Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 4,636
- 15,247
Kwa hiyo tushushe bendera nusu mlingoti??🤓Mzee Mtei ni tunu ya taifa hili,
Kwa hiyo tushushe bendera nusu mlingoti??🤓Mzee Mtei ni tunu ya taifa hili,
Hapa Tanzania haifanyi ubebari kwa sasa? Au haujui maana ya ubebari? Tatizo hapa ni wanafiki hamtaki kukiri nyie ni mabepari ndiyo maana Mtei alikataa unafiki wenu akajitenga na nyie wanafiki. Na alikuwa sahihi. Mlichokataa 1979 ndicho mlikuja kuimplement kwenye utawala wa Mwinyi.Huo ubepari alioutaka unaihangaisha dunia nzima hivi sasa, maandamano kila kukicha huko USA maana yake sera hizo pia zinafeli tena kwa kasi.
Nyerere alishachoka pia alihisi dunia itambadilikia mbele ya safari.Hapa Tanzania haifanyi ubebari kwa sasa? Au haujui maana ya ubebari? Tatizo hapa ni wanafiki hamtaki kukiri nyoe ni mabepari ndiyo maana Mtei alikataa unafiki wenu akajitenga na nyie wanafiki. Na alikuwa sahihi. Mlichokataa 1979 ndicho mlikuja kuimplement kwenye utawala wa Mwinyi.
Hata kuondoka Nyerere madarakani ni baada ya kuona sera zake za kinafiki zimefeli akaona aibu kula matapishi yake
Ila Polepole alisema bado ni mwanaccm mtiifu na ndiyo hapo alipozingua au muda haukumtosha kufanya maamuzi tofauti. Hata Warioba nilishangaa hivi karibuni aliposema yeye bado ni mwanaccm mtiifu.Mtei kama Polepole vile.
Ukiona hukubaliani na namna nchi inavyo endeshwa unajitoa kwenye huo uongozi.
Hapa kwenye kutumia pesa zake na rasilimali zake.Kuasisi CHADEMA
Baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1992, Mtei alikuwa mmoja wa waasisi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alihudumu kama Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho na alitumia rasilimali zake na ushawishi wake kukijenga tangu kikiwa kidogo hadi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.
Miaka 93? Anataka nini zaidi? kaondoka vizuri kwa mafanikio makubwa. Sio huyo shetani wenu ataondoka na majuto kwa kuua watu.Kafa vibaya au kawaida?
Hamkuchoma mabasi yake oktoba,yeye siyo fisadi/mwizi?Miaka 93? Anataka nini zaidi? kaondoka vizuri kwa mafanikio makubwa. Sio huyo shetani wenu ataondoka na majuto kwa kuua watu.
Kama una soft copy ya kitabu chake tafadhali share mkuu.Pumzika Mzee Mtei.
Pole kwa familia.View attachment 3532143
Kama mpenda vitabu nimefurahia sana kusoma kitabu cha maisha yake "From Goatherd to Governor : The Autobiography of Edwin Mtei".
Kitabu kina historia kubwa sana sio tu ya Mtei, bali pia ya Tanzania.
May his soul rest in eternal peace!Wakuu,
Heche kupitia mtandaoni ametangaza kifo cha mwasisi wa chama chao CHADEMA, Mzee Edwin Mtei baada ya familia kuthibitisha huku mipango ya mazishi ikiendelea nyumbani kwake Tengeru, Arusha.
=====
Elimu,"Shahada ya Sanaa (Political Science, History, Geography) - Makerere (1957)"
BoT, Gavana wa kwanza (1966–1974)
Uwaziri, Waziri wa Fedha (1977–1979)
Siasa, Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA (1992)
Tawasifu, From Goatherd to Governor (2009)
1. Safari ya "Kutoka Chini"
Mtei alizaliwa mwaka 1932 huko Marangu, Moshi. Katika tawasifu yake (autobiography) iitwayo "From Goatherd to Governor", anaelezea jinsi alivyokulia katika mazingira duni, akichunga mbuzi baada ya masomo ya "bush school". Alisoma katika shule za Old Moshi na Tabora Boys kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwaka 1953.
2. Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu (BoT)
Wengi wanaijua CHADEMA, lakini hawajui kuwa Mtei ndiye alikuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati ilipoanzishwa mwaka 1966. Alisimamia mchakato wa kwanza wa kutoa sarafu ya Tanzania (shilingi) baada ya kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki. Alishikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane (1966–1974).
3. Msuguano na Mwalimu Nyerere
Mtei alikuwa Waziri wa Fedha katika serikali ya Mwalimu Julius Nyerere. Hata hivyo, alijiuzulu nafasi hiyo mwaka 1979 kutokana na kutofautiana na Nyerere kuhusu sera za kiuchumi, hasa mapendekezo ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambayo Nyerere aliyakataa. Kitendo chake cha kujiuzulu kwa hiari kilihesabika kama ujasiri mkubwa wa kimaslahi wakati huo.
4. Nyadhifa za Kimataifa
Kabla ya kuingia kwenye siasa za ushindani, alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na pia alifanya kazi katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kama Mkurugenzi Mtendaji (Executive Director) akiwakilisha kundi la nchi za Kiafrika.
5. Kuasisi CHADEMA
Baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1992, Mtei alikuwa mmoja wa waasisi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alihudumu kama Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho na alitumia rasilimali zake na ushawishi wake kukijenga tangu kikiwa kidogo hadi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.
6. Uhusiano wa Kifamilia na Freeman Mbowe
Jambo ambalo wengi hulitolea macho ni uhusiano wake na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Edwin Mtei ni mkwe wa Freeman Mbowe (Mbowe amemuoa binti wa Mtei, Lillian). Hii mara nyingi imekuwa ikitumiwa na wapinzani wao wa kisiasa, lakini ndani ya chama inaonekana kama muendelezo wa misingi aliyoiweka.
Huo ujamaa wa kuwatajirisha viongozi ni upi? Ingekuwa ni ubepari si ungekuta familia ya Nyerere ndio wanamiliki njia nyingi za uchumi hapa Bongo.Mtei alikataa ujinga wa sera za ujamaa zilizofilisi nchi huku viongozi wakineemeka na ndiyo sababu ya yeye kupingana na Nyerere na hatimaye kuondoka Serikalini
Unavyoongea utadhani wewe ni mtoto wa Mwinyi, Mkapa, Kikwete au Samia.Huo ujamaa wa kuwatajirisha viongozi ni upi? Ingekuwa ni ubepari si ungekuta familia ya Nyerere ndio wanamiliki njia nyingi za uchumi hapa Bongo.
Uwe upinzani alafu uwe fisadi si angeshafilisiwa na Nyerere na angeshanyongwa kwa uhaini!! Kuwa opposition kibongo bongo ni kuwa kwenye risk ya kufuatiliwa kila siku so no room for errors.Hamkuchoma mabasi yake oktoba,yeye siyo fisadi/mwizi?