Kesi ya mkataba wa bandari Mbeya: Wakili aeleza sababu za kuchelewa kukata rufaa. Mahakama haijawapa mwenendo wa kesi na nyaraka zingine...

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,344

==============================================
Kwa ufupi (quotes)

"Immediate baada ya hukumu tarehe 10/8/2023, mara moja tulianza mchakato wa kukata rufaa kwa kuiandikia mahakama barua ya kuomba nyaraka muhimu za kesi kwa ajili ya rufaa ikiwemo proceedings (mwenendo) wa kesi na viambata vyake", Wakili.

"...Mpaka sasa hatujajibiwa barua yetu hiyo na hatujapewa hizo nyaraka ikiwemo mwenendo mzima wa shauri hili"...Wakili

"...Hatuwezi kusema mahakama imechelewa au imewahi Kwa sababu siku zote, michakato ya kisheria na kimahakama inahitaji umakini"... Wakili

"Jambo la kufurahisha kidogo ni kwamba, serikali imeandoa mswaada wa marekebisho ya sheria No. 5 na 6 ilizopeleka bungeni wakati shauri likiendelea mahakamani. Moja ya hoja yetu mahakamani ilikuwa ni mkataba huu kukiuka sheria hizi kuhusu ulinzi wa rasrimali asili za nchi na mahakama kukubaliana na hoja yetu ktk hukumu yake".. Wakili

"...Jambo muhimu ni kuwa, endeleeni kutuombea kwa Mungu maana tunatishwa na kuwindwa ili tuuwawe na tuumizwe kuliko kawaida na ushahidi wa haya tunao. Lakini niwakumbushe tu, sisi hatutishwi na wajue kuwa kila mwanadamu ambaye pua yake imetazama chini, basi ajue tu kuwa na yeye siku moja atakwenda huko chini (atakufa) tu".. Wakili.
===================================================
Mwisho wa nukuu za wakili..

Lord denning na FaizaFoxy na THE BIG SHOW kwanini mnawatisha hawa mawakili? Mnataka ushindi wa mezani? Kama mko sawa, mnaogopa nini kutetea jambo lenu kwa hoja?
 
Back
Top Bottom