TANZIA Mwasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei afariki Dunia

TANZIA Mwasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei afariki Dunia

Usiache unachotaka maishani, ghafla tu kwa kufata ulichotamani, ielewe ikuelewe kama oxygen na carbon, hauwezi hmgame bila pain muulize saigon
Naishi kibosi na usanii haupotei,
NATUMIA NOTE, TANGU INA SAHIHI YA MTEI

R.i.p mzee mtei
Usiniletee mabumunda,mjeshi nkiwa vitani,nikikuta mnaabudu punda, ntapelekea majani...yooooh yooo
 
Nchi imempoteza mwamba wa demokrasia. Apumzike kwa amani, mzee Mtei.
 
Nilijua ni wanaCcm tu ndo wanakufa na watu wanashangilia, kumbe hadi upande wa pili!!!? kweli KIFO hakina mwenyewe. 😒
Ulielewa tofauti na hii huenda ni kwa sababu mentor wako anaweza kuwa Kihongosi.
Watu wote wanajua kila mtu atakufa ila kuna watu wakifa ni afadhali na wengine wakifa ni majonzi, mfano rahisi kama ulipoolewa wakwe zako inawezekana waliona wameletwa majanga na matatizo kwa roho yako mbaya ya kuchukia ndugu wa mume na wakati Kuna shoga yako alipoolewa imekuwa furaha tupu kwa wakwe zake lakini zote ni ndoa.
 
Watu kama hawa sasa ndiyo wanahitajika kwa wingi nchini. Na siyo haya machawa yanayojua kusifia tu na kutukuza baadhi ya watu, hata pale hao watu wanapofanya madudu.

Rest in peace Mzee Edwin Mtei.
Marehemu Mzee Mtei ni mfano wa kuigwa na vijana wa nchi hii kwa misimamo ya kupigania ukweli na mapenzi kwa nchi yake na huo ndio uzalendo!!
Vijana mkiendekeza “ uchawa” mnaofanya kwa Samia matokeo yake ni nchi kuzorota na hivyo kugawanyika kwa misingi ya kidini na kiasili hivyo kuwa rahisi kushambuliwa na maadui na kupora maliasili zetu!!
Pumzika kwa amani Mzee Mtei umeonesha njia kwa wananchi wa Tanganyika.
 
Mungu amlaze pema. Tunamshukuru kwa kumrithisha mkwe wake CHADEMA ila akaishia kuporwa na Mnyampaa wa Singida. Mkwe alimwangusha sana.
 
Usiache unachotaka maishani, ghafla tu kwa kufata ulichotamani, ielewe ikuelewe kama oxygen na carbon, hauwezi hmgame bila pain muulize saigon
Naishi kibosi na usanii haupotei,
NATUMIA NOTE, TANGU INA SAHIHI YA MTEI

R.i.p mzee mtei
📌📌📌📍🔨🥺
 
Mtei kama Polepole vile.
Ukiona hukubaliani na namna nchi inavyo endeshwa unajitoa kwenye huo uongozi.
 
Wakuu,

Heche kupitia mtandaoni ametangaza kifo cha mwasisi wa chama chao CHADEMA, Mzee Edwin Mtei baada ya familia kuthibitisha huku mipango ya mazishi ikiendelea nyumbani kwake Tengeru, Arusha.

=====

View attachment 3532056

Baadhi ya mambo muhimu kuhusu Ediwin Mtei ambayo pengine ulikuwa hufahamu

Elimu,"Shahada ya Sanaa (Political Science, History, Geography) - Makerere (1957)"
BoT, Gavana wa kwanza (1966–1974)
Uwaziri, Waziri wa Fedha (1977–1979)
Siasa, Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA (1992)
Tawasifu, From Goatherd to Governor (2009)

1. Safari ya "Kutoka Chini"
Mtei alizaliwa mwaka 1932 huko Marangu, Moshi. Katika tawasifu yake (autobiography) iitwayo "From Goatherd to Governor", anaelezea jinsi alivyokulia katika mazingira duni, akichunga mbuzi baada ya masomo ya "bush school". Alisoma katika shule za Old Moshi na Tabora Boys kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1953.

2. Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu (BoT)
Wengi wanaijua CHADEMA, lakini hawajui kuwa Mtei ndiye alikuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati ilipoanzishwa mwaka 1966. Alisimamia mchakato wa kwanza wa kutoa sarafu ya Tanzania (shilingi) baada ya kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki. Alishikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane (1966–1974).

3. Msuguano na Mwalimu Nyerere
Mtei alikuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya Mwalimu Julius Nyerere. Hata hivyo, alijiuzulu nafasi hiyo mwaka 1979 kutokana na kutofautiana na Nyerere kuhusu sera za kiuchumi, hasa mapendekezo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambayo Nyerere aliyakataa. Kitendo chake cha kujiuzulu kwa hiari kilihesabika kama ujasiri mkubwa wa kimaslahi wakati huo.

4. Nyadhifa za Kimataifa
Kabla ya kuingia kwenye siasa za ushindani, alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na pia alifanya kazi katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kama Mkurugenzi Mtendaji (Executive Director) akiwakilisha kundi la nchi za Kiafrika.

5. Kuasisi CHADEMA
Baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1992, Mtei alikuwa mmoja wa waasisi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alihudumu kama Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho na alitumia rasilimali zake na ushawishi wake kukijenga tangu kikiwa kidogo hadi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

6. Uhusiano wa Kifamilia na Freeman Mbowe
Jambo ambalo wengi hulitolea macho ni uhusiano wake na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Edwin Mtei ni mkwe wa Freeman Mbowe (Mbowe amemuoa binti wa Mtei, Lillian). Hii mara nyingi imekuwa ikitumiwa na wapinzani wao wa kisiasa, lakini ndani ya chama inaonekana kama muendelezo wa misingi aliyoiweka.

RIP Mr. Mtei.
 
Back
Top Bottom