Gina alimshuhudia Chiba akianguka kutoka katika lile tanki kwa msukumo mkubwa sana, akajishika mdomo kwa kiganja cha mkono wake, akili ikaja haraka, akageuka huku na kule, na kuona kabati lenye gas mask, akalivunja na kuchukua, akaivaa haraka kisha akakimbilia kule aliko Chiba akiwa na mask nyingine iliyojazwa hewa ya oksijeni na kumvika Chiba.
“Msaada!” alipiga kelele ndipo vijana wa jeshi walipoona jambo lile, nao haraka wakawahi mask na kwenda kufungaa mfuniko wa tanki lile kwa tabu sana kwani mkandamizo wa gesi ulikuwa ni mkubwa hivyo mvujo wake nao ulikuwa wa nguvu sana. Bkutokana na ujasiri na ukakamavu wa vijana hao walifanikiwa kuufunga na kupunguza athari ya gesi hiyo.
Hali ya Chiba ilikuwa mbaya, Gina akamkokota na kutoka nae katika eneo leneye hewa, kwa bahati nzurti katika banda hilo kulikuwa na gari ya wagonjwa iliyowekwa kwa ajili ya maonesho, kmpakia Chiaba nay eye akaketi katika usukani, na kuitoa gari hiyo kwa kasi eneo lile huku akiwa amewasha ving’ora vyote. Akainua simu na kumpigia dokta Jasmine. Dr Jasmine akamwelekeza moja kwa moja ampeleke hospitali ya taifa Muhimbili, Gina alitoka katika geti la uwanja huo kwa kasi na kuingia barabara ya Kilwa kurudi mjini.
Kamanda Amata alipishana na ile gari ya wagonjwa lakini hakujua kuna nini ijapokuwa dereva wa gari ile aliweza kumfananisha. Alikimbia haraka mpaka kwenye banda husika na kukuta vijana wa jeshi wakihaha huku na huku kujarib u kudhibiti hali iliyokuwepo hapo. Kamanda Amata alipofika alizuiwa kupita eneo hilo lakini kwa kitambulisho chake alairuhusiwa huku akipewa mask na kuivaa, akaingia ndani ya banda hilo na kukuta baadhi ya wanajeshi wakijaribu kutoa huduma ya kwanza kwa wafanyakazi ambao walikuwamo ndani ya banda hilo lakini gesi ile iliwaathiri. Kamanda Amata akaiwahi kompyuta ya Chiba iliyokuwa juu ya meza Fulani, ilikuwa inaendeleaa na kazi ambayo Chiba alikuwa anaifanya.
Akatazama kwenye kioo cha kompyuta hiyo, akaelewa kilichokuwa kinafanyika mara ya mwisho. Chiba kabla hajaenda kutafuta sehemu ya mlipuko alikuwa akijaribu kutafuta uelekeo wa wapi mawimbi yale ya kielektroniki yalikuwa yakitokea, mpaka yeye anaiacha kompyuta hiyo bado ilikuwa ikiendelea, Kamanda Amata akasoma nyuzi (degrees) zilizojiandika, akaelewa, kilikuwa kipimo cha ardhi katika longitude na latitude, na eneo husika lililolengwa kadiri ya nyuzi hizo aligundua ni maeneo ya Kigamboni, akaendelea kuperuzi na kwa chini kidogo, akasoma kwa makini sana namba zile zilizokuwa zikibadsilishana hapa na pale ili kupata uelekeo sahihi.
“Kigamboni Kaskazini,” akajisemea na kisha akiinua ile kompyuta na kutoka nayo mpaka nje, akatzama huku na kule na kuiona gari ya chiba akaiendea, akaingi na kujifungi ndani yake, kama anavyofanya Chiba, akaunganisha ile kompyuta na kijimtambo maalum kilichofungwa ndani ya gari hiyo, sasa akaweza kusoma eneo halisi kwa kutumia screen ndogo iliyopo ndani ya gari hiyo, akaiwasha na kutoka katika uwanja huo, akachukua simu ya upepo iliyo ndani ya gari hiyo na kubofya kitufe Fulani.
“Madam S, Madam S,” akaita kwa mtindo huo.
“Nakupata Chiba,” madam S akajibu.
“Hapana sio Chiba, hapa ni Kamanda Amata,” akamrekebisha.
“Nimekusoma nipe ripoti,” akaendelea Madam.
“Natoka uwanja wa maonesho wa sabasaba, hali sio mbaya sana lakini Chiba inaonekana ana hali mbaya ameondolewa na Gina kuelekea hospitalini, la pili inaonekana kuna jambo maeneo ya Kigamboni kadiri ya tafutishi nilizozikuta katika kioo cha Chiba, niko mbioni kuelekea huko, haraka iwezekanavyo.” Kamanda akabofya kitufe kingine katika redio hiyo.
“Umesomeka Kamanda, mama anabadili uelekeo, tukutane Kigamboni,” madam S akamaliza na kukata ile simu.
Simanzi na majonzi viliwajaa Shakrum, Shailan na wengine waliokuwa ndani ya boti, ukimya ulitawala wakati injini ya boti hiyo ikiwa inaunguruma kwani muda ulikuwa tayari umewadia wa kung’oa nanga. Kutoka mbali Shailani aliona kitu kama boti ndogo inayokuja kwa kasi, akachukua darubini na kutazama hakuamini macho yake kwa kile anachokiona, Tashrini na wengine wawili walikuwa katika boti hiyo wakija kwa ajili ya safari. Ingawa wao walisalimika lakini maumivu makaubwa yalibaki kwa ndugu yao Jegan Grashan. Dakika tatu tu ile boti ilifika ukingoni kabisa mwa ile boti kubwa ya akini Shakrum, wakashuka na kuhamia katika boti hiyo kisha milango ikafungwa tayari kwa kuondoka.
“Maafa yaliyotokea ni makubwa sana,” Tajan alimweleza Shailan.
“Nini?” aliuliza Shakrum.
“Akiba yote ya mafuta kamanda Amata kalipua yadi zote mbili hivi tunavyoongea zinateketea kwa moto. Scolleti amekwishauawa na Yule mwanamke wa Kihindi, Jegan nae kapigwa risasi na mtu asiyejulikana,” Tajan alitoa ripoti. Shakrum alikuwa amesimama akimsikiliza, mara hiyo akajiegemeza katika moja ya nguzo zilizo katikati ya boti hiyo akiwatazama wenzake hao.
“Na mlipuko wetu umetenguliwa kule sabasaba, wametuweza, kiukweli sikufikiri kama hawa jamaa watakubali Jegan aondoke hivihivi,” Shakrum alieleza.
“Jamani, hapa tumeshacheza pata potea, washa mashine tuondoke, si ajabu na sisi wakatukamata hapahapa au wakatushushia kombola moja tu tukapotea wote,” Shaiilan aliwaeleza wenzake, injini ikawashwa, milango ikafungwa, kiyoyozi kikaanza kuyoyoza, taratibu chombo kikaanza kuondoka eneo hilo kikichanganya polepole na kugeuka kuelekea upande mwingine, kila mmoja ndani ya chombo hicho alikuwa tayari ameketi mahala pake aliyekuwa anafungua kinywaji sawa, aliyesoma gazeti sawa, tayari walikuwa wamekwishaamua kuondoka.
§§§§§

OFISI ZA UBALOZI WA KHAZAKISTAN

Gari za ubalozi ziliingia katika kiwanja cha ofisi hizo, maofisa wa usalama wakashuka na kuiendea gari iliyokuwa haina kioo, ndani yake alikuwamoi Jegan Grashan.
“Nilijua hawawezi kukuacha hivihivi,” alisema mmoja wa maofisa hao alipokuwa anamvua bullet proof Jegan.
“Dah! Mungu mkubwa, nashukuru mlijiandaa Yule jamaa alikuwa ananimaliza kabisa,” Jegan alijibu huku akimkabizi Yule mwanausalama lile koti. Jegan Grashan akateremka garini na kukanyaga ardhi ya uraiani, kwa hatua za polepole huku akiwa ameshikwa mkono na mmoja wa wanausalama ambaye mkononi mwake alikuwa amekamata short gun alisindikizwa kuingia ndani ya jengo hilo.
“Ni saa nne sasa karibu na dakika arobaini na tano, boti itakuwa inang’oa nanga, kwa vyovyote vile wao wanajua wewe umekwishakufa,” ofisa mwingine wa ubalozi alimweleza Jegan.
“Haina shaka, naweza ungana nao sasa na kuondoka, asanteni sana,” Jegan aliwashukuru na kuwakumbatia mmoja mmoja, kisha akakiendea chombo cha mawasiliano na kuwasiliana na ndugu zake hao walioko ndani ya boti.
Jegan aliingizwa kwenye chombo maalum na kufungiwa ndani yake kisha ikabonyezwa swichi Fulani na chombo kile kikawasha injini zake ndani ya chumba maalumu kilichojazwa maji ambacho moja kwa moja kinatokea kwenye mkondo wa bahari. Dakika moja baadaye kile chombo kikasukumwa kwa nguvu na kutoka ndani ya jengo kwa kupitia kidirisha Fulani, kikapaa na kujibwaga baharini kisha kwa mwendo wa kasi kikapotelea baharini.
Ndani ya boti saa 4:45 asubuhi
Furaha na shangwe ziliijaza boti hiyo baada ya kusikia sauti ya mpendwa wao Jegan ikawahakikishia kuwa yuko hai, hajafa. Furaha ilikuwa mara mbili ya ile ya kwanza pale walipokipokea chombo maalumu kilichomhifadhi Jegan, na walipofungua ndani walimtoa ndugu yao huyo na sherehe ikawa sherehe, shampein, risasi za hewani vyote vililindima katika boti hiyo, nyimbo zikaimbwa na kuchezwa, kati yao wote hakuna aliyepotea, wote walikutana tena kama ndoto yao ilivyokuwa.
“Nimeachiwa huru, asanteni sana kwa juhudi zenu za kuishinikiza serikali ya Tanzania, mmefanya lililo jema hata sasa niko nanyi. Lakini huu sio mwisho wa mapambano, huu ni mwanzo, lazima tuikomboe nchi takatifu kutoka katika mikono ya watu wa Maghalibi na vibaraka vyao. Nisingeelewa kanchi kama haka ka Afrika mashariki kajifanye kana sauti ya kupambana na sisi, dunia yenyewe inapiga magoti mbele yetu, wao ni nani? Hawakujiuliza kuwa kwa nini Amerika na washirika wake kama Uingereza, Ufaransa na wengineo wako kimya? Wote hao wanajua kuwa freedom fighters tunajua tunachokifanya wanajua hilo ndo maana walibaki kimya,” Jegan Grashan alitoa hotuba ya nyodo katika boti na kufuatiwa na nderemo za wafuasi wake. Hakukuwa na linguine zaidi ya kuondoka, safari ikaanza taratibu, boti ile ilikuwa ikiambaa na maji ya bahari ya Indi ikichana mawimbi kuelekea Mombasa ambako wenzi wao walikuwa wakiwasubiri.
§§§§§
Kamanda Amata alijirusha majini na kupiga mbizi, akipita chini kwa chini kuielekea ile boti ambayo ilionekana kwa mitambo maalumu ya kijeshi pale kigamboni. Msoma rada alieleza wazi kuwa walikuwa wakiichunguza boti hiyo karibu masaa kumi tangu imefika eneo hilo, hawakuitilia nashaka kwa kuwa ilikuwa ikipepeza bendera ya ya Tanzania. Siku hii ndipo walipogundua kuwa haikuwa boti ya kawaida bali imeingia hapo kwa shughuli maalumu.
Madam S alimtazama Amata akipotelea majini, nay eye alirudi upande mwingine ambako kulikuwa na wanajeshi wanamaji waliojiandaa tayari kwa lolote lile. Kamanda Amata alipewa maagizo ya kuhakikisha kuwa waliopo wanakamatika wakiwa hai na uhai wao. Aliifikia ile boti kwa muda mfupi tu, bahati nzuri alipoifikia na chombo kilichombeba Jegan Grashan kilikuwa kikiwasili, aliona pale kilipoingilia ma yeye akajipenyeza hapohapo.
Wakiwa ndani ya boti wanashangilia ushindi huo, ndipo Kamanda Amata alipomshuhudia Jegan Grashan ambaye alijua wazi kuwa amemuua kule Tazara akiwa hai mbele ya macho ya wengine. Jambo hili lilimtia hasira na uchungu, akabadili mpango wake haraka na kujitokeza mzima mzima. Wakati wao wanapiga shampeini na risasi za hewani kushangilia ushindi, Kamanda Amata alikuwa kazimama mbela yao kama mzuka.
“Jegan Grashan, nani aliyekwambia kuwa utaondoka ndani ya nchi hii ukiwa na pumzi yako? Kama ulijuwa kuwa umepona sasa ndio mwisho wa maisha yako, nafikiri hukutaka kufa peke yako ulikuwa na akili sana na sasa mtakufa wote pamoja kwa mkono wangu huu, wasalimie kuzimu, mwanaharamu, mwanadamu ambaye hukustahili hata kuzaliwa,” Kamanda Amata alishikwa na hasira kali, akisema maneno hayo hakuna aliyeamini kama mbele yao yupo kiumbe huyo anayeogopwa kila kona ya sayari yetu, kabla hawajajiweka sawa wakiwa bado kwenye butwaa, kichwa cha Jegan Grashan kilifumuliwa kwa risasi mbili kutoka katika bastola ya Amata, mara hii alihakikisha anakufa.
Kamanda Amata alijirusha upande wa pili na risasi yab tatu ikamfumua Yule aliyeshika shotgun aliyekuwa akimlenga Kamnda, hola! Alifanikiwa kupiga viti na vyupa vya pombe wakati Kamanda akijiviringa kuelekea upande mwingine. Ilikuwa ni hali ya taharuki kwa freedom fighters.
“Muueni shetani mweusi!” Shakrum alipiga kelele huku akitafuta pa kujificha. Tayari watu watatu walikuwa chini bila uhai.
“Jegannnnnn!!!!!!” Ilikuwa sauti ya Shailan aliyekuwa akilia kwa uchungu aliposhuhudia mwana mapinduzi wao akifumuka kichwa. Dakika moja baadae wote walikuwa chali sakafuni, Shakrum alibaki hai kwa kuwa aliwahi kujificha. Kamanda Amata akatazamana na Shailan.
Jicho la hasira la Kamanda Amata lilikuwa likimwangalia Shailan aliyekuwa amemshika Jegan mfu akilia kwa uchungu.
“Kama kuna aliyewaambia kuwa mtaondoka nchi hii mkiwa hai amewadanganya kabisa, hamkustahili kuishi wala kuzaliwa,” Kamanda Amata aliongea hayo na kufyatua risasi moja iliyopiga kifua cha Shailan na kumtupa nyuma. Alipotaka kufyatua risasi ya pili akajikuta ameishiwa risasi. Mara akajikuta akidakwa kwa nyuma, kabla hajakaa sawa, alikabwa shingo. Amata akafikiri la kufanya kwa haraka, akainama na kumyanyua huyo mtu na kumbwaga mbele, Shakrum. Hasira za Amata zikawaka maradufu, Shakrum akanyanyuka na kumkabili Kamanda Amata.
“Nilikuwa nakutamani sana wewe kiumbe! Na sasa umeingia mkononi mwangu, sitakupa hata nukta ya kuomba sala ya mwisho,” Shakrum alimwambia Kamanda Amata, alipomaliza sentensi yake alimvamia Kamanda kwa jinsi ya ajabu, akampiga ngwara moja maridadi, Kamanda alijirusha hewani akaichanua miguu yake na kuipata shingo ya Shakrum, alimpiga teke kwa mguu wake wa kulia nyuma ya shingo, Shakrum aliyumba na kujipigiza ukutani. Akaruka sarakasi na kusimama wima, akaweka mikono katika mtindo wa kuvutia wa mapigo ya karate, Kamnda Amata naye akajipanga kivingine. Shakrum alitoa mapigo ya kasi mfululizo kumuelekea Kamnda Amata lakini hakuna hata pigo moja lililomfikia Amata, mapigo yote yalipanguliwa kiufundi sana, mwisho wa yote Kamanda Amata akajirusha sarakasi na kumpa Shakrum nafasi ya mita kama tano kutoka kwake. Kwa sekunde chache alizozipata Amata alijipanga na kupeleka mapigo ya kazi ambayo yote yalimuioshia Shakrum na kumtupa chini akiwa hoi.
“Mi nilifikiri unajua kupigana kumbe ni mwanafunzi namna hiyo!” Amata alimwambia shakrum aliyekuwa akitambaa chini huku yeye akimfuata kwa nyuma.
“Ulipigania Jegan kuachiwa huru, sasa wewe utakaa jela badala yake,” Amata alimwambia Shakrum na kumkamata ukosi wa fulana yake na kumvuta kwa nguvu mpaka kijana huyo akakohoa, akamuinua kwa nguvu na kumbamiza ukutani. Shakrum hakuwa na la kufanya, Kamanda Amata akatoa pingu tayari kumfunga Shakrum lakini lo, bomu aina ya grunet lililoondolewa pini ya usalama likaanguka kutoka mkononi mwa Shakrum na kutua chini liokadunda mara ya kwanza na likaelekea kugoinga sakafu mara ya pili.
Shakrum alimshika kamanda kwa nguvu zake zote.
“Hatoki mtu hapa, kama wewe umeua ndugu zangu, lazima nawe ufe na sisi,” Shakrum alimwambia Amata.
“Kamwe haiwezekani!” Kamanda Amata akajibu na kumpiga kichwa cha nguvu kilichomfanya Shakruma amwachie. Kamanda Amata hakupoteza sekunde, alikimbia kwa kasi yake yote, hakukuwa na mlango ila dirisha kubwa la kioo mbele yake, alichumpa na kutanguliza kichwa akakipiga kioo nay eye mwenyewe kutoka nje kupitia hapo. Nyuma yake ulitokea mlipuko mkubwa, ile boti yote ikateketea kwa moto.
§§§§§
Madam S alijishika kichwa baada ya kuushuhudia mlipuko ule kupitian chomb o maalumu katka kambi ya jeshi la wanamaji Kigamboni.
“Oooh! My son! (Oooh Kijana wangu!)” alipiga kelele.
Moyo ulimwenda mbio hakujua afanye nini. Akikumbuka Chiba kaumizwa na gesi, sasa Kamanda ndani ya mlipuko, Madam S alijikuta anabaki peke yake, machozi ya uzee yalimdondoka huku mikono yake ikifunika kinywa chake kwa uchungu.
Chumba kizima walichokuwa maofisa wa Jeshi pamoja na Madam S wakishuhudia tukio lile kilikuwa kimya, hakuna hata aliyekohoa. Madam S alihisi akishikwa bega. Akageuka na kumtazama aliyemshika, alikuwa waziri wa ulinzi aliyefika muda huo katika kambi hiyo ya wanamaji.
“Pole Madam, lakini vijana wetu wamekufa kishujaa!” alimwambia Madam S.
“Nani aliyekwambia vijana wangu wamekufa?” madam S alijikuta akipiga kelele kupingana na kauli hiyo. Mara kelele zikaibuka katika chumba kile, Madam alipogeuka alimuona Kamanda Amata akiogelea majini baada ya kuibuka.
“Mpe msaada haraka!” illikuwa ni sauti ya waziri wa ulinzi, na mara hiyo hiyo boti iendayo kazi ikaanza safari yake na kumfuata Kamanda Amata.
Madam S alijikuta akifurahi kwa tukio hilo, hakuamini kab isa anachokiona mbela yake.
“Mungu mkubwa!” alishukuru.
MADAM S aliinua simu yake baada ya kushusha pumzi ndefu, katika sakata hilo ni yeye tu aliyekuwa upande wa peke yake tangu mwanzoni baada ya kusikiliza kile ambacho Kamanda Amata alimwambia tangu mwanzo kuwa hakubaliani na kuachiwa huru Jegan. Ijapokuwa Madam S aliwasikiliza wajumbe wengine katika jopo lile la baraza la usalama la taifa chini ya waziri wa ulinzi, aligeuka baadae kwa kuungana na kijana wake, TSA 1 lakini swala moja walikuwa wakitofautiana. Kamanda Amata aliapa wazi kuwa laiti Jegan akiachiwa huru yeye atamrudisha kwa risasi, uamuzi huu ungekuwa kinyume na maadili ya kazi kama kungetolewa hati ya jambo hilo. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Kamanda Amata alimpiga risasi Jegan Grashan katika msafara wa gari za ubalozi. Ijapokuwa Jegan alikuwa amevikwa nguo zisizoingia risasi na kusalimika katika tukio hilo. Aligadhibika sana alipomuona Jegan akiwa hai ndani ya boti ile, akipongezana na wenzake na kutoa maneno ya kashfa, Kamanda Amata hakushindwa kutumia bastola ile ile iliyofanya kazi katika tukio la kwanza, na sasa alifumua kichwa kabisa maana labda angekuwa na nguo nyingine isiyopitisha risasi. Alijua alilolifanya.
‘Liwalo na liwe!’ alijisemea moyoni huku akiitazama boti ile iliyokuwa ikiteketea kwa moto, hakuna hata mtu aliyetoka, hakikusalia hata chuma juu ya chuma kingine. Kazi ilikuwa imekwisha namna hiyo. Akajigeuza na kuendelea kuogelea kuelekea pwani ambako palikuwa na umbali kidogo lakini alipoanza kuogelea tu, aliona helkopta kubwa ya jeshi ikija eneo lile, akaipungia mkono na chombo kile kikasogea hadi pale alipo na kumteremshia kamba iliyofuingwa kwa mafundo mafundo, akaikamata na dude lile likaondoka nae kutoka pale kwenda nae nchi kavu.

KIGAMBONI – KAMBI YA JESHI LA WANAMAJI

saa 7:14 mchana
MADAM S alisimama kwenye uwanja wa kushukia helkopta, pembeni yake kulikuwa na waziri wa ulinzi, walikuwa wakimwangalia Kamanda Amata alipokuwa akija upande wao akiwa chapachapa, ametota maji.
Madam S alimkumbatia Kamanda Amata kwa nguvu zote bila kujali kama kalowa maji, alimbusu mashavuni.
“Kazi nzuri kijana wangu, nimefurahi sana kwa ulilofanya, nina uhakika hakuna aliyetoka mle ndani,” Madam S alimwambia Amata.
“Hakuna anyeweza kutoka kwenye mikono ya Kamanda aamuapo jambo, si Jegan, si Shailan wala Shakrum, wote leo nyama zao zinaliwa na watoto wa samaki, lazima ulimwengu ujue kuwa kuna wana usalama makini katika kazi, Mungu ibariki Tanzania, nahitaji kumuona kaka yangu Chiba,” Kamanda alimwambia Madam S, akamtazama waziri wa ulinzi kisha akapita b ila kumsalimia na kuingia kwenye gari ya usalama, akaketi katika siti ya nyuma na Madam akaingia siti ya mbele nyuma ya usukani wakaiacha kambi hiyo na kuelekea mjini.
MUHIMBILI saa 7:54
CHIBA alitolewa kwenye chumba cha daktari na kupelekwa sehemu maalumu ambayo ni yeye peke yake alikuwa amehifadhiwa humo, chumba maalum chenye mitambo tiba ya kila aina ambayo ina uwezo wa kukushikia roho yako wakati wewe ukifanya mambo mengine. Alilazwa kitandani na kuwekewa hewa ya oksijeni ili imsaidie kupumua huku mitambo mbalimbali ikishirikiana kuonesha mwenendo mzima wa maisha ya mtaalamu huyo. Ijapokuwa ni yeye alikuwa mtaalamu wa kompyuta lakini mara hii kompyuta zilikuwa zikimuongoza yeye. Hakuweza kufungua macho ndani ya ubongo wake alikuwa akipitiwa na mapito mengi mabaya nay a kutisha, aliota Kamanda Amata anakufa kifo cha moto, na mara akaota Kamanda Amata anafukuzwa kazi. Ndoto mbaya zaidi ilikuja baada ya muda mfupi, alipoota wapelelezi wawili maarufu sana wa Tanzania wakiuawa vibaya katika sehemu moja ya Afrika wakiwa wanataimiza majukumu yao ya kiserikali. Mara vile vyombo vikaanza kupiga kelele na kuonesha kuwa mapigo yake ya moyo yanashuka kwa kasi. Muuguzi aliyekuwa hapo akamwita dakatari haraka. Dr Jasmin, alikuwa akitokwa na jasho akijaribu kuokoa maisha ya Chiba, Chiba alikuwa akipigania maisha yake ya mwisho, ulikuwa mpambano mkali na shetani. Katia maono yake alikuwa akipambana na joka kubwa lenye vichwa saba, haukuwa mpambano wa kitoto, lakini Chiba alijitahidi kutumia nguvu na ujuzi wake wote ili kulishinda joka hilo, lakini haikuwa hivyo. Joka lilimdhibiti Chiba likamkaba mwilia wake na kumnyonga.
Mitambo tiba iliyokuwa ikipima mwenendo wa moyo wa Chiba ilionesha mstari ulionyooka kuashiria kuwa Chiba hana uhai tena. Dr Jasmine alishindwa kuvumilia hali hiyo alijikuta akilia kama mtoto. Nukta hiyohiyo Madam S na Kamanda Amata waliingia ndani ya wodi hiyo wakiwa haihai walipofika pale walikuta vurugu ya madaktari wakisaidiana na wauguzi, wakati huo Gina alikuwa hana hali kwa kilioo cha vikwifuvikwifu.
“Nini Gina?” Kamanda aliuliza.
“Man down Kamanda,” Gina alimwambia huku akilia. Kamanda Amata alielewa haraka maana ya neno hilo likimaanisha Chiba amekufa, Kamanda Amata hakusubiri linguine, haraka alikimbilia walipo madaktari ambapo tayari Madam S alikuwa amekumbatiana na Dr Jasmine wakilia kwa uchungu.
“Noooooooooo!!!!!!!” kamnda Amata alipiga kelele na kuwatawanya madaktari waliokuwa pale, wengine wakaanguka na wengine wakayumba na kusimama wima. Kamanda Amata alimtazama Chiba ambaye alikuwa ametulia kimya macho yake yakiwa meupe, mboni zake hazikuonekana, “No my brother, don’t leave me!!!!!!” (Hapana ndugu yangu, usiniache peke yangu,) Kamanda Amata kama kawaida yake huwa hakubali kushindwa jambo, wakati madaktari wakimshika amuache Chiba hakukubaliana nao, alitazama huku na huku, akaona waya wa umeme wa 6.0mm uliokuwa ukipitisha umeme kuelekea kwenye mitambo ya oksijen, Kamanda kutoka aliposimama alikanyaga kimeza cha dawa za mgonnjwa na kuukamata ule waya akaning’inia nao mpaka ule waya ukachomoka katika joint box, akashika jirani na miisho yake ambayo ilikuwa ni nyaya mbili, nyekundu na nyeusi, bila huruma wala kuchelewa akampiga shoti Chiba akiwa kitandani, akarudia mara ya pili.
Jambo lisiloaminika likajitokeza, mashine iliyokuwa ikipima mapigo ya moyo ikaanza kusoma mapigo ya juu sana na baada ya sekunde kumi ikatulia na kuonesha mapigo yaliyo sawa. Chiba akafumbua macho, akamtazama Kamanda, Madam S, Madaktari na wauguzi waliopo katika wodi ile. Chiba akaondoa mwenyewe kwa mikono yake ile barakoa ya oksijeni, akainuka na kuketi kitandani.
“Kamanda Amata, umepona?” akauliza Chiba.
“Nimepona kaka,” Kamanda akajibu.
“Jegan najua amekufa na wenzake je?” Chiba akauliza tena.
“Wote wamekufa, hakuna aliyesalia,” Kamanda akajibu, Chiba akampa ishara Kamanda Amata ya kuwa asogee jirani, akamkumbatia kwa nguvu. Kamanda akautupa ule waya chini, na wakati huo fundi umeme alikuwa keshafika baada ya kuitwa haraka.
“Asante Kamanda Amata,” Chiba akashukuru.
“Asante na wewe kwa kuokoa maisha ya Watanzania wengi,” Kamanda akamshukuru Chiba. Wale madaktari wakamchomoa vifaa vyote vilivyokuwa mwilini mwake. Chiba akatoka kitandani na kuongozana na Madam S, Kamanda Amata, Gina na Dr Jasmine wakatoka na kuingia kwenye gari kisha wakaliacha eneo la Muhimbili na kutokomea zao.
§§§§§

BAADA YA SIKU MBILI
OFISI NYETI

KAMANDA Amata akiwa amesimama mbele ya meza kubwa, safi ambayo unaweza kujiona mwenyewe, alikuwa akitazamana na Madam S ambaye naye alikuwa amesimama wima, wote wakiwa katika vazi la kufanana, suti nyeusi, shati jeupe na tai ndefu nyeusi kasoro Madam S. Chiba alikuwa pembeni na watui wengine wawili akiwamo Dr Jasmine.
“Tukisimama hivi unaelkewa kabisa kuwa tunahitaji nkuongea kiofisi zaidi,” Madam S alimwambia Kamanda Amata ambaye alikuwa kimya bila kujibu lolote, akatoa kitambaa chake cheupe na kufuta machozi yaliyokuwa yanayajaza macho yake angavu, kisha akaendelea, “Baada ya kikao cha jopo lilelile lililokuwa likikaa tangu mwanzo wa sakata hili mpaka jana limekaa tena. Na agenda kubwa ilikuwa ni juu yako Kamanda wangu, kwanza unapongezwa sana kwa kazi nzuri uliyoifanya kwa kushirikiana na wenzako wote, mmeudhihirishia ulimwengu kuwa usalama wan chi hii upo mikononi mwetu wenyewe, lakini pamoja na pongezi hizo Kamanda, kuna habari mbaya nay a kusikitisha juu yako na juu ya ofisi yetu pia,” akakohoa kidogo na kuendelea tena, “Siku zote kwenye kitambaa cheupe kinachoonekana ni doa jeusi tu, watu hawaangalii wema ila mabaya yako na kukupatiliza kwayo, ndani ya kazi yako nzuri ambayo sisi kama wanausalama tumeiweka kwene kablasha linalojulikana kama JULAI 7, Kamanda umeonekana kufanya kazi kijeuri bila utii kwa maamuzi yako mwenyewe na kupinga maagizo ya jopo la usalama na kwa sababu hiyo baraza la usalama limekupa barua ya kusimamisha kazi katika kitengo cha ujasusi cha TSA, utakivua cheo chako cha TSA1 na kukabidhiwa mtu mwingine kuanzia nimalizapo kusema haya, haijatolewa kama ombi bali ni amri na itekelezwe mara moja, imesainiwa na waziri wa Ulinzi kwa niaba ya baraza zima la usalama wa taifa.” Madam S alimaliza na kufuta machozi.
Kamanda Amata alitulia kama dakika moja, kimya kilitawala, hakuna aliyeongea isipokuwa kufuta machozi na makamasi yaliyokuwa yakiwatoka waliopo kwa uchungu. Aliyekuwa ngangari ni katibu wa wizara ya ulinzi tu, akasogea na bahasha ya khaki, akatoa karatasi tatu nyeupe zilizochapwa kwa mashine ya kisasa, upande mmoja ilisainiwa na waziri wa ulinzi na upande wa pili zilibaki saini mbili moja ya Kamanda na nyingine ya Madam S kama mkuu wa kitengi maalumu, kitengo cha kijasusi kisicho na mipaka. Akaipokea ile barua na kusaini kisha akampa Madam S nae akazisaini kisha, wakagawana moja kwa ofisi ya baraza la usalama wa Taifa, nyingine kwa ofisi ya TSS nay a mwisho akapewa Kamanda Amata, naye akamkabidhi Gina.
Baada ya hapo, Kamanda Amata akavua beji maalumu ya usalama wa taifa na kumkabidhi Madam S, beji ya dhahabu, kimkoba kidogo cha bastola ambacho ndani yake kilikuwa na vifaa kadhaa vya kijasusi ambavyo alikabidhiwa pindi alipopewa kazi hiyo maalumu. Mwisho akapeana mikono na wote waliopo ndani ya ofisi hiyo nyeti.
Ilikuwa ngumu kuzuia machozi ya kila mmoja lakini hali halisi ilikuwa hiyo.
“Nakuhitaji nyumbani Kamanda ndani ya masaa matatu, wewe na wenzi wako kwa chakula,” Madam S alimpa ujumbe Amata.

NYUMBANI KWA MADAM S

“Sikuweza kukutetea tana Kamanda, ijapokuwa wapo nwaliojaribu lakini wengine walikazia ufukuzwe kazi” Madam S alimwambia Kamanda Amata walipokuwa wameketi katika bustani kubwa ya nyumba hiyo, Gina, Chiba na Dr Jasmine walikuwa ndani wakiendele kupata vinywaji.
“Usijali Madam, yote maisha, mimi nimetoka TSS atakuja mwingine naye kutimiza wajibu wake,” Kamanda alimwambia Madam S.
“Najua, lakini kwa sasa kumpata mtu shupavu, mwelevu, mwepesi, mwenye mbinu na ujuzi wa mipango ya kumsaka adui au kummaliza, mbabe kama wewe itachukua miaka mingi sana, usijali Kamanda naamini kuwa muda mfupi tu mataifa makubwa yatakuchukua, mi nakutakia maisha mema sana Kamanda, kwa lolote tuwasiliane mimi ni mama yako na wewe ni mwanangu,” Madam S akamaliza, wakakumbatiana kwa nguvu kila mmoja akimwaga machozi ya uchungu kisha wakaachana na kurudi ndani.
§§§§§
Gina na Kamanda Amata waliondoka kwa Madam S na kupitia vijiwe kadhaa kabla hawajafika nyumbani.
“Nikupeleke kwako au?” Kamanda akauliza.
“Sitaki, leo nataka kulala kwako,” Gina akamwambia Kamanda Amata kisha wakaendelea na safari mpaka nyumbani kwa Kamanda Amata. Walikuwa wamelewa, Gina alifika na kuingia chumbani akifuatiwa na Kamanda. “Kamanda Amata, uliyekuwa TSA1 wenye roho mbaya wamekufukuza kazi, usijali mimi leo nataka nikupe kazi njione kama kweli we mwanaume,” Gina aliongea kwa sauti ya kilevilevi.
“Gina ulale sasa,” Kamanda alisititiza na kutoka kwenda sebuleni. Gina akachukua nafasi hiyo kwenda maliwato, akaoga na kurudi kisha akaingia ndani ya kitanda kikubwa na kujifunika kwa shuka safi yenye maua ya kuvutia, akazima taa kali na kuwasha ile ya buluu.
Dakika chache baadae Amata aliingia chumbani, naye vivyo hivyo, akaenda kuoga na kurudi, Gina kwa hila zake akajifunua shuka na kulitupa pembeni akabaki kama alivyozaliwa.
“Njoo Kamanda, najua una mambo mengi leo, njoo nikufariji,” Gina alimwambia Kamnda huku akiwa anjipindapinda pale kitandani.
Kamanda Amata akamtazama mrembo huyu ambaye siku zote walikuwa wakiheshimiana sana lakini leo hii heshima ilikuwa inataka kubadili uelekeo.
Gina alikuwa akimtazama Kamanda, Kamanda alikuwa akimtazama Gina aliyekuwa kajilaza pale kitandani, mwanga wa taa buluu ulifanya umbo la Gina lionekane kama madini ya Tanzanite, lilimvtia Kamanda, akapatwa na wakati mgumu, kabla hajaamua la kufanya. Gina aliinuka na kumtoa taulo Kamanda kisha akaizungusha mikono yake na kuiokutanisha nyuma ya shingo ya Kamanda Amata.
“Nakupenda sana Kamanda Amata”.

MWISHO

Sent using Jamii Forums mobile app

Safi sana...

Chapter Closed...


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom