Mwekezaji 'kusaidia kujenga Mahakama ya Rufaa' siyo sawa!

Wale Wanyama walipewa Wawekezaji. Nasikia Mzee ruksa alipeleka Tausi sijui wapi kwa wawezekaji wengine.Kuna haja hata Bunge tuwape Wawekezaji maana limezidisha maigizo (Mbowe kasema).
Khe khe khe kheeee hivi jamani on a serious note, wale wanyama pale magogoni bado wapo?
 
Atatujengea historia? Hilo jengo si Mahakama tu bali ni sehemu muhimu ya historia na urithi wetu. Lakini kwa vile inaelekea tumekubali kuwa sisi hatuna historia basi apewe na Mahakama Kuu, Wizara ya Mambo ya Nje, jengo la Magereza, Mahakama ya Biashara na kadhalika ili watujengee majengo ya kisasa ili hao tunaowaabudu watambue kuwa nasi ni watu kama wao. Wakati huo tukienda kwao, wakituonyesha majengo yao yenye miaka 600 na kuendelee tuwabeze kwa kuwaambia kuwa kwetu kila kitu ni kipya na kimepanda juu, isipokuwa maji hatuna, umeme hatuna, usafiri shida, njia za maji chafu hatuna na tulipokuwa nazo tunamwaga kinyesi kibichi baharini, zima moto za kimachinga n.k! Aibu tupu. Amandla.......
.....Ngawetu!
WoS, kuna wakati nyumba niliyokuwa nimepanga ilikuwa na mfereji mchafu ukumbini. Nikamwambia baba mwenye nyumba aniruhusu niujenge ili harufu isiingie ndani. Alihamaki na kukataa kata kata! alichonijibu ni kuwa nimpe kodi ya miezi 3 zaidi ya mkataba wangu mpya atumie kujenga. Nikafanya hivyo naye akatimiza wajibu. Naona huyu baba anafikiri zaidi kuliko serikali yetu.

F.mchundo umenitekenya! kuna hili suala tusilolijua kuwa majengo ya zamani ni sehemu ya mipango miji na historia ya nchi. Popote duniani majengo hayo yapo na yanaheshimiwa. Kaangalie Olympic stadium Greece, Italy na Roma(colisium?) n.k. Kwa wenzetu kuna miji ya kale na historia na miji mipya. Manchester sio London kwa muonekano.Mwaka jana London walivunja jumba leney miaka 180 kwasababu halifai kurepea kwa hali yoyote na kubaki kama lilivyo. Ilikuwa ni issue hata hivyo.

Lilipotaka kubomolewa jengo la posta ya zamani lenye majina ya waingereza ubalozi uliingilia kati na tunakumbuka Yule mwingereza aliyerudi kuangalia ukarabati kwa vile alifanya kazi hapo wakati wa mkoloni. Ni lazima tuwe na Old Dar itakayokuwa na mandhari yake na new Dar.

Hili la mahakama ya rufaa, nabaki kujiuliza mbona mjengo wa Dodoma haukujengwa na mwekezaji?
Kwanini kuna mabilioni yanatengwa kila mwaka kurepea Ikulu na si mahakama?
Kama Jairo peke yake aliweza kuchangisha taasisi kwa ajili ya bajeti, kwanini serikali yenye taasisi zaidi ya 100 ishindwe kuchangisha pesa za jengo la mahakama ya rufaa!

Kwanini tusipitishe bakuli kwa wananchi na akina voda, tigo, barric,Utalii, n.k wachangie kama wanavochangia michezo.
Kwanini akina NSSF waliojenga mafuta house na sasa kigamboni bridge wasifikirie kuwa wawekezaji hadi tumtafute 'W.Buffet' kutusaidia.

Huyu mwekezaji kwanini apende mahakama zaidi na si hospitali ya Temeke wazazi wanakozalia sakafuni kama anataka kutupa zawadi?
Ni wapi duniani majengo ya mhimili mkuu wa dola yamejengwa na mwekezaji.
 
Hii Forodhani Hotel wakati wa Ukoloni ilikuwa inaitwa Dar Es Salaam Club. Ilikuwa ni bar ya wazungu wanaume wenye status. Mwafrika au mwanamke alikuwa haruhusiwi kugusa ndani. Hata ma waiter walikuwa ni Wahindi, hasa ma Singasinga.

Leo hii tumeifanya hii bar kuwa Mahakama ya Rufaa.

Najaribu kufikiri jinsi wazungu wanavyotuchukulia wanapoona kuwa baada ya miaka 50, hatujajenga jengo la Mahakama ya Rufaa (hata jengo la Mahakama Kuu wamejenga Waingereza), na badala yake tunatumia bar yao ku-dispense justice.
 
Mahakama kama mhimili wa uongozi wa TZ si kuidhalilisha kujengewa jengo na mwekezaji?Kwani ni sahihi mwekezaji kwa mfano kuijengea serikali jengo la Wizara, au jengo la Mkuu wa Wilaya au Mkoa?
 
Ni aibu sana halafu kama wanataka kujenga kwa nini wasijenge kwanza ili watakapotaka kubomoa mahakama ya rufaa iwe kwenye ofisi yake huu unaweza kuwa ni utapeli tu!
 
Ndo taabu ya kuwa na viongozi ambao to the them even common sense is not common!
Ivi uyo atakayejenga si lazima atakuwa juu ya sheria?
 
Mimi ni wasiwasi na uwezo wa Waziri wetu wa sheria.Hivi kweli Serikali haina fedha za kujengea Jengo Zuri la mahakama hadi ijengwe na mwekezaji.Jamani hizi njaa za 10% zitaiangamiza nchi yetu, tunabadilisha historia ya nchi kupitia majengo ya zamani kwa kuwa tu ikiuzwa 10% ipo oneni aibu jamani.JK angalia tutakukumbuka kwa aibu hii utakapong'atuka madarakani.
 
Hii Forodhani Hotel wakati wa Ukoloni ilikuwa inaitwa Dar Es Salaam Club. Ilikuwa ni bar ya wazungu wanaume wenye status. Mwafrika au mwanamke alikuwa haruhusiwi kugusa ndani. Hata ma waiter walikuwa ni Wahindi, hasa ma Singasinga.

Leo hii tumeifanya hii bar kuwa Mahakama ya Rufaa.

Najaribu kufikiri jinsi wazungu wanavyotuchukulia wanapoona kuwa baada ya miaka 50, hatujajenga jengo la Mahakama ya Rufaa (hata jengo la Mahakama Kuu wamejenga Waingereza), na badala yake tunatumia bar yao ku-dispense justice.

hapo kwenye red mkuu, hiyo inaweza ikawa ni moja ya historia nzuri sana kuliko kumpa muwekezaji abomoe na kuweka maegesho pale, jengo la kihistoria libaki hivyo.
 
Mwana JF. Masemaje kuhusu mpango wa Serikali ya JK kutaka kuuza jengo la Mahakamu kuu ili kupisha ati wamiliki wa hotel ya kempusk kutengeneza maegesho ya magari ya wateja wao. Mimi haiingiii akilini. Sijui labda wana kiwanja Mbagala kizuiani cha kujenga Mahakama kuu.
 
hata kama wangekuwa na kiwanja mbagala ama kwingineko, but serikali kumuuzia mtu binafsi jengo la mahakama kuu?katika namna yoyote ile hilo jengo hata kama halifai si libaki kwa ajili ya maonesho?viongozi hawa cjui wanatumia ma.ta.ko kufikiri......?
 
Mwana JF. Masemaje kuhusu mpango wa Serikali ya JK kutaka kuuza jengo la Mahakamu kuu ili kupisha ati wamiliki wa hotel ya kempusk kutengeneza maegesho ya magari ya wateja wao. Mimi haiingiii akilini. Sijui labda wana kiwanja Mbagala kizuiani cha kujenga Mahakama kuu.

Wavunje tu hilo jengo halina faida kwa sasa, magofu katikati ya mji ni uchafu na kwa sisi tusiopenda historia ya ukolini majengo hayo yanatukumbusha mateso ya ukoloni vunja haraka.
 
Wavunje tu hilo jengo halina faida kwa sasa, magofu katikati ya mji ni uchafu na kwa sisi tusiopenda historia ya ukolini majengo hayo yanatukumbusha mateso ya ukoloni vunja haraka.

Acha kuwaza kwa MASABURI WEWEEEEEEEE.... &%$@*?"'~%$ZAKOOOOOOO
 
Kaanze kwanza kuwauwa Baba na Mama yako, uje na Mababu/Mabibi maana hawana faida kwa taifa hili na wanamaliza tu dawa zetu vijana huko hospital zetu. Kama na wewe ni Mzee, basi chukua kamba ujitundike.
Wavunje tu hilo jengo halina faida kwa sasa, magofu katikati ya mji ni uchafu na kwa sisi tusiopenda historia ya ukolini majengo hayo yanatukumbusha mateso ya ukoloni vunja haraka.
 
ni uzandiki kuuza lile jengo ni bora pale ihamie mahakama ya jiji, na serikali ijenge mahaka mpya ya rufaa palipo kiwanja chao karibia na agha khan hospital, siafiki eti kwa vile anapewa mwekezaji kwann wasimpe ikulu akajenga pale afu yeye akajenga ikulu mpya?? hivi na lile jengo jipya alilozindua waziri mkuu mwaka huu mwanzoni kama sio mwaka jana lenye kumbukumbu ya jaji fulani nalo hawakuona hilo wkt wanalijenga na kuhamishia ofisi zote za uhasibu na baadhi ya wasajili wanakaa kule nao pia wanauzwa humo humo ndani???? dis contry iz not serious kwa kweli. wacha tuone kama jaji mkuu na jk atakubali huu uozo basi tutapanda hadi juu ya kilele cha milim ayote tanzania kudai nchi yetu mpya.
 
Back
Top Bottom