Mahakama zenye mamlaka (jurisdiction) ya kusikiliza kesi za ndoa nchini Tanzania

Apr 26, 2022
64
100
Mahakama za kesi za ndoa.

Habari mpendwa msomaji!

Leo nitatoa elimu ya Mahakama zinazosikiliza kesi za ndoa na unafikaje hapo Mahakamani.

Kwa kusoma makala hii utajua mambo yafuatayo:

-Jinsi ya kufungua shauri au kesi ya ndoa.
-Masharti kabla ya kufungua kesi ya ndoa.
-Ukomo wa muda wa kufungua kesi, na
-Nyaraka (documents).

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa (the Law of Marriage Act [CAP. 29 R.E. 2019], kifungu cha 76, hizi ndizo forums (mahakama) zenye uwezo au mamlaka ya kusikiliza migogoro ya ndoa.

  • Mabaraza ya usuluhishi wa ndoa (Marriage conciliation boards).
  • Mahakama ya mwanzo (Primary court)
  • Mahakama ya Wilaya (District court.
  • Mahakama ya hakimu mkazi (Court of a resident magistrate) na
  • Mahakama Kuu (High court).

Inapokuja suala la ndoa, Mahakama zote (hapo juu) zina mamlaka sawa (concurrent jurisdiction).

Nanukuu kifungu cha 76 cha sheria ya ndoa (the Law of Marriage Act), inasema, “original jurisdiction in matrimonial proceedings shall be vested CONCURRENTLY in the High Court, a court of a resident magistrate, a district court and a primary court.”

Sasa tumeona kuwa kwenye kesi za ndoa Mahakama zote nilizotaja hapo juu zina mamlaka sawa (concurrent jurisdiction).

Swali, je unaweza kuruka mahakama ya mwanzo ukaenda moja kwa moja kufungua kesi ya ndoa Mahakama Kuu? Jibu ni hapana! Lazima uanzie Mahakama ya chini kabisa, alafu ukishindwa kwenye Mahakama moja unakata rufaa kwenye Mahakama ya juu inayofata. Lakini kifungu cha 78 cha Sheria ya Ndoa kinaruhusu kesi kuhamishwa kwenda Mahakama Kuu kama kuna sababu za msingi.

Kwa mkoa wa Dar es Salaam, mashauri yanayohusu masuala ya kifamilia (ndoa na talaka) ndani ya Dar es Salaam, yanasikilizwa kwenye kituo jumuishi cha Mahakama Temeke. (Temeke one Stop Judicial Centre). Hiki ni kituo au Mahakama Maalum wilayani Temeke jijini Dar es salaam inayoshughulikia mashauri yanayohusiana na masuala ya Mirathi, Ndoa na Talaka.

Jinsi ya kufungua shauri au kesi ya ndoa Mahakamani.

-Unaandaa nyaraka (document) inaitwa Petition au chamber summons na kiapo (inategemeana na unaomba nini - mfano talaka, matunzo ya mwanamke au watoto n.k).
-Unaambatanisha na cheti cha ndoa kama kipo.
-Maandishi au barua ya uthibitisho kutoka baraza la usuluhishi (kama ulianzia huko) n.k.

Baadhi ya masharti kabla ya kufungua kesi ya ndoa.

-Kama unataka kuomba talaka au kuvunja ndoa zingatia mambo yafuatayo;

(i) Kwanza hakikisha umemaliza miaka miwili kwenye ndoa, kama ndoa yako haijafikisha miaka miwili hauwezi kuomba kupewa talaka Mahakamani.

Soma kifungu cha 100(1) cha sheria ya ndoa (section 100(1) of the Law of Marriage Act), sheria inasema: “No person shall, without the prior leave of the court, petition for divorce before the expiry of two years from the date of the marriage which it is sought to dissolve.”

Lakini kuna exception (kuna mbadala) kwenye kifungu hicho hicho, ambapo unaweza kuruhusiwa kuomba talaka ndani ya miaka miwili au kabla hujafikisha au kabla haujamaliza miaka miwili kwenye ndoa: “Unatakiwa kuomba idhini au ruhusa ya Mahakama kufanya hivyo.”

Kwa mujibu wa sheria, sababu inayoweza kufanya upewe idhini ya kuomba talaka kabla ya kumaliza miaka miwili kwenye ndoa, ni kama unapitia ugumu usio wa kawaida. Nanukuu, kifungu cha 100(2), Sheria ya Ndoa inasema;

“leave shall not be granted to petition for divorce within two years of the marriage except where it is shown that exceptional hardship is being suffered by the person applying for such leave.”

(ii) Pili, kama unataka kuomba talaka au kuvunja ndoa hakikisha umeanzia au umepitia kwenye baraza la usuluhishi wa ndoa linalotambuliwa kisheria, mfano Kanisani au Baraza la sheria la Kata, BAKWATA, n.k. kutegemeana na aina ya ndoa yako.

Ni lazima kupita kwenye baraza, vinginevyo Mahakama haitakua na uwezo wa kusikiliza malalamiko yako: Soma kifungu cha 101 cha sheria ya ndoa (section 101 of the Law of Marriage Act), sheria inasema:

“No person shall petition for divorce unless he or she has first referred the matrimonial dispute or matter to a Board and the Board has certified that it has failed to reconcile the parties.”

Kwa hiyo unatakiwa kuanzia kwenye baraza la usuluhishi, alafu baraza likishindwa kuwasuluhisha, litatoa cheti au maandishi kuthibitisha kwamba limeshindwa hivyo wahusika waende mbele Mahakamani.

Lakini kuna exceptions (mazingira mbadala), ambapo unaweza usipite kwenye baraza kama una sababu zilizotajwa kwenye sheria kifungu hicho hicho cha 101(a) - (f).

Remedies (nafuu) zilizopo kama hujaridhika na maamuzi ya Mahakama.

-Ikiwa unahisi uamuzi wa mahakama hauko sahihi au sio haki, unatakiwa kukata rufaa kwenda Mahakama ya juu inayofatia.

Sheria ya ndoa kifungu cha 80(1), inasema, “any person aggrieved by any decision or order of a Primary Court, or by any decision or order of a District Court, may appeal from that court, respectively, to the district court or the High Court.”

Kama maamuzi yamefanyika na Mahakama Kuu, unakata rufaa Mahakama ya Rufaa.

“any person aggrieved by a decision or order of the High Court in its original jurisdiction may appeal therefrom to the Court of Appeal.”

Muda wa kukata rufaa ni siku 45. Soma sheria ya ndoa kifungu cha 80(2).

NB: Kama unakata rufaa kutoka MAHAKAMA YA MWANZO sio lazima kuambatanisha nakala ya hukumu na tuzo (decree), usije kukaa unasubiri nakala ya hukumu mwisho ukajikuta umechelewa uko nje ya muda. Hautaeleweka kwa sababu hiyo!

Je, ni nyaraka (documents) zipi zinatumika kukatia rufaa?

Na je, utafanyaje ukikuta umechelewa kukata rufaa ya kesi ya ndoa?

Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke - Advocate Candidate
zakariamaseke@gmail.com
(0754575246 WhatsApp).
 
Tatizo la wanasheria mnapenda sana kurefusha Mambo kwa visababu vidogo vidogo visivyokua na msingi!!
 
Huu uzi ni tiba kabisa
Nimepitia haya nimeusoma
Nami nafasi ipo bado

Asante sana mwandishi
Mungu akubariki
 
Back
Top Bottom