Mwekezaji 'kusaidia kujenga Mahakama ya Rufaa' siyo sawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwekezaji 'kusaidia kujenga Mahakama ya Rufaa' siyo sawa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Aug 25, 2011.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Namsikiliza Mh Waziri wa Sheria na Katiba akijenga hoja kuwa kuna mwekezaji anajitolea kujenga mahakama ya rufaa kama atapewa hilo jengo la Mahakama ya Rufaa - iliyokuwa Forodhani Hotel.

  Mimi naona hata kama ndivyo haitakuwa sawa kwa mwekezaji kutujengea MAHAKAMA YA RUFAA - THE HIGHEST COURT IN THE COUNTRY.

  Ni bora Serikali isihusishe ujenzi huo na mwekezaji hata kama ndio PPP...NASEMA HAPANA!
   
 2. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  JAMAA anataka kuweka maegesho ya wageni wake kwani maegesho yake yamefikia Pomoni!Siku jamaa akihukumiwa na hiyo mahakama sijui itakuwaje!sheria inaweza pindishwa kwa ajili yake au akadai kuwa yeye ndio mmiliki wa jengo hilo!
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Kikwete ni ya kibahatishaji, ni juzi tuu wametoka kuikarabati hiyo mahakama kwa bilion plus, hivi hawana mipango ya mda mrefu hawa watu?? kwasababu wangekuwa wanajua itabomolewa wasingeikarabati kwa hizo pesa, maana zingetumika kufanya mambo mengine ya msingi. Kweli bongo kichwa cha mwenda wazimu
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Na ndio mantiki ya hoja yangu. Kutujengea kutaathiri uhuru wa mahakama na integrity yetu.Ingekuwa kujenga jengo lingine sawa lakini siyo MAHAKAMA hata ingekuwa ile ya Mwanzo kijijini.
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hivi nini kimekula macho na ubongo wa serikali yetu kiasi kwamba hawaoni mbali wala hawana tena ule uwezo wa Nyerere wa ku- analyse mambo kisomi. Hata madhara ya hili wanataka wapewe ushauri wakati hii ni wazi kabisa kwamba ni "MGOGORO WA KIMASLAHI" Uvivu wa kufikiri, kupenda rahis na papara kutaipeleka serikali ya Tanzania pabaya
   
 6. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #6
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Kama kweli serikali ni sikivu basi watasikia kilio chako...
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wasikie wasisikie... haihitaj kuvaa miwani kuona kuwa kitendo hicho kitapelekea "KUUZA UHURU WA MAHAKAMA".

  Hata mtu binafsi huwa anatafakari sana kabla ya kujiingiza kwenye mambo kama haya.Lazima kupima pros and cons ya kila kitu.
  Kujadili hapa kutasaidia kama hawakuliangalia hilo wajue kuwa wananchi tunajiuliza maswali...
   
 8. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  hii nchi tutaendelea kuona na kusikia mengi............
   
 9. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Baba askofu Sikio la kufa ....
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Serikali ina amini kwa dhati, "bila wawekezaji nchi haiwezi kuendelea" Unategemea nini? Serikali imeshindwa kabisa kupambana na malaria!!! Kazi kushinda kutwa kucha na mabakuli nje kuomba!! JK huwa ananiudhi sana akiwa nje. Utamuona kapendeeeeza, nice suit, tie shoes etc. Kila anachosema, manemo matatu tu, malaria, inafuatiwa na kuomba msaada!!!

  Uvivu wa kufikiri umetawala in the GOV!!!
   
 11. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Serikali ya chukua chako mapema. Rushwa imekuwa kama grisi kwa uendeshaji wa serikali. Too dangerous
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  just a political talk
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nasubiri wawekezaji waje waanze kutununulia hadi Chupi. Ikibidi wawezeke hadi kwenye vitanda vyetu kwani wake zetu soon watagundua tumeshindwa kazi. Sisi ni Ufisadi, Kula, Kunywa na Nyumba Ndogo (mwisho kulala kwa mama kubwa huku umechoka hoooi).
   
 14. k

  kibunda JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana jf,

  kama serikali inawaza na imekubali kuifanyia biashara mahakama ya rufaa, mimi binafsi nawaza, hivi mwekezaji akifika bei ya kuihamisha ikulu au hata bunge, pale awekeze hata choo cha kulipia, si atapewa? Kwa kweli tumefikia pabaya. Serikali inawezaje kubinafsisha mamlaka ya nchi? Tujadili
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama Taifa huru (a soveregn nation) tuna mihimili mitatu ya dola na Mahakama ni mmoja wa hiyo mihimili mitatu.
  Wakati tunasheherekea miaka 50 ya uhuru ni aibu na fedheha kubwa kujengewa jengo la mhimili wa dola. Mahakam kuu ndio chombo cha juu kabisa kinachosimamia utoaji wa haki kwa raia wa nchi huru hii ya Tanzania.

  Naomba viongozi watuondelee hii aibu ya KI-HISTORIA maana vizazi vya nchi hii vitatalumu wote tuliosimamia hii aibu. Ni afadhali mara elfu serikali ingeomba wananchi wooote wachange ili kujenga hili jengo kuliko huu 'uwekezaji. Na hakika wananchi pamoja na umasikini watu tungechanga ili kulinda heshma ya hii nchi leo na kesho na siku zijazo, na wana wa nchii wajue hivyo. Sidhani kama tutaweza kujidhalilisha kiasi hiki. Hii omba omba au hii tafsiri ya uwekezaji inaweza kupita hii scandal! Mahakama kuu kujengwa na mwekezaji? hapana. Ni aibu yetu sote.
   
 16. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kwani serikali yetu tukufu haina hela za kujenga jengo la mahakama ya rufaa?

  Kuna muwekezaji mwingine yuko tayari kurekebisha reli ya kati Dar to Kigoma kama akipewa jengo hilo na mwekezaji mwigine yu radhi kujenga hospitali ya rufaa Tabora kama atapewa jengo hilohilo, nani kawashindanisha hawa wawekezaji kuona kuwa huyo wa mahakama ndio anafaa kuliko hao wengine wawili?

  At the bottom line tunaweza kujenga wenyewe kwa hela yetu.
   
 17. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  nchi hii ya kifalme kila kitu kinawezekana
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Rasirimali tunazo, tunashindwa nini kutwa kucha kuomba tuu, maneno haya lazima utayasikia tuu, kwa hisani ya................, mwekezaji, mfadhili

  Uhuru uko wapi wakati kila kitu tunategemea?????
   
 19. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ngali, ikishindikana basi, wapitishe bakuli nchi nzima, tutapata angalau za kuanzia. Bakuli lipite kuanzia watu wa kawaida, wafanyakazi, etc. Kama kuna wizara iliweza kukusanya more than 500millions in just a couple of weeks kwa ajili tu ya ku-facilitate upitaji wa bajeti whay not hili?

  Dhana ya kujitegemea imekufa vichwani mwa viongozi wetu, wamelewa madaraka, wanafikiria vya rahisi rahisi tu. Kwa mtindo huu, hawana tofauti na mateja, wananadi dala dala kwa ujira mdogo kumaliza matatizo yaliyo mbele ya mboni zao.....

  my foot this gov.....
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Aug 25, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Yaani mwekezaji hadi kwenye mahakama? It's ludicrous to even entertain such a thought. But that's just me.
   
Loading...