Mwanza jiji zima hakuna Brown Bread?

Mwanza jiji zima hakuna Brown Bread?

Ukiongelea miji ya kisasa huwezi kuitaja mwanza. Mwanza inabebwa na population ila ukisasa, kama modern city huwezi kufananisha na Arusha. Arusha jiji proper ni kubwa kuliko mwanza jiji/ilemela. Watu hawaelewi. Arusha ni mji upo exposed kimataifa. Huwa nachekaga sana watu wa mwanza wakishindana na Arusha. Majiji ya kisasa ni mawili tu Tanzania. Arusha na Dar es Salaam.
Arusha tunapajua sana. Hakuna sehemu ya kishamba kama Arusha. Town Centre ndogo hapo sanawari tu tayari uko kijijini migombani. Hakuna jiji pale ni michosho tu.
 
Aisee...😂
Nikiuliza cappuccino au macchiato skinny latte, sio watasema nawatukana?
 
Aisee...
Nikiuliza cappuccino au macchiato skinny latte, sio watasema nawatukana?
Sasa wewe hata hiyo cappuccino yenyewe unaijua au ndiyo umegoogle ukaja hapa kucomment.Hebu tupisheni hapa nyie chalii wa Arusha na ushamba wenu wa kufakamia mibangi ovyo ovyo mnajikuta mnaishi Jamaica
 
Mimi kwenye hilo jiji la watu ni mgeni ila mbona Royal ipo Mkuu. Wewe kautafute mwenyewe sio kuuliza watu, kuna watu wanaiona daily na hawaijui jina.
 
Binadamu wengi kwa sasa wamehami kula vyakula vilivyokobolewa, huenda Mwanza wako mbele zaidi
 
Brown bread ya nini wakati mna samaki wa kutosha...kuleni sato na sangara inatosha acheni mbwembwe.
 
HUU MKATE UNAWAFAA WENYE KISUKARI IRINGA IPO SANA SUPERMARKETS

Tanzania nzima hakuna mkoa wanatengeneza mikate bora kama Iringa na utapata aina zote za mikate naona TOSTI anakimbiza sana siku hizi hadi wenye sukari wanafurahia huduma bora, kwa zamani ilikua Arusha lakini Arusha kwa sasa wamepoteana
 
Binadamu wengi kwa sasa wamehami kula vyakula vilivyokobolewa, huenda Mwanza wako mbele zaidi
Mwanza kwanza siku zote chakula kikuu ni ugali wa dona uliochanganywa na Muhogo na samaki wa kuchemsha or kuchoma.Mwanza Chips ni kitu cha ziada kwao wala hakuna mtu anahangaika nazo zaidi ya wageni.Brown breads ipo ya kutosha tu,kuna Royal Bakery,Pizzeria,Supermarkets za Wahindi zimejaa.Huyu lengo lake halikuwa kusema amekosa mikate,alitaka tu kulitweza Jiji la Mwanza.
 
Juzi kati nilikuwa Mwanza, sasa huwa mimi sipatani sana na hivi vitu vilivyo kobolewa aunatakaga kupunguza, kwamba vingine basi viwe ni vile havijakobolewa kama ngano.

Nikauliza wenyeji wangu kwamba nitapata brown bread Mwanza? Wakaniambia ndio nini hio nikawaambia mikate ambayo ngano yake haijakobolewa, wakaniambia hawajawahi ziona na hawazijui, Ikabidi sasa nianze kuzunguka kwenye Super Market ndogo ndogo zote hakuna, nikapata wazo la kwenda Rock city Mall, Kufika kule yaani ndio kabisa hata staff hawaijui, nilichoka sana fikiria Jiji kubwa kama lile hakuna products kama zile.

Ikabidi ninunue unga wa ngano wa Atta nikapike Chapati nyumbani.

Nikakumbuka Arusha au Dar mikate kama ile unakuta nayo maduka ya mitaani kabisa ukiachana na Super Markets.

Mwanza ni ukubwa tu ila ni jiji la kishamba sana huwezi compare na Arusha au Dar, tuiacha Dar ni kubwa sana ila huwezi ilinganisha na Arusha kamwe.
Mwanza, wenye mahitaji kama yako huenda hawapo au wakawa wachache sana, wafanyabiashara hawawezi kuweka dukani bidhaa isiyonunuliwa, ni hasara kwao.
 
Usijitambe Sana dar unakula brown bread ...pure brown bread utapata supermarket kubwa kama shoppers ,mlimani city etc...hizi brown bread kwenye maduka ya akina mangi au min supermarket nyingi sio ..maana unakuwa mkate wa kawaida ila wanaweka kitu kinaitwa BLACK JACK kuonekana brown

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ukiona hivyo ujue asilimia kubwa ya watu wako healthy hawana haja ya kucontrol sugar wanayokula as brown bread ni kwa ajili ya special diet ila kula kawaida ule mkate hapana kwakweli mana hauna tofauti na pumba za kuku ladha yake!
 
Ukiona hivyo ujue asilimia kubwa ya watu wako healthy hawana haja ya kucontrol sugar wanayokula as brown bread ni kwa ajili ya special diet ila kula kawaida ule mkate hapana kwakweli mana hauna tofauti na pumba za kuku ladha yake!
Anakuja hapa na afya yake ya mgogoro inayochagua hata vyakula halafu anatutambia kabisa amekosa brown bread.
 
Back
Top Bottom