Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 3,301
- 17,162
Wasalaam.
Leo ilikuwa ni Ufunguzi wa Mikutano ya Hadhara kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), iliyofanyika uwanja wa Furahisha mkoani Mwanza.
Pamoja na mengine mengi, hotuba ya Mwenyekiti wa Chama, Mh Freeman Aikaeli Mbowe imebeba dira na mwelekeo wa Chama hicho.
Katika hotuba hiyo, Mh Mbowe amesisitiza tuungane kama nchi pasivyo ya mgawanyo wa Vyama kuisukuma Tanzania mbele kuwa nchi yenye furaha na amani. Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa hatuwezi kugawana vipande vipande kwa minajili vya vyama vyetu vya kisiasa.
Kwa kumsikiliza tu, mtu mwenye akili anapata ufahamu kuwa Mbowe sasa anataka kuibadili CHADEMA kutoka kuwa Chama cha Kiharakati na kuwa Chama cha Siasa jumuivu. Anayaendeleza yale ambayo Mh Lowassa, alikuwa akiyahubiri katika mikutano yake ya kisiasa alipopewa jukumu la Kuwa mgombea nafasi ya Uraisi kwa muunganiko wa Vyama kadhaa (UKAWA).
Lakini, sehemu kubwa ya Wanachama wa CHADEMA wana damu inayotokota kiharakati. Kwa wao, vyama vingine haswa CCM ni maadui wao. Na hapa ndipo ninapoona ugumu wa safari ya Mbowe katika kufanikisha hilo.
Hivi karibuni, ilisambaa video ya kaka (ndugu) wa Mh Heche akimkataza mwananchi mmoja kuingia katika kilinge chake cha kazi kwa sababu tu amevaa nguo ya Chama cha Mapinduzi. Wapo waliojitokeza kulaani.
Nilipitia baadhi ya Comments za wale ninaodhani ni wanachama ama wafuasi wa CHADEMA. Kwa hakika, wanaonyesha kufurahia jambo hilo na ipo chuki ya wazi juu ya wanachama wa vyama vingine vya kisiasa.
Sehemu kubwa ya Wanachama pamoja na viongozi, wana damu na ari ya kiharakati. Ni ngumu sana Mh Mbowe kuwabadilisha. Kelele zile za kusema Mh Mwenyekiti analamba asali zitazidi mara mia ya hapo awali.
Ni ama Mh Mbowe abadili mawazo yake ama aachie ngazi kwa damu nyingine.
Tupo hapa kusubiri.