Point kubwa sana. Nyerere pamoja na mapungufu yake kuna jinsi aliacha mafundisho fulani ambayo tungekaa pamoja kama taifa yangetusaidia sana.Pumzika kwa amani Mzee Mtei
Mtei ali 'set the bar' katika utumishi wa Umma. Kwamba alimkatalia Nyerere sera za kifedha na kujiuzulu.
Mwl Nyerere alikubaliana naye, wote wakaishi nchi moja bila kutekana, kuviziana au kutungiana kesi za uhaini. Kwamba walikubaliana kutokukubaliana bila visasi chuki au indhara.
Mtei alikataa UCHAWA! wakati watu wanaandamana kupinga sera za IMF kishabiki, mtei aliwapinga hadharani.
Leo hii tunaishi na sera zile zile alizozisimamia Mzee Mtei ingawa zilikataliwa
Mzee Mtei na Bob Makani (RIP) walianzisha CHADEMA Nyerere akiwa hai! hawakupewa kesi za uhaini!! Hawakupokea simu za vitisho au Familia zao kuhujumiwa. Tuliishi Nchi moja ya Tanzania kwa Amani.
Tuliishi kwa AMANI kwasababu wao walitenda HAKI na walitendewa HAKI.
Mazishi ya Mzee Mtei yanapaswa kuchukua sura ya Kitaifa!
JokaKuu Mzee Mwanakijiji
Ndo alianzisha BOTNilikuwa nasikia tu alikuwa Gavana wa Benki Kuu, Mwanzilishi wa Chadema, Mkwe wa Freeman Mbowe, Mfanyibiashara Maarufu, alikuwa Mwenyekiti na Mjumbe wa Bodi mbalimbali za Taasisi za Umma na Binafsi. Akikataa kupewa ubalozi, n.k.
MUNGU akawe mfariji kwa familia katika kipindi hiki kigumu wanachopitia
Aligombea Ubunge Arusha Mjini akashindwa na Makongoro.Pumzika Mzee Mtei.
Pole kwa familia.View attachment 3532143
Kama mpenda vitabu nimefurahia sana kusoma kitabu cha maisha yake "From Goatherd to Governor : The Autobiography of Edwin Mtei".
Kitabu kina historia kubwa sana sio tu ya Mtei, bali pia ya Tanzania.
Inakuwa shida kubwa, unapoingia kwa mlango huu na kuuacha ule wa kawaida!Apumzike kwa amani mwanzilishi wa CHADEMA.
Kichwa halisi nyuma ya sera zilizoungwa mkono na hayati Mwalimu Nyerere.
Siyo rahisi kiasi hicho. 'Structural adjustment' lilikuwa ni tatizo kote duniani!Mtei alikataa ujinga wa sera za ujamaa zilizofilisi nchi huku viongozi wakineemeka na ndiyo sababu ya yeye kupingana na Nyerere na hatimaye kuondoka Serikalini
Du, nilidhani alikuwa mchumi! Kumbe alisoma siasa, historia na jiografia na kuzigeuza uchumi!Wakuu,
Heche kupitia mtandaoni ametangaza kifo cha mwasisi wa chama chao CHADEMA, Mzee Edwin Mtei baada ya familia kuthibitisha huku mipango ya mazishi ikiendelea nyumbani kwake Tengeru, Arusha.
=====
Elimu,"Shahada ya Sanaa (Political Science, History, Geography) - Makerere (1957)"
BoT, Gavana wa kwanza (1966–1974)
Uwaziri, Waziri wa Fedha (1977–1979)
Siasa, Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA (1992)
Tawasifu, From Goatherd to Governor (2009)
1. Safari ya "Kutoka Chini"
Mtei alizaliwa mwaka 1932 huko Marangu, Moshi. Katika tawasifu yake (autobiography) iitwayo "From Goatherd to Governor", anaelezea jinsi alivyokulia katika mazingira duni, akichunga mbuzi baada ya masomo ya "bush school". Alisoma katika shule za Old Moshi na Tabora Boys kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1953.
2. Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu (BoT)
Wengi wanaijua CHADEMA, lakini hawajui kuwa Mtei ndiye alikuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati ilipoanzishwa mwaka 1966. Alisimamia mchakato wa kwanza wa kutoa sarafu ya Tanzania (shilingi) baada ya kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki. Alishikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane (1966–1974).
3. Msuguano na Mwalimu Nyerere
Mtei alikuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya Mwalimu Julius Nyerere. Hata hivyo, alijiuzulu nafasi hiyo mwaka 1979 kutokana na kutofautiana na Nyerere kuhusu sera za kiuchumi, hasa mapendekezo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambayo Nyerere aliyakataa. Kitendo chake cha kujiuzulu kwa hiari kilihesabika kama ujasiri mkubwa wa kimaslahi wakati huo.
4. Nyadhifa za Kimataifa
Kabla ya kuingia kwenye siasa za ushindani, alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na pia alifanya kazi katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kama Mkurugenzi Mtendaji (Executive Director) akiwakilisha kundi la nchi za Kiafrika.
5. Kuasisi CHADEMA
Baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1992, Mtei alikuwa mmoja wa waasisi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alihudumu kama Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho na alitumia rasilimali zake na ushawishi wake kukijenga tangu kikiwa kidogo hadi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.
6. Uhusiano wa Kifamilia na Freeman Mbowe
Jambo ambalo wengi hulitolea macho ni uhusiano wake na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Edwin Mtei ni mkwe wa Freeman Mbowe (Mbowe amemuoa binti wa Mtei, Lillian). Hii mara nyingi imekuwa ikitumiwa na wapinzani wao wa kisiasa, lakini ndani ya chama inaonekana kama muendelezo wa misingi aliyoiweka.
Acha uzwazwa. Kwani, wewe utaishi milele senzi kabisaAcha kuleta siasa kwenye taarifa za msiba
CCM na vyama vingine mpaka sasa ndiyo vinapumulia mashine. CHADEMA ya Lissu na Heche haiwezi kufa kwa sababu inaungwa mkono na wananchi walio wengi wenye itikadi tofauti! Na hii ni baada ya kujipambanua ka chama cha kupigania maslahi ya Tanganyika, nchi ambayo inanyonywa kwa miaka mingi na Zanzibar kwa kisingizio cha muungano.chama kinakwenda kufa kifo cha mende kama TLP
Sina siasa za kitoto nauheshimu mchango wa Mzee Mtei, yeye Bob Makani na Victor Kimesela walianzisha CHADEMA mwaka ule wa 1992, wote wametangulia mbele ya haki.Inakuwa shida kubwa, unapoingia kwa mlango huu na kuuacha ule wa kawaida!
Actually, ninakubaliana nawe; huna siasa kabisa. Wewe ni mmoja wa kundi hatari ndani ya nchi hii. Unaumma huku ukipuliza saana; kama unashughulika na watu wasiokuwa na akili.Sina siasa za kitoto nauheshimu mchango wa Mzee Mtei, yeye Bob Makani na Victor Kimesela walianzisha CHADEMA mwaka ule wa 1992, wote wametangulia mbele ya haki.
Mzee Kala chumviTumshuku Mungu kwaajili ya maisha ya Edwin Mtei ambaye maisha yake hapa Duniani yaligusa watu wengi, kuanzia nyakati ngumu za uchumi hadi mwisho wa maisha yake hapa Duniani. Huyu anatajwa kama mtu aliykuwa na jasiri wa kuunena ukweli na kumshauri Hayati Nyerere RIP, pale ambapo sera zetu za uchumi zilikuwa zinaua uchumi. Hakuwahi kuwa chawa kama wateuliwa wa nyakati hizi.
Poleni sana wanafamilia, ndugu na jamii yote ya Watanzania.
RIP MteiWakuu,
Heche kupitia mtandaoni ametangaza kifo cha mwasisi wa chama chao CHADEMA, Mzee Edwin Mtei baada ya familia kuthibitisha huku mipango ya mazishi ikiendelea nyumbani kwake Tengeru, Arusha.
=====
Elimu,"Shahada ya Sanaa (Political Science, History, Geography) - Makerere (1957)"
BoT, Gavana wa kwanza (1966–1974)
Uwaziri, Waziri wa Fedha (1977–1979)
Siasa, Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA (1992)
Tawasifu, From Goatherd to Governor (2009)
1. Safari ya "Kutoka Chini"
Mtei alizaliwa mwaka 1932 huko Marangu, Moshi. Katika tawasifu yake (autobiography) iitwayo "From Goatherd to Governor", anaelezea jinsi alivyokulia katika mazingira duni, akichunga mbuzi baada ya masomo ya "bush school". Alisoma katika shule za Old Moshi na Tabora Boys kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1953.
2. Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu (BoT)
Wengi wanaijua CHADEMA, lakini hawajui kuwa Mtei ndiye alikuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati ilipoanzishwa mwaka 1966. Alisimamia mchakato wa kwanza wa kutoa sarafu ya Tanzania (shilingi) baada ya kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki. Alishikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane (1966–1974).
3. Msuguano na Mwalimu Nyerere
Mtei alikuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya Mwalimu Julius Nyerere. Hata hivyo, alijiuzulu nafasi hiyo mwaka 1979 kutokana na kutofautiana na Nyerere kuhusu sera za kiuchumi, hasa mapendekezo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambayo Nyerere aliyakataa. Kitendo chake cha kujiuzulu kwa hiari kilihesabika kama ujasiri mkubwa wa kimaslahi wakati huo.
4. Nyadhifa za Kimataifa
Kabla ya kuingia kwenye siasa za ushindani, alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na pia alifanya kazi katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kama Mkurugenzi Mtendaji (Executive Director) akiwakilisha kundi la nchi za Kiafrika.
5. Kuasisi CHADEMA
Baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1992, Mtei alikuwa mmoja wa waasisi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alihudumu kama Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho na alitumia rasilimali zake na ushawishi wake kukijenga tangu kikiwa kidogo hadi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.
6. Uhusiano wa Kifamilia na Freeman Mbowe
Jambo ambalo wengi hulitolea macho ni uhusiano wake na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Edwin Mtei ni mkwe wa Freeman Mbowe (Mbowe amemuoa binti wa Mtei, Lillian). Hii mara nyingi imekuwa ikitumiwa na wapinzani wao wa kisiasa, lakini ndani ya chama inaonekana kama muendelezo wa misingi aliyoiweka.
Umeshafika Tengeru msibani?, au ni chawa mpiga kelele wa humu JF!.Actually, ninakubaliana nawe; huna siasa kabisa. Wewe ni mmoja wa kundi hatari ndani ya nchi hii. Unaumma huku ukipuliza saana; kama unashughulika na watu wasiokuwa na akili.
Huwezi kushabikia hizo siasa za enzi za akina Mtei; halafu leo hii unageuka na kuwa mshangiliaji mkubwa; hapana, siyo mshangiliaji, bali mhusika wa mauaji ya waTanzania.
You're worse than a devil; if there's such a possibility.
The worst scum that has ever been existent in our beloved nation.
R.I.P Mzee Gavana,may your soul rest in ertenal peace.Wakuu,